\p \v=29 \v~=Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapo \nd Bwana\nd* amesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maana \nd Bwana\nd* ameahidi mambo mema kwa Israeli.” \¬v \¬p