\p \v=6 \v~=Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. Huenda \nd Bwana\nd* atatenda kwa ajili yetu. Hakuna chochote kitakachoweza kumzuia \nd Bwana\nd* kuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.” \¬v \¬p