\v=3 \v~=na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la \nd Bwana\nd* Mwenyezi. Hili ndilo \nd Bwana\nd* Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu. \¬v