1 Mambo Ya Nyakati 11 Mambo Ya NyakatiKumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Abrahamu (Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26) Adamu Hadi Wana Wa Noa

1 1:1Adamu, Sethi, Enoshi, 2 1:2Kenani, Mahalaleli, Yaredi, 3 1:3Enoki, Methusela, Lameki, Noa.

  • 4 1:4Wana wa Noa walikuwa:
  • Shemu, Hamu na Yafethi. Wana Wa Yafethi
  • 5 1:5Wana wa Yafethi walikuwa:
  • Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
  • 6 1:6Wana wa Gomeri walikuwa:
  • Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
  • 7 1:7Wana wa Yavani walikuwa:
  • Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Wana Wa Hamu
  • 8 1:8Wana wa Hamu walikuwa:
  • Kushi, Misraimu, 1:8 Yaani Misri. Putu na Kanaani.
  • 9 1:9Wana wa Kushi walikuwa:
  • Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
  • Wana wa Raama walikuwa:
  • Sheba na Dedani.
  • 10 1:10Kushi akamzaa
  • Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.
  • 11 1:11Misraimu akawazaa:
  • Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 12 1:12Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.
  • 13 1:13Wana wa Kanaani walikuwa:
  • Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, 14 1:14Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 15 1:15Wahivi, Waariki, Wasini, 16 1:16Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana Wa Shemu
  • 17 1:17Wana wa Shemu walikuwa:
  • Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
  • Wana wa Aramu walikuwa:
  • Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
  • 18 1:18Arfaksadi akamzaa Shela,
  • Shela akamzaa Eberi.
  • 19 1:19Eberi alipata wana wawili:
  • Mmoja wao aliitwa Pelegi, 1:19 Pelegi maana yake Mgawanyiko. kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
  • 20 1:20Wana wa Yoktani walikuwa:
  • Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 21 1:21Hadoramu, Uzali, Dikla, 22 1:22Obali, Abimaeli, Sheba, 23 1:23Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani. 24 1:24Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela, 25 1:25Eberi, Pelegi, Reu, 26 1:26Serugi, Nahori, Tera, 27 1:27Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu). Jamaa Ya Abrahamu
  • 28 1:28Abrahamu alikuwa na wana wawili:
  • Isaki na Ishmaeli. Wazao Wa Hagari (Mwanzo 25:12-16)
  • 29 1:29Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:
  • Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 30 1:30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31 1:31Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Wazao Wa Ketura
  • 32 1:32Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:
  • Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.
  • Wana wa Yokshani walikuwa:
  • Sheba na Dedani.
  • 33 1:33Wana wa Midiani walikuwa:
  • Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.
  • Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.
  • Wazao Wa Sara
  • 34 1:34Abrahamu alikuwa baba wa Isaki.
  • Wana wa Isaki walikuwa:
  • Esau na Israeli. Wana Wa Esau (Mwanzo 36:1-19)
  • 35 1:35Wana wa Esau walikuwa:
  • Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
  • 36 1:36Wana wa Elifazi walikuwa:
  • Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi; Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.
  • 37 1:37Wana wa Reueli walikuwa:
  • Nahathi, Zera, Shama na Miza. Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu (Mwanzo 36:20-30)
  • 38 1:38Wana wa Seiri walikuwa:
  • Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
  • 39 1:39Wana wa Lotani walikuwa wawili:
  • Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
  • 40 1:40Wana wa Shobali walikuwa:
  • Alvani, 1:40 Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian. Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
  • Wana wa Sibeoni walikuwa:
  • Aiya na Ana.
  • 41 1:41Mwana wa Ana alikuwa:
  • Dishoni.
  • Nao wana wa Dishoni walikuwa:
  • Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
  • 42 1:42Wana wa Eseri walikuwa:
  • Bilhani, Zaavani na Akani.
  • Wana wa Dishani walikuwa:
  • Usi na Arani. Watawala Wa Edomu (Mwanzo 36:31-43)
  • 43 1:43Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:
  • Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba. 44 1:44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. 45 1:45Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. 46 1:46Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. 47 1:47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. 48 1:48Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake. 49 1:49Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. 50 1:50Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 51 1:51Naye Hadadi pia akafa.
  • Wakuu wa Edomu walikuwa:
  • Timna, Alva, Yethethi, 52 1:52Oholibama, Ela, Pinoni, 53 1:53Kenazi, Temani, Mibsari, 54 1:54Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu. 2Wana Wa Israeli
  • 1 2:1Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:
  • Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, 2 2:2Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri. Yuda Hadi Wana Wa Hesroni
  • 3 2:3Wana wa Yuda walikuwa:
  • Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua. 4 2:4Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.
  • 5 2:5Wana wa Peresi walikuwa:
  • Hesroni na Hamuli.
  • 6 2:6Wana wa Zera walikuwa:
  • Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
  • 7 2:7Mwana wa Karmi alikuwa:
  • Akari, 2:7 Akari maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yos 6:1-26; 22:20). ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.
  • 8 2:8Mwana wa Ethani alikuwa:
  • Azariya.
  • 9 2:9Wana wa Hesroni walikuwa:
  • Yerameeli, Ramu na Kalebu. Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni
  • 10 2:10Ramu alimzaa
  • Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda. 11 2:11Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, 12 2:12Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.
  • 13 2:13Yese akawazaa
  • Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea, 2:13 Au: Shima, maana yake Sifa njema (pia 1Sam 16:9; 17:13). 14 2:14wa nne Nethaneli, wa tano Radai, 15 2:15wa sita Osemu, na wa saba Daudi. 16 2:16Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli. 17 2:17Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli. Kalebu Mwana Wa Hesroni
  • 18 2:18Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni. 19 2:19Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri. 20 2:20Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.
  • 21 2:21Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu. 22 2:22Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi. 23 2:23(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.
  • 24 2:24Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.
  • Yerameeli Mwana Wa Hesroni
  • 25 2:25Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:
  • Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. 26 2:26Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.
  • 27 2:27Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:
  • Maasi, Yamini na Ekeri.
  • 28 2:28Wana wa Onamu walikuwa:
  • Shamai na Yada.
  • Wana wa Shamai walikuwa:
  • Nadabu na Abishuri.
  • 29 2:29Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.
  • 30 2:30Wana wa Nadabu walikuwa
  • Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.
  • 31 2:31Apaimu akamzaa:
  • Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani. Sheshani akamzaa Alai.
  • 32 2:32Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:
  • Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.
  • 33 2:33Wana wa Yonathani walikuwa:
  • Pelethi na Zaza.
  • Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.
  • 34 2:34Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu.
  • Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha. 35 2:35Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.
  • 36 2:36Atai akamzaa Nathani,
  • Nathani akamzaa Zabadi, 37 2:37Zabadi akamzaa Eflali, Eflali akamzaa Obedi, 38 2:38Obedi akamzaa Yehu, Yehu akamzaa Azaria, 39 2:39Azaria akamzaa Helesi, Helesi akamzaa Eleasa, 40 2:40Eleasa akamzaa Sismai, Sismai akamzaa Shalumu, 41 2:41Shalumu akamzaa Yekamia, naye Yekamia akamzaa Elishama. Koo Za Kalebu
  • 42 2:42Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:
  • Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.
  • 43 2:43Hebroni alikuwa na wana wanne:
  • Kora, Tapua, Rekemu na Shema. 44 2:44Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai. 45 2:45Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.
  • 46 2:46Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.
  • 47 2:47Wana wa Yadai walikuwa:
  • Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
  • 48 2:48Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana. 49 2:49Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa. 50 2:50Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu.
  • Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa:
  • Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu, 51 2:51Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.
  • 52 2:52Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:
  • Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi, 53 2:53pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.
  • 54 2:54Wazao wa Salma walikuwa:
  • Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori, 55 2:55pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu. 3Wana Wa Daudi
  • 1 3:1Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:
  • Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli; 2 3:2wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi; 3 3:3wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali; wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla. 4 3:4Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita. Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu, 5 3:5nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, 3:5 Sawa na Shimea; maana yake ni Mashuhuri, Maarufu. Shobabu, Nathani na Solomoni. 6 3:6Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti, 7 3:7Noga, Nefegi, Yafia, 8 3:8Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa. 9 3:9Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao. Wafalme Wa Yuda
  • 10 3:10Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu,
  • mwanawe huyo alikuwa Abiya, mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati, mwanawe huyo alikuwa Asa, 11 3:11mwanawe huyo alikuwa Yehoramu, mwanawe huyo alikuwa Ahazia, mwanawe huyo alikuwa Yoashi, 12 3:12mwanawe huyo alikuwa Amazia, mwanawe huyo alikuwa Azaria, mwanawe huyo alikuwa Yothamu, 13 3:13mwanawe huyo alikuwa Ahazi, mwanawe huyo alikuwa Hezekia, mwanawe huyo alikuwa Manase, 14 3:14mwanawe huyo alikuwa Amoni na mwanawe huyo alikuwa Yosia.
  • 15 3:15Wana wa Yosia walikuwa:
  • Yohanani mzaliwa wake wa kwanza, Yehoyakimu mwanawe wa pili, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
  • 16 3:16Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni:
  • Yekonia mwanawe, na Sedekia. Ukoo Wa Kifalme Baada Ya Uhamisho
  • 17 3:17Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka:
  • Shealtieli mwanawe, 18 3:18Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.
  • 19 3:19Wana wa Pedaya walikuwa:
  • Zerubabeli na Shimei.
  • Wana wa Zerubabeli walikuwa:
  • Meshulamu na Hanania. Shelomithi alikuwa dada yao. 20 3:20Pia walikuwepo wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.
  • 21 3:21Wazao wa Hanania walikuwa:
  • Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
  • 22 3:22Wazao wa Shekania:
  • Shemaya na wanawe: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.
  • 23 3:23Wana wa Nearia walikuwa:
  • Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.
  • 24 3:24Wana wa Elioenai walikuwa:
  • Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba. 4Koo Nyingine Za Yuda
  • 1 4:1Wana wa Yuda walikuwa:
  • Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.
  • 2 4:2Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Wasorathi.
  • 3 4:3Hawa ndio waliokuwa wana wa Etamu:
  • Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi. 4 4:4Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha.
  • Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu.
  • 5 4:5Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
  • 6 4:6Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.
  • 7 4:7Wana wa Hela walikuwa:
  • Serethi, Sohari, Ethnani, 8 4:8na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.

    9 4:9Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.” 10 4:10Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

  • 11 4:11Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni. 12 4:12Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Iri-Nahashi. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Reka.
  • 13 4:13Wana wa Kenazi walikuwa:
  • Othnieli na Seraya.
  • Wana wa Othnieli walikuwa:
  • Hathathi na Meonathai. 14 4:14Meonathai akamzaa Ofra.
  • Seraya akamzaa Yoabu,
  • baba wa Ge-Harashimu. 4:14 Maana yake Bonde la Mafundi. Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi.
  • 15 4:15Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu:
  • Iru, Ela na Naamu.
  • Naye mwana wa Ela alikuwa:
  • Kenazi.
  • 16 4:16Wana wa Yahaleleli walikuwa:
  • Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.
  • 17 4:17Wana wa Ezra walikuwa:
  • Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Mmojawapo wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa. 18 4:18Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa.
  • 19 4:19Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa:
  • baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi.
  • 20 4:20Wana wa Shimoni walikuwa:
  • Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni.
  • Wazao wa Ishi walikuwa:
  • Zohethi na Ben-Zohethi.
  • 21 4:21Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa:
  • Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi waliokuwa wakiishi huko Beth-Ashbea, 22 4:22Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yashubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.) 23 4:23Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme. Simeoni
  • 24 4:24Wazao wa Simeoni walikuwa:
  • Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli. 25 4:25Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma.
  • 26 4:26Wazao wa Mishma walikuwa:
  • Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei.

    27 4:27Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda. 28 4:28Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hasar-Shuali, 29 4:29Bilha, Esemu, Toladi, 30 4:30Bethueli, Horma, Siklagi, 31 4:31Beth-Markabothi, Hasar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi. 32 4:32Vijiji vilivyoizunguka vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani; jumla miji mitano: 33 4:33pamoja na vijiji vyote kuizunguka hii miji hadi huko Baali. Haya yalikuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao.

    34 4:34Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia, 35 4:35Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli. 36 4:36Pia Elioenai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya, 37 4:37Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya.

    38 4:38Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao. Jamaa zao ziliongezeka sana, 39 4:39wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. 40 4:40Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.

    41 4:41Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao. 42 4:42Watu wa kabila la wa Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri. 43 4:43Wakawaua Waamaleki waliobaki, waliokuwa wamenusurika, nao wanaishi huko hadi leo.

    5Wana Wa Reubeni

    1 5:1Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa. 2 5:2Na ingawa Yuda alikuwa na nguvu zaidi ya ndugu zake wote, na mtawala alitoka kwake, haki za mzaliwa wa kwanza zilikuwa za Yosefu.) 3 5:3Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli walikuwa:

  • Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.
  • 4 5:4Wazao wa Yoeli walikuwa:
  • Shemaya mwanawe, Gogu mwanawe; Shimei mwanawe, 5 5:5Mika mwanawe, Reaya mwanawe, Baali mwanawe, 6 5:6na Beera mwanawe, ambaye Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alimchukua kwenda uhamishoni. Beera alikuwa kiongozi wa Wareubeni.
  • 7 5:7Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa kufuata koo zao kama ifuatavyo:
  • Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria, 8 5:8Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni. 9 5:9Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi. 10 5:10Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi. Wana Wa Gadi
  • 11 5:11Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka.
  • 12 5:12Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani.
  • 13 5:13Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba:
  • Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi. 14 5:14Hawa walikuwa ndio wana wa Abihaili mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yahdo, mwana wa Buzi. 15 5:15Ahi mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa ndiye kiongozi wa jamaa yao.
  • 16 5:16Wagadi waliishi Gileadi, huko Bashani pamoja na vijiji vilivyoizunguka, pia katika nchi yote ya malisho ya Sharoni kote walikoenea.
  • 17 5:17Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.

    18 5:18Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo. 19 5:19Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu. 20 5:20Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea. 21 5:21Walitwaa mifugo ya Wahagari: ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000. Pia wakateka watu 100,000, 22 5:22na wengine wengi waliuawa kwa sababu vita vilikuwa ni vya Mungu. Nao waliendelea kuikalia nchi hiyo mpaka wakati wa uhamisho.

    Nusu Ya Kabila La Manase

    23 5:23Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni.

    24 5:24Hawa ndio waliokuwa viongozi wa jamaa za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yahdieli. Walikuwa askari shujaa watu maarufu, viongozi wa jamaa zao. 25 5:25Lakini hawakuwa waaminifu kwa Mungu wa baba zao, nao wakafanya ukahaba kwa miungu ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameyaangamiza mbele yao. 26 5:26Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

    6Wana Wa Lawi
  • 1 6:1Wana wa Lawi walikuwa:
  • Gershoni, Kohathi na Merari.
  • 2 6:2Wana wa Kohathi walikuwa:
  • Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
  • 3 6:3Amramu alikuwa na wana:
  • Aroni, Mose, na Miriamu.
  • Aroni alikuwa na wana:
  • Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 4 6:4Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, 5 6:5Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, 6 6:6Uzi akamzaa Zerahia, Zerahia akamzaa Merayothi, 7 6:7Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 8 6:8Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi, 9 6:9Ahimaasi akamzaa Azaria, Azaria akamzaa Yohanani, 10 6:10Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu), 11 6:11Azaria akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 12 6:12Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Shalumu, 13 6:13Shalumu akamzaa Hilkia, Hilkia akamzaa Azaria, 14 6:14Azaria akamzaa Seraya, Seraya akamzaa Yehosadaki. 15 6:15Yehosadaki alihamishwa wakati Bwana aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.
  • 16 6:16Wana wa Lawi walikuwa:
  • Gershoni, Kohathi na Merari.
  • 17 6:17Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:
  • Libni na Shimei.
  • 18 6:18Wana wa Kohathi walikuwa:
  • Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
  • 19 6:19Wana wa Merari walikuwa:
  • Mahli na Mushi.
  • Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao:
  • 20 6:20Wazao wa Gershoni:
  • Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima, 21 6:21Zima akamzaa Yoa, Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, Zera akamzaa Yeatherai.
  • 22 6:22Wazao wa Kohathi:
  • Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, Kora akamzaa Asiri, 23 6:23Asiri akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri, 24 6:24Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.
  • 25 6:25Wazao wa Elikana walikuwa:
  • Amasai na Ahimothi, 26 6:26Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi, 27 6:27Nahathi akamzaa Eliabu, Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Samweli.
  • 28 6:28Wana wa Samweli walikuwa:
  • Yoeli mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya mwanawe wa pili.
  • 29 6:29Wafuatao ndio wazao wa Merari:
  • Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza, 30 6:30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya. Waimbaji Wa Hekalu

    31 6:31Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32 6:32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

    33 6:33Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:

  • Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
  • Hemani, mpiga kinanda, alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli, 34 6:34mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa, 35 6:35mwana wa Sufu, mwana wa Elikana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai, 36 6:36mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania, 37 6:37mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, 38 6:38mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;
  • 39 6:39na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:
  • Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea, 40 6:40mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya, 41 6:41mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaya, 42 6:42mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei, 43 6:43mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.
  • 44 6:44Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:
  • Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki, 45 6:45mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia, 46 6:46mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri, 47 6:47mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

    48 6:48Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. 49 6:49Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.

  • 50 6:50Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:
  • Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, 51 6:51Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia, 52 6:52Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 53 6:53Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi.

    54 6:54Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

    55 6:55Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka. 56 6:56Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune. 57 6:57Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, 58 6:58Hileni, Debiri, 59 6:59Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. 60 6:60Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho. Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.

    61 6:61Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

    62 6:62Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

    63 6:63Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

    64 6:64Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho. 65 6:65Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

    66 6:66Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.

    67 6:67Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, 68 6:68Yokmeamu, Beth-Horoni, 69 6:69Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho. 70 6:70Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.
  • 71 6:71Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:
  • Katika nusu ya kabila la Manase:
  • walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
  • 72 6:72Kutoka kabila la Isakari
  • walipokea Kedeshi, Daberathi, 73 6:73Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
  • 74 6:74Kutoka kabila la Asheri
  • walipokea Mashali, Abdoni, 75 6:75Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
  • 76 6:76Kutoka kabila la Naftali
  • walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
  • 77 6:77Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:
  • kutoka kabila la Zabuloni walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.
  • 78 6:78Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko
  • walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa, 79 6:79Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.
  • 80 6:80Na kutoka kabila la Gadi
  • walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu, 81 6:81Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho. 7Wana Wa Isakari
  • 1 7:1Wana wa Isakari walikuwa:
  • Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.
  • 2 7:2Wana wa Tola walikuwa:
  • Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.
  • 3 7:3Mwana wa Uzi alikuwa:
  • Izrahia.
  • Wana wa Izrahia walikuwa:
  • Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. 4 7:4Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.
  • 5 7:5Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.
  • Wana Wa Benyamini
  • 6 7:6Wana watatu wa Benyamini walikuwa:
  • Bela, Bekeri na Yediaeli.
  • 7 7:7Wana wa Bela walikuwa:
  • Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.
  • 8 7:8Wana wa Bekeri walikuwa:
  • Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. 9 7:9Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.
  • 10 7:10Mwana wa Yediaeli alikuwa:
  • Bilhani.
  • Wana wa Bilhani walikuwa:
  • Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. 11 7:11Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
  • 12 7:12Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.
  • Wana Wa Naftali
  • 13 7:13Wana wa Naftali walikuwa:
  • Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha. Wana Wa Manase
  • 14 7:14Wana wa Manase walikuwa:
  • Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. 15 7:15Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu. 16 7:16Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.
  • 17 7:17Mwana wa Ulamu alikuwa:
  • Bedani.
  • Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase. 18 7:18Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.
  • 19 7:19Wana wa Shemida walikuwa:
  • Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu. Wana Wa Efraimu
  • 20 7:20Wana wa Efraimu walikuwa:
  • Shuthela, ambaye alimzaa Beredi, Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada, Eleada akamzaa Tahathi, 21 7:21Tahathi akamzaa Zabadi, na Zabadi akamzaa Shuthela. Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. 22 7:22Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. 23 7:23Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. 24 7:24Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.
  • 25 7:25Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,
  • Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani, 26 7:26Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama, 27 7:27Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua.

    28 7:28Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. 29 7:29Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.

    Wana Wa Asheri
  • 30 7:30Wana wa Asheri walikuwa:
  • Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.
  • 31 7:31Wana wa Beria walikuwa:
  • Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.
  • 32 7:32Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.
  • 33 7:33Wana wa Yafleti walikuwa:
  • Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti.
  • 34 7:34Wana wa Shemeri walikuwa:
  • Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.
  • 35 7:35Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa:
  • Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.
  • 36 7:36Wana wa Sofa walikuwa:
  • Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, 37 7:37Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani 7:37 Kwa jina lingine Yetheri. na Beera.
  • 38 7:38Wana wa Yetheri walikuwa:
  • Yefune, Pispa na Ara.
  • 39 7:39Wana wa Ula walikuwa:
  • Ara, Hanieli na Risia.

    40 7:40Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.

    8Ukoo Wa Sauli Mbenyamini
  • 1 8:1Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza,
  • Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu, 2 8:2Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.
  • 3 8:3Wana wa Bela walikuwa:
  • Adari, Gera, Abihudi, 4 8:4Abishua, Naamani, Ahoa, 5 8:5Gera, Shefufani na Huramu.
  • 6 8:6Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:
  • 7 8:7Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.
  • 8 8:8Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara. 9 8:9Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, 10 8:10Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. 11 8:11Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.
  • 12 8:12Wana wa Elpaali walikuwa:
  • Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka), 13 8:13na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.
  • 14 8:14Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15 8:15Zebadia, Aradi, Ederi, 16 8:16Mikaeli, Ishpa, na Yoha.
  • 17 8:17Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, 18 8:18Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.
  • 19 8:19Yakimu, Zikri, Zabdi, 20 8:20Elienai, Silethai, Elieli, 21 8:21Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.
  • 22 8:22Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, 23 8:23Abdoni, Zikri, Hanani, 24 8:24Hanania, Elamu, Anthothiya, 25 8:25Ifdeya na Penueli.
  • 26 8:26Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27 8:27Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.
  • 28 8:28Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

  • 29 8:29Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.
  • Mke wake aliitwa Maaka. 30 8:30Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 31 8:31Gedori, Ahio, Zekeri, 32 8:32na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
  • 33 8:33Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.
  • 34 8:34Yonathani akamzaa:
  • Merib-Baali, 8:34 Merib-Baali maana yake ni Baali na Ashindane naye (Amu 6:32); ni jina lingine la mwana wa Yonathani, Mefiboshethi ambalo nalo maana yake ni Mtu wa Aibu (ona 2Sam 4:4). naye Merib-Baali akamzaa Mika.
  • 35 8:35Wana wa Mika walikuwa:
  • Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi. 36 8:36Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 37 8:37Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
  • 38 8:38Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:
  • Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.
  • 39 8:39Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:
  • Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. 40 8:40Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150.
  • Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.
  • 91 9:1Waisraeli wote waliorodheshwa katika koo zilizoandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa Israeli.

    Watu Katika Yerusalemu

    Watu wa Yuda walichukuliwa mateka kwenda Babeli kwa sababu ya kukosa uaminifu kwa Mungu. 2 9:2Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na watumishi wa Hekalu. 9:2 Yaani Wanethini.

    3 9:3Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa:

    Jamaa Za Yuda
  • 4 9:4Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
  • 5 9:5Wazao wa Washiloni waliorudi ni:
  • Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe.
  • 6 9:6Kwa wana wa Zera:
  • Yeueli. Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690. Jamaa Za Benyamini
  • 7 9:7Kwa Benyamini walikuwa:
  • Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua; 8 9:8Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya. 9 9:9Watu kutoka Benyamini kama walivyoorodheshwa katika koo zao jumla yao ni 956. Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao. Jamaa Za Makuhani
  • 10 9:10Wa jamaa za makuhani walikuwa:
  • Yedaya, Yehoyaribu na Yakini; 11 9:11Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa afisa kiongozi wa nyumba ya Mungu. 12 9:12Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yahzera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri. 13 9:13Makuhani waliokuwa viongozi wa jamaa zao walikuwa 1,760. Walikuwa watu wenye uwezo, waliowajibika kuhudumu katika nyumba ya Mungu. Jamaa Za Walawi
  • 14 9:14Jamaa za Walawi walikuwa:
  • Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari. 15 9:15Bakbakari, Hereshi, Galali na Matania mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu. 16 9:16Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elikana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi. Jamaa Za Mabawabu
  • 17 9:17Mabawabu katika Hekalu la Bwana waliorudi walikuwa:
  • Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu. 18 9:18Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi. 19 9:19Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya Bwana. 20 9:20Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye Bwana alikuwa pamoja naye: 21 9:21Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania.

    22 9:22Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli. 23 9:23Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya Bwana, nyumba iliyoitwa Hema. 24 9:24Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. 25 9:25Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba. 26 9:26Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu. 27 9:27Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.

    28 9:28Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. 29 9:29Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. 30 9:30Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo. 31 9:31Mlawi aliyeitwa Matithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka. 32 9:32Baadhi ya ndugu zao wa ukoo wa Kohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate ya Wonyesho kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani.

    33 9:33Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana.

    34 9:34Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa za Walawi, wakuu kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

    Ukoo Wa Sauli (1 Nyakati 8:29-38)
  • 35 9:35Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka, 36 9:36mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 37 9:37Gedori, Ahio, Zekaria na Miklothi. 38 9:38Miklothi akamzaa Shimeamu. Wao pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.
  • 39 9:39Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli. Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali. 9:39 Anajulikana pia kwa jina la Ish-Boshethi, maana yake Mtu wa Aibu (2Sam 2:8).
  • 40 9:40Yonathani akamzaa Merib-Baali, 9:40 Pia anajulikana kwa jina la Mefiboshethi.
  • naye Merib-Baali akamzaa Mika.
  • 41 9:41Wana wa Mika walikuwa:
  • Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi. 42 9:42Ahazi akamzaa Yara, Yara akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 43 9:43Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.
  • 44 9:44Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao:
  • Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Aseli. 10Sauli Ajiua (1 Samweli 31:1-13)

    1 10:1Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika mlima Gilboa. 2 10:2Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. 3 10:3Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi.

    4 10:4Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.”

    Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. 5 10:5Mbeba silaha wake alipoona kwamba Sauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake akafa. 6 10:6Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote.

    7 10:7Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.

    8 10:8Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa. 9 10:9Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao. 10 10:10Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni.

    11 10:11Wakazi wote wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yote Wafilisti waliyomtendea Sauli, 12 10:12mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba.

    13 10:13Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa Bwana. Hakulishika neno la Bwana, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, 14 10:14hakumuuliza Bwana. Kwa hiyo Bwana alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.

    11Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Israeli (2 Samweli 5:1-10)

    1 11:1Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako. 2 11:2Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Bwana Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”

    3 11:3Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na Bwana alivyoahidi kupitia kwa Samweli.

    Daudi Ateka Yerusalemu

    4 11:4Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo 5 11:5wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

    6 11:6Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.

    7 11:7Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi. 8 11:8Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu. 9 11:9Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.

    Mashujaa Wa Daudi (2 Samweli 23:8-39)

    10 11:10Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama Bwana alivyoahidi. 11 11:11Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi:

    Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.

    12 11:12Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. 13 11:13Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti. 14 11:14Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

    15 11:15Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. 16 11:16Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. 17 11:17Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!” 18 11:18Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. 19 11:19Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa.

    Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

    20 11:20Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. 21 11:21Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

    22 11:22Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. 23 11:23Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano. 11:23 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao. 24 11:24Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. 25 11:25Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

  • 26 11:26Wale watu mashujaa walikuwa:
  • Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu, 27 11:27Shamothi Mharori, Helesi Mpeloni, 28 11:28Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa, Abiezeri kutoka Anathothi, 29 11:29Sibekai Mhushathi, Ilai Mwahohi, 30 11:30Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi, 31 11:31Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini, Benaya Mpirathoni, 32 11:32Hurai kutoka mabonde ya Gaashi, Abieli Mwaribathi, 33 11:33Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni, 34 11:34wana wa Hashemu Mgiloni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari, 35 11:35Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifale mwana wa Uru, 36 11:36Heferi Mmekerathi, Ahiya Mpeloni, 37 11:37Hezro Mkarmeli, Naarai mwana wa Ezbai, 38 11:38Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri, 39 11:39Seleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya, 40 11:40Ira Mwithiri, Garebu Mwithiri, 41 11:41Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai, 42 11:42Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini, 43 11:43Hanani mwana wa Maaka, Yoshafati Mmithni, 44 11:44Uzia Mwashterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri, 45 11:45Yediaeli mwana wa Shimri, nduguye Yoha Mtizi, 46 11:46Elieli Mmahawi, Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, Ithma Mmoabu, 47 11:47Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai. 12Mashujaa Waungana Na Daudi

    1 12:1Hawa ndio watu waliomjia Daudi huko Siklagi, wakati alikuwa amefukuzwa mbele ya Sauli mwana wa Kishi (walikuwa miongoni mwa mashujaa waliomsaidia Daudi vitani, 2 12:2walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):

    3 12:3Mkuu wao alikuwa Ahiezeri, na wa pili Yoashi, wote wana wa Shemaa Mgibeathi; pia Yezieli na Peleti wana wa Azmawethi; Beraka, Yehu Mwanathothi, 4 12:4na Ishmaya Mgibeoni, shujaa miongoni mwa wale Thelathini, ambaye alikuwa kiongozi wa wale Thelathini; Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi, Mgederathi, 5 12:5Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi; 6 12:6Elikana, Ishia, Azareli, Yoezeri na Yashobeamu, wana wa Kora; 7 12:7Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori.

    8 12:8Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani.

  • 9 12:9Ezeri alikuwa mkuu wao,
  • Obadia alikuwa wa pili katika uongozi, Eliabu wa tatu,
  • 10 12:10Mishmana wa nne, Yeremia wa tano,
  • 11 12:11Atai wa sita, Elieli wa saba,
  • 12 12:12Yohanani wa nane, Elzabadi wa tisa,
  • 13 12:13Yeremia wa kumi, na Makbanai wa kumi na moja.
  • 14 12:14Hawa Wagadi walikuwa majemadari. Aliyekuwa wa mwisho kuliko wote aliweza kuongoza askari 100, na aliyekuwa na uweza zaidi ya wote aliongoza 1,000. 15 12:15Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi.

    16 12:16Wabenyamini wengine na baadhi ya watu kutoka Yuda pia walikuja kwa Daudi katika ngome yake. 17 12:17Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mimi mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.”

    18 12:18Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema:

    “Sisi tu watu wako, ee Daudi! Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese! Ushindi, naam, ushindi uwe kwako, pia ushindi kwa wale walio upande wako, kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.”

    Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi.

    19 12:19Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”) 20 12:20Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase. 21 12:21Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake. 22 12:22Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.

    Wengine Waungana Na Daudi Huko Hebroni

    23 12:23Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama Bwana alivyokuwa amesema:

  • 24 12:24watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita.
  • 25 12:25Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100.
  • 26 12:26Watu wa Lawi walikuwa 4,600, 27 12:27pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Aroni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700, 28 12:28na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake.
  • 29 12:29Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo.
  • 30 12:30Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao.
  • 31 12:31Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000.
  • 32 12:32Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.
  • 33 12:33Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000.
  • 34 12:34Watu wa Naftali, maafisa 1,000, pamoja na watu 37,000 waliochukua ngao na mikuki.
  • 35 12:35Watu wa Dani 28,600 waliokuwa tayari kwa vita.
  • 36 12:36Watu wa Asheri, askari 40,000 wenye uzoefu mkubwa waliondaliwa kwa ajili ya vita.
  • 37 12:37Na pia watu kutoka mashariki ya Yordani, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakiwa na kila aina ya silaha, watu 120,000.
  • 38 12:38Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme. 39 12:39Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao. 40 12:40Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ngʼombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.

    13Kurudishwa Kwa Sanduku La Mungu (2 Samweli 6:1-11)

    1 13:1Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia. 2 13:2Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi ya Bwana Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao, waje waungane na sisi. 3 13:3Sisi na tulirudishe Sanduku la Mungu wetu kwetu kwa maana hatukujali wakati wa utawala wa Sauli.” 4 13:4Kusanyiko lote likakubaliana kufanya hivyo, kwa sababu ilionekana vyema kwa watu wote.

    5 13:5Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu. 6 13:6Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu Bwana, yeye anayeketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake, kutoka huko.

    7 13:7Wakalisafirisha Sanduku la Mungu kwa gari jipya la kukokotwa na maksai kutoka nyumba ya Abinadabu, Uza na Ahio wakiliongoza gari hilo. 8 13:8Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.

    9 13:9Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Kidoni, Uza akaunyoosha mkono wake ili kulizuia Sanduku, kwa sababu maksai walijikwaa. 10 13:10Hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu.

    11 13:11Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya Bwana ilifurika dhidi ya Uza, mahali pale pakaitwa Peres-Uza 13:11 Maana yake ni Gadhabu dhidi ya Uza. hadi leo.

    12 13:12Siku ile Daudi akamwogopa Mungu naye akauliza. “Nitawezaje kulichukua Sanduku la Mungu kwangu?” 13 13:13Hakulichukua hilo Sanduku akae nalo katika Mji wa Daudi. Badala yake, akalipeleka nyumbani kwa Obed-Edomu, Mgiti. 14 13:14Sanduku la Mungu likabaki pamoja na jamaa ya Obed-Edomu, nyumbani kwake kwa miezi mitatu, naye Bwana akaibariki nyumba yake pamoja na kila kitu alichokuwa nacho.

    14Nyumba Ya Daudi Na Jamaa Yake (2 Samweli 5:11-16)

    1 14:1Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme. 2 14:2Naye Daudi akatambua kwamba Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.

    3 14:3Huko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi. 4 14:4Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, 5 14:5Ibihari, Elishua, Elpeleti, 6 14:6Noga, Nefegi, Yafia, 7 14:7Elishama, Beeliada na Elifeleti.

    Daudi Awashinda Wafilisti (2 Samweli 5:17-25)

    8 14:8Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao. 9 14:9Basi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai, 10 14:10Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”

    Bwana akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”

    11 14:11Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, 14:11 Maana yake ni Bwana Afurikae. akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. 12 14:12Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto.

    13 14:13Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; 14 14:14hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi. 15 14:15Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.” 16 14:16Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.

    17 14:17Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye Bwana akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.

    15Sanduku La Agano Laletwa Yerusalemu (2 Samweli 6:12-22)

    1 15:1Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake. 2 15:2Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu Bwana aliwachagua kulibeba Sanduku la Bwana na kuhudumu mbele zake milele.”

    3 15:3Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake. 4 15:4Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

  • 5 15:5Kutoka wazao wa Kohathi,
  • Urieli kiongozi na ndugu zake 120,
  • 6 15:6Kutoka wazao wa Merari,
  • Asaya kiongozi na ndugu zake 220.
  • 7 15:7Kutoka wazao wa Gershoni, 15:7 Namna nyingine ya kutaja Gershomu.
  • Yoeli kiongozi na ndugu zake 130.
  • 8 15:8Kutoka wazao wa Elisafani,
  • Shemaya kiongozi na ndugu zake 200.
  • 9 15:9Kutoka wazao wa Hebroni,
  • Elieli kiongozi na ndugu zake 80.
  • 10 15:10Kutoka wazao wa Uzieli,
  • Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112.

    11 15:11Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu. 12 15:12Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake. 13 15:13Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha Bwana Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.” 14 15:14Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli. 15 15:15Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno la Bwana.

    16 15:16Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi.

    17 15:17Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya; 18 15:18hawa ndio waliochaguliwa kuwa wasaidizi wao: Zekaria, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaya, Maaseya, Matithia, Elifelehu, Mikneya, pamoja na mabawabu Obed-Edomu na Yehieli.

    19 15:19Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba; 20 15:20Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti ya alamothi, 15:20 Huenda ni aina ya uimbaji. 21 15:21na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya sheminithi. 15:21 Huenda ni aina ya uimbaji. 22 15:22Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo.

    23 15:23Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku. 24 15:24Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku.

    25 15:25Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe. 26 15:26Kwa sababu Mungu alikuwa amewasaidia Walawi waliokuwa wanalichukua Sanduku la Agano la Bwana, mafahali saba na kondoo dume saba walitolewa dhabihu. 27 15:27Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi. 28 15:28Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la Bwana kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.

    29 15:29Sanduku la Agano la Bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.

    16Sanduku Lawekwa Ndani Ya Hema

    1 16:1Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 2 16:2Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana. 3 16:3Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.

    4 16:4Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli: 5 16:5Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, 6 16:6nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.

    Zaburi Ya Daudi Ya Shukrani (Zaburi 105:1-15; 96:1-13; 106:1, 47-48)

    7 16:7Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:

    8 16:8Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. 9 16:9Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; waambieni matendo yake yote ya ajabu. 10 16:10Lishangilieni jina lake takatifu; mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi. 11 16:11Mtafuteni Bwana na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote. 12 16:12Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, 13 16:13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake. 14 16:14Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote. 15 16:15Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, 16 16:16agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki. 17 16:17Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele: 18 16:18“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.” 19 16:19Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake, 20 16:20walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. 21 16:21Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: 22 16:22“Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.” 23 16:23Mwimbieni Bwana dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. 24 16:24Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. 25 16:25Kwa kuwa Bwana ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. 26 16:26Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu. 27 16:27Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. 28 16:28Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu, 29 16:29mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake. Leteni sadaka na mje katika nyua zake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake. 30 16:30Dunia yote na itetemeke mbele zake! Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa. 31 16:31Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; semeni katikati ya mataifa, “Bwana anatawala!” 32 16:32Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake. 33 16:33Kisha miti ya msituni itaimba, itaimba kwa furaha mbele za Bwana, kwa maana anakuja kuihukumu dunia. 34 16:34Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. 35 16:35Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe. Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako.” 36 16:36Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni Bwana.”

    37 16:37Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la Bwana ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku. 38 16:38Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.

    39 16:39Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya Bwana katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni 40 16:40ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Bwana kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya Bwana ambayo alikuwa amempa Israeli. 41 16:41Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.” 42 16:42Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.

    43 16:43Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.

    17Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi (2 Samweli 7:1-17)

    1 17:1Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano la Bwana liko ndani ya hema.”

    2 17:2Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.” 3 17:3Usiku ule neno la Mungu likamjia Nathani, kusema:

    4 17:4“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Wewe hutanijengea mimi nyumba ili nikae humo. 5 17:5Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine. 6 17:6Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’ 7 17:7“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli. 8 17:8Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. 9 17:9Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, 10 17:10na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote. “ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba Bwana atakujengea nyumba: 11 17:11Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake. 12 17:12Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele. 13 17:13Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. 14 17:14Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ”

    15 17:15Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

    Maombi Ya Daudi (2 Samweli 7:18-29)

    16 17:16Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:

    “Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? 17 17:17Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee Bwana Mungu. 18 17:18“Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako, 19 17:19Ee Bwana Mungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana. 20 17:20“Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana Mungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe. 21 17:21Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? 22 17:22Uliwafanya watu wako Israeli kuwa watu wako wewe mwenyewe milele, nawe, Ee Bwana Mungu, umekuwa Mungu wao. 23 17:23“Sasa basi, Bwana ahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi, 24 17:24ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako. 25 17:25“Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya. 26 17:26Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. 27 17:27Basi imekupendeza kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu milele machoni pako; kwa ajili yako, Ee Bwana, umeibariki, nayo itabarikiwa milele.” 18Ushindi Wa Daudi (2 Samweli 8:1-18)

    1 18:1Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Gathi pamoja na vijiji vinavyouzunguka kutoka utawala wa Wafilisti.

    2 18:2Pia Daudi akawashinda Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru.

    3 18:3Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alikwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Frati. 4 18:4Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.

    5 18:5Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao. 6 18:6Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumwa wa Daudi, na kumlipa ushuru. Bwana akampa Daudi ushindi kote alipokwenda.

    7 18:7Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizokuwa za maafisa wa Hadadezeri na kuzileta Yerusalemu. 8 18:8Kutoka miji ya Tibhathi na Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi sana, ambayo Solomoni aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.

    9 18:9Tou mfalme wa Hamathi aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri mfalme wa Soba, 10 18:10akamtuma mwanawe, Hadoramu kwa Mfalme Daudi ili kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Mfalme Hadadezeri, kwa kuwa alikuwa amepigana vita mara nyingi na Tou. Hadoramu akamletea Daudi vifaa mbalimbali vya dhahabu, fedha na shaba.

    11 18:11Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa Bwana kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki.

    12 18:12Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi. 13 18:13Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. Bwana akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.

    Maafisa Wa Daudi

    14 18:14Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote. 15 18:15Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu; 16 18:16Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; Shausha alikuwa mwandishi; 17 18:17naye Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa msimamizi wa Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi walikuwa maafisa wakuu katika utumishi wa mfalme.

    19Vita Dhidi Ya Waamoni (2 Samweli 10:1-19)

    1 19:1Baada ya muda, Nahashi mfalme wa Waamoni akafa, mwanawe akaingia mahali pake. 2 19:2Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea wema.”

    Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji, 3 19:3wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?” 4 19:4Kwa hiyo Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa ndevu akakata nguo zao katikati kwenye matako, akawaacha waende zao.

    5 19:5Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mje.”

    6 19:6Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000 19:6 Talanta 1,000 za fedha ni sawa na tani 34. za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu, 19:6 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. Aramu-Maaka na Soba. 7 19:7Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita.

    8 19:8Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji. 9 19:9Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani.

    10 19:10Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu. 11 19:11Akawaweka wale wanajeshi wengine waliobaki chini ya amri ya Abishai ndugu yake, nao wakapangwa ili wakabiliane na Waamoni. 12 19:12Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe unisaidie; lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakusaidia. 13 19:13Uwe hodari na tupigane kwa ujasiri kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu. Bwana atafanya lile lililo jema machoni pake.”

    14 19:14Basi Yoabu na vikosi vyake wakasonga mbele kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia mbele yake. 15 19:15Waamoni walipoona Waaramu wanakimbia, nao pia wakakimbia mbele ya nduguye Abishai na kuingia ndani ya mji. Basi Yoabu akarudi Yerusalemu.

    16 19:16Baada ya Waaramu kuona kwamba wameshindwa na Israeli, wakapeleka wajumbe na kuwataka Waaramu wengine kutoka ngʼambo ya Mto Frati, wakiongozwa na Shofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri.

    17 19:17Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake. 18 19:18Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.

    19 19:19Raiya wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi, wakawa watumishi wake.

    Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

    20Kutekwa Kwa Raba (2 Samweli 12:26-31)

    1 20:1Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni, na akaenda Raba na kuuzingira, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akashambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu. 2 20:2Daudi akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu, 20:2 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34. nayo ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mjini huo. 3 20:3Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.

    Vita Na Wafilisti (2 Samweli 21:15-22)

    4 20:4Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai, 20:4 Yaani majitu. nao Wafilisti wakashindwa.

    5 20:5Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.

    6 20:6Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. 7 20:7Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua.

    8 20:8Hawa walikuwa ndio wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.

    21Daudi Ahesabu Wapiganaji (2 Samweli 24:1-25)

    1 21:1Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli. 2 21:2Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.”

    3 21:3Yoabu akajibu, “Bwana na aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana wangu, kwani hawa wote si raiya wa bwana wangu? Kwa nini bwana wangu unataka kufanya hivi? Kwa nini kuleta hatia juu ya Israeli?”

    4 21:4Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu; kwa hiyo Yoabu akaondoka na kuzunguka Israeli yote kisha akarudi Yerusalemu. 5 21:5Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000.

    6 21:6Lakini Yoabu hakuwahesabu Walawi na Wabenyamini, kwa sababu alichukizwa sana na amri ya mfalme. 7 21:7Amri hii ilikuwa mbaya machoni pa Mungu pia; hivyo akaiadhibu Israeli.

    8 21:8Kisha Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Sasa, ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”

    9 21:9 Bwana akamwambia Gadi, mwonaji wa Daudi, 10 21:10“Nenda ukamwambie Daudi, hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

    11 21:11Kwa hiyo Gadi akamwendea Daudi akamwambia, “Hili ndilo Bwana asemalo: ‘Chagua: 12 21:12miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa Bwana, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa Bwana akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”

    13 21:13Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa Bwana kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”

    14 21:14Basi Bwana akatuma tauni katika Israeli, watu 70,000 wa Israeli wakafa. 15 21:15Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo, Bwana akaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Bwana alikuwa amesimama katika sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna 21:15 Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania. Myebusi.

    16 21:16Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa Bwana akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.

    17 21:17Daudi akamwambia Mungu, “Je, si mimi ndiye niliyeamuru watu wahesabiwe? Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Ee Bwana, Mungu wangu, mkono wako na uwe juu yangu mimi na jamaa yangu, lakini usiache tauni hii iendelee juu ya watu wako.”

    18 21:18Kisha malaika wa Bwana akamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengea Bwana madhabahu kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi. 19 21:19Kwa hiyo Daudi akakwea, akalitii lile neno ambalo Gadi alikuwa amelisema katika jina la Bwana.

    20 21:20Arauna alipokuwa akipura ngano, akageuka akamwona yule malaika. Wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha, yeye akaendelea kupura ngano. 21 21:21Kisha Daudi akakaribia, Arauna alipotazama na kumwona, akaondoka kwenye uwanja wa kupuria nafaka akamsujudia Daudi akiuinamisha uso wake ardhini.

    22 21:22Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu ya Bwana tauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”

    23 21:23Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.”

    24 21:24Lakini Mfalme Daudi akamjibu Arauna, “La hasha! Lakini ninasisitiza kwamba nitalipa bei yake kamili. Sitachukua kilicho chako kwa ajili ya Bwana au kutoa sadaka ya kuteketezwa ambayo hainigharimu chochote.”

    25 21:25Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600 21:25 Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 7. kwa ajili ya ule uwanja. 26 21:26Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita Bwana naye Bwana akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.

    27 21:27Kisha Bwana akanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake. 28 21:28Wakati huo, Daudi alipoona kwamba Bwana amemjibu kule kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna Myebusi, akatoa dhabihu huko. 29 21:29Maskani ya Bwana ambayo Mose aliitengeneza kule jangwani, pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa wakati huo vilikuwa viko mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni. 30 21:30Lakini Daudi hakuthubutu kuisogelea ili kumuuliza Mungu, kwa sababu aliuogopa upanga wa yule malaika wa Bwana.

    221 22:1Ndipo Daudi akasema, “Nyumba ya Bwana Mungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.”

    Maandalizi Kwa Ajili Ya Hekalu

    2 22:2Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. 3 22:3Daudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika. 4 22:4Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi.

    5 22:5Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili ya Bwana inatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake.

    6 22:6Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili ya Bwana, Mungu wa Israeli. 7 22:7Daudi akamwambia Solomoni: “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wangu. 8 22:8Lakini neno hili la Bwana likanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu. 9 22:9Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake. 10 22:10Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’

    11 22:11“Sasa, mwanangu, Bwana awe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba ya Bwana Mungu wako, kama alivyosema utafanya. 12 22:12 Bwana na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya Bwana Mungu wako. 13 22:13Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria Bwana alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.

    14 22:14“Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Bwana: talanta 100,000 22:14 Talanta 100,000 za dhahabu ni sawa na tani 3,750. za dhahabu, talanta 1,000,000 22:14 Talanta 1,000,000 za fedha ni sawa na tani 37,500. za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. 15 22:15Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi 16 22:16wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye Bwana awe pamoja nawe.”

    17 22:17Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe. 18 22:18Akawaambia, “Je, Bwana Mungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini ya Bwana na watu wake. 19 22:19Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta Bwana Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya Bwana Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la Bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la Bwana.”

    23Jamaa Za Walawi Na Utendaji Wao

    1 23:1Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

    2 23:2Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. 3 23:3Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000. 4 23:4Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi, 5 23:5na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”

    6 23:6Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

    Wagershoni
  • 7 23:7Wana wa Wagershoni walikuwa wawili:
  • Ladani na Shimei.
  • 8 23:8Wana wa Ladani walikuwa watatu:
  • Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.
  • 9 23:9Wana wa Shimei walikuwa watatu:
  • Shelomothi, 23:9 Yaani Shelomithi; maana yake ni Mpenda amani. Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.
  • 10 23:10Nao wana wa Shimei walikuwa wanne:
  • Yahathi, Zina, 23:10 Tafsiri zingine zinamwita Ziza. Yeushi na Beria. 11 23:11Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja. Wakohathi
  • 12 23:12Wana wa Kohathi walikuwa wanne:
  • Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
  • 13 23:13Wana wa Amramu walikuwa:
  • Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele. 14 23:14Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.
  • 15 23:15Wana wa Mose walikuwa:
  • Gershomu na Eliezeri.
  • 16 23:16Wazao wa Gershomu:
  • Shebueli alikuwa wa kwanza.
  • 17 23:17Wazao wa Eliezeri:
  • Rehabia alikuwa wa kwanza. Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
  • 18 23:18Wana wa Ishari:
  • Shelomithi alikuwa wa kwanza.
  • 19 23:19Wana wa Hebroni walikuwa:
  • Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.
  • 20 23:20Wana wa Uzieli walikuwa:
  • Mika wa kwanza na Ishia wa pili. Wamerari
  • 21 23:21Wana wa Merari walikuwa:
  • Mahli na Mushi.
  • Wana wa Mahli walikuwa:
  • Eleazari na Kishi. 22 23:22Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
  • 23 23:23Wana wa Mushi:
  • Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.

    24 23:24Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la Bwana. 25 23:25Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile Bwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele, 26 23:26Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.” 27 23:27Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

    28 23:28Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la Bwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu. 29 23:29Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa. 30 23:30Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni 31 23:31na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.

    32 23:32Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la Bwana.

    24Migawanyo Ya Makuhani

    1 24:1Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:

    Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 2 24:2Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani. 3 24:3Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao. 4 24:4Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari. 5 24:5Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

    6 24:6Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

  • 7 24:7Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,
  • ya pili Yedaya,
  • 8 24:8ya tatu Harimu,
  • ya nne Seorimu,
  • 9 24:9ya tano Malkiya,
  • ya sita Miyamini,
  • 10 24:10ya saba Hakosi,
  • ya nane Abiya,
  • 11 24:11ya tisa Yeshua,
  • ya kumi Shekania,
  • 12 24:12ya kumi na moja Eliashibu,
  • ya kumi na mbili Yakimu,
  • 13 24:13ya kumi na tatu Hupa,
  • ya kumi na nne Yeshebeabu,
  • 14 24:14ya kumi na tano Bilga,
  • ya kumi na sita Imeri,
  • 15 24:15ya kumi na saba Heziri,
  • ya kumi na nane Hapisesi,
  • 16 24:16ya kumi na tisa Pethahia,
  • ya ishirini Yehezkeli,
  • 17 24:17ya ishirini na moja Yakini,
  • ya ishirini na mbili Gamuli,
  • 18 24:18ya ishirini na tatu Delaya,
  • ya ishirini na nne Maazia.
  • 19 24:19Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

    Walawi Waliobaki 20 24:20Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki:
  • Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;
  • kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya. 21 24:21Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe: Ishia alikuwa wa kwanza.
  • 22 24:22Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,
  • kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.
  • 23 24:23Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
  • 24 24:24Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;
  • kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri. 25 24:25Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia; na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.
  • 26 24:26Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.
  • Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.
  • 27 24:27Wana wa Merari:
  • kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.
  • 28 24:28Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.
  • 29 24:29Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:
  • alikuwa Yerameeli.
  • 30 24:30Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.
  • Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao. 31 24:31Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

    25Waimbaji

    1 25:1Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:

  • 2 25:2Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa:
  • Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.
  • 3 25:3Wana wa Yeduthuni walikuwa sita:
  • Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza Bwana.
  • 4 25:4Wana wa Hemani walikuwa:
  • Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi. 5 25:5Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

    6 25:6Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. 7 25:7Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana. Idadi yao walikuwa 288. 8 25:8Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.

    9 25:9Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, wanawe na jamaa zake, 12 Ya pili ikamwangukia Gedalia, yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12 10 25:10Ya tatu ikamwangukia Zakuri, wanawe na jamaa zake, 12 11 25:11ya nne ikamwangukia Isri, 25:11 Isri jina lingine ni Seri. wanawe na jamaa zake, 12 12 25:12ya tano ikamwangukia Nethania, wanawe na jamaa zake, 12 13 25:13ya sita ikamwangukia Bukia, wanawe na jamaa zake, 12 14 25:14ya saba ikamwangukia Yesarela, 25:14 Yesarela jina lingine ni Asarela. wanawe na jamaa zake, 12 15 25:15ya nane ikamwangukia Yeshaya, wanawe na jamaa zake, 12 16 25:16ya tisa ikamwangukia Matania, wanawe na jamaa zake, 12 17 25:17ya kumi ikamwangukia Shimei, wanawe na jamaa zake, 12 18 25:18ya kumi na moja ikamwangukia Azareli, 25:18 Azareli jina lingine ni Uzieli. wanawe na jamaa zake, 12 19 25:19ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, wanawe na jamaa zake, 12 20 25:20ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, wanawe na jamaa zake, 12 21 25:21ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, wanawe na jamaa zake, 12 22 25:22ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi, wanawe na jamaa zake, 12 23 25:23Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, wanawe na jamaa zake, 12 24 25:24ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, wanawe na jamaa zake, 12 25 25:25ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, wanawe na jamaa zake, 12 26 25:26ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, wanawe na jamaa zake, 12 27 25:27ya ishirini ikamwangukia Eliatha, wanawe na jamaa zake, 12 28 25:28ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, wanawe na jamaa zake, 12 29 25:29ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, wanawe na jamaa zake, 12 30 25:30ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, wanawe na jamaa zake, 12 31 25:31ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, wanawe na jamaa zake, 12.
    26Mabawabu

    1 26:1Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu:

  • Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu.
  • 2 26:2Meshelemia alikuwa na wana wafuatao:
  • Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wa pili, Zebadia wa tatu, Yathnieli wa nne, 3 26:3Elamu wa tano Yehohanani wa sita na Eliehoenai wa saba.
  • 4 26:4Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:
  • Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili, Yoa wa tatu, Sakari wa nne, Nethaneli wa tano, 5 26:5Amieli wa sita, Isakari wa saba, na Peulethai wa nane. (Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.)
  • 6 26:6Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. 7 26:7Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. 8 26:8Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili.
  • 9 26:9Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane.
  • 10 26:10Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), 11 26:11Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu.
  • 12 26:12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 13 26:13Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.

    14 26:14Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia. 26:14 Shelemia jina lingine ni Meshelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 15 26:15Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 16 26:16Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.

    Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: 17 26:17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. 18 26:18Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.

    19 26:19Hii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.

    Watunza Hazina Na Maafisa Wengine

    20 26:20Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

    21 26:21Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, 22 26:22wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la Bwana.

    23 26:23Kutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli:

  • 24 26:24Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. 25 26:25Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi. 26 26:26Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. 27 26:27Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Bwana. 28 26:28Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake.
  • 29 26:29Kutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli.
  • 30 26:30Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za Bwana na utumishi wa mfalme. 31 26:31Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. 32 26:32Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.
  • 27Vikosi Vya Jeshi

    1 27:1Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.

  • 2 27:2Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake. 3 27:3Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
  • 4 27:4Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 5 27:5Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000. 6 27:6Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake.
  • 7 27:7Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 8 27:8Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 9 27:9Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 10 27:10Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 11 27:11Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 12 27:12Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 13 27:13Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 14 27:14Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • 15 27:15Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.
  • Maafisa Wa Makabila
  • 16 27:16Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa:
  • Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;
  • kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;
  • 17 27:17kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli;
  • kwa Aroni: Sadoki;
  • 18 27:18kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi;
  • kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli;
  • 19 27:19kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia;
  • kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli;
  • 20 27:20kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;
  • kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya;
  • 21 27:21kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;
  • kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri;
  • 22 27:22kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.
  • Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli.

    23 27:23Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. 24 27:24Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.

    Wasimamizi Wa Mali Za Mfalme

    25 27:25Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.

    Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.

    26 27:26Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba.

    27 27:27Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.

    Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.

    28 27:28Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.

    Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni.

    29 27:29Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni.

    Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni.

    30 27:30Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.

    Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda.

    31 27:31Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.

    Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi.

    32 27:32Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.

    33 27:33Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.

    Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme. 34 27:34Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.

    Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.

    28Maandalizi Ya Daudi Ya Kujenga Hekalu

    1 28:1Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na askari wote walio hodari.

    2 28:2Mfalme Daudi akainuka na kusema: “Nisikilizeni ndugu zangu nanyi watu wangu. Nilikuwa na nia ya kujenga nyumba ili iwe mahali pa kukaa Sanduku la Agano la Bwana kwa ajili ya kuwa mahali pa kuwekea miguu ya Mungu wetu, nami nikafanya maandalizi ya kuijenga. 3 28:3Lakini Mungu akaniambia, ‘Wewe hutajenga nyumba kwa Jina langu, kwa sababu wewe umepigana vita na umemwaga damu.’

    4 28:4“Hata hivyo, Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote. 5 28:5Miongoni mwa wanangu wote, naye Bwana amenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme wa Bwana juu ya Israeli. 6 28:6Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. 7 28:7Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’

    8 28:8“Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la Bwana naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za Bwana Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.

    9 28:9“Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana Bwana huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele. 10 28:10Angalia basi, kwa maana Bwana amekuchagua wewe ili ujenge Hekalu kuwa mahali patakatifu. Uwe hodari ukafanye kazi hiyo.”

    11 28:11Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho. 12 28:12Akampa vielelezo vya yote Roho alikuwa ameviweka moyoni mwake kwa ajili ya kumbi za Hekalu la Bwana na vyumba vyote vilivyolizunguka, kwa ajili ya hazina za Hekalu la Mungu na kwa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. 13 28:13Mfalme pia akampa Solomoni maelekezo kwa ajili ya migawanyo ya huduma za makuhani na Walawi, pia kwa ajili ya kazi zote za huduma katika Hekalu la Bwana. Akampa pia maelezo kuhusu vifaa vyote vya kutumika katika huduma ya Hekalu. 14 28:14Akamwagizia uzito wa dhahabu kwa ajili ya vitu vyote vya dhahabu vya kutumika katika huduma mbalimbali, uzito wa fedha kwa ajili ya vitu vyote vya fedha vya kutumika katika huduma mbalimbali. 15 28:15Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake, pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara; 16 28:16uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha; 17 28:17uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha; 18 28:18na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano la Bwana.

    19 28:19Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwa Bwana ulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.”

    20 28:20Daudi pia akamwambia Solomoni mwanawe, “Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maana Bwana aliye Mungu, Mungu wangu yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia mpaka kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu la Bwana itakapokamilika. 21 28:21Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yoyote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”

    29Matoleo Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Hekalu

    1 29:1Ndipo Mfalme Daudi akaliambia kusanyiko lote: “Mwanangu Solomoni, yeye ambaye Mungu amemchagua, ni kijana mdogo na asiye na uzoefu. Kazi hii ni kubwa, kwa sababu Hekalu hili la fahari si kwa ajili ya mwanadamu bali ni kwa ajili ya Bwana. 2 29:2Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno. 3 29:3Zaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu: 4 29:4talanta 3,000 29:4 Talanta 3,000 za dhahabu sawa na tani 110. za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000 29:4 Talanta 7,000 za fedha ni sawa na tani 260. za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu, 5 29:5kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa Bwana leo?”

    6 29:6Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.

    7 29:7Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000 29:7 Talanta 5,000 za dhahabu ni sawa na tani 190. na darkoni 10,000 29:7 Darkoni 10,000 za dhahabu ni sawa na kilo 84. za dhahabu, talanta 10,000 29:7 Talanta 10,000 za fedha ni sawa na tani 375. za fedha, talanta 18,000 29:7 Talanta 18,000 za shaba ni sawa na tani 675. za shaba na talanta 100,000 29:7 Talanta 100,000 za chuma ni sawa na tani 3,750. za chuma. 8 29:8Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. 9 29:9Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.

    Maombi Ya Daudi

    10 29:10Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:

    “Uhimidiwe wewe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, tangu milele hata milele. 11 29:11Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee Bwana, ufalme ni wako; umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote. 12 29:12Utajiri na heshima vyatoka kwako; wewe ndiwe utawalaye vitu vyote. Mikononi mwako kuna nguvu na uweza ili kuinua na kuwapa wote nguvu, 13 29:13Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kulisifu Jina lako tukufu.

    14 29:14“Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako. 15 29:15Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini. 16 29:16Ee Bwana Mungu wetu, kwa wingi wote huu ambao tumekutolea kwa kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina lako Takatifu, vimetoka mkononi mwako, navyo vyote ni mali yako. 17 29:17Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe. 18 29:18Ee Bwana, Mungu wa baba zetu Abrahamu, Isaki na Israeli, weka shauku hii ndani ya mioyo ya watu wako daima na uifanye mioyo yao iwe na uaminifu kwako. 19 29:19Nawe umpe mwanangu Solomoni kujitolea kwako kwa moyo wote ili kuzishika amri zako, masharti yako, maagizo yako na kufanya kila kitu ili kujenga Hekalu hili la fahari ambalo kwa ajili yake nimetoa.”

    20 29:20Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini Bwana Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za Bwana na mfalme.

    Solomoni Akubalika Kuwa Mfalme

    21 29:21Siku ya pili yake wakamtolea Bwana dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo dume 1,000 na wana-kondoo dume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli. 22 29:22Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Bwana siku ile.

    Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya Bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani. 23 29:23Solomoni akaketi kwenye kiti cha enzi cha Bwana kuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii. 24 29:24Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni.

    25 29:25 Bwana akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.

    Muhtasari Wa Utawala Wa Daudi

    26 29:26Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote. 27 29:27Alitawala Israeli kwa miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.

    28 29:28Daudi akafa akiwa mzee mwenye umri mwema, akiwa ameshiba siku, utajiri na heshima. Naye Solomoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

    29 29:29Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi, 30 29:30pamoja na habari zote za utawala wake, nguvu zake na matukio yaliyompata yeye, na Israeli, na falme za nchi nyingine zote.