\p \v=13 \v~=Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama \nd Bwana\nd* yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, \nd Bwana\nd* hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa \nd Bwana\nd* ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.” \¬v \¬p