\v=22 \v~=Kamwe usimtolee \nd Bwana\nd* mnyama aliye kipofu, aliyejeruhiwa wala aliye kilema, au chochote kilicho na uvimbe, au chenye upele au vidonda vinavyotoka usaha. Kamwe chochote cha aina hii kisiwekwe juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa \nd Bwana\nd* ya kuteketezwa kwa moto. \¬v