\v=6 \v~=Ndipo nikasikia kile kilichokuwa kama sauti katikati ya wale viumbe wanne wenye uhai ikisema, “Kipimo kimoja\f + \fr 6:6 \ft Ni kama lita moja.\f* cha ngano kwa mshahara wa kibarua wa siku moja,\f + \fr 6:6 \ft Sawa na dinari moja.\f* na vipimo vitatu vya shayiri kwa mshahara wa kibarua cha siku moja. Lakini usiharibu mafuta wala divai!” \¬v \¬p