\p \v=8 \v~=Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea \nd Bwana\nd* madhabahu na akaliitia jina la \nd Bwana\nd*. \¬v