\v=11 \v~=Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa \nd Bwana\nd*. Wao huweka mikate juu ya meza safi kwa taratibu za kiibada na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za \nd Bwana\nd* Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu. \¬v