\p \v=17 \v~=Kisha Yeremia akamwambia Sedekia, “Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Ikiwa utajisalimisha kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, maisha yako yatasalimika, na mji huu hautateketezwa kwa moto. Pia wewe na jamaa yako mtaishi. \¬v