id = 'PHM - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version' rem = 'Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.' headers = h = 'Filemoni' toc1 = 'Filemoni' toc2 = 'Filemoni' toc3 = 'Flm' mt1 = 'Filemoni' ¬headers = chapters = c = '1' p = '' c# = '1' v = '1' v~ = 'Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, pamoja na Timotheo ndugu yetu:' ¬p = p = '' p~ = 'Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu,' ¬v = '1' v = '2' v~ = 'kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kanisa lile likutanalo nyumbani mwako:' ¬v = '2' ¬p = p = '' v = '3' v~ = 'Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.' ¬v = '3' ¬p = v= = '4' s1 = 'Shukrani Na Maombi' p = '' v = '4' v~ = 'Siku zote ninamshukuru Mungu ninapokukumbuka katika maombi yangu,' ¬v = '4' v = '5' v~ = 'kwa sababu ninasikia juu ya imani yako katika Bwana Yesu na upendo wako kwa watakatifu wote.' ¬v = '5' v = '6' v~ = 'Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya Kristo.' ¬v = '6' v = '7' v~ = 'Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.' ¬v = '7' ¬p = v= = '8' s1 = 'Maombi Ya Paulo Ya Kumtetea Onesimo' p = '' v = '8' v~ = 'Hata hivyo, ingawa katika Kristo ningeweza kuwa na ujasiri na kukuagiza yale yakupasayo kutenda,' ¬v = '8' v = '9' v~ = 'lakini ninakuomba kwa upendo, mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Kristo Yesu,' ¬v = '9' v = '10' v~ = 'nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo.' EXTRA( fn @ 39 = '+ \\fr 1:10 \\fq Onesimo \\ft maana yake ni \\fqa Wa manufaa.') ¬v = '10' v = '11' v~ = 'Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia.' ¬v = '11' ¬p = p = '' v = '12' v~ = 'Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa.' ¬v = '12' v = '13' v~ = 'Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili.' ¬v = '13' v = '14' v~ = 'Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari.' ¬v = '14' v = '15' v~ = 'Huenda sababu ya yeye kutengwa nawe kwa kitambo kidogo ni ili uwe naye daima.' ¬v = '15' v = '16' v~ = 'Si kama mtumwa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana.' ¬v = '16' ¬p = p = '' v = '17' v~ = 'Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika wako, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe.' ¬v = '17' v = '18' v~ = 'Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi.' ¬v = '18' v = '19' v~ = 'Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa. Sitaji kwamba nakudai hata nafsi yako.' ¬v = '19' v = '20' v~ = 'Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana, uuburudishe moyo wangu katika Kristo.' ¬v = '20' v = '21' v~ = 'Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.' ¬v = '21' ¬p = p = '' v = '22' v~ = 'Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu.' ¬v = '22' ¬p = v= = '23' s1 = 'Salamu Za Mwisho Na Dua Ya Kuwatakia Heri' p = '' v = '23' v~ = 'Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu, anakusalimu.' ¬v = '23' v = '24' v~ = 'Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu.' ¬v = '24' ¬p = p = '' v = '25' v~ = 'Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.' ¬v = '25' ¬p = ¬c = '1' ¬chapters =