\v=19 \v~=Sasa mfalme bwana wangu na asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama \nd Bwana\nd* amekuchochea dhidi yangu, basi yeye na aipokee sadaka yangu. Lakini hata hivyo, kama ni wanadamu waliofanya hivyo, walaaniwe mbele za \nd Bwana\nd*! Wao sasa wamenifukuza kutoka sehemu yangu katika urithi wa \nd Bwana\nd* wangu wakisema, ‘Nenda ukatumikie miungu mingine.’ \¬v