\p \v=6 \v~=Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000\f + \fr 19:6 \ft Talanta 1,000 za fedha ni sawa na tani 34.\f* za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu,\f + \fr 19:6 \ft Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi.\f* Aramu-Maaka na Soba. \¬v