\v=31 \v~=kama Mose mtumishi wa \nd Bwana\nd* alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Sheria ya Mose: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea \nd Bwana\nd* sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.\f + \fr 8:31 \ft Sadaka za ushirika\ft*.\f* \¬v