\p \v=9 \v~=Lakini kulikuwako huko nabii wa \nd Bwana\nd* aliyeitwa Odedi, akaondoka ili kukutana na jeshi liliporejea Samaria. Akawaambia, “Kwa kuwa \nd Bwana\nd*, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, aliwatia mikononi mwenu. Lakini mmewachinja kwa hasira ambayo imefika hadi mbinguni. \¬v