id = '2TI - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version' rem = 'Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.' headers = h = '2 Timotheo' toc1 = '2 Timotheo' toc2 = '2 Timotheo' toc3 = '2Tim' mt1 = '2 Timotheo' ¬headers = chapters = c = '1' p = '' c# = '1' v = '1' v~ = 'Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu.' ¬v = '1' ¬p = p = '' v = '2' v~ = 'Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa:' ¬p = p = '' p~ = 'Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.' ¬p = ¬v = '2' v= = '3' s1 = 'Shukrani Na Kutiwa Moyo' p = '' v = '3' v~ = 'Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.' ¬v = '3' v = '4' v~ = 'Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nipate kujawa na furaha.' ¬v = '4' v = '5' v~ = 'Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo.' ¬v = '5' v = '6' v~ = 'Kwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu, iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu.' ¬v = '6' v = '7' v~ = 'Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.' ¬v = '7' ¬p = p = '' v = '8' v~ = 'Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu,' ¬v = '8' v = '9' v~ = 'ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele.' ¬v = '9' v = '10' v~ = 'Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Kristo Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili.' ¬v = '10' v = '11' v~ = 'Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii.' ¬v = '11' v = '12' v~ = 'Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.' ¬v = '12' ¬p = p = '' v = '13' v~ = 'Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu.' ¬v = '13' v = '14' v~ = 'Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.' ¬v = '14' ¬p = p = '' v = '15' v~ = 'Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.' ¬v = '15' ¬p = p = '' v = '16' v~ = 'Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu.' ¬v = '16' v = '17' v~ = 'Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata.' ¬v = '17' v = '18' v~ = 'Bwana na amjalie kupata rehema zake siku ile! Nawe unajua vyema jinsi alivyonisaidia huko Efeso.' ¬v = '18' ¬p = ¬c = '1' c = '2' v= = '1' s1 = 'Askari Mwema Wa Kristo Yesu' p = '' c# = '2' v = '1' v~ = 'Basi, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu.' ¬v = '1' v = '2' v~ = 'Nayo mambo yale uliyonisikia nikiyasema mbele ya mashahidi wengi, uwakabidhi watu waaminifu watakaoweza kuwafundisha watu wengine vilevile.' ¬v = '2' v = '3' v~ = 'Vumilia taabu pamoja nasi kama askari mwema wa Kristo Yesu.' ¬v = '3' v = '4' v~ = 'Hakuna askari yeyote ambaye akiwa vitani hujishughulisha na mambo ya kawaida ya maisha haya kwa sababu nia yake ni kumpendeza yule aliyemwandika awe askari.' ¬v = '4' v = '5' v~ = 'Vivyo hivyo, yeye ashindanaye katika michezo hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano.' ¬v = '5' v = '6' v~ = 'Mkulima mwenye bidii ya kazi ndiye anayestahili kuwa wa kwanza kupata fungu la mavuno.' ¬v = '6' v = '7' v~ = 'Fikiri sana kuhusu haya nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo hayo yote.' ¬v = '7' ¬p = p = '' v = '8' v~ = 'Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, yeye aliye wa uzao wa Daudi. Hii ndiyo Injili yangu,' ¬v = '8' v = '9' v~ = 'ambayo kwayo ninateseka hata kufikia hatua ya kufungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halifungwi.' ¬v = '9' v = '10' v~ = 'Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.' ¬v = '10' ¬p = p = '' v = '11' v~ = 'Hili ni neno la kuaminiwa:' ¬p = q1 = '' p~ = 'Kwa maana kama tumekufa pamoja naye,' ¬q1 = q2 = '' p~ = 'tutaishi pia pamoja naye.' ¬q2 = ¬v = '11' q1 = '' v = '12' v~ = 'Kama tukistahimili,' ¬q1 = q2 = '' p~ = 'pia tutatawala pamoja naye.' ¬q2 = q1 = '' p~ = 'Kama tukimkana yeye,' ¬q1 = q2 = '' p~ = 'naye atatukana sisi.' ¬q2 = ¬v = '12' q1 = '' v = '13' v~ = 'Kama tusipoamini,' ¬q1 = q2 = '' p~ = 'yeye hudumu kuwa mwaminifu,' ¬q2 = q2 = '' p~ = 'kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.' ¬q2 = ¬v = '13' v= = '14' s1 = 'Mfanyakazi Aliyekubaliwa Na Mungu' p = '' v = '14' v~ = 'Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.' ¬v = '14' v = '15' v~ = 'Jitahidi kujionyesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli.' ¬v = '15' v = '16' v~ = 'Jiepushe na maneno mabaya, yasiyo na maana, yasiyo ya utauwa, kwa maana hayo huzidi kuwatosa watu katika kukosa heshima kwa Mungu.' ¬v = '16' v = '17' v~ = 'Mafundisho yao yataenea kama kidonda kisichopona. Miongoni mwao wamo Himenayo na Fileto' ¬v = '17' v = '18' v~ = 'ambao wameiacha kweli, wakisema kwamba ufufuo wa wafu umekwisha kuwako, nao huharibu imani ya baadhi ya watu.' ¬v = '18' v = '19' v~ = 'Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, ukiwa na muhuri wenye maandishi haya: “Bwana anawajua walio wake”; tena, “Kila alitajaye jina la Bwana, na auache uovu.”' ¬v = '19' ¬p = p = '' v = '20' v~ = 'Katika nyumba kubwa si kwamba kuna vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali pia vimo vyombo vya miti na vya udongo; vingine kwa matumizi maalum, na vingine kwa matumizi ya kawaida.' ¬v = '20' v = '21' v~ = 'Basi ikiwa mtu amejitakasa na kujitenga na hayo niliyoyataja, atakuwa chombo maalum, kilichotengwa na ambacho kinamfaa mwenye nyumba, kimeandaliwa tayari kwa kila kazi njema.' ¬v = '21' ¬p = p = '' v = '22' v~ = 'Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.' ¬v = '22' v = '23' v~ = 'Jiepushe na mabishano ya kipumbavu na yasiyo na maana, kwa kuwa wajua ya kwamba hayo huzaa magomvi.' ¬v = '23' v = '24' v~ = 'Tena haimpasi mtumishi wa Bwana kuwa mgomvi, bali inampasa awe mwema kwa kila mtu, awezaye kufundisha, tena mvumilivu.' ¬v = '24' v = '25' v~ = 'Inampasa kuwaonya kwa upole wale wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli,' ¬v = '25' v = '26' v~ = 'ili fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke katika mtego wa ibilisi ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake.' ¬v = '26' ¬p = ¬c = '2' c = '3' v= = '1' s1 = 'Hatari Za Siku Za Mwisho' p = '' c# = '3' v = '1' v~ = 'Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari.' ¬v = '1' v = '2' v~ = 'Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu,' ¬v = '2' v = '3' v~ = 'wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema,' ¬v = '3' v = '4' v~ = 'wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu:' ¬v = '4' v = '5' v~ = 'wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo.' ¬v = '5' ¬p = p = '' v = '6' v~ = 'Miongoni mwao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu na kuwachukua mateka wanawake wajinga, waliolemewa na dhambi zao na kuyumbishwa na aina zote za tamaa mbaya.' ¬v = '6' v = '7' v~ = 'Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli.' ¬v = '7' v = '8' v~ = 'Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Mose, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani.' ¬v = '8' v = '9' v~ = 'Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu wawili.' ¬v = '9' ¬p = v= = '10' s1 = 'Paulo Amwagiza Timotheo' p = '' v = '10' v~ = 'Lakini wewe umeyajua mafundisho yangu, mwenendo, makusudi, imani, uvumilivu, upendo, ustahimilivu,' ¬v = '10' v = '11' v~ = 'mateso na taabu, yaani mambo yote yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Listra, mateso yote niliyostahimili, lakini Bwana aliniokoa katika hayo yote.' ¬v = '11' v = '12' v~ = 'Naam, yeyote anayetaka kuishi maisha ya utauwa ndani ya Kristo Yesu atateswa.' ¬v = '12' v = '13' v~ = 'Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.' ¬v = '13' v = '14' v~ = 'Bali wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani,' ¬v = '14' v = '15' v~ = 'na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.' ¬v = '15' v = '16' v~ = 'Kila Andiko limevuviwa na Mungu na lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki,' ¬v = '16' v = '17' v~ = 'ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.' ¬v = '17' ¬p = ¬c = '3' c = '4' v= = '1' s1 = 'Maagizo Ya Mwisho' p = '' c# = '4' v = '1' v~ = 'Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu watu walio hai na waliokufa wakati wa kuja kwake na ufalme wake, kwamba:' ¬v = '1' v = '2' v~ = 'Hubiri Neno; kuwa tayari wakati ufaao na wakati usiofaa; karipia, kemea na utie moyo kwa uvumilivu wote na kwa mafundisho mazuri.' ¬v = '2' v = '3' v~ = 'Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia.' ¬v = '3' v = '4' v~ = 'Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo.' ¬v = '4' v = '5' v~ = 'Kwa habari yako wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako.' ¬v = '5' ¬p = p = '' v = '6' v~ = 'Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya kuondoka imetimia.' ¬v = '6' v = '7' v~ = 'Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda.' ¬v = '7' v = '8' v~ = 'Sasa nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.' ¬v = '8' ¬p = v= = '9' s1 = 'Maelekezo Ya Binafsi' p = '' v = '9' v~ = 'Jitahidi kuja kwangu upesi' ¬v = '9' v = '10' v~ = 'kwa sababu Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha na amekwenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia.' ¬v = '10' v = '11' v~ = 'Ni Luka peke yake aliye hapa pamoja nami. Mtafute Marko uje naye kwa sababu ananifaa sana katika huduma yangu.' ¬v = '11' v = '12' v~ = 'Nimemtuma Tikiko huko Efeso.' ¬v = '12' v = '13' v~ = 'Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu vyangu, hasa vile vya ngozi.' ¬v = '13' ¬p = p = '' v = '14' v~ = 'Aleksanda yule mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Bwana atamlipa kwa ajili ya yale aliyotenda.' ¬v = '14' v = '15' v~ = 'Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.' ¬v = '15' ¬p = p = '' v = '16' v~ = 'Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza, hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila mmoja aliniacha. Namwomba Mungu wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.' ¬v = '16' v = '17' v~ = 'Lakini Bwana alisimama upande wangu akanitia nguvu, ili kupitia kwangu lile Neno lihubiriwe kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka kinywa cha simba.' ¬v = '17' v = '18' v~ = 'Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen.' ¬v = '18' ¬p = v= = '19' s1 = 'Salamu Za Mwisho' p = '' v = '19' v~ = 'Wasalimu Prisila na Akila, na wote wa nyumbani kwa Onesiforo.' EXTRA( fn @ 16 = '+ \\fr 4:19 \\ft Prisila kwa Kiyunani ni Priska, hivyo tafsiri nyingine zimemuita Priska.') ¬v = '19' v = '20' v~ = 'Erasto alibaki Korintho. Nami nikamwacha Trofimo huko Mileto akiwa mgonjwa.' ¬v = '20' v = '21' v~ = 'Jitahidi ufike huku kabla ya majira ya baridi. Eubulo anakusalimu, vivyo hivyo Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.' ¬v = '21' ¬p = p = '' v = '22' v~ = 'Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.' ¬v = '22' ¬p = ¬c = '4' ¬chapters =