\p \v=15 \v~=“ ‘Hili ndilo \nd Bwana\nd* Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini\f + \fr 31:15 \ft Yaani Kuzimu, Sheol kwa Kiebrania; pia mstari 16, 17.\f* nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka. \¬v