Zaburi KITABU CHA KWANZA (Zaburi 1–41) Zaburi 1ZaburiFuraha Ya Kweli 1 Zaburi 1:1Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha. 2 Zaburi 1:2Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana. 3 Zaburi 1:3Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa. Huzuni Ya Waovu 4 Zaburi 1:4Sivyo walivyo waovu! Wao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. 5 Zaburi 1:5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu, wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki. 6 Zaburi 1:6Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia. Zaburi 2Mfalme Aliyechaguliwa Na Mungu 1 Zaburi 2:1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure? 2 Zaburi 2:2Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. 3 Zaburi 2:3Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” 4 Zaburi 2:4Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. 5 Zaburi 2:5Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, 6 Zaburi 2:6“Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” Ushindi Wa Mfalme 7 Zaburi 2:7Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa. 8 Zaburi 2:8Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako. 9 Zaburi 2:9Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.” 10 Zaburi 2:10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. 11 Zaburi 2:11Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka. 12 Zaburi 2:12Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia. Zaburi 3Sala Ya Asubuhi Ya Kuomba Msaada Zaburi ya Daudi. Alipomkimbia mwanawe Absalomu. 1 Zaburi 3:1Ee Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu! 2 Zaburi 3:2Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” 3 Zaburi 3:3Lakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. 4 Zaburi 3:4Ninamlilia Bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. 5 Zaburi 3:5Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza. 6 Zaburi 3:6Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande. 7 Zaburi 3:7Ee Bwana, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu. 8 Zaburi 3:8Kwa maana wokovu watoka kwa Bwana. Baraka yako na iwe juu ya watu wako. Zaburi 4Sala Ya Jioni Ya Kuomba Msaada Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 4:1Nijibu nikuitapo, Ee Mungu wangu mwenye haki! Nipumzishe katika shida zangu; nirehemu, usikie ombi langu. 2 Zaburi 4:2Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu kuwa aibu mpaka lini? Mtapenda udanganyifu na kufuata miungu ya uongo mpaka lini? 3 Zaburi 4:3Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga wale wamchao kwa ajili yake; Bwana atanisikia nimwitapo. 4 Zaburi 4:4Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu. 5 Zaburi 4:5Toeni dhabihu zilizo haki; mtegemeeni Bwana. 6 Zaburi 4:6Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye kutuonyesha jema lolote?” Ee Bwana, tuangazie nuru ya uso wako. 7 Zaburi 4:7Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi. 8 Zaburi 4:8Nitajilaza chini na kulala kwa amani, kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana, waniwezesha kukaa kwa salama. Zaburi 5Sala Kwa Ajili Ya Ulinzi Wakati Wa Hatari Kwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 5:1Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. 2 Zaburi 5:2Sikiliza kilio changu ili unisaidie, Mfalme wangu na Mungu wangu, kwa maana kwako ninaomba. 3 Zaburi 5:3Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana; asubuhi naleta haja zangu mbele zako, na kusubiri kwa matumaini. 4 Zaburi 5:4Wewe si Mungu unayefurahia uovu, kwako mtu mwovu hataishi. 5 Zaburi 5:5Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya. 6 Zaburi 5:6Unawaangamiza wasemao uongo. Bwana huwachukia wamwagao damu na wadanganyifu. 7 Zaburi 5:7Lakini mimi, kwa rehema zako kuu, nitakuja katika nyumba yako, kwa unyenyekevu, nitasujudu kuelekea Hekalu lako takatifu. 8 Zaburi 5:8Niongoze katika haki yako, Ee Bwana, kwa sababu ya adui zangu, nyoosha njia yako mbele yangu. 9 Zaburi 5:9Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika, mioyo yao imejaa maangamizi. Koo lao ni kaburi lililo wazi, kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu. 10 Zaburi 5:10Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu! Hila zao ziwe anguko lao wenyewe. Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi, kwa kuwa wamekuasi wewe. 11 Zaburi 5:11Lakini wote wakimbiliao kwako na wafurahi, waimbe kwa shangwe daima. Ueneze ulinzi wako juu yao, ili wale wapendao jina lako wapate kukushangilia. 12 Zaburi 5:12Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki, unawazunguka kwa wema wako kama ngao. Zaburi 6Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. 6:0 Sheminithi ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 6:1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. 2 Zaburi 6:2Unirehemu Bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee Bwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali. 3 Zaburi 6:3Nafsi yangu ina uchungu mwingi. Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini? 4 Zaburi 6:4Geuka Ee Bwana, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako. 5 Zaburi 6:5Hakuna mtu anayekukumbuka akiwa amekufa. Ni nani awezaye kukusifu akiwa kuzimu? 6 Zaburi 6:6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; usiku kucha nafurikisha kitanda changu kwa machozi; nimelowesha viti vyangu vya fahari kwa machozi. 7 Zaburi 6:7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote. 8 Zaburi 6:8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu. 9 Zaburi 6:9 Bwana amesikia kilio changu kwa huruma, Bwana amekubali sala yangu. 10 Zaburi 6:10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula. Zaburi 7Sala Ya Mtu Anayedhulumiwa Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini. 1 Zaburi 7:1Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia, 2 Zaburi 7:2la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. 3 Zaburi 7:3Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu, 4 Zaburi 7:4au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu, 5 Zaburi 7:5basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini. 6 Zaburi 7:6Amka kwa hasira yako, Ee Bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki. 7 Zaburi 7:7Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu. 8 Zaburi 7:8 Bwana na awahukumu kabila za watu. Nihukumu Ee Bwana, kwa kadiri ya haki yangu, kwa kadiri ya uadilifu wangu, Ewe Uliye Juu Sana. 9 Zaburi 7:9Ee Mungu mwenye haki, uchunguzaye mawazo na mioyo, komesha ghasia za waovu na ufanye wenye haki waishi kwa amani. 10 Zaburi 7:10Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, awaokoaye wanyofu wa moyo. 11 Zaburi 7:11Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku. 12 Zaburi 7:12Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. 13 Zaburi 7:13Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto. 14 Zaburi 7:14Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo. 15 Zaburi 7:15Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe. 16 Zaburi 7:16Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani. 17 Zaburi 7:17Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana. Zaburi 8Utukufu Wa Mungu Na Heshima Ya Mwanadamu Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 8:1Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu. 2 Zaburi 8:2Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa, kwa sababu ya watesi wako, kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. 3 Zaburi 8:3Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha, 4 Zaburi 8:4mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali? 5 Zaburi 8:5Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima. 6 Zaburi 8:6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya miguu yake. 7 Zaburi 8:7Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni, 8 Zaburi 8:8ndege wa angani na samaki wa baharini, naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari. 9 Zaburi 8:9Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! 9 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 10 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 9Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni. 9:0 Muth-labeni ni mtajo mmojawapo katika lugha za muziki. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 9:1Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. 2 Zaburi 9:2Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. 3 Zaburi 9:3Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako. 4 Zaburi 9:4Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki. 5 Zaburi 9:5Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu; umeyafuta majina yao milele na milele. 6 Zaburi 9:6Uharibifu usiokoma umempata adui, umeingʼoa miji yao; hata kumbukumbu lao limetoweka. 7 Zaburi 9:7 Bwana anatawala milele, ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu. 8 Zaburi 9:8Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki, atatawala mataifa kwa haki. 9 Zaburi 9:9 Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida. 10 Zaburi 9:10Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, kwa maana wewe Bwana, hujawaacha kamwe wakutafutao. 11 Zaburi 9:11Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda. 12 Zaburi 9:12Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, hapuuzi kilio cha wanaoonewa. 13 Zaburi 9:13Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti, 14 Zaburi 9:14ili niweze kutangaza sifa zako katika malango ya Binti Sayuni na huko niushangilie wokovu wako. 15 Zaburi 9:15Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha. 16 Zaburi 9:16 Bwana anajulikana kwa haki yake, waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao. 17 Zaburi 9:17Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. 18 Zaburi 9:18Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea. 19 Zaburi 9:19Ee Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde. Mataifa na yahukumiwe mbele zako. 20 Zaburi 9:20Ee Bwana, wapige kwa hofu, mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu. 10 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 10Sala Kwa Ajili Ya Haki 1 Zaburi 10:1Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali? Kwa nini unajificha wakati wa shida? 2 Zaburi 10:2Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. 3 Zaburi 10:3Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana Bwana. 4 Zaburi 10:4Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu. 5 Zaburi 10:5Njia zake daima hufanikiwa; hujivuna na amri zako ziko mbali naye, huwacheka kwa dharau adui zake wote. 6 Zaburi 10:6Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa, daima nitakuwa na furaha, kamwe sitakuwa na shida.” 7 Zaburi 10:7Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho; shida na ubaya viko chini ya ulimi wake. 8 Zaburi 10:8Huvizia karibu na vijiji; kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia, akivizia wapitaji. 9 Zaburi 10:9Huvizia kama simba aliye mawindoni; huvizia kumkamata mnyonge, huwakamata wanyonge na kuwaburuza katika wavu wake. 10 Zaburi 10:10Mateka wake hupondwa, huzimia; wanaanguka katika nguvu zake. 11 Zaburi 10:11Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.” 12 Zaburi 10:12Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge. 13 Zaburi 10:13Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu? Kwa nini anajiambia mwenyewe, “Hataniita nitoe hesabu?” 14 Zaburi 10:14Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima. 15 Zaburi 10:15Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya, mwite atoe hesabu ya maovu yake ambayo yasingejulikana. 16 Zaburi 10:16 Bwana ni Mfalme milele na milele, mataifa wataangamia watoke nchini mwake. 17 Zaburi 10:17Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao, 18 Zaburi 10:18ukiwatetea yatima na walioonewa, ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena. Zaburi 11Kumtumaini Bwana Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 11:1Kwa Bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako. 2 Zaburi 11:2Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo. 3 Zaburi 11:3Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?” 4 Zaburi 11:4 Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu. 5 Zaburi 11:5 Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia. 6 Zaburi 11:6Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao. 7 Zaburi 11:7Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake. Zaburi 12Kuomba Msaada Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 12:1 Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu. 2 Zaburi 12:2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu. 3 Zaburi 12:3 Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno, 4 Zaburi 12:4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?” 5 Zaburi 12:5“Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge na kulia kwa uchungu kwa wahitaji, nitainuka sasa,” asema Bwana. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.” 6 Zaburi 12:6Maneno ya Bwana ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba. 7 Zaburi 12:7Ee Bwana, utatuweka salama na kutulinda na kizazi hiki milele. 8 Zaburi 12:8Watu waovu huenda wakiringa kila mahali wakati ambapo yule aliye mbaya sana ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu. Zaburi 13Sala Ya Kuomba Msaada Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 13:1Mpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako mpaka lini? 2 Zaburi 13:2Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini? 3 Zaburi 13:3Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti. 4 Zaburi 13:4Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka. 5 Zaburi 13:5Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako. 6 Zaburi 13:6Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu. Zaburi 14Uovu Wa Wanadamu (Zaburi 53) Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 14:1Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema. 2 Zaburi 14:2 Bwana anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. 3 Zaburi 14:3Wote wamepotoka, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja! 4 Zaburi 14:4Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza: wale ambao huwala watu wangu kama watu walavyo mkate, hao ambao hawamwiti Bwana? 5 Zaburi 14:5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu, maana Mungu yupo pamoja na wenye haki. 6 Zaburi 14:6Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini, bali Bwana ndiye kimbilio lao. 7 Zaburi 14:7Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni! Wakati Bwana arejeshapo wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi! Zaburi 15Kitu Mungu Anachotaka Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 15:1 Bwana, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? 2 Zaburi 15:2Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake, 3 Zaburi 15:3na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake, 4 Zaburi 15:4ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia. 5 Zaburi 15:5Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika. Zaburi 16Sala Ya Matumaini Utenzi wa Daudi. 1 Zaburi 16:1Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia. 2 Zaburi 16:2Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” 3 Zaburi 16:3Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. 4 Zaburi 16:4Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu. 5 Zaburi 16:5 Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama. 6 Zaburi 16:6Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri. 7 Zaburi 16:7Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha. 8 Zaburi 16:8Nimemweka Bwana mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika. 9 Zaburi 16:9Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama, 10 Zaburi 16:10kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu. 11 Zaburi 16:11Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume. Zaburi 17Sala Ya Mtu Asiye Na Hatia Sala ya Daudi. 1 Zaburi 17:1Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu. 2 Zaburi 17:2Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki. 3 Zaburi 17:3Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi. 4 Zaburi 17:4Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri. 5 Zaburi 17:5Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza. 6 Zaburi 17:6Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu. 7 Zaburi 17:7Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao. 8 Zaburi 17:8Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako 9 Zaburi 17:9kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka. 10 Zaburi 17:10Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno. 11 Zaburi 17:11Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini. 12 Zaburi 17:12Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni. 13 Zaburi 17:13Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako. 14 Zaburi 17:14Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. 15 Zaburi 17:15Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako. Zaburi 18Wimbo Wa Daudi Wa Ushindi (2 Samweli 22:1-51) Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana aliyomwimbia Bwana wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Alisema hivi: 1 Zaburi 18:1Nakupenda wewe, Ee Bwana, nguvu yangu. 2 Zaburi 18:2 Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu. 3 Zaburi 18:3Ninamwita Bwana anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. 4 Zaburi 18:4Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. 5 Zaburi 18:5Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. 6 Zaburi 18:6Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake. 7 Zaburi 18:7Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya milima ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. 8 Zaburi 18:8Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake. 9 Zaburi 18:9Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. 10 Zaburi 18:10Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo. 11 Zaburi 18:11Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika, hema lake kumzunguka, mawingu meusi ya mvua ya angani. 12 Zaburi 18:12Kutokana na mwanga wa uwepo wake mawingu yalisogea, ikanyesha mvua ya mawe na umeme wa radi. 13 Zaburi 18:13 Bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. 14 Zaburi 18:14Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza. 15 Zaburi 18:15Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako. 16 Zaburi 18:16Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. 17 Zaburi 18:17Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. 18 Zaburi 18:18Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu. 19 Zaburi 18:19Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. 20 Zaburi 18:20 Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. 21 Zaburi 18:21Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. 22 Zaburi 18:22Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. 23 Zaburi 18:23Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi. 24 Zaburi 18:24 Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake. 25 Zaburi 18:25Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia. 26 Zaburi 18:26Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi. 27 Zaburi 18:27Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini huwashusha wenye kiburi. 28 Zaburi 18:28Wewe, Ee Bwana, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka; Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga. 29 Zaburi 18:29Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta. 30 Zaburi 18:30Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. 31 Zaburi 18:31Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? 32 Zaburi 18:32Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. 33 Zaburi 18:33Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. 34 Zaburi 18:34Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. 35 Zaburi 18:35Hunipa ngao yako ya ushindi, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, unajishusha chini ili kuniinua. 36 Zaburi 18:36Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze. 37 Zaburi 18:37Niliwafuatia adui zangu na nikawapata, sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa. 38 Zaburi 18:38Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena; walianguka chini ya miguu yangu. 39 Zaburi 18:39Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. 40 Zaburi 18:40Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, nami nikawaangamiza adui zangu. 41 Zaburi 18:41Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu. 42 Zaburi 18:42Niliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo; niliwamwaga nje kama tope barabarani. 43 Zaburi 18:43Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu; umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa, watu ambao sikuwajua wananitumikia. 44 Zaburi 18:44Mara wanisikiapo hunitii, wageni hunyenyekea mbele yangu. 45 Zaburi 18:45Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. 46 Zaburi 18:46 Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu! 47 Zaburi 18:47Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, awatiishaye mataifa chini yangu, 48 Zaburi 18:48aniokoaye na adui zangu. Uliniinua juu ya adui zangu; uliniokoa toka kwa watu wajeuri. 49 Zaburi 18:49Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana; nitaliimbia sifa jina lako. 50 Zaburi 18:50Humpa mfalme wake ushindi mkuu, huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, kwa Daudi na wazao wake milele. Zaburi 19Utukufu Wa Mungu Katika Uumbaji Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 19:1Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake. 2 Zaburi 19:2Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa. 3 Zaburi 19:3Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki. 4 Zaburi 19:4Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu. Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua, 5 Zaburi 19:5linafanana na bwana arusi akitoka chumbani mwake, kama shujaa afurahiavyo kukamilisha kushindana kwake. 6 Zaburi 19:6Huchomoza upande mmoja wa mbingu, na kufanya mzunguko wake hadi upande mwingine. Hakuna kilichojificha joto lake. 7 Zaburi 19:7Sheria ya Bwana ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima. 8 Zaburi 19:8Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni. 9 Zaburi 19:9Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki. 10 Zaburi 19:10Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega. 11 Zaburi 19:11Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa. 12 Zaburi 19:12Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. 13 Zaburi 19:13Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa. 14 Zaburi 19:14Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu. Zaburi 20Maombi Kwa Ajili Ya Ushindi Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 20:1 Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako. 2 Zaburi 20:2Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni. 3 Zaburi 20:3Na azikumbuke dhabihu zako zote, na azikubali sadaka zako za kuteketezwa. 4 Zaburi 20:4Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote. 5 Zaburi 20:5Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Bwana na akupe haja zako zote. 6 Zaburi 20:6Sasa nafahamu kuwa Bwana humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume. 7 Zaburi 20:7Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu. 8 Zaburi 20:8Wao wameshushwa chini na kuanguka, bali sisi tunainuka na kusimama imara. 9 Zaburi 20:9Ee Bwana, mwokoe mfalme! Tujibu tunapokuita! Zaburi 21Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Ushindi Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 21:1Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa! 2 Zaburi 21:2Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake. 3 Zaburi 21:3Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. 4 Zaburi 21:4Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele. 5 Zaburi 21:5Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu. 6 Zaburi 21:6Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako. 7 Zaburi 21:7Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa. 8 Zaburi 21:8Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako. 9 Zaburi 21:9Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza. 10 Zaburi 21:10Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu. 11 Zaburi 21:11Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa, 12 Zaburi 21:12kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka kwenye upinde wako. 13 Zaburi 21:13Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako. Zaburi 22Kilio Cha Uchungu Na Wimbo Wa Sifa Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 22:1Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu? 2 Zaburi 22:2Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi. 3 Zaburi 22:3Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli. 22:3 Tafsiri zingine zinasema: uketiye juu ya sifa za Israeli. 4 Zaburi 22:4Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa. 5 Zaburi 22:5Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika. 6 Zaburi 22:6Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau. 7 Zaburi 22:7Wote wanionao hunidhihaki, hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao: 8 Zaburi 22:8Husema, “Anamtegemea Bwana, basi Bwana na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.” 9 Zaburi 22:9Hata hivyo ulinitoa tumboni, ukanifanya nikutegemee, hata nilipokuwa ninanyonya matiti ya mama yangu. 10 Zaburi 22:10Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa, toka tumboni mwa mama yangu umekuwa Mungu wangu. 11 Zaburi 22:11Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia. 12 Zaburi 22:12Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira. 13 Zaburi 22:13Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu. 14 Zaburi 22:14Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu. 15 Zaburi 22:15Nguvu zangu zimekauka kama kigae, ulimi wangu umegandamana na kaakaa la kinywa changu, kwa sababu umenilaza katika mavumbi ya kifo. 16 Zaburi 22:16Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira, wametoboa mikono yangu na miguu yangu. 17 Zaburi 22:17Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, watu wananikodolea macho na kunisimanga. 18 Zaburi 22:18Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, na vazi langu wanalipigia kura. 19 Zaburi 22:19Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie. 20 Zaburi 22:20Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa. 21 Zaburi 22:21Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu. 22 Zaburi 22:22Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe. 23 Zaburi 22:23Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli! 24 Zaburi 22:24Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie. 25 Zaburi 22:25Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe. 26 Zaburi 22:26Maskini watakula na kushiba, wale wamtafutao Bwana watamsifu: mioyo yenu na iishi milele! 27 Zaburi 22:27Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia Bwana, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake, 28 Zaburi 22:28kwa maana ufalme ni wa Bwana naye hutawala juu ya mataifa. 29 Zaburi 22:29Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu. Wote waendao mavumbini watapiga magoti mbele yake, wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao. 30 Zaburi 22:30Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana. 31 Zaburi 22:31Watatangaza haki yake kwa watu ambao hawajazaliwa bado, kwa maana yeye ametenda hili. Zaburi 23Bwana Mchungaji Wetu Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 23:1 Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. 2 Zaburi 23:2Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, 3 Zaburi 23:3hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 4 Zaburi 23:4Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji. 5 Zaburi 23:5Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika. 6 Zaburi 23:6Hakika wema na upendo vitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. Zaburi 24Mfalme Mkuu Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 24:1Dunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake, ulimwengu, na wote waishio ndani yake, 2 Zaburi 24:2maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji. 3 Zaburi 24:3Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake? 4 Zaburi 24:4Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo. 5 Zaburi 24:5Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake. 6 Zaburi 24:6Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao, wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. 7 Zaburi 24:7Inueni vichwa vyenu, enyi malango, inukeni enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia. 8 Zaburi 24:8Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Ni Bwana aliye na nguvu na uweza, ni Bwana aliye hodari katika vita. 9 Zaburi 24:9Inueni vichwa vyenu, enyi malango, viinueni juu enyi milango ya kale, ili Mfalme wa utukufu apate kuingia. 10 Zaburi 24:10Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? Ni Bwana Mwenye Nguvu Zote; yeye ndiye Mfalme wa utukufu. 25 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 25Kumwomba Mungu Uongozi Na Ulinzi Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 25:1Kwako wewe, Ee Bwana, nainua nafsi yangu, 2 Zaburi 25:2ni wewe ninayekutumainia, Ee Mungu wangu. Usiniache niaibike, wala usiache adui zangu wakanishinda. 3 Zaburi 25:3Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea atakayeaibishwa, bali wataaibishwa wafanyao hila bila sababu. 4 Zaburi 25:4Nionyeshe njia zako, Ee Bwana, nifundishe mapito yako, 5 Zaburi 25:5niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote. 6 Zaburi 25:6Kumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo, kwa maana zimekuwepo tangu zamani. 7 Zaburi 25:7Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala njia zangu za uasi, sawasawa na upendo wako unikumbuke, kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana. 8 Zaburi 25:8 Bwana ni mwema na mwenye adili, kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake. 9 Zaburi 25:9Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake. 10 Zaburi 25:10Njia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake. 11 Zaburi 25:11Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. 12 Zaburi 25:12Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana? Atamfundisha katika njia atakayoichagua kwa ajili yake. 13 Zaburi 25:13Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi. 14 Zaburi 25:14Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, yeye huwajulisha agano lake. 15 Zaburi 25:15Macho yangu humwelekea Bwana daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego. 16 Zaburi 25:16Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka. 17 Zaburi 25:17Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu. 18 Zaburi 25:18Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote. 19 Zaburi 25:19Tazama adui zangu walivyo wengi, pia uone jinsi wanavyonichukia vikali! 20 Zaburi 25:20Uyalinde maisha yangu na uniokoe, usiniache niaibike, kwa maana nimekukimbilia wewe. 21 Zaburi 25:21Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako. 22 Zaburi 25:22Ee Mungu, wakomboe Israeli, katika shida zao zote! Zaburi 26Maombi Ya Mtu Mwema Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 26:1Ee Bwana, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Bwana bila kusitasita. 2 Zaburi 26:2Ee Bwana, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu; 3 Zaburi 26:3kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako. 4 Zaburi 26:4Siketi pamoja na watu wadanganyifu, wala siandamani na wanafiki, 5 Zaburi 26:5ninachukia kusanyiko la watenda mabaya na ninakataa kuketi pamoja na waovu. 6 Zaburi 26:6Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia, naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana, 7 Zaburi 26:7nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa, huku nikisimulia matendo yako ya ajabu. 8 Zaburi 26:8Ee Bwana, naipenda nyumba yako mahali unakoishi, mahali ambapo utukufu wako hukaa. 9 Zaburi 26:9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi, wala uhai wangu pamoja na wamwagao damu, 10 Zaburi 26:10ambao mikononi mwao kuna mipango miovu, ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa. 11 Zaburi 26:11Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; nikomboe na unihurumie. 12 Zaburi 26:12Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare; katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana. Zaburi 27Sala Ya Kusifu Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 27:1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani? 2 Zaburi 27:2Waovu watakaposogea dhidi yangu ili wanile nyama yangu, adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia, watajikwaa na kuanguka. 3 Zaburi 27:3Hata jeshi linizunguke pande zote, moyo wangu hautaogopa; hata vita vitokee dhidi yangu, hata hapo nitakuwa na ujasiri. 4 Zaburi 27:4Jambo moja ninamwomba Bwana, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana na kumtafuta hekaluni mwake. 5 Zaburi 27:5Kwa kuwa siku ya shida, atanihifadhi salama katika maskani yake, atanificha uvulini mwa hema yake na kuniweka juu kwenye mwamba. 6 Zaburi 27:6Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia Bwana na kumsifu. 7 Zaburi 27:7Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana, unihurumie na unijibu. 8 Zaburi 27:8Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, Bwana “Nitautafuta.” 9 Zaburi 27:9Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa hasira; wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu. 10 Zaburi 27:10Hata kama baba yangu na mama wakiniacha, Bwana atanipokea. 11 Zaburi 27:11Nifundishe njia yako, Ee Bwana, niongoze katika njia iliyonyooka kwa sababu ya watesi wangu. 12 Zaburi 27:12Usiniachilie kwa nia za adui zangu, kwa maana mashahidi wa uongo wameinuka dhidi yangu, wakipumua ujeuri. 13 Zaburi 27:13Nami bado nina tumaini hili: nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai. 14 Zaburi 27:14Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana. Zaburi 28Kuomba Msaada Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 28:1Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni. 2 Zaburi 28:2Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako. 3 Zaburi 28:3Usiniburute pamoja na waovu, pamoja na hao watendao mabaya, ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri, lakini mioyoni mwao wameficha chuki. 4 Zaburi 28:4Walipe sawasawa na matendo yao, sawasawa na matendo yao maovu; walipe sawasawa na kazi za mikono yao, uwalipe wanavyostahili. 5 Zaburi 28:5Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana, na yale ambayo mikono yake imetenda, atawabomoa na kamwe hatawajenga tena. 6 Zaburi 28:6 Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie. 7 Zaburi 28:7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo. 8 Zaburi 28:8 Bwana ni nguvu ya watu wake, ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake. 9 Zaburi 28:9Waokoe watu wako na uubariki urithi wako; uwe mchungaji wao na uwabebe milele. Zaburi 29Sauti Ya Bwana Wakati Wa Dhoruba Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 29:1Mpeni Bwana, enyi mashujaa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. 2 Zaburi 29:2Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake. 3 Zaburi 29:3Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu. 4 Zaburi 29:4Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu. 5 Zaburi 29:5Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni. 6 Zaburi 29:6Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, Sirioni 29:6 Yaani Mlima Hermoni. urukaruke kama mwana nyati. 7 Zaburi 29:7Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi. 8 Zaburi 29:8Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi. 9 Zaburi 29:9Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!” 10 Zaburi 29:10 Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika; Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele. 11 Zaburi 29:11 Bwana huwapa watu wake nguvu; Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani. Zaburi 30Maombi Ya Shukrani Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 30:1Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu. 2 Zaburi 30:2Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. 3 Zaburi 30:3Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. 4 Zaburi 30:4Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu. 5 Zaburi 30:5Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha. 6 Zaburi 30:6Nilipofanikiwa nilisema, “Sitatikiswa kamwe.” 7 Zaburi 30:7Ee Bwana, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika. 8 Zaburi 30:8Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, kwa Bwana niliomba rehema: 9 Zaburi 30:9“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako? 10 Zaburi 30:10Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, Ee Bwana, uwe msaada wangu.” 11 Zaburi 30:11Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe, 12 Zaburi 30:12ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele. Zaburi 31Maombi Na Sifa Kwa Kuokolewa Kutoka Kwa Adui Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 31:1Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe. 2 Zaburi 31:2Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka; uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa. 3 Zaburi 31:3Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako. 4 Zaburi 31:4Uniepushe na mtego niliotegewa, maana wewe ndiwe kimbilio langu. 5 Zaburi 31:5Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako, unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli. 6 Zaburi 31:6Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili; mimi ninamtumaini Bwana. 7 Zaburi 31:7Nitafurahia na kushangilia upendo wako, kwa kuwa uliona mateso yangu na ulijua maumivu ya nafsi yangu. 8 Zaburi 31:8Hukunikabidhi kwa adui yangu bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi. 9 Zaburi 31:9Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; macho yangu yanafifia kwa huzuni, nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko. 10 Zaburi 31:10Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa. 11 Zaburi 31:11Kwa sababu ya adui zangu wote, nimedharauliwa kabisa na jirani zangu, hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho, wale wanionao barabarani hunikimbia. 12 Zaburi 31:12Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa, nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika. 13 Zaburi 31:13Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi; vitisho viko pande zote; kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu, na kula njama kuniua. 14 Zaburi 31:14Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana; nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.” 15 Zaburi 31:15Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako, uniokoe mikononi mwa adui zangu na wale wanifuatiao. 16 Zaburi 31:16Mwangazie mtumishi wako uso wako, uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma. 17 Zaburi 31:17Usiniache niaibike, Ee Bwana, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu. 18 Zaburi 31:18Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, kwa maana kwa kiburi na dharau wao husema kwa majivuno dhidi ya wenye haki. 19 Zaburi 31:19Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako, uliowawekea akiba wakuchao, ambao huwapa wale wakukimbiliao machoni pa watu. 20 Zaburi 31:20Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako kutokana na hila za wanadamu; katika makao yako huwaweka salama kutokana na ndimi za mashtaka. 21 Zaburi 31:21Atukuzwe Bwana, kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu nilipokuwa katika mji uliozingirwa. 22 Zaburi 31:22Katika hofu yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie. 23 Zaburi 31:23Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote! Bwana huwahifadhi waaminifu, lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu. 24 Zaburi 31:24Kuweni hodari na mjipe moyo, ninyi nyote mnaomtumaini Bwana. Zaburi 32Furaha Ya Msamaha Zaburi ya Daudi. Funzo. 1 Zaburi 32:1Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa. 2 Zaburi 32:2Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi, na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu. 3 Zaburi 32:3Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa. 4 Zaburi 32:4Usiku na mchana mkono wako ulinilemea, nguvu zangu zilinyonywa kama vile katika joto la kiangazi. 5 Zaburi 32:5Kisha nilikujulisha dhambi yangu wala sikuficha uovu wangu. Nilisema, “Nitaungama makosa yangu kwa Bwana.” Ndipo uliponisamehe hatia ya dhambi yangu. 6 Zaburi 32:6Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe wakati unapopatikana, hakika maji makuu yatakapofurika hayatamfikia yeye. 7 Zaburi 32:7Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, utaniepusha na taabu na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu. 8 Zaburi 32:8Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; nitakushauri na kukuangalia. 9 Zaburi 32:9Usiwe kama farasi au nyumbu wasio na akili, ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu la sivyo hawatakukaribia. 10 Zaburi 32:10Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa Bwana unamzunguka mtu anayemtumaini. 11 Zaburi 32:11Shangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki! Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo! Zaburi 33Ukuu Na Wema Wa Mungu 1 Zaburi 33:1Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki; kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. 2 Zaburi 33:2Msifuni Bwana kwa kinubi, mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi. 3 Zaburi 33:3Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe. 4 Zaburi 33:4Maana neno la Bwana ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo. 5 Zaburi 33:5 Bwana hupenda uadilifu na haki; dunia imejaa upendo wake usiokoma. 6 Zaburi 33:6Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa, jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake. 7 Zaburi 33:7Ameyakusanya maji ya bahari kama kwenye chungu; vilindi vya bahari ameviweka katika ghala. 8 Zaburi 33:8Dunia yote na imwogope Bwana, watu wote wa dunia wamche. 9 Zaburi 33:9Kwa maana Mungu alisema, na ikawa, aliamuru na ikasimama imara. 10 Zaburi 33:10 Bwana huzuia mipango ya mataifa, hupinga makusudi ya mataifa. 11 Zaburi 33:11Lakini mipango ya Bwana inasimama imara milele, makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote. 12 Zaburi 33:12Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake. 13 Zaburi 33:13Kutoka mbinguni Bwana hutazama chini na kuwaona wanadamu wote; 14 Zaburi 33:14kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani: 15 Zaburi 33:15yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda. 16 Zaburi 33:16Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake; hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake. 17 Zaburi 33:17Farasi ni tumaini la bure kwa wokovu, licha ya nguvu zake nyingi, hawezi kuokoa. 18 Zaburi 33:18Lakini macho ya Bwana yako kwa wale wamchao, kwa wale tumaini lao liko katika upendo wake usio na kikomo, 19 Zaburi 33:19ili awaokoe na mauti, na kuwahifadhi wakati wa njaa. 20 Zaburi 33:20Sisi tunamngojea Bwana kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu. 21 Zaburi 33:21Mioyo yetu humshangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu. 22 Zaburi 33:22Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Bwana, tunapoliweka tumaini letu kwako. 34 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 34Sifa Na Wema Wa Mungu Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. 1 Zaburi 34:1Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote. 2 Zaburi 34:2Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi. 3 Zaburi 34:3Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja. 4 Zaburi 34:4Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. 5 Zaburi 34:5Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. 6 Zaburi 34:6Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote. 7 Zaburi 34:7Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa. 8 Zaburi 34:8Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia. 9 Zaburi 34:9Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote. 10 Zaburi 34:10Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema. 11 Zaburi 34:11Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana. 12 Zaburi 34:12Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema, 13 Zaburi 34:13basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo. 14 Zaburi 34:14Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia. 15 Zaburi 34:15Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao. 16 Zaburi 34:16Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, ili kufuta kumbukumbu lao duniani. 17 Zaburi 34:17Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote. 18 Zaburi 34:18 Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho. 19 Zaburi 34:19Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote, 20 Zaburi 34:20huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika. 21 Zaburi 34:21Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa. 22 Zaburi 34:22 Bwana huwakomboa watumishi wake, yeyote anayemkimbilia yeye hatahukumiwa kamwe. Zaburi 35Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 35:1Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami, upigane na hao wanaopigana nami. 2 Zaburi 35:2Chukua ngao na kigao. Inuka unisaidie. 3 Zaburi 35:3Inua mkuki wako na fumo 35:3 Fumo ni sawa na sagai, maana yake ni mkuki mfupi. lako dhidi ya hao wanaonifuatia. Iambie nafsi yangu, “Mimi ni wokovu wako.” 4 Zaburi 35:4Wafedheheshwe na waaibishwe wale wanaotafuta uhai wangu. Wanaofanya shauri kuniangamiza warudishwe nyuma kwa hofu. 5 Zaburi 35:5Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo, malaika wa Bwana akiwafukuza. 6 Zaburi 35:6Njia yao na iwe giza na ya utelezi, malaika wa Bwana akiwafuatilia. 7 Zaburi 35:7Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu, na bila sababu wamenichimbia shimo, 8 Zaburi 35:8maafa na yawapate ghafula: wavu walionifichia na uwatege wenyewe, na waanguke katika shimo hilo, kwa maangamizo yao. 9 Zaburi 35:9Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana na kuufurahia wokovu wake. 10 Zaburi 35:10Nitapaza sauti yangu nikisema, “Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana? Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao, maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!” 11 Zaburi 35:11Mashahidi wakatili wanainuka, wananiuliza mambo nisiyoyajua. 12 Zaburi 35:12Wananilipa baya kwa jema na kuiacha nafsi yangu ukiwa. 13 Zaburi 35:13Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia na nikajinyenyekesha kwa kufunga. Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa, 14 Zaburi 35:14niliendelea kuomboleza kama vile wao ni rafiki au ndugu. Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni kama ninayemwombolezea mama yangu. 15 Zaburi 35:15Lakini nilipojikwaa, walikusanyika kwa shangwe; washambuliaji walijikusanya dhidi yangu bila mimi kujua. Walinisingizia pasipo kukoma. 16 Zaburi 35:16Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki, wamenisagia meno. 17 Zaburi 35:17Ee Bwana, utatazama mpaka lini? Niokoe maisha yangu na maangamizi yao, uhai wangu wa thamani kutokana na simba hawa. 18 Zaburi 35:18Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa, nitakusifu katikati ya watu wengi. 19 Zaburi 35:19Usiwaache wale wanaonisimanga, wale ambao ni adui zangu bila sababu; usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu wakonyeze jicho kwa hila. 20 Zaburi 35:20Hawazungumzi kwa amani, bali wanatunga mashtaka ya uongo dhidi ya wale wanaoishi kwa utulivu katika nchi. 21 Zaburi 35:21Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha! Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.” 22 Zaburi 35:22Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya. Usiwe mbali nami, Ee Bwana. 23 Zaburi 35:23Amka, inuka unitetee! Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu. 24 Zaburi 35:24Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu, sawasawa na haki yako; usiwaache wakusimange. 25 Zaburi 35:25Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!” Au waseme, “Tumemmeza.” 26 Zaburi 35:26Wote wanaofurahia dhiki yangu waaibishwe na wachanganyikiwe; hao wanaojiinua dhidi yangu wavikwe aibu na dharau. 27 Zaburi 35:27Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “Bwana atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.” 28 Zaburi 35:28Ulimi wangu utanena haki yako na sifa zako mchana kutwa. Zaburi 36Uovu Wa Mwanadamu Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Bwana. 1 Zaburi 36:1Kuna neno moyoni mwangu kuhusu hali ya dhambi ya mwovu. Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake. 2 Zaburi 36:2Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. 3 Zaburi 36:3Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema. 4 Zaburi 36:4Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya. 5 Zaburi 36:5Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga. 6 Zaburi 36:6Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. 7 Zaburi 36:7Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako. 8 Zaburi 36:8Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. 9 Zaburi 36:9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru. 10 Zaburi 36:10Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo. 11 Zaburi 36:11Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu, wala mkono wa mwovu usinifukuze. 12 Zaburi 36:12Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka: wametupwa chini, hawawezi kuinuka! 37 Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 37Mwisho Wa Mwovu Na Urithi Wa Mwenye Haki Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 37:1Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, wala usiwaonee wivu watendao mabaya, 2 Zaburi 37:2kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara. 3 Zaburi 37:3Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. 4 Zaburi 37:4Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako. 5 Zaburi 37:5Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili: 6 Zaburi 37:6Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri. 7 Zaburi 37:7Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu. 8 Zaburi 37:8Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu. 9 Zaburi 37:9Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi. 10 Zaburi 37:10Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana, ingawa utawatafuta, hawataonekana. 11 Zaburi 37:11Bali wanyenyekevu watairithi nchi na wafurahie amani tele. 12 Zaburi 37:12Waovu hula njama dhidi ya wenye haki na kuwasagia meno, 13 Zaburi 37:13bali Bwana huwacheka waovu, kwa sababu anajua siku yao inakuja. 14 Zaburi 37:14Waovu huchomoa upanga na kupinda upinde, ili wawaangushe maskini na wahitaji, kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu. 15 Zaburi 37:15Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe, na pinde zao zitavunjwa. 16 Zaburi 37:16Bora kidogo walicho nacho wenye haki kuliko wingi wa mali wa waovu wengi; 17 Zaburi 37:17kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini Bwana humtegemeza mwenye haki. 18 Zaburi 37:18 Bwana anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele. 19 Zaburi 37:19Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. 20 Zaburi 37:20Lakini waovu wataangamia: Adui za Bwana watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi. 21 Zaburi 37:21Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu. 22 Zaburi 37:22Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali. 23 Zaburi 37:23Kama Bwana akipendezwa na njia ya mtu, yeye huimarisha hatua zake, 24 Zaburi 37:24ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana Bwana humtegemeza kwa mkono wake. 25 Zaburi 37:25Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula. 26 Zaburi 37:26Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. Watoto wao watabarikiwa. 27 Zaburi 37:27Acha ubaya na utende wema, nawe utaishi katika nchi milele. 28 Zaburi 37:28Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki naye hatawaacha waaminifu wake. Watalindwa milele, lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali. 29 Zaburi 37:29Wenye haki watairithi nchi, na kuishi humo milele. 30 Zaburi 37:30Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima, nao ulimi wake huzungumza lililo haki. 31 Zaburi 37:31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; nyayo zake hazitelezi. 32 Zaburi 37:32Watu waovu huvizia wenye haki, wakitafuta kuwaua; 33 Zaburi 37:33lakini Bwana hatawaacha mikononi mwao wala hatawaacha wahukumiwe kuwa wakosa wanaposhtakiwa. 34 Zaburi 37:34Mngojee Bwana, na uishike njia yake. Naye atakutukuza uirithi nchi, waovu watakapokatiliwa mbali, utaliona hilo. 35 Zaburi 37:35Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi kama mwerezi wa Lebanoni, 36 Zaburi 37:36lakini alitoweka mara na hakuonekana, ingawa nilimtafuta, hakupatikana. 37 Zaburi 37:37Watafakari watu wasio na hatia, wachunguze watu wakamilifu, kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani. 38 Zaburi 37:38Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa, mafanikio yao yatakatiliwa mbali. 39 Zaburi 37:39Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana, yeye ni ngome yao wakati wa shida. 40 Zaburi 37:40 Bwana huwasaidia na kuwaokoa, huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, kwa maana wanamkimbilia. Zaburi 38Maombi Ya Mtu Anayeteseka Zaburi ya Daudi. Maombi. 1 Zaburi 38:1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. 2 Zaburi 38:2Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia. 3 Zaburi 38:3Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu. 4 Zaburi 38:4Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika. 5 Zaburi 38:5Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. 6 Zaburi 38:6Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. 7 Zaburi 38:7Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu. 8 Zaburi 38:8Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. 9 Zaburi 38:9Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako. 10 Zaburi 38:10Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza. 11 Zaburi 38:11Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani zangu wanakaa mbali nami. 12 Zaburi 38:12Wale wanaotafuta uhai wangu wanatega mitego yao, wale ambao wangetaka kunidhuru huongea juu ya maangamizi yangu; hufanya shauri la hila mchana kutwa. 13 Zaburi 38:13Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia, ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake, 14 Zaburi 38:14nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu. 15 Zaburi 38:15Ee Bwana, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu. 16 Zaburi 38:16Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.” 17 Zaburi 38:17Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote. 18 Zaburi 38:18Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu. 19 Zaburi 38:19Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari, wale wanaonichukia bila sababu ni wengi. 20 Zaburi 38:20Wanaolipa maovu kwa wema wangu hunisingizia ninapofuata lililo jema. 21 Zaburi 38:21Ee Bwana, usiniache, usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu. 22 Zaburi 38:22Ee Bwana Mwokozi wangu, uje upesi kunisaidia. Zaburi 39Maombi Ya Mtu Anayeteseka Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 39:1Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” 2 Zaburi 39:2Lakini niliponyamaza kimya na kutulia, hata pasipo kusema lolote jema, uchungu wangu uliongezeka. 3 Zaburi 39:3Moyo wangu ulipata moto ndani yangu, nilipotafakari, moto uliwaka, ndipo nikasema kwa ulimi wangu: 4 Zaburi 39:4“Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu na hesabu ya siku zangu; nijalie kujua jinsi maisha yangu yanavyopita upesi. 5 Zaburi 39:5Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi. 6 Zaburi 39:6Hakika kila binadamu ni kama njozi aendapo huku na huko: hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili; anakusanya mali nyingi, wala hajui ni nani atakayeifaidi. 7 Zaburi 39:7“Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako. 8 Zaburi 39:8Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote, usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu. 9 Zaburi 39:9Nilinyamaza kimya, sikufumbua kinywa changu, kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili. 10 Zaburi 39:10Niondolee mjeledi wako, nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako. 11 Zaburi 39:11Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu. 12 Zaburi 39:12“Ee Bwana, usikie maombi yangu, usikie kilio changu unisaidie, usiwe kiziwi kwa kulia kwangu. Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni, kama walivyokuwa baba zangu wote, 13 Zaburi 39:13Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena kabla sijaondoka na nisiwepo tena.” Zaburi 40Wimbo Wa Sifa Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 40:1Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu. 2 Zaburi 40:2Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama. 3 Zaburi 40:3Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa na kuweka tumaini lao kwa Bwana. 4 Zaburi 40:4Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo. 5 Zaburi 40:5Ee Bwana Mungu wangu, umefanya mambo mengi ya ajabu. Mambo uliyopanga kwa ajili yetu hakuna awezaye kukuhesabia; kama ningesema na kuyaelezea, yangekuwa mengi mno kuyaelezea. 6 Zaburi 40:6Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu; 40:6 Au: bali mwili uliniandalia. sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji. 7 Zaburi 40:7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu. 8 Zaburi 40:8Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.” 9 Zaburi 40:9Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee Bwana, kama ujuavyo. 10 Zaburi 40:10Sikuficha haki yako moyoni mwangu; ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako. Sikuficha upendo wako na kweli yako mbele ya kusanyiko kubwa. 11 Zaburi 40:11Ee Bwana, usizuilie huruma zako, upendo wako na kweli yako daima vinilinde. 12 Zaburi 40:12Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka, dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, nao moyo unazimia ndani yangu. 13 Zaburi 40:13Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie. 14 Zaburi 40:14Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu. 15 Zaburi 40:15Wale waniambiao, “Aha! Aha!” wafadhaishwe na iwe aibu yao. 16 Zaburi 40:16Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, Bwana atukuzwe!” 17 Zaburi 40:17Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Bwana na anifikirie. Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu; Ee Mungu wangu, usikawie. Zaburi 41Maombi Ya Mtu Mgonjwa Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 41:1Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida. 2 Zaburi 41:2 Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, atambariki katika nchi na hatamwacha katika tamaa ya adui zake. 3 Zaburi 41:3 Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake. 4 Zaburi 41:4Nilisema, “Ee Bwana nihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.” 5 Zaburi 41:5Adui zangu wanasema kwa hila, “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.” 6 Zaburi 41:6Kila anapokuja mtu kunitazama, huzungumza uongo, huku moyo wake hukusanya masingizio; kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko. 7 Zaburi 41:7Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu, hao huniwazia mabaya sana, wakisema, 8 Zaburi 41:8“Ugonjwa mbaya sana umempata, kamwe hatainuka tena kitandani mwake.” 9 Zaburi 41:9Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, yule aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake. 10 Zaburi 41:10Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie, ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi. 11 Zaburi 41:11Najua kwamba wapendezwa nami, kwa kuwa adui yangu hanishindi. 12 Zaburi 41:12Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele. 13 Zaburi 41:13Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Amen na Amen. KITABU CHA PILI (Zaburi 42–72) Zaburi 42Maombi Ya Mtu Aliye Uhamishoni Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. 1 Zaburi 42:1Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. 2 Zaburi 42:2Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? 3 Zaburi 42:3Machozi yangu yamekuwa chakula changu usiku na mchana, huku watu wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” 4 Zaburi 42:4Mambo haya nayakumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati uliosherehekea. 5 Zaburi 42:5Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na 6 Zaburi 42:6Mungu wangu. Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; kwa hiyo nitakukumbuka kutoka nchi ya Yordani, katika vilele vya Hermoni, kutoka Mlima Mizari. 7 Zaburi 42:7Kilindi huita kilindi, katika ngurumo za maporomoko ya maji yako; mawimbi yako yote pamoja na viwimbi vimepita juu yangu. 8 Zaburi 42:8Mchana Bwana huelekeza upendo wake, usiku wimbo wake uko nami: maombi kwa Mungu wa uzima wangu. 9 Zaburi 42:9Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, “Kwa nini umenisahau? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiwa nimeonewa na adui?” 10 Zaburi 42:10Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali adui zangu wanaponidhihaki, wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” 11 Zaburi 42:11Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na Mungu wangu. Zaburi 43Maombi Ya Mtu Aliyeko Uhamishoni Yanaendelea 1 Zaburi 43:1Ee Mungu unihukumu, nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu, niokoe na watu wadanganyifu na waovu. 2 Zaburi 43:2Wewe ni Mungu ngome yangu. Kwa nini umenikataa? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiwa nimeonewa na adui? 3 Zaburi 43:3Tuma hima nuru yako na kweli yako na viniongoze; vinilete mpaka mlima wako mtakatifu, mpaka mahali unapoishi. 4 Zaburi 43:4Ndipo nitakwenda madhabahuni pa Mungu, kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu. Nitakusifu kwa kinubi, Ee Mungu, Mungu wangu. 5 Zaburi 43:5Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu Mwokozi wangu na Mungu wangu. Zaburi 44Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. 1 Zaburi 44:1Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametueleza yale uliyotenda katika siku zao, siku za kale. 2 Zaburi 44:2Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu. 3 Zaburi 44:3Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda. 4 Zaburi 44:4Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo. 5 Zaburi 44:5Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu. 6 Zaburi 44:6Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi; 7 Zaburi 44:7bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, unawaaibisha watesi wetu. 8 Zaburi 44:8Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, nasi tutalisifu jina lako milele. 9 Zaburi 44:9Lakini sasa umetukataa na kutudhili, wala huendi tena na jeshi letu. 10 Zaburi 44:10Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui, nao watesi wetu wametuteka nyara. 11 Zaburi 44:11Umetuacha tutafunwe kama kondoo na umetutawanya katika mataifa. 12 Zaburi 44:12Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao. 13 Zaburi 44:13Umetufanya lawama kwa jirani zetu, dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka. 14 Zaburi 44:14Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa, mataifa hutikisa vichwa vyao. 15 Zaburi 44:15Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, na uso wangu umejaa aibu tele, 16 Zaburi 44:16kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi. 17 Zaburi 44:17Hayo yote yametutokea, ingawa tulikuwa hatujakusahau wala hatujaenda kinyume na agano lako. 18 Zaburi 44:18Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako. 19 Zaburi 44:19Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, na ukatufunika kwa giza nene. 20 Zaburi 44:20Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni, 21 Zaburi 44:21je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo? 22 Zaburi 44:22Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. 23 Zaburi 44:23Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? Zinduka! Usitukatae milele. 24 Zaburi 44:24Kwa nini unauficha uso wako na kusahau taabu na mateso yetu? 25 Zaburi 44:25Tumeshushwa hadi mavumbini, miili yetu imegandamana na ardhi. 26 Zaburi 44:26Inuka na utusaidie, utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho. Zaburi 45Wimbo Wa Arusi Ya Kifalme Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi.” Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi. 1 Zaburi 45:1Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi. 2 Zaburi 45:2Wewe ni bora kuliko watu wengine wote na midomo yako imepakwa neema, kwa kuwa Mungu amekubariki milele. 3 Zaburi 45:3Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, jivike fahari na utukufu. 4 Zaburi 45:4Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi, kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki, mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha. 5 Zaburi 45:5Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme, mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako. 6 Zaburi 45:6Ee Mungu, kiti chako cha enzi kitadumu milele na milele, fimbo ya utawala wa haki itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako. 7 Zaburi 45:7Unaipenda haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako, kwa kukupaka mafuta ya furaha. 8 Zaburi 45:8Mavazi yako yote yana harufu nzuri ya manemane, udi na mdalasini; kutoka kwenye majumba ya kifalme yaliyopambwa kwa pembe za ndovu, sauti za vinanda vya nyuzi zinakufanya ufurahi. 9 Zaburi 45:9Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa; kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri. 10 Zaburi 45:10Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio: Sahau watu wako na nyumba ya baba yako. 11 Zaburi 45:11Mfalme ameshangazwa na uzuri wako; mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako. 12 Zaburi 45:12Binti wa Tiro atakuletea zawadi, watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako. 13 Zaburi 45:13Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake; vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. 14 Zaburi 45:14Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, mabikira wenzake wanamfuata na wanaletwa kwako. 15 Zaburi 45:15Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, na kuingia katika jumba la mfalme. 16 Zaburi 45:16Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, mtawafanya wakuu katika nchi yote. 17 Zaburi 45:17Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote, kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele. Zaburi 46Mungu Yuko Pamoja Nasi Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi. 1 Zaburi 46:1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. 2 Zaburi 46:2Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari. 3 Zaburi 46:3Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake. 4 Zaburi 46:4Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. 5 Zaburi 46:5Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema. 6 Zaburi 46:6Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka. 7 Zaburi 46:7 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. 8 Zaburi 46:8Njooni mkaone kazi za Bwana jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. 9 Zaburi 46:9Anakomesha vita hata miisho ya dunia, anakata upinde na kuvunjavunja mkuki, anateketeza ngao kwa moto. 10 Zaburi 46:10“Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu; nitatukuzwa katikati ya mataifa, nitatukuzwa katika dunia.” 11 Zaburi 46:11 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. Zaburi 47Mtawala Mwenye Enzi Yote Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. 1 Zaburi 47:1Pigeni makofi, enyi mataifa yote, mpigieni Mungu kelele za shangwe! 2 Zaburi 47:2Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote! 3 Zaburi 47:3Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu. 4 Zaburi 47:4Alituchagulia urithi wetu, fahari ya Yakobo, aliyempenda. 5 Zaburi 47:5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, Bwana kwa sauti za tarumbeta. 6 Zaburi 47:6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa, mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. 7 Zaburi 47:7Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. 8 Zaburi 47:8Mungu anatawala juu ya mataifa, Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu. 9 Zaburi 47:9Wakuu wa mataifa wanakusanyika kama watu wa Mungu wa Abrahamu, kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu; yeye ametukuka sana. Zaburi 48Sayuni, Mji Wa Mungu Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. 1 Zaburi 48:1 Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu. 2 Zaburi 48:2Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, furaha ya dunia yote. Kama vilele vya juu sana vya Safoni 48:2 Safoni inaweza ikawa na maana ya mlima mtakatifu au upande wa kaskazini. ni Mlima Sayuni, mji wa Mfalme Mkuu. 3 Zaburi 48:3Mungu yuko katika ngome zake; amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake. 4 Zaburi 48:4Wakati wafalme walipounganisha nguvu, waliposonga mbele pamoja, 5 Zaburi 48:5walimwona nao wakashangaa, wakakimbia kwa hofu. 6 Zaburi 48:6Kutetemeka kuliwashika huko, maumivu kama ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa. 7 Zaburi 48:7Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi zilizovunjwa na upepo wa mashariki. 8 Zaburi 48:8Kama tulivyokuwa tumesikia, ndivyo tulivyoona katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote, katika mji wa Mungu wetu: Mungu ataufanya uwe salama milele. 9 Zaburi 48:9Ee Mungu, hekaluni mwako tunatafakari upendo wako usiokoma. 10 Zaburi 48:10Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, mkono wako wa kuume umejazwa na haki. 11 Zaburi 48:11Mlima Sayuni unashangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako. 12 Zaburi 48:12Tembeeni katika Sayuni, uzungukeni mji, hesabuni minara yake; 13 Zaburi 48:13yatafakarini vyema maboma yake, angalieni ngome zake, ili mpate kusimulia habari zake kwa kizazi kijacho. 14 Zaburi 48:14Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; atakuwa kiongozi wetu hata mwisho. Zaburi 49Upumbavu Wa Kutegemea Mali Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. 1 Zaburi 49:1Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii. 2 Zaburi 49:2Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja: 3 Zaburi 49:3Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu. 4 Zaburi 49:4Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze: 5 Zaburi 49:5Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka, 6 Zaburi 49:6wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi? 7 Zaburi 49:7Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake. 8 Zaburi 49:8Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha, 9 Zaburi 49:9ili kwamba aishi milele na asione uharibifu. 10 Zaburi 49:10Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao. 11 Zaburi 49:11Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao. 12 Zaburi 49:12Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye. 13 Zaburi 49:13Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao. 14 Zaburi 49:14Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, 49:14 Kaburini hapa ina maana ya Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu. nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. 15 Zaburi 49:15Lakini Mungu atakomboa uhai 49:15 Au: nafsi. wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake. 16 Zaburi 49:16Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka, 17 Zaburi 49:17kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye. 18 Zaburi 49:18Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa, 19 Zaburi 49:19atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima. 20 Zaburi 49:20Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao. Zaburi 50Ibada Ya Kweli Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 50:1Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana, asema na kuiita dunia, tangu mawio ya jua hadi mahali pake liendapo kutua. 2 Zaburi 50:2Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, Mungu anaangaza. 3 Zaburi 50:3Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali. 4 Zaburi 50:4Anaziita mbingu zilizo juu, na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake: 5 Zaburi 50:5“Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu, waliofanya agano nami kwa dhabihu.” 6 Zaburi 50:6Nazo mbingu zinatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu. 7 Zaburi 50:7“Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema, ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu: Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu. 8 Zaburi 50:8Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, au sadaka zako za kuteketezwa, ambazo daima ziko mbele zangu. 9 Zaburi 50:9Sina haja ya fahali wa banda lako, au mbuzi wa zizi lako. 10 Zaburi 50:10Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. 11 Zaburi 50:11Ninamjua kila ndege mlimani, nao viumbe wa kondeni ni wangu. 12 Zaburi 50:12Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi, kwa maana ulimwengu ni wangu, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. 13 Zaburi 50:13Je, mimi hula nyama ya mafahali au kunywa damu ya mbuzi? 14 Zaburi 50:14Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana, 15 Zaburi 50:15na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”

16 Zaburi 50:16Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema:

“Una haki gani kunena sheria zangu au kuchukua agano langu midomoni mwako? 17 Zaburi 50:17Unachukia mafundisho yangu na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. 18 Zaburi 50:18Unapomwona mwizi, unaungana naye, unapiga kura yako pamoja na wazinzi. 19 Zaburi 50:19Unakitumia kinywa chako kwa mabaya na kuuongoza ulimi wako kwa hila. 20 Zaburi 50:20Wanena daima dhidi ya ndugu yako na kumsingizia mwana wa mama yako. 21 Zaburi 50:21Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya, ukafikiri Mimi nami ni kama wewe. Lakini nitakukemea na kuweka mashtaka mbele yako. 22 Zaburi 50:22“Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu, ama sivyo nitawararua vipande vipande, wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwaokoa: 23 Zaburi 50:23Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, naye aiandaa njia yake ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu.” Zaburi 51Kuomba Msamaha Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba. 1 Zaburi 51:1Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu. 2 Zaburi 51:2Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu. 3 Zaburi 51:3Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima. 4 Zaburi 51:4Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, na kuwa na haki utoapo hukumu. 5 Zaburi 51:5Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu. 6 Zaburi 51:6Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni, ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima. 7 Zaburi 51:7Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. 8 Zaburi 51:8Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi. 9 Zaburi 51:9Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote. 10 Zaburi 51:10Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. 11 Zaburi 51:11Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu. 12 Zaburi 51:12Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze. 13 Zaburi 51:13Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe. 14 Zaburi 51:14Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako. 15 Zaburi 51:15Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako. 16 Zaburi 51:16Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa. 17 Zaburi 51:17Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau. 18 Zaburi 51:18Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, ukazijenge upya kuta za Yerusalemu. 19 Zaburi 51:19Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, pia mafahali watatolewa madhabahuni mwako. Zaburi 52Hukumu Ya Mungu Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi amekwenda nyumbani kwa Ahimeleki.” 1 Zaburi 52:1Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? Kwa nini unajivuna mchana kutwa, wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu? 2 Zaburi 52:2Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila. 3 Zaburi 52:3Unapenda mabaya kuliko mema, uongo kuliko kusema kweli. 4 Zaburi 52:4Unapenda kila neno lenye kudhuru, ewe ulimi wenye hila! 5 Zaburi 52:5Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema yako, atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai. 6 Zaburi 52:6Wenye haki wataona na kuogopa, watamcheka, wakisema, 7 Zaburi 52:7“Huyu ni yule mtu ambaye hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, bali alitumainia wingi wa utajiri wake, na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!” Neema Ya Mungu 8 Zaburi 52:8Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni unaostawi katika nyumba ya Mungu, nautegemea upendo wa Mungu usiokoma milele na milele. 9 Zaburi 52:9Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. Nitakusifu mbele ya watakatifu wako. Zaburi 53Uovu Wa Wanadamu (Zaburi 14) Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi. 1 Zaburi 53:1Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema. 2 Zaburi 53:2Mungu anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. 3 Zaburi 53:3Kila mmoja amegeukia mbali, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja! 4 Zaburi 53:4Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza: wale ambao huwala watu wangu kama watu walavyo mkate, hao ambao hawamwiti Mungu? 5 Zaburi 53:5Hapo waliingiwa na hofu kuu, ambapo hapakuwa cha kutetemesha. Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia; uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau. 6 Zaburi 53:6Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni! Wakati Mungu arejeshapo wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi! Zaburi 54Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kutokana Na Adui Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” 1 Zaburi 54:1Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako. 2 Zaburi 54:2Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu. 3 Zaburi 54:3Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu. 4 Zaburi 54:4Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza. 5 Zaburi 54:5Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize. 6 Zaburi 54:6Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema. 7 Zaburi 54:7Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi. Zaburi 55Maombi Ya Mtu Aliyesalitiwa Na Rafiki Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi. 1 Zaburi 55:1Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, wala usidharau hoja yangu. 2 Zaburi 55:2Nisikie na unijibu. Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa 3 Zaburi 55:3kwa sauti ya adui, kwa kukaziwa macho na waovu, kwa sababu wananiletea mateso juu yangu na kunitukana kwa hasira zao. 4 Zaburi 55:4Moyo wangu umejaa uchungu, hofu ya kifo imenishambulia. 5 Zaburi 55:5Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha. 6 Zaburi 55:6Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika. 7 Zaburi 55:7Ningalitorokea mbali sana na kukaa jangwani, 8 Zaburi 55:8ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, mbali na tufani kali na dhoruba.” 9 Zaburi 55:9Ee Bwana, uwatahayarishe waovu na uwachanganyishie semi zao, maana nimeona jeuri na ugomvi mjini. 10 Zaburi 55:10Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake, uovu na dhuluma vimo ndani yake. 11 Zaburi 55:11Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini, vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake. 12 Zaburi 55:12Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia, kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, ningejificha asinione. 13 Zaburi 55:13Kumbe ni wewe, mwenzangu, mshiriki na rafiki yangu wa karibu, 14 Zaburi 55:14ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri, tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu. 15 Zaburi 55:15Kifo na kiwajie adui zangu ghafula, na washuke kuzimu wangali hai, kwa maana uovu upo ndani yao. 16 Zaburi 55:16Lakini ninamwita Mungu, naye Bwana huniokoa. 17 Zaburi 55:17Jioni, asubuhi na adhuhuri ninalia kwa huzuni, naye husikia sauti yangu. 18 Zaburi 55:18Huniokoa nikawa salama katika vita vilivyopangwa dhidi yangu, ingawa watu wengi hunipinga. 19 Zaburi 55:19Mungu anayemiliki milele, atawasikia na kuwaadhibu, watu ambao hawabadilishi njia zao, wala hawana hofu ya Mungu. 20 Zaburi 55:20Mwenzangu hushambulia rafiki zake, naye huvunja agano lake. 21 Zaburi 55:21Mazungumzo yake ni laini kama siagi, hata hivyo vita vimo moyoni mwake. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa. 22 Zaburi 55:22Mtwike Bwana fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke. 23 Zaburi 55:23Lakini wewe, Ee Mungu, utawashusha waovu katika shimo la uharibifu. Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila, hawataishi nusu ya siku zao. Lakini mimi ninakutumaini wewe. Zaburi 56Kumtumaini Mungu Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Njiwa mkimya wa mbali.” Utenzi wa Daudi. Baada ya kukamatwa na Wafilisti huko Gathi. 1 Zaburi 56:1Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao. 2 Zaburi 56:2Wasingiziaji wangu wananifuatia mchana kutwa, wengi wananishambulia kwa kiburi chao. 3 Zaburi 56:3Wakati ninapoogopa, nitakutumaini wewe. 4 Zaburi 56:4Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Mungu ninatumaini; sitaogopa. Mwanadamu apatikanaye na kufa, atanitenda nini? 5 Zaburi 56:5Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, siku zote wanapanga shauri la kunidhuru. 6 Zaburi 56:6Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu. 7 Zaburi 56:7Wasiepuke kwa vyovyote, Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa. 8 Zaburi 56:8Andika maombolezo yangu, orodhesha machozi yangu katika gombo lako: je, haya hayapo katika kumbukumbu zako? 9 Zaburi 56:9Ndipo adui zangu watarudi nyuma ninapoita msaada. Kwa hili nitajua kwamba Mungu yuko upande wangu. 10 Zaburi 56:10Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu, katika Bwana, ambaye neno lake ninalisifu, 11 Zaburi 56:11katika Mungu ninatumaini, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? 12 Zaburi 56:12Ee Mungu, nina nadhiri kwako, nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani. 13 Zaburi 56:13Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili niweze kuenenda mbele za Mungu katika nuru ya uzima. Zaburi 57Kuomba Msaada Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni. 1 Zaburi 57:1Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite. 2 Zaburi 57:2Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. 3 Zaburi 57:3Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. 4 Zaburi 57:4Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali. 5 Zaburi 57:5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. 6 Zaburi 57:6Waliitegea miguu yangu nyavu, nikainamishwa chini na dhiki. Wamechimba shimo katika njia yangu, lakini wametumbukia humo wao wenyewe. 7 Zaburi 57:7Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 8 Zaburi 57:8Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. 9 Zaburi 57:9Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. 10 Zaburi 57:10Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, uaminifu wako unazifikia anga. 11 Zaburi 57:11Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni, utukufu wako na uwe duniani pote. Zaburi 58Mungu Kuwaadhibu Waovu Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. 1 Zaburi 58:1Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki? Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu? 2 Zaburi 58:2La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu, na mikono yenu hupima jeuri duniani. 3 Zaburi 58:3Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao, toka tumboni mwa mama zao ni wakaidi na husema uongo. 4 Zaburi 58:4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake, 5 Zaburi 58:5ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi, hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani. 6 Zaburi 58:6Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao; Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba! 7 Zaburi 58:7Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi, wavutapo pinde zao, mishale yao na iwe butu. 8 Zaburi 58:8Kama konokono ayeyukavyo akitembea, kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu, wasilione jua. 9 Zaburi 58:9Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba, zikiwa mbichi au kavu, waovu watakuwa wamefagiliwa mbali. 10 Zaburi 58:10Wenye haki watafurahi waonapo wakilipizwa kisasi, watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu. 11 Zaburi 58:11Ndipo wanadamu watasema, “Hakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu, hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.” Zaburi 59Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Wakati Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue. 1 Zaburi 59:1Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. 2 Zaburi 59:2Uniponye na watu watendao mabaya, uniokoe kutokana na wamwagao damu. 3 Zaburi 59:3Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea wala kutenda dhambi. 4 Zaburi 59:4Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia. Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya! 5 Zaburi 59:5Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli! Zinduka uyaadhibu mataifa yote, usionyeshe huruma kwa wasaliti. 6 Zaburi 59:6Hurudi wakati wa jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. 7 Zaburi 59:7Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao, hutema upanga kutoka midomo yao, nao husema, “Ni nani atakayetusikia?” 8 Zaburi 59:8Lakini wewe, Bwana, uwacheke; unayadharau mataifa hayo yote. 9 Zaburi 59:9Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, 10 Zaburi 59:10Mungu wangu unipendaye. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwachekelee wale wanaonisingizia. 11 Zaburi 59:11Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, au sivyo watu wangu watasahau. Katika uwezo wako wafanye watangetange na uwashushe chini. 12 Zaburi 59:12Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, kwa ajili ya maneno ya midomo yao, waache wanaswe katika kiburi chao. Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka, 13 Zaburi 59:13wateketeze katika ghadhabu, wateketeze hadi wasiwepo tena. Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo. 14 Zaburi 59:14Hurudi jioni, wakibweka kama mbwa, wakiuzurura mji. 15 Zaburi 59:15Wanatangatanga wakitafuta chakula, wasipotosheka hubweka kama mbwa. 16 Zaburi 59:16Lakini mimi nitaziimba nguvu zako, asubuhi nitaimba juu ya upendo wako; kwa maana wewe ndiwe ngome yangu na kimbilio langu wakati wa shida. 17 Zaburi 59:17Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa. Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, Mungu unipendaye. Zaburi 60Kuomba Kuokolewa Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi.” Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Wakati alipopigana na Waaramu kutoka Aramu-Naharaimu na Aramu-Soba, naye Yoabu akarudi nyuma na kuwaua Waedomu 12,000 katika Bonde la Chumvi. 1 Zaburi 60:1Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu, umekasirika: sasa turejeshe upya! 2 Zaburi 60:2Umetetemesha nchi na kuipasua; uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka. 3 Zaburi 60:3Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa; umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha. 4 Zaburi 60:4Kwa wale wanaokucha wewe, umewainulia bendera, ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde. 5 Zaburi 60:5Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa. 6 Zaburi 60:6Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi. 7 Zaburi 60:7Gileadi ni yangu na Manase ni yangu; Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. 8 Zaburi 60:8Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” 9 Zaburi 60:9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? 10 Zaburi 60:10Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? 11 Zaburi 60:11Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. 12 Zaburi 60:12Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu. Zaburi 61Kuomba Ulinzi Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 61:1Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu. 2 Zaburi 61:2Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi. 3 Zaburi 61:3Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. 4 Zaburi 61:4Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako. 5 Zaburi 61:5Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako. 6 Zaburi 61:6Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi. 7 Zaburi 61:7Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde. 8 Zaburi 61:8Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku. Zaburi 62Mungu Kimbilio La Pekee Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 62:1Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake. 2 Zaburi 62:2Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe. 3 Zaburi 62:3Mtamshambulia mtu hata lini? Je, ninyi nyote mtamtupa chini, ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika? 4 Zaburi 62:4Walikusudia kikamilifu kumwangusha toka mahali pake pa fahari; wanafurahia uongo. Kwa vinywa vyao hubariki, lakini ndani ya mioyo yao hulaani. 5 Zaburi 62:5Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake. 6 Zaburi 62:6Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; ndiye ngome yangu, sitatikisika. 7 Zaburi 62:7Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu, ndiye mwamba wangu wenye nguvu na kimbilio langu. 8 Zaburi 62:8Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, miminieni mioyo yenu kwake, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu. 9 Zaburi 62:9Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu, nao wa ngazi ya juu ni uongo tu; wakipimwa kwenye mizani, si chochote; wote kwa pamoja ni pumzi tu. 10 Zaburi 62:10Usitumainie vya udhalimu wala usijivune kwa vitu vya wizi; ingawa utajiri wako utaongezeka, usiviwekee moyo wako. 11 Zaburi 62:11Jambo moja Mungu amelisema, mambo mawili nimeyasikia: kwamba, Ee Mungu, wewe una nguvu, 12 Zaburi 62:12na kwamba, Ee Bwana, wewe ni mwenye upendo. Hakika utampa kila mtu thawabu kwa kadiri ya alivyotenda. Zaburi 63Shauku Kwa Ajili Ya Uwepo Wa Mungu Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda. 1 Zaburi 63:1Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji. 2 Zaburi 63:2Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako. 3 Zaburi 63:3Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha. 4 Zaburi 63:4Nitakusifu siku zote za maisha yangu, na kwa jina lako nitainua mikono yangu. 5 Zaburi 63:5Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe. 6 Zaburi 63:6Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku. 7 Zaburi 63:7Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba. 8 Zaburi 63:8Nafsi yangu inaambatana nawe, mkono wako wa kuume hunishika. 9 Zaburi 63:9Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa, watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia. 10 Zaburi 63:10Watatolewa wafe kwa upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha. 11 Zaburi 63:11Bali mfalme atafurahi katika Mungu, wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu, bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa. Zaburi 64Kuomba Ulinzi Dhidi Ya Maadui Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 64:1Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu, uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui. 2 Zaburi 64:2Unifiche kutokana na shauri la siri la waovu, kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya. 3 Zaburi 64:3Wananoa ndimi zao kama panga na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha. 4 Zaburi 64:4Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga. 5 Zaburi 64:5Kila mmoja humtia moyo mwenzake katika mipango mibaya; huzungumza juu ya kuficha mitego yao, nao husema, “Ni nani ataiona?” 6 Zaburi 64:6Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema, “Tumebuni mpango mkamilifu!” Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila. 7 Zaburi 64:7Bali Mungu atawapiga kwa mishale, nao ghafula wataangushwa. 8 Zaburi 64:8Atageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao na kuwaleta kwenye maangamizi; wote wawaonao watatikisa vichwa vyao kwa dharau. 9 Zaburi 64:9Wanadamu wote wataogopa, watatangaza kazi za Mungu na kutafakari yale aliyoyatenda. 10 Zaburi 64:10Wenye haki na wafurahi katika Bwana, na wakimbilie kwake; wanyofu wote wa moyo na wamsifu yeye! Zaburi 65Kusifu Na Kushukuru Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo. 1 Zaburi 65:1Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa. 2 Zaburi 65:2Ewe usikiaye maombi, kwako wewe watu wote watakuja. 3 Zaburi 65:3Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi, wewe ulisamehe makosa yetu. 4 Zaburi 65:4Heri wale uliowachagua na kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako! Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako, mema ya Hekalu lako takatifu. 5 Zaburi 65:5Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki, Ee Mungu Mwokozi wetu, tumaini la miisho yote ya duniani na la bahari zilizo mbali sana, 6 Zaburi 65:6uliyeumba milima kwa uwezo wako, ukiwa umejivika nguvu, 7 Zaburi 65:7uliyenyamazisha dhoruba za bahari, ngurumo za mawimbi yake, na ghasia za mataifa. 8 Zaburi 65:8Wale wanaoishi mbali sana wanaogopa maajabu yako, kule asubuhi ipambazukiapo na kule jioni inakofifilia umeziita nyimbo za furaha. 9 Zaburi 65:9Waitunza nchi na kuinyeshea, waitajirisha kwa wingi. Vijito vya Mungu vimejaa maji ili kuwapa watu nafaka, kwa maana wewe umeviamuru. 10 Zaburi 65:10Umeilowesha mifereji yake na kusawazisha kingo zake; umeilainisha kwa manyunyu na kuibariki mimea yake. 11 Zaburi 65:11Umeuvika mwaka taji ya baraka, magari yako yanafurika kwa wingi. 12 Zaburi 65:12Mbuga za majani za jangwani umezineemesha; vilima vimevikwa furaha. 13 Zaburi 65:13Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama, na mabonde yamepambwa kwa mavuno; vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba. Zaburi 66Kusifu Mungu Kwa Ajili Ya Wema Wake Kwa mwimbishaji. Wimbo. Zaburi. 1 Zaburi 66:1Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote! 2 Zaburi 66:2Imbeni utukufu wa jina lake; mpeni sifa zake kwa utukufu! 3 Zaburi 66:3Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako! Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba adui wananyenyekea mbele zako. 4 Zaburi 66:4Dunia yote yakusujudia, wanakuimbia wewe sifa, wanaliimbia sifa jina lako.” 5 Zaburi 66:5Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda, mambo ya kutisha aliyoyatenda miongoni mwa wanadamu! 6 Zaburi 66:6Alifanya bahari kuwa nchi kavu, wakapita kati ya maji kwa miguu, njooni, tumshangilie. 7 Zaburi 66:7Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, macho yake huangalia mataifa yote: waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake. 8 Zaburi 66:8Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu, sauti ya sifa yake isikike, 9 Zaburi 66:9ameyahifadhi maisha yetu na kuizuia miguu yetu kuteleza. 10 Zaburi 66:10Ee Mungu, wewe ulitujaribu, ukatusafisha kama fedha. 11 Zaburi 66:11Umetuingiza kwenye nyavu na umetubebesha mizigo mizito migongoni mwetu. 12 Zaburi 66:12Uliwaruhusu watu watukalie vichwani, tulipita kwenye moto na kwenye maji, lakini ulituleta kwenye nchi iliyojaa utajiri tele. 13 Zaburi 66:13Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa na kukutimizia nadhiri zangu: 14 Zaburi 66:14nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi na nilizotamka kwa kinywa changu nilipokuwa katika shida. 15 Zaburi 66:15Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono na sadaka za kondoo dume, nitakutolea mafahali na mbuzi. 16 Zaburi 66:16Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu, nami niwaambie aliyonitendea. 17 Zaburi 66:17Nilimlilia kwa kinywa changu, sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu. 18 Zaburi 66:18Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, Bwana asingekuwa amenisikiliza; 19 Zaburi 66:19lakini hakika Mungu amenisikiliza na amesikia sauti yangu katika maombi. 20 Zaburi 66:20Sifa apewe Mungu, ambaye hakulikataa ombi langu wala kunizuilia upendo wake! Zaburi 67Mataifa Yahimizwa Kumsifu Mungu Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. 1 Zaburi 67:1Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake, 2 Zaburi 67:2ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. 3 Zaburi 67:3Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. 4 Zaburi 67:4Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. 5 Zaburi 67:5Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. 6 Zaburi 67:6Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. 7 Zaburi 67:7Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye. Zaburi 68Wimbo Wa Taifa Wa Shangwe Kwa Ushindi Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo. 1 Zaburi 68:1Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike, adui zake na wakimbie mbele zake. 2 Zaburi 68:2Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo, vivyo hivyo uwapeperushe mbali, kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto, vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu. 3 Zaburi 68:3Bali wenye haki na wafurahi, washangilie mbele za Mungu, wafurahi na kushangilia. 4 Zaburi 68:4Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake, mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu: jina lake ni Bwana, furahini mbele zake. 5 Zaburi 68:5Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu. 6 Zaburi 68:6Mungu huwaweka wapweke katika jamaa, huwaongoza wafungwa wakiimba, bali waasi huishi katika nchi kame. 7 Zaburi 68:7Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako, ulipopita nyikani, 8 Zaburi 68:8dunia ilitikisika, mbingu zikanyesha mvua, mbele za Mungu, Yule wa Sinai, mbele za Mungu, Mungu wa Israeli. 9 Zaburi 68:9Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka. 10 Zaburi 68:10Ee Mungu, watu wako waliishi huko, nawe kwa wingi wa utajiri wako uliwapa maskini mahitaji yao. 11 Zaburi 68:11Bwana alitangaza neno, waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa: 12 Zaburi 68:12“Wafalme na majeshi walikimbia upesi, watu waliobaki kambini waligawana nyara. 13 Zaburi 68:13Hata ulalapo katikati ya mioto ya kambini, mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha, manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.” 14 Zaburi 68:14Wakati Mwenyezi 68:14 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. alipowatawanya wafalme katika nchi, ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni. 15 Zaburi 68:15Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka, milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka. 16 Zaburi 68:16Enyi milima yenye vilele vilivyochongoka, kwa nini mnakazia macho kwa wivu, katika mlima Mungu anaochagua kutawala, ambako Bwana mwenyewe ataishi milele? 17 Zaburi 68:17Magari ya Mungu ni makumi ya maelfu, na maelfu ya maelfu; Bwana amekuja kutoka Sinai hadi katika patakatifu pake. 18 Zaburi 68:18Ulipopanda juu, uliteka mateka, ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu, hata kutoka kwa wale walioasi, ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko. 19 Zaburi 68:19Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. 20 Zaburi 68:20Mungu wetu ni Mungu aokoaye, Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo. 21 Zaburi 68:21Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi. 22 Zaburi 68:22Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, 23 Zaburi 68:23ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.” 24 Zaburi 68:24Ee Mungu, maandamano yako yameonekana, maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu, yakielekea patakatifu pake. 25 Zaburi 68:25Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda, pamoja nao wako wanawali wakipiga matari. 26 Zaburi 68:26Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli. 27 Zaburi 68:27Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza, wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda, hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali. 28 Zaburi 68:28Ee Mungu, amuru uwezo wako, Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako, kama ulivyofanya hapo awali. 29 Zaburi 68:29Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu wafalme watakuletea zawadi. 30 Zaburi 68:30Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi, kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa. Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea. Tawanya mataifa yapendayo vita. 31 Zaburi 68:31Wajumbe watakuja kutoka Misri, Kushi 68:31 Kushi hapa ina maana maeneo ya Naili ya juu, yaani Ethiopia. atajisalimisha kwa Mungu. 32 Zaburi 68:32Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia, mwimbieni Bwana sifa, 33 Zaburi 68:33mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu, yeye angurumaye kwa sauti kuu. 34 Zaburi 68:34Tangazeni uwezo wa Mungu, ambaye fahari yake iko juu ya Israeli, ambaye uwezo wake uko katika anga. 35 Zaburi 68:35Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako, Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu. Mungu Asifiwe! Zaburi 69Kilio Cha Kuomba Msaada Wakati Wa Dhiki Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 69:1Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni. 2 Zaburi 69:2Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga, Nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha. 3 Zaburi 69:3Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu. 4 Zaburi 69:4Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba. 5 Zaburi 69:5Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako. 6 Zaburi 69:6Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. 7 Zaburi 69:7Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu. 8 Zaburi 69:8Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. 9 Zaburi 69:9Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia. 10 Zaburi 69:10Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi. 11 Zaburi 69:11Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau. 12 Zaburi 69:12Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi. 13 Zaburi 69:13Lakini Ee Bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika. 14 Zaburi 69:14Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji. 15 Zaburi 69:15Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu. 16 Zaburi 69:16Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie. 17 Zaburi 69:17Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. 18 Zaburi 69:18Njoo karibu uniokoe, nikomboe kwa sababu ya adui zangu. 19 Zaburi 69:19Unajua jinsi ninavyodharauliwa, kufedheheshwa na kuaibishwa, adui zangu wote unawajua. 20 Zaburi 69:20Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata, wa kunituliza, lakini sikumpata. 21 Zaburi 69:21Waliweka nyongo katika chakula changu na walinipa siki nilipokuwa na kiu. 22 Zaburi 69:22Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego, nayo iwe upatilizo na tanzi. 23 Zaburi 69:23Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, nayo migongo yao iinamishwe daima. 24 Zaburi 69:24Uwamwagie ghadhabu yako, hasira yako kali na iwapate. 25 Zaburi 69:25Mahali pao na pawe ukiwa, wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao. 26 Zaburi 69:26Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi, na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza. 27 Zaburi 69:27Walipize uovu juu ya uovu, usiwaache washiriki katika wokovu wako. 28 Zaburi 69:28Wafutwe kutoka kitabu cha uzima na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki. 29 Zaburi 69:29Mimi niko katika maumivu na dhiki; Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi. 30 Zaburi 69:30Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani. 31 Zaburi 69:31Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume, zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake. 32 Zaburi 69:32Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi! 33 Zaburi 69:33 Bwana huwasikia wahitaji wala hadharau watu wake waliotekwa. 34 Zaburi 69:34Mbingu na dunia zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake, 35 Zaburi 69:35kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na kuijenga tena miji ya Yuda. Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki, 36 Zaburi 69:36watoto wa watumishi wake watairithi na wale wote walipendao jina lake wataishi humo. Zaburi 70Kuomba Msaada (Zaburi 40:13-17) Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi. 1 Zaburi 70:1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie. 2 Zaburi 70:2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu. 3 Zaburi 70:3Wale waniambiao, “Aha! Aha!” warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. 4 Zaburi 70:4Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!” 5 Zaburi 70:5Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Bwana, usikawie. Zaburi 71Kuomba Ulinzi Na Msaada Siku Zote Za Maisha 1 Zaburi 71:1Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe. 2 Zaburi 71:2Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe. 3 Zaburi 71:3Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu. 4 Zaburi 71:4Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili. 5 Zaburi 71:5Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, tegemeo langu tangu ujana wangu. 6 Zaburi 71:6Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, ulinitoa tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu wewe daima. 7 Zaburi 71:7Nimekuwa kama kioja kwa wengi, lakini wewe ni kimbilio langu imara. 8 Zaburi 71:8Kinywa changu kimejazwa sifa zako, nikitangaza utukufu wako mchana kutwa. 9 Zaburi 71:9Usinitupe wakati wa uzee, wala usiniache nguvu zangu zinapopungua. 10 Zaburi 71:10Kwa maana adui zangu wananisengenya, wale wanaonivizia kuniua wafanya hila. 11 Zaburi 71:11Wanasema, “Mungu amemwacha, mkimbilieni mkamkamate, kwani hakuna wa kumwokoa.” 12 Zaburi 71:12Ee Mungu, usiwe mbali nami, njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu. 13 Zaburi 71:13Washtaki wangu na waangamie kwa aibu, wale wanaotaka kunidhuru na wafunikwe kwa dharau na fedheha. 14 Zaburi 71:14Lakini mimi, nitatumaini siku zote, nitakusifu zaidi na zaidi. 15 Zaburi 71:15Kinywa changu kitasimulia haki yako, wokovu wako mchana kutwa, ingawa sifahamu kipimo chake. 16 Zaburi 71:16Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja na kutangaza matendo yako makuu, nitatangaza haki yako, yako peke yako. 17 Zaburi 71:17Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu, hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu. 18 Zaburi 71:18Ee Mungu, usiniache, hata niwapo mzee wa mvi, mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye. 19 Zaburi 71:19Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu, wewe ambaye umefanya mambo makuu. Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe? 20 Zaburi 71:20Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu, utanihuisha tena, kutoka vilindi vya dunia utaniinua tena. 21 Zaburi 71:21Utaongeza heshima yangu na kunifariji tena. 22 Zaburi 71:22Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako; Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, nitakuimbia sifa kwa zeze. 23 Zaburi 71:23Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha ninapokuimbia sifa, mimi, ambaye umenikomboa. 24 Zaburi 71:24Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki mchana kutwa, kwa maana wale waliotaka kunidhuru, wameaibishwa na kufadhaishwa. Zaburi 72Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme Zaburi ya Solomoni. 1 Zaburi 72:1Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako. 2 Zaburi 72:2Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki. 3 Zaburi 72:3Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki. 4 Zaburi 72:4Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu. 5 Zaburi 72:5Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote. 6 Zaburi 72:6Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi. 7 Zaburi 72:7Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma. 8 Zaburi 72:8Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto 72:8 Yaani Mto Frati. mpaka miisho ya dunia. 9 Zaburi 72:9Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi. 10 Zaburi 72:10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi. 11 Zaburi 72:11Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia. 12 Zaburi 72:12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia. 13 Zaburi 72:13Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti. 14 Zaburi 72:14Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake. 15 Zaburi 72:15Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa. 16 Zaburi 72:16Nafaka ijae tele katika nchi yote, juu ya vilele vya vilima na istawi. Tunda lake na listawi kama Lebanoni, listawi kama majani ya kondeni. 17 Zaburi 72:17Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa. 18 Zaburi 72:18 Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu. 19 Zaburi 72:19Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen. 20 Zaburi 72:20Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese. KITABU CHA TATU (Zaburi 73–89) Zaburi 73Haki Ya Mungu Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 73:1Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale ambao mioyo yao ni safi. 2 Zaburi 73:2Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama. 3 Zaburi 73:3Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna nilipoona kufanikiwa kwa waovu. 4 Zaburi 73:4Wao hawana taabu, 73:4 Tafsiri nyingine zinasema: hawana maumivu katika kufa kwao. miili yao ina afya na nguvu. 5 Zaburi 73:5Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine, wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine. 6 Zaburi 73:6Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao, wamejivika jeuri. 7 Zaburi 73:7Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi, majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo. 8 Zaburi 73:8Hudhihaki na kusema kwa ukorofi, katika majivuno yao wanatishia kutesa. 9 Zaburi 73:9Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu, nazo ndimi zao humiliki duniani. 10 Zaburi 73:10Kwa hiyo watu wao huwageukia na kunywa maji tele. 73:10 Au: na kupokea yote wasemayo. 11 Zaburi 73:11Wanasema, “Mungu awezaje kujua? Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?” 12 Zaburi 73:12Hivi ndivyo walivyo waovu: siku zote hawajali, wanaongezeka katika utajiri. 13 Zaburi 73:13Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure, ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia. 14 Zaburi 73:14Mchana kutwa nimetaabika, nimeadhibiwa kila asubuhi. 15 Zaburi 73:15Kama ningesema, “Nitasema hivi,” ningelikuwa nimewasaliti watoto wako. 16 Zaburi 73:16Nilipojaribu kuelewa haya yote, yalikuwa magumu kwangu kuelewa. 17 Zaburi 73:17Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao. 18 Zaburi 73:18Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu. 19 Zaburi 73:19Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho! 20 Zaburi 73:20Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto. 21 Zaburi 73:21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu, 22 Zaburi 73:22nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako. 23 Zaburi 73:23Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume. 24 Zaburi 73:24Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu. 25 Zaburi 73:25Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe. 26 Zaburi 73:26Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele. 27 Zaburi 73:27Wale walio mbali nawe wataangamia, unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako. 28 Zaburi 73:28Lakini kwangu mimi, ni vyema kuwa karibu na Mungu. Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu; nami nitayasimulia matendo yako yote. Zaburi 74Maombi Kwa Ajili Ya Taifa Kuokolewa Utenzi wa Asafu. 1 Zaburi 74:1Ee Mungu, mbona umetukataa milele? Mbona hasira yako inatoka moshi juu ya kondoo wa malisho yako? 2 Zaburi 74:2Kumbuka watu uliowanunua zamani, kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: Mlima Sayuni, ambamo uliishi. 3 Zaburi 74:3Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu. 4 Zaburi 74:4Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi, wanaweka bendera zao kama alama. 5 Zaburi 74:5Walifanya kama watu wanaotumia mashoka kukata kichaka cha miti. 6 Zaburi 74:6Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa kwa mashoka na vishoka vyao. 7 Zaburi 74:7Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu, wakayanajisi makao ya Jina lako. 8 Zaburi 74:8Walisema mioyoni mwao, “Tutawaponda kabisa!” Walichoma kila mahali ambapo Mungu aliabudiwa katika nchi. 9 Zaburi 74:9Hatukupewa ishara za miujiza; hakuna manabii waliobaki, hakuna yeyote kati yetu ajuaye hali hii itachukua muda gani. 10 Zaburi 74:10Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? Je, adui watalitukana jina lako milele? 11 Zaburi 74:11Kwa nini unazuia mkono wako, mkono wako wa kuume? Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako na uwaangamize! 12 Zaburi 74:12Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani, unaleta wokovu duniani. 13 Zaburi 74:13Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji. 14 Zaburi 74:14Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani 74:14 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. nawe ukamtoa kama chakula kwa viumbe vya jangwani. 15 Zaburi 74:15Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito, ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima. 16 Zaburi 74:16Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia, uliziweka jua na mwezi. 17 Zaburi 74:17Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, ulifanya kiangazi na masika. 18 Zaburi 74:18Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki, jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako. 19 Zaburi 74:19Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu; usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele. 20 Zaburi 74:20Likumbuke agano lako, maana mara kwa mara mambo ya jeuri yamejaa katika sehemu za giza nchini. 21 Zaburi 74:21Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu; maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako. 22 Zaburi 74:22Inuka, Ee Mungu, ujitetee; kumbuka jinsi wapumbavu wanavyokudhihaki mchana kutwa. 23 Zaburi 74:23Usipuuze makelele ya watesi wako, ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo. Zaburi 75Mungu Ni Mwamuzi Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo. 1 Zaburi 75:1Ee Mungu, tunakushukuru, tunakushukuru wewe, kwa kuwa jina lako li karibu; watu husimulia matendo yako ya ajabu. 2 Zaburi 75:2Unasema, “Ninachagua wakati maalum; ni mimi nihukumuye kwa haki. 3 Zaburi 75:3Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka, ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara. 4 Zaburi 75:4Kwa wale wenye majivuno ninasema, ‘Msijisifu tena,’ kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu. 5 Zaburi 75:5Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ” 6 Zaburi 75:6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu. 7 Zaburi 75:7Bali Mungu ndiye ahukumuye: Humshusha huyu na kumkweza mwingine. 8 Zaburi 75:8Mkononi mwa Bwana kuna kikombe kilichojaa mvinyo unaotoka povu uliochanganywa na vikolezo; huumimina, nao waovu wote wa dunia hunywa mpaka tone la mwisho. 9 Zaburi 75:9Bali mimi, nitatangaza hili milele; nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo. 10 Zaburi 75:10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote, bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu. Zaburi 76Mungu Wa Israeli Ni Mhukumu Wa Dunia Yote Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo. 1 Zaburi 76:1Katika Yuda, Mungu anajulikana, jina lake ni kuu katika Israeli. 2 Zaburi 76:2Hema lake liko Salemu, makao yake katika Sayuni. 3 Zaburi 76:3Huko alivunja mishale imetametayo, ngao na panga, silaha za vita. 4 Zaburi 76:4Wewe unangʼaa kwa mwanga, mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori. 5 Zaburi 76:5Mashujaa hulala wametekwa nyara, hulala usingizi wao wa mwisho; hakuna hata mmoja wa watu wa vita anayeweza kuinua mikono yake. 6 Zaburi 76:6Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, farasi na gari la vita vilikaa kimya. 7 Zaburi 76:7Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa. Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika? 8 Zaburi 76:8Kutoka mbinguni ulitamka hukumu, nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya: 9 Zaburi 76:9wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu, kuwaokoa wote walioonewa katika nchi. 10 Zaburi 76:10Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa, na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi. 11 Zaburi 76:11Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza; nchi zote za jirani na walete zawadi kwa Yule astahiliye kuogopwa. 12 Zaburi 76:12Huvunja roho za watawala; anaogopwa na wafalme wa dunia. Zaburi 77Matendo Makuu Ya Mungu Yanakumbukwa Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 77:1Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie. 2 Zaburi 77:2Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika. 3 Zaburi 77:3Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; nikatafakari, roho yangu ikadhoofika. 4 Zaburi 77:4Ulizuia macho yangu kufumba; nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema. 5 Zaburi 77:5Nilitafakari juu ya siku zilizopita, miaka mingi iliyopita, 6 Zaburi 77:6nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. Moyo wangu ulitafakari na roho yangu ikauliza: 7 Zaburi 77:7“Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena? 8 Zaburi 77:8Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote? 9 Zaburi 77:9Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?” 10 Zaburi 77:10Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.” 11 Zaburi 77:11Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. 12 Zaburi 77:12Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu. 13 Zaburi 77:13Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? 14 Zaburi 77:14Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa. 15 Zaburi 77:15Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu. 16 Zaburi 77:16Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka. 17 Zaburi 77:17Mawingu yalimwaga maji, mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, mishale yako ikametameta huku na huko. 18 Zaburi 77:18Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, umeme wako wa radi ukaangaza dunia, nchi ikatetemeka na kutikisika. 19 Zaburi 77:19Njia yako ilipita baharini, mapito yako kwenye maji makuu, ingawa nyayo zako hazikuonekana. 20 Zaburi 77:20Uliongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Mose na Aroni. Zaburi 78Mungu Na Watu Wake Utenzi wa Asafu. 1 Zaburi 78:1Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu. 2 Zaburi 78:2Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: 3 Zaburi 78:3yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia. 4 Zaburi 78:4Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. 5 Zaburi 78:5Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao, 6 Zaburi 78:6ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao. 7 Zaburi 78:7Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake. 8 Zaburi 78:8Ili wasifanane na baba zao, waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake, ambao roho zao hazikumwamini. 9 Zaburi 78:9Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita. 10 Zaburi 78:10Hawakulishika agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake. 11 Zaburi 78:11Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonyesha. 12 Zaburi 78:12Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, huko Soani, katika nchi ya Misri. 13 Zaburi 78:13Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta. 14 Zaburi 78:14Aliwaongoza kwa wingu mchana na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha. 15 Zaburi 78:15Alipasua miamba jangwani na akawapa maji tele kama bahari, 16 Zaburi 78:16alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka, akayafanya maji yatiririke kama mito. 17 Zaburi 78:17Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana. 18 Zaburi 78:18Kwa makusudi walimjaribu Mungu, wakidai vyakula walivyovitamani. 19 Zaburi 78:19Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani? 20 Zaburi 78:20Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, vijito vikatiririka maji mengi. Lakini je, aweza kutupa chakula pia? Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?” 21 Zaburi 78:21 Bwana alipowasikia, alikasirika sana, moto wake ukawa dhidi ya Yakobo, na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli, 22 Zaburi 78:22kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake. 23 Zaburi 78:23Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu na kufungua milango ya mbingu, 24 Zaburi 78:24akawanyeshea mana ili watu wale; aliwapa nafaka ya mbinguni. 25 Zaburi 78:25Watu walikula mkate wa malaika, akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula. 26 Zaburi 78:26Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake. 27 Zaburi 78:27Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, ndege warukao kama mchanga wa pwani. 28 Zaburi 78:28Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, kuzunguka mahema yao yote. 29 Zaburi 78:29Walikula na kusaza, kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani. 30 Zaburi 78:30Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao, 31 Zaburi 78:31hasira ya Mungu ikawaka juu yao, akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, akiwaangusha vijana wa Israeli. 32 Zaburi 78:32Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini. 33 Zaburi 78:33Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho. 34 Zaburi 78:34Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku. 35 Zaburi 78:35Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. 36 Zaburi 78:36Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, 37 Zaburi 78:37mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. 38 Zaburi 78:38Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote. 39 Zaburi 78:39Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi. 40 Zaburi 78:40Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani! 41 Zaburi 78:41Walimjaribu Mungu mara kwa mara, wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 42 Zaburi 78:42Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi, 43 Zaburi 78:43siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani. 44 Zaburi 78:44Aligeuza mito yao kuwa damu, hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao. 45 Zaburi 78:45Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, na vyura wakawaharibu. 46 Zaburi 78:46Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige. 47 Zaburi 78:47Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji. 48 Zaburi 78:48Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi. 49 Zaburi 78:49Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu. 50 Zaburi 78:50Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni. 51 Zaburi 78:51Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu. 52 Zaburi 78:52Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani. 53 Zaburi 78:53Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao. 54 Zaburi 78:54Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa. 55 Zaburi 78:55Aliyafukuza mataifa mbele yao, na kuwagawia nchi zao kama urithi, aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao. 56 Zaburi 78:56Lakini wao walimjaribu Mungu, na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, wala hawakuzishika sheria zake. 57 Zaburi 78:57Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu, wakawa wasioweza kutegemewa kama upinde wenye kasoro. 58 Zaburi 78:58Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, wakachochea wivu wake kwa sanamu zao. 59 Zaburi 78:59Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa. 60 Zaburi 78:60Akaiacha hema ya Shilo, hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu. 61 Zaburi 78:61Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui. 62 Zaburi 78:62Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake. 63 Zaburi 78:63Moto uliwaangamiza vijana wao, na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, 64 Zaburi 78:64makuhani wao waliuawa kwa upanga, wala wajane wao hawakuweza kulia. 65 Zaburi 78:65Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo. 66 Zaburi 78:66Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele. 67 Zaburi 78:67Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, hakulichagua kabila la Efraimu, 68 Zaburi 78:68lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda. 69 Zaburi 78:69Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele. 70 Zaburi 78:70Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. 71 Zaburi 78:71Kutoka kuchunga kondoo alimleta kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, wa Israeli urithi wake. 72 Zaburi 78:72Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza. Zaburi 79Maombi Kwa Ajili Ya Wokovu Wa Taifa Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 79:1Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako, wamelinajisi Hekalu lako takatifu, wameifanya Yerusalemu kuwa magofu. 2 Zaburi 79:2Wametoa maiti za watumishi kuwa chakula cha ndege wa angani na nyama ya watakatifu wako kwa wanyama wa nchi. 3 Zaburi 79:3Wamemwaga damu kama maji kuzunguka Yerusalemu yote, wala hakuna yeyote wa kuwazika. 4 Zaburi 79:4Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu, cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. 5 Zaburi 79:5Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele? Wivu wako utawaka kama moto hadi lini? 6 Zaburi 79:6Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali, juu ya falme za hao wasioliitia jina lako, 7 Zaburi 79:7kwa maana wamemrarua Yakobo na kuharibu nchi ya makao yake. 8 Zaburi 79:8Usituhesabie dhambi za baba zetu, huruma yako na itujie hima, kwa maana tu wahitaji mno. 9 Zaburi 79:9Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie, kwa ajili ya utukufu wa jina lako; tuokoe na kutusamehe dhambi zetu kwa ajili ya jina lako. 10 Zaburi 79:10Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wenu?” Mbele ya macho yetu, dhihirisha kati ya mataifa kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa ya watumishi wako. 11 Zaburi 79:11Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako; kwa nguvu za mkono wako hifadhi wale waliohukumiwa kufa. 12 Zaburi 79:12Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwao aibu walizovurumisha juu yako, Ee Bwana. 13 Zaburi 79:13Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako, tutakusifu milele; toka kizazi hadi kizazi tutasimulia sifa zako. Zaburi 80Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 80:1Ee Mchungaji wa Israeli tusikie, wewe umwongozaye Yosefu kama kundi; wewe uketiye katika kiti cha enzi katikati ya makerubi, angaza 2 Zaburi 80:2mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. Uamshe nguvu zako, uje utuokoe. 3 Zaburi 80:3Ee Mungu, uturejeshe, utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa. 4 Zaburi 80:4Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi dhidi ya maombi ya watu wako? 5 Zaburi 80:5Umewalisha kwa mkate wa machozi, umewafanya wanywe machozi bakuli tele. 6 Zaburi 80:6Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu, na adui zetu wanatudhihaki. 7 Zaburi 80:7Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, nasi tuweze kuokolewa. 8 Zaburi 80:8Ulileta mzabibu kutoka Misri, ukawafukuza mataifa, ukaupanda. 9 Zaburi 80:9Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi. 10 Zaburi 80:10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, matawi yake yakafunika mierezi mikubwa. 11 Zaburi 80:11Matawi yake yalienea mpaka Baharini, 80:11 Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania. machipukizi yake mpaka kwenye Mto. 80:11 Yaani Mto Frati. 12 Zaburi 80:12Mbona umebomoa kuta zake ili wote wapitao karibu wazichume zabibu zake? 13 Zaburi 80:13Nguruwe mwitu wanauharibu na wanyama wa kondeni hujilisha humo. 14 Zaburi 80:14Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote! Tazama chini kutoka mbinguni na uone! Linda mzabibu huu, 15 Zaburi 80:15mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, mwana uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe. 16 Zaburi 80:16Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto, unapowakemea, watu wako huangamia. 17 Zaburi 80:17Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume, mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe. 18 Zaburi 80:18Ndipo hatutakuacha tena, utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako. 19 Zaburi 80:19Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, ili tuweze kuokolewa. Zaburi 81Wimbo Wa Sikukuu Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 81:1Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! 2 Zaburi 81:2Anzeni wimbo, pigeni matari, pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri. 3 Zaburi 81:3Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume wakati wa Mwandamo wa Mwezi, na wakati wa mwezi mpevu, katika siku ya Sikukuu yetu; 4 Zaburi 81:4hii ni amri kwa Israeli, agizo la Mungu wa Yakobo. 5 Zaburi 81:5Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu alipotoka dhidi ya Misri, huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa. 6 Zaburi 81:6Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu. 7 Zaburi 81:7Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; nilikujaribu katika maji ya Meriba. 8 Zaburi 81:8“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli! 9 Zaburi 81:9Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; msimsujudie mungu wa kigeni. 10 Zaburi 81:10Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza. 11 Zaburi 81:11“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii. 12 Zaburi 81:12Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe. 13 Zaburi 81:13“Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza, kama Israeli wangalifuata njia zangu, 14 Zaburi 81:14ningaliwatiisha adui zao kwa haraka, na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! 15 Zaburi 81:15Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele. 16 Zaburi 81:16Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora, na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.” Zaburi 82Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 82:1Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”: 2 Zaburi 82:2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu? 3 Zaburi 82:3Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa. 4 Zaburi 82:4Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu. 5 Zaburi 82:5“Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika. 6 Zaburi 82:6“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’ 7 Zaburi 82:7Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.” 8 Zaburi 82:8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako. Zaburi 83Maombi Kwa Ajili Ya Kushindwa Kwa Adui Wa Israeli Wimbo. Zaburi ya Asafu. 1 Zaburi 83:1Ee Mungu, usinyamaze kimya, usinyamaze, Ee Mungu, usitulie. 2 Zaburi 83:2Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao. 3 Zaburi 83:3Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako, wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda. 4 Zaburi 83:4Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa, ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.” 5 Zaburi 83:5Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja, wanafanya muungano dhidi yako, 6 Zaburi 83:6mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari, 7 Zaburi 83:7Gebali, 83:7 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). Amoni na Amaleki, Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro. 8 Zaburi 83:8Hata Ashuru wameungana nao kuwapa nguvu wazao wa Loti. 9 Zaburi 83:9Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani, na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini hapo kijito cha Kishoni, 10 Zaburi 83:10ambao waliangamia huko Endori na wakawa kama takataka juu ya nchi. 11 Zaburi 83:11Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, watawala wao kama Zeba na Salmuna, 12 Zaburi 83:12ambao walisema, “Na tumiliki nchi ya malisho ya Mungu.” 13 Zaburi 83:13Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli, kama makapi yapeperushwayo na upepo. 14 Zaburi 83:14Kama vile moto uteketezavyo msitu au mwali wa moto unavyounguza milima, 15 Zaburi 83:15wafuatilie kwa tufani yako na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako. 16 Zaburi 83:16Funika nyuso zao kwa aibu ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana. 17 Zaburi 83:17Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele, na waangamie kwa aibu. 18 Zaburi 83:18Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana, kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote. Zaburi 84Kuionea Shauku Nyumba Ya Mungu Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora. 1 Zaburi 84:1Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini! 2 Zaburi 84:2Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za Bwana; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai. 3 Zaburi 84:3Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu. 4 Zaburi 84:4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima. 5 Zaburi 84:5Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. 6 Zaburi 84:6Wanapopita katika Bonde la Baka, 84:6 Yaani Bonde la Vilio. hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi. 84:6 Au: baraka. 7 Zaburi 84:7Huendelea toka nguvu hadi nguvu, hadi kila mmoja afikapo mbele za Mungu huko Sayuni. 8 Zaburi 84:8Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo. 9 Zaburi 84:9Ee Mungu, uitazame ngao yetu, mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako. 10 Zaburi 84:10Siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu kuliko kukaa katika mahema ya waovu. 11 Zaburi 84:11Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, Bwana hutoa wema na heshima; hakuna kitu chema anachowanyima wale ambao hawana hatia. 12 Zaburi 84:12Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe. Zaburi 85Maombi Kwa Ajili Ya Ustawi Wa Taifa Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. 1 Zaburi 85:1Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake. 85:1 Au: Uliwarudisha mateka wa Yakobo. 2 Zaburi 85:2Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote. 3 Zaburi 85:3Uliweka kando ghadhabu yako yote na umegeuka na kuiacha hasira yako kali. 4 Zaburi 85:4Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, nawe uiondoe chuki yako juu yetu. 5 Zaburi 85:5Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote? 6 Zaburi 85:6Je, hutatuhuisha tena, ili watu wako wakufurahie? 7 Zaburi 85:7Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, utupe wokovu wako. 8 Zaburi 85:8Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: lakini nao wasirudie upumbavu. 9 Zaburi 85:9Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, ili utukufu wake udumu katika nchi yetu. 10 Zaburi 85:10Upendo na uaminifu hukutana pamoja, haki na amani hubusiana. 11 Zaburi 85:11Uaminifu huchipua kutoka nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni. 12 Zaburi 85:12Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, nayo nchi yetu itazaa mavuno yake. 13 Zaburi 85:13Haki itatangulia mbele yake na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake. Zaburi 86Kuomba Msaada Maombi ya Daudi. 1 Zaburi 86:1Ee Bwana, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji. 2 Zaburi 86:2Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, wewe ni Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako anayekutumaini. 3 Zaburi 86:3Ee Bwana, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa. 4 Zaburi 86:4Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu. 5 Zaburi 86:5Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao. 6 Zaburi 86:6Ee Bwana, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie. 7 Zaburi 86:7Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu. 8 Zaburi 86:8Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe, hakuna matendo ya kulinganishwa na yako. 9 Zaburi 86:9Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya yatakuja na kuabudu mbele zako; wataliletea utukufu jina lako. 10 Zaburi 86:10Kwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu; wewe peke yako ndiwe Mungu. 11 Zaburi 86:11Ee Bwana, nifundishe njia yako, nami nitakwenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako. 12 Zaburi 86:12Ee Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitaliadhimisha jina lako milele. 13 Zaburi 86:13Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi. 86:13 Yaani Kuzimu. 14 Zaburi 86:14Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia; kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu: watu wasiokuheshimu wewe. 15 Zaburi 86:15Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu. 16 Zaburi 86:16Nigeukie na unihurumie; mpe mtumishi wako nguvu zako, mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike. 86:16 Au: mwokoe mwanao mwaminifu. 17 Zaburi 86:17Nipe ishara ya wema wako, ili adui zangu waione nao waaibishwe, kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umenisaidia na kunifariji. Zaburi 87Sifa Za Yerusalemu Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. 1 Zaburi 87:1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 2 Zaburi 87:2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. 3 Zaburi 87:3Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: 4 Zaburi 87:4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu 87:4 Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri. na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, 87:4 Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia. nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” 5 Zaburi 87:5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” 6 Zaburi 87:6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” 7 Zaburi 87:7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.” Zaburi 88Kilio Kwa Ajili Ya Kuomba Msaada Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi. 1 Zaburi 88:1Ee Bwana, Mungu uniokoaye, nimelia mbele zako usiku na mchana. 2 Zaburi 88:2Maombi yangu yafike mbele zako, utegee kilio changu sikio lako. 3 Zaburi 88:3Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi. 88:3 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 4 Zaburi 88:4Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni, niko kama mtu asiye na nguvu. 5 Zaburi 88:5Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako. 6 Zaburi 88:6Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana, katika vina vya giza nene. 7 Zaburi 88:7Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu, umenigharikisha kwa mawimbi yako yote. 8 Zaburi 88:8Umenitenga na rafiki zangu wa karibu na kunifanya chukizo kwao. Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka; 9 Zaburi 88:9nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu. 10 Zaburi 88:10Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu? 11 Zaburi 88:11Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu? 88:11 Yaani Abadon. 12 Zaburi 88:12Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu? 13 Zaburi 88:13Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie; asubuhi maombi yangu huja mbele zako. 14 Zaburi 88:14Ee Bwana, kwa nini unanikataa na kunificha uso wako? 15 Zaburi 88:15Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa. 16 Zaburi 88:16Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza. 17 Zaburi 88:17Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko; zimenimeza kabisa. 18 Zaburi 88:18Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu; giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote. Zaburi 89Wimbo Wakati Wa Taabu Ya Kitaifa Utenzi wa Ethani Mwezrahi. 1 Zaburi 89:1Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote. 2 Zaburi 89:2Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni. 3 Zaburi 89:3Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia mtumishi wangu Daudi, 4 Zaburi 89:4‘Nitaimarisha uzao wako milele na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ” 5 Zaburi 89:5Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako, uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu. 6 Zaburi 89:6Kwa kuwa ni nani katika mbingu anayeweza kulinganishwa na Bwana? Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni aliye kama Bwana? 7 Zaburi 89:7Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana, anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka. 8 Zaburi 89:8Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, ni nani aliye kama wewe? Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu, na uaminifu wako unakuzunguka. 9 Zaburi 89:9Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza. 10 Zaburi 89:10Wewe ulimponda Rahabu 89:10 Rahabu hapa ina maana jina la Misri kwa fumbo, yaani mwenye majivuno (lakini sio Rahabu wa Yos 2). kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako. 11 Zaburi 89:11Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako, uliuwekea ulimwengu msingi pamoja na vyote vilivyomo. 12 Zaburi 89:12Uliumba kaskazini na kusini; Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha. 13 Zaburi 89:13Mkono wako umejaa uwezo; mkono wako una nguvu, mkono wako wa kuume umetukuzwa. 14 Zaburi 89:14Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi; upendo na uaminifu vinakutangulia. 15 Zaburi 89:15Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe, wanaotembea katika mwanga wa uwepo wako, Ee Bwana. 16 Zaburi 89:16Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa, wanafurahi katika haki yako. 17 Zaburi 89:17Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao, kwa wema wako unatukuza pembe 89:17 Pembe inawakilisha nguvu. yetu. 18 Zaburi 89:18Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana, na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli. 19 Zaburi 89:19Ulizungumza wakati fulani katika maono, kwa watu wako waaminifu, ukasema: “Nimeweka nguvu kwa shujaa, nimemwinua kijana miongoni mwa watu. 20 Zaburi 89:20Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimemtia mafuta yangu matakatifu. 21 Zaburi 89:21Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu. 22 Zaburi 89:22Hakuna adui atakayemtoza ushuru, hakuna mtu mwovu atakayemwonea. 23 Zaburi 89:23Nitawaponda adui zake mbele zake na kuwaangamiza watesi wake. 24 Zaburi 89:24Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa. 25 Zaburi 89:25Nitauweka mkono wake juu ya bahari, mkono wake wa kuume juu ya mito. 26 Zaburi 89:26Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’ 27 Zaburi 89:27Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia. 28 Zaburi 89:28Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara. 29 Zaburi 89:29Nitaudumisha uzao wake milele, kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu. 30 Zaburi 89:30“Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu, 31 Zaburi 89:31kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu, 32 Zaburi 89:32nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga, 33 Zaburi 89:33lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe. 34 Zaburi 89:34Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. 35 Zaburi 89:35Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi: 36 Zaburi 89:36kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua; 37 Zaburi 89:37kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.” 38 Zaburi 89:38Lakini wewe umemkataa, umemdharau, umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako. 39 Zaburi 89:39Umelikana agano lako na mtumishi wako, na umeinajisi taji yake mavumbini. 40 Zaburi 89:40Umebomoa kuta zake zote, na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu. 41 Zaburi 89:41Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake; amekuwa dharau kwa jirani zake. 42 Zaburi 89:42Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake, umewafanya watesi wake wote washangilie. 43 Zaburi 89:43Umegeuza makali ya upanga wake, na hukumpa msaada katika vita. 44 Zaburi 89:44Umeikomesha fahari yake, na kukiangusha kiti chake cha enzi. 45 Zaburi 89:45Umezifupisha siku za ujana wake, umemfunika kwa vazi la aibu. 46 Zaburi 89:46Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini? 47 Zaburi 89:47Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka. Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu! 48 Zaburi 89:48Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? 89:48 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 49 Zaburi 89:49Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni, ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi? 50 Zaburi 89:50Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa, jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote, 51 Zaburi 89:51dhihaka ambazo kwazo adui zako wamenisimanga, Ee Bwana, ambazo kwazo wamesimanga kila hatua ya mpakwa mafuta wako. 52 Zaburi 89:52Msifuni Bwana milele! Amen na Amen. KITABU CHA NNE (Zaburi 90–106) Zaburi 90Umilele Wa Mungu Na Udhaifu Wa Mwanadamu Maombi ya Mose, mtu wa Mungu. 1 Zaburi 90:1 Bwana, wewe umekuwa makao yetu katika vizazi vyote. 2 Zaburi 90:2Kabla ya kuzaliwa milima au hujaumba dunia na ulimwengu, wewe ni Mungu tangu milele hata milele. 3 Zaburi 90:3Huwarudisha watu mavumbini, ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.” 4 Zaburi 90:4Kwa maana kwako miaka elfu ni kama siku moja iliyokwisha pita, au kama kesha la usiku. 5 Zaburi 90:5Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo, nao ni kama majani machanga ya asubuhi: 6 Zaburi 90:6ingawa asubuhi yanachipua, ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka. 7 Zaburi 90:7Tumeangamizwa kwa hasira yako na tumetishwa kwa ghadhabu yako. 8 Zaburi 90:8Umeyaweka maovu yetu mbele yako, dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako. 9 Zaburi 90:9Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako, tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza. 10 Zaburi 90:10Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, au miaka themanini ikiwa tuna nguvu, lakini yote ni ya shida na taabu, nazo zapita haraka, nasi twatoweka. 11 Zaburi 90:11Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako? Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako. 12 Zaburi 90:12Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri, ili tujipatie moyo wa hekima. 13 Zaburi 90:13Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini? Wahurumie watumishi wako. 14 Zaburi 90:14Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma, ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote. 15 Zaburi 90:15Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu, kulingana na miaka tuliyotaabika. 16 Zaburi 90:16Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, utukufu wako kwa watoto wao. 17 Zaburi 90:17Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu; uzithibitishe kazi za mikono yetu: naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu. Zaburi 91Mungu Mlinzi Wetu 1 Zaburi 91:1Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. 91:1 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. 2 Zaburi 91:2Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.” 3 Zaburi 91:3Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua. 4 Zaburi 91:4Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. 5 Zaburi 91:5Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana, 6 Zaburi 91:6wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri. 7 Zaburi 91:7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe. 8 Zaburi 91:8Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu. 9 Zaburi 91:9Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako: naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu, 10 Zaburi 91:10basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, hakuna maafa yataikaribia hema yako. 11 Zaburi 91:11Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote. 12 Zaburi 91:12Mikononi mwao watakuinua, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe. 13 Zaburi 91:13Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu. 14 Zaburi 91:14 Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa; nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu. 15 Zaburi 91:15Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu. 16 Zaburi 91:16Kwa siku nyingi nitamshibisha na kumwonyesha wokovu wangu.” Zaburi 92Wimbo Wa Kumsifu Mungu Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato. 1 Zaburi 92:1Ni vyema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana, 2 Zaburi 92:2kuutangaza upendo wako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku, 3 Zaburi 92:3kwa zeze yenye nyuzi kumi na kwa sauti ya kinubi. 4 Zaburi 92:4Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako. 5 Zaburi 92:5Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako, tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako! 6 Zaburi 92:6Mjinga hafahamu, mpumbavu haelewi, 7 Zaburi 92:7ingawa waovu huchipua kama majani na wote watendao mabaya wanastawi, wataangamizwa milele. 8 Zaburi 92:8Bali wewe, Ee Bwana, utatukuzwa milele. 9 Zaburi 92:9Ee Bwana, hakika adui zako, hakika adui zako wataangamia. Wote watendao mabaya watatawanyika. 10 Zaburi 92:10Umeitukuza pembe 92:10 Pembe inawakilisha nguvu. yangu kama ile ya nyati dume, mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu. 11 Zaburi 92:11Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa, masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu. 12 Zaburi 92:12Wenye haki watastawi kama mtende, watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni, 13 Zaburi 92:13waliopandwa katika nyumba ya Bwana, watastawi katika nyua za Mungu wetu. 14 Zaburi 92:14Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu, 15 Zaburi 92:15wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu; yeye ni Mwamba wangu, na ndani yake hamna uovu.” Zaburi 93Mungu Mfalme 1 Zaburi 93:1 Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa. 2 Zaburi 93:2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele. 3 Zaburi 93:3Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake. 4 Zaburi 93:4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu. 5 Zaburi 93:5Ee Bwana, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho. Zaburi 94Mungu Mlipiza Kisasi Kwa Ajili Ya Wenye Haki 1 Zaburi 94:1Ee Bwana, ulipizaye kisasi, Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa. 2 Zaburi 94:2Ee Mhukumu wa dunia, inuka, uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili. 3 Zaburi 94:3Hata lini, waovu, Ee Bwana, hata lini waovu watashangilia? 4 Zaburi 94:4Wanamimina maneno ya kiburi, watenda mabaya wote wamejaa majivuno. 5 Zaburi 94:5Ee Bwana, wanawaponda watu wako, wanawaonea urithi wako. 6 Zaburi 94:6Wanamchinja mjane na mgeni, na kuwaua yatima. 7 Zaburi 94:7Nao husema, “Bwana haoni, Mungu wa Yakobo hafahamu.” 8 Zaburi 94:8Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu; enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima? 9 Zaburi 94:9Je, aliyeweka sikio asisikie? Aliyeumba jicho asione? 10 Zaburi 94:10Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu? Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa? 11 Zaburi 94:11 Bwana anajua mawazo ya mwanadamu; anajua kwamba ni ubatili. 12 Zaburi 94:12Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe, mtu unayemfundisha kwa sheria yako, 13 Zaburi 94:13unampa utulivu siku za shida, mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa kwa ajili ya mwovu. 14 Zaburi 94:14Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake, hatauacha urithi wake. 15 Zaburi 94:15Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki, wote walio na mioyo minyofu wataifuata. 16 Zaburi 94:16Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu? Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu? 17 Zaburi 94:17Kama Bwana asingelinisaidia upesi, ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo. 18 Zaburi 94:18Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia. 19 Zaburi 94:19Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu. 20 Zaburi 94:20Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe, ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake? 21 Zaburi 94:21Huungana kuwashambulia wenye haki, kuwahukumu kufa wasio na hatia. 22 Zaburi 94:22Lakini Bwana amekuwa ngome yangu, na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia. 23 Zaburi 94:23Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao; Bwana Mungu wetu atawaangamiza. Zaburi 95Wimbo Wa Kumsifu Mungu 1 Zaburi 95:1Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu. 2 Zaburi 95:2Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo. 3 Zaburi 95:3Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote. 4 Zaburi 95:4Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake. 5 Zaburi 95:5Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu. 6 Zaburi 95:6Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu, 7 Zaburi 95:7kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo, 8 Zaburi 95:8msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya kule Meriba, 95:8 Meriba maana yake ni Kugombana. kama mlivyofanya siku ile kule Masa 95:8 Masa maana yake ni Kujaribiwa. jangwani, 9 Zaburi 95:9ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima, ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu. 10 Zaburi 95:10Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile, nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.” 11 Zaburi 95:11Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.” Zaburi 96Mungu Mfalme Mkuu (1 Nyakati 16:23-33) 1 Zaburi 96:1Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote. 2 Zaburi 96:2Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. 3 Zaburi 96:3Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. 4 Zaburi 96:4Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. 5 Zaburi 96:5Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu. 6 Zaburi 96:6Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. 7 Zaburi 96:7Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. 8 Zaburi 96:8Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. 9 Zaburi 96:9Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake. 10 Zaburi 96:10Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu. 11 Zaburi 96:11Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; 12 Zaburi 96:12mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; 13 Zaburi 96:13itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake. Zaburi 97Mungu Mtawala Mkuu 1 Zaburi 97:1 Bwana anatawala, nchi na ifurahi, visiwa vyote vishangilie. 2 Zaburi 97:2Mawingu na giza nene vinamzunguka, haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi. 3 Zaburi 97:3Moto hutangulia mbele zake na huteketeza adui zake pande zote. 4 Zaburi 97:4Umeme wake wa radi humulika dunia, nchi huona na kutetemeka. 5 Zaburi 97:5Milima huyeyuka kama nta mbele za Bwana, mbele za Bwana wa dunia yote. 6 Zaburi 97:6Mbingu zinatangaza haki yake, na mataifa yote huona utukufu wake. 7 Zaburi 97:7Wote waabuduo sanamu waaibishwa, wale wajisifiao sanamu: mwabuduni yeye, enyi miungu yote! 8 Zaburi 97:8Sayuni husikia na kushangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana. 9 Zaburi 97:9Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote; umetukuka sana juu ya miungu yote. 10 Zaburi 97:10Wale wanaompenda Bwana na wauchukie uovu, kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu. 11 Zaburi 97:11Nuru huangaza wenye haki na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. 12 Zaburi 97:12Furahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu. Zaburi 98Mungu Mtawala Wa Dunia Zaburi. 1 Zaburi 98:1Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu umemfanyia wokovu. 2 Zaburi 98:2 Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane na amedhihirisha haki yake kwa mataifa. 3 Zaburi 98:3Ameukumbuka upendo wake na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu. 4 Zaburi 98:4Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote, ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda; 5 Zaburi 98:5mwimbieni Bwana kwa kinubi, kwa kinubi na sauti za kuimba, 6 Zaburi 98:6kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume: shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme. 7 Zaburi 98:7Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake, dunia na wote wakaao ndani yake. 8 Zaburi 98:8Mito na ipige makofi, milima na iimbe pamoja kwa furaha, 9 Zaburi 98:9vyote na viimbe mbele za Bwana, kwa maana yuaja kuhukumu dunia. Atahukumu dunia kwa haki na mataifa kwa haki. Zaburi 99Mungu Mfalme Mkuu 1 Zaburi 99:1 Bwana anatawala, mataifa na yatetemeke; anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi, dunia na itikisike. 2 Zaburi 99:2 Bwana ni mkuu katika Sayuni; ametukuzwa juu ya mataifa yote. 3 Zaburi 99:3Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa: yeye ni mtakatifu! 4 Zaburi 99:4Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki, wewe umethibitisha adili; katika Yakobo umefanya yaliyo haki na sawa. 5 Zaburi 99:5Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu. 6 Zaburi 99:6Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita Bwana, naye aliwajibu. 7 Zaburi 99:7Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa. 8 Zaburi 99:8Ee Bwana, wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya. 9 Zaburi 99:9Mtukuzeni Bwana Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu. Zaburi 100Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu Zaburi ya shukrani. 1 Zaburi 100:1Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote. 2 Zaburi 100:2Mwabuduni Bwana kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. 3 Zaburi 100:3Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake. 4 Zaburi 100:4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. 5 Zaburi 100:5Kwa maana Bwana ni mwema na upendo wake wadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote. Zaburi 101Ahadi Ya Kuishi Kwa Uadilifu Na Kwa Haki Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 101:1Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa. 2 Zaburi 101:2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama: utakuja kwangu lini? Nitatembea nyumbani mwangu kwa moyo usio na lawama. 3 Zaburi 101:3Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; hawatashikamana nami. 4 Zaburi 101:4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; nitajitenga na kila ubaya. 5 Zaburi 101:5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri, huyo nitamnyamazisha; mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi huyo sitamvumilia. 6 Zaburi 101:6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, ili waweze kuishi pamoja nami; yeye ambaye moyo wake hauna lawama atanitumikia. 7 Zaburi 101:7Mdanganyifu hatakaa nyumbani mwangu, yeye asemaye kwa uongo hatasimama mbele yangu. 8 Zaburi 101:8Kila asubuhi nitawanyamazisha waovu wote katika nchi; nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya kutoka mji wa Bwana. Zaburi 102Maombi Ya Mtu Mwenye Taabu Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa Bwana. 1 Zaburi 102:1Ee Bwana, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. 2 Zaburi 102:2Usinifiche uso wako ninapokuwa katika shida. Unitegee sikio lako, ninapoita, unijibu kwa upesi. 3 Zaburi 102:3Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi, mifupa yangu inaungua kama kaa la moto. 4 Zaburi 102:4Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani, ninasahau kula chakula changu. 5 Zaburi 102:5Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu, nimebakia ngozi na mifupa. 6 Zaburi 102:6Nimekuwa kama bundi wa jangwani, kama bundi kwenye magofu. 7 Zaburi 102:7Nilalapo sipati usingizi, nimekuwa kama ndege mpweke kwenye paa la nyumba. 8 Zaburi 102:8Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki, wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana. 9 Zaburi 102:9Ninakula majivu kama chakula changu na nimechanganya kinywaji changu na machozi 10 Zaburi 102:10kwa sababu ya ghadhabu yako kuu, kwa maana umeniinua na kunitupa kando. 11 Zaburi 102:11Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, ninanyauka kama jani. 12 Zaburi 102:12Lakini wewe, Ee Bwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele, sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote. 13 Zaburi 102:13Utainuka na kuihurumia Sayuni, kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema; wakati uliokubalika umewadia. 14 Zaburi 102:14Kwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako, vumbi lake lenyewe hulionea huruma. 15 Zaburi 102:15Mataifa wataogopa jina la Bwana, wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako. 16 Zaburi 102:16Kwa maana Bwana ataijenga tena Sayuni na kutokea katika utukufu wake. 17 Zaburi 102:17Ataitikia maombi ya mtu mkiwa, wala hatadharau hoja yao. 18 Zaburi 102:18Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho, ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana: 19 Zaburi 102:19Bwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu, kutoka mbinguni alitazama dunia, 20 Zaburi 102:20kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.” 21 Zaburi 102:21Kwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu, 22 Zaburi 102:22wakati mataifa na falme zitakapokusanyika ili kumwabudu Bwana. 23 Zaburi 102:23Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu, akafupisha siku zangu. 24 Zaburi 102:24Ndipo niliposema: “Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; miaka yako inaendelea vizazi vyote. 25 Zaburi 102:25Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. 26 Zaburi 102:26Hizi zitatoweka, lakini wewe utadumu, zote zitachakaa kama vazi. Utazibadilisha kama nguo nazo zitaondoshwa. 27 Zaburi 102:27Lakini wewe, U yeye yule, nayo miaka yako haikomi kamwe. 28 Zaburi 102:28Watoto wa watumishi wako wataishi mbele zako; wazao wao wataimarishwa mbele zako.” Zaburi 103Upendo Wa Mungu Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 103:1Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. 2 Zaburi 103:2Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, wala usisahau wema wake wote, 3 Zaburi 103:3akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote, 4 Zaburi 103:4aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma, 5 Zaburi 103:5atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai. 6 Zaburi 103:6 Bwana hutenda haki, naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa. 7 Zaburi 103:7Alijulisha Mose njia zake, na wana wa Israeli matendo yake. 8 Zaburi 103:8 Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo. 9 Zaburi 103:9Yeye hatalaumu siku zote, wala haweki hasira yake milele, 10 Zaburi 103:10yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu. 11 Zaburi 103:11Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; 12 Zaburi 103:12kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi. 13 Zaburi 103:13Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha; 14 Zaburi 103:14kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi. 15 Zaburi 103:15Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, anachanua kama ua la shambani; 16 Zaburi 103:16upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, mahali pake hapalikumbuki tena. 17 Zaburi 103:17Lakini kutoka milele hata milele upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao: 18 Zaburi 103:18kwa wale walishikao agano lake na kukumbuka kuyatii mausia yake. 19 Zaburi 103:19 Bwana ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, ufalme wake unatawala juu ya vyote. 20 Zaburi 103:20Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake, ninyi mnaotii neno lake. 21 Zaburi 103:21Mhimidini Bwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake. 22 Zaburi 103:22Mhimidini Bwana, kazi zake zote kila mahali katika milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Zaburi 104Kumsifu Muumba 1 Zaburi 104:1Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. 2 Zaburi 104:2Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema 3 Zaburi 104:3na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na hupanda kwenye mbawa za upepo. 4 Zaburi 104:4Huzifanya pepo kuwa wajumbe 104:4 Au: malaika. wake, miali ya moto watumishi wake. 5 Zaburi 104:5Ameiweka dunia kwenye misingi yake, haiwezi kamwe kuondoshwa. 6 Zaburi 104:6Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi, maji yalisimama juu ya milima. 7 Zaburi 104:7Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia, kwa sauti ya radi yako yakatoroka, 8 Zaburi 104:8yakapanda milima, yakateremka mabondeni, hadi mahali pale ulipoyakusudia. 9 Zaburi 104:9Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka, kamwe hayataifunika dunia tena. 10 Zaburi 104:10Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni, hutiririka kati ya milima. 11 Zaburi 104:11Huwapa maji wanyama wote wa kondeni, punda-mwitu huzima kiu yao. 12 Zaburi 104:12Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji, huimba katikati ya matawi. 13 Zaburi 104:13Huinyeshea milima kutoka orofa zake, dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake. 14 Zaburi 104:14Huyafanya majani ya mifugo yaote, na mimea kwa watu kulima, wajipatie chakula kutoka ardhini: 15 Zaburi 104:15divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu, mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake, na mkate wa kutia mwili nguvu. 16 Zaburi 104:16Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. 17 Zaburi 104:17Humo ndege hufanya viota vyao, korongo ana nyumba yake kwenye msunobari. 18 Zaburi 104:18Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu, majabali ni kimbilio la pelele. 19 Zaburi 104:19Mwezi hugawanya majira, na jua hutambua wakati wake wa kutua. 20 Zaburi 104:20Unaleta giza, kunakuwa usiku, wanyama wote wa mwituni huzurura. 21 Zaburi 104:21Simba hunguruma kwa mawindo yao, na kutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu. 22 Zaburi 104:22Jua huchomoza, nao huondoka, hurudi na kulala katika mapango yao. 23 Zaburi 104:23Kisha mwanadamu huenda kazini mwake, katika kazi yake mpaka jioni. 24 Zaburi 104:24Ee Bwana, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako. 25 Zaburi 104:25Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. 26 Zaburi 104:26Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, 104:26 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. uliyemuumba acheze ndani yake. 27 Zaburi 104:27Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. 28 Zaburi 104:28Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema. 29 Zaburi 104:29Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini. 30 Zaburi 104:30Unapopeleka Roho wako, wanaumbwa, nawe huufanya upya uso wa dunia. 31 Zaburi 104:31Utukufu wa Bwana na udumu milele, Bwana na azifurahie kazi zake: 32 Zaburi 104:32yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka, aigusaye milima, nayo ikatoa moshi. 33 Zaburi 104:33Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote; nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi. 34 Zaburi 104:34Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, ninapofurahi katika Bwana. 35 Zaburi 104:35Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia na waovu wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, msifu Bwana. Msifuni Bwana. 104:35 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah. Zaburi 105Uaminifu Wa Mungu Kwa Israeli (1 Nyakati 16:8-22) 1 Zaburi 105:1Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake, wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. 2 Zaburi 105:2Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, waambieni matendo yake yote ya ajabu. 3 Zaburi 105:3Lishangilieni jina lake takatifu, mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi. 4 Zaburi 105:4Mtafuteni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote. 5 Zaburi 105:5Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, 6 Zaburi 105:6enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake. 7 Zaburi 105:7Yeye ndiye Bwana Mungu wetu, hukumu zake zimo duniani pote. 8 Zaburi 105:8Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, 9 Zaburi 105:9agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki. 10 Zaburi 105:10Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele: 11 Zaburi 105:11“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.” 12 Zaburi 105:12Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake, 13 Zaburi 105:13walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. 14 Zaburi 105:14Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: 15 Zaburi 105:15“Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.” 16 Zaburi 105:16Akaiita njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote, 17 Zaburi 105:17naye akatuma mtu mbele yao, Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa. 18 Zaburi 105:18Walichubua miguu yake kwa minyororo, shingo yake ilifungwa kwa chuma, 19 Zaburi 105:19hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, hadi neno la Bwana lilipomthibitisha. 20 Zaburi 105:20Mfalme alituma watu wakamfungua, mtawala wa watu alimwachia huru. 21 Zaburi 105:21Alimfanya mkuu wa nyumba yake, mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo, 22 Zaburi 105:22kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo na kuwafundisha wazee wake hekima. 23 Zaburi 105:23Kisha Israeli akaingia Misri, Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu. 24 Zaburi 105:24 Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana, akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao, 25 Zaburi 105:25ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, wakatenda hila dhidi ya watumishi wake. 26 Zaburi 105:26Akamtuma Mose mtumishi wake, pamoja na Aroni, aliyemchagua. 27 Zaburi 105:27Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao, miujiza yake katika nchi ya Hamu. 28 Zaburi 105:28Alituma giza na nchi ikajaa giza, kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake? 29 Zaburi 105:29Aligeuza maji yao kuwa damu, ikasababisha samaki wao kufa. 30 Zaburi 105:30Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao. 31 Zaburi 105:31Alisema, yakaja makundi ya mainzi, na viroboto katika nchi yao yote. 32 Zaburi 105:32Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe, yenye umeme wa radi nchini yao yote, 33 Zaburi 105:33akaharibu mizabibu yao na miti ya tini, na akaangamiza miti ya nchi yao. 34 Zaburi 105:34Alisema, nzige wakaja, tunutu wasio na idadi, 35 Zaburi 105:35wakala kila jani katika nchi yao, wakala mazao ya ardhi yao. 36 Zaburi 105:36Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao, matunda ya kwanza ya ujana wao wote. 37 Zaburi 105:37Akawatoa Israeli katika nchi wakiwa na fedha na dhahabu nyingi, wala hakuna hata mmoja kutoka kabila zao aliyejikwaa. 38 Zaburi 105:38Misri ilifurahi walipoondoka, kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia. 39 Zaburi 105:39Alitandaza wingu kama kifuniko, na moto kuwamulikia usiku. 40 Zaburi 105:40Waliomba, naye akawaletea kware, akawashibisha kwa mkate wa mbinguni. 41 Zaburi 105:41Alipasua mwamba, maji yakabubujika, yakatiririka jangwani kama mto. 42 Zaburi 105:42Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake. 43 Zaburi 105:43Aliwatoa watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za shangwe, 44 Zaburi 105:44akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi wa mali wengine walikuwa wameitaabikia: 45 Zaburi 105:45alifanya haya ili wayashike mausia yake na kuzitii sheria zake. Msifuni Bwana. 105:45 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah. Zaburi 106Wema Wa Bwana Kwa Watu Wake 1 Zaburi 106:1Msifuni Bwana. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. 2 Zaburi 106:2Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana au kutangaza kikamilifu sifa zake? 3 Zaburi 106:3Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema. 4 Zaburi 106:4Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, uwe msaada wangu unapowaokoa, 5 Zaburi 106:5ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, na kuungana na urithi wako katika kukusifu. 6 Zaburi 106:6Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, tumekosa na tumetenda uovu. 7 Zaburi 106:7Wakati baba zetu walipokuwa Misri, hawakuzingatia maajabu yako, wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu. 8 Zaburi 106:8Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu. 9 Zaburi 106:9Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani. 10 Zaburi 106:10Aliwaokoa mikononi mwa adui; kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa. 11 Zaburi 106:11Maji yaliwafunika adui zao, hakunusurika hata mmoja. 12 Zaburi 106:12Ndipo walipoamini ahadi zake, nao wakaimba sifa zake. 13 Zaburi 106:13Lakini mara walisahau aliyowatendea, wala hawakungojea shauri lake. 14 Zaburi 106:14Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani. 15 Zaburi 106:15Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha. 16 Zaburi 106:16Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana. 17 Zaburi 106:17Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, ikawazika Abiramu na kundi lake. 18 Zaburi 106:18Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, mwali wa moto uliwateketeza waovu. 19 Zaburi 106:19Huko Horebu walitengeneza ndama, na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma. 20 Zaburi 106:20Waliubadilisha Utukufu wao kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani. 21 Zaburi 106:21Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri, 22 Zaburi 106:22miujiza katika nchi ya Hamu na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu. 23 Zaburi 106:23Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: kama Mose mteule wake, asingesimama kati yao na Mungu kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza. 24 Zaburi 106:24Kisha waliidharau ile nchi nzuri, hawakuiamini ahadi yake. 25 Zaburi 106:25Walinungʼunika ndani ya mahema yao, wala hawakumtii Bwana. 26 Zaburi 106:26Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba atawafanya waanguke jangwani, 27 Zaburi 106:27kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, na kuwatawanya katika nchi zote. 28 Zaburi 106:28Walijifunga nira na Baali wa Peori, wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai. 29 Zaburi 106:29Waliichochea hasira ya Bwana, wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, nayo tauni ikazuka katikati yao. 30 Zaburi 106:30Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, nayo tauni ikazuiliwa. 31 Zaburi 106:31Hili likahesabiwa kwake haki, kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo. 32 Zaburi 106:32Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, janga likampata Mose kwa sababu yao; 33 Zaburi 106:33kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose. 34 Zaburi 106:34Hawakuyaangamiza yale mataifa kama Bwana alivyowaagiza, 35 Zaburi 106:35bali walijichanganya na mataifa na wakazikubali desturi zao. 36 Zaburi 106:36Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao. 37 Zaburi 106:37Wakawatoa wana wao na binti zao dhabihu kwa mashetani. 38 Zaburi 106:38Walimwaga damu isiyo na hatia, damu za wana wao na binti zao, ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, nayo nchi ikanajisika kwa damu zao. 39 Zaburi 106:39Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba. 40 Zaburi 106:40Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake na akauchukia sana urithi wake. 41 Zaburi 106:41Akawakabidhi kwa mataifa na adui zao wakawatawala. 42 Zaburi 106:42Adui zao wakawaonea na kuwatia chini ya mamlaka yao. 43 Zaburi 106:43Mara nyingi aliwaokoa lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, nao wakajiharibu katika dhambi zao. 44 Zaburi 106:44Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao; 45 Zaburi 106:45kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake. 46 Zaburi 106:46Akawafanya wahurumiwe na wote waliowashikilia mateka. 47 Zaburi 106:47Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako. 48 Zaburi 106:48Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Watu wote na waseme, “Amen!” Msifuni Bwana. KITABU CHA TANO (Zaburi 107–150) Zaburi 107Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake 1 Zaburi 107:1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, upendo wake wadumu milele. 2 Zaburi 107:2Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui, 3 Zaburi 107:3wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini. 4 Zaburi 107:4Baadhi yao walitangatanga jangwani, hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi. 5 Zaburi 107:5Walikuwa na njaa na kiu, nafsi zao zikadhoofika. 6 Zaburi 107:6Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. 7 Zaburi 107:7Akawaongoza kwa njia iliyo sawa hadi mji ambao wangeweza kuishi. 8 Zaburi 107:8Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, 9 Zaburi 107:9kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema. 10 Zaburi 107:10Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, wafungwa wakiteseka katika minyororo, 11 Zaburi 107:11kwa sababu walikuwa wameasi dhidi ya maneno ya Mungu na kudharau shauri la Aliye Juu Sana. 12 Zaburi 107:12Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia. 13 Zaburi 107:13Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. 14 Zaburi 107:14Akawatoa katika giza na huzuni kuu na akavunja minyororo yao. 15 Zaburi 107:15Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, 16 Zaburi 107:16kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma. 17 Zaburi 107:17Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao, wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao. 18 Zaburi 107:18Wakachukia kabisa vyakula vyote, wakakaribia malango ya mauti. 19 Zaburi 107:19Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. 20 Zaburi 107:20Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo yao. 21 Zaburi 107:21Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. 22 Zaburi 107:22Na watoe dhabihu za kushukuru, na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha. 23 Zaburi 107:23Wengine walisafiri baharini kwa meli, walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu. 24 Zaburi 107:24Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini. 25 Zaburi 107:25Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu. 26 Zaburi 107:26Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka. 27 Zaburi 107:27Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, ujanja wao ukafikia ukomo. 28 Zaburi 107:28Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, naye akawatoa kwenye taabu yao. 29 Zaburi 107:29Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia. 30 Zaburi 107:30Walifurahi ilipokuwa shwari, naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani. 31 Zaburi 107:31Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. 32 Zaburi 107:32Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee. 33 Zaburi 107:33Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu, 34 Zaburi 107:34nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa, kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo. 35 Zaburi 107:35Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji, nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo; 36 Zaburi 107:36aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, nao wakajenga mji wangeweza kuishi. 37 Zaburi 107:37Walilima mashamba na kupanda mizabibu, nayo ikazaa matunda mengi, 38 Zaburi 107:38Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana, wala hakuruhusu mifugo yao kupungua. 39 Zaburi 107:39Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa kwa kuonewa, maafa na huzuni. 40 Zaburi 107:40Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu, aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia. 41 Zaburi 107:41Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao, na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo. 42 Zaburi 107:42Wanyofu wataona na kufurahi, lakini waovu wote watafunga vinywa vyao. 43 Zaburi 107:43Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya, na atafakari upendo mkuu wa Bwana. Zaburi 108Kuomba Msaada Dhidi Ya Adui (Zaburi 57:7-11; 60:5-12) Wimbo. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 108:1Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 2 Zaburi 108:2Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. 3 Zaburi 108:3Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. 4 Zaburi 108:4Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; uaminifu wako unazifikia anga. 5 Zaburi 108:5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. 6 Zaburi 108:6Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, ili wale uwapendao wapate kuokolewa. 7 Zaburi 108:7Mungu amenena kutoka patakatifu pake: “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi na kulipima Bonde la Sukothi. 8 Zaburi 108:8Gileadi ni yangu, Manase ni yangu, Efraimu ni kofia yangu ya chuma, nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. 9 Zaburi 108:9Moabu ni sinia langu la kunawia, juu ya Edomu natupa kiatu changu; nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” 10 Zaburi 108:10Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? 11 Zaburi 108:11Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, na hutoki tena na majeshi yetu? 12 Zaburi 108:12Tuletee msaada dhidi ya adui, kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. 13 Zaburi 108:13Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, naye atawaponda adui zetu. Zaburi 109Lalamiko La Mtu Aliyeko Kwenye Shida Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 109:1Ee Mungu, ambaye ninakusifu, usiwe kimya, 2 Zaburi 109:2kwa maana watu waovu na wadanganyifu wamefungua vinywa vyao dhidi yangu; wasema dhidi yangu kwa ndimi za udanganyifu. 3 Zaburi 109:3Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, wananishambulia bila sababu. 4 Zaburi 109:4Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, lakini mimi ninawaombea. 5 Zaburi 109:5Wananilipiza mabaya kwa mema, chuki badala ya urafiki wangu. 6 Zaburi 109:6Agiza mtu mwovu ampinge, mshtaki 109:6 Mshtaki hapa maana yake ni Shetani. asimame mkono wake wa kuume. 7 Zaburi 109:7Anapohukumiwa, apatikane na hatia, nayo maombi yake yamhukumu. 8 Zaburi 109:8Siku zake za kuishi na ziwe chache, nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine. 9 Zaburi 109:9Watoto wake na waachwe yatima, mke wake na awe mjane. 10 Zaburi 109:10Watoto wake na watangetange wakiomba, na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao. 11 Zaburi 109:11Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo, matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni. 12 Zaburi 109:12Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema wala wa kuwahurumia yatima wake. 13 Zaburi 109:13Uzao wake na ukatiliwe mbali, majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho. 14 Zaburi 109:14Maovu ya baba zake na yakumbukwe mbele za Bwana, dhambi ya mama yake isifutwe kamwe. 15 Zaburi 109:15Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani. 16 Zaburi 109:16Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. 17 Zaburi 109:17Alipenda kulaani, nayo laana ikampata; hakupenda kubariki, kwa hiyo baraka na ikae mbali naye. 18 Zaburi 109:18Alivaa kulaani kama vazi lake, nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji, kwenye mifupa yake kama mafuta. 19 Zaburi 109:19Na iwe kama joho alilozungushiwa, kama mshipi aliofungiwa daima. 20 Zaburi 109:20Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya. 21 Zaburi 109:21Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wa pendo lako. 22 Zaburi 109:22Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. 23 Zaburi 109:23Ninafifia kama kivuli cha jioni, nimerushwa-rushwa kama nzige. 24 Zaburi 109:24Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, mwili wangu umedhoofika na kukonda. 25 Zaburi 109:25Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, wanionapo, hutikisa vichwa vyao. 26 Zaburi 109:26Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie, niokoe sawasawa na upendo wako. 27 Zaburi 109:27Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili. 28 Zaburi 109:28Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, watakaposhambulia wataaibishwa, lakini mtumishi wako atashangilia. 29 Zaburi 109:29Washtaki wangu watavikwa fedheha, na kufunikwa na aibu kama joho. 30 Zaburi 109:30Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana, katika umati mkubwa nitamsifu. 31 Zaburi 109:31Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji, kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu. Zaburi 110Bwana Na Mfalme Wake Mteule Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 110:1 Bwana amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako.” 2 Zaburi 110:2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako. 3 Zaburi 110:3Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako. 110:3 Au: vijana wako watakujia kama umande. 4 Zaburi 110:4 Bwana ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” 5 Zaburi 110:5Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. 6 Zaburi 110:6Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga na kuwaponda watawala wa dunia nzima. 7 Zaburi 110:7Atakunywa maji katika kijito kando ya njia, 110:7 Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka. kwa hiyo atainua kichwa chake juu. 111 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 111Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu 1 Zaburi 111:1Msifuni Bwana. Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko. 2 Zaburi 111:2Kazi za Bwana ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari. 3 Zaburi 111:3Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima. 4 Zaburi 111:4Amefanya maajabu yake yakumbukwe, Bwana ni mwenye neema na huruma. 5 Zaburi 111:5Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele. 6 Zaburi 111:6Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine. 7 Zaburi 111:7Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika. 8 Zaburi 111:8Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu. 9 Zaburi 111:9Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa. 10 Zaburi 111:10Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele. 112 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 112Baraka Za Mwenye Haki 1 Zaburi 112:1Msifuni Bwana. Heri mtu yule amchaye Bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake. 2 Zaburi 112:2Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. 3 Zaburi 112:3Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, haki yake hudumu milele. 4 Zaburi 112:4Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki. 5 Zaburi 112:5Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, anayefanya mambo yake kwa haki. 6 Zaburi 112:6Hakika hatatikisika kamwe, mtu mwenye haki atakumbukwa milele. 7 Zaburi 112:7Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana. 8 Zaburi 112:8Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake. 9 Zaburi 112:9Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; haki yake hudumu milele; pembe yake itatukuzwa kwa heshima. 10 Zaburi 112:10Mtu mwovu ataona na kuchukizwa, atasaga meno yake na kutoweka, kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu. Zaburi 113Kumsifu Bwana Kwa Wema Wake 1 Zaburi 113:1Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana. 2 Zaburi 113:2Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele. 3 Zaburi 113:3Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa. 4 Zaburi 113:4 Bwana ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu. 5 Zaburi 113:5Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu, Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi, 6 Zaburi 113:6ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi? 7 Zaburi 113:7Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala, 8 Zaburi 113:8huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. 9 Zaburi 113:9Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Bwana. Zaburi 114Maajabu Ya Mungu Wakati Israeli Walipotoka Misri 1 Zaburi 114:1Wakati Israeli walipotoka Misri, nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni, 2 Zaburi 114:2Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu, Israeli akawa milki yake. 3 Zaburi 114:3Bahari ilitazama ikakimbia, Yordani ulirudi nyuma, 4 Zaburi 114:4milima ilirukaruka kama kondoo dume, vilima kama wana-kondoo. 5 Zaburi 114:5Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia, nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma, 6 Zaburi 114:6enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume, enyi vilima, kama wana-kondoo? 7 Zaburi 114:7Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana, mbele za Mungu wa Yakobo, 8 Zaburi 114:8aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji, mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji. Zaburi 115Mungu Mmoja Wa Kweli 1 Zaburi 115:1Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako. 2 Zaburi 115:2Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wao?” 3 Zaburi 115:3Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lolote limpendezalo. 4 Zaburi 115:4Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 5 Zaburi 115:5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona; 6 Zaburi 115:6zina masikio, lakini haziwezi kusikia, zina pua, lakini haziwezi kunusa; 7 Zaburi 115:7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala koo zao haziwezi kutoa sauti. 8 Zaburi 115:8Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. 9 Zaburi 115:9Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao. 10 Zaburi 115:10Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao. 11 Zaburi 115:11Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao. 12 Zaburi 115:12 Bwana anatukumbuka na atatubariki: ataibariki nyumba ya Israeli, ataibariki nyumba ya Aroni, 13 Zaburi 115:13atawabariki wale wanaomcha Bwana, wadogo kwa wakubwa. 14 Zaburi 115:14 Bwana na awawezeshe kuongezeka, ninyi na watoto wenu. 15 Zaburi 115:15Mbarikiwe na Bwana Muumba wa mbingu na dunia. 16 Zaburi 115:16Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana, lakini dunia amempa mwanadamu. 17 Zaburi 115:17Sio wafu wanaomsifu Bwana, wale washukao mahali pa kimya, 115:17 Mahali pa kimya maana yake ni Kuzimu, yaani Sheol kwa Kiebrania. 18 Zaburi 115:18bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, sasa na hata milele. Msifuni Bwana. 115:18 Msifuni Bwana ni Kiebrania Hallelu Yah. Zaburi 116Shukrani Kwa Kuokolewa Kutoka Mauti 1 Zaburi 116:1Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie. 2 Zaburi 116:2Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu. 3 Zaburi 116:3Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. 4 Zaburi 116:4Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!” 5 Zaburi 116:5 Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma. 6 Zaburi 116:6 Bwana huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa. 7 Zaburi 116:7Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako. 8 Zaburi 116:8Kwa kuwa wewe, Ee Bwana, umeniokoa nafsi yangu na mauti, macho yangu kutokana na machozi, miguu yangu kutokana na kujikwaa, 9 Zaburi 116:9ili niweze kutembea mbele za Bwana, katika nchi ya walio hai. 10 Zaburi 116:10Niliamini, kwa hiyo nilisema, “Mimi nimeteseka sana.” 11 Zaburi 116:11Katika taabu yangu nilisema, “Wanadamu wote ni waongo.” 12 Zaburi 116:12Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea? 13 Zaburi 116:13Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana. 14 Zaburi 116:14Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote. 15 Zaburi 116:15Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa Bwana. 16 Zaburi 116:16Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; 116:16 Au: mwanao mwaminifu. umeniweka huru toka katika minyororo yangu. 17 Zaburi 116:17Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la Bwana. 18 Zaburi 116:18Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote, 19 Zaburi 116:19katika nyua za nyumba ya Bwana, katikati yako, ee Yerusalemu. Msifuni Bwana. Zaburi 117Sifa Za Bwana 1 Zaburi 117:1Msifuni Bwana, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote. 2 Zaburi 117:2Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, uaminifu wa Bwana unadumu milele. Msifuni Bwana. Zaburi 118Shukrani Kwa Ajili Ya Ushindi 1 Zaburi 118:1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. 2 Zaburi 118:2Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” 3 Zaburi 118:3Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” 4 Zaburi 118:4Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” 5 Zaburi 118:5Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana, naye akanijibu kwa kuniweka huru. 6 Zaburi 118:6 Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? 7 Zaburi 118:7 Bwana yuko pamoja nami, yeye ni msaidizi wangu. Nitawatazama adui zangu wakiwa wameshindwa. 8 Zaburi 118:8Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kumtumainia mwanadamu. 9 Zaburi 118:9Ni bora kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wakuu. 10 Zaburi 118:10Mataifa yote yalinizunguka, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. 11 Zaburi 118:11Walinizunguka pande zote, lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. 12 Zaburi 118:12Walinizunguka kama kundi la nyuki, lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. 13 Zaburi 118:13Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka, lakini Bwana alinisaidia. 14 Zaburi 118:14 Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu. 15 Zaburi 118:15Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu! 16 Zaburi 118:16Mkono wa kuume wa Bwana umeinuliwa juu, mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!” 17 Zaburi 118:17Sitakufa, bali nitaishi, nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda. 18 Zaburi 118:18 Bwana ameniadhibu vikali, lakini hakuniacha nife. 19 Zaburi 118:19Nifungulie malango ya haki, nami nitaingia na kumshukuru Bwana. 20 Zaburi 118:20Hili ni lango la Bwana ambalo wenye haki wanaweza kuliingia. 21 Zaburi 118:21Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu. 22 Zaburi 118:22Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. 23 Zaburi 118:23 Bwana ametenda hili, nalo ni la kushangaza machoni petu. 24 Zaburi 118:24Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya, tushangilie na kufurahi ndani yake. 25 Zaburi 118:25Ee Bwana, tuokoe, Ee Bwana, utujalie mafanikio. 26 Zaburi 118:26Heri yule ajaye kwa jina la Bwana. Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki. 27 Zaburi 118:27 Bwana ndiye Mungu, naye ametuangazia nuru yake. Mkiwa na matawi mkononi, unganeni kwenye maandamano ya sikukuu hadi kwenye pembe za madhabahu. 28 Zaburi 118:28Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza. 29 Zaburi 118:29Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. 119:0 Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi 22 za alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T). Zaburi 119Sifa Za Sheria Ya Bwana Kujifunza Sheria Ya Bwana 1 Zaburi 119:1Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya Bwana. 2 Zaburi 119:2Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote. 3 Zaburi 119:3Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake. 4 Zaburi 119:4Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu. 5 Zaburi 119:5Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako! 6 Zaburi 119:6Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote. 7 Zaburi 119:7Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki. 8 Zaburi 119:8Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa. Kutii Sheria Ya Bwana 9 Zaburi 119:9Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. 10 Zaburi 119:10Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako. 11 Zaburi 119:11Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi. 12 Zaburi 119:12Sifa ni zako, Ee Bwana, nifundishe maagizo yako. 13 Zaburi 119:13Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako. 14 Zaburi 119:14Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi. 15 Zaburi 119:15Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako. 16 Zaburi 119:16Ninafurahia maagizo yako, wala sitalipuuza neno lako. Furaha Katika Sheria Ya Bwana 17 Zaburi 119:17Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi; nitalitii neno lako. 18 Zaburi 119:18Yafungue macho yangu nipate kuona mambo ya ajabu katika sheria yako. 19 Zaburi 119:19Mimi ni mgeni duniani, usinifiche amri zako. 20 Zaburi 119:20Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa juu ya sheria zako wakati wote. 21 Zaburi 119:21Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa waendao mbali na amri zako. 22 Zaburi 119:22Niondolee dharau na dhihaka, kwa kuwa ninazishika sheria zako. 23 Zaburi 119:23Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia, mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako. 24 Zaburi 119:24Sheria zako ni furaha yangu, nazo ni washauri wangu. Kuamua Kuitii Sheria Ya Bwana 25 Zaburi 119:25Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. 26 Zaburi 119:26Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako. 27 Zaburi 119:27Nijulishe mafundisho ya mausia yako, nami nitatafakari maajabu yako. 28 Zaburi 119:28Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako. 29 Zaburi 119:29Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako. 30 Zaburi 119:30Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako. 31 Zaburi 119:31Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana, usiniache niaibishwe. 32 Zaburi 119:32Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru. Maombi Ili Kupata Ufahamu Wa Sheria 33 Zaburi 119:33Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho. 34 Zaburi 119:34Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote. 35 Zaburi 119:35Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha. 36 Zaburi 119:36Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi. 37 Zaburi 119:37Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. 38 Zaburi 119:38Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa. 39 Zaburi 119:39Niondolee aibu ninayoiogopa, kwa kuwa sheria zako ni njema. 40 Zaburi 119:40Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako. Kuitumainia Sheria Ya Bwana 41 Zaburi 119:41Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie, wokovu wako sawasawa na ahadi yako, 42 Zaburi 119:42ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki, kwa kuwa ninalitumainia neno lako. 43 Zaburi 119:43Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako. 44 Zaburi 119:44Nitaitii amri yako daima, naam, milele na milele. 45 Zaburi 119:45Nitatembea nikiwa huru, kwa kuwa nimejifunza mausia yako. 46 Zaburi 119:46Nitasema sheria zako mbele za wafalme wala sitaaibishwa, 47 Zaburi 119:47kwa kuwa ninazifurahia amri zako kwa sababu ninazipenda. 48 Zaburi 119:48Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu, nami ninatafakari juu ya maagizo yako. Matumaini Katika Sheria Ya Bwana 49 Zaburi 119:49Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako, kwa sababu umenipa tumaini. 50 Zaburi 119:50Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu. 51 Zaburi 119:51Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka, hata hivyo sitaiacha sheria yako. 52 Zaburi 119:52Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani, nazo zinanifariji. 53 Zaburi 119:53Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu, ambao wameacha sheria yako. 54 Zaburi 119:54Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu popote ninapoishi. 55 Zaburi 119:55Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako, nami nitatii sheria yako. 56 Zaburi 119:56Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako. Kujitolea Katika Sheria Ya Bwana 57 Zaburi 119:57Ee Bwana, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako. 58 Zaburi 119:58Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako. 59 Zaburi 119:59Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako. 60 Zaburi 119:60Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako. 61 Zaburi 119:61Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako. 62 Zaburi 119:62Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki. 63 Zaburi 119:63Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao, kwa wote wanaofuata mausia yako. 64 Zaburi 119:64Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako, nifundishe maagizo yako. Thamani Ya Sheria Ya Bwana 65 Zaburi 119:65Mtendee wema mtumishi wako Ee Bwana, sawasawa na neno lako. 66 Zaburi 119:66Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri, kwa kuwa ninaamini amri zako. 67 Zaburi 119:67Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako. 68 Zaburi 119:68Wewe ni mwema, unalotenda ni jema, nifundishe maagizo yako. 69 Zaburi 119:69Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo, nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote. 70 Zaburi 119:70Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako. 71 Zaburi 119:71Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako. 72 Zaburi 119:72Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu. Haki Ya Sheria Ya Bwana 73 Zaburi 119:73Mikono yako ilinifanya na kuniumba, nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako. 74 Zaburi 119:74Wakuchao wafurahie wanaponiona, kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako. 75 Zaburi 119:75Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu. 76 Zaburi 119:76Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu, sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako. 77 Zaburi 119:77Huruma yako na inijie ili nipate kuishi, kwa kuwa naifurahia sheria yako. 78 Zaburi 119:78Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako. 79 Zaburi 119:79Wale wakuchao na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako. 80 Zaburi 119:80Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe. Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa 81 Zaburi 119:81Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako, lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako. 82 Zaburi 119:82Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako; ninasema, “Utanifajiri lini?” 83 Zaburi 119:83Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi, bado sijasahau maagizo yako. 84 Zaburi 119:84Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini? Ni lini utawaadhibu washtaki wangu? 85 Zaburi 119:85Wenye majivuno wananichimbia mashimo, kinyume na sheria yako. 86 Zaburi 119:86Amri zako zote ni za kuaminika; unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu. 87 Zaburi 119:87Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia, lakini sijaacha mausia yako. 88 Zaburi 119:88Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako, nami nitatii sheria za kinywa chako. Imani Katika Sheria Ya Bwana 89 Zaburi 119:89Ee Bwana, neno lako ni la milele, linasimama imara mbinguni. 90 Zaburi 119:90Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote, umeiumba dunia, nayo inadumu. 91 Zaburi 119:91Sheria zako zinadumu hadi leo, kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia. 92 Zaburi 119:92Kama nisingefurahia sheria yako, ningeangamia katika taabu zangu. 93 Zaburi 119:93Sitasahau mausia yako kamwe, kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu. 94 Zaburi 119:94Uniokoe, kwa maana mimi ni wako, kwa kuwa nimetafuta mausia yako. 95 Zaburi 119:95Waovu wanangojea kuniangamiza, bali mimi ninatafakari sheria zako. 96 Zaburi 119:96Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo, lakini amri zako hazina mpaka. Kuipenda Sheria Ya Bwana 97 Zaburi 119:97Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa. 98 Zaburi 119:98Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima. 99 Zaburi 119:99Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako. 100 Zaburi 119:100Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako. 101 Zaburi 119:101Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako. 102 Zaburi 119:102Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe. 103 Zaburi 119:103Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu! 104 Zaburi 119:104Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu. Nuru Kutoka Kwenye Sheria Ya Bwana 105 Zaburi 119:105Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu. 106 Zaburi 119:106Nimeapa na nimethibitisha, kwamba nitafuata sheria zako za haki. 107 Zaburi 119:107Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana, sawasawa na neno lako. 108 Zaburi 119:108Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako. 109 Zaburi 119:109Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote, sitasahau sheria yako. 110 Zaburi 119:110Waovu wamenitegea mtego, lakini sijayakiuka maagizo yako. 111 Zaburi 119:111Sheria zako ni urithi wangu milele, naam ni furaha ya moyo wangu. 112 Zaburi 119:112Nimekusudia moyoni mwangu kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho. Usalama Ndani Ya Sheria Ya Bwana 113 Zaburi 119:113Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako. 114 Zaburi 119:114Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu, nimeweka tumaini langu katika neno lako. 115 Zaburi 119:115Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya, ili niweze kushika amri za Mungu wangu! 116 Zaburi 119:116Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa. 117 Zaburi 119:117Nitegemeze, nami nitaokolewa, nami daima nitayaheshimu maagizo yako. 118 Zaburi 119:118Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako, kwa maana udanganyifu wao ni bure. 119 Zaburi 119:119Waovu wa nchi unawatupa kama takataka, kwa hivyo nazipenda sheria zako. 120 Zaburi 119:120Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe, ninaziogopa sheria zako. Kuitii Sheria Ya Bwana 121 Zaburi 119:121Nimetenda yaliyo haki na sawa, usiniache mikononi mwa watesi wangu. 122 Zaburi 119:122Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee. 123 Zaburi 119:123Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli. 124 Zaburi 119:124Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako. 125 Zaburi 119:125Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu ili niweze kuelewa sheria zako. 126 Zaburi 119:126Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa. 127 Zaburi 119:127Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi, 128 Zaburi 119:128na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, nachukia kila njia potovu. Shauku Ya Kuitii Sheria Ya Bwana 129 Zaburi 119:129Sheria zako ni za ajabu, hivyo ninazitii. 130 Zaburi 119:130Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu. 131 Zaburi 119:131Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako. 132 Zaburi 119:132Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako. 133 Zaburi 119:133Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale. 134 Zaburi 119:134Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako. 135 Zaburi 119:135Mwangazie mtumishi wako uso wako na unifundishe amri zako. 136 Zaburi 119:136Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi. Haki Ya Sheria Ya Bwana 137 Zaburi 119:137Ee Bwana, wewe ni mwenye haki, sheria zako ni sahihi. 138 Zaburi 119:138Sheria ulizoziweka ni za haki, ni za kuaminika kikamilifu. 139 Zaburi 119:139Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu wanayapuuza maneno yako. 140 Zaburi 119:140Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu, mtumishi wako anazipenda. 141 Zaburi 119:141Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa, sisahau mausia yako. 142 Zaburi 119:142Haki yako ni ya milele, na sheria yako ni kweli. 143 Zaburi 119:143Shida na dhiki zimenipata, lakini amri zako ni furaha yangu. 144 Zaburi 119:144Sheria zako ni sahihi milele, hunipa ufahamu ili nipate kuishi. Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa 145 Zaburi 119:145Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote, nami nitayatii maagizo yako. 146 Zaburi 119:146Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako. 147 Zaburi 119:147Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako. 148 Zaburi 119:148Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako. 149 Zaburi 119:149Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako. 150 Zaburi 119:150Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, lakini wako mbali na sheria yako. 151 Zaburi 119:151Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu, na amri zako zote ni za kweli. 152 Zaburi 119:152Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele. Maombi Kwa Ajili Ya Msaada 153 Zaburi 119:153Yaangalie mateso yangu, uniokoe, kwa kuwa sijasahau sheria yako. 154 Zaburi 119:154Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako. 155 Zaburi 119:155Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako. 156 Zaburi 119:156Ee Bwana, huruma zako ni kuu, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako. 157 Zaburi 119:157Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako. 158 Zaburi 119:158Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako. 159 Zaburi 119:159Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako. 160 Zaburi 119:160Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele. Kujiweka Wakfu Kwa Sheria Ya Bwana 161 Zaburi 119:161Watawala wamenitesa bila sababu, lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako. 162 Zaburi 119:162Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi. 163 Zaburi 119:163Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo, lakini napenda sheria yako. 164 Zaburi 119:164Ninakusifu mara saba kwa siku, kwa ajili ya sheria zako za haki. 165 Zaburi 119:165Wanaopenda sheria yako wana amani tele, wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza. 166 Zaburi 119:166Ee Bwana, ninangojea wokovu wako, nami ninafuata amri zako, 167 Zaburi 119:167Ninazitii sheria zako, kwa sababu ninazipenda mno. 168 Zaburi 119:168Nimetii mausia yako na sheria zako, kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako. Kuomba Msaada 169 Zaburi 119:169Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako, nipe ufahamu sawasawa na neno lako. 170 Zaburi 119:170Maombi yangu na yafike mbele zako, niokoe sawasawa na ahadi yako. 171 Zaburi 119:171Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako. 172 Zaburi 119:172Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki. 173 Zaburi 119:173Mkono wako uwe tayari kunisaidia, kwa kuwa nimechagua mausia yako. 174 Zaburi 119:174Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu. 175 Zaburi 119:175Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, na sheria zako zinitegemeze. 176 Zaburi 119:176Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. Mtafute mtumishi wako, kwa kuwa sijasahau amri zako. Zaburi 120Kuomba Msaada Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 120:1Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu. 2 Zaburi 120:2Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu. 3 Zaburi 120:3Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu? 4 Zaburi 120:4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. 5 Zaburi 120:5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari! 6 Zaburi 120:6Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani. 7 Zaburi 120:7Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita. Zaburi 121Bwana Mlinzi Wetu Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 121:1Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi? 2 Zaburi 121:2Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. 3 Zaburi 121:3Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, 4 Zaburi 121:4hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. 5 Zaburi 121:5 Bwana anakulinda, Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume, 6 Zaburi 121:6jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku. 7 Zaburi 121:7 Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, 8 Zaburi 121:8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele. Zaburi 122Sifa Kwa Yerusalemu Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Zaburi 122:1Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.” 2 Zaburi 122:2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako. 3 Zaburi 122:3Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja. 4 Zaburi 122:4Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli. 5 Zaburi 122:5Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. 6 Zaburi 122:6Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama. 7 Zaburi 122:7Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.” 8 Zaburi 122:8Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.” 9 Zaburi 122:9Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako. Zaburi 123Kuomba Rehema Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 123:1Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni. 2 Zaburi 123:2Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mtumishi wa kike yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu, mpaka atakapotuhurumia. 3 Zaburi 123:3Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi. 4 Zaburi 123:4Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno. Zaburi 124Shukrani Kwa Ukombozi Wa Israeli Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Zaburi 124:1Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa: 2 Zaburi 124:2kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia, 3 Zaburi 124:3wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai, 4 Zaburi 124:4mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika, 5 Zaburi 124:5maji yaendayo kasi yangalituchukua. 6 Zaburi 124:6 Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. 7 Zaburi 124:7Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka. 8 Zaburi 124:8Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. Zaburi 125Usalama Wa Watu Wa Mungu Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 125:1Wale wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele. 2 Zaburi 125:2Kama milima inavyozunguka Yerusalemu, ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake sasa na hata milele. 3 Zaburi 125:3Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi waliopewa wenye haki, ili wenye haki wasije wakatumia mikono yao kutenda ubaya. 4 Zaburi 125:4Ee Bwana, watendee mema walio wema, wale walio wanyofu wa moyo. 5 Zaburi 125:5Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya. Amani iwe juu ya Israeli. Zaburi 126Kurejezwa Kutoka Utumwani Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 126:1 Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto. 2 Zaburi 126:2Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu.” 3 Zaburi 126:3 Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha. 4 Zaburi 126:4Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu. 5 Zaburi 126:5Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe. 6 Zaburi 126:6Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake. Zaburi 127Bila Mungu, Kazi Ya Mwanadamu Haifai Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni. 1 Zaburi 127:1 Bwana asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure. 2 Zaburi 127:2Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake. 3 Zaburi 127:3Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake. 4 Zaburi 127:4Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. 5 Zaburi 127:5Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni. Zaburi 128Thawabu Ya Kumtii Bwana Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 128:1Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake. 2 Zaburi 128:2Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. 3 Zaburi 128:3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. 4 Zaburi 128:4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana. 5 Zaburi 128:5 Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, 6 Zaburi 128:6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli. Zaburi 129Maombi Dhidi Ya Adui Za Israeli Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 129:1Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: 2 Zaburi 129:2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. 3 Zaburi 129:3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. 4 Zaburi 129:4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. 5 Zaburi 129:5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. 6 Zaburi 129:6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7 Zaburi 129:7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. 8 Zaburi 129:8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.” Zaburi 130Kuomba Msaada Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 130:1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana. 2 Zaburi 130:2Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie. 3 Zaburi 130:3Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama? 4 Zaburi 130:4Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa. 5 Zaburi 130:5Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu. 6 Zaburi 130:6Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi. 7 Zaburi 130:7Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili. 8 Zaburi 130:8Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote. Zaburi 131Kumtegemea Mungu Kwa Unyenyekevu Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Zaburi 131:1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu. 2 Zaburi 131:2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu. 3 Zaburi 131:3Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele. Zaburi 132Maskani Ya Mungu Ya Milele Katika Sayuni Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 132:1Ee Bwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili. 2 Zaburi 132:2Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: 3 Zaburi 132:3“Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu: 4 Zaburi 132:4sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia, 5 Zaburi 132:5mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” 6 Zaburi 132:6Tulisikia habari hii huko Efrathi, tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara: 132:6 Yaani Kiriath-Yearimu. 7 Zaburi 132:7“Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; 8 Zaburi 132:8inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. 9 Zaburi 132:9Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” 10 Zaburi 132:10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako. 11 Zaburi 132:11 Bwana alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe katika kiti chako cha enzi, 12 Zaburi 132:12kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.” 13 Zaburi 132:13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake: 14 Zaburi 132:14“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku: 15 Zaburi 132:15Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula. 16 Zaburi 132:16Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha. 17 Zaburi 132:17“Hapa nitamchipushia Daudi pembe, 132:17 Pembe inawakilisha nguvu. na kuweka taa kwa ajili ya masiya 132:17 Masiya yaani mpakwa mafuta. wangu. 18 Zaburi 132:18Adui zake nitawavika aibu, bali taji kichwani pake itangʼaa sana.” Zaburi 133Sifa Za Pendo La Undugu Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. 1 Zaburi 133:1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! 2 Zaburi 133:2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. 3 Zaburi 133:3Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele. Zaburi 134Wito Wa Kumsifu Mungu Wimbo wa kwenda juu. 1 Zaburi 134:1Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana. 2 Zaburi 134:2Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana. 3 Zaburi 134:3Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni. Zaburi 135Wimbo Wa Sifa Kwa Mungu 1 Zaburi 135:1Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana, 2 Zaburi 135:2ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. 3 Zaburi 135:3Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza. 4 Zaburi 135:4Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani. 5 Zaburi 135:5Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu, kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote. 6 Zaburi 135:6 Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote. 7 Zaburi 135:7Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake. 8 Zaburi 135:8Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama. 9 Zaburi 135:9Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote. 10 Zaburi 135:10Aliyapiga mataifa mengi, na akaua wafalme wenye nguvu: 11 Zaburi 135:11Mfalme Sihoni na Waamori, Ogu mfalme wa Bashani na wafalme wote wa Kanaani: 12 Zaburi 135:12akatoa nchi yao kuwa urithi, urithi kwa watu wake Israeli. 13 Zaburi 135:13Ee Bwana, jina lako ladumu milele, kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote. 14 Zaburi 135:14Maana Bwana atawathibitisha watu wake, na kuwahurumia watumishi wake. 15 Zaburi 135:15Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 16 Zaburi 135:16Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona; 17 Zaburi 135:17zina masikio, lakini haziwezi kusikia, wala hakuna pumzi katika vinywa vyao. 18 Zaburi 135:18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. 19 Zaburi 135:19Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana; 20 Zaburi 135:20ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana; ninyi mnaomcha, msifuni Bwana. 21 Zaburi 135:21Msifuni Bwana kutoka Sayuni, msifuni yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Bwana. Zaburi 136Wimbo Wa Kumshukuru Mungu 1 Zaburi 136:1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele. 2 Zaburi 136:2Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. 3 Zaburi 136:3Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele. 4 Zaburi 136:4Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele. 5 Zaburi 136:5Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele. 6 Zaburi 136:6Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele. 7 Zaburi 136:7Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele. 8 Zaburi 136:8Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele. 9 Zaburi 136:9Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele. 10 Zaburi 136:10Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele. 11 Zaburi 136:11Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele. 12 Zaburi 136:12Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele. 13 Zaburi 136:13Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. 14 Zaburi 136:14Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele. 15 Zaburi 136:15Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. 16 Zaburi 136:16Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele. 17 Zaburi 136:17Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. 18 Zaburi 136:18Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. 19 Zaburi 136:19Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele. 20 Zaburi 136:20Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele. 21 Zaburi 136:21Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele. 22 Zaburi 136:22Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele. 23 Zaburi 136:23Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele. 24 Zaburi 136:24Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele. 25 Zaburi 136:25Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele. 26 Zaburi 136:26Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele. Zaburi 137Maombolezo Ya Israeli Uhamishoni 1 Zaburi 137:1Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni. 2 Zaburi 137:2Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu, 3 Zaburi 137:3kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!” 4 Zaburi 137:4Tutaimbaje nyimbo za Bwana, tukiwa nchi ya kigeni? 5 Zaburi 137:5Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. 6 Zaburi 137:6Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa. 7 Zaburi 137:7Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, Bomoa mpaka kwenye misingi yake!” 8 Zaburi 137:8Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, heri yeye atakayekulipiza wewe kwa yale uliyotutenda sisi: 9 Zaburi 137:9yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga na kuwaponda juu ya miamba. Zaburi 138Maombi Ya Shukrani Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 138:1Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote, mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako. 2 Zaburi 138:2Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote. 3 Zaburi 138:3Nilipoita, ulinijibu; ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari. 4 Zaburi 138:4Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana, wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. 5 Zaburi 138:5Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana, kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu. 6 Zaburi 138:6Ingawa Bwana yuko juu, humwangalia mnyonge, bali mwenye kiburi yeye anamjua kutokea mbali. 7 Zaburi 138:7Nijapopita katikati ya shida, wewe unayahifadhi maisha yangu, unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, kwa mkono wako wa kuume unaniokoa. 8 Zaburi 138:8 Bwana atatimiza kusudi lake kwangu, Ee Bwana, upendo wako wadumu milele: usiziache kazi za mikono yako. Zaburi 139Mungu Asiyeweza Kukwepwa Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 139:1Ee Bwana, umenichunguza na kunijua. 2 Zaburi 139:2Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali. 3 Zaburi 139:3Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. 4 Zaburi 139:4Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana. 5 Zaburi 139:5Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu. 6 Zaburi 139:6Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, ni ya juu sana kwangu kuyafikia. 7 Zaburi 139:7Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? 8 Zaburi 139:8Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi 139:8 Vilindi ina maana ya Kuzimu, ambayo ni Sheol kwa Kiebrania. kuwa kitanda changu, wewe uko huko. 9 Zaburi 139:9Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko, kama nikikaa pande za mbali za bahari, 10 Zaburi 139:10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. 11 Zaburi 139:11Kama nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” 12 Zaburi 139:12hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako. 13 Zaburi 139:13Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. 14 Zaburi 139:14Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu. 15 Zaburi 139:15Umbile langu halikufichika kwako, nilipoumbwa mahali pa siri. Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, 16 Zaburi 139:16macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwepo hata moja. 17 Zaburi 139:17Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! Jinsi jumla yake ilivyo kubwa! 18 Zaburi 139:18Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi kuliko mchanga. Niamkapo, bado niko pamoja nawe. 19 Zaburi 139:19Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu! 20 Zaburi 139:20Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, adui zako wanatumia vibaya jina lako. 21 Zaburi 139:21Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako? 22 Zaburi 139:22Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, ninawahesabu ni adui zangu. 23 Zaburi 139:23Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu. 24 Zaburi 139:24Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele. Zaburi 140Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 140:1Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu; nilinde na watu wenye jeuri, 2 Zaburi 140:2ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, na kuchochea vita siku zote. 3 Zaburi 140:3Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao. 4 Zaburi 140:4Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu; nilinde na watu wenye jeuri wanaopanga kunikwaza miguu yangu. 5 Zaburi 140:5Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, wametandaza kamba za wavu wao, wametega mitego kwenye njia yangu. 6 Zaburi 140:6Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia. 7 Zaburi 140:7Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, unikingaye kichwa changu siku ya vita: 8 Zaburi 140:8Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao, usiache mipango yao ikafanikiwa, wasije wakajisifu. 9 Zaburi 140:9Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida zinazosababishwa na midomo yao. 10 Zaburi 140:10Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe. 11 Zaburi 140:11Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri. 12 Zaburi 140:12Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji. 13 Zaburi 140:13Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako. Zaburi 141Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 141:1Ee Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima. Sikia sauti yangu ninapokuita. 2 Zaburi 141:2Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni. 3 Zaburi 141:3Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu, weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu. 4 Zaburi 141:4Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya, nisije nikashiriki katika matendo maovu pamoja na watu watendao mabaya, wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa. 5 Zaburi 141:5Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma; na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu. Kichwa changu hakitalikataa. Hata hivyo, maombi yangu daima ni kinyume cha watenda mabaya, 6 Zaburi 141:6watawala wao watatupwa chini kutoka kwenye majabali, waovu watajifunza kwamba maneno yangu yalikuwa kweli. 7 Zaburi 141:7Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” 8 Zaburi 141:8Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi, ndani yako nimekimbilia, usiniache nife. 9 Zaburi 141:9Niepushe na mitego waliyonitegea, kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya. 10 Zaburi 141:10Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe, wakati mimi ninapita salama. Zaburi 142Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Watesi Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Maombi. 1 Zaburi 142:1Namlilia Bwana kwa sauti, nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie. 2 Zaburi 142:2Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu. 3 Zaburi 142:3Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego. 4 Zaburi 142:4Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu. 5 Zaburi 142:5Ee Bwana, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.” 6 Zaburi 142:6Sikiliza kilio changu, kwa sababu mimi ni mhitaji sana; niokoe na wale wanaonifuatilia, kwa kuwa wamenizidi nguvu. 7 Zaburi 142:7Nifungue kutoka kifungo changu, ili niweze kulisifu jina lako. Ndipo wenye haki watanizunguka, kwa sababu ya wema wako kwangu. Zaburi 143Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Adui Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 143:1Ee Bwana, sikia sala yangu, sikiliza kilio changu unihurumie; katika uaminifu na haki yako njoo unisaidie. 2 Zaburi 143:2Usimhukumu mtumishi wako, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako. 3 Zaburi 143:3Adui hunifuatilia, hunipondaponda chini; hunifanya niishi gizani kama wale waliokufa zamani. 4 Zaburi 143:4Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. 5 Zaburi 143:5Nakumbuka siku za zamani; natafakari juu ya kazi zako zote, naangalia juu ya kazi ambazo mikono yako imezifanya. 6 Zaburi 143:6Nanyoosha mikono yangu kwako, nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. 7 Zaburi 143:7Ee Bwana, unijibu haraka, roho yangu inazimia. Usinifiche uso wako, ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni. 8 Zaburi 143:8Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. Nionyeshe njia nitakayoiendea, kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. 9 Zaburi 143:9Ee Bwana, uniokoe na adui zangu, kwa kuwa nimejificha kwako. 10 Zaburi 143:10Nifundishe kufanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, Roho wako mwema na aniongoze katika nchi tambarare. 11 Zaburi 143:11Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu, kwa haki yako nitoe katika taabu. 12 Zaburi 143:12Kwa upendo wako usiokoma, nyamazisha adui zangu; waangamize watesi wangu wote, kwa kuwa mimi ni mtumishi wako. Zaburi 144Mfalme Amshukuru Mungu Kwa Ushindi Zaburi ya Daudi. 1 Zaburi 144:1Sifa ni kwa Bwana Mwamba wangu, aifundishaye mikono yangu vita, na vidole vyangu kupigana. 2 Zaburi 144:2Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, ngome yangu na mwokozi wangu, ngao yangu ninayemkimbilia, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. 3 Zaburi 144:3Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie? 4 Zaburi 144:4Mwanadamu ni kama pumzi, siku zake ni kama kivuli kinachopita. 5 Zaburi 144:5Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, gusa milima ili itoe moshi. 6 Zaburi 144:6Peleka umeme uwatawanye adui, lenga mishale yako uwashinde. 7 Zaburi 144:7Nyoosha mkono wako kutoka juu, nikomboe na kuniokoa kutoka maji makuu, kutoka mikononi mwa wageni 8 Zaburi 144:8ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. 9 Zaburi 144:9Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia, 10 Zaburi 144:10kwa Yule awapaye wafalme ushindi, ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari. 11 Zaburi 144:11Nikomboe na uniokoe kutoka mikononi mwa wageni ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. 12 Zaburi 144:12Kisha wana wetu wakati wa ujana wao watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa kurembesha jumba la kifalme. 13 Zaburi 144:13Ghala zetu zitajazwa aina zote za mahitaji. Kondoo zetu watazaa kwa maelfu, kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu; 14 Zaburi 144:14maksai wetu watakokota mizigo mizito. Hakutakuwa na kubomoka kuta, hakuna kuchukuliwa mateka, wala kilio cha taabu katika barabara zetu. 15 Zaburi 144:15Heri watu ambao hili ni kweli; heri wale ambao Bwana ni Mungu wao. 145:1 Zaburi hii imetungwa kila mstari (ikiwa ni pamoja na 13b) ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. Zaburi 145Wimbo Wa Kusifu Ukuu Na Wema Wa Mungu Wimbo wa Sifa. Wa Daudi. 1 Zaburi 145:1Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele. 2 Zaburi 145:2Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele. 3 Zaburi 145:3 Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki. 4 Zaburi 145:4Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu. 5 Zaburi 145:5Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. 6 Zaburi 145:6Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu. 7 Zaburi 145:7Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako. 8 Zaburi 145:8 Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo. 9 Zaburi 145:9 Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya. 10 Zaburi 145:10Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza. 11 Zaburi 145:11Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako, 12 Zaburi 145:12ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako. 13 Zaburi 145:13Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. 14 Zaburi 145:14 Bwana huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao. 15 Zaburi 145:15Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake. 16 Zaburi 145:16Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. 17 Zaburi 145:17 Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. 18 Zaburi 145:18 Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. 19 Zaburi 145:19Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa. 20 Zaburi 145:20 Bwana huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza. 21 Zaburi 145:21Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele. Zaburi 146Kumsifu Mungu Mwokozi 1 Zaburi 146:1Msifuni Bwana! 146:1 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah. Ee nafsi yangu, umsifu Bwana, 2 Zaburi 146:2Nitamsifu Bwana maisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu sifa wakati wote niishipo. 3 Zaburi 146:3Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa. 4 Zaburi 146:4Roho yao itokapo hurudi mavumbini, siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma. 5 Zaburi 146:5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake, 6 Zaburi 146:6Muumba wa mbingu na nchi, na bahari na vyote vilivyomo ndani yake: Bwana anayedumu kuwa mwaminifu milele na milele. 7 Zaburi 146:7Naye huwapatia haki walioonewa na kuwapa wenye njaa chakula. Bwana huwaweka wafungwa huru, 8 Zaburi 146:8 Bwana huwafumbua vipofu macho, Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao, Bwana huwapenda wenye haki. 9 Zaburi 146:9 Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu. 10 Zaburi 146:10 Bwana atamiliki milele, Mungu wako, ee Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Bwana. Zaburi 147Kumsifu Mungu Mwenye Nguvu Zote 1 Zaburi 147:1Msifuni Bwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye! 2 Zaburi 147:2 Bwana hujenga Yerusalemu, huwakusanya Israeli walio uhamishoni. 3 Zaburi 147:3Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao. 4 Zaburi 147:4Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake. 5 Zaburi 147:5Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo. 6 Zaburi 147:6 Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini. 7 Zaburi 147:7Mwimbieni Bwana kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi. 8 Zaburi 147:8Yeye huzifunika anga kwa mawingu, huinyeshea ardhi mvua, na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima. 9 Zaburi 147:9Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia. 10 Zaburi 147:10Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu. 11 Zaburi 147:11 Bwana hupendezwa na wale wamchao, wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma. 12 Zaburi 147:12Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu, msifu Mungu wako, ee Sayuni, 13 Zaburi 147:13kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako na huwabariki watu wako walio ndani yako. 14 Zaburi 147:14Huwapa amani mipakani mwenu na kukushibisha kwa ngano safi kabisa. 15 Zaburi 147:15Hutuma amri yake duniani, neno lake hukimbia kasi. 16 Zaburi 147:16Anatandaza theluji kama sufu na kutawanya umande kama majivu. 17 Zaburi 147:17Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake? 18 Zaburi 147:18Hutuma neno lake na kuviyeyusha, huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka. 19 Zaburi 147:19Amemfunulia Yakobo neno lake, sheria zake na maagizo yake kwa Israeli. 20 Zaburi 147:20Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, hawazijui sheria zake. Msifuni Bwana. Zaburi 148Mwito Kwa Ulimwengu Kumsifu Mungu 1 Zaburi 148:1Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni. 2 Zaburi 148:2Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. 3 Zaburi 148:3Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo. 4 Zaburi 148:4Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga. 5 Zaburi 148:5Vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa. 6 Zaburi 148:6Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele. 7 Zaburi 148:7Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari, 8 Zaburi 148:8umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake, 9 Zaburi 148:9ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote, 10 Zaburi 148:10wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao, 11 Zaburi 148:11wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia, 12 Zaburi 148:12wanaume vijana na wanawali, wazee na watoto. 13 Zaburi 148:13Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu. 14 Zaburi 148:14Amewainulia watu wake pembe, 148:14 Pembe hapa inawakilisha mwenye nguvu, yaani mfalme. sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana. Zaburi 149Wimbo Wa Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake 1 Zaburi 149:1Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu. 2 Zaburi 149:2Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao. 3 Zaburi 149:3Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi. 4 Zaburi 149:4Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu. 5 Zaburi 149:5Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao. 6 Zaburi 149:6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao, 7 Zaburi 149:7ili walipize mataifa kisasi na adhabu juu ya mataifa, 8 Zaburi 149:8wawafunge wafalme wao kwa minyororo, wakuu wao kwa pingu za chuma, 9 Zaburi 149:9ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Bwana. Zaburi 150Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake 1 Zaburi 150:1Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu. 2 Zaburi 150:2Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Zaburi 150:3Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze, 4 Zaburi 150:4msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, 5 Zaburi 150:5msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Zaburi 150:6Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!