\p \v=19 \v~=Uzia, ambaye alikuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la \nd Bwana\nd*, ukoma ukamtokea penye kipaji chake cha uso. \¬v