\p \v=5 \v~=Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta 100\f + \fr 27:5 \ft Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75.\f* za fedha, kori 10,000\f + \fr 27:5 \ft Kori 10,000 za ngano ni sawa na tani 2.2.\f* za ngano na kori 10,000 za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu. \¬v \¬p