; TITLE: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version ; ABBREVIATION: KCV ; HAS ITALICS ; HAS FOOTNOTES ; HAS REDLETTER (Zaburi 1–41) Zaburi 1 $$ PSA 1:1 Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha. $$ PSA 1:2 Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana. $$ PSA 1:3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa. $$ PSA 1:4 Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. $$ PSA 1:5 Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki. $$ PSA 1:6 Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia. Zaburi 2 $$ PSA 2:1 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure? $$ PSA 2:2 Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. $$ PSA 2:3 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” $$ PSA 2:4 Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. $$ PSA 2:5 Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, $$ PSA 2:6 “Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” $$ PSA 2:7 Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa. $$ PSA 2:8 Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako. $$ PSA 2:9 Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.” $$ PSA 2:10 Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. $$ PSA 2:11 Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka. $$ PSA 2:12 Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia. Zaburi 3 Zaburi ya Daudi. Alipomkimbia mwanawe Absalomu. $$ PSA 3:1 Ee Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu! $$ PSA 3:2 Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” $$ PSA 3:3 Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. $$ PSA 3:4 Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. $$ PSA 3:5 Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza. $$ PSA 3:6 Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande. $$ PSA 3:7 Ee Bwana, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu. $$ PSA 3:8 Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana. Baraka yako na iwe juu ya watu wako. Zaburi 4 Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 4:1 Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu. $$ PSA 4:2 Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu mpaka lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo mpaka lini? $$ PSA 4:3 Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga wale wamchao kwa ajili yake; Bwana atanisikia nimwitapo. $$ PSA 4:4 Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu. $$ PSA 4:5 Toeni dhabihu zilizo haki; mtegemeeni Bwana. $$ PSA 4:6 Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonyesha jema lolote?” Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako. $$ PSA 4:7 Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi. $$ PSA 4:8 Nitajilaza chini na kulala kwa amani, kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana, waniwezesha kukaa kwa salama. Zaburi 5 Kwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 5:1 Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. $$ PSA 5:2 Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba. $$ PSA 5:3 Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini. $$ PSA 5:4 Wewe si Mungu unayefurahia uovu, kwako mtu mwovu hataishi. $$ PSA 5:5 Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya. $$ PSA 5:6 Unawaangamiza wasemao uongo. Bwana huwachukia wamwagao damu na wadanganyifu. $$ PSA 5:7 Lakini mimi, kwa rehema zako kuu, nitakuja katika nyumba yako, kwa unyenyekevu, nitasujudu kuelekea Hekalu lako takatifu. $$ PSA 5:8 Niongoze katika haki yako, Ee Bwana, kwa sababu ya adui zangu, nyoosha njia yako mbele yangu. $$ PSA 5:9 Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, mioyo yao imejaa maangamizi. Koo lao ni kaburi lililo wazi, kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu. $$ PSA 5:10 Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu! Hila zao ziwe anguko lao wenyewe. Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi, kwa kuwa wamekuasi wewe. $$ PSA 5:11 Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wapendao jina lako wapate kukushangilia. $$ PSA 5:12 Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao. Zaburi 6 Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 6:1 Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. $$ PSA 6:2 Unirehemu Bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee Bwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali. $$ PSA 6:3 Nafsi yangu ina uchungu mwingi. Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini? $$ PSA 6:4 Geuka Ee Bwana, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako. $$ PSA 6:5 Hakuna mtu anayekukumbuka akiwa amekufa. Ni nani awezaye kukusifu akiwa kuzimu? $$ PSA 6:6 Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; usiku kucha nafurikisha kitanda changu kwa machozi; nimelowesha viti vyangu vya fahari kwa machozi. $$ PSA 6:7 Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote. $$ PSA 6:8 Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu. $$ PSA 6:9 Bwana amesikia kilio changu kwa huruma, Bwana amekubali sala yangu. $$ PSA 6:10 Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula. Zaburi 7 Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini. $$ PSA 7:1 Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia, $$ PSA 7:2 la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. $$ PSA 7:3 Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu, $$ PSA 7:4 au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu, $$ PSA 7:5 basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini. $$ PSA 7:6 Amka kwa hasira yako, Ee Bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki. $$ PSA 7:7 Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu. $$ PSA 7:8 Bwana na awahukumu kabila za watu. Nihukumu Ee Bwana, kwa kadiri ya haki yangu, kwa kadiri ya uadilifu wangu, Ewe Uliye Juu Sana. $$ PSA 7:9 Ee Mungu mwenye haki, uchunguzaye mawazo na mioyo, komesha ghasia za waovu na ufanye wenye haki waishi kwa amani. $$ PSA 7:10 Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, awaokoaye wanyofu wa moyo. $$ PSA 7:11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku. $$ PSA 7:12 Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. $$ PSA 7:13 Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto. $$ PSA 7:14 Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo. $$ PSA 7:15 Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe. $$ PSA 7:16 Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani. $$ PSA 7:17 Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana. Zaburi 8 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 8:1 Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu. $$ PSA 8:2 Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa, kwa sababu ya watesi wako, kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. $$ PSA 8:3 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha, $$ PSA 8:4 mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali? $$ PSA 8:5 Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima. $$ PSA 8:6 Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake. $$ PSA 8:7 Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni, $$ PSA 8:8 ndege wa angani na samaki wa baharini, naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari. $$ PSA 8:9 Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Zaburi 9 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 9:1 Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. $$ PSA 9:2 Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. $$ PSA 9:3 Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako. $$ PSA 9:4 Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki. $$ PSA 9:5 Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu; umeyafuta majina yao milele na milele. $$ PSA 9:6 Uharibifu usiokoma umempata adui, umeingʼoa miji yao; hata kumbukumbu lao limetoweka. $$ PSA 9:7 Bwana anatawala milele, ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu. $$ PSA 9:8 Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki, atatawala mataifa kwa haki. $$ PSA 9:9 Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida. $$ PSA 9:10 Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao. $$ PSA 9:11 Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda. $$ PSA 9:12 Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa. $$ PSA 9:13 Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti, $$ PSA 9:14 ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni na huko niushangilie wokovu wako. $$ PSA 9:15 Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha. $$ PSA 9:16 Bwana anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao. $$ PSA 9:17 Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. $$ PSA 9:18 Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea. $$ PSA 9:19 Ee Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde. Mataifa na yahukumiwe mbele zako. $$ PSA 9:20 Ee Bwana, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu. Zaburi 10 $$ PSA 10:1 Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida? $$ PSA 10:2 Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. $$ PSA 10:3 Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana Bwana. $$ PSA 10:4 Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu. $$ PSA 10:5 Njia zake daima hufanikiwa; hujivuna na amri zako ziko mbali naye, huwacheka kwa dharau adui zake wote. $$ PSA 10:6 Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, daima nitakuwa na furaha, kamwe sitakuwa na shida.” $$ PSA 10:7 Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; shida na ubaya viko chini ya ulimi wake. $$ PSA 10:8 Huvizia karibu na vijiji; kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia, akivizia wapitaji. $$ PSA 10:9 Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake. $$ PSA 10:10 Mateka wake hupondwa, huzimia; wanaanguka katika nguvu zake. $$ PSA 10:11 Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.” $$ PSA 10:12 Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge. $$ PSA 10:13 Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? Kwa nini anajiambia mwenyewe, “Hataniita nitoe hesabu?” $$ PSA 10:14 Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima. $$ PSA 10:15 Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana. $$ PSA 10:16 Bwana ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake. $$ PSA 10:17 Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao, $$ PSA 10:18 ukiwatetea yatima na walioonewa, ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena. Zaburi 11 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 11:1 Kwa Bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako. $$ PSA 11:2 Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo. $$ PSA 11:3 Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?” $$ PSA 11:4 Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu. $$ PSA 11:5 Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia. $$ PSA 11:6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao. $$ PSA 11:7 Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake. Zaburi 12 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 12:1 Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu. $$ PSA 12:2 Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu. $$ PSA 12:3 Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno, $$ PSA 12:4 ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?” $$ PSA 12:5 “Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge na kulia kwa uchungu kwa wahitaji, nitainuka sasa,” asema Bwana. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.” $$ PSA 12:6 Maneno ya Bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba. $$ PSA 12:7 Ee Bwana, utatuweka salama na kutulinda na kizazi hiki milele. $$ PSA 12:8 Watu waovu huenda wakiringa kila mahali wakati ambapo yule aliye mbaya sana ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu. Zaburi 13 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 13:1 Mpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako mpaka lini? $$ PSA 13:2 Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini? $$ PSA 13:3 Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti. $$ PSA 13:4 Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka. $$ PSA 13:5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako. $$ PSA 13:6 Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu. Zaburi 14 (Zaburi 53) Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 14:1 Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema. $$ PSA 14:2 Bwana anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. $$ PSA 14:3 Wote wamepotoka, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja! $$ PSA 14:4 Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza: wale ambao huwala watu wangu kama watu walavyo mkate, hao ambao hawamwiti Bwana? $$ PSA 14:5 Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu, maana Mungu yupo pamoja na wenye haki. $$ PSA 14:6 Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini, bali Bwana ndiye kimbilio lao. $$ PSA 14:7 Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni! Wakati Bwana arejeshapo wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi! Zaburi 15 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 15:1 Bwana, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? $$ PSA 15:2 Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake, $$ PSA 15:3 na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake, $$ PSA 15:4 ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia. $$ PSA 15:5 Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika. Zaburi 16 Utenzi wa Daudi. $$ PSA 16:1 Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia. $$ PSA 16:2 Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” $$ PSA 16:3 Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. $$ PSA 16:4 Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu. $$ PSA 16:5 Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama. $$ PSA 16:6 Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri. $$ PSA 16:7 Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha. $$ PSA 16:8 Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika. $$ PSA 16:9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama, $$ PSA 16:10 kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu. $$ PSA 16:11 Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume. Zaburi 17 Sala ya Daudi. $$ PSA 17:1 Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu. $$ PSA 17:2 Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki. $$ PSA 17:3 Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi. $$ PSA 17:4 Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri. $$ PSA 17:5 Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza. $$ PSA 17:6 Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu. $$ PSA 17:7 Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao. $$ PSA 17:8 Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako $$ PSA 17:9 kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka. $$ PSA 17:10 Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno. $$ PSA 17:11 Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini. $$ PSA 17:12 Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni. $$ PSA 17:13 Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako. $$ PSA 17:14 Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. $$ PSA 17:15 Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako. Zaburi 18 (2 Samweli 22:1-51) Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana aliyomwimbia Bwana wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Alisema hivi: $$ PSA 18:1 Nakupenda wewe, Ee Bwana, nguvu yangu. $$ PSA 18:2 Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu. $$ PSA 18:3 Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. $$ PSA 18:4 Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. $$ PSA 18:5 Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. $$ PSA 18:6 Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake. $$ PSA 18:7 Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. $$ PSA 18:8 Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake. $$ PSA 18:9 Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. $$ PSA 18:10 Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo. $$ PSA 18:11 Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, hema lake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua ya angani. $$ PSA 18:12 Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi. $$ PSA 18:13 Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. $$ PSA 18:14 Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza. $$ PSA 18:15 Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako. $$ PSA 18:16 Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. $$ PSA 18:17 Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. $$ PSA 18:18 Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu. $$ PSA 18:19 Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. $$ PSA 18:20 Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. $$ PSA 18:21 Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. $$ PSA 18:22 Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. $$ PSA 18:23 Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi. $$ PSA 18:24 Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake. $$ PSA 18:25 Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia. $$ PSA 18:26 Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi. $$ PSA 18:27 Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini huwashusha wenye kiburi. $$ PSA 18:28 Wewe, Ee Bwana, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka; Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga. $$ PSA 18:29 Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta. $$ PSA 18:30 Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. $$ PSA 18:31 Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? $$ PSA 18:32 Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. $$ PSA 18:33 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. $$ PSA 18:34 Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. $$ PSA 18:35 Hunipa ngao yako ya ushindi, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, unajishusha chini ili kuniinua. $$ PSA 18:36 Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze. $$ PSA 18:37 Niliwafuatia adui zangu na nikawapata, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa. $$ PSA 18:38 Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu. $$ PSA 18:39 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. $$ PSA 18:40 Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu. $$ PSA 18:41 Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu. $$ PSA 18:42 Niliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo; niliwamwaga nje kama tope barabarani. $$ PSA 18:43 Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu; umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa, watu ambao sikuwajua wananitumikia. $$ PSA 18:44 Mara wanisikiapo hunitii, wageni hunyenyekea mbele yangu. $$ PSA 18:45 Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. $$ PSA 18:46 Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu! $$ PSA 18:47 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, awatiishaye mataifa chini yangu, $$ PSA 18:48 aniokoaye na adui zangu. Uliniinua juu ya adui zangu; uliniokoa toka kwa watu wajeuri. $$ PSA 18:49 Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana; nitaliimbia sifa jina lako. $$ PSA 18:50 Humpa mfalme wake ushindi mkuu, huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na wazao wake milele. Zaburi 19 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 19:1 Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake. $$ PSA 19:2 Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa. $$ PSA 19:3 Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki. $$ PSA 19:4 Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu. Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua, $$ PSA 19:5 linafanana na bwana arusi akitoka chumbani mwake, kama shujaa afurahiavyo kukamilisha kushindana kwake. $$ PSA 19:6 Huchomoza upande mmoja wa mbingu, na kufanya mzunguko wake hadi upande mwingine. Hakuna kilichojificha joto lake. $$ PSA 19:7 Sheria ya Bwana ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima. $$ PSA 19:8 Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni. $$ PSA 19:9 Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki. $$ PSA 19:10 Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega. $$ PSA 19:11 Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa. $$ PSA 19:12 Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. $$ PSA 19:13 Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa. $$ PSA 19:14 Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu. Zaburi 20 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 20:1 Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako. $$ PSA 20:2 Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni. $$ PSA 20:3 Na azikumbuke dhabihu zako zote, na azikubali sadaka zako za kuteketezwa. $$ PSA 20:4 Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote. $$ PSA 20:5 Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Bwana na akupe haja zako zote. $$ PSA 20:6 Sasa nafahamu kuwa Bwana humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume. $$ PSA 20:7 Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu. $$ PSA 20:8 Wao wameshushwa chini na kuanguka, bali sisi tunainuka na kusimama imara. $$ PSA 20:9 Ee Bwana, mwokoe mfalme! Tujibu tunapokuita! Zaburi 21 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 21:1 Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa! $$ PSA 21:2 Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake. $$ PSA 21:3 Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. $$ PSA 21:4 Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele. $$ PSA 21:5 Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu. $$ PSA 21:6 Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako. $$ PSA 21:7 Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa. $$ PSA 21:8 Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako. $$ PSA 21:9 Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza. $$ PSA 21:10 Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu. $$ PSA 21:11 Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa, $$ PSA 21:12 kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka kwenye upinde wako. $$ PSA 21:13 Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako. Zaburi 22 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi. $$ PSA 22:1 Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu? $$ PSA 22:2 Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi. $$ PSA 22:3 Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli. $$ PSA 22:4 Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa. $$ PSA 22:5 Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika. $$ PSA 22:6 Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau. $$ PSA 22:7 Wote wanionao hunidhihaki, hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao: $$ PSA 22:8 Husema, “Anamtegemea Bwana, basi Bwana na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.” $$ PSA 22:9 Hata hivyo ulinitoa tumboni, ukanifanya nikutegemee, hata nilipokuwa ninanyonya matiti ya mama yangu. $$ PSA 22:10 Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa, toka tumboni mwa mama yangu umekuwa Mungu wangu. $$ PSA 22:11 Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia. $$ PSA 22:12 Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira. $$ PSA 22:13 Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu. $$ PSA 22:14 Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu. $$ PSA 22:15 Nguvu zangu zimekauka kama kigae, ulimi wangu umegandamana na kaakaa la kinywa changu, kwa sababu umenilaza katika mavumbi ya kifo. $$ PSA 22:16 Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira, wametoboa mikono yangu na miguu yangu. $$ PSA 22:17 Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, watu wananikodolea macho na kunisimanga. $$ PSA 22:18 Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, na vazi langu wanalipigia kura. $$ PSA 22:19 Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie. $$ PSA 22:20 Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa. $$ PSA 22:21 Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu. $$ PSA 22:22 Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe. $$ PSA 22:23 Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli! $$ PSA 22:24 Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie. $$ PSA 22:25 Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe. $$ PSA 22:26 Maskini watakula na kushiba, wale wamtafutao Bwana watamsifu: mioyo yenu na iishi milele! $$ PSA 22:27 Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia Bwana, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake, $$ PSA 22:28 kwa maana ufalme ni wa Bwana naye hutawala juu ya mataifa. $$ PSA 22:29 Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu. Wote waendao mavumbini watapiga magoti mbele yake, wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao. $$ PSA 22:30 Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana. $$ PSA 22:31 Watatangaza haki yake kwa watu ambao hawajazaliwa bado, kwa maana yeye ametenda hili. Zaburi 23 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 23:1 Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. $$ PSA 23:2 Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, $$ PSA 23:3 hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. $$ PSA 23:4 Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji. $$ PSA 23:5 Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika. $$ PSA 23:6 Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. Zaburi 24 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 24:1 Dunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake, ulimwengu, na wote waishio ndani yake, $$ PSA 24:2 maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji. $$ PSA 24:3 Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake? $$ PSA 24:4 Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo. $$ PSA 24:5 Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake. $$ PSA 24:6 Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao, wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. $$ PSA 24:7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, inukeni enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia. $$ PSA 24:8 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Ni Bwana aliye na nguvu na uweza, ni Bwana aliye hodari katika vita. $$ PSA 24:9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango, viinueni juu enyi milango ya kale, ili Mfalme wa utukufu apate kuingia. $$ PSA 24:10 Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? Ni Bwana Mwenye Nguvu Zote; yeye ndiye Mfalme wa utukufu. Zaburi 25 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 25:1 Kwako wewe, Ee Bwana, nainua nafsi yangu, $$ PSA 25:2 ni wewe ninayekutumainia, Ee Mungu wangu. Usiniache niaibike, wala usiache adui zangu wakanishinda. $$ PSA 25:3 Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea atakayeaibishwa, bali wataaibishwa wafanyao hila bila sababu. $$ PSA 25:4 Nionyeshe njia zako, Ee Bwana, nifundishe mapito yako, $$ PSA 25:5 niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote. $$ PSA 25:6 Kumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo, kwa maana zimekuwepo tangu zamani. $$ PSA 25:7 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala njia zangu za uasi, sawasawa na upendo wako unikumbuke, kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana. $$ PSA 25:8 Bwana ni mwema na mwenye adili, kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake. $$ PSA 25:9 Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake. $$ PSA 25:10 Njia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake. $$ PSA 25:11 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. $$ PSA 25:12 Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana? Atamfundisha katika njia atakayoichagua kwa ajili yake. $$ PSA 25:13 Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi. $$ PSA 25:14 Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, yeye huwajulisha agano lake. $$ PSA 25:15 Macho yangu humwelekea Bwana daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego. $$ PSA 25:16 Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka. $$ PSA 25:17 Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu. $$ PSA 25:18 Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote. $$ PSA 25:19 Tazama adui zangu walivyo wengi, pia uone jinsi wanavyonichukia vikali! $$ PSA 25:20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe, usiniache niaibike, kwa maana nimekukimbilia wewe. $$ PSA 25:21 Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako. $$ PSA 25:22 Ee Mungu, wakomboe Israeli, katika shida zao zote! Zaburi 26 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 26:1 Ee Bwana, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Bwana bila kusitasita. $$ PSA 26:2 Ee Bwana, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu; $$ PSA 26:3 kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako. $$ PSA 26:4 Siketi pamoja na watu wadanganyifu, wala siandamani na wanafiki, $$ PSA 26:5 ninachukia kusanyiko la watenda mabaya na ninakataa kuketi pamoja na waovu. $$ PSA 26:6 Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia, naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana, $$ PSA 26:7 nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa, huku nikisimulia matendo yako ya ajabu. $$ PSA 26:8 Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi, mahali ambapo utukufu wako hukaa. $$ PSA 26:9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi, wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu, $$ PSA 26:10 ambao mikononi mwao kuna mipango miovu, ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa. $$ PSA 26:11 Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; nikomboe na unihurumie. $$ PSA 26:12 Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare; katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana. Zaburi 27 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 27:1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani? $$ PSA 27:2 Waovu watakaposogea dhidi yangu ili wanile nyama yangu, adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia, watajikwaa na kuanguka. $$ PSA 27:3 Hata jeshi linizunguke pande zote, moyo wangu hautaogopa; hata vita vitokee dhidi yangu, hata hapo nitakuwa na ujasiri. $$ PSA 27:4 Jambo moja ninamwomba Bwana, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana na kumtafuta hekaluni mwake. $$ PSA 27:5 Kwa kuwa siku ya shida, atanihifadhi salama katika maskani yake, atanificha uvulini mwa hema yake na kuniweka juu kwenye mwamba. $$ PSA 27:6 Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia Bwana na kumsifu. $$ PSA 27:7 Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana, unihurumie na unijibu. $$ PSA 27:8 Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, Bwana “Nitautafuta.” $$ PSA 27:9 Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa hasira; wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu. $$ PSA 27:10 Hata kama baba yangu na mama wakiniacha, Bwana atanipokea. $$ PSA 27:11 Nifundishe njia yako, Ee Bwana, niongoze katika njia iliyonyooka kwa sababu ya watesi wangu. $$ PSA 27:12 Usiniachilie kwa nia za adui zangu, kwa maana mashahidi wa uongo wameinuka dhidi yangu, wakipumua ujeuri. $$ PSA 27:13 Nami bado nina tumaini hili: nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai. $$ PSA 27:14 Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana. Zaburi 28 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 28:1 Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni. $$ PSA 28:2 Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako. $$ PSA 28:3 Usiniburute pamoja na waovu, pamoja na hao watendao mabaya, ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri, lakini mioyoni mwao wameficha chuki. $$ PSA 28:4 Walipe sawasawa na matendo yao, sawasawa na matendo yao maovu; walipe sawasawa na kazi za mikono yao, uwalipe wanavyostahili. $$ PSA 28:5 Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana, na yale ambayo mikono yake imetenda, atawabomoa na kamwe hatawajenga tena. $$ PSA 28:6 Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie. $$ PSA 28:7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo. $$ PSA 28:8 Bwana ni nguvu ya watu wake, ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake. $$ PSA 28:9 Waokoe watu wako na uubariki urithi wako; uwe mchungaji wao na uwabebe milele. Zaburi 29 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 29:1 Mpeni Bwana, enyi mashujaa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. $$ PSA 29:2 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake. $$ PSA 29:3 Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu. $$ PSA 29:4 Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu. $$ PSA 29:5 Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni. $$ PSA 29:6 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, Sirioni urukaruke kama mwana nyati. $$ PSA 29:7 Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi. $$ PSA 29:8 Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi. $$ PSA 29:9 Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!” $$ PSA 29:10 Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele. $$ PSA 29:11 Bwana huwapa watu wake nguvu; Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani. Zaburi 30 Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 30:1 Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu. $$ PSA 30:2 Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. $$ PSA 30:3 Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. $$ PSA 30:4 Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu. $$ PSA 30:5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha. $$ PSA 30:6 Nilipofanikiwa nilisema, “Sitatikiswa kamwe.” $$ PSA 30:7 Ee Bwana, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika. $$ PSA 30:8 Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, kwa Bwana niliomba rehema: $$ PSA 30:9 “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako? $$ PSA 30:10 Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, Ee Bwana, uwe msaada wangu.” $$ PSA 30:11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe, $$ PSA 30:12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele. Zaburi 31 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 31:1 Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe. $$ PSA 31:2 Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka; uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa. $$ PSA 31:3 Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako. $$ PSA 31:4 Uniepushe na mtego niliotegewa, maana wewe ndiwe kimbilio langu. $$ PSA 31:5 Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli. $$ PSA 31:6 Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili; mimi ninamtumaini Bwana. $$ PSA 31:7 Nitafurahia na kushangilia upendo wako, kwa kuwa uliona mateso yangu na ulijua maumivu ya nafsi yangu. $$ PSA 31:8 Hukunikabidhi kwa adui yangu bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi. $$ PSA 31:9 Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; macho yangu yanafifia kwa huzuni, nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko. $$ PSA 31:10 Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa. $$ PSA 31:11 Kwa sababu ya adui zangu wote, nimedharauliwa kabisa na jirani zangu, hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, wale wanionao barabarani hunikimbia. $$ PSA 31:12 Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa, nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika. $$ PSA 31:13 Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua. $$ PSA 31:14 Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana; nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” $$ PSA 31:15 Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, uniokoe mikononi mwa adui zangu na wale wanifuatiao. $$ PSA 31:16 Mwangazie mtumishi wako uso wako, uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma. $$ PSA 31:17 Usiniache niaibike, Ee Bwana, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu. $$ PSA 31:18 Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, kwa maana kwa kiburi na dharau wao husema kwa majivuno dhidi ya wenye haki. $$ PSA 31:19 Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako, uliowawekea akiba wakuchao, ambao huwapa wale wakukimbiliao machoni pa watu. $$ PSA 31:20 Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako kutokana na hila za wanadamu; katika makao yako huwaweka salama kutokana na ndimi za mashtaka. $$ PSA 31:21 Atukuzwe Bwana, kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu nilipokuwa katika mji uliozingirwa. $$ PSA 31:22 Katika hofu yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie. $$ PSA 31:23 Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote! Bwana huwahifadhi waaminifu, lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu. $$ PSA 31:24 Kuweni hodari na mjipe moyo, ninyi nyote mnaomtumaini Bwana. Zaburi 32 Zaburi ya Daudi. Funzo. $$ PSA 32:1 Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa. $$ PSA 32:2 Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi, na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu. $$ PSA 32:3 Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa. $$ PSA 32:4 Usiku na mchana mkono wako ulinilemea, nguvu zangu zilinyonywa kama vile katika joto la kiangazi. $$ PSA 32:5 Kisha nilikujulisha dhambi yangu wala sikuficha uovu wangu. Nilisema, “Nitaungama makosa yangu kwa Bwana.” Ndipo uliponisamehe hatia ya dhambi yangu. $$ PSA 32:6 Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe wakati unapopatikana, hakika maji makuu yatakapofurika hayatamfikia yeye. $$ PSA 32:7 Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, utaniepusha na taabu na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu. $$ PSA 32:8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri na kukuangalia. $$ PSA 32:9 Usiwe kama farasi au nyumbu wasio na akili, ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu la sivyo hawatakukaribia. $$ PSA 32:10 Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa Bwana unamzunguka mtu anayemtumaini. $$ PSA 32:11 Shangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki! Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo! Zaburi 33 $$ PSA 33:1 Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki; kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. $$ PSA 33:2 Msifuni Bwana kwa kinubi, mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi. $$ PSA 33:3 Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe. $$ PSA 33:4 Maana neno la Bwana ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo. $$ PSA 33:5 Bwana hupenda uadilifu na haki; dunia imejaa upendo wake usiokoma. $$ PSA 33:6 Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa, jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake. $$ PSA 33:7 Ameyakusanya maji ya bahari kama kwenye chungu; vilindi vya bahari ameviweka katika ghala. $$ PSA 33:8 Dunia yote na imwogope Bwana, watu wote wa dunia wamche. $$ PSA 33:9 Kwa maana Mungu alisema, na ikawa, aliamuru na ikasimama imara. $$ PSA 33:10 Bwana huzuia mipango ya mataifa, hupinga makusudi ya mataifa. $$ PSA 33:11 Lakini mipango ya Bwana inasimama imara milele, makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote. $$ PSA 33:12 Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake. $$ PSA 33:13 Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini na kuwaona wanadamu wote; $$ PSA 33:14 kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani: $$ PSA 33:15 yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda. $$ PSA 33:16 Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake; hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake. $$ PSA 33:17 Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu, licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa. $$ PSA 33:18 Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo, $$ PSA 33:19 ili awaokoe na mauti, na kuwahifadhi wakati wa njaa. $$ PSA 33:20 Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu. $$ PSA 33:21 Mioyo yetu humshangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu. $$ PSA 33:22 Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana, tunapoliweka tumaini letu kwako. Zaburi 34 Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. $$ PSA 34:1 Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote. $$ PSA 34:2 Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi. $$ PSA 34:3 Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja. $$ PSA 34:4 Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. $$ PSA 34:5 Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. $$ PSA 34:6 Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote. $$ PSA 34:7 Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa. $$ PSA 34:8 Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia. $$ PSA 34:9 Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote. $$ PSA 34:10 Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema. $$ PSA 34:11 Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana. $$ PSA 34:12 Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema, $$ PSA 34:13 basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo. $$ PSA 34:14 Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia. $$ PSA 34:15 Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao. $$ PSA 34:16 Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, ili kufuta kumbukumbu lao duniani. $$ PSA 34:17 Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote. $$ PSA 34:18 Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho. $$ PSA 34:19 Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote, $$ PSA 34:20 huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika. $$ PSA 34:21 Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa. $$ PSA 34:22 Bwana huwakomboa watumishi wake, yeyote anayemkimbilia yeye hatahukumiwa kamwe. Zaburi 35 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 35:1 Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami, upigane na hao wanaopigana nami. $$ PSA 35:2 Chukua ngao na kigao. Inuka unisaidie. $$ PSA 35:3 Inua mkuki wako na fumo lako dhidi ya hao wanaonifuatia. Iambie nafsi yangu, “Mimi ni wokovu wako.” $$ PSA 35:4 Wafedheheshwe na waaibishwe wale wanaotafuta uhai wangu. Wanaofanya shauri kuniangamiza warudishwe nyuma kwa hofu. $$ PSA 35:5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo, malaika wa Bwana akiwafukuza. $$ PSA 35:6 Njia yao na iwe giza na ya utelezi, malaika wa Bwana akiwafuatilia. $$ PSA 35:7 Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu, na bila sababu wamenichimbia shimo, $$ PSA 35:8 maafa na yawapate ghafula: wavu walionifichia na uwatege wenyewe, na waanguke katika shimo hilo, kwa maangamizo yao. $$ PSA 35:9 Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana na kuufurahia wokovu wake. $$ PSA 35:10 Nitapaza sauti yangu nikisema, “Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana? Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao, maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!” $$ PSA 35:11 Mashahidi wakatili wanainuka, wananiuliza mambo nisiyoyajua. $$ PSA 35:12 Wananilipa baya kwa jema na kuiacha nafsi yangu ukiwa. $$ PSA 35:13 Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia na nikajinyenyekesha kwa kufunga. Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa, $$ PSA 35:14 niliendelea kuomboleza kama vile wao ni rafiki au ndugu. Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni kama ninayemwombolezea mama yangu. $$ PSA 35:15 Lakini nilipojikwaa, walikusanyika kwa shangwe; washambuliaji walijikusanya dhidi yangu bila mimi kujua. Walinisingizia pasipo kukoma. $$ PSA 35:16 Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki, wamenisagia meno. $$ PSA 35:17 Ee Bwana, utatazama mpaka lini? Niokoe maisha yangu na maangamizi yao, uhai wangu wa thamani kutokana na simba hawa. $$ PSA 35:18 Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, nitakusifu katikati ya watu wengi. $$ PSA 35:19 Usiwaache wale wanaonisimanga, wale ambao ni adui zangu bila sababu; usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu wakonyeze jicho kwa hila. $$ PSA 35:20 Hawazungumzi kwa amani, bali wanatunga mashtaka ya uongo dhidi ya wale wanaoishi kwa utulivu katika nchi. $$ PSA 35:21 Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha! Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.” $$ PSA 35:22 Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya. Usiwe mbali nami, Ee Bwana. $$ PSA 35:23 Amka, inuka unitetee! Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu. $$ PSA 35:24 Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu, sawasawa na haki yako; usiwaache wakusimange. $$ PSA 35:25 Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!” Au waseme, “Tumemmeza.” $$ PSA 35:26 Wote wanaofurahia dhiki yangu waaibishwe na wachanganyikiwe; hao wanaojiinua dhidi yangu wavikwe aibu na dharau. $$ PSA 35:27 Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “Bwana atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.” $$ PSA 35:28 Ulimi wangu utanena haki yako na sifa zako mchana kutwa. Zaburi 36 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana. $$ PSA 36:1 Kuna neno moyoni mwangu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. $$ PSA 36:2 Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. $$ PSA 36:3 Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema. $$ PSA 36:4 Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya. $$ PSA 36:5 Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga. $$ PSA 36:6 Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. $$ PSA 36:7 Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako. $$ PSA 36:8 Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. $$ PSA 36:9 Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru. $$ PSA 36:10 Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo. $$ PSA 36:11 Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, wala mkono wa mwovu usinifukuze. $$ PSA 36:12 Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka: wametupwa chini, hawawezi kuinuka! Zaburi 37 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 37:1 Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, wala usiwaonee wivu watendao mabaya, $$ PSA 37:2 kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara. $$ PSA 37:3 Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. $$ PSA 37:4 Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako. $$ PSA 37:5 Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili: $$ PSA 37:6 Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri. $$ PSA 37:7 Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu. $$ PSA 37:8 Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu. $$ PSA 37:9 Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi. $$ PSA 37:10 Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana, ingawa utawatafuta, hawataonekana. $$ PSA 37:11 Bali wanyenyekevu watairithi nchi na wafurahie amani tele. $$ PSA 37:12 Waovu hula njama dhidi ya wenye haki na kuwasagia meno, $$ PSA 37:13 bali Bwana huwacheka waovu, kwa sababu anajua siku yao inakuja. $$ PSA 37:14 Waovu huchomoa upanga na kupinda upinde, ili wawaangushe maskini na wahitaji, kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu. $$ PSA 37:15 Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe, na pinde zao zitavunjwa. $$ PSA 37:16 Bora kidogo walicho nacho wenye haki kuliko wingi wa mali wa waovu wengi; $$ PSA 37:17 kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini Bwana humtegemeza mwenye haki. $$ PSA 37:18 Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele. $$ PSA 37:19 Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. $$ PSA 37:20 Lakini waovu wataangamia: Adui za Bwana watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi. $$ PSA 37:21 Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu. $$ PSA 37:22 Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali. $$ PSA 37:23 Kama Bwana akipendezwa na njia ya mtu, yeye huimarisha hatua zake, $$ PSA 37:24 ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana Bwana humtegemeza kwa mkono wake. $$ PSA 37:25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula. $$ PSA 37:26 Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. Watoto wao watabarikiwa. $$ PSA 37:27 Acha ubaya na utende wema, nawe utaishi katika nchi milele. $$ PSA 37:28 Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki naye hatawaacha waaminifu wake. Watalindwa milele, lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali. $$ PSA 37:29 Wenye haki watairithi nchi, na kuishi humo milele. $$ PSA 37:30 Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima, nao ulimi wake huzungumza lililo haki. $$ PSA 37:31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; nyayo zake hazitelezi. $$ PSA 37:32 Watu waovu huvizia wenye haki, wakitafuta kuwaua; $$ PSA 37:33 lakini Bwana hatawaacha mikononi mwao wala hatawaacha wahukumiwe kuwa wakosa wanaposhtakiwa. $$ PSA 37:34 Mngojee Bwana, na uishike njia yake. Naye atakutukuza uirithi nchi, waovu watakapokatiliwa mbali, utaliona hilo. $$ PSA 37:35 Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi kama mwerezi wa Lebanoni, $$ PSA 37:36 lakini alitoweka mara na hakuonekana, ingawa nilimtafuta, hakupatikana. $$ PSA 37:37 Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani. $$ PSA 37:38 Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa, mafanikio yao yatakatiliwa mbali. $$ PSA 37:39 Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana, yeye ni ngome yao wakati wa shida. $$ PSA 37:40 Bwana huwasaidia na kuwaokoa, huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, kwa maana wanamkimbilia. Zaburi 38 Zaburi ya Daudi. Maombi. $$ PSA 38:1 Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. $$ PSA 38:2 Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia. $$ PSA 38:3 Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu. $$ PSA 38:4 Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika. $$ PSA 38:5 Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. $$ PSA 38:6 Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. $$ PSA 38:7 Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu. $$ PSA 38:8 Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. $$ PSA 38:9 Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako. $$ PSA 38:10 Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza. $$ PSA 38:11 Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani zangu wanakaa mbali nami. $$ PSA 38:12 Wale wanaotafuta uhai wangu wanatega mitego yao, wale ambao wangetaka kunidhuru huongea juu ya maangamizi yangu; hufanya shauri la hila mchana kutwa. $$ PSA 38:13 Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia, ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake, $$ PSA 38:14 nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu. $$ PSA 38:15 Ee Bwana, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu. $$ PSA 38:16 Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.” $$ PSA 38:17 Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote. $$ PSA 38:18 Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu. $$ PSA 38:19 Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari, wale wanaonichukia bila sababu ni wengi. $$ PSA 38:20 Wanaolipa maovu kwa wema wangu hunisingizia ninapofuata lililo jema. $$ PSA 38:21 Ee Bwana, usiniache, usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu. $$ PSA 38:22 Ee Bwana Mwokozi wangu, uje upesi kunisaidia. Zaburi 39 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 39:1 Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” $$ PSA 39:2 Lakini niliponyamaza kimya na kutulia, hata pasipo kusema lolote jema, uchungu wangu uliongezeka. $$ PSA 39:3 Moyo wangu ulipata moto ndani yangu, nilipotafakari, moto uliwaka, ndipo nikasema kwa ulimi wangu: $$ PSA 39:4 “Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu na hesabu ya siku zangu; nijalie kujua jinsi maisha yangu yanavyopita upesi. $$ PSA 39:5 Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi. $$ PSA 39:6 Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi. $$ PSA 39:7 “Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako. $$ PSA 39:8 Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu. $$ PSA 39:9 Nilinyamaza kimya, sikufumbua kinywa changu, kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili. $$ PSA 39:10 Niondolee mjeledi wako, nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako. $$ PSA 39:11 Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu. $$ PSA 39:12 “Ee Bwana, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote, $$ PSA 39:13 Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena kabla sijaondoka na nisiwepo tena.” Zaburi 40 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 40:1 Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu. $$ PSA 40:2 Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama. $$ PSA 40:3 Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa na kuweka tumaini lao kwa Bwana. $$ PSA 40:4 Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo. $$ PSA 40:5 Ee Bwana Mungu wangu, umefanya mambo mengi ya ajabu. Mambo uliyopanga kwa ajili yetu hakuna awezaye kukuhesabia; kama ningesema na kuyaelezea, yangekuwa mengi mno kuyaelezea. $$ PSA 40:6 Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu; sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji. $$ PSA 40:7 Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu. $$ PSA 40:8 Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” $$ PSA 40:9 Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee Bwana, kama ujuavyo. $$ PSA 40:10 Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa. $$ PSA 40:11 Ee Bwana, usizuilie huruma zako, upendo wako na kweli yako daima vinilinde. $$ PSA 40:12 Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka, dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, nao moyo unazimia ndani yangu. $$ PSA 40:13 Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie. $$ PSA 40:14 Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu. $$ PSA 40:15 Wale waniambiao, “Aha! Aha!” wafadhaishwe na iwe aibu yao. $$ PSA 40:16 Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Bwana atukuzwe!” $$ PSA 40:17 Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Bwana na anifikirie. Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu; Ee Mungu wangu, usikawie. Zaburi 41 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 41:1 Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida. $$ PSA 41:2 Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, atambariki katika nchi na hatamwacha katika tamaa ya adui zake. $$ PSA 41:3 Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake. $$ PSA 41:4 Nilisema, “Ee Bwana nihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.” $$ PSA 41:5 Adui zangu wanasema kwa hila, “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.” $$ PSA 41:6 Kila anapokuja mtu kunitazama, huzungumza uongo, huku moyo wake hukusanya masingizio; kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko. $$ PSA 41:7 Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu, hao huniwazia mabaya sana, wakisema, $$ PSA 41:8 “Ugonjwa mbaya sana umempata, kamwe hatainuka tena kitandani mwake.” $$ PSA 41:9 Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, yule aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake. $$ PSA 41:10 Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie, ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi. $$ PSA 41:11 Najua kwamba wapendezwa nami, kwa kuwa adui yangu hanishindi. $$ PSA 41:12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele. $$ PSA 41:13 Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Amen na Amen. (Zaburi 42–72) Zaburi 42 Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. $$ PSA 42:1 Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. $$ PSA 42:2 Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? $$ PSA 42:3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu usiku na mchana, huku watu wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” $$ PSA 42:4 Mambo haya nayakumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati uliosherehekea. $$ PSA 42:5 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na $$ PSA 42:6 Mungu wangu. Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; kwa hiyo nitakukumbuka kutoka nchi ya Yordani, katika vilele vya Hermoni, kutoka Mlima Mizari. $$ PSA 42:7 Kilindi huita kilindi, katika ngurumo za maporomoko ya maji yako; mawimbi yako yote pamoja na viwimbi vimepita juu yangu. $$ PSA 42:8 Mchana Bwana huelekeza upendo wake, usiku wimbo wake uko nami: maombi kwa Mungu wa uzima wangu. $$ PSA 42:9 Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, “Kwa nini umenisahau? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiwa nimeonewa na adui?” $$ PSA 42:10 Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali adui zangu wanaponidhihaki, wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” $$ PSA 42:11 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na Mungu wangu. Zaburi 43 $$ PSA 43:1 Ee Mungu unihukumu, nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu, niokoe na watu wadanganyifu na waovu. $$ PSA 43:2 Wewe ni Mungu ngome yangu. Kwa nini umenikataa? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiwa nimeonewa na adui? $$ PSA 43:3 Tuma hima nuru yako na kweli yako na viniongoze; vinilete mpaka mlima wako mtakatifu, mpaka mahali unapoishi. $$ PSA 43:4 Ndipo nitakwenda madhabahuni pa Mungu, kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu. Nitakusifu kwa kinubi, Ee Mungu, Mungu wangu. $$ PSA 43:5 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu Mwokozi wangu na Mungu wangu. Zaburi 44 Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. $$ PSA 44:1 Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametueleza yale uliyotenda katika siku zao, siku za kale. $$ PSA 44:2 Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu. $$ PSA 44:3 Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda. $$ PSA 44:4 Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo. $$ PSA 44:5 Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu. $$ PSA 44:6 Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi; $$ PSA 44:7 bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, unawaaibisha watesi wetu. $$ PSA 44:8 Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, nasi tutalisifu jina lako milele. $$ PSA 44:9 Lakini sasa umetukataa na kutudhili, wala huendi tena na jeshi letu. $$ PSA 44:10 Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui, nao watesi wetu wametuteka nyara. $$ PSA 44:11 Umetuacha tutafunwe kama kondoo na umetutawanya katika mataifa. $$ PSA 44:12 Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao. $$ PSA 44:13 Umetufanya lawama kwa jirani zetu, dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka. $$ PSA 44:14 Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa, mataifa hutikisa vichwa vyao. $$ PSA 44:15 Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, na uso wangu umejaa aibu tele, $$ PSA 44:16 kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi. $$ PSA 44:17 Hayo yote yametutokea, ingawa tulikuwa hatujakusahau wala hatujaenda kinyume na agano lako. $$ PSA 44:18 Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako. $$ PSA 44:19 Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, na ukatufunika kwa giza nene. $$ PSA 44:20 Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni, $$ PSA 44:21 je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo? $$ PSA 44:22 Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. $$ PSA 44:23 Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? Zinduka! Usitukatae milele. $$ PSA 44:24 Kwa nini unauficha uso wako na kusahau taabu na mateso yetu? $$ PSA 44:25 Tumeshushwa hadi mavumbini, miili yetu imegandamana na ardhi. $$ PSA 44:26 Inuka na utusaidie, utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho. Zaburi 45 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi.” Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi. $$ PSA 45:1 Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi. $$ PSA 45:2 Wewe ni bora kuliko watu wengine wote na midomo yako imepakwa neema, kwa kuwa Mungu amekubariki milele. $$ PSA 45:3 Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, jivike fahari na utukufu. $$ PSA 45:4 Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi, kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki, mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha. $$ PSA 45:5 Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme, mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako. $$ PSA 45:6 Ee Mungu, kiti chako cha enzi kitadumu milele na milele, fimbo ya utawala wa haki itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako. $$ PSA 45:7 Unaipenda haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako, kwa kukupaka mafuta ya furaha. $$ PSA 45:8 Mavazi yako yote yana harufu nzuri ya manemane, udi na mdalasini; kutoka kwenye majumba ya kifalme yaliyopambwa kwa pembe za ndovu, sauti za vinanda vya nyuzi zinakufanya ufurahi. $$ PSA 45:9 Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa; kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri. $$ PSA 45:10 Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio: Sahau watu wako na nyumba ya baba yako. $$ PSA 45:11 Mfalme ameshangazwa na uzuri wako; mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako. $$ PSA 45:12 Binti wa Tiro atakuletea zawadi, watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako. $$ PSA 45:13 Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake; vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. $$ PSA 45:14 Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, mabikira wenzake wanamfuata na wanaletwa kwako. $$ PSA 45:15 Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, na kuingia katika jumba la mfalme. $$ PSA 45:16 Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, mtawafanya wakuu katika nchi yote. $$ PSA 45:17 Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote, kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele. Zaburi 46 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi. $$ PSA 46:1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. $$ PSA 46:2 Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari. $$ PSA 46:3 Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake. $$ PSA 46:4 Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. $$ PSA 46:5 Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema. $$ PSA 46:6 Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka. $$ PSA 46:7 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. $$ PSA 46:8 Njooni mkaone kazi za Bwana jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. $$ PSA 46:9 Anakomesha vita hata miisho ya dunia, anakata upinde na kuvunjavunja mkuki, anateketeza ngao kwa moto. $$ PSA 46:10 “Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu; nitatukuzwa katikati ya mataifa, nitatukuzwa katika dunia.” $$ PSA 46:11 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. Zaburi 47 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. $$ PSA 47:1 Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe! $$ PSA 47:2 Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote! $$ PSA 47:3 Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu. $$ PSA 47:4 Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda. $$ PSA 47:5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti za tarumbeta. $$ PSA 47:6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. $$ PSA 47:7 Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. $$ PSA 47:8 Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu. $$ PSA 47:9 Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana. Zaburi 48 Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. $$ PSA 48:1 Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu. $$ PSA 48:2 Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, furaha ya dunia yote. Kama vilele vya juu sana vya Safoni ni Mlima Sayuni, mji wa Mfalme Mkuu. $$ PSA 48:3 Mungu yuko katika ngome zake; amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake. $$ PSA 48:4 Wakati wafalme walipounganisha nguvu, waliposonga mbele pamoja, $$ PSA 48:5 walimwona nao wakashangaa, wakakimbia kwa hofu. $$ PSA 48:6 Kutetemeka kuliwashika huko, maumivu kama ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa. $$ PSA 48:7 Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi zilizovunjwa na upepo wa mashariki. $$ PSA 48:8 Kama tulivyokuwa tumesikia, ndivyo tulivyoona katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote, katika mji wa Mungu wetu: Mungu ataufanya uwe salama milele. $$ PSA 48:9 Ee Mungu, hekaluni mwako tunatafakari upendo wako usiokoma. $$ PSA 48:10 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, mkono wako wa kuume umejazwa na haki. $$ PSA 48:11 Mlima Sayuni unashangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako. $$ PSA 48:12 Tembeeni katika Sayuni, uzungukeni mji, hesabuni minara yake; $$ PSA 48:13 yatafakarini vyema maboma yake, angalieni ngome zake, ili mpate kusimulia habari zake kwa kizazi kijacho. $$ PSA 48:14 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; atakuwa kiongozi wetu hata mwisho. Zaburi 49 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. $$ PSA 49:1 Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii. $$ PSA 49:2 Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja: $$ PSA 49:3 Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu. $$ PSA 49:4 Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze: $$ PSA 49:5 Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka, $$ PSA 49:6 wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi? $$ PSA 49:7 Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake. $$ PSA 49:8 Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha, $$ PSA 49:9 ili kwamba aishi milele na asione uharibifu. $$ PSA 49:10 Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao. $$ PSA 49:11 Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao. $$ PSA 49:12 Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye. $$ PSA 49:13 Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao. $$ PSA 49:14 Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. $$ PSA 49:15 Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake. $$ PSA 49:16 Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka, $$ PSA 49:17 kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye. $$ PSA 49:18 Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa, $$ PSA 49:19 atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima. $$ PSA 49:20 Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao. Zaburi 50 Zaburi ya Asafu. $$ PSA 50:1 Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana, asema na kuiita dunia, tangu mawio ya jua hadi mahali pake liendapo kutua. $$ PSA 50:2 Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, Mungu anaangaza. $$ PSA 50:3 Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali. $$ PSA 50:4 Anaziita mbingu zilizo juu, na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake: $$ PSA 50:5 “Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu, waliofanya agano nami kwa dhabihu.” $$ PSA 50:6 Nazo mbingu zinatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu. $$ PSA 50:7 “Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema, ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu: Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu. $$ PSA 50:8 Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, au sadaka zako za kuteketezwa, ambazo daima ziko mbele zangu. $$ PSA 50:9 Sina haja ya fahali wa banda lako, au mbuzi wa zizi lako. $$ PSA 50:10 Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. $$ PSA 50:11 Ninamjua kila ndege mlimani, nao viumbe wa kondeni ni wangu. $$ PSA 50:12 Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi, kwa maana ulimwengu ni wangu, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. $$ PSA 50:13 Je, mimi hula nyama ya mafahali au kunywa damu ya mbuzi? $$ PSA 50:14 Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana, $$ PSA 50:15 na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.” $$ PSA 50:16 ¶ Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: “Una haki gani kunena sheria zangu au kuchukua agano langu midomoni mwako? $$ PSA 50:17 Unachukia mafundisho yangu na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. $$ PSA 50:18 Unapomwona mwizi, unaungana naye, unapiga kura yako pamoja na wazinzi. $$ PSA 50:19 Unakitumia kinywa chako kwa mabaya na kuuongoza ulimi wako kwa hila. $$ PSA 50:20 Wanena daima dhidi ya ndugu yako na kumsingizia mwana wa mama yako. $$ PSA 50:21 Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya, ukafikiri Mimi nami ni kama wewe. Lakini nitakukemea na kuweka mashtaka mbele yako. $$ PSA 50:22 “Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu, ama sivyo nitawararua vipande vipande, wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwaokoa: $$ PSA 50:23 Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, naye aiandaa njia yake ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu.” Zaburi 51 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba. $$ PSA 51:1 Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu. $$ PSA 51:2 Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu. $$ PSA 51:3 Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima. $$ PSA 51:4 Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, na kuwa na haki utoapo hukumu. $$ PSA 51:5 Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu. $$ PSA 51:6 Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni, ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima. $$ PSA 51:7 Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. $$ PSA 51:8 Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi. $$ PSA 51:9 Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote. $$ PSA 51:10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. $$ PSA 51:11 Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu. $$ PSA 51:12 Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze. $$ PSA 51:13 Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe. $$ PSA 51:14 Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako. $$ PSA 51:15 Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako. $$ PSA 51:16 Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa. $$ PSA 51:17 Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau. $$ PSA 51:18 Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, ukazijenge upya kuta za Yerusalemu. $$ PSA 51:19 Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, pia mafahali watatolewa madhabahuni mwako. Zaburi 52 Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi amekwenda nyumbani kwa Ahimeleki.” $$ PSA 52:1 Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? Kwa nini unajivuna mchana kutwa, wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu? $$ PSA 52:2 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila. $$ PSA 52:3 Unapenda mabaya kuliko mema, uongo kuliko kusema kweli. $$ PSA 52:4 Unapenda kila neno lenye kudhuru, ewe ulimi wenye hila! $$ PSA 52:5 Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema yako, atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai. $$ PSA 52:6 Wenye haki wataona na kuogopa, watamcheka, wakisema, $$ PSA 52:7 “Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!” $$ PSA 52:8 Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni unaostawi katika nyumba ya Mungu, nautegemea upendo wa Mungu usiokoma milele na milele. $$ PSA 52:9 Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. Nitakusifu mbele ya watakatifu wako. Zaburi 53 (Zaburi 14) Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi. $$ PSA 53:1 Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema. $$ PSA 53:2 Mungu anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. $$ PSA 53:3 Kila mmoja amegeukia mbali, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja! $$ PSA 53:4 Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza: wale ambao huwala watu wangu kama watu walavyo mkate, hao ambao hawamwiti Mungu? $$ PSA 53:5 Hapo waliingiwa na hofu kuu, ambapo hapakuwa cha kutetemesha. Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia; uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau. $$ PSA 53:6 Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni! Wakati Mungu arejeshapo wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi! Zaburi 54 Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” $$ PSA 54:1 Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako. $$ PSA 54:2 Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu. $$ PSA 54:3 Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu. $$ PSA 54:4 Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza. $$ PSA 54:5 Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize. $$ PSA 54:6 Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema. $$ PSA 54:7 Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi. Zaburi 55 Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi. $$ PSA 55:1 Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, wala usidharau hoja yangu. $$ PSA 55:2 Nisikie na unijibu. Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa $$ PSA 55:3 kwa sauti ya adui, kwa kukaziwa macho na waovu, kwa sababu wananiletea mateso juu yangu na kunitukana kwa hasira zao. $$ PSA 55:4 Moyo wangu umejaa uchungu, hofu ya kifo imenishambulia. $$ PSA 55:5 Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha. $$ PSA 55:6 Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika. $$ PSA 55:7 Ningalitorokea mbali sana na kukaa jangwani, $$ PSA 55:8 ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, mbali na tufani kali na dhoruba.” $$ PSA 55:9 Ee Bwana, uwatahayarishe waovu na uwachanganyishie semi zao, maana nimeona jeuri na ugomvi mjini. $$ PSA 55:10 Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake, uovu na dhuluma vimo ndani yake. $$ PSA 55:11 Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini, vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake. $$ PSA 55:12 Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia, kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, ningejificha asinione. $$ PSA 55:13 Kumbe ni wewe, mwenzangu, mshiriki na rafiki yangu wa karibu, $$ PSA 55:14 ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri, tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu. $$ PSA 55:15 Kifo na kiwajie adui zangu ghafula, na washuke kuzimu wangali hai, kwa maana uovu upo ndani yao. $$ PSA 55:16 Lakini ninamwita Mungu, naye Bwana huniokoa. $$ PSA 55:17 Jioni, asubuhi na adhuhuri ninalia kwa huzuni, naye husikia sauti yangu. $$ PSA 55:18 Huniokoa nikawa salama katika vita vilivyopangwa dhidi yangu, ingawa watu wengi hunipinga. $$ PSA 55:19 Mungu anayemiliki milele, atawasikia na kuwaadhibu, watu ambao hawabadilishi njia zao, wala hawana hofu ya Mungu. $$ PSA 55:20 Mwenzangu hushambulia rafiki zake, naye huvunja agano lake. $$ PSA 55:21 Mazungumzo yake ni laini kama siagi, hata hivyo vita vimo moyoni mwake. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa. $$ PSA 55:22 Mtwike Bwana fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke. $$ PSA 55:23 Lakini wewe, Ee Mungu, utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, hawataishi nusu ya siku zao. Lakini mimi ninakutumaini wewe. Zaburi 56 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Njiwa mkimya wa mbali.” Utenzi wa Daudi. Baada ya kukamatwa na Wafilisti huko Gathi. $$ PSA 56:1 Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao. $$ PSA 56:2 Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa, wengi wananishambulia kwa kiburi chao. $$ PSA 56:3 Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe. $$ PSA 56:4 Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu apatikanaye na kufa, atanitenda nini? $$ PSA 56:5 Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, siku zote wanapanga shauri la kunidhuru. $$ PSA 56:6 Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu. $$ PSA 56:7 Wasiepuke kwa vyovyote, Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa. $$ PSA 56:8 Andika maombolezo yangu, orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako? $$ PSA 56:9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma ninapoita msaada. Kwa hili nitajua kwamba Mungu yuko upande wangu. $$ PSA 56:10 Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Bwana, ambaye neno lake ninalisifu, $$ PSA 56:11 katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? $$ PSA 56:12 Ee Mungu, nina nadhiri kwako, nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani. $$ PSA 56:13 Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili niweze kuenenda mbele za Mungu katika nuru ya uzima. Zaburi 57 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni. $$ PSA 57:1 Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite. $$ PSA 57:2 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. $$ PSA 57:3 Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. $$ PSA 57:4 Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali. $$ PSA 57:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. $$ PSA 57:6 Waliitegea miguu yangu nyavu, nikainamishwa chini na dhiki. Wamechimba shimo katika njia yangu, lakini wametumbukia humo wao wenyewe. $$ PSA 57:7 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. $$ PSA 57:8 Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. $$ PSA 57:9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. $$ PSA 57:10 Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, uaminifu wako unazifikia anga. $$ PSA 57:11 Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni, utukufu wako na uwe duniani pote. Zaburi 58 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. $$ PSA 58:1 Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki? Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu? $$ PSA 58:2 La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu, na mikono yenu hupima jeuri duniani. $$ PSA 58:3 Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao, toka tumboni mwa mama zao ni wakaidi na husema uongo. $$ PSA 58:4 Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake, $$ PSA 58:5 ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi, hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani. $$ PSA 58:6 Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao; Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba! $$ PSA 58:7 Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi, wavutapo pinde zao, mishale yao na iwe butu. $$ PSA 58:8 Kama konokono ayeyukavyo akitembea, kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu, wasilione jua. $$ PSA 58:9 Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba, zikiwa mbichi au kavu, waovu watakuwa wamefagiliwa mbali. $$ PSA 58:10 Wenye haki watafurahi waonapo wakilipizwa kisasi, watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu. $$ PSA 58:11 Ndipo wanadamu watasema, “Hakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu, hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.” Zaburi 59 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Wakati Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue. $$ PSA 59:1 Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. $$ PSA 59:2 Uniponye na watu watendao mabaya, uniokoe kutokana na wamwagao damu. $$ PSA 59:3 Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea wala kutenda dhambi. $$ PSA 59:4 Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia. Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya! $$ PSA 59:5 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli! Zinduka uyaadhibu mataifa yote, usionyeshe huruma kwa wasaliti. $$ PSA 59:6 Hurudi wakati wa jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. $$ PSA 59:7 Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao, hutema upanga kutoka midomo yao, nao husema, “Ni nani atakayetusikia?” $$ PSA 59:8 Lakini wewe, Bwana, uwacheke; unayadharau mataifa hayo yote. $$ PSA 59:9 Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, $$ PSA 59:10 Mungu wangu unipendaye. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwachekelee wale wanaonisingizia. $$ PSA 59:11 Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, au sivyo watu wangu watasahau. Katika uwezo wako wafanye watangetange na uwashushe chini. $$ PSA 59:12 Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, kwa ajili ya maneno ya midomo yao, waache wanaswe katika kiburi chao. Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka, $$ PSA 59:13 wateketeze katika ghadhabu, wateketeze hadi wasiwepo tena. Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo. $$ PSA 59:14 Hurudi jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. $$ PSA 59:15 Wanatangatanga wakitafuta chakula, wasipotosheka hubweka kama mbwa. $$ PSA 59:16 Lakini mimi nitaziimba nguvu zako, asubuhi nitaimba juu ya upendo wako; kwa maana wewe ndiwe ngome yangu na kimbilio langu wakati wa shida. $$ PSA 59:17 Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa. Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, Mungu unipendaye. Zaburi 60 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi.” Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Wakati alipopigana na Waaramu kutoka Aramu-Naharaimu na Aramu-Soba, naye Yoabu akarudi nyuma na kuwaua Waedomu 12,000 katika Bonde la Chumvi. $$ PSA 60:1 Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, umekasirika: sasa turejeshe upya! $$ PSA 60:2 Umetetemesha nchi na kuipasua; uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka. $$ PSA 60:3 Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa; umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha. $$ PSA 60:4 Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. $$ PSA 60:5 Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa. $$ PSA 60:6 Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi. $$ PSA 60:7 Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. $$ PSA 60:8 Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” $$ PSA 60:9 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? $$ PSA 60:10 Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? $$ PSA 60:11 Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. $$ PSA 60:12 Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu. Zaburi 61 Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 61:1 Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu. $$ PSA 61:2 Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi. $$ PSA 61:3 Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. $$ PSA 61:4 Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako. $$ PSA 61:5 Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako. $$ PSA 61:6 Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi. $$ PSA 61:7 Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde. $$ PSA 61:8 Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku. Zaburi 62 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 62:1 Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake. $$ PSA 62:2 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe. $$ PSA 62:3 Mtamshambulia mtu hata lini? Je, ninyi nyote mtamtupa chini, ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika? $$ PSA 62:4 Walikusudia kikamilifu kumwangusha toka mahali pake pa fahari; wanafurahia uongo. Kwa vinywa vyao hubariki, lakini ndani ya mioyo yao hulaani. $$ PSA 62:5 Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake. $$ PSA 62:6 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika. $$ PSA 62:7 Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, ndiye mwamba wangu wenye nguvu na kimbilio langu. $$ PSA 62:8 Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, miminieni mioyo yenu kwake, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu. $$ PSA 62:9 Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu, nao wa ngazi ya juu ni uongo tu; wakipimwa kwenye mizani, si chochote; wote kwa pamoja ni pumzi tu. $$ PSA 62:10 Usitumainie vya udhalimu wala usijivune kwa vitu vya wizi; ingawa utajiri wako utaongezeka, usiviwekee moyo wako. $$ PSA 62:11 Jambo moja Mungu amelisema, mambo mawili nimeyasikia: kwamba, Ee Mungu, wewe una nguvu, $$ PSA 62:12 na kwamba, Ee Bwana, wewe ni mwenye upendo. Hakika utampa kila mtu thawabu kwa kadiri ya alivyotenda. Zaburi 63 Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda. $$ PSA 63:1 Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji. $$ PSA 63:2 Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako. $$ PSA 63:3 Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha. $$ PSA 63:4 Nitakusifu siku zote za maisha yangu, na kwa jina lako nitainua mikono yangu. $$ PSA 63:5 Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe. $$ PSA 63:6 Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku. $$ PSA 63:7 Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba. $$ PSA 63:8 Nafsi yangu inaambatana nawe, mkono wako wa kuume hunishika. $$ PSA 63:9 Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa, watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia. $$ PSA 63:10 Watatolewa wafe kwa upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha. $$ PSA 63:11 Bali mfalme atafurahi katika Mungu, wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu, bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa. Zaburi 64 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 64:1 Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu, uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui. $$ PSA 64:2 Unifiche kutokana na shauri la siri la waovu, kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya. $$ PSA 64:3 Wananoa ndimi zao kama panga na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha. $$ PSA 64:4 Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga. $$ PSA 64:5 Kila mmoja humtia moyo mwenzake katika mipango mibaya; huzungumza juu ya kuficha mitego yao, nao husema, “Ni nani ataiona?” $$ PSA 64:6 Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema, “Tumebuni mpango mkamilifu!” Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila. $$ PSA 64:7 Bali Mungu atawapiga kwa mishale, nao ghafula wataangushwa. $$ PSA 64:8 Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao na kuwaleta kwenye maangamizi; wote wawaonao watatikisa vichwa vyao kwa dharau. $$ PSA 64:9 Wanadamu wote wataogopa, watatangaza kazi za Mungu na kutafakari yale aliyoyatenda. $$ PSA 64:10 Wenye haki na wafurahi katika Bwana, na wakimbilie kwake; wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye! Zaburi 65 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo. $$ PSA 65:1 Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa. $$ PSA 65:2 Ewe usikiaye maombi, kwako wewe watu wote watakuja. $$ PSA 65:3 Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu. $$ PSA 65:4 Heri wale uliowachagua na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako, mema ya Hekalu lako takatifu. $$ PSA 65:5 Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki, Ee Mungu Mwokozi wetu, tumaini la miisho yote ya duniani na la bahari zilizo mbali sana, $$ PSA 65:6 uliyeumba milima kwa uwezo wako, ukiwa umejivika nguvu, $$ PSA 65:7 uliyenyamazisha dhoruba za bahari, ngurumo za mawimbi yake, na ghasia za mataifa. $$ PSA 65:8 Wale wanaoishi mbali sana wanaogopa maajabu yako, kule asubuhi ipambazukiapo na kule jioni inakofifilia umeziita nyimbo za furaha. $$ PSA 65:9 Waitunza nchi na kuinyeshea, waitajirisha kwa wingi. Vijito vya Mungu vimejaa maji ili kuwapa watu nafaka, kwa maana wewe umeviamuru. $$ PSA 65:10 Umeilowesha mifereji yake na kusawazisha kingo zake; umeilainisha kwa manyunyu na kuibariki mimea yake. $$ PSA 65:11 Umeuvika mwaka taji ya baraka, magari yako yanafurika kwa wingi. $$ PSA 65:12 Mbuga za majani za jangwani umezineemesha; vilima vimevikwa furaha. $$ PSA 65:13 Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama, na mabonde yamepambwa kwa mavuno; vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba. Zaburi 66 Kwa mwimbishaji. Wimbo. Zaburi. $$ PSA 66:1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote! $$ PSA 66:2 Imbeni utukufu wa jina lake; mpeni sifa zake kwa utukufu! $$ PSA 66:3 Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako! Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba adui wananyenyekea mbele zako. $$ PSA 66:4 Dunia yote yakusujudia, wanakuimbia wewe sifa, wanaliimbia sifa jina lako.” $$ PSA 66:5 Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda, mambo ya kutisha aliyoyatenda miongoni mwa wanadamu! $$ PSA 66:6 Alifanya bahari kuwa nchi kavu, wakapita kati ya maji kwa miguu, njooni, tumshangilie. $$ PSA 66:7 Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, macho yake huangalia mataifa yote: waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake. $$ PSA 66:8 Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu, sauti ya sifa yake isikike, $$ PSA 66:9 ameyahifadhi maisha yetu na kuizuia miguu yetu kuteleza. $$ PSA 66:10 Ee Mungu, wewe ulitujaribu, ukatusafisha kama fedha. $$ PSA 66:11 Umetuingiza kwenye nyavu na umetubebesha mizigo mizito migongoni mwetu. $$ PSA 66:12 Uliwaruhusu watu watukalie vichwani, tulipita kwenye moto na kwenye maji, lakini ulituleta kwenye nchi iliyojaa utajiri tele. $$ PSA 66:13 Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa na kukutimizia nadhiri zangu: $$ PSA 66:14 nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi na nilizotamka kwa kinywa changu nilipokuwa katika shida. $$ PSA 66:15 Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono na sadaka za kondoo dume, nitakutolea mafahali na mbuzi. $$ PSA 66:16 Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu, nami niwaambie aliyonitendea. $$ PSA 66:17 Nilimlilia kwa kinywa changu, sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu. $$ PSA 66:18 Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, Bwana asingekuwa amenisikiliza; $$ PSA 66:19 lakini hakika Mungu amenisikiliza na amesikia sauti yangu katika maombi. $$ PSA 66:20 Sifa apewe Mungu, ambaye hakulikataa ombi langu wala kunizuilia upendo wake! Zaburi 67 Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. $$ PSA 67:1 Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake, $$ PSA 67:2 ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. $$ PSA 67:3 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. $$ PSA 67:4 Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. $$ PSA 67:5 Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. $$ PSA 67:6 Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. $$ PSA 67:7 Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye. Zaburi 68 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo. $$ PSA 68:1 Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike, adui zake na wakimbie mbele zake. $$ PSA 68:2 Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo, vivyo hivyo uwapeperushe mbali, kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto, vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu. $$ PSA 68:3 Bali wenye haki na wafurahi, washangilie mbele za Mungu, wafurahi na kushangilia. $$ PSA 68:4 Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu: jina lake ni Bwana, furahini mbele zake. $$ PSA 68:5 Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu. $$ PSA 68:6 Mungu huwaweka wapweke katika jamaa, huwaongoza wafungwa wakiimba, bali waasi huishi katika nchi kame. $$ PSA 68:7 Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako, ulipopita nyikani, $$ PSA 68:8 dunia ilitikisika, mbingu zikanyesha mvua, mbele za Mungu, Yule wa Sinai, mbele za Mungu, Mungu wa Israeli. $$ PSA 68:9 Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka. $$ PSA 68:10 Ee Mungu, watu wako waliishi huko, nawe kwa wingi wa utajiri wako uliwapa maskini mahitaji yao. $$ PSA 68:11 Bwana alitangaza neno, waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa: $$ PSA 68:12 “Wafalme na majeshi walikimbia upesi, watu waliobaki kambini waligawana nyara. $$ PSA 68:13 Hata ulalapo katikati ya mioto ya kambini, mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha, manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.” $$ PSA 68:14 Wakati Mwenyezi alipowatawanya wafalme katika nchi, ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni. $$ PSA 68:15 Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka, milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka. $$ PSA 68:16 Enyi milima yenye vilele vilivyochongoka, kwa nini mnakazia macho kwa wivu, katika mlima Mungu anaochagua kutawala, ambako Bwana mwenyewe ataishi milele? $$ PSA 68:17 Magari ya Mungu ni makumi ya maelfu, na maelfu ya maelfu; Bwana amekuja kutoka Sinai hadi katika patakatifu pake. $$ PSA 68:18 Ulipopanda juu, uliteka mateka, ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu, hata kutoka kwa wale walioasi, ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko. $$ PSA 68:19 Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. $$ PSA 68:20 Mungu wetu ni Mungu aokoaye, Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo. $$ PSA 68:21 Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi. $$ PSA 68:22 Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, $$ PSA 68:23 ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.” $$ PSA 68:24 Ee Mungu, maandamano yako yameonekana, maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, yakielekea patakatifu pake. $$ PSA 68:25 Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda, pamoja nao wako wanawali wakipiga matari. $$ PSA 68:26 Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli. $$ PSA 68:27 Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza, wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda, hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali. $$ PSA 68:28 Ee Mungu, amuru uwezo wako, Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako, kama ulivyofanya hapo awali. $$ PSA 68:29 Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu wafalme watakuletea zawadi. $$ PSA 68:30 Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi, kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa. Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. Tawanya mataifa yapendayo vita. $$ PSA 68:31 Wajumbe watakuja kutoka Misri, Kushi atajisalimisha kwa Mungu. $$ PSA 68:32 Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa, $$ PSA 68:33 mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu. $$ PSA 68:34 Tangazeni uwezo wa Mungu, ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, ambaye uwezo wake uko katika anga. $$ PSA 68:35 Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. Mungu Asifiwe! Zaburi 69 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi. $$ PSA 69:1 Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni. $$ PSA 69:2 Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga, Nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha. $$ PSA 69:3 Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu. $$ PSA 69:4 Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba. $$ PSA 69:5 Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako. $$ PSA 69:6 Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. $$ PSA 69:7 Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu. $$ PSA 69:8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. $$ PSA 69:9 Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia. $$ PSA 69:10 Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi. $$ PSA 69:11 Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau. $$ PSA 69:12 Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi. $$ PSA 69:13 Lakini Ee Bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika. $$ PSA 69:14 Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji. $$ PSA 69:15 Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu. $$ PSA 69:16 Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie. $$ PSA 69:17 Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. $$ PSA 69:18 Njoo karibu uniokoe, nikomboe kwa sababu ya adui zangu. $$ PSA 69:19 Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua. $$ PSA 69:20 Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata. $$ PSA 69:21 Waliweka nyongo katika chakula changu na walinipa siki nilipokuwa na kiu. $$ PSA 69:22 Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, nayo iwe upatilizo na tanzi. $$ PSA 69:23 Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima. $$ PSA 69:24 Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate. $$ PSA 69:25 Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao. $$ PSA 69:26 Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza. $$ PSA 69:27 Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako. $$ PSA 69:28 Wafutwe kutoka kitabu cha uzima na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki. $$ PSA 69:29 Mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi. $$ PSA 69:30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani. $$ PSA 69:31 Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. $$ PSA 69:32 Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi! $$ PSA 69:33 Bwana huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa. $$ PSA 69:34 Mbingu na dunia zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake, $$ PSA 69:35 kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, $$ PSA 69:36 watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo. Zaburi 70 (Zaburi 40:13-17) Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi. $$ PSA 70:1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie. $$ PSA 70:2 Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu. $$ PSA 70:3 Wale waniambiao, “Aha! Aha!” warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. $$ PSA 70:4 Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!” $$ PSA 70:5 Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Bwana, usikawie. Zaburi 71 $$ PSA 71:1 Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe. $$ PSA 71:2 Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe. $$ PSA 71:3 Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu. $$ PSA 71:4 Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili. $$ PSA 71:5 Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu. $$ PSA 71:6 Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima. $$ PSA 71:7 Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara. $$ PSA 71:8 Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa. $$ PSA 71:9 Usinitupe wakati wa uzee, wala usiniache nguvu zangu zinapopungua. $$ PSA 71:10 Kwa maana adui zangu wananisengenya, wale wanaonivizia kuniua wafanya hila. $$ PSA 71:11 Wanasema, “Mungu amemwacha, mkimbilieni mkamkamate, kwani hakuna wa kumwokoa.” $$ PSA 71:12 Ee Mungu, usiwe mbali nami, njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu. $$ PSA 71:13 Washtaki wangu na waangamie kwa aibu, wale wanaotaka kunidhuru na wafunikwe kwa dharau na fedheha. $$ PSA 71:14 Lakini mimi, nitatumaini siku zote, nitakusifu zaidi na zaidi. $$ PSA 71:15 Kinywa changu kitasimulia haki yako, wokovu wako mchana kutwa, ingawa sifahamu kipimo chake. $$ PSA 71:16 Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja na kutangaza matendo yako makuu, nitatangaza haki yako, yako peke yako. $$ PSA 71:17 Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu, hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu. $$ PSA 71:18 Ee Mungu, usiniache, hata niwapo mzee wa mvi, mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye. $$ PSA 71:19 Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu, wewe ambaye umefanya mambo makuu. Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe? $$ PSA 71:20 Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu, utanihuisha tena, kutoka vilindi vya dunia utaniinua tena. $$ PSA 71:21 Utaongeza heshima yangu na kunifariji tena. $$ PSA 71:22 Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako; Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, nitakuimbia sifa kwa zeze. $$ PSA 71:23 Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha ninapokuimbia sifa, mimi, ambaye umenikomboa. $$ PSA 71:24 Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki mchana kutwa, kwa maana wale waliotaka kunidhuru, wameaibishwa na kufadhaishwa. Zaburi 72 Zaburi ya Solomoni. $$ PSA 72:1 Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako. $$ PSA 72:2 Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki. $$ PSA 72:3 Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki. $$ PSA 72:4 Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu. $$ PSA 72:5 Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote. $$ PSA 72:6 Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi. $$ PSA 72:7 Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma. $$ PSA 72:8 Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia. $$ PSA 72:9 Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi. $$ PSA 72:10 Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi. $$ PSA 72:11 Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia. $$ PSA 72:12 Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia. $$ PSA 72:13 Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti. $$ PSA 72:14 Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake. $$ PSA 72:15 Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa. $$ PSA 72:16 Nafaka ijae tele katika nchi yote, juu ya vilele vya vilima na istawi. Tunda lake na listawi kama Lebanoni, listawi kama majani ya kondeni. $$ PSA 72:17 Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa. $$ PSA 72:18 Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu. $$ PSA 72:19 Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen. $$ PSA 72:20 Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese. (Zaburi 73–89) Zaburi 73 Zaburi ya Asafu. $$ PSA 73:1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale ambao mioyo yao ni safi. $$ PSA 73:2 Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama. $$ PSA 73:3 Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu. $$ PSA 73:4 Wao hawana taabu, miili yao ina afya na nguvu. $$ PSA 73:5 Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine. $$ PSA 73:6 Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri. $$ PSA 73:7 Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi, majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo. $$ PSA 73:8 Hudhihaki na kusema kwa ukorofi, katika majivuno yao wanatishia kutesa. $$ PSA 73:9 Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu, nazo ndimi zao humiliki duniani. $$ PSA 73:10 Kwa hiyo watu wao huwageukia na kunywa maji tele. $$ PSA 73:11 Wanasema, “Mungu awezaje kujua? Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?” $$ PSA 73:12 Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri. $$ PSA 73:13 Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia. $$ PSA 73:14 Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi. $$ PSA 73:15 Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako. $$ PSA 73:16 Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa. $$ PSA 73:17 Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao. $$ PSA 73:18 Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu. $$ PSA 73:19 Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho! $$ PSA 73:20 Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto. $$ PSA 73:21 Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu, $$ PSA 73:22 nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako. $$ PSA 73:23 Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume. $$ PSA 73:24 Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu. $$ PSA 73:25 Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe. $$ PSA 73:26 Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele. $$ PSA 73:27 Wale walio mbali nawe wataangamia, unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako. $$ PSA 73:28 Lakini kwangu mimi, ni vyema kuwa karibu na Mungu. Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu; nami nitayasimulia matendo yako yote. Zaburi 74 Utenzi wa Asafu. $$ PSA 74:1 Ee Mungu, mbona umetukataa milele? Mbona hasira yako inatoka moshi juu ya kondoo wa malisho yako? $$ PSA 74:2 Kumbuka watu uliowanunua zamani, kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: Mlima Sayuni, ambamo uliishi. $$ PSA 74:3 Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu. $$ PSA 74:4 Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi, wanaweka bendera zao kama alama. $$ PSA 74:5 Walifanya kama watu wanaotumia mashoka kukata kichaka cha miti. $$ PSA 74:6 Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa kwa mashoka na vishoka vyao. $$ PSA 74:7 Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu, wakayanajisi makao ya Jina lako. $$ PSA 74:8 Walisema mioyoni mwao, “Tutawaponda kabisa!” Walichoma kila mahali ambapo Mungu aliabudiwa katika nchi. $$ PSA 74:9 Hatukupewa ishara za miujiza; hakuna manabii waliobaki, hakuna yeyote kati yetu ajuaye hali hii itachukua muda gani. $$ PSA 74:10 Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? Je, adui watalitukana jina lako milele? $$ PSA 74:11 Kwa nini unazuia mkono wako, mkono wako wa kuume? Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako na uwaangamize! $$ PSA 74:12 Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani, unaleta wokovu duniani. $$ PSA 74:13 Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji. $$ PSA 74:14 Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani nawe ukamtoa kama chakula kwa viumbe vya jangwani. $$ PSA 74:15 Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito, ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima. $$ PSA 74:16 Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia, uliziweka jua na mwezi. $$ PSA 74:17 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, ulifanya kiangazi na masika. $$ PSA 74:18 Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki, jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako. $$ PSA 74:19 Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu; usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele. $$ PSA 74:20 Likumbuke agano lako, maana mara kwa mara mambo ya jeuri yamejaa katika sehemu za giza nchini. $$ PSA 74:21 Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu; maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako. $$ PSA 74:22 Inuka, Ee Mungu, ujitetee; kumbuka jinsi wapumbavu wanavyokudhihaki mchana kutwa. $$ PSA 74:23 Usipuuze makelele ya watesi wako, ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo. Zaburi 75 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo. $$ PSA 75:1 Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu. $$ PSA 75:2 Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki. $$ PSA 75:3 Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara. $$ PSA 75:4 Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu. $$ PSA 75:5 Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ” $$ PSA 75:6 Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu. $$ PSA 75:7 Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine. $$ PSA 75:8 Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho. $$ PSA 75:9 Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo. $$ PSA 75:10 Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu. Zaburi 76 Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo. $$ PSA 76:1 Katika Yuda, Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli. $$ PSA 76:2 Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni. $$ PSA 76:3 Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita. $$ PSA 76:4 Wewe unangʼaa kwa mwanga, mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori. $$ PSA 76:5 Mashujaa hulala wametekwa nyara, hulala usingizi wao wa mwisho; hakuna hata mmoja wa watu wa vita anayeweza kuinua mikono yake. $$ PSA 76:6 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, farasi na gari la vita vilikaa kimya. $$ PSA 76:7 Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa. Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika? $$ PSA 76:8 Kutoka mbinguni ulitamka hukumu, nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya: $$ PSA 76:9 wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi. $$ PSA 76:10 Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa, na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi. $$ PSA 76:11 Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza; nchi zote za jirani na walete zawadi kwa Yule astahiliye kuogopwa. $$ PSA 76:12 Huvunja roho za watawala; anaogopwa na wafalme wa dunia. Zaburi 77 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. $$ PSA 77:1 Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie. $$ PSA 77:2 Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika. $$ PSA 77:3 Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; nikatafakari, roho yangu ikadhoofika. $$ PSA 77:4 Ulizuia macho yangu kufumba; nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema. $$ PSA 77:5 Nilitafakari juu ya siku zilizopita, miaka mingi iliyopita, $$ PSA 77:6 nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. Moyo wangu ulitafakari na roho yangu ikauliza: $$ PSA 77:7 “Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena? $$ PSA 77:8 Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote? $$ PSA 77:9 Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?” $$ PSA 77:10 Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.” $$ PSA 77:11 Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. $$ PSA 77:12 Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu. $$ PSA 77:13 Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? $$ PSA 77:14 Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa. $$ PSA 77:15 Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu. $$ PSA 77:16 Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka. $$ PSA 77:17 Mawingu yalimwaga maji, mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, mishale yako ikametameta huku na huko. $$ PSA 77:18 Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, umeme wako wa radi ukaangaza dunia, nchi ikatetemeka na kutikisika. $$ PSA 77:19 Njia yako ilipita baharini, mapito yako kwenye maji makuu, ingawa nyayo zako hazikuonekana. $$ PSA 77:20 Uliongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Mose na Aroni. Zaburi 78 Utenzi wa Asafu. $$ PSA 78:1 Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu. $$ PSA 78:2 Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: $$ PSA 78:3 yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia. $$ PSA 78:4 Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. $$ PSA 78:5 Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao, $$ PSA 78:6 ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao. $$ PSA 78:7 Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake. $$ PSA 78:8 Ili wasifanane na baba zao, waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake, ambao roho zao hazikumwamini. $$ PSA 78:9 Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita. $$ PSA 78:10 Hawakulishika agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake. $$ PSA 78:11 Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonyesha. $$ PSA 78:12 Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, huko Soani, katika nchi ya Misri. $$ PSA 78:13 Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta. $$ PSA 78:14 Aliwaongoza kwa wingu mchana na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha. $$ PSA 78:15 Alipasua miamba jangwani na akawapa maji tele kama bahari, $$ PSA 78:16 alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka, akayafanya maji yatiririke kama mito. $$ PSA 78:17 Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana. $$ PSA 78:18 Kwa makusudi walimjaribu Mungu, wakidai vyakula walivyovitamani. $$ PSA 78:19 Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani? $$ PSA 78:20 Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, vijito vikatiririka maji mengi. Lakini je, aweza kutupa chakula pia? Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?” $$ PSA 78:21 Bwana alipowasikia, alikasirika sana, moto wake ukawa dhidi ya Yakobo, na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli, $$ PSA 78:22 kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake. $$ PSA 78:23 Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu na kufungua milango ya mbingu, $$ PSA 78:24 akawanyeshea mana ili watu wale; aliwapa nafaka ya mbinguni. $$ PSA 78:25 Watu walikula mkate wa malaika, akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula. $$ PSA 78:26 Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake. $$ PSA 78:27 Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, ndege warukao kama mchanga wa pwani. $$ PSA 78:28 Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, kuzunguka mahema yao yote. $$ PSA 78:29 Walikula na kusaza, kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani. $$ PSA 78:30 Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao, $$ PSA 78:31 hasira ya Mungu ikawaka juu yao, akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, akiwaangusha vijana wa Israeli. $$ PSA 78:32 Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini. $$ PSA 78:33 Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho. $$ PSA 78:34 Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku. $$ PSA 78:35 Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. $$ PSA 78:36 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, $$ PSA 78:37 mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. $$ PSA 78:38 Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote. $$ PSA 78:39 Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi. $$ PSA 78:40 Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani! $$ PSA 78:41 Walimjaribu Mungu mara kwa mara, wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. $$ PSA 78:42 Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi, $$ PSA 78:43 siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani. $$ PSA 78:44 Aligeuza mito yao kuwa damu, hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao. $$ PSA 78:45 Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, na vyura wakawaharibu. $$ PSA 78:46 Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige. $$ PSA 78:47 Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji. $$ PSA 78:48 Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi. $$ PSA 78:49 Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu. $$ PSA 78:50 Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni. $$ PSA 78:51 Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu. $$ PSA 78:52 Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani. $$ PSA 78:53 Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao. $$ PSA 78:54 Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa. $$ PSA 78:55 Aliyafukuza mataifa mbele yao, na kuwagawia nchi zao kama urithi, aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao. $$ PSA 78:56 Lakini wao walimjaribu Mungu, na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, wala hawakuzishika sheria zake. $$ PSA 78:57 Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu, wakawa wasioweza kutegemewa kama upinde wenye kasoro. $$ PSA 78:58 Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, wakachochea wivu wake kwa sanamu zao. $$ PSA 78:59 Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa. $$ PSA 78:60 Akaiacha hema ya Shilo, hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu. $$ PSA 78:61 Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui. $$ PSA 78:62 Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake. $$ PSA 78:63 Moto uliwaangamiza vijana wao, na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, $$ PSA 78:64 makuhani wao waliuawa kwa upanga, wala wajane wao hawakuweza kulia. $$ PSA 78:65 Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo. $$ PSA 78:66 Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele. $$ PSA 78:67 Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, hakulichagua kabila la Efraimu, $$ PSA 78:68 lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda. $$ PSA 78:69 Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele. $$ PSA 78:70 Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. $$ PSA 78:71 Kutoka kuchunga kondoo alimleta kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, wa Israeli urithi wake. $$ PSA 78:72 Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza. Zaburi 79 Zaburi ya Asafu. $$ PSA 79:1 Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako, wamelinajisi Hekalu lako takatifu, wameifanya Yerusalemu kuwa magofu. $$ PSA 79:2 Wametoa maiti za watumishi kuwa chakula cha ndege wa angani na nyama ya watakatifu wako kwa wanyama wa nchi. $$ PSA 79:3 Wamemwaga damu kama maji kuzunguka Yerusalemu yote, wala hakuna yeyote wa kuwazika. $$ PSA 79:4 Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu, cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. $$ PSA 79:5 Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele? Wivu wako utawaka kama moto hadi lini? $$ PSA 79:6 Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali, juu ya falme za hao wasioliitia jina lako, $$ PSA 79:7 kwa maana wamemrarua Yakobo na kuharibu nchi ya makao yake. $$ PSA 79:8 Usituhesabie dhambi za baba zetu, huruma yako na itujie hima, kwa maana tu wahitaji mno. $$ PSA 79:9 Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie, kwa ajili ya utukufu wa jina lako; tuokoe na kutusamehe dhambi zetu kwa ajili ya jina lako. $$ PSA 79:10 Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wenu?” Mbele ya macho yetu, dhihirisha kati ya mataifa kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa ya watumishi wako. $$ PSA 79:11 Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako; kwa nguvu za mkono wako hifadhi wale waliohukumiwa kufa. $$ PSA 79:12 Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwao aibu walizovurumisha juu yako, Ee Bwana. $$ PSA 79:13 Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako, tutakusifu milele; toka kizazi hadi kizazi tutasimulia sifa zako. Zaburi 80 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu. $$ PSA 80:1 Ee Mchungaji wa Israeli tusikie, wewe umwongozaye Yosefu kama kundi; wewe uketiye katika kiti cha enzi katikati ya makerubi, angaza $$ PSA 80:2 mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. Uamshe nguvu zako, uje utuokoe. $$ PSA 80:3 Ee Mungu, uturejeshe, utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa. $$ PSA 80:4 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi dhidi ya maombi ya watu wako? $$ PSA 80:5 Umewalisha kwa mkate wa machozi, umewafanya wanywe machozi bakuli tele. $$ PSA 80:6 Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu, na adui zetu wanatudhihaki. $$ PSA 80:7 Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, nasi tuweze kuokolewa. $$ PSA 80:8 Ulileta mzabibu kutoka Misri, ukawafukuza mataifa, ukaupanda. $$ PSA 80:9 Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi. $$ PSA 80:10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, matawi yake yakafunika mierezi mikubwa. $$ PSA 80:11 Matawi yake yalienea mpaka Baharini, machipukizi yake mpaka kwenye Mto. $$ PSA 80:12 Mbona umebomoa kuta zake ili wote wapitao karibu wazichume zabibu zake? $$ PSA 80:13 Nguruwe mwitu wanauharibu na wanyama wa kondeni hujilisha humo. $$ PSA 80:14 Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote! Tazama chini kutoka mbinguni na uone! Linda mzabibu huu, $$ PSA 80:15 mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, mwana uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe. $$ PSA 80:16 Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto, unapowakemea, watu wako huangamia. $$ PSA 80:17 Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume, mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe. $$ PSA 80:18 Ndipo hatutakuacha tena, utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako. $$ PSA 80:19 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa. Zaburi 81 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu. $$ PSA 81:1 Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! $$ PSA 81:2 Anzeni wimbo, pigeni matari, pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri. $$ PSA 81:3 Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume wakati wa Mwandamo wa Mwezi, na wakati wa mwezi mpevu, katika siku ya Sikukuu yetu; $$ PSA 81:4 hii ni amri kwa Israeli, agizo la Mungu wa Yakobo. $$ PSA 81:5 Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu alipotoka dhidi ya Misri, huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa. $$ PSA 81:6 Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu. $$ PSA 81:7 Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba. $$ PSA 81:8 “Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli! $$ PSA 81:9 Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; msimsujudie mungu wa kigeni. $$ PSA 81:10 Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza. $$ PSA 81:11 “Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii. $$ PSA 81:12 Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe. $$ PSA 81:13 “Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza, kama Israeli wangalifuata njia zangu, $$ PSA 81:14 ningaliwatiisha adui zao kwa haraka, na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! $$ PSA 81:15 Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele. $$ PSA 81:16 Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora, na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.” Zaburi 82 Zaburi ya Asafu. $$ PSA 82:1 Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”: $$ PSA 82:2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu? $$ PSA 82:3 Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa. $$ PSA 82:4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu. $$ PSA 82:5 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika. $$ PSA 82:6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’ $$ PSA 82:7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.” $$ PSA 82:8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako. Zaburi 83 Wimbo. Zaburi ya Asafu. $$ PSA 83:1 Ee Mungu, usinyamaze kimya, usinyamaze, Ee Mungu, usitulie. $$ PSA 83:2 Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao. $$ PSA 83:3 Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako, wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda. $$ PSA 83:4 Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.” $$ PSA 83:5 Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja, wanafanya muungano dhidi yako, $$ PSA 83:6 mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari, $$ PSA 83:7 Gebali, Amoni na Amaleki, Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro. $$ PSA 83:8 Hata Ashuru wameungana nao kuwapa nguvu wazao wa Loti. $$ PSA 83:9 Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini hapo kijito cha Kishoni, $$ PSA 83:10 ambao waliangamia huko Endori na wakawa kama takataka juu ya nchi. $$ PSA 83:11 Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, watawala wao kama Zeba na Salmuna, $$ PSA 83:12 ambao walisema, “Na tumiliki nchi ya malisho ya Mungu.” $$ PSA 83:13 Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi yapeperushwayo na upepo. $$ PSA 83:14 Kama vile moto uteketezavyo msitu au mwali wa moto unavyounguza milima, $$ PSA 83:15 wafuatilie kwa tufani yako na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako. $$ PSA 83:16 Funika nyuso zao kwa aibu ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana. $$ PSA 83:17 Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele, na waangamie kwa aibu. $$ PSA 83:18 Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote. Zaburi 84 Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora. $$ PSA 84:1 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini! $$ PSA 84:2 Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za Bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai. $$ PSA 84:3 Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu. $$ PSA 84:4 Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima. $$ PSA 84:5 Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. $$ PSA 84:6 Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi. $$ PSA 84:7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni. $$ PSA 84:8 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo. $$ PSA 84:9 Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako. $$ PSA 84:10 Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu. $$ PSA 84:11 Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia. $$ PSA 84:12 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe. Zaburi 85 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. $$ PSA 85:1 Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake. $$ PSA 85:2 Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote. $$ PSA 85:3 Uliweka kando ghadhabu yako yote na umegeuka na kuiacha hasira yako kali. $$ PSA 85:4 Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu. $$ PSA 85:5 Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote? $$ PSA 85:6 Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie? $$ PSA 85:7 Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, utupe wokovu wako. $$ PSA 85:8 Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: lakini nao wasirudie upumbavu. $$ PSA 85:9 Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, ili utukufu wake udumu katika nchi yetu. $$ PSA 85:10 Upendo na uaminifu hukutana pamoja, haki na amani hubusiana. $$ PSA 85:11 Uaminifu huchipua kutoka nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni. $$ PSA 85:12 Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, nayo nchi yetu itazaa mavuno yake. $$ PSA 85:13 Haki itatangulia mbele yake na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake. Zaburi 86 Maombi ya Daudi. $$ PSA 86:1 Ee Bwana, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji. $$ PSA 86:2 Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, wewe ni Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako anayekutumaini. $$ PSA 86:3 Ee Bwana, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa. $$ PSA 86:4 Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu. $$ PSA 86:5 Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao. $$ PSA 86:6 Ee Bwana, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie. $$ PSA 86:7 Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu. $$ PSA 86:8 Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe, hakuna matendo ya kulinganishwa na yako. $$ PSA 86:9 Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya yatakuja na kuabudu mbele zako; wataliletea utukufu jina lako. $$ PSA 86:10 Kwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu; wewe peke yako ndiwe Mungu. $$ PSA 86:11 Ee Bwana, nifundishe njia yako, nami nitakwenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako. $$ PSA 86:12 Ee Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitaliadhimisha jina lako milele. $$ PSA 86:13 Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi. $$ PSA 86:14 Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia; kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu: watu wasiokuheshimu wewe. $$ PSA 86:15 Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu. $$ PSA 86:16 Nigeukie na unihurumie; mpe mtumishi wako nguvu zako, mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike. $$ PSA 86:17 Nipe ishara ya wema wako, ili adui zangu waione nao waaibishwe, kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umenisaidia na kunifariji. Zaburi 87 Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. $$ PSA 87:1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; $$ PSA 87:2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. $$ PSA 87:3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: $$ PSA 87:4 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” $$ PSA 87:5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” $$ PSA 87:6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” $$ PSA 87:7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.” Zaburi 88 Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi. $$ PSA 88:1 Ee Bwana, Mungu uniokoaye, nimelia mbele zako usiku na mchana. $$ PSA 88:2 Maombi yangu yafike mbele zako, utegee kilio changu sikio lako. $$ PSA 88:3 Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi. $$ PSA 88:4 Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni, niko kama mtu asiye na nguvu. $$ PSA 88:5 Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako. $$ PSA 88:6 Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana, katika vina vya giza nene. $$ PSA 88:7 Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu, umenigharikisha kwa mawimbi yako yote. $$ PSA 88:8 Umenitenga na rafiki zangu wa karibu na kunifanya chukizo kwao. Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka; $$ PSA 88:9 nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu. $$ PSA 88:10 Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu? $$ PSA 88:11 Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu? $$ PSA 88:12 Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu? $$ PSA 88:13 Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie; asubuhi maombi yangu huja mbele zako. $$ PSA 88:14 Ee Bwana, kwa nini unanikataa na kunificha uso wako? $$ PSA 88:15 Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa. $$ PSA 88:16 Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza. $$ PSA 88:17 Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko; zimenimeza kabisa. $$ PSA 88:18 Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu; giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote. Zaburi 89 Utenzi wa Ethani Mwezrahi. $$ PSA 89:1 Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote. $$ PSA 89:2 Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni. $$ PSA 89:3 Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi, $$ PSA 89:4 ‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ” $$ PSA 89:5 Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu. $$ PSA 89:6 Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana? $$ PSA 89:7 Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka. $$ PSA 89:8 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, ni nani aliye kama wewe? Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka. $$ PSA 89:9 Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza. $$ PSA 89:10 Wewe ulimponda Rahabu kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako. $$ PSA 89:11 Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo. $$ PSA 89:12 Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. $$ PSA 89:13 Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa. $$ PSA 89:14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia. $$ PSA 89:15 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana. $$ PSA 89:16 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako. $$ PSA 89:17 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe yetu. $$ PSA 89:18 Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli. $$ PSA 89:19 Ulizungumza wakati fulani katika maono, kwa watu wako waaminifu, ukasema: “Nimeweka nguvu kwa shujaa, nimemwinua kijana miongoni mwa watu. $$ PSA 89:20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimemtia mafuta yangu matakatifu. $$ PSA 89:21 Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu. $$ PSA 89:22 Hakuna adui atakayemtoza ushuru, hakuna mtu mwovu atakayemwonea. $$ PSA 89:23 Nitawaponda adui zake mbele zake na kuwaangamiza watesi wake. $$ PSA 89:24 Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa. $$ PSA 89:25 Nitauweka mkono wake juu ya bahari, mkono wake wa kuume juu ya mito. $$ PSA 89:26 Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’ $$ PSA 89:27 Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia. $$ PSA 89:28 Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara. $$ PSA 89:29 Nitaudumisha uzao wake milele, kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu. $$ PSA 89:30 “Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu, $$ PSA 89:31 kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu, $$ PSA 89:32 nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga, $$ PSA 89:33 lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe. $$ PSA 89:34 Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. $$ PSA 89:35 Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi: $$ PSA 89:36 kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua; $$ PSA 89:37 kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.” $$ PSA 89:38 Lakini wewe umemkataa, umemdharau, umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako. $$ PSA 89:39 Umelikana agano lako na mtumishi wako, na umeinajisi taji yake mavumbini. $$ PSA 89:40 Umebomoa kuta zake zote, na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu. $$ PSA 89:41 Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; amekuwa dharau kwa jirani zake. $$ PSA 89:42 Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, umewafanya watesi wake wote washangilie. $$ PSA 89:43 Umegeuza makali ya upanga wake, na hukumpa msaada katika vita. $$ PSA 89:44 Umeikomesha fahari yake, na kukiangusha kiti chake cha enzi. $$ PSA 89:45 Umezifupisha siku za ujana wake, umemfunika kwa vazi la aibu. $$ PSA 89:46 Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini? $$ PSA 89:47 Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu! $$ PSA 89:48 Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? $$ PSA 89:49 Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni, ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi? $$ PSA 89:50 Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote, $$ PSA 89:51 dhihaka ambazo kwazo adui zako wamenisimanga, Ee Bwana, ambazo kwazo wamesimanga kila hatua ya mpakwa mafuta wako. $$ PSA 89:52 Msifuni Bwana milele! Amen na Amen. (Zaburi 90–106) Zaburi 90 Maombi ya Mose, mtu wa Mungu. $$ PSA 90:1 Bwana, wewe umekuwa makao yetu katika vizazi vyote. $$ PSA 90:2 Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele. $$ PSA 90:3 Huwarudisha watu mavumbini, ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.” $$ PSA 90:4 Kwa maana kwako miaka elfu ni kama siku moja iliyokwisha pita, au kama kesha la usiku. $$ PSA 90:5 Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo, nao ni kama majani machanga ya asubuhi: $$ PSA 90:6 ingawa asubuhi yanachipua, ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka. $$ PSA 90:7 Tumeangamizwa kwa hasira yako na tumetishwa kwa ghadhabu yako. $$ PSA 90:8 Umeyaweka maovu yetu mbele yako, dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako. $$ PSA 90:9 Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako, tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza. $$ PSA 90:10 Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, au miaka themanini ikiwa tuna nguvu, lakini yote ni ya shida na taabu, nazo zapita haraka, nasi twatoweka. $$ PSA 90:11 Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako? Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako. $$ PSA 90:12 Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili tujipatie moyo wa hekima. $$ PSA 90:13 Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini? Wahurumie watumishi wako. $$ PSA 90:14 Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma, ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote. $$ PSA 90:15 Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu, kulingana na miaka tuliyotaabika. $$ PSA 90:16 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, utukufu wako kwa watoto wao. $$ PSA 90:17 Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu; uzithibitishe kazi za mikono yetu: naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu. Zaburi 91 $$ PSA 91:1 Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. $$ PSA 91:2 Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.” $$ PSA 91:3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua. $$ PSA 91:4 Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. $$ PSA 91:5 Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana, $$ PSA 91:6 wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri. $$ PSA 91:7 Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe. $$ PSA 91:8 Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu. $$ PSA 91:9 Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako: naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu, $$ PSA 91:10 basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, hakuna maafa yataikaribia hema yako. $$ PSA 91:11 Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote. $$ PSA 91:12 Mikononi mwao watakuinua, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe. $$ PSA 91:13 Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu. $$ PSA 91:14 Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa; nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu. $$ PSA 91:15 Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu. $$ PSA 91:16 Kwa siku nyingi nitamshibisha na kumwonyesha wokovu wangu.” Zaburi 92 Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. $$ PSA 92:1 Ni vyema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana, $$ PSA 92:2 kuutangaza upendo wako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku, $$ PSA 92:3 kwa zeze yenye nyuzi kumi na kwa sauti ya kinubi. $$ PSA 92:4 Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako. $$ PSA 92:5 Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako, tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako! $$ PSA 92:6 Mjinga hafahamu, mpumbavu haelewi, $$ PSA 92:7 ingawa waovu huchipua kama majani na wote watendao mabaya wanastawi, wataangamizwa milele. $$ PSA 92:8 Bali wewe, Ee Bwana, utatukuzwa milele. $$ PSA 92:9 Ee Bwana, hakika adui zako, hakika adui zako wataangamia. Wote watendao mabaya watatawanyika. $$ PSA 92:10 Umeitukuza pembe yangu kama ile ya nyati dume, mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu. $$ PSA 92:11 Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa, masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu. $$ PSA 92:12 Wenye haki watastawi kama mtende, watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni, $$ PSA 92:13 waliopandwa katika nyumba ya Bwana, watastawi katika nyua za Mungu wetu. $$ PSA 92:14 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu, $$ PSA 92:15 wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu; yeye ni Mwamba wangu, na ndani yake hamna uovu.” Zaburi 93 $$ PSA 93:1 Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa. $$ PSA 93:2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele. $$ PSA 93:3 Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake. $$ PSA 93:4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu. $$ PSA 93:5 Ee Bwana, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho. Zaburi 94 $$ PSA 94:1 Ee Bwana, ulipizaye kisasi, Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa. $$ PSA 94:2 Ee Mhukumu wa dunia, inuka, uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili. $$ PSA 94:3 Hata lini, waovu, Ee Bwana, hata lini waovu watashangilia? $$ PSA 94:4 Wanamimina maneno ya kiburi, watenda mabaya wote wamejaa majivuno. $$ PSA 94:5 Ee Bwana, wanawaponda watu wako, wanawaonea urithi wako. $$ PSA 94:6 Wanamchinja mjane na mgeni, na kuwaua yatima. $$ PSA 94:7 Nao husema, “Bwana haoni, Mungu wa Yakobo hafahamu.” $$ PSA 94:8 Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu; enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima? $$ PSA 94:9 Je, aliyeweka sikio asisikie? Aliyeumba jicho asione? $$ PSA 94:10 Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu? Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa? $$ PSA 94:11 Bwana anajua mawazo ya mwanadamu; anajua kwamba ni ubatili. $$ PSA 94:12 Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe, mtu unayemfundisha kwa sheria yako, $$ PSA 94:13 unampa utulivu siku za shida, mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa kwa ajili ya mwovu. $$ PSA 94:14 Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake, hatauacha urithi wake. $$ PSA 94:15 Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki, wote walio na mioyo minyofu wataifuata. $$ PSA 94:16 Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu? Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu? $$ PSA 94:17 Kama Bwana asingelinisaidia upesi, ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo. $$ PSA 94:18 Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia. $$ PSA 94:19 Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu. $$ PSA 94:20 Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe, ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake? $$ PSA 94:21 Huungana kuwashambulia wenye haki, kuwahukumu kufa wasio na hatia. $$ PSA 94:22 Lakini Bwana amekuwa ngome yangu, na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia. $$ PSA 94:23 Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao; Bwana Mungu wetu atawaangamiza. Zaburi 95 $$ PSA 95:1 Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. $$ PSA 95:2 Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. $$ PSA 95:3 Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote. $$ PSA 95:4 Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake. $$ PSA 95:5 Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu. $$ PSA 95:6 Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu, $$ PSA 95:7 kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo, $$ PSA 95:8 msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya kule Meriba, kama mlivyofanya siku ile kule Masa jangwani, $$ PSA 95:9 ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu. $$ PSA 95:10 Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile, nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.” $$ PSA 95:11 Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.” Zaburi 96 (1 Nyakati 16:23-33) $$ PSA 96:1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote. $$ PSA 96:2 Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. $$ PSA 96:3 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. $$ PSA 96:4 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. $$ PSA 96:5 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu. $$ PSA 96:6 Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. $$ PSA 96:7 Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. $$ PSA 96:8 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. $$ PSA 96:9 Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake. $$ PSA 96:10 Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu. $$ PSA 96:11 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; $$ PSA 96:12 mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; $$ PSA 96:13 itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake. Zaburi 97 $$ PSA 97:1 Bwana anatawala, nchi na ifurahi, visiwa vyote vishangilie. $$ PSA 97:2 Mawingu na giza nene vinamzunguka, haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi. $$ PSA 97:3 Moto hutangulia mbele zake na huteketeza adui zake pande zote. $$ PSA 97:4 Umeme wake wa radi humulika dunia, nchi huona na kutetemeka. $$ PSA 97:5 Milima huyeyuka kama nta mbele za Bwana, mbele za Bwana wa dunia yote. $$ PSA 97:6 Mbingu zinatangaza haki yake, na mataifa yote huona utukufu wake. $$ PSA 97:7 Wote waabuduo sanamu waaibishwa, wale wajisifiao sanamu: mwabuduni yeye, enyi miungu yote! $$ PSA 97:8 Sayuni husikia na kushangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana. $$ PSA 97:9 Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; umetukuka sana juu ya miungu yote. $$ PSA 97:10 Wale wanaompenda Bwana na wauchukie uovu, kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu. $$ PSA 97:11 Nuru huangaza wenye haki na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. $$ PSA 97:12 Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu. Zaburi 98 Zaburi. $$ PSA 98:1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu. $$ PSA 98:2 Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane na amedhihirisha haki yake kwa mataifa. $$ PSA 98:3 Ameukumbuka upendo wake na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu. $$ PSA 98:4 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda; $$ PSA 98:5 mwimbieni Bwana kwa kinubi, kwa kinubi na sauti za kuimba, $$ PSA 98:6 kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme. $$ PSA 98:7 Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake, dunia na wote wakaao ndani yake. $$ PSA 98:8 Mito na ipige makofi, milima na iimbe pamoja kwa furaha, $$ PSA 98:9 vyote na viimbe mbele za Bwana, kwa maana yuaja kuhukumu dunia. Atahukumu dunia kwa haki na mataifa kwa haki. Zaburi 99 $$ PSA 99:1 Bwana anatawala, mataifa na yatetemeke; anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi, dunia na itikisike. $$ PSA 99:2 Bwana ni mkuu katika Sayuni; ametukuzwa juu ya mataifa yote. $$ PSA 99:3 Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: yeye ni mtakatifu! $$ PSA 99:4 Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa. $$ PSA 99:5 Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu. $$ PSA 99:6 Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu. $$ PSA 99:7 Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa. $$ PSA 99:8 Ee Bwana, wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya. $$ PSA 99:9 Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu. Zaburi 100 Zaburi ya shukrani. $$ PSA 100:1 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote. $$ PSA 100:2 Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. $$ PSA 100:3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake. $$ PSA 100:4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. $$ PSA 100:5 Kwa maana Bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote. Zaburi 101 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 101:1 Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa. $$ PSA 101:2 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama. $$ PSA 101:3 Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; hawatashikamana nami. $$ PSA 101:4 Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; nitajitenga na kila ubaya. $$ PSA 101:5 Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri, huyo nitamnyamazisha; mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi huyo sitamvumilia. $$ PSA 101:6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, ili waweze kuishi pamoja nami; yeye ambaye moyo wake hauna lawama atanitumikia. $$ PSA 101:7 Mdanganyifu hatakaa nyumbani mwangu, yeye asemaye kwa uongo hatasimama mbele yangu. $$ PSA 101:8 Kila asubuhi nitawanyamazisha waovu wote katika nchi; nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya kutoka mji wa Bwana. Zaburi 102 Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa Bwana. $$ PSA 102:1 Ee Bwana, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. $$ PSA 102:2 Usinifiche uso wako ninapokuwa katika shida. Unitegee sikio lako, ninapoita, unijibu kwa upesi. $$ PSA 102:3 Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi, mifupa yangu inaungua kama kaa la moto. $$ PSA 102:4 Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani, ninasahau kula chakula changu. $$ PSA 102:5 Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu, nimebakia ngozi na mifupa. $$ PSA 102:6 Nimekuwa kama bundi wa jangwani, kama bundi kwenye magofu. $$ PSA 102:7 Nilalapo sipati usingizi, nimekuwa kama ndege mpweke kwenye paa la nyumba. $$ PSA 102:8 Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki, wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana. $$ PSA 102:9 Ninakula majivu kama chakula changu na nimechanganya kinywaji changu na machozi $$ PSA 102:10 kwa sababu ya ghadhabu yako kuu, kwa maana umeniinua na kunitupa kando. $$ PSA 102:11 Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, ninanyauka kama jani. $$ PSA 102:12 Lakini wewe, Ee Bwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele, sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote. $$ PSA 102:13 Utainuka na kuihurumia Sayuni, kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema; wakati uliokubalika umewadia. $$ PSA 102:14 Kwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako, vumbi lake lenyewe hulionea huruma. $$ PSA 102:15 Mataifa wataogopa jina la Bwana, wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako. $$ PSA 102:16 Kwa maana Bwana ataijenga tena Sayuni na kutokea katika utukufu wake. $$ PSA 102:17 Ataitikia maombi ya mtu mkiwa, wala hatadharau hoja yao. $$ PSA 102:18 Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho, ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana: $$ PSA 102:19 “Bwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu, kutoka mbinguni alitazama dunia, $$ PSA 102:20 kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.” $$ PSA 102:21 Kwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu, $$ PSA 102:22 wakati mataifa na falme zitakapokusanyika ili kumwabudu Bwana. $$ PSA 102:23 Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu, akafupisha siku zangu. $$ PSA 102:24 Ndipo niliposema: “Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; miaka yako inaendelea vizazi vyote. $$ PSA 102:25 Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. $$ PSA 102:26 Hizi zitatoweka, lakini wewe utadumu, zote zitachakaa kama vazi. Utazibadilisha kama nguo nazo zitaondoshwa. $$ PSA 102:27 Lakini wewe, U yeye yule, nayo miaka yako haikomi kamwe. $$ PSA 102:28 Watoto wa watumishi wako wataishi mbele zako; wazao wao wataimarishwa mbele zako.” Zaburi 103 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 103:1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. $$ PSA 103:2 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, wala usisahau wema wake wote, $$ PSA 103:3 akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote, $$ PSA 103:4 aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma, $$ PSA 103:5 atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai. $$ PSA 103:6 Bwana hutenda haki, naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa. $$ PSA 103:7 Alijulisha Mose njia zake, na wana wa Israeli matendo yake. $$ PSA 103:8 Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo. $$ PSA 103:9 Yeye hatalaumu siku zote, wala haweki hasira yake milele, $$ PSA 103:10 yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu. $$ PSA 103:11 Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; $$ PSA 103:12 kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi. $$ PSA 103:13 Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha; $$ PSA 103:14 kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi. $$ PSA 103:15 Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, anachanua kama ua la shambani; $$ PSA 103:16 upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, mahali pake hapalikumbuki tena. $$ PSA 103:17 Lakini kutoka milele hata milele upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao: $$ PSA 103:18 kwa wale walishikao agano lake na kukumbuka kuyatii mausia yake. $$ PSA 103:19 Bwana ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, ufalme wake unatawala juu ya vyote. $$ PSA 103:20 Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake, ninyi mnaotii neno lake. $$ PSA 103:21 Mhimidini Bwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake. $$ PSA 103:22 Mhimidini Bwana, kazi zake zote kila mahali katika milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Zaburi 104 $$ PSA 104:1 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. $$ PSA 104:2 Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema $$ PSA 104:3 na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo. $$ PSA 104:4 Huzifanya pepo kuwa wajumbe wake, miali ya moto watumishi wake. $$ PSA 104:5 Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa. $$ PSA 104:6 Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima. $$ PSA 104:7 Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka, $$ PSA 104:8 yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia. $$ PSA 104:9 Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena. $$ PSA 104:10 Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima. $$ PSA 104:11 Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao. $$ PSA 104:12 Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, huimba katikati ya matawi. $$ PSA 104:13 Huinyeshea milima kutoka orofa zake, dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake. $$ PSA 104:14 Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini: $$ PSA 104:15 divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu. $$ PSA 104:16 Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. $$ PSA 104:17 Humo ndege hufanya viota vyao, korongo ana nyumba yake kwenye msunobari. $$ PSA 104:18 Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu, majabali ni kimbilio la pelele. $$ PSA 104:19 Mwezi hugawanya majira, na jua hutambua wakati wake wa kutua. $$ PSA 104:20 Unaleta giza, kunakuwa usiku, wanyama wote wa mwituni huzurura. $$ PSA 104:21 Simba hunguruma kwa mawindo yao, na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu. $$ PSA 104:22 Jua huchomoza, nao huondoka, hurudi na kulala katika mapango yao. $$ PSA 104:23 Kisha mwanadamu huenda kazini mwake, katika kazi yake mpaka jioni. $$ PSA 104:24 Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako. $$ PSA 104:25 Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. $$ PSA 104:26 Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake. $$ PSA 104:27 Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. $$ PSA 104:28 Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema. $$ PSA 104:29 Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini. $$ PSA 104:30 Unapopeleka Roho wako, wanaumbwa, nawe huufanya upya uso wa dunia. $$ PSA 104:31 Utukufu wa Bwana na udumu milele, Bwana na azifurahie kazi zake: $$ PSA 104:32 yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, aigusaye milima, nayo ikatoa moshi. $$ PSA 104:33 Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote; nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi. $$ PSA 104:34 Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, ninapofurahi katika Bwana. $$ PSA 104:35 Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia na waovu wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, msifu Bwana. Msifuni Bwana. Zaburi 105 (1 Nyakati 16:8-22) $$ PSA 105:1 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. $$ PSA 105:2 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu. $$ PSA 105:3 Lishangilieni jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi. $$ PSA 105:4 Mtafuteni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote. $$ PSA 105:5 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, $$ PSA 105:6 enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake. $$ PSA 105:7 Yeye ndiye Bwana Mungu wetu, hukumu zake zimo duniani pote. $$ PSA 105:8 Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, $$ PSA 105:9 agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki. $$ PSA 105:10 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele: $$ PSA 105:11 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.” $$ PSA 105:12 Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake, $$ PSA 105:13 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. $$ PSA 105:14 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: $$ PSA 105:15 “Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.” $$ PSA 105:16 Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote, $$ PSA 105:17 naye akatuma mtu mbele yao, Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa. $$ PSA 105:18 Walichubua miguu yake kwa minyororo, shingo yake ilifungwa kwa chuma, $$ PSA 105:19 hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, hadi neno la Bwana lilipomthibitisha. $$ PSA 105:20 Mfalme alituma watu wakamfungua, mtawala wa watu alimwachia huru. $$ PSA 105:21 Alimfanya mkuu wa nyumba yake, mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo, $$ PSA 105:22 kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo na kuwafundisha wazee wake hekima. $$ PSA 105:23 Kisha Israeli akaingia Misri, Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu. $$ PSA 105:24 Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana, akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao, $$ PSA 105:25 ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, wakatenda hila dhidi ya watumishi wake. $$ PSA 105:26 Akamtuma Mose mtumishi wake, pamoja na Aroni, aliyemchagua. $$ PSA 105:27 Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao, miujiza yake katika nchi ya Hamu. $$ PSA 105:28 Alituma giza na nchi ikajaa giza, kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake? $$ PSA 105:29 Aligeuza maji yao kuwa damu, ikasababisha samaki wao kufa. $$ PSA 105:30 Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao. $$ PSA 105:31 Alisema, yakaja makundi ya mainzi, na viroboto katika nchi yao yote. $$ PSA 105:32 Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe, yenye umeme wa radi nchini yao yote, $$ PSA 105:33 akaharibu mizabibu yao na miti ya tini, na akaangamiza miti ya nchi yao. $$ PSA 105:34 Alisema, nzige wakaja, tunutu wasio na idadi, $$ PSA 105:35 wakala kila jani katika nchi yao, wakala mazao ya ardhi yao. $$ PSA 105:36 Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao, matunda ya kwanza ya ujana wao wote. $$ PSA 105:37 Akawatoa Israeli katika nchi wakiwa na fedha na dhahabu nyingi, wala hakuna hata mmoja kutoka kabila zao aliyejikwaa. $$ PSA 105:38 Misri ilifurahi walipoondoka, kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia. $$ PSA 105:39 Alitandaza wingu kama kifuniko, na moto kuwamulikia usiku. $$ PSA 105:40 Waliomba, naye akawaletea kware, akawashibisha kwa mkate wa mbinguni. $$ PSA 105:41 Alipasua mwamba, maji yakabubujika, yakatiririka jangwani kama mto. $$ PSA 105:42 Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake. $$ PSA 105:43 Aliwatoa watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za shangwe, $$ PSA 105:44 akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi wa mali wengine walikuwa wameitaabikia: $$ PSA 105:45 alifanya haya ili wayashike mausia yake na kuzitii sheria zake. Msifuni Bwana. Zaburi 106 $$ PSA 106:1 Msifuni Bwana. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. $$ PSA 106:2 Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana au kutangaza kikamilifu sifa zake? $$ PSA 106:3 Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema. $$ PSA 106:4 Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa, $$ PSA 106:5 ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, na kuungana na urithi wako katika kukusifu. $$ PSA 106:6 Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, tumekosa na tumetenda uovu. $$ PSA 106:7 Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu. $$ PSA 106:8 Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu. $$ PSA 106:9 Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani. $$ PSA 106:10 Aliwaokoa mikononi mwa adui; kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa. $$ PSA 106:11 Maji yaliwafunika adui zao, hakunusurika hata mmoja. $$ PSA 106:12 Ndipo walipoamini ahadi zake, nao wakaimba sifa zake. $$ PSA 106:13 Lakini mara walisahau aliyowatendea, wala hawakungojea shauri lake. $$ PSA 106:14 Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani. $$ PSA 106:15 Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha. $$ PSA 106:16 Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana. $$ PSA 106:17 Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, ikawazika Abiramu na kundi lake. $$ PSA 106:18 Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, mwali wa moto uliwateketeza waovu. $$ PSA 106:19 Huko Horebu walitengeneza ndama, na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma. $$ PSA 106:20 Waliubadilisha Utukufu wao kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani. $$ PSA 106:21 Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri, $$ PSA 106:22 miujiza katika nchi ya Hamu na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu. $$ PSA 106:23 Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: kama Mose mteule wake, asingesimama kati yao na Mungu kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza. $$ PSA 106:24 Kisha waliidharau ile nchi nzuri, hawakuiamini ahadi yake. $$ PSA 106:25 Walinungʼunika ndani ya mahema yao, wala hawakumtii Bwana. $$ PSA 106:26 Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba atawafanya waanguke jangwani, $$ PSA 106:27 kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, na kuwatawanya katika nchi zote. $$ PSA 106:28 Walijifunga nira na Baali wa Peori, wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai. $$ PSA 106:29 Waliichochea hasira ya Bwana, wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, nayo tauni ikazuka katikati yao. $$ PSA 106:30 Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, nayo tauni ikazuiliwa. $$ PSA 106:31 Hili likahesabiwa kwake haki, kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo. $$ PSA 106:32 Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, janga likampata Mose kwa sababu yao; $$ PSA 106:33 kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose. $$ PSA 106:34 Hawakuyaangamiza yale mataifa kama Bwana alivyowaagiza, $$ PSA 106:35 bali walijichanganya na mataifa na wakazikubali desturi zao. $$ PSA 106:36 Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao. $$ PSA 106:37 Wakawatoa wana wao na binti zao dhabihu kwa mashetani. $$ PSA 106:38 Walimwaga damu isiyo na hatia, damu za wana wao na binti zao, ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikanajisika kwa damu zao. $$ PSA 106:39 Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba. $$ PSA 106:40 Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake na akauchukia sana urithi wake. $$ PSA 106:41 Akawakabidhi kwa mataifa na adui zao wakawatawala. $$ PSA 106:42 Adui zao wakawaonea na kuwatia chini ya mamlaka yao. $$ PSA 106:43 Mara nyingi aliwaokoa lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, nao wakajiharibu katika dhambi zao. $$ PSA 106:44 Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao; $$ PSA 106:45 kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake. $$ PSA 106:46 Akawafanya wahurumiwe na wote waliowashikilia mateka. $$ PSA 106:47 Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako. $$ PSA 106:48 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Watu wote na waseme, “Amen!” Msifuni Bwana. (Zaburi 107–150) Zaburi 107 $$ PSA 107:1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele. $$ PSA 107:2 Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui, $$ PSA 107:3 wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini. $$ PSA 107:4 Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi. $$ PSA 107:5 Walikuwa na njaa na kiu, nafsi zao zikadhoofika. $$ PSA 107:6 Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. $$ PSA 107:7 Akawaongoza kwa njia iliyo sawa hadi mji ambao wangeweza kuishi. $$ PSA 107:8 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, $$ PSA 107:9 kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema. $$ PSA 107:10 Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, wafungwa wakiteseka katika minyororo, $$ PSA 107:11 kwa sababu walikuwa wameasi dhidi ya maneno ya Mungu na kudharau shauri la Aliye Juu Sana. $$ PSA 107:12 Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia. $$ PSA 107:13 Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. $$ PSA 107:14 Akawatoa katika giza na huzuni kuu na akavunja minyororo yao. $$ PSA 107:15 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, $$ PSA 107:16 kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma. $$ PSA 107:17 Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao, wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao. $$ PSA 107:18 Wakachukia kabisa vyakula vyote, wakakaribia malango ya mauti. $$ PSA 107:19 Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. $$ PSA 107:20 Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo yao. $$ PSA 107:21 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. $$ PSA 107:22 Na watoe dhabihu za kushukuru, na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha. $$ PSA 107:23 Wengine walisafiri baharini kwa meli, walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu. $$ PSA 107:24 Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini. $$ PSA 107:25 Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu. $$ PSA 107:26 Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka. $$ PSA 107:27 Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo. $$ PSA 107:28 Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao. $$ PSA 107:29 Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia. $$ PSA 107:30 Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani. $$ PSA 107:31 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. $$ PSA 107:32 Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee. $$ PSA 107:33 Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu, $$ PSA 107:34 nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa, kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo. $$ PSA 107:35 Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji, nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo; $$ PSA 107:36 aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, nao wakajenga mji wangeweza kuishi. $$ PSA 107:37 Walilima mashamba na kupanda mizabibu, nayo ikazaa matunda mengi, $$ PSA 107:38 Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana, wala hakuruhusu mifugo yao kupungua. $$ PSA 107:39 Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa kwa kuonewa, maafa na huzuni. $$ PSA 107:40 Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu, aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia. $$ PSA 107:41 Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao, na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo. $$ PSA 107:42 Wanyofu wataona na kufurahi, lakini waovu wote watafunga vinywa vyao. $$ PSA 107:43 Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya, na atafakari upendo mkuu wa Bwana. Zaburi 108 (Zaburi 57:7-11; 60:5-12) Wimbo. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 108:1 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. $$ PSA 108:2 Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. $$ PSA 108:3 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. $$ PSA 108:4 Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; uaminifu wako unazifikia anga. $$ PSA 108:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. $$ PSA 108:6 Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa. $$ PSA 108:7 Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi. $$ PSA 108:8 Gileadi ni yangu, Manase ni yangu, Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. $$ PSA 108:9 Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” $$ PSA 108:10 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? $$ PSA 108:11 Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? $$ PSA 108:12 Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. $$ PSA 108:13 Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu. Zaburi 109 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 109:1 Ee Mungu, ambaye ninakusifu, usiwe kimya, $$ PSA 109:2 kwa maana watu waovu na wadanganyifu wamefungua vinywa vyao dhidi yangu; wasema dhidi yangu kwa ndimi za udanganyifu. $$ PSA 109:3 Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, wananishambulia bila sababu. $$ PSA 109:4 Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, lakini mimi ninawaombea. $$ PSA 109:5 Wananilipiza mabaya kwa mema, chuki badala ya urafiki wangu. $$ PSA 109:6 Agiza mtu mwovu ampinge, mshtaki asimame mkono wake wa kuume. $$ PSA 109:7 Anapohukumiwa, apatikane na hatia, nayo maombi yake yamhukumu. $$ PSA 109:8 Siku zake za kuishi na ziwe chache, nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine. $$ PSA 109:9 Watoto wake na waachwe yatima, mke wake na awe mjane. $$ PSA 109:10 Watoto wake na watangetange wakiomba, na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao. $$ PSA 109:11 Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo, matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni. $$ PSA 109:12 Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema wala wa kuwahurumia yatima wake. $$ PSA 109:13 Uzao wake na ukatiliwe mbali, majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho. $$ PSA 109:14 Maovu ya baba zake na yakumbukwe mbele za Bwana, dhambi ya mama yake isifutwe kamwe. $$ PSA 109:15 Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani. $$ PSA 109:16 Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. $$ PSA 109:17 Alipenda kulaani, nayo laana ikampata; hakupenda kubariki, kwa hiyo baraka na ikae mbali naye. $$ PSA 109:18 Alivaa kulaani kama vazi lake, nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji, kwenye mifupa yake kama mafuta. $$ PSA 109:19 Na iwe kama joho alilozungushiwa, kama mshipi aliofungiwa daima. $$ PSA 109:20 Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya. $$ PSA 109:21 Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wa pendo lako. $$ PSA 109:22 Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. $$ PSA 109:23 Ninafifia kama kivuli cha jioni, nimerushwa-rushwa kama nzige. $$ PSA 109:24 Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, mwili wangu umedhoofika na kukonda. $$ PSA 109:25 Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, wanionapo, hutikisa vichwa vyao. $$ PSA 109:26 Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie, niokoe sawasawa na upendo wako. $$ PSA 109:27 Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili. $$ PSA 109:28 Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, watakaposhambulia wataaibishwa, lakini mtumishi wako atashangilia. $$ PSA 109:29 Washtaki wangu watavikwa fedheha, na kufunikwa na aibu kama joho. $$ PSA 109:30 Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana, katika umati mkubwa nitamsifu. $$ PSA 109:31 Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji, kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu. Zaburi 110 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 110:1 Bwana amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.” $$ PSA 110:2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako. $$ PSA 110:3 Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako. $$ PSA 110:4 Bwana ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” $$ PSA 110:5 Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. $$ PSA 110:6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga na kuwaponda watawala wa dunia nzima. $$ PSA 110:7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia, kwa hiyo atainua kichwa chake juu. Zaburi 111 $$ PSA 111:1 Msifuni Bwana. Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko. $$ PSA 111:2 Kazi za Bwana ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari. $$ PSA 111:3 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima. $$ PSA 111:4 Amefanya maajabu yake yakumbukwe, Bwana ni mwenye neema na huruma. $$ PSA 111:5 Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele. $$ PSA 111:6 Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine. $$ PSA 111:7 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika. $$ PSA 111:8 Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu. $$ PSA 111:9 Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa. $$ PSA 111:10 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele. Zaburi 112 $$ PSA 112:1 Msifuni Bwana. Heri mtu yule amchaye Bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake. $$ PSA 112:2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. $$ PSA 112:3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, haki yake hudumu milele. $$ PSA 112:4 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki. $$ PSA 112:5 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, anayefanya mambo yake kwa haki. $$ PSA 112:6 Hakika hatatikisika kamwe, mtu mwenye haki atakumbukwa milele. $$ PSA 112:7 Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana. $$ PSA 112:8 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake. $$ PSA 112:9 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; haki yake hudumu milele; pembe yake itatukuzwa kwa heshima. $$ PSA 112:10 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa, atasaga meno yake na kutoweka, kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu. Zaburi 113 $$ PSA 113:1 Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana. $$ PSA 113:2 Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele. $$ PSA 113:3 Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa. $$ PSA 113:4 Bwana ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu. $$ PSA 113:5 Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi, $$ PSA 113:6 ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi? $$ PSA 113:7 Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala, $$ PSA 113:8 huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. $$ PSA 113:9 Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Bwana. Zaburi 114 $$ PSA 114:1 Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni, $$ PSA 114:2 Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake. $$ PSA 114:3 Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma, $$ PSA 114:4 milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo. $$ PSA 114:5 Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma, $$ PSA 114:6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo? $$ PSA 114:7 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo, $$ PSA 114:8 aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji. Zaburi 115 $$ PSA 115:1 Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako. $$ PSA 115:2 Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wao?” $$ PSA 115:3 Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lolote limpendezalo. $$ PSA 115:4 Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. $$ PSA 115:5 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona; $$ PSA 115:6 zina masikio, lakini haziwezi kusikia, zina pua, lakini haziwezi kunusa; $$ PSA 115:7 zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala koo zao haziwezi kutoa sauti. $$ PSA 115:8 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. $$ PSA 115:9 Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao. $$ PSA 115:10 Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao. $$ PSA 115:11 Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao. $$ PSA 115:12 Bwana anatukumbuka na atatubariki: ataibariki nyumba ya Israeli, ataibariki nyumba ya Aroni, $$ PSA 115:13 atawabariki wale wanaomcha Bwana, wadogo kwa wakubwa. $$ PSA 115:14 Bwana na awawezeshe kuongezeka, ninyi na watoto wenu. $$ PSA 115:15 Mbarikiwe na Bwana Muumba wa mbingu na dunia. $$ PSA 115:16 Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana, lakini dunia amempa mwanadamu. $$ PSA 115:17 Sio wafu wanaomsifu Bwana, wale washukao mahali pa kimya, $$ PSA 115:18 bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, sasa na hata milele. Msifuni Bwana. Zaburi 116 $$ PSA 116:1 Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie. $$ PSA 116:2 Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu. $$ PSA 116:3 Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. $$ PSA 116:4 Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!” $$ PSA 116:5 Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma. $$ PSA 116:6 Bwana huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa. $$ PSA 116:7 Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako. $$ PSA 116:8 Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umeniokoa nafsi yangu na mauti, macho yangu kutokana na machozi, miguu yangu kutokana na kujikwaa, $$ PSA 116:9 ili niweze kutembea mbele za Bwana, katika nchi ya walio hai. $$ PSA 116:10 Niliamini, kwa hiyo nilisema, “Mimi nimeteseka sana.” $$ PSA 116:11 Katika taabu yangu nilisema, “Wanadamu wote ni waongo.” $$ PSA 116:12 Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea? $$ PSA 116:13 Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana. $$ PSA 116:14 Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote. $$ PSA 116:15 Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa Bwana. $$ PSA 116:16 Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umeniweka huru toka katika minyororo yangu. $$ PSA 116:17 Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la Bwana. $$ PSA 116:18 Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote, $$ PSA 116:19 katika nyua za nyumba ya Bwana, katikati yako, ee Yerusalemu. Msifuni Bwana. Zaburi 117 $$ PSA 117:1 Msifuni Bwana, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote. $$ PSA 117:2 Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, uaminifu wa Bwana unadumu milele. Msifuni Bwana. Zaburi 118 $$ PSA 118:1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. $$ PSA 118:2 Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” $$ PSA 118:3 Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” $$ PSA 118:4 Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” $$ PSA 118:5 Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana, naye akanijibu kwa kuniweka huru. $$ PSA 118:6 Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? $$ PSA 118:7 Bwana yuko pamoja nami, yeye ni msaidizi wangu. Nitawatazama adui zangu wakiwa wameshindwa. $$ PSA 118:8 Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kumtumainia mwanadamu. $$ PSA 118:9 Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wakuu. $$ PSA 118:10 Mataifa yote yalinizunguka, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. $$ PSA 118:11 Walinizunguka pande zote, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. $$ PSA 118:12 Walinizunguka kama kundi la nyuki, lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. $$ PSA 118:13 Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka, lakini Bwana alinisaidia. $$ PSA 118:14 Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu. $$ PSA 118:15 Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu! $$ PSA 118:16 Mkono wa kuume wa Bwana umeinuliwa juu, mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!” $$ PSA 118:17 Sitakufa, bali nitaishi, nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda. $$ PSA 118:18 Bwana ameniadhibu vikali, lakini hakuniacha nife. $$ PSA 118:19 Nifungulie malango ya haki, nami nitaingia na kumshukuru Bwana. $$ PSA 118:20 Hili ni lango la Bwana ambalo wenye haki wanaweza kuliingia. $$ PSA 118:21 Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu. $$ PSA 118:22 Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. $$ PSA 118:23 Bwana ametenda hili, nalo ni la kushangaza machoni petu. $$ PSA 118:24 Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya, tushangilie na kufurahi ndani yake. $$ PSA 118:25 Ee Bwana, tuokoe, Ee Bwana, utujalie mafanikio. $$ PSA 118:26 Heri yule ajaye kwa jina la Bwana. Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki. $$ PSA 118:27 Bwana ndiye Mungu, naye ametuangazia nuru yake. Mkiwa na matawi mkononi, unganeni kwenye maandamano ya sikukuu hadi kwenye pembe za madhabahu. $$ PSA 118:28 Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza. $$ PSA 118:29 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. Zaburi 119 $$ PSA 119:1 Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana. $$ PSA 119:2 Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote. $$ PSA 119:3 Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake. $$ PSA 119:4 Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu. $$ PSA 119:5 Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako! $$ PSA 119:6 Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote. $$ PSA 119:7 Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki. $$ PSA 119:8 Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa. $$ PSA 119:9 Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. $$ PSA 119:10 Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako. $$ PSA 119:11 Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi. $$ PSA 119:12 Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako. $$ PSA 119:13 Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako. $$ PSA 119:14 Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi. $$ PSA 119:15 Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako. $$ PSA 119:16 Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako. $$ PSA 119:17 Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako. $$ PSA 119:18 Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako. $$ PSA 119:19 Mimi ni mgeni duniani, usinifiche amri zako. $$ PSA 119:20 Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa juu ya sheria zako wakati wote. $$ PSA 119:21 Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako. $$ PSA 119:22 Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika sheria zako. $$ PSA 119:23 Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako. $$ PSA 119:24 Sheria zako ni furaha yangu, nazo ni washauri wangu. $$ PSA 119:25 Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. $$ PSA 119:26 Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako. $$ PSA 119:27 Nijulishe mafundisho ya mausia yako, nami nitatafakari maajabu yako. $$ PSA 119:28 Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako. $$ PSA 119:29 Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako. $$ PSA 119:30 Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako. $$ PSA 119:31 Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, usiniache niaibishwe. $$ PSA 119:32 Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru. $$ PSA 119:33 Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho. $$ PSA 119:34 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote. $$ PSA 119:35 Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha. $$ PSA 119:36 Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi. $$ PSA 119:37 Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. $$ PSA 119:38 Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa. $$ PSA 119:39 Niondolee aibu ninayoiogopa, kwa kuwa sheria zako ni njema. $$ PSA 119:40 Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako. $$ PSA 119:41 Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako, $$ PSA 119:42 ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako. $$ PSA 119:43 Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako. $$ PSA 119:44 Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele. $$ PSA 119:45 Nitatembea nikiwa huru, kwa kuwa nimejifunza mausia yako. $$ PSA 119:46 Nitasema sheria zako mbele za wafalme wala sitaaibishwa, $$ PSA 119:47 kwa kuwa ninazifurahia amri zako kwa sababu ninazipenda. $$ PSA 119:48 Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, nami ninatafakari juu ya maagizo yako. $$ PSA 119:49 Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini. $$ PSA 119:50 Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu. $$ PSA 119:51 Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, hata hivyo sitaiacha sheria yako. $$ PSA 119:52 Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani, nazo zinanifariji. $$ PSA 119:53 Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako. $$ PSA 119:54 Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi. $$ PSA 119:55 Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako. $$ PSA 119:56 Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako. $$ PSA 119:57 Ee Bwana, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako. $$ PSA 119:58 Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako. $$ PSA 119:59 Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako. $$ PSA 119:60 Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako. $$ PSA 119:61 Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako. $$ PSA 119:62 Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki. $$ PSA 119:63 Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao, kwa wote wanaofuata mausia yako. $$ PSA 119:64 Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako. $$ PSA 119:65 Mtendee wema mtumishi wako Ee Bwana, sawasawa na neno lako. $$ PSA 119:66 Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako. $$ PSA 119:67 Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako. $$ PSA 119:68 Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako. $$ PSA 119:69 Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote. $$ PSA 119:70 Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako. $$ PSA 119:71 Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako. $$ PSA 119:72 Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu. $$ PSA 119:73 Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako. $$ PSA 119:74 Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako. $$ PSA 119:75 Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu. $$ PSA 119:76 Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako. $$ PSA 119:77 Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako. $$ PSA 119:78 Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako. $$ PSA 119:79 Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako. $$ PSA 119:80 Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe. $$ PSA 119:81 Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako. $$ PSA 119:82 Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?” $$ PSA 119:83 Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako. $$ PSA 119:84 Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu? $$ PSA 119:85 Wenye majivuno wananichimbia mashimo, kinyume na sheria yako. $$ PSA 119:86 Amri zako zote ni za kuaminika; unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu. $$ PSA 119:87 Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako. $$ PSA 119:88 Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako. $$ PSA 119:89 Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni. $$ PSA 119:90 Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu. $$ PSA 119:91 Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia. $$ PSA 119:92 Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu. $$ PSA 119:93 Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu. $$ PSA 119:94 Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako. $$ PSA 119:95 Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako. $$ PSA 119:96 Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka. $$ PSA 119:97 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa. $$ PSA 119:98 Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima. $$ PSA 119:99 Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako. $$ PSA 119:100 Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako. $$ PSA 119:101 Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako. $$ PSA 119:102 Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe. $$ PSA 119:103 Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu! $$ PSA 119:104 Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu. $$ PSA 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu. $$ PSA 119:106 Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki. $$ PSA 119:107 Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana, sawasawa na neno lako. $$ PSA 119:108 Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako. $$ PSA 119:109 Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako. $$ PSA 119:110 Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako. $$ PSA 119:111 Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu. $$ PSA 119:112 Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho. $$ PSA 119:113 Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako. $$ PSA 119:114 Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako. $$ PSA 119:115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu! $$ PSA 119:116 Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa. $$ PSA 119:117 Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako. $$ PSA 119:118 Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure. $$ PSA 119:119 Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako. $$ PSA 119:120 Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako. $$ PSA 119:121 Nimetenda yaliyo haki na sawa, usiniache mikononi mwa watesi wangu. $$ PSA 119:122 Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee. $$ PSA 119:123 Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli. $$ PSA 119:124 Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako. $$ PSA 119:125 Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu ili niweze kuelewa sheria zako. $$ PSA 119:126 Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa. $$ PSA 119:127 Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi, $$ PSA 119:128 na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, nachukia kila njia potovu. $$ PSA 119:129 Sheria zako ni za ajabu, hivyo ninazitii. $$ PSA 119:130 Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu. $$ PSA 119:131 Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako. $$ PSA 119:132 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako. $$ PSA 119:133 Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale. $$ PSA 119:134 Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako. $$ PSA 119:135 Mwangazie mtumishi wako uso wako na unifundishe amri zako. $$ PSA 119:136 Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi. $$ PSA 119:137 Ee Bwana, wewe ni mwenye haki, sheria zako ni sahihi. $$ PSA 119:138 Sheria ulizoziweka ni za haki, ni za kuaminika kikamilifu. $$ PSA 119:139 Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu wanayapuuza maneno yako. $$ PSA 119:140 Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, mtumishi wako anazipenda. $$ PSA 119:141 Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, sisahau mausia yako. $$ PSA 119:142 Haki yako ni ya milele, na sheria yako ni kweli. $$ PSA 119:143 Shida na dhiki zimenipata, lakini amri zako ni furaha yangu. $$ PSA 119:144 Sheria zako ni sahihi milele, hunipa ufahamu ili nipate kuishi. $$ PSA 119:145 Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote, nami nitayatii maagizo yako. $$ PSA 119:146 Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako. $$ PSA 119:147 Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako. $$ PSA 119:148 Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako. $$ PSA 119:149 Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako. $$ PSA 119:150 Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, lakini wako mbali na sheria yako. $$ PSA 119:151 Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu, na amri zako zote ni za kweli. $$ PSA 119:152 Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele. $$ PSA 119:153 Yaangalie mateso yangu, uniokoe, kwa kuwa sijasahau sheria yako. $$ PSA 119:154 Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako. $$ PSA 119:155 Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako. $$ PSA 119:156 Ee Bwana, huruma zako ni kuu, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako. $$ PSA 119:157 Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako. $$ PSA 119:158 Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako. $$ PSA 119:159 Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako. $$ PSA 119:160 Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele. $$ PSA 119:161 Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako. $$ PSA 119:162 Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi. $$ PSA 119:163 Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo, lakini napenda sheria yako. $$ PSA 119:164 Ninakusifu mara saba kwa siku, kwa ajili ya sheria zako za haki. $$ PSA 119:165 Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza. $$ PSA 119:166 Ee Bwana, ninangojea wokovu wako, nami ninafuata amri zako, $$ PSA 119:167 Ninazitii sheria zako, kwa sababu ninazipenda mno. $$ PSA 119:168 Nimetii mausia yako na sheria zako, kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako. $$ PSA 119:169 Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako, nipe ufahamu sawasawa na neno lako. $$ PSA 119:170 Maombi yangu na yafike mbele zako, niokoe sawasawa na ahadi yako. $$ PSA 119:171 Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako. $$ PSA 119:172 Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki. $$ PSA 119:173 Mkono wako uwe tayari kunisaidia, kwa kuwa nimechagua mausia yako. $$ PSA 119:174 Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu. $$ PSA 119:175 Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, na sheria zako zinitegemeze. $$ PSA 119:176 Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. Mtafute mtumishi wako, kwa kuwa sijasahau amri zako. Zaburi 120 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 120:1 Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu. $$ PSA 120:2 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu. $$ PSA 120:3 Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu? $$ PSA 120:4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. $$ PSA 120:5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari! $$ PSA 120:6 Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani. $$ PSA 120:7 Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita. Zaburi 121 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 121:1 Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi? $$ PSA 121:2 Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. $$ PSA 121:3 Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, $$ PSA 121:4 hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. $$ PSA 121:5 Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, $$ PSA 121:6 jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku. $$ PSA 121:7 Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, $$ PSA 121:8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele. Zaburi 122 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. $$ PSA 122:1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.” $$ PSA 122:2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako. $$ PSA 122:3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja. $$ PSA 122:4 Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli. $$ PSA 122:5 Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. $$ PSA 122:6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama. $$ PSA 122:7 Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.” $$ PSA 122:8 Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.” $$ PSA 122:9 Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako. Zaburi 123 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 123:1 Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni. $$ PSA 123:2 Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mtumishi wa kike yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu, mpaka atakapotuhurumia. $$ PSA 123:3 Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi. $$ PSA 123:4 Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno. Zaburi 124 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. $$ PSA 124:1 Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa: $$ PSA 124:2 kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia, $$ PSA 124:3 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai, $$ PSA 124:4 mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika, $$ PSA 124:5 maji yaendayo kasi yangalituchukua. $$ PSA 124:6 Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. $$ PSA 124:7 Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka. $$ PSA 124:8 Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. Zaburi 125 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 125:1 Wale wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele. $$ PSA 125:2 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu, ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake sasa na hata milele. $$ PSA 125:3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi waliopewa wenye haki, ili wenye haki wasije wakatumia mikono yao kutenda ubaya. $$ PSA 125:4 Ee Bwana, watendee mema walio wema, wale walio wanyofu wa moyo. $$ PSA 125:5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya. Amani iwe juu ya Israeli. Zaburi 126 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 126:1 Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto. $$ PSA 126:2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “Bwana amewatendea mambo makuu.” $$ PSA 126:3 Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha. $$ PSA 126:4 Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu. $$ PSA 126:5 Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe. $$ PSA 126:6 Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake. Zaburi 127 Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni. $$ PSA 127:1 Bwana asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure. $$ PSA 127:2 Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake. $$ PSA 127:3 Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake. $$ PSA 127:4 Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. $$ PSA 127:5 Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni. Zaburi 128 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 128:1 Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake. $$ PSA 128:2 Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. $$ PSA 128:3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. $$ PSA 128:4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana. $$ PSA 128:5 Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, $$ PSA 128:6 nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli. Zaburi 129 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 129:1 Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: $$ PSA 129:2 wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. $$ PSA 129:3 Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. $$ PSA 129:4 Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. $$ PSA 129:5 Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. $$ PSA 129:6 Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; $$ PSA 129:7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. $$ PSA 129:8 Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.” Zaburi 130 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 130:1 Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana. $$ PSA 130:2 Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie. $$ PSA 130:3 Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama? $$ PSA 130:4 Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa. $$ PSA 130:5 Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu. $$ PSA 130:6 Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi. $$ PSA 130:7 Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili. $$ PSA 130:8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote. Zaburi 131 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. $$ PSA 131:1 Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu. $$ PSA 131:2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu. $$ PSA 131:3 Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele. Zaburi 132 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 132:1 Ee Bwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili. $$ PSA 132:2 Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: $$ PSA 132:3 “Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu: $$ PSA 132:4 sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia, $$ PSA 132:5 mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” $$ PSA 132:6 Tulisikia habari hii huko Efrathi, tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara: $$ PSA 132:7 “Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; $$ PSA 132:8 inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. $$ PSA 132:9 Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” $$ PSA 132:10 Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako. $$ PSA 132:11 Bwana alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe katika kiti chako cha enzi, $$ PSA 132:12 kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.” $$ PSA 132:13 Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake: $$ PSA 132:14 “Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku: $$ PSA 132:15 Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula. $$ PSA 132:16 Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha. $$ PSA 132:17 “Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu. $$ PSA 132:18 Adui zake nitawavika aibu, bali taji kichwani pake itangʼaa sana.” Zaburi 133 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. $$ PSA 133:1 Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! $$ PSA 133:2 Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. $$ PSA 133:3 Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele. Zaburi 134 Wimbo wa kwenda juu. $$ PSA 134:1 Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana. $$ PSA 134:2 Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana. $$ PSA 134:3 Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni. Zaburi 135 $$ PSA 135:1 Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana, $$ PSA 135:2 ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. $$ PSA 135:3 Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza. $$ PSA 135:4 Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani. $$ PSA 135:5 Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu, kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote. $$ PSA 135:6 Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote. $$ PSA 135:7 Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake. $$ PSA 135:8 Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama. $$ PSA 135:9 Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote. $$ PSA 135:10 Aliyapiga mataifa mengi, na akaua wafalme wenye nguvu: $$ PSA 135:11 Mfalme Sihoni na Waamori, Ogu mfalme wa Bashani na wafalme wote wa Kanaani: $$ PSA 135:12 akatoa nchi yao kuwa urithi, urithi kwa watu wake Israeli. $$ PSA 135:13 Ee Bwana, jina lako ladumu milele, kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote. $$ PSA 135:14 Maana Bwana atawathibitisha watu wake, na kuwahurumia watumishi wake. $$ PSA 135:15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. $$ PSA 135:16 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona; $$ PSA 135:17 zina masikio, lakini haziwezi kusikia, wala hakuna pumzi katika vinywa vyao. $$ PSA 135:18 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. $$ PSA 135:19 Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana; $$ PSA 135:20 ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana; ninyi mnaomcha, msifuni Bwana. $$ PSA 135:21 Msifuni Bwana kutoka Sayuni, msifuni yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Bwana. Zaburi 136 $$ PSA 136:1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:2 Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:3 Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:4 Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:5 Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:6 Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:7 Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:8 Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:9 Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:10 Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:11 Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:12 Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:13 Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:14 Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:15 Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:16 Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:17 Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:18 Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:19 Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:20 Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:21 Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:22 Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:23 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:24 Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:25 Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele. $$ PSA 136:26 Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele. Zaburi 137 $$ PSA 137:1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni. $$ PSA 137:2 Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu, $$ PSA 137:3 kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!” $$ PSA 137:4 Tutaimbaje nyimbo za Bwana, tukiwa nchi ya kigeni? $$ PSA 137:5 Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. $$ PSA 137:6 Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa. $$ PSA 137:7 Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, Bomoa mpaka kwenye misingi yake!” $$ PSA 137:8 Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, heri yeye atakayekulipiza wewe kwa yale uliyotutenda sisi: $$ PSA 137:9 yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga na kuwaponda juu ya miamba. Zaburi 138 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 138:1 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote, mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako. $$ PSA 138:2 Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote. $$ PSA 138:3 Nilipoita, ulinijibu; ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari. $$ PSA 138:4 Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana, wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. $$ PSA 138:5 Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana, kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu. $$ PSA 138:6 Ingawa Bwana yuko juu, humwangalia mnyonge, bali mwenye kiburi yeye anamjua kutokea mbali. $$ PSA 138:7 Nijapopita katikati ya shida, wewe unayahifadhi maisha yangu, unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, kwa mkono wako wa kuume unaniokoa. $$ PSA 138:8 Bwana atatimiza kusudi lake kwangu, Ee Bwana, upendo wako wadumu milele: usiziache kazi za mikono yako. Zaburi 139 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 139:1 Ee Bwana, umenichunguza na kunijua. $$ PSA 139:2 Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali. $$ PSA 139:3 Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. $$ PSA 139:4 Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana. $$ PSA 139:5 Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu. $$ PSA 139:6 Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, ni ya juu sana kwangu kuyafikia. $$ PSA 139:7 Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? $$ PSA 139:8 Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko. $$ PSA 139:9 Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko, kama nikikaa pande za mbali za bahari, $$ PSA 139:10 hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. $$ PSA 139:11 Kama nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” $$ PSA 139:12 hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako. $$ PSA 139:13 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. $$ PSA 139:14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu. $$ PSA 139:15 Umbile langu halikufichika kwako, nilipoumbwa mahali pa siri. Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, $$ PSA 139:16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwepo hata moja. $$ PSA 139:17 Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! Jinsi jumla yake ilivyo kubwa! $$ PSA 139:18 Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi kuliko mchanga. Niamkapo, bado niko pamoja nawe. $$ PSA 139:19 Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu! $$ PSA 139:20 Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, adui zako wanatumia vibaya jina lako. $$ PSA 139:21 Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako? $$ PSA 139:22 Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, ninawahesabu ni adui zangu. $$ PSA 139:23 Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu. $$ PSA 139:24 Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele. Zaburi 140 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. $$ PSA 140:1 Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu; nilinde na watu wenye jeuri, $$ PSA 140:2 ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, na kuchochea vita siku zote. $$ PSA 140:3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao. $$ PSA 140:4 Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu; nilinde na watu wenye jeuri wanaopanga kunikwaza miguu yangu. $$ PSA 140:5 Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, wametandaza kamba za wavu wao, wametega mitego kwenye njia yangu. $$ PSA 140:6 Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia. $$ PSA 140:7 Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, unikingaye kichwa changu siku ya vita: $$ PSA 140:8 Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao, usiache mipango yao ikafanikiwa, wasije wakajisifu. $$ PSA 140:9 Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida zinazosababishwa na midomo yao. $$ PSA 140:10 Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe. $$ PSA 140:11 Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri. $$ PSA 140:12 Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji. $$ PSA 140:13 Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako. Zaburi 141 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 141:1 Ee Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima. Sikia sauti yangu ninapokuita. $$ PSA 141:2 Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni. $$ PSA 141:3 Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu, weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu. $$ PSA 141:4 Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya, nisije nikashiriki katika matendo maovu pamoja na watu watendao mabaya, wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa. $$ PSA 141:5 Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma; na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu. Kichwa changu hakitalikataa. Hata hivyo, maombi yangu daima ni kinyume cha watenda mabaya, $$ PSA 141:6 watawala wao watatupwa chini kutoka kwenye majabali, waovu watajifunza kwamba maneno yangu yalikuwa kweli. $$ PSA 141:7 Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” $$ PSA 141:8 Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi, ndani yako nimekimbilia, usiniache nife. $$ PSA 141:9 Niepushe na mitego waliyonitegea, kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya. $$ PSA 141:10 Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe, wakati mimi ninapita salama. Zaburi 142 Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Maombi. $$ PSA 142:1 Namlilia Bwana kwa sauti, nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie. $$ PSA 142:2 Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu. $$ PSA 142:3 Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego. $$ PSA 142:4 Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu. $$ PSA 142:5 Ee Bwana, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.” $$ PSA 142:6 Sikiliza kilio changu, kwa sababu mimi ni mhitaji sana; niokoe na wale wanaonifuatilia, kwa kuwa wamenizidi nguvu. $$ PSA 142:7 Nifungue kutoka kifungo changu, ili niweze kulisifu jina lako. Ndipo wenye haki watanizunguka, kwa sababu ya wema wako kwangu. Zaburi 143 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 143:1 Ee Bwana, sikia sala yangu, sikiliza kilio changu unihurumie; katika uaminifu na haki yako njoo unisaidie. $$ PSA 143:2 Usimhukumu mtumishi wako, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako. $$ PSA 143:3 Adui hunifuatilia, hunipondaponda chini; hunifanya niishi gizani kama wale waliokufa zamani. $$ PSA 143:4 Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. $$ PSA 143:5 Nakumbuka siku za zamani; natafakari juu ya kazi zako zote, naangalia juu ya kazi ambazo mikono yako imezifanya. $$ PSA 143:6 Nanyoosha mikono yangu kwako, nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. $$ PSA 143:7 Ee Bwana, unijibu haraka, roho yangu inazimia. Usinifiche uso wako, ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni. $$ PSA 143:8 Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. Nionyeshe njia nitakayoiendea, kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. $$ PSA 143:9 Ee Bwana, uniokoe na adui zangu, kwa kuwa nimejificha kwako. $$ PSA 143:10 Nifundishe kufanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, Roho wako mwema na aniongoze katika nchi tambarare. $$ PSA 143:11 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu, kwa haki yako nitoe katika taabu. $$ PSA 143:12 Kwa upendo wako usiokoma, nyamazisha adui zangu; waangamize watesi wangu wote, kwa kuwa mimi ni mtumishi wako. Zaburi 144 Zaburi ya Daudi. $$ PSA 144:1 Sifa ni kwa Bwana Mwamba wangu, aifundishaye mikono yangu vita, na vidole vyangu kupigana. $$ PSA 144:2 Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, ngome yangu na mwokozi wangu, ngao yangu ninayemkimbilia, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. $$ PSA 144:3 Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie? $$ PSA 144:4 Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita. $$ PSA 144:5 Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, gusa milima ili itoe moshi. $$ PSA 144:6 Peleka umeme uwatawanye adui, lenga mishale yako uwashinde. $$ PSA 144:7 Nyoosha mkono wako kutoka juu, nikomboe na kuniokoa kutoka maji makuu, kutoka mikononi mwa wageni $$ PSA 144:8 ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. $$ PSA 144:9 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia, $$ PSA 144:10 kwa Yule awapaye wafalme ushindi, ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari. $$ PSA 144:11 Nikomboe na uniokoe kutoka mikononi mwa wageni ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. $$ PSA 144:12 Kisha wana wetu wakati wa ujana wao watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa kurembesha jumba la kifalme. $$ PSA 144:13 Ghala zetu zitajazwa aina zote za mahitaji. Kondoo zetu watazaa kwa maelfu, kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu; $$ PSA 144:14 maksai wetu watakokota mizigo mizito. Hakutakuwa na kubomoka kuta, hakuna kuchukuliwa mateka, wala kilio cha taabu katika barabara zetu. $$ PSA 144:15 Heri watu ambao hili ni kweli; heri wale ambao Bwana ni Mungu wao. Zaburi 145 Wimbo wa Sifa. Wa Daudi. $$ PSA 145:1 Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele. $$ PSA 145:2 Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele. $$ PSA 145:3 Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki. $$ PSA 145:4 Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu. $$ PSA 145:5 Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. $$ PSA 145:6 Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu. $$ PSA 145:7 Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako. $$ PSA 145:8 Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo. $$ PSA 145:9 Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya. $$ PSA 145:10 Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza. $$ PSA 145:11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako, $$ PSA 145:12 ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako. $$ PSA 145:13 Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. $$ PSA 145:14 Bwana huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao. $$ PSA 145:15 Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake. $$ PSA 145:16 Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. $$ PSA 145:17 Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. $$ PSA 145:18 Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. $$ PSA 145:19 Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa. $$ PSA 145:20 Bwana huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza. $$ PSA 145:21 Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele. Zaburi 146 $$ PSA 146:1 Msifuni Bwana! Ee nafsi yangu, umsifu Bwana, $$ PSA 146:2 Nitamsifu Bwana maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu sifa wakati wote niishipo. $$ PSA 146:3 Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa. $$ PSA 146:4 Roho yao itokapo hurudi mavumbini, siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma. $$ PSA 146:5 Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake, $$ PSA 146:6 Muumba wa mbingu na nchi, na bahari na vyote vilivyomo ndani yake: Bwana anayedumu kuwa mwaminifu milele na milele. $$ PSA 146:7 Naye huwapatia haki walioonewa na kuwapa wenye njaa chakula. Bwana huwaweka wafungwa huru, $$ PSA 146:8 Bwana huwafumbua vipofu macho, Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao, Bwana huwapenda wenye haki. $$ PSA 146:9 Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu. $$ PSA 146:10 Bwana atamiliki milele, Mungu wako, ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Bwana. Zaburi 147 $$ PSA 147:1 Msifuni Bwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye! $$ PSA 147:2 Bwana hujenga Yerusalemu, huwakusanya Israeli walio uhamishoni. $$ PSA 147:3 Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao. $$ PSA 147:4 Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake. $$ PSA 147:5 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo. $$ PSA 147:6 Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini. $$ PSA 147:7 Mwimbieni Bwana kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi. $$ PSA 147:8 Yeye huzifunika anga kwa mawingu, huinyeshea ardhi mvua, na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima. $$ PSA 147:9 Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia. $$ PSA 147:10 Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu. $$ PSA 147:11 Bwana hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma. $$ PSA 147:12 Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu, msifu Mungu wako, ee Sayuni, $$ PSA 147:13 kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako. $$ PSA 147:14 Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa. $$ PSA 147:15 Hutuma amri yake duniani, neno lake hukimbia kasi. $$ PSA 147:16 Anatandaza theluji kama sufu na kutawanya umande kama majivu. $$ PSA 147:17 Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake? $$ PSA 147:18 Hutuma neno lake na kuviyeyusha, huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka. $$ PSA 147:19 Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli. $$ PSA 147:20 Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, hawazijui sheria zake. Msifuni Bwana. Zaburi 148 $$ PSA 148:1 Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni. $$ PSA 148:2 Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. $$ PSA 148:3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo. $$ PSA 148:4 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga. $$ PSA 148:5 Vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa. $$ PSA 148:6 Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele. $$ PSA 148:7 Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari, $$ PSA 148:8 umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake, $$ PSA 148:9 ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote, $$ PSA 148:10 wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao, $$ PSA 148:11 wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia, $$ PSA 148:12 wanaume vijana na wanawali, wazee na watoto. $$ PSA 148:13 Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu. $$ PSA 148:14 Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana. Zaburi 149 $$ PSA 149:1 Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu. $$ PSA 149:2 Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao. $$ PSA 149:3 Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi. $$ PSA 149:4 Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu. $$ PSA 149:5 Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao. $$ PSA 149:6 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao, $$ PSA 149:7 ili walipize mataifa kisasi na adhabu juu ya mataifa, $$ PSA 149:8 wawafunge wafalme wao kwa minyororo, wakuu wao kwa pingu za chuma, $$ PSA 149:9 ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Bwana. Zaburi 150 $$ PSA 150:1 Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu. $$ PSA 150:2 Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. $$ PSA 150:3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze, $$ PSA 150:4 msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, $$ PSA 150:5 msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana. $$ PSA 150:6 Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!