\v=8 \v~=Nikatazama, na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mwenye rangi ya kijivujivu! Yeye aliyempanda aliitwa Mauti, naye Kuzimu\f + \fr 6:8 \ft Kuzimu linalotokana na neno Hades la Kiyunani au Sheol kwa Kiebrania.\f* alikuwa akimfuata nyuma yake kwa karibu. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia. \¬v \¬p