\p \v=18 \v~=“Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtakwenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘\nd Bwana\nd*, Mungu wa Waebrania ametutokea. Turuhusu twende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwa \nd Bwana\nd* Mungu wetu.’ \¬v