\v=3 \v~=Kuweni na hakika leo kwamba \nd Bwana\nd* Mungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama \nd Bwana\nd* alivyowaahidi. \¬v \¬p