\v=14 \v~=Alipokaribia Lehi, Wafilisti wakamjia wakipiga kelele. Roho wa \nd Bwana\nd* akamjia juu yake kwa nguvu. Kamba zilizomfunga mikono yake zikawa kama kitani iliyochomwa kwa moto, na vifungo vyake vikaanguka chini toka mikononi mwake. \¬v