\p \v=11 \v~=Kisha wazee pamoja na watu wote waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni mashahidi. \nd Bwana\nd* na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wanawake wawili ambao pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrathi na uwe mashuhuri katika Bethlehemu. \¬v