\p \v=18 \v~=Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imeachwa katika hazina za Hekalu la \nd Bwana\nd* na za jumba lake mwenyewe la kifalme. Akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu,\f + \fr 15:18 \ft Yaani Shamu (ambayo leo ni Syria).\f* aliyekuwa akitawala Dameski. \¬v