\v=15 \v~=Lakini msipoona vyema kumtumikia \nd Bwana\nd*, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia \nd Bwana\nd*.” \¬v \¬p