\p \v=8 \v~=Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mawili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na hesabu ya kabila za Waisraeli kama \nd Bwana\nd* alivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini mwao, mahali walipoyatua chini. \¬v