\p \v=16 \v~=Ndipo akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya \nd Bwana\nd*, nako huko katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, walikuwepo wanaume wapatao ishirini na watano. Wakiwa wamelipa kisogo Hekalu la \nd Bwana\nd* na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua huko mashariki. \¬v \¬p