\v=11 \v~=naye Solomoni akampa Hiramu kori 20,000\f + \fr 5:11 \ft Kori 20,000 ni sawa na madebe 240,000.\f* za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi 20,000.\f + \fr 5:11 \ft Bathi 20,000 ni sawa na madebe 200.\f* Solomoni aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka. \¬v