\p \v=10 \v~=“Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi za efa\f + \fr 14:10 \ft Sehemu tatu za kumi za efa ni sawa na kilo 3.\f* za unga laini uliochanganywa na mafuta, kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi moja\f + \fr 14:10 \ft Logi ni kipimo cha ujazo ambacho ni sawa na lita 0.3.\f* ya mafuta. \¬v