; TITLE: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version ; ABBREVIATION: KCV ; HAS ITALICS ; HAS FOOTNOTES ; HAS REDLETTER $$ PHM 1:1 ¶ Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, pamoja na Timotheo ndugu yetu: Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu, $$ PHM 1:2 ¶ kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kanisa lile likutanalo nyumbani mwako: $$ PHM 1:3 ¶ Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. $$ PHM 1:4 ¶ Siku zote ninamshukuru Mungu ninapokukumbuka katika maombi yangu, $$ PHM 1:5 kwa sababu ninasikia juu ya imani yako katika Bwana Yesu na upendo wako kwa watakatifu wote. $$ PHM 1:6 Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya Kristo. $$ PHM 1:7 Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu. $$ PHM 1:8 ¶ Hata hivyo, ingawa katika Kristo ningeweza kuwa na ujasiri na kukuagiza yale yakupasayo kutenda, $$ PHM 1:9 lakini ninakuomba kwa upendo, mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Kristo Yesu, $$ PHM 1:10 nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo. $$ PHM 1:11 Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia. $$ PHM 1:12 ¶ Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa. $$ PHM 1:13 Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili. $$ PHM 1:14 Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari. $$ PHM 1:15 Huenda sababu ya yeye kutengwa nawe kwa kitambo kidogo ni ili uwe naye daima. $$ PHM 1:16 Si kama mtumwa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana. $$ PHM 1:17 ¶ Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika wako, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe. $$ PHM 1:18 Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi. $$ PHM 1:19 Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa. Sitaji kwamba nakudai hata nafsi yako. $$ PHM 1:20 Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana, uuburudishe moyo wangu katika Kristo. $$ PHM 1:21 Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba. $$ PHM 1:22 ¶ Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu. $$ PHM 1:23 ¶ Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu, anakusalimu. $$ PHM 1:24 Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu. $$ PHM 1:25 ¶ Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.