Mithali 1MithaliUtangulizi: Kusudi Na Kiini

1 1:1Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:

2 1:2Kwa kupata hekima na nidhamu; kwa kufahamu maneno ya busara; 3 1:3kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea; 4 1:4huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana; 5 1:5wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, wenye kupambanua na wapate mwongozo; 6 1:6kwa kufahamu mithali na mifano, misemo na vitendawili vya wenye hekima. 7 1:7Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Onyo Dhidi Ya Ushawishi Wa Marafiki Waovu 8 1:8Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 9 1:9Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu wa kuipamba shingo yako. 10 1:10Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao. 11 1:11Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; 12 1:12tuwameze wakiwa hai kama kaburi, 1:12 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni. 13 1:13Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara. 14 1:14Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.” 15 1:15Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao, 16 1:16kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu. 17 1:17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu wakati ndege wote wanakuona! 18 1:18Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe; hujivizia tu wenyewe! 19 1:19Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila; huuondoa uhai wa wale wenye mali. Onyo Dhidi Ya Kukataa Hekima 20 1:20Hekima huita kwa sauti kuu barabarani, hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa; 21 1:21kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake: 22 1:22“Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha, na wapumbavu kuchukia maarifa? 23 1:23Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu. 24 1:24Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu, 25 1:25kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu, 26 1:26mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata: 27 1:27wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea. 28 1:28“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata. 29 1:29Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana, 30 1:30kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu, 31 1:31watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao. 32 1:32Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza. 33 1:33Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.” 2Faida Za Hekima 1 2:1Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, 2 2:2kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, 3 2:3na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu, 4 2:4na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, 5 2:5ndipo utakapoelewa kumcha Bwana na kupata maarifa ya Mungu. 6 2:6Kwa maana Bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. 7 2:7Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama, 8 2:8kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake. 9 2:9Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki na sawa: yaani kila njia nzuri. 10 2:10Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako. 11 2:11Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda. 12 2:12Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu, kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka, 13 2:13wale waachao mapito yaliyonyooka wakatembea katika njia za giza, 14 2:14wale wapendao kutenda mabaya na kufurahia upotovu wa ubaya, 15 2:15ambao mapito yao yamepotoka na ambao ni wapotovu katika njia zao. 16 2:16Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba, kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno ya kushawishi kutenda ubaya, 17 2:17aliyemwacha mwenzi wa ujana wake na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu. 18 2:18Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo na mapito yake kwenye roho za waliokufa. 19 2:19Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi, au kufikia mapito ya uzima. 20 2:20Hivyo utatembea katika njia za watu wema na kushikamana na mapito ya wenye haki. 21 2:21Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake. 22 2:22Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo. 3Faida Nyingine Za Hekima 1 3:1Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, 2 3:2kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio. 3 3:3Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe; vifunge shingoni mwako, viandike katika ubao wa moyo wako. 4 3:4Ndipo utapata kibali na jina zuri mbele za Mungu na mwanadamu. 5 3:5Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6 3:6katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako. 7 3:7Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche Bwana ukajiepushe na uovu. 8 3:8Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako. 9 3:9Mheshimu Bwana kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote; 10 3:10ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya. 11 3:11Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana na usichukie kukaripiwa naye, 12 3:12kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye. 13 3:13Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu, 14 3:14kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. 15 3:15Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye. 16 3:16Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume; katika mkono wake wa kushoto kuna utajiri na heshima. 17 3:17Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani. 18 3:18Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia; wale wamshikao watabarikiwa. 19 3:19Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia, kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake; 20 3:20kwa maarifa yake vilindi viligawanywa, nayo mawingu yanadondosha umande. 21 3:21Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako; 22 3:22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako. 23 3:23Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa; 24 3:24ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu. 25 3:25Usiogope maafa ya ghafula au maangamizi yanayowapata waovu, 26 3:26kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego. 27 3:27Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. 28 3:28Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. 29 3:29Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini. 30 3:30Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lolote. 31 3:31Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri wala kuchagua njia yake iwayo yote, 32 3:32kwa kuwa Bwana humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki. 33 3:33Laana ya Bwana i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki. 34 3:34Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu. 35 3:35Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu. 4Hekima Ni Bora Kupita Vitu Vyote 1 4:1Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu; sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu. 2 4:2Ninawapa mafundisho ya maana, kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. 3 4:3Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu, ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu, 4 4:4baba alinifundisha akisema, “Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote; yashike maagizo yangu na wewe utaishi. 5 4:5Pata hekima, pata ufahamu; usiyasahau maneno yangu wala usiyaache. 6 4:6Usimwache hekima naye atakuweka salama; mpende, naye atakulinda. 7 4:7Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu. 8 4:8Mstahi, naye atakukweza; mkumbatie, naye atakuheshimu. 9 4:9Atakuvika shada la neema kichwani mwako na kukupa taji ya utukufu.” 10 4:10Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia, nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi. 11 4:11Ninakuongoza katika njia ya hekima na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka. 12 4:12Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa; ukimbiapo, hutajikwaa. 13 4:13Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; mshike, maana yeye ni uzima wako. 14 4:14Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya watu wabaya. 15 4:15Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo; achana nayo, na uelekee njia yako. 16 4:16Kwa kuwa hawawezi kulala mpaka watende uovu; wanashindwa hata kusinzia mpaka wamwangushe mtu. 17 4:17Wanakula mkate wa uovu, na kunywa mvinyo wa jeuri. 18 4:18Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu. 19 4:19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae. 20 4:20Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia; sikiliza kwa makini maneno yangu. 21 4:21Usiruhusu yaondoke machoni pako, yahifadhi ndani ya moyo wako; 22 4:22kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili wote wa mwanadamu. 23 4:23Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. 24 4:24Epusha kinywa chako na ukaidi; weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako. 25 4:25Macho yako na yatazame mbele, kaza macho yako moja kwa moja mbele yako. 26 4:26Sawazisha mapito ya miguu yako na njia zako zote ziwe zimethibitika. 27 4:27Usigeuke kulia wala kushoto; epusha mguu wako na ubaya. 5Onyo Dhidi Ya Uzinzi 1 5:1Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara, 2 5:2ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa. 3 5:3Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta; 4 5:4lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. 5 5:5Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. 5:5 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 6 5:6Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui. 7 5:7Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia. 8 5:8Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake, 9 5:9usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine na miaka yako kwa aliye mkatili, 10 5:10wageni wasije wakasherehekea utajiri wako na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine. 11 5:11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa. 12 5:12Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo! 13 5:13Sikuwatii walimu wangu wala kuwasikiliza wakufunzi wangu. 14 5:14Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa katikati ya kusanyiko lote.” 15 5:15Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe. 16 5:16Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani? 17 5:17Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni. 18 5:18Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako. 19 5:19Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake. 20 5:20Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine? 21 5:21Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, naye huyapima mapito yake yote. 22 5:22Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu. 23 5:23Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe. 6Maonyo Dhidi Ya Upumbavu 1 6:1Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako, ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi kwa ajili ya mwingine, 2 6:2kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako, 3 6:3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: Nenda ukajinyenyekeshe kwake; msihi jirani yako! 4 6:4Usiruhusu usingizi machoni pako, usiruhusu kope zako zisinzie. 5 6:5Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji, kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji. 6 6:6Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima! 7 6:7Kwa maana yeye hana msimamizi, wala mwangalizi, au mtawala, 8 6:8lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. 9 6:9Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaamka lini kutoka usingizi wako? 10 6:10Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: 11 6:11hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha. 12 6:12Mtu mbaya sana na mlaghai, ambaye huzungukazunguka na maneno ya upotovu, 13 6:13ambaye anakonyeza kwa jicho lake, anayetoa ishara kwa miguu yake na kuashiria kwa vidole vyake, 14 6:14ambaye hupanga ubaya kwa udanganyifu moyoni mwake: daima huchochea fitina. 15 6:15Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula; ataangamizwa mara, pasipo msaada. 16 6:16Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: 17 6:17macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, 18 6:18moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu, 19 6:19shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu. Onyo Dhidi Ya Uasherati 20 6:20Mwanangu, zishike amri za baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 21 6:21Yafunge katika moyo wako daima, yakaze kuizunguka shingo yako. 22 6:22Wakati utembeapo, yatakuongoza; wakati ulalapo, yatakulinda; wakati uamkapo, yatazungumza nawe. 23 6:23Kwa maana amri hizi ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima, 24 6:24yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka. 25 6:25Moyo wako usitamani uzuri wake wala macho yake yasikuteke, 26 6:26kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa. 27 6:27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua? 28 6:28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka bila miguu yake kuungua? 29 6:29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa. 30 6:30Watu hawamdharau mwizi kama akiiba kukidhi njaa yake wakati ana njaa. 31 6:31Pamoja na hayo, kama akikamatwa, lazima alipe mara saba, ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake. 32 6:32Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe. 33 6:33Mapigo na aibu ni fungu lake na aibu yake haitafutika kamwe; 34 6:34kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume, naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi. 35 6:35Hatakubali fidia yoyote; atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani. 7Onyo Dhidi Ya Mwanamke Mzinzi 1 7:1Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. 2 7:2Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. 3 7:3Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako. 4 7:4Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako; 5 7:5watakuepusha na mwanamke mzinzi, kutokana na mwanamke mpotovu na maneno yake ya kubembeleza. 6 7:6Kwenye dirisha la nyumba yangu nilitazama nje kupitia upenyo kwenye mwimo wa dirisha. 7 7:7Niliona miongoni mwa wajinga, nikagundua miongoni mwa wanaume vijana, kijana asiye na akili. 8 7:8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke 9 7:9wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia. 10 7:10Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu. 11 7:11(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani; 12 7:12mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.) 13 7:13Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia: 14 7:14“Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu. 15 7:15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata! 16 7:16Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri. 17 7:17Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini. 18 7:18Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi! 19 7:19Mume wangu hayupo nyumbani; amekwenda safari ya mbali. 20 7:20Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwepo nyumbani karibuni.” 21 7:21Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini. 22 7:22Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi, 23 7:23mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake. 24 7:24Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo. 25 7:25Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake. 26 7:26Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa. 27 7:27Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, 7:27 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti. 8Wito Wa Hekima 1 8:1Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti? 2 8:2Juu ya miinuko karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo; 3 8:3kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema: 4 8:4“Ni ninyi wanaume, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote. 5 8:5Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili; ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu. 6 8:6Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema; ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa. 7 8:7Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu. 8 8:8Maneno yote ya kinywa changu ni haki; hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi. 9 8:9Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi; hayana kasoro kwa wale wenye maarifa. 10 8:10Chagua mafundisho yangu badala ya fedha, maarifa badala ya dhahabu safi, 11 8:11kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye. 12 8:12“Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; ninamiliki maarifa na busara. 13 8:13Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu. 14 8:14Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu. 15 8:15Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki, 16 8:16kwa msaada wangu wakuu hutawala, na wenye vyeo wote watawalao dunia. 17 8:17Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. 18 8:18Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri udumuo na mafanikio. 19 8:19Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi; kile nitoacho hupita fedha iliyo bora. 20 8:20Natembea katika njia ya unyofu katika mapito ya haki, 21 8:21nawapa utajiri wale wanipendao na kuzijaza hazina zao. 22 8:22Bwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake, kabla ya matendo yake ya zamani; 23 8:23niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa. 24 8:24Wakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa, wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji; 25 8:25kabla milima haijawekwa mahali pake, kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa, 26 8:26kabla hajaumba dunia wala mashamba yake au vumbi lolote la dunia. 27 8:27Nilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake, wakati alichora mstari wa upeo wa macho juu ya uso wa kilindi, 28 8:28wakati aliweka mawingu juu na kuziweka imara chemchemi za bahari, 29 8:29wakati aliiwekea bahari mpaka wake ili maji yasivunje agizo lake, na wakati aliweka misingi ya dunia. 30 8:30Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake. Nilijazwa na furaha siku baada ya siku, nikifurahi daima mbele zake, 31 8:31nikifurahi katika dunia yake yote nami nikiwafurahia wanadamu. 32 8:32“Basi sasa wanangu, nisikilizeni; heri wale wanaozishika njia zangu. 33 8:33Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima; msiyapuuze. 34 8:34Heri mtu yule anisikilizaye mimi, akisubiri siku zote malangoni mwangu, akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu. 35 8:35Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana. 36 8:36Lakini yeyote ashindwaye kunipata hujiumiza mwenyewe; na wote wanichukiao mimi hupenda mauti.” 9Makaribisho Ya Hekima Na Ya Upumbavu 1 9:1Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo zake saba. 2 9:2Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake. 3 9:3Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji. 4 9:4Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa! 5 9:5Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya. 6 9:6Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. 7 9:7“Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi. 8 9:8Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda. 9 9:9Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika. 10 9:10“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu. 11 9:11Kwa maana kwa msaada wangu siku zako zitakuwa nyingi, na miaka itaongezwa katika maisha yako. 12 9:12Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; kama wewe ni mtu wa mzaha, wewe mwenyewe ndiwe utateseka.” 13 9:13Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele; hana adabu na hana maarifa. 14 9:14Huketi kwenye mlango wa nyumba yake, juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji, 15 9:15akiita wale wapitao karibu, waendao moja kwa moja kwenye njia yao. 16 9:16Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!” 17 9:17“Maji yaliyoibiwa ni matamu; chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!” 18 9:18Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo, kwamba wageni wake huyo mwanamke wako katika vilindi vya kuzimu. 10Mithali Za Solomoni

1 10:1Mithali za Solomoni:

Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. 2 10:2Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. 3 10:3 Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. 4 10:4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri. 5 10:5Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. 6 10:6Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 7 10:7Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza. 8 10:8Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia. 9 10:9Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa. 10 10:10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia. 11 10:11Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu. 12 10:12Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote. 13 10:13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu. 14 10:14Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi. 15 10:15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini. 16 10:16Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu. 17 10:17Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine. 18 10:18Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu. 19 10:19Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara. 20 10:20Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora, bali moyo wa mwovu una thamani ndogo. 21 10:21Midomo ya mwenye haki hulisha wengi, lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu. 22 10:22Baraka ya Bwana hutajirisha, wala haichanganyi huzuni. 23 10:23Mpumbavu hufurahia tabia mbaya, lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima. 24 10:24Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa. 25 10:25Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele. 26 10:26Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma. 27 10:27Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha, lakini miaka ya mwovu inafupishwa. 28 10:28Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu. 29 10:29Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya. 30 10:30Kamwe wenye haki hawataondolewa, bali waovu hawatasalia katika nchi. 31 10:31Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa upotovu utakatwa. 32 10:32Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu. 111 11:1 Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake. 2 11:2Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima. 3 11:3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao. 4 11:4Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini. 5 11:5Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe. 6 11:6Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya. 7 11:7Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka; yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu. 8 11:8Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, naye mtu mwovu huingia humo badala yake. 9 11:9Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa. 10 11:10Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha. 11 11:11Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa. 12 11:12Mtu asiye na akili humdharau jirani yake, bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake. 13 11:13Masengenyo husaliti tumaini, bali mtu mwaminifu hutunza siri. 14 11:14Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka, bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika. 15 11:15Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka, bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama. 16 11:16Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu. 17 11:17Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe. 18 11:18Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika. 19 11:19Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake. 20 11:20 Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama. 21 11:21Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru. 22 11:22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara. 23 11:23Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema, bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu. 24 11:24Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, mwingine huzuia, lakini huwa maskini. 25 11:25Mtu mkarimu atastawi; yeye awaburudishaye wengine ataburudishwa mwenyewe. 26 11:26Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka, bali baraka itamkalia kichwani kama taji yeye aliye radhi kuiuza. 27 11:27Yeye atafutaye mema hupata ukarimu, bali ubaya huja kwake yeye autafutaye. 28 11:28Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka, bali mwenye haki atastawi kama jani bichi. 29 11:29Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo, naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima. 30 11:30Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huvuta roho za watu. 31 11:31Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi? 12Mafundisho Ya Kifamilia Na Ya Kijamii 1 12:1Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa, bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu. 2 12:2Mtu mwema hupata kibali kutoka kwa Bwana, bali Bwana humhukumu mwenye hila. 3 12:3Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa. 4 12:4Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe. 5 12:5Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu. 6 12:6Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa. 7 12:7Watu waovu huondolewa na kutoweka, bali nyumba ya mwenye haki husimama imara. 8 12:8Mtu husifiwa kulingana na hekima yake, bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa. 9 12:9Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi, kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula. 10 12:10Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake, bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili. 11 12:11Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili. 12 12:12Waovu hutamani mateka ya watu wabaya, bali shina la mwenye haki hustawi. 13 12:13Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi, bali mwenye haki huepuka taabu. 14 12:14Kutokana na tunda la midomo yake mtu hujazwa na mambo mema, hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza. 15 12:15Njia ya mpumbavu huonekana sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri. 16 12:16Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja, bali mtu wa busara hupuuza matukano. 17 12:17Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika, bali shahidi wa uongo husema uongo. 18 12:18Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji. 19 12:19Midomo isemayo kweli hudumu milele, bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu. 20 12:20Upo udanganyifu katika mioyo ya wale ambao hupanga mabaya, bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani. 21 12:21Hakuna dhara linalompata mwenye haki, bali waovu wana taabu nyingi. 22 12:22 Bwana anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli. 23 12:23Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe, bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu. 24 12:24Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa. 25 12:25Moyo wa wasiwasi humlemea mtu, bali neno la huruma humfurahisha. 26 12:26Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki, bali njia ya waovu huwapotosha. 27 12:27Mtu mvivu haoki mawindo yake, bali mtu mwenye bidii ana mali za thamani. 28 12:28Katika njia ya haki kuna uzima; katika mapito hayo kuna maisha ya milele. 13Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu 1 13:1Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye, bali mwenye dharau hasikilizi maonyo. 2 13:2Kutoka tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema, bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri. 3 13:3Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake, bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia. 4 13:4Mvivu hutamani sana na hapati kitu, bali nafsi ya mwenye bidii hutoshelezwa kikamilifu. 5 13:5Mwenye haki huchukia uongo, bali waovu huleta aibu na fedheha. 6 13:6Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi. 7 13:7Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi. 8 13:8Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho. 9 13:9Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana, bali taa ya mwovu itazimwa. 10 13:10Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri. 11 13:11Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka. 12 13:12Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua, bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima. 13 13:13Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi, bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo. 14 13:14Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. 15 13:15Ufahamu mzuri hupata upendeleo, bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu. 16 13:16Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa, bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake. 17 13:17Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu, bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji. 18 13:18Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu, bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa. 19 13:19Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi, bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya. 20 13:20Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima, bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara. 21 13:21Balaa humwandama mtenda dhambi, bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki. 22 13:22Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi, bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa kwa ajili ya wenye haki. 23 13:23Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi, bali dhuluma hukifutilia mbali. 24 13:24Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe, bali yeye ampendaye huwa mwangalifu kumwadibisha. 25 13:25Mwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake, bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa. 141 14:1Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. 2 14:2Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana, bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. 3 14:3Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake, bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake. 4 14:4Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu, bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi. 5 14:5Shahidi mwaminifu hadanganyi, bali shahidi wa uongo humimina uongo. 6 14:6Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati, bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua. 7 14:7Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake. 8 14:8Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. 9 14:9Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu. 10 14:10Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake. 11 14:11Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. 12 14:12Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. 13 14:13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi. 14 14:14Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao, naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake. 15 14:15Mtu mjinga huamini kila kitu, bali mwenye busara hufikiria hatua zake. 16 14:16Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe. 17 14:17Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu, naye mtu wa hila huchukiwa. 18 14:18Mjinga hurithi upumbavu, bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji. 19 14:19Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema, nao waovu kwenye malango ya wenye haki. 20 14:20Maskini huepukwa hata na majirani zao, bali matajiri wana marafiki wengi. 21 14:21Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi, bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji. 22 14:22Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki? Bali wale wanaopanga kilicho chema hupata upendo na uaminifu. 23 14:23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. 24 14:24Utajiri wa wenye hekima ni taji yao, bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu. 25 14:25Shahidi wa kweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu. 26 14:26Yeye amchaye Bwana ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio. 27 14:27Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. 28 14:28Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme, bali pasipo watu mkuu huangamia. 29 14:29Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu. 30 14:30Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa. 31 14:31Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. 32 14:32Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu, bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio. 33 14:33Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu. 34 14:34Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote. 35 14:35Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, bali ghadhabu yake humwangukia mtumishi mwenye kuaibisha. 151 15:1Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira. 2 15:2Ulimi wa mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hufoka upumbavu. 3 15:3Macho ya Bwana yako kila mahali, yakiwaangalia waovu na wema. 4 15:4Ulimi uletao uponyaji ni mti wa uzima, bali ulimi udanganyao huponda roho. 5 15:5Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake, bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara. 6 15:6Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu. 7 15:7Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. 8 15:8 Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu. 9 15:9 Bwana huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki. 10 15:10Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa. 11 15:11Mauti 15:11 Yaani Sheol, maana yake ni Kuzimu. na Uharibifu 15:11 Kwa Kiebrania ni Abadon. viko wazi mbele za Bwana: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu! 12 15:12Mwenye mzaha huchukia maonyo; hatataka shauri kwa mwenye hekima. 13 15:13Moyo wenye furaha hufanya uso uchangamke, bali maumivu ya moyoni huponda roho. 14 15:14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hujilisha upumbavu. 15 15:15Siku zote za wanaoonewa ni za taabu, bali moyo mchangamfu una karamu ya kudumu. 16 15:16Afadhali kuwa na kidogo pamoja na kumcha Bwana, kuliko mali nyingi pamoja na ghasia. 17 15:17Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki. 18 15:18Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi. 19 15:19Njia ya mvivu imezibwa na miiba, bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu. 20 15:20Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake. 21 15:21Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka. 22 15:22Mipango hushindwa kufanikiwa kwa ajili ya kukosa ushauri, bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa. 23 15:23Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa: je, ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake! 24 15:24Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima kumwepusha asiende chini kaburini. 25 15:25 Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe. 26 15:26 Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. 27 15:27Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi. 28 15:28Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya. 29 15:29 Bwana yuko mbali na waovu, bali husikia maombi ya wenye haki. 30 15:30Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, nazo habari njema huipa mifupa afya. 31 15:31Yeye asikilizaye maonyo yatoayo uzima atakuwa miongoni mwa wenye hekima. 32 15:32Yeye anayedharau maonyo hujidharau mwenyewe, bali yeyote anayekubali maonyo hupata ufahamu. 33 15:33Kumcha Bwana humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima. 161 16:1Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana. 2 16:2Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na Bwana. 3 16:3Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. 4 16:4 Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi. 5 16:5 Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa. 6 16:6Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya. 7 16:7Njia za mtu zinapompendeza Bwana, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani. 8 16:8Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. 9 16:9Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake. 10 16:10Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, wala kinywa chake hakipotoshi haki. 11 16:11Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye. 12 16:12Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki. 13 16:13Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu; humthamini mtu asemaye kweli. 14 16:14Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti, bali mtu mwenye hekima ataituliza. 15 16:15Uso wa mfalme ungʼaapo, inamaanisha uhai; upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli. 16 16:16Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha! 17 16:17Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake. 18 16:18Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko. 19 16:19Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho miongoni mwa walioonewa kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi. 20 16:20Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana. 21 16:21Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu, na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho. 22 16:22Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao, bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu. 23 16:23Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho. 24 16:24Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa. 25 16:25Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. 26 16:26Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi; njaa yake humsukuma aendelee. 27 16:27Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya, maneno yake ni kama moto uunguzao. 28 16:28Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu. 29 16:29Mtu mkali humvuta jirani yake na kumwongoza katika mapito yale mabaya. 30 16:30Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu; naye akazaye midomo yake amenuia mabaya. 31 16:31Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu. 32 16:32Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji. 33 16:33Kura hupigwa kwa siri, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana. 171 17:1Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi. 2 17:2Mtumishi mwenye hekima atatawala juu ya mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu. 3 17:3Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru ni kwa ajili ya dhahabu, bali Bwana huujaribu moyo. 4 17:4Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara. 5 17:5Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. 6 17:6Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao. 7 17:7Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala! 8 17:8Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kokote kigeukiapo, hufanikiwa. 9 17:9Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo, bali yeyote arudiaye jambo hutenganisha marafiki wa karibu. 10 17:10Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua kuliko mapigo mia kwa mpumbavu. 11 17:11Mtu mbaya hupenda kuasi tu; mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake. 12 17:12Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake. 13 17:13Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake. 14 17:14Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza. 15 17:15Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Bwana huwachukia sana wote wawili. 16 17:16Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu, wakati yeye hana haja ya kupata hekima? 17 17:17Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida. 18 17:18Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani, naye huweka dhamana kwa jirani yake. 19 17:19Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake 17:19 Kuinua lango maana yake ni kusema kwa majivuno. hutafuta uharibifu. 20 17:20Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu. 21 17:21Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu. 22 17:22Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa. 23 17:23Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri ili kupotosha njia ya haki. 24 17:24Mtu wa ufahamu huitazama hekima, lakini macho ya mpumbavu huhangaika hadi kwenye miisho ya dunia. 25 17:25Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa. 26 17:26Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia, au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao. 27 17:27Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu. 28 17:28Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima kama akinyamaza, na mwenye ufahamu kama akiuzuia ulimi wake. 181 18:1Mtu ajitengaye na wengine hufuata matakwa yake mwenyewe; hupiga vita kila shauri jema. 2 18:2Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe. 3 18:3Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia, pamoja na aibu huja lawama. 4 18:4Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji, bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika. 5 18:5Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu, au kumnyima haki asiye na hatia. 6 18:6Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi na kinywa chake hualika kipigo. 7 18:7Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake. 8 18:8Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu. 9 18:9Mtu aliye mlegevu katika kazi yake ni ndugu na yule anayeharibu. 10 18:10Jina la Bwana ni ngome imara, wenye haki huikimbilia na kuwa salama. 11 18:11Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa. 12 18:12Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi, bali unyenyekevu hutangulia heshima. 13 18:13Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza, huo ni upumbavu wake na aibu yake. 14 18:14Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili? 15 18:15Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa, masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa. 16 18:16Zawadi humfungulia njia mtoaji, nayo humleta mbele ya wakuu. 17 18:17Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi, hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali. 18 18:18Kupiga kura hukomesha mashindano na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana. 19 18:19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika kuliko mji uliozungushiwa ngome, nayo mabishano ni kama malango ya ngome yenye makomeo. 20 18:20Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake, atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake. 21 18:21Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake. 22 18:22Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa Bwana. 23 18:23Mtu maskini huomba kuhurumiwa bali tajiri hujibu kwa ukali. 24 18:24Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu, bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu. 191 19:1Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka. 2 19:2Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia. 3 19:3Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana. 4 19:4Mali huleta marafiki wengi, bali rafiki wa mtu maskini humwacha. 5 19:5Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru. 6 19:6Wengi hujipendekeza kwa mtawala na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi. 7 19:7Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote: Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani! Ingawa huwafuata kwa kuwasihi, hawapatikani popote. 8 19:8Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi. 9 19:9Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo ataangamia. 10 19:10Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu. 11 19:11Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa. 12 19:12Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi. 13 19:13Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha. 14 19:14Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana. 15 19:15Uvivu huleta usingizi mzito, naye mtu mzembe huona njaa. 16 19:16Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake, bali yeye anayezidharau njia zake atakufa. 17 19:17Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, naye atamtuza kwa aliyotenda. 18 19:18Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini, usiwe mshirika katika mauti yake. 19 19:19Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake, kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena. 20 19:20Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho, nawe mwishoni utakuwa na hekima. 21 19:21Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu, lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama. 22 19:22Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho, afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo. 23 19:23Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima, kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, bila kuguswa na shida. 24 19:24Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake! 25 19:25Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara, mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa. 26 19:26Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake ni mwana aletaye aibu na fedheha. 27 19:27Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utatangatanga mbali na maneno ya maarifa. 28 19:28Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi. 29 19:29Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu. 201 20:1Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi; yeyote apotoshwaye navyo hana hekima. 2 20:2Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. 3 20:3Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana. 4 20:4Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati chochote. 5 20:5Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. 6 20:6Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata? 7 20:7Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake. 8 20:8Wakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu, hupepeta ubaya wote kwa macho yake. 9 20:9Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi; mimi ni safi na sina dhambi?” 10 20:10Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, Bwana huchukia vyote viwili. 11 20:11Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni safi na adili. 12 20:12Masikio yasikiayo na macho yaonayo, Bwana ndiye alivifanya vyote viwili. 13 20:13Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. 14 20:14“Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake. 15 20:15Dhahabu kunayo, na marijani kwa wingi, lakini midomo inenayo maarifa ni kito cha thamani kilicho adimu. 16 20:16Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu. 17 20:17Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu, bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe. 18 20:18Fanya mipango kwa kutafuta mashauri, ukipigana vita, tafuta maelekezo. 19 20:19Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika, kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi. 20 20:20Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itazimwa katika giza nene. 21 20:21Urithi upatikanao haraka mwanzoni, hautabarikiwa mwishoni. 22 20:22Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!” Mngojee Bwana, naye atakuokoa. 23 20:23 Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu, nazo mizani zisizo halali hazimpendezi. 24 20:24Hatua za mtu huongozwa na Bwana. Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe? 25 20:25Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake. 26 20:26Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu, hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao. 27 20:27Taa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani. 28 20:28Upendo na uaminifu humweka mfalme salama, kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama. 29 20:29Utukufu wa vijana ni nguvu zao, mvi ni fahari ya uzee. 30 20:30Mapigo na majeraha huusafisha ubaya, nayo michapo hutakasa utu wa ndani. 211 21:1Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana; huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo. 2 21:2Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali Bwana huupima moyo. 3 21:3Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu. 4 21:4Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi! 5 21:5Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini. 6 21:6Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha. 7 21:7Jeuri ya waovu itawaburuta mbali, kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa. 8 21:8Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu, bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu. 9 21:9Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. 10 21:10Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake. 11 21:11Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, mjinga hupata hekima; wakati mtu mwenye hekima afundishwapo, hupata maarifa. 12 21:12Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu, naye atawaangamiza waovu. 13 21:13Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini, yeye pia atalia, wala hatajibiwa. 14 21:14Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. 15 21:15Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali kitisho kwa watenda mabaya. 16 21:16Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa. 17 21:17Mtu apendaye anasa atakuwa maskini, yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri. 18 21:18Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki, nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu. 19 21:19Ni afadhali kuishi jangwani kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi. 20 21:20Katika nyumba ya mwenye hekima kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta, lakini mtu mpumbavu hutafuna vyote alivyo navyo. 21 21:21Yeye afuatiaye haki na upendo hupata uzima, mafanikio na heshima. 22 21:22Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu, na kuangusha ngome wanazozitegemea. 23 21:23Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake hujilinda na maafa. 24 21:24Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake; hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi. 25 21:25Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake, kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi. 26 21:26Mchana kutwa hutamani zaidi, lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia. 27 21:27Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo, si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya! 28 21:28Shahidi wa uongo ataangamia, bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu. 29 21:29Mtu mwovu ana uso wa ushupavu, bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake. 30 21:30Hakuna hekima, wala akili, wala mpango unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana. 31 21:31Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Bwana. 221 22:1Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi, kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu. 2 22:2Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: Bwana ni Muumba wao wote. 3 22:3Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa. 4 22:4Unyenyekevu na kumcha Bwana huleta utajiri, heshima na uzima. 5 22:5Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego, bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo. 6 22:6Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee. 7 22:7Matajiri huwatawala maskini naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye. 8 22:8Yeye aupandaye uovu huvuna taabu, nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa. 9 22:9Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini. 10 22:10Mfukuze mwenye dhihaka, na mvutano utatoweka; ugomvi na matukano vitakoma. 11 22:11Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake. 12 22:12Macho ya Bwana hulinda maarifa, bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu. 13 22:13Mvivu husema, “Yuko simba nje!” au, “Nitauawa katika mitaa!” 14 22:14Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu; yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana atatumbukia ndani yake. 15 22:15Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye. 16 22:16Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali, naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini. Misemo Ya Wenye Hekima 17 22:17Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, 18 22:18kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako. 19 22:19Ili tumaini lako liwe katika Bwana, hata wewe, ninakufundisha leo. 20 22:20Je, sijakuandikia misemo thelathini, misemo ya mashauri na maarifa, 21 22:21kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika, ili uweze kutoa majibu sahihi kwake yeye aliyekutuma? 22 22:22Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini, wala kumdhulumu mhitaji mahakamani, 23 22:23kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao naye atawateka wao waliowateka. 24 22:24Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka, usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika, 25 22:25la sivyo utajifunza njia zake na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego. 26 22:26Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani, au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni. 27 22:27Kama ukikosa njia ya kulipa, kitanda chako kitachukuliwa ukiwa umekilalia. 28 22:28Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani lililowekwa na baba zako. 29 22:29Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake? Atahudumu mbele ya wafalme; hatahudumu mbele ya watu duni. 231 23:1Uketipo kula chakula na mtawala, angalia vyema kile kilicho mbele yako, 2 23:2na utie kisu kooni mwako kama ukiwa mlafi. 3 23:3Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila. 4 23:4Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonyesha kujizuia. 5 23:5Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafula, ukaruka na kutoweka angani kama tai. 6 23:6Usile chakula cha mtu mchoyo, usitamani vyakula vyake vitamu, 7 23:7kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe. 8 23:8Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu. 9 23:9Usizungumze na mpumbavu, kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako. 10 23:10Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima, 11 23:11kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu, atalichukua shauri lao dhidi yako. 12 23:12Elekeza moyo wako kwenye mafundisho na masikio yako kwenye maneno ya maarifa. 13 23:13Usimnyime mtoto adhabu, ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa. 14 23:14Mwadhibu kwa fimbo na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini. 23:14 Mautini maana yake ni Kuzimu. 15 23:15Mwanangu, kama moyo wako una hekima, basi moyo wangu utafurahi, 16 23:16utu wangu wa ndani utafurahi, wakati midomo yako itakapozungumza lililo sawa. 17 23:17Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana. 18 23:18Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali. 19 23:19Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima, weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa. 20 23:20Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa, 21 23:21kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara. 22 23:22Msikilize baba yako, aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee. 23 23:23Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu. 24 23:24Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa, naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia. 25 23:25Baba yako na mama yako na wafurahi, mama aliyekuzaa na ashangilie! 26 23:26Mwanangu, nipe moyo wako, macho yako na yafuate njia zangu, 27 23:27kwa maana kahaba ni shimo refu na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba. 28 23:28Kama mnyangʼanyi, hungojea akivizia, naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume. 29 23:29Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani mwenye macho mekundu? 30 23:30Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo, hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa. 31 23:31Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu, wakati unapometameta kwenye bilauri, wakati ushukapo taratibu! 32 23:32Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu. 33 23:33Macho yako yataona mambo mageni na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka. 34 23:34Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari, alalaye juu ya kamba ya merikebu. 35 23:35Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! Wamenichapa, lakini sisikii! Nitaamka lini ili nikanywe tena?” 241 24:1Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao; 2 24:2kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara. 3 24:3Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa 4 24:4kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza. 5 24:5Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu, 6 24:6kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi. 7 24:7Hekima i juu mno kwa mpumbavu, katika kusanyiko langoni hana lolote la kusema. 8 24:8Yeye apangaye mabaya atajulikana kama mtu wa hila. 9 24:9Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka. 10 24:10Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo! 11 24:11Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. 12 24:12Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda? 13 24:13Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja. 14 24:14Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali. 15 24:15Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake, 16 24:16Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa. 17 24:17Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie. 18 24:18 Bwana asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye. 19 24:19Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya wala usiwaonee wivu waovu, 20 24:20kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa. 21 24:21Mwanangu, mche Bwana na mfalme, wala usijiunge na waasi, 22 24:22kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta? Misemo Zaidi Ya Wenye Hekima

23 24:23Hii pia ni misemo ya wenye hekima:

Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema: 24 24:24Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” Kabila zitamlaani na mataifa yatamkana. 25 24:25Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, nazo baraka tele zitawajilia juu yao. 26 24:26Jawabu la uaminifu ni kama busu la midomoni. 27 24:27Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako. 28 24:28Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya. 29 24:29Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.” 30 24:30Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, 31 24:31miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka. 32 24:32Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona: 33 24:33Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: 34 24:34hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha. 25Mithali Zaidi Za Solomoni

1 25:1Hizi ni mithali zaidi za Solomoni, zilizonakiliwa na watu wa Hezekia mfalme wa Yuda:

2 25:2Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo. 3 25:3Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini, ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki. 4 25:4Ondoa takataka kwenye madini ya fedha, nako ndani yake kutatokea chombo cha mfua fedha. 5 25:5Ondoa waovu mbele ya mfalme, nacho kiti chake cha enzi kitaimarishwa kwa njia ya haki. 6 25:6Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu; 7 25:7ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu. Kile ulichokiona kwa macho yako 8 25:8usiharakishe kukipeleka mahakamani, maana utafanya nini mwishoni kama jirani yako atakuaibisha? 9 25:9Kama ukifanya shauri na jirani yako, usisaliti siri ya mtu mwingine, 10 25:10ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka. 11 25:11Neno lisemwalo kwa wakati ufaao ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha. 12 25:12Kama vile kipuli cha dhahabu au pambo la dhahabu safi, ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima kwa sikio lisikilizalo. 13 25:13Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao, huburudisha roho za bwana zake. 14 25:14Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi. 15 25:15Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa, nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa. 16 25:16Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha, ukila zaidi, utatapika. 17 25:17Ingiza mguu wako nyumbani kwa jirani yako mara chache, ukizidisha, atakukinai na atakuchukia. 18 25:18Kama vile rungu au upanga au mshale mkali ndivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake. 19 25:19Kama vile jino bovu au mguu uliolemaa, ndivyo ilivyo kumtegemea mtu asiye mwaminifu wakati wa shida. 20 25:20Kama vile avuaye mavazi siku ya baridi, au kama siki iliyomwagwa juu ya magadi, ndivyo alivyo yeye amuimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito. 21 25:21Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale; kama ana kiu, mpe maji anywe. 22 25:22Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake, naye Bwana atakupa thawabu. 23 25:23Kama vile upepo wa kaskazini uletavyo mvua, ndivyo ulimi usingiziao uletavyo uso wa hasira. 24 25:24Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. 25 25:25Kama vile maji baridi kwa nafsi iliyochoka ndivyo zilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali. 26 25:26Kama vile chemchemi iliyotibuliwa matope au kisima kilichotiwa taka ndivyo alivyo mtu mwenye haki akishiriki na waovu. 27 25:27Si vyema kula asali nyingi sana, wala si heshima kujitafutia heshima yako mwenyewe. 28 25:28Kama vile mji ambao kuta zake zimebomoka ndivyo alivyo mtu ambaye hawezi kujitawala mwenyewe. 261 26:1Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu. 2 26:2Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu. 3 26:3Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu! 4 26:4Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye. 5 26:5Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe. 6 26:6Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu. 7 26:7Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu. 8 26:8Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima. 9 26:9Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu. 10 26:10Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani. 11 26:11Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake. 12 26:12Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake. 13 26:13Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!” 14 26:14Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake. 15 26:15Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake. 16 26:16Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara. 17 26:17Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu. 18 26:18Kama mtu mwendawazimu atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha, 19 26:19ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!” 20 26:20Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika. 21 26:21Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi. 22 26:22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu. 23 26:23Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya. 24 26:24Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu. 25 26:25Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. 26 26:26Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko. 27 26:27Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia. 28 26:28Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu. 271 27:1Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. 2 27:2Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe. 3 27:3Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili. 4 27:4Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu? 5 27:5Afadhali karipio la wazi kuliko upendo uliofichika. 6 27:6Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. 7 27:7Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, bali kwa mwenye njaa hata kile kilicho kichungu kwake ni kitamu. 8 27:8Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake. 9 27:9Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu. 10 27:10Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali. 11 27:11Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau. 12 27:12Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa. 13 27:13Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu. 14 27:14Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kama ni laana. 15 27:15Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua. 16 27:16Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono. 17 27:17Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake. 18 27:18Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa. 19 27:19Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo. 20 27:20Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu. 21 27:21Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo. 22 27:22Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake. 23 27:23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako. 24 27:24Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote. 25 27:25Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa, 26 27:26wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba. 27 27:27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike. 281 28:1Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, bali wenye haki ni wajasiri kama simba. 2 28:2Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu. 3 28:3Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao. 4 28:4Wale waiachao sheria huwasifu waovu, bali wale waishikao sheria huwapinga. 5 28:5Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu. 6 28:6Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu. 7 28:7Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu, bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake. 8 28:8Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini. 9 28:9Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo. 10 28:10Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema. 11 28:11Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe, bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua. 12 28:12Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, bali waovu watawalapo, watu hujificha. 13 28:13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. 14 28:14Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huangukia kwenye taabu. 15 28:15Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge. 16 28:16Mtawala dhalimu hana akili, bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu atafurahia maisha marefu. 17 28:17Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro mpaka kufa; mtu yeyote na asimsaidie. 18 28:18Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula. 19 28:19Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha. 20 28:20Mtu mwaminifu atabarikiwa sana, bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka hataacha kuadhibiwa. 21 28:21Kuonyesha upendeleo si vizuri, hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate. 22 28:22Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri, naye hana habari kuwa umaskini unamngojea. 23 28:23Yeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi, kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili. 24 28:24Yeye amwibiaye babaye au mamaye na kusema, “Si kosa,” yeye ni mwenzi wa yule aharibuye. 25 28:25Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa. 26 28:26Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu, bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama. 27 28:27Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu chochote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi. 28 28:28Wakati waovu watawalapo, watu huenda mafichoni, bali waovu wanapoangamia, wenye haki hufanikiwa. 291 29:1Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi, ataangamia ghafula, wala hapati dawa. 2 29:2Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. 3 29:3Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake. 4 29:4Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza. 5 29:5Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. 6 29:6Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi. 7 29:7Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo. 8 29:8Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira. 9 29:9Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. 10 29:10Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu. 11 29:11Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia. 12 29:12Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu. 13 29:13Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: Bwana hutia nuru macho yao wote wawili. 14 29:14Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote. 15 29:15Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake. 16 29:16Wakati waovu wanapostawi, pia dhambi vivyo hivyo, lakini wenye haki wataliona anguko lao. 17 29:17Mrudi mwanao, naye atakupa amani, atakufurahisha nafsi yako. 18 29:18Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia, bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. 19 29:19Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, ajapoelewa, hataitikia. 20 29:20Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye. 21 29:21Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni. 22 29:22Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi. 23 29:23Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima. 24 29:24Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia. 25 29:25Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama. 26 29:26Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana. 27 29:27Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki. 30Misemo Ya Aguri

1 30:1Misemo ya Aguri mwana wa Yake, usia:

Huyu mtu alimwambia Ithieli, naam, kwa Ithieli na kwa Ukali: 2 30:2“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu. 3 30:3Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu. 4 30:4Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua! 5 30:5“Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia. 6 30:6Usiongeze kwenye maneno yake, ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo. 7 30:7“Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana; usininyime kabla sijafa: 8 30:8Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. 9 30:9Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘Bwana ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu. 10 30:10“Usimchongee mtumishi kwa bwana wake, asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo. 11 30:11“Wako watu wale ambao huwalaani baba zao na wala hawawabariki mama zao; 12 30:12wale ambao ni safi machoni pao wenyewe kumbe hawakuoshwa uchafu wao; 13 30:13wale ambao daima macho yao ni ya kiburi, ambao kutazama kwao ni kwa dharau; 14 30:14wale ambao meno yao ni panga na ambao mataya yao yamewekwa visu kuwaangamiza maskini katika nchi, na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu. 15 30:15“Mruba anao binti wawili waliao, ‘Nipe! Nipe!’ “Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe, naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’: 16 30:16Ni kaburi, tumbo lisilozaa, nchi isiyoshiba maji kamwe, na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ 17 30:17“Jicho lile limdhihakilo baba, lile linalodharau kumtii mama, litangʼolewa na kunguru wa bondeni, litaliwa na tai. 18 30:18“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana, naam, vinne nisivyovielewa: 19 30:19Ni mwendo wa tai katika anga, mwendo wa nyoka juu ya mwamba, mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari, nao mwendo wa mtu pamoja na msichana. 20 30:20“Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi, hula akapangusa kinywa chake na kusema, ‘Sikufanya chochote kibaya.’ 21 30:21“Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia: 22 30:22Mtumwa awapo mfalme, mpumbavu ashibapo chakula, 23 30:23mwanamke asiyependwa aolewapo, naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake. 24 30:24“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana: 25 30:25Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi. 26 30:26Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba. 27 30:27Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi. 28 30:28Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme. 29 30:29“Viko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao, naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha: 30 30:30simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, asiyerudi nyuma kwa chochote; 31 30:31jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu, naye mfalme pamoja na jeshi lake lililomzunguka. 32 30:32“Ikiwa umefanya upumbavu na ukajitukuza mwenyewe, au kama umepanga mabaya, basi funika mdomo wako na mkono wako. 33 30:33Kwa maana kama vile kusukasuka maziwa hutoa siagi, na pia kule kufinya pua hutoa damu, kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.” 31Misemo Ya Mfalme Lemueli

1 31:1Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

2 31:2“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu, ee mwana wa nadhiri zangu, 31:2 Au: Ewe uliye jibu la maombi yangu. 3 31:3Usitumie nguvu zako kwa wanawake, uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme. 4 31:4“Ee Lemueli, haifai wafalme, haifai wafalme kunywa mvinyo, haifai watawala kutamani sana kileo, 5 31:5wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa. 6 31:6Wape kileo wale wanaoangamia, mvinyo wale walio na uchungu, 7 31:7Wanywe na kusahau umaskini wao na wasikumbuke taabu yao tena. 8 31:8“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea, kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa. 9 31:9Sema na uamue kwa haki, tetea haki za maskini na wahitaji.” Maneno Ya Mwisho: Mke Mwenye Sifa Nzuri 10 31:10Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani. 31:10 Mithali 31:10-31 imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 11 31:11Mume wake anamwamini kikamilifu wala hakosi kitu chochote cha thamani. 12 31:12Humtendea mumewe mema, wala si mabaya, siku zote za maisha yake. 13 31:13Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii. 14 31:14Yeye ni kama meli za biashara akileta chakula chake kutoka mbali. 15 31:15Yeye huamka kungali bado giza huwapa jamaa yake chakula na mafungu kwa watumishi wake wa kike. 16 31:16Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu. 17 31:17Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake. 18 31:18Huona kwamba biashara yake ina faida, wala taa yake haizimiki usiku. 19 31:19Huweka mikono yake kwenye pia, navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi. 20 31:20Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake. 21 31:21Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto. 22 31:22Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake, yeye huvaa kitani safi na urujuani. 23 31:23Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi. 24 31:24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi. 25 31:25Amevikwa nguvu na heshima, anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo. 26 31:26Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake. 27 31:27Huangalia mambo ya nyumbani mwake wala hali chakula cha uvivu. 28 31:28Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa, mumewe pia humsifu, akisema: 29 31:29“Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri, lakini wewe umewapita wote.” 30 31:30Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi, bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa. 31 31:31Mpe thawabu anayostahili, nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.