\m \v=19 \v~=Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumcha \nd Bwana\nd* na kuhitaji msaada wake? Je, \nd Bwana\nd* hakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!” \¬v \¬m