\v=17 \v~=Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane.\f + \fr 25:17 \ft Dhiraa 18 ni sawa na mita 8.2.\f* Sehemu ya shaba juu ya nguzo moja ilikuwa na urefu wa dhiraa tatu\f + \fr 25:17 \ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\f* na ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine pamoja na wavu wake ilifanana na hiyo ya kwanza. \¬v \¬p