\p \v=8 \v~=Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya \nd Bwana\nd* iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la \nd Bwana\nd*. \¬v \¬p