NENO
BIBLIA TAKATIFU
 
AGANO LA KALE
NA
AGANO JIPYA
 
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
 
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
 
“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc. Used with permission.
 
  ――――――
 
This work is made available under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 4‪.0 International License (CC BY-SA). To view a copy of this license, visit http://creativecommons.org/licenses/by-sa/4‪.0 or send a letter to Creative Commons, PO Box 1866, Mountain View, CA 94042, USA.
  ‪
‪Biblica® is a trademark registered by Biblica, Inc., and use of the Biblica® trademark requires the written permission of Biblica, Inc. Under the terms of the CC BY-SA license, you may copy and redistribute this unmodified work as long as you keep the Biblica® trademark intact. If you modify a copy or translate this work, thereby creating a derivative work, you must remove the Biblica® trademark. On the derivative work, you must indicate what changes you have made and attribute the work as follows: “The original work by Biblica, Inc. is available for free at www.biblica.com and open.bible.”
 
‪Notice of copyright must appear on the title or copyright page of the work as follows:
 
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
 
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
 
“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc. Used with permission.
  ‪
‪You must also make your derivative work available under the same license (CC BY-SA).
  ‪
‪If you would like to notify Biblica, Inc. regarding your translation of this work, please contact us at https://open.bible/contact-us.
 
  ――――――
 
Dibaji
Hii ni tafsiri mpya ya Neno la Mungu katika lugha ya Kiswahili. Tafsiri hii ya Neno: Biblia Takatifu imetafsiriwa na Wakristo kutoka Tanzania na Kenya wa madhehebu mbalimbali. Imefanywa kwa ajili ya kutumiwa na Wakristo wa Kanisa la Mungu katika nchi zote ambako Kiswahili hutumika kama lugha ya mawasiliano.
Ziko tafsiri mbalimbali zilizotangulia kufanywa za Agano la Kale na Agano Jipya. Tunawashukuru sana wale waliofanya tafsiri hizi ambazo zimekuwa baraka kubwa kiroho. Basi kama ilivyo ada, lugha hukua. Kutokana na kukua huku, maneno mapya, misamiati, na hata matumizi hubadilika. Kadri mabadiliko yanavyotokea, watu wanajipata wakihitaji kupata ufahamu wa kiroho katika lugha itakayoeleweka kwa wepesi, bila kupoteza ile maana ya asili, usahihi, na uwazi ambavyo vitamwezesha msomaji kuelewa vyema yale anayoyasoma. Kutokana na hayo, imeonekana ni vyema kuwa na tafsiri hii ambayo itaeleweka kwa urahisi, na hatimaye kujenga umoja wa kiroho katika Kanisa la Mungu.
Tafsiri hii ya Neno: Biblia Takatifu ni toleo la kwanza ambalo limezingatia tafsiri za lugha za awali ili kupata maana zilizokusudiwa, na kuhakikisha kwamba kila neno limehakikiwa kwa ajili ya kuondoa utata wowote ambao ungeweza kujitokeza. Tafsiri hii ilipoanza kufanywa, ilipasa kutumia tafsiri mbalimbali za zamani au zilizotangulia ili kuweza kupata tafsiri ambayo itakidhi haja, njaa na kiu ya msomaji. Tulijitahidi kuepuka kila neno ambalo lingepunguza nguvu na mamlaka ya Neno la Mungu. Hivyo tulimwomba Roho Mtakatifu atupe neno au maneno yatakayobeba ujumbe alioukusudia. Kwa msingi huo, isidhaniwe kwamba kwenye tafsiri hii kuna mageuzi yoyote yaliyofanywa kwa Neno la Mungu. Jambo hilo kamwe halikufanyika.
Inatubidi tujue na tukumbuke kwamba Neno la Mungu halikuandikwa kwanza kwa Kiingereza wala Kiswahili. Roho Mtakatifu aliwavuvia watu watakatifu wa kale, yaani, Wayahudi na Wakristo, ili kuudhihirisha na kuutangaza ujumbe wa Mungu. Wayahudi waliandika ujumbe huo kwa Kiebrania na Kiaramu (iliyokuwa lugha ya biashara) na mahali pengine Kikaldayo katika Agano la Kale. Wakristo ambao idadi yao kubwa walikuwa watu wenye asili ya Kiyahudi waliandika Agano Jipya kwa Kiyunani, iliyokuwa lugha rasmi ya mawasiliano na biashara wakati huo. Kiaramu pia kimetumika sehemu mbalimbali.
Hivyo basi, watu wanaotafsiri Biblia katika lugha za kisasa kwanza huwa waangilifu sana ili kuhifadhi maana ya maneno ya asili ya lugha za awali, kisha hujitahidi kuandika tafsiri iliyo halisi. Haiwezekani kupata maana, mtiririko na ufahamu ikiwa ni tafsiri sisisi, yaani tafsiri ya neno kwa neno. Hivyo, watafsiri wa toleo hili wamezingatia umuhimu na kueleweka kwa neno husika. Wameepuka kutumia fafanusi na fasiri ambazo zingeadhiri maana za asili. Basi katika tafsiri hii, tumejitahidi kutumia maneno yanayoleta maana iliyokusudiwa na waandishi.
Watafsiri wamejaribu kuepuka mgongano wowote ambao ungeweza kujitokeza katika matumizi ya majina. Kwa mfano, Jina la Mungu katika Agano la Kale “Yehova,” yaani, “Yhwh” kwa Kiebrania, limeandikwa Bwana, ikiwa na maana Yehova. Majina ya watu imebidi yafikiriwe na kuwekwa katika asili yake, kwa mfano Eva, Noa, Abrahamu, Yosefu, Mose, Maria, na kadhalika. Kwa hivyo majina ya watu na ya mahali imebidi yarekebishwe, jambo ambalo limeifanya kazi kuwa kubwa sana, kwani lilihitaji hadhari kubwa. Pale ambapo ilionekana neno halijulikani sana na hapatakuwa na budi kulitumia, neno hilo limewekwa kwenye rejeo chini ya ukurasa, au orodha ya maneno magumu mwishoni mwa kitabu, ili kumsaidia msomaji kupata maana.
Wakristo wote wanafahamu matumizi ya neno “Amin” au “Amen” kwa sababu yametumika kwa muda mrefu. Neno “Amin” linapotumika mwanzo wa usemi lina maana “Ni kweli.” Neno “Amen” linapotumika mwisho wa usemi lina maana “Iwe hivyo.”
Toleo hili limezingatia kuweka vidokezo mbalimbali vya kumsaidia msomaji kutumia na kuweza kuelewa vizuri anaposoma Biblia. Baadhi ya vidokezo hivi ni: Utangulizi wa kila kitabu, kuweka vichwa vikuu na vidogo, kuweka maelezo ya neno au maneno ya Biblia ya asili chini ya ukurasa (rejeo), sura na aya zilizokolezwa, Itifaki, orodha ya maneno magumu, ramani na vielelezo, tabia za wanafunzi wa Yesu, uoanisho wa Injili, na utimilizo wa unabii wa Masiya katika Agano Jipya.
Tunawasihi mtuombee sisi tulioshirikiana katika kazi hii, ili Mungu atubariki sisi, na matunda ya kazi hii yawe mengi, tena yatakayompa Mungu utukufu. Maombi yetu ni kwamba Neno la Mungu litakuwa nuru kwa wengi, na litasababisha waijue kweli ya Mungu. Pia Neno la Mungu lilete umoja wa imani katika Kanisa la Mungu.
Nasi tunawaombea ninyi mtakaosoma Biblia hii, kwamba Roho Mtakatifu awape ufunuo wa kweli, na hili Neno liwe halisi katika maisha yenu ya kila siku. Mwisho, ombeni ili Roho Mtakatifu aiangazie mioyo ya wote wasomao na kutumia hili Neno, waweze kudumisha na kuendeleza utukufu Wake na kulijenga Kanisa la Yesu Kristo Bwana wetu.
 
Ni sisi,
Wenye kutafsiri.
Majina na Taratibu ya Vitabu Vyote Vya
AGANO LA KALE
Mwanzo (Mwa) 1
AGANO JIPYA
Mathayo (Mt) ####
AGANO LA KALE
AGANO JIPYA