\v=15 \v~=bali watasema, ‘Hakika kama \nd Bwana\nd* aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia.’ Maana nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao. \¬v \¬p