\id GEN - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version \rem Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc. \h Mwanzo \toc1 Mwanzo \toc2 Mwanzo \toc3 Mwa \mt1 Mwanzo \c 1 \s1 Siku Sita Za Uumbaji Na Sabato \pi \v 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. \v 2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji. \b \li \v 3 Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. \v 4 Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. \v 5 Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza. \li \v 6 Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” \v 7 Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo. \v 8 Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili. \li \v 9 Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo. \v 10 Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema. \pi \v 11 Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo. \v 12 Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema. \v 13 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu. \li \v 14 Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka, \v 15 nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo. \v 16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota. \v 17 Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia, \v 18 itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema. \v 19 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne. \li \v 20 Mungu akasema, “Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.” \v 21 Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. \v 22 Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.” \v 23 Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano. \li \v 24 Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo. \v 25 Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. \pi \v 26 Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.” \q1 \v 27 Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, \q2 kwa mfano wa Mungu alimuumba; \q2 mwanaume na mwanamke aliwaumba. \pi \v 28 Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.” \pi \v 29 Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu. \v 30 Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo. \pi \v 31 Mungu akaona vyote alivyoumba, na tazama, ilikuwa vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita. \b \c 2 \pi \v 1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo. \b \li \v 2 Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. \v 3 Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya. \s1 Adamu Na Eva \p \v 4 Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. \b \p \nd Bwana\nd* Mungu alipoziumba mbingu na dunia, \v 5 hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa \nd Bwana\nd* Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, \v 6 lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: \v 7 \nd Bwana\nd* Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi\f + \fr 2:7 \ft Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina Adamu.\f* ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai. \p \v 8 Basi \nd Bwana\nd* Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. \v 9 \nd Bwana\nd* Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya. \p \v 10 Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne. \v 11 Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. \v 12 (Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) \v 13 Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. \v 14 Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Frati. \p \v 15 \nd Bwana\nd* Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. \v 16 \nd Bwana\nd* Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani, \v 17 lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.” \p \v 18 \nd Bwana\nd* Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.” \p \v 19 Basi \nd Bwana\nd* Mungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. \v 20 Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini. \p Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. \v 21 Hivyo \nd Bwana\nd* Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. \v 22 Kisha \nd Bwana\nd* Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. \p \v 23 Huyo mwanaume akasema, \q1 “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu \q2 na nyama ya nyama yangu, \q1 ataitwa ‘mwanamke,’\f + \fr 2:23 \ft Jina la Kiebrania la mwanamke linafanana na lile la mwanaume.\f* \q2 kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.” \m \v 24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. \p \v 25 Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu. \c 3 \s1 Kuanguka Kwa Mwanadamu \p \v 1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao \nd Bwana\nd* Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?” \p \v 2 Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, \v 3 lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ” \p \v 4 Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. \v 5 Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” \p \v 6 Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala. \v 7 Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika. \p \v 8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya \nd Bwana\nd* Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za \nd Bwana\nd* Mungu katikati ya miti ya bustani. \v 9 Lakini \nd Bwana\nd* Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?” \p \v 10 Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.” \p \v 11 Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?” \p \v 12 Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.” \p \v 13 Ndipo \nd Bwana\nd* Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.” \p \v 14 Hivyo \nd Bwana\nd* Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili, \q1 “Umelaaniwa kuliko wanyama wote \q2 wa kufugwa na wa porini! \q1 Utatambaa kwa tumbo lako \q2 na kula mavumbi \q2 siku zote za maisha yako. \q1 \v 15 Nami nitaweka uadui \q2 kati yako na huyo mwanamke, \q2 na kati ya uzao wako na wake, \q1 yeye atakuponda kichwa, \q2 nawe utamuuma kisigino.” \p \v 16 Kwa mwanamke akasema, \q1 “Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako; \q2 kwa utungu utazaa watoto. \q1 Tamaa yako itakuwa kwa mumeo \q2 naye atakutawala.” \p \v 17 Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’ \q1 “Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako, \q2 kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo \q2 siku zote za maisha yako. \q1 \v 18 Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako, \q2 nawe utakula mimea ya shambani. \q1 \v 19 Kwa jasho la uso wako \q2 utakula chakula chako \q1 hadi utakaporudi ardhini, \q2 kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, \q1 kwa kuwa wewe u mavumbi \q2 na mavumbini wewe utarudi.” \p \v 20 Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai. \p \v 21 \nd Bwana\nd* Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. \v 22 Kisha \nd Bwana\nd* Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.” \v 23 Hivyo \nd Bwana\nd* Mungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa. \v 24 Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima. \c 4 \s1 Kaini Na Abeli \p \v 1 Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa \nd Bwana\nd* nimemzaa mwanaume.” \v 2 Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake. \p Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima. \v 3 Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa \nd Bwana\nd*. \v 4 Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. \nd Bwana\nd* akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake, \v 5 lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni. \p \v 6 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? \v 7 Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.” \p \v 8 Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua. \p \v 9 Kisha \nd Bwana\nd* akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?” \p Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” \p \v 10 \nd Bwana\nd* akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini. \v 11 Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako. \v 12 Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.” \p \v 13 Kaini akamwambia \nd Bwana\nd*, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili. \v 14 Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.” \p \v 15 Lakini \nd Bwana\nd* akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” Kisha \nd Bwana\nd* akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue. \v 16 Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za \nd Bwana\nd* akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni. \p \v 17 Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Enoki. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Enoki jina la mtoto wake. \v 18 Enoki akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki. \p \v 19 Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila. \v 20 Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama. \v 21 Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi. \v 22 Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini. \p \v 23 Lameki akawaambia wake zake, \q1 “Ada na Sila nisikilizeni mimi; \q2 wake wa Lameki sikieni maneno yangu. \q1 Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, \q2 kijana mdogo kwa kuniumiza. \q1 \v 24 Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba, \q2 basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.” \p \v 25 Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Abeli, kwa kuwa Kaini alimuua.” \v 26 Naye Sethi akamzaa mwana, akamwita Enoshi. \p Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la \nd Bwana\nd*. \c 5 \s1 Kutoka Adamu Hadi Noa \r (1 Nyakati 1:1-4) \p \v 1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. \b \p Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. \v 2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.” \p \v 3 Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi. \v 4 Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 5 Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa. \p \v 6 Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. \v 7 Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 8 Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa. \p \v 9 Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. \v 10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 11 Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa. \p \v 12 Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. \v 13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 14 Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa. \p \v 15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. \v 16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 17 Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa. \p \v 18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki. \v 19 Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 20 Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa. \p \v 21 Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. \v 22 Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 23 Enoki aliishi jumla ya miaka 365. \v 24 Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua. \p \v 25 Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki. \v 26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 27 Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa. \p \v 28 Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. \v 29 Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na \nd Bwana\nd*.” \v 30 Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. \v 31 Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa. \p \v 32 Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi. \c 6 \s1 Gharika Kuu \p \v 1 Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao, \v 2 wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua. \v 3 Ndipo \nd Bwana\nd* akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.” \p \v 4 Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo. \p \v 5 \nd Bwana\nd* akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. \v 6 \nd Bwana\nd* akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko. \v 7 Kwa hiyo \nd Bwana\nd* akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” \v 8 Lakini Noa akapata kibali machoni pa \nd Bwana\nd*. \b \p \v 9 Hivi ndivyo vizazi vya Noa. \b \p Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. \v 10 Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. \p \v 11 Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu. \v 12 Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. \v 13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia. \v 14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. \v 15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,\f + \fr 6:15 \ft Dhiraa 300 ni sawa na mita 135.\f* upana wake dhiraa hamsini\f + \fr 6:15 \ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5.\f* na kimo chake dhiraa thelathini.\f + \fr 6:15 \ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5.\f* \v 16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja\f + \fr 6:16 \ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\f* juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu. \v 17 Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia. \v 18 Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao. \v 19 Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe. \v 20 Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama na wa kila aina ya kitambaacho ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai. \v 21 Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.” \p \v 22 Noa akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru. \c 7 \p \v 1 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. \v 2 Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike. \v 3 Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote. \v 4 Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.” \p \v 5 Noa akafanya yote kama \nd Bwana\nd* alivyomwamuru. \p \v 6 Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia. \v 7 Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. \v 8 Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo, \v 9 wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa. \v 10 Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia. \p \v 11 Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa. \v 12 Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana. \p \v 13 Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina. \v 14 Nao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa. \v 15 Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Noa viwili viwili, vikaingia katika safina. \v 16 Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipo \nd Bwana\nd* akamfungia ndani. \p \v 17 Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi. \v 18 Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. \v 19 Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. \v 20 Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.\f + \fr 7:20 \ft Dhiraa 15 ni sawa na mita 7.\f* \v 21 Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote. \v 22 Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. \v 23 Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. \p \v 24 Maji yakaifunika dunia kwa siku 150. \c 8 \s1 Mwisho Wa Gharika \p \v 1 Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka. \v 2 Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani. \v 3 Maji yakaendelea kupungua taratibu katika nchi. Kunako mwisho wa siku ya 150, maji yalikuwa yamepungua, \v 4 katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati. \v 5 Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana. \p \v 6 Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina \v 7 na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi. \v 8 Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi. \v 9 Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina. \v 10 Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina. \v 11 Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia. \v 12 Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa. \p \v 13 Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka. \v 14 Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili dunia ilikuwa imekauka kabisa. \p \v 15 Ndipo Mungu akamwambia Noa, \v 16 “Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao. \v 17 Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.” \p \v 18 Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao. \v 19 Wanyama wote na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi na ndege wote, kila kitu kiendacho juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina, kila aina ya kiumbe, kimoja baada ya kingine. \s1 Noa Atoa Dhabihu \p \v 20 Kisha Noa akamjengea \nd Bwana\nd* madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. \v 21 \nd Bwana\nd* akasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawa kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya. \q1 \v 22 “Kwa muda dunia idumupo, \q1 wakati wa kupanda na wa kuvuna, \q1 wakati wa baridi na wa joto, \q1 wakati wa kiangazi na wa masika, \q1 usiku na mchana \q1 kamwe havitakoma.” \c 9 \s1 Mungu Aweka Agano Na Noa \p \v 1 Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia. \v 2 Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. \v 3 Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu. \p \v 4 “Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai. \v 5 Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake. \q1 \v 6 “Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu, \q2 damu yake itamwagwa na mwanadamu, \q1 kwa kuwa katika mfano wa Mungu, \q2 Mungu alimuumba mwanadamu. \m \v 7 Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.” \p \v 8 Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye: \v 9 “Sasa mimi ninaweka Agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu, \v 10 pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani. \v 11 Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.” \p \v 12 Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo: \v 13 Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia. \v 14 Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukijitokeza mawinguni, \v 15 nitakumbuka Agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote. \v 16 Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.” \p \v 17 Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.” \s1 Wana Wa Noa \p \v 18 Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) \v 19 Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia. \p \v 20 Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. \v 21 Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. \v 22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. \v 23 Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao. \p \v 24 Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea, \v 25 akasema, \q1 “Alaaniwe Kanaani! \q2 Atakuwa mtumwa wa chini sana \q2 kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.” \p \v 26 Pia akasema, \q1 “Abarikiwe \nd Bwana\nd*, Mungu wa Shemu! \q2 Kanaani na awe mtumwa wa Shemu. \q1 \v 27 Mungu na apanue mipaka ya Yafethi; \q2 Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu, \q2 na Kanaani na awe mtumwa wake.” \p \v 28 Baada ya gharika Noa aliishi miaka 350. \v 29 Noa alikuwa na jumla ya miaka 950, ndipo akafa. \c 10 \s1 Mataifa Yaliyotokana Na Noa \r (1 Nyakati 1:5-23) \p \v 1 Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika. \s2 Wazao Wa Yafethi \li1 \v 2 Wana wa Yafethi walikuwa: \li2 Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. \li1 \v 3 Wana wa Gomeri walikuwa: \li2 Ashkenazi, Rifathi na Togarma. \li1 \v 4 Wana wa Yavani walikuwa: \li2 Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. \v 5 (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.) \s2 Wazao Wa Hamu \li1 \v 6 Wana wa Hamu walikuwa: \li2 Kushi, Misraimu,\f + \fr 10:6 \ft Yaani \fqa Misri\ft .\f* Putu na Kanaani. \li1 \v 7 Wana wa Kushi walikuwa: \li2 Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. \li1 Wana wa Raama walikuwa: \li2 Sheba na Dedani. \b \p \v 8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. \v 9 Alikuwa mwindaji hodari mbele za \nd Bwana\nd*. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za \nd Bwana\nd*.” \v 10 Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. \v 11 Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, \v 12 na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa. \b \li1 \v 13 Misraimu alikuwa baba wa: \li2 Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, \v 14 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori. \li1 \v 15 Kanaani alikuwa baba wa: \li2 Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, \v 16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, \v 17 Wahivi, Waariki, Wasini, \v 18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. \b \p Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, \v 19 na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha. \p \v 20 Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao. \s2 Wazao Wa Shemu \p \v 21 Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi. \b \li1 \v 22 Wana wa Shemu walikuwa: \li2 Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. \li1 \v 23 Wana wa Aramu walikuwa: \li2 Usi, Huli, Getheri na Mesheki. \li1 \v 24 Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, \li2 naye Shela akamzaa Eberi. \li1 \v 25 Eberi akapata wana wawili: \li2 Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. \li1 \v 26 Yoktani alikuwa baba wa: \li2 Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, \v 27 Hadoramu, Uzali, Dikla, \v 28 Obali, Abimaeli, Sheba, \v 29 Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani. \b \m \v 30 Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki. \p \v 31 Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao. \b \p \v 32 Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika. \c 11 \s1 Mnara Wa Babeli \p \v 1 Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. \v 2 Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari\f + \fr 11:2 \ft Shinari ndio Babeli.\f* nao wakaishi huko. \p \v 3 Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. \v 4 Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.” \p \v 5 Lakini \nd Bwana\nd* akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga. \v 6 \nd Bwana\nd* akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. \v 7 Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.” \p \v 8 Hivyo \nd Bwana\nd* akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. \v 9 Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo \nd Bwana\nd* alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo \nd Bwana\nd* akawatawanya katika uso wa dunia yote. \s1 Shemu Hadi Abramu \r (1 Nyakati 1:24-27) \p \v 10 Hivi ndivyo vizazi vya Shemu. \b \p Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi. \v 11 Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 12 Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela. \v 13 Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 14 Shela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi. \v 15 Shela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 16 Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. \v 17 Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 18 Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu. \v 19 Baada ya Pelegi kumzaa Reu, aliishi miaka 209, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 20 Reu alipokuwa na miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. \v 21 Baada ya Reu kumzaa Serugi, aliishi miaka 207, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 22 Serugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori. \v 23 Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 24 Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. \v 25 Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike. \p \v 26 Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani. \s1 Wazao Wa Tera \p \v 27 Hawa ndio wazao wa Tera. \b \p Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. \v 28 Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa. \v 29 Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. \v 30 Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto. \p \v 31 Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko. \p \v 32 Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205. \c 12 \s1 Wito Wa Abramu \p \v 1 \nd Bwana\nd* akawa amemwambia Abramu, “Ondoka kutoka nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha. \q1 \v 2 “Mimi nitakufanya taifa kubwa \q2 na nitakubariki, \q1 Nitalikuza jina lako, \q2 nawe utakuwa baraka. \q1 \v 3 Nitawabariki wale wanaokubariki, \q2 na yeyote akulaaniye nitamlaani; \q1 na kupitia kwako mataifa yote duniani \q2 yatabarikiwa.” \p \v 4 Hivyo Abramu akaondoka kama \nd Bwana\nd* alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano. \v 5 Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko. \p \v 6 Abramu akasafiri katika nchi hiyo akafika huko Shekemu, mahali penye mti wa mwaloni ulioko More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo. \v 7 \nd Bwana\nd* akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa akamjengea madhabahu \nd Bwana\nd* aliyekuwa amemtokea. \p \v 8 Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea \nd Bwana\nd* madhabahu na akaliitia jina la \nd Bwana\nd*. \v 9 Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu. \s1 Abramu Katika Nchi Ya Misri \p \v 10 Basi kulikuwako na njaa katika nchi, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali. \v 11 Alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. \v 12 Wakati Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Ndipo wataniua, lakini wewe watakuacha hai. \v 13 Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako.” \p \v 14 Abramu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana wa sura. \v 15 Maafisa wa Farao walipomwona, wakamsifia kwa Farao; ndipo Sarai akapelekwa kwa nyumba ya mfalme. \v 16 Kwa ajili ya Sarai, Farao akamtendea Abramu mema, naye Abramu akapata kondoo, ngʼombe, punda, ngamia na watumishi wa kiume na wa kike. \p \v 17 Lakini \nd Bwana\nd* akamwadhibu Farao na nyumba yake kwa maradhi ya kufisha kwa sababu ya kumchukua Sarai, mke wa Abramu. \v 18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akamuuliza, “Umenifanyia nini? Kwa nini hukuniambia ni mke wako? \v 19 Kwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu,’ hata nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa basi, mke wako huyu hapa. Mchukue uende zako!” \v 20 Kisha Farao akawapa watu wake amri kuhusu Abramu, wakamsindikiza pamoja na mke wake na kila alichokuwa nacho. \c 13 \s1 Abramu Na Loti Watengana \p \v 1 Hivyo Abramu akakwea kutoka Misri kwenda Negebu, yeye na mkewe na kila kitu alichokuwa nacho, pia Loti akaenda pamoja naye. \v 2 Wakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu. \p \v 3 Kutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai \v 4 hapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la \nd Bwana\nd*. \p \v 5 Basi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ngʼombe na mahema. \v 6 Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao. \v 7 Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Loti. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo. \p \v 8 Hivyo Abramu akamwambia Loti, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu. \v 9 Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.” \p \v 10 Loti akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya \nd Bwana\nd*, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla \nd Bwana\nd* hajaharibu Sodoma na Gomora.) \v 11 Hivyo Loti akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana: \v 12 Abramu akaishi katika nchi ya Kanaani, wakati Loti aliishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma. \v 13 Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya \nd Bwana\nd*. \p \v 14 Baada ya Loti kuondoka \nd Bwana\nd* akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. \v 15 Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. \v 16 Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. \v 17 Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.” \p \v 18 Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea \nd Bwana\nd* madhabahu. \c 14 \s1 Abramu Amwokoa Loti \p \v 1 Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu \v 2 kwa pamoja walikwenda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari). \v 3 Hawa wote waliotajwa mwishoni waliunganisha majeshi yao kutoka Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi). \v 4 Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na miwili, lakini mwaka wa kumi na tatu waliasi. \p \v 5 Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu, \v 6 na Wahori katika nchi ya kilima cha Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa. \v 7 Kisha wakarudi wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori waliokuwa wakiishi Hasason-Tamari. \p \v 8 Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu \v 9 dhidi ya Kedorlaoma, mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano. \v 10 Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani. \v 11 Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao. \v 12 Pia walimteka Loti mwana wa ndugu yake Abramu pamoja na mali zake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma. \p \v 13 Mtu mmoja aliyekuwa ametoroka akaja kumpa Abramu Mwebrania taarifa. Wakati huu Abramu alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mamre Mwamori, aliyekuwa ndugu yake Eshkoli na Aneri, ambao wote walikuwa wameungana na Abramu. \v 14 Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu 318 wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani. \v 15 Wakati wa usiku Abramu aliwagawa watu wake katika vikosi ili awashambulie, na akawafuatilia, akawafukuza hadi Hoba, kaskazini ya Dameski. \v 16 Akarudisha mali zote, na akamrudisha Loti jamaa yake na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine. \p \v 17 Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme). \p \v 18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. \v 19 Naye akambariki Abramu, akisema, \q1 “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, \q2 Muumba wa mbingu na nchi. \q1 \v 20 Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana, \q2 ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.” \m Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu. \p \v 21 Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe.” \p \v 22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa \nd Bwana\nd*, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa \v 23 kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’ \v 24 Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula na sehemu ambayo ni fungu la watu waliokwenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.” \c 15 \s1 Agano La Mungu Na Abramu \p \v 1 Baada ya jambo hili, neno la \nd Bwana\nd* likamjia Abramu katika maono: \q1 “Usiogope, Abramu. \q2 Mimi ni ngao yako, \q2 na thawabu yako kubwa sana.” \p \v 2 Lakini Abramu akasema, “Ee \nd Bwana\nd* Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” \v 3 Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.” \p \v 4 Ndipo neno la \nd Bwana\nd* lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.” \v 5 Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.” \p \v 6 Abramu akamwamini \nd Bwana\nd*, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki. \p \v 7 Pia akamwambia, “Mimi ndimi \nd Bwana\nd*, niliyekutoa toka Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.” \p \v 8 Lakini Abramu akasema, “Ee \nd Bwana\nd* Mwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitapata kuimiliki?” \p \v 9 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia, “Niletee mtamba wa ngʼombe, mbuzi na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.” \p \v 10 Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili. \v 11 Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza. \p \v 12 Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake. \v 13 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. \v 14 Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi. \v 15 Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema. \v 16 Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.” \p \v 17 Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama. \v 18 Siku hiyo \nd Bwana\nd* akafanya Agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri\f + \fr 15:18 \fq Kijito cha Misri \ft hapa ina maana \fqa Wadi-el-Arish \ft kwenye mpaka wa kusini wa Yuda.\f* hadi mto ule mkubwa, Frati, \v 19 yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, \v 20 Wahiti, Waperizi, Warefai, \v 21 Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.” \c 16 \s1 Hagari Na Ishmaeli \p \v 1 Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mtumishi wa kike Mmisri jina lake Hagari, \v 2 hivyo Sarai akamwambia Abramu, “\nd Bwana\nd* amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” \p Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema. \v 3 Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake. \v 4 Akakutana kimwili na Hagari, naye akapata mimba. \p Hagari alipojua kuwa ana mimba, alianza kumdharau Sarai. \v 5 Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. \nd Bwana\nd* na aamue kati yako na mimi.” \p \v 6 Abramu akamwambia, “Mtumishi wako yuko mikononi mwako. Mtendee lolote unalofikiri ni bora zaidi.” Ndipo Sarai akamtesa Hagari, hivyo akamtoroka. \p \v 7 Malaika wa \nd Bwana\nd* akamkuta Hagari karibu na chemchemi huko jangwani; ilikuwa chemchemi ile iliyokuwa kando ya barabara iendayo Shuri. \v 8 Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi?” \p Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.” \p \v 9 Ndipo malaika wa \nd Bwana\nd* akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” \v 10 Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.” \p \v 11 Pia malaika wa \nd Bwana\nd* akamwambia: \q1 “Wewe sasa una mimba \q2 nawe utamzaa mwana. \q1 Utamwita jina lake Ishmaeli,\f + \fr 16:11 \ft Ishmaeli maana yake Mungu husikia.\f* \q2 kwa sababu \nd Bwana\nd* amesikia juu ya huzuni yako. \q1 \v 12 Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu, \q2 mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu \q2 na mkono wa kila mtu dhidi yake, \q1 naye ataishi kwa uhasama \q2 na ndugu zake wote.” \p \v 13 Hagari akampa \nd Bwana\nd* aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.” \v 14 Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi,\f + \fr 16:14 \ft Beer-Lahai-Roi maana yake Yeye Aliye Hai Anionaye Mimi.\f* ambacho bado kipo huko hata leo kati ya Kadeshi na Beredi. \p \v 15 Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli. \v 16 Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hagari alipomzalia Ishmaeli. \c 17 \s1 Agano La Tohara \p \v 1 Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, \nd Bwana\nd* akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi;\f + \fr 17:1 \ft Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\f* enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu. \v 2 Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.” \p \v 3 Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, \v 4 “Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. \v 5 Jina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Abrahamu,\f + \fr 17:5 \ft Abrahamu maana yake Baba wa watu wengi.\f* kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi. \v 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako. \v 7 Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako. \v 8 Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.” \p \v 9 Ndipo Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, lazima ushike Agano langu, wewe na wazao wako kwa ajili ya vizazi vijavyo. \v 10 Hili ni Agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, Agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. \v 11 Mtafanyiwa tohara na hii itakuwa ni alama ya Agano kati yangu na ninyi. \v 12 Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako. \v 13 Awe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima watahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni Agano la milele. \v 14 Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake, amelivunja Agano langu.” \p \v 15 Pia \nd Bwana\nd* akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai bali jina lake litakuwa Sara. \v 16 Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.” \p \v 17 Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” \v 18 Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!” \p \v 19 Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki.\f + \fr 17:19 \ft Isaki maana yake Kucheka.\f* Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. \v 20 Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. \v 21 Lakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” \v 22 Wakati alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Abrahamu. \p \v 23 Siku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. \v 24 Abrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa, \v 25 naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu. \v 26 Abrahamu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku ile ile, \v 27 Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye. \c 18 \s1 Wageni Watatu \p \v 1 \nd Bwana\nd* akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. \v 2 Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi. \p \v 3 Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. \v 4 Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. \v 5 Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.” \p Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.” \p \v 6 Hivyo Abrahamu akaharakisha akaingia hemani kwa Sara, akamwambia, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.” \p \v 7 Kisha Abrahamu akakimbia kwenda kwenye kundi, akachagua ndama mzuri, laini na akampa mtumishi, ambaye aliharakisha kumtayarisha. \v 8 Kisha akaleta jibini, maziwa na nyama ya yule ndama iliyoandaliwa, akaviweka mbele ya wageni. Walipokuwa wakila, alisimama karibu nao chini ya mti. \p \v 9 Wakamuuliza, “Yuko wapi Sara mkeo?” \p Akasema, “Yuko huko, ndani ya hema.” \p \v 10 Kisha \nd Bwana\nd* akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.” \p Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake. \v 11 Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. \v 12 Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?” \p \v 13 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’ \v 14 Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa \nd Bwana\nd*? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.” \p \v 15 Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.” \p Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!” \s1 Abrahamu Aiombea Sodoma \p \v 16 Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Abrahamu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize. \v 17 Ndipo \nd Bwana\nd* akasema, “Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia kufanya? \v 18 Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa. \v 19 Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya \nd Bwana\nd*, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili \nd Bwana\nd* atimize ahadi yake kwa Abrahamu.” \p \v 20 Basi \nd Bwana\nd* akasema, “Kilio dhidi ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na dhambi yao inasikitisha sana, \v 21 kwamba nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo, nitajua.” \p \v 22 Basi wale watu wakageuka wakaenda kuelekea Sodoma, lakini Abrahamu akabaki amesimama mbele za \nd Bwana\nd*. \v 23 Ndipo Abrahamu akamsogelea akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu? \v 24 Je, ikiwa watakuwepo watu wenye haki hamsini katika mji huo, hivi kweli utauangamiza na wala hutauacha kwa ajili ya hao watu hamsini wenye haki waliomo ndani yake? \v 25 Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?” \p \v 26 \nd Bwana\nd* akasema, “Kama nikipata watu hamsini wenye haki katika mji wa Sodoma, nitausamehe huo mji wote kwa ajili yao.” \p \v 27 Kisha Abrahamu akasema tena: “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu; \v 28 je, kama hesabu ya wenye haki imepungua watano katika hamsini, utauangamiza huo mji wote kwa ajili ya hao watano waliopungua?” \p Bwana akamwambia, “Kama nikiwakuta huko watu arobaini na watano, sitauangamiza.” \p \v 29 Abrahamu akazungumza naye kwa mara nyingine, “Je, kama huko watapatikana watu arobaini tu?” \p Akamjibu, “Kwa ajili ya hao arobaini, sitauangamiza.” \p \v 30 Ndipo akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze. Je, kama huko watakuwepo thelathini tu?” \p Akajibu, “Sitapaangamiza ikiwa nitawakuta huko watu thelathini.” \p \v 31 Abrahamu akasema, “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri sana kuzungumza na Bwana, je, kama wakipatikana huko watu ishirini tu?” \p Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao ishirini, sitauangamiza.” \p \v 32 Abrahamu akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze tena mara moja tu. Itakuwaje kama watapatikana huko watu kumi tu?” \p Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao kumi, sitauangamiza.” \p \v 33 \nd Bwana\nd* alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, akaondoka, naye Abrahamu akarudi nyumbani kwake. \c 19 \s1 Kuangamizwa Kwa Sodoma Na Gomora \p \v 1 Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Loti alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini. \v 2 Akasema, “Bwana zangu, tafadhali karibuni kwenye nyumba ya mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala hapa kisha asubuhi na mapema mwendelee na safari yenu.” \p Wakamjibu, “La hasha, tutalala hapa nje uwanjani.” \p \v 3 Lakini akasisitiza kwa nguvu kwamba waingie pamoja naye nyumbani kwake. Akawaandalia chakula, mikate isiyotiwa chachu, nao wakala. \v 4 Kabla hawajaenda kulala, watu wote kutoka kila sehemu ya mji wa Sodoma, vijana kwa wazee, waliizunguka nyumba. \v 5 Wakamwita Loti wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.” \p \v 6 Loti akatoka nje kuonana nao, akaufunga mlango nyuma yake, \v 7 akasema, “La hasha, rafiki zangu. Msifanye jambo hili ovu. \v 8 Tazama, ninao binti wawili ambao kamwe hawajakutana kimwili na mwanaume. Acha niwatoe nje kwenu, nanyi mnaweza kuwafanyia lolote mnalotaka. Lakini msiwafanyie chochote watu hawa, kwa sababu wako kwenye ulinzi chini ya dari langu.” \p \v 9 Wakamjibu, “Tuondokee mbali.” Wakaendelea kusema, “Huyu mtu alikuja hapa kama mgeni na sasa anataka kuwa mwamuzi wetu! Tutakutenda vibaya kuliko wao.” Waliendelea kumlazimisha Loti na kusonga mbele ili kuvunja mlango. \p \v 10 Lakini watu wale waliokuwa ndani wakanyoosha mkono wakamvuta Loti ndani ya nyumba na kufunga mlango. \v 11 Kisha wakawapiga kwa upofu wale watu waliokuwa mlangoni mwa ile nyumba, vijana kwa wazee, hivyo hawakuweza kuupata mlango. \p \v 12 Wale watu wawili wakamwambia Loti, “Una mtu mwingine yeyote hapa, wakwe zako, wana au binti, ama yeyote mwingine aliye wako katika mji huu? Waondoe hapa, \v 13 kwa sababu tunapaangamiza mahali hapa. Kilio kwa \nd Bwana\nd* dhidi ya watu wa hapa ni kikubwa kiasi kwamba ametutuma kupaangamiza.” \p \v 14 Kwa hiyo Loti alitoka ili kuzungumza na wakwe zake, waliokuwa wamewaposa binti zake. Akawaambia, “Fanyeni haraka kuondoka mahali hapa, kwa kuwa \nd Bwana\nd* yu karibu kuangamiza mji huu!” Lakini wakwe zake walifikiri kwamba alikuwa akitania. \p \v 15 Kunako mapambazuko, malaika wakamhimiza Loti, wakamwambia, “Fanya haraka! Mchukue mke wako na binti zako wawili walioko hapa, la sivyo utaangamizwa wakati mji utakapoadhibiwa.” \p \v 16 Alipositasita, wale watu wakamshika mkono wake na mikono ya mke wake na binti zake wawili na kuwaongoza salama nje ya mji, kwa kuwa \nd Bwana\nd* alikuwa na huruma kwao. \v 17 Mara walipokwisha kuwatoa nje, mmoja wao akawaambia, “Mkimbie kwa usalama wenu! Msitazame nyuma, wala msisimame popote katika nchi tambarare! Kimbilieni milimani, ama sivyo mtaangamizwa!” \p \v 18 Lakini Loti akawajibu, “La hasha, bwana zangu, tafadhalini! \v 19 Mtumishi wenu amepata kibali mbele ya macho yenu, nanyi mmeonyesha wema mkubwa kwangu kwa kuokoa maisha yangu. Lakini siwezi kukimbilia milimani, janga hili litanikumba, nami nitakufa. \v 20 Tazama, hapa kuna mji karibu wa kukimbilia, nao ni mdogo. Niruhusuni nikimbilie humo, ni mdogo sana, ama sivyo? Ndipo maisha yangu yatasalimika.” \p \v 21 Akamwambia, “Vema sana, nitalikubali hili ombi pia, sitauangamiza mji ulioutaja. \v 22 Lakini ukimbilie huko haraka, kwa sababu sitaweza kufanya lolote mpaka ufike huko.” (Ndiyo maana mji huo ukaitwa Soari.\f + \fr 19:22 \ft Soari maana yake Mdogo.\f*) \p \v 23 Wakati Loti alipofika Soari, jua lilikuwa limechomoza katika nchi. \v 24 Ndipo \nd Bwana\nd* akanyesha moto wa kiberiti uliotoka mbinguni kwa \nd Bwana\nd* juu ya Sodoma na Gomora. \v 25 Hivyo akaiteketeza miji ile na eneo lote la tambarare, pamoja na wote waliokuwa wanaishi katika miji, hata pia mimea yote katika nchi. \v 26 Lakini mke wa Loti akatazama nyuma, hivyo akawa nguzo ya chumvi. \p \v 27 Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Abrahamu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele za \nd Bwana\nd*. \v 28 Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka kwenye nchi, kama moshi utokao kwenye tanuru. \p \v 29 Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare alimkumbuka Abrahamu, akamtoa Loti kutoka kwenye lile janga lililoharibu miji ile ambamo Loti alikuwa ameishi. \s1 Loti Na Binti Zake \p \v 30 Loti na binti zake wawili waliondoka Soari na kufanya makao yao kule milimani, kwa maana aliogopa kukaa Soari. Yeye na binti zake wawili waliishi katika pango. \v 31 Siku moja binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee na hakuna mwanaume mahali hapa atakayekutana na sisi kimwili, kama ilivyo desturi ya mahali pote duniani. \v 32 Tumnyweshe baba yetu mvinyo kisha tukutane naye kimwili ili tuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” \p \v 33 Usiku ule walimnywesha baba yao mvinyo, alipolewa binti yake mkubwa akaingia na kukutana naye kimwili. Baba yao hakujua wakati binti yake alipoingia kulala naye wala alipotoka. \p \v 34 Siku iliyofuata binti mkubwa akamwambia yule mdogo, “Usiku uliopita mimi nilikutana kimwili na baba yangu. Tumnyweshe divai tena, usiku huu nawe ukutane naye kimwili ili tuweze kuhifadhi uzao wetu kupitia baba yetu.” \v 35 Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo tena usiku ule, naye binti yake mdogo akaingia, akakutana naye kimwili. Kwa mara nyingine baba yao hakujua binti yake alipolala naye wala alipoondoka. \p \v 36 Hivyo binti wawili wa Loti wakapata mimba kwa baba yao. \v 37 Binti mkubwa akamzaa mwana, akamwita jina lake Moabu; ndio baba wa Wamoabu hata leo. \v 38 Binti mdogo naye pia akamzaa mwana, naye akamwita Benami; ndiye baba wa Waamoni hata leo. \c 20 \s1 Abrahamu Na Abimeleki \p \v 1 Basi Abrahamu akaendelea mbele kutoka huko hadi nchi ya Negebu na akaishi kati ya Kadeshi na Shuri. Kwa muda mfupi alikaa Gerari kama mgeni, \v 2 huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua. \p \v 3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto wakati wa usiku na kumwambia, “Wewe ni kama mfu kwa sababu ya huyu mwanamke uliyemchukua; yeye ni mke wa mtu.” \p \v 4 Wakati huo Abimeleki alikuwa bado hajamsogelea, kwa hiyo akasema, “Je, Bwana utaliharibu taifa lisilo na hatia? \v 5 Hakusema kwangu, ‘Huyu ni dada yangu,’ naye Sara pia hakusema, ‘Huyu ni kaka yangu’? Nimefanya haya kwa dhamiri njema na mikono safi.” \p \v 6 Kisha Mungu akamwambia katika ndoto, “Ndiyo, najua ya kwamba umefanya haya kwa dhamiri safi, kwa hiyo nimekuzuia usinitende dhambi. Ndiyo sababu sikukuacha umguse. \v 7 Sasa umrudishe huyo mke wa mtu, kwa maana ni nabii, naye atakuombea nawe utaishi. Lakini kama hutamrudisha, ujue kwa hakika kuwa wewe na watu wako wote mtakufa.” \p \v 8 Kesho yake asubuhi na mapema Abimeleki akawaita maafisa wake wote, na baada ya kuwaambia yote yaliyotokea, waliogopa sana. \v 9 Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu na kumwambia, “Wewe umetufanyia nini? Nimekukosea nini hata ukaleta hatia kubwa namna hii juu yangu na ufalme wangu? Umenifanyia mambo ambayo hayakupasa kufanyika.” \v 10 Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ulikuwa na kusudi gani kufanya hivi?” \p \v 11 Abrahamu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’ \v 12 Pamoja na hayo, ni kweli kwamba yeye ni dada yangu, binti wa baba yangu ingawa si mtoto wa mama yangu; basi akawa mke wangu. \v 13 Wakati \nd Bwana\nd* aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ” \p \v 14 Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ngʼombe, na watumwa wa kiume na wa kike akampa Abrahamu, akamrudisha Sara kwa mumewe. \v 15 Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako, ishi popote unapotaka.” \p \v 16 Akamwambia Sara, “Ninampa kaka yako shekeli elfu moja za fedha. Hii ni kufidia kosa lililofanyika dhidi yako mbele ya wote walio pamoja nawe; haki yako imethibitishwa kabisa.” \p \v 17 Kisha Abrahamu akamwomba Mungu, naye Mungu akamponya Abimeleki, mke wake, na watumwa wake wa kike kwamba waweze kupata watoto tena, \v 18 kwa kuwa \nd Bwana\nd* alikuwa ameyafunga matumbo ya wote katika nyumba ya Abimeleki kwa sababu ya Sara, mke wa Abrahamu. \c 21 \s1 Kuzaliwa Kwa Isaki \p \v 1 Wakati huu \nd Bwana\nd* akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye \nd Bwana\nd* akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. \v 2 Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. \v 3 Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. \v 4 Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. \v 5 Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa. \p \v 6 Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” \v 7 Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake.” \s1 Hagari Na Ishmaeli Wafukuzwa \p \v 8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya. Siku hiyo Isaki alipoachishwa kunyonya, Abrahamu alifanya sherehe kubwa. \v 9 Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hagari, Mmisri, aliyemzalia Abrahamu alikuwa anadhihaki, \v 10 Sara akamwambia Abrahamu, “Mwondoe mwanamke huyo mtumwa pamoja na mwanawe, kwa kuwa mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwanangu Isaki.” \p \v 11 Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe. \v 12 Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki. \v 13 Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.” \p \v 14 Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba. \p \v 15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka. \v 16 Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni. \p \v 17 Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale. \v 18 Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.” \p \v 19 Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe. \p \v 20 Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde. \v 21 Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri. \s1 Mapatano Katika Beer-Sheba \p \v 22 Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. \v 23 Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.” \p \v 24 Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.” \p \v 25 Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya. \v 26 Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.” \p \v 27 Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ngʼombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. \v 28 Abrahamu akatenga kondoo wa kike saba kutoka kwenye kundi, \v 29 Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?” \p \v 30 Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.” \p \v 31 Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo. \p \v 32 Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti. \v 33 Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la \nd Bwana\nd*, Mungu wa milele. \v 34 Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu. \c 22 \s1 Kujua Uthabiti Wa Abrahamu \p \v 1 Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” \p Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 2 Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.” \p \v 3 Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia. \v 4 Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali. \v 5 Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunakwenda kule. Tutakwenda kuabudu na kisha tutawarudia.” \p \v 6 Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, \v 7 Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!” \p Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.” \p Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?” \p \v 8 Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja. \p \v 9 Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. \v 10 Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. \v 11 Lakini malaika wa \nd Bwana\nd* akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!” \p Akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 12 Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.” \p \v 13 Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. \v 14 Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.\f + \fr 22:14 \ft Yehova-Yire maana yake \+nd Bwana\+nd* atatupa.\f* Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa \nd Bwana\nd* itapatikana.” \p \v 15 Basi malaika wa \nd Bwana\nd* akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, \v 16 akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema \nd Bwana\nd*, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee, \v 17 hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, \v 18 na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.” \p \v 19 Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba. \s1 Wana Wa Nahori \p \v 20 Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana: \v 21 Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu), \v 22 Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” \v 23 Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane. \v 24 Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka. \c 23 \s1 Kifo Cha Sara \p \v 1 Sara aliishi akawa na umri wa miaka mia na ishirini na saba. \v 2 Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, Abrahamu akamwombolezea na kumlilia Sara. \p \v 3 Ndipo Abrahamu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema, \v 4 “Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. Niuzieni sehemu ya ardhi yenu ili niweze kumzika maiti wangu.” \p \v 5 Wahiti wakamjibu Abrahamu, \v 6 “Bwana, tusikilize. Wewe ni mtawala mkuu sana miongoni mwetu. Zika maiti wako katika kaburi unalolipenda kati ya makaburi yetu. Hakuna mtu wa kwetu atakayekuzuia kaburi lake ili kuzika maiti wako.” \p \v 7 Abrahamu akainuka na akasujudu mbele ya wenyeji wa nchi, yaani Wahiti. \v 8 Akawaambia, “Kama mnaniruhusu kumzika maiti wangu, basi nisikilizeni mkamsihi Efroni mwana wa Sohari kwa niaba yangu \v 9 ili aniuzie pango la Makpela, lililo mali yake, nalo liko mwisho wa shamba lake. Mwambieni aniuzie kwa bei kamili atakayosema ili liwe mahali pangu pa kuzikia miongoni mwenu.” \p \v 10 Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake, akamjibu Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokuwepo katika lango la mji. \v 11 “La hasha, bwana wangu, nisikilize, nakupa shamba, pia nakupa pango lililomo ndani yake. Nakupa mbele ya watu wangu. Uzike maiti wako.” \p \v 12 Abrahamu akasujudu tena, mbele ya wenyeji wa nchi, \v 13 akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.” \p \v 14 Efroni akamjibu Abrahamu, \v 15 “Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli 400 za fedha,\f + \fr 23:15 \ft Shekeli 400 za fedha ni sawa na kilo 4.5.\f* lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.” \p \v 16 Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara. \p \v 17 Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwamo ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa, \v 18 kwa Abrahamu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji. \v 19 Baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe kwenye pango ndani ya shamba la Makpela karibu na Mamre (huko Hebroni) katika nchi ya Kanaani. \v 20 Hivyo Wahiti wakamkabidhi Abrahamu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia. \c 24 \s1 Isaki Na Rebeka \p \v 1 Wakati huu Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, naye \nd Bwana\nd* alikuwa amembariki katika kila njia. \v 2 Akamwambia mtumishi wake mkuu wa vitu vyote katika nyumba yake, yule aliyekuwa msimamizi wa vitu vyote alivyokuwa navyo, “Weka mkono wako chini ya paja langu, \v 3 Ninataka uape kwa \nd Bwana\nd*, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke kutoka binti za Wakanaani, ambao ninaishi miongoni mwao, \v 4 bali utakwenda katika nchi yangu na jamaa zangu umpatie Isaki mwanangu mke.” \p \v 5 Yule mtumishi akamuuliza, “Je, kama huyo mwanamke atakataa kuja nami katika nchi hii? Je, nimpeleke mwanao katika hiyo nchi uliyotoka?” \p \v 6 Abrahamu akasema, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu huko. \v 7 \nd Bwana\nd*, Mungu wa mbingu, aliyenitoa nyumbani kwa baba yangu na nchi yangu niliyozaliwa na aliyesema nami na akaniahidi kwa kiapo, akisema, ‘Nitawapa watoto wako nchi hii,’ atatuma malaika wake akutangulie ili umpatie mwanangu mke kutoka huko. \v 8 Kama huyo mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi utafunguliwa kutoka kiapo nilichokuapisha. Ila usimrudishe mwanangu huko.” \v 9 Basi yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la bwana wake Abrahamu akamwapia kuhusu shauri hili. \p \v 10 Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimu\f + \fr 24:10 \ft Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi.\f* na kushika njia kwenda mji wa Nahori. \v 11 Akawapigisha ngamia magoti karibu na kisima cha maji nje ya mji, ilikuwa inaelekea jioni, wakati ambapo wanawake wanakuja kuteka maji. \p \v 12 Kisha akaomba, “Ee \nd Bwana\nd*, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nipatie ushindi leo, uonyeshe huruma kwa bwana wangu Abrahamu. \v 13 Tazama, nimesimama karibu na kisima hiki cha maji, nao binti za watu wa mji huu wanakuja kuteka maji. \v 14 Basi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmojawapo, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji,’ naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia.’ Basi na awe ndiye uliyemchagua kwa ajili ya mtumishi wako Isaki. Kwa hili nitajua umemhurumia bwana wangu.” \p \v 15 Ikawa kabla hajamaliza kuomba, Rebeka akatokea akiwa na mtungi begani mwake. Alikuwa binti wa Bethueli. Bethueli alikuwa mwana wa Milka aliyekuwa mke wa Nahori ndugu wa Abrahamu. \v 16 Huyu msichana alikuwa mzuri sana wa sura, bikira, ambaye hakuna mtu aliyekuwa amekutana naye kimwili. Aliteremka kisimani, akajaza mtungi wake akapanda juu. \p \v 17 Ndipo yule mtumishi akaharakisha kukutana naye akamwambia, “Tafadhali nipe maji kidogo katika mtungi wako.” \p \v 18 Yule msichana akasema, “Kunywa, bwana wangu.” Akashusha kwa haraka mtungi mkononi mwake na akampa, akanywa. \p \v 19 Baada ya kumpa yule mtumishi yale maji, akamwambia, “Nitateka maji kwa ajili ya ngamia zako pia mpaka wote watosheke.” \v 20 Akafanya haraka kumimina maji kwenye birika ya kunyweshea wanyama, akakimbia kisimani kuteka maji mengine na akateka ya kuwatosha ngamia wake wote. \v 21 Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kama \nd Bwana\nd* ameifanikisha safari yake, au la. \p \v 22 Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka moja\f + \fr 24:22 \ft Beka moja ya dhahabu ni sawa na gramu 5.5.\f* na bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.\f + \fr 24:22 \ft Shekeli 10 za dhahabu ni sawa na gramu 110.\f* \v 23 Kisha akamuuliza, “Wewe ni binti wa nani? Tafadhali uniambie, je, kuna nafasi katika nyumba ya baba yako tutakapoweza kulala?” \p \v 24 Yule msichana akamjibu, “Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Milka aliyemzalia Nahori.” \v 25 Akaendelea kusema, “Kwetu kuna majani mengi na malisho, tena kuna nafasi kwa ajili yenu kulala.” \p \v 26 Yule mtumishi akasujudu na kumwabudu \nd Bwana\nd*, \v 27 akisema, “Atukuzwe \nd Bwana\nd*, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuondoa wema na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mimi nami, \nd Bwana\nd* ameniongoza safarini akanifikisha nyumbani kwa jamaa za bwana wangu.” \p \v 28 Yule msichana akakimbia akawaeleza watu wa nyumbani mwa mama yake kuhusu mambo haya. \v 29 Rebeka alikuwa na kaka aliyeitwa Labani, huyo akaharakisha kukutana na yule mtumishi kule kisimani. \v 30 Mara alipoiona ile pete puani, na bangili mikononi mwa dada yake na kusikia yale maneno Rebeka aliyoambiwa na huyo mtumishi, alimwendea huyo mtumishi, akamkuta amesimama karibu na ngamia wake pale karibu na kisima. \v 31 Akamwambia, “Karibu nyumbani wewe uliyebarikiwa na \nd Bwana\nd*, kwa nini unasimama huko nje? Mimi nimekuandalia nyumba na mahali kwa ajili ya ngamia.” \p \v 32 Hivyo yule mtumishi akaenda nyumbani, mizigo ikaondolewa juu ya ngamia. Majani na malisho yakaletwa kwa ajili ya ngamia na maji kwa ajili yake na watu wake ili kunawa miguu. \v 33 Ndipo chakula kikaandaliwa kwa ajili yake, lakini akasema, “Sitakula mpaka niwe nimewaambia yale niliyo nayo ya kusema.” \p Labani akasema, “Basi tuambie.” \p \v 34 Hivyo akasema, “Mimi ni mtumishi wa Abrahamu. \v 35 \nd Bwana\nd* amembariki sana bwana wangu, amekuwa tajiri. Amempa kondoo na ngʼombe, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda. \v 36 Sara mkewe bwana wangu amemzalia mwana katika uzee wake, naye amempa kila kitu alichokuwa nacho. \v 37 Naye bwana wangu ameniapisha na akasema, ‘Kamwe usimtwalie mwanangu mke katika binti za Wakanaani, ambao ninaishi katika nchi yao, \v 38 ila uende mpaka kwa jamaa ya baba yangu na ukoo wangu mwenyewe, ukamtwalie mwanangu mke huko.’ \p \v 39 “Kisha nikamuuliza bwana wangu, ‘Je, kama huyo mwanamke hatakubali kurudi nami?’ \p \v 40 “Akanijibu, ‘\nd Bwana\nd* ambaye nimetembea mbele zake, atatuma malaika wake pamoja nawe, na kuifanikisha safari yako, ili uweze kupata mke kwa ajili ya mwanangu katika ukoo wangu na kutoka jamaa ya baba yangu. \v 41 Kisha, utakapokwenda kwenye ukoo wangu, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu hata kama wakikataa kukupa huyo binti, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu.’ \p \v 42 “Nilipokuja kisimani leo nilisema, ‘Ee \nd Bwana\nd*, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ikikupendeza, naomba uifanikishe safari niliyoijia. \v 43 Tazama, ninasimama kando ya kisima hiki, kama mwanamwali akija kuteka maji nami nikimwambia, tafadhali niruhusu ninywe maji kidogo kutoka kwenye mtungi wako, \v 44 naye kama akiniambia, “Kunywa, nami nitateka maji kwa ajili ya ngamia wako pia,” basi huyo awe ndiye mke ambaye \nd Bwana\nd* amemchagulia mwana wa bwana wangu.’ \p \v 45 “Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, Rebeka akatokea, amebeba mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka maji, nami nikamwambia, ‘Tafadhali nipe maji ninywe.’ \p \v 46 “Akafanya haraka kushusha mtungi wake begani na kusema, ‘Kunywa na nitawanywesha ngamia wako pia,’ basi nikanywa, akawanywesha na ngamia pia. \p \v 47 “Nikamuuliza, ‘Wewe ni binti wa nani?’ \p “Akasema, ‘Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia.’ \p “Ndipo nilipotia pete puani mwake na bangili mikononi mwake, \v 48 nikasujudu na nikamwabudu \nd Bwana\nd*. Nikamtukuza \nd Bwana\nd*, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, aliyeniongoza katika njia sahihi ili nimtwalie mwana na bwana wangu mke katika jamaa zake. \v 49 Ikiwa mtaonyesha wema na uaminifu kwa bwana wangu, mniambie, la sivyo, mniambie, ili niweze kujua njia ya kugeukia.” \p \v 50 Labani na Bethueli wakajibu, “Jambo hili limetoka kwa \nd Bwana\nd*, hatuwezi kukuambia jambo lolote baya au jema. \v 51 Rebeka yuko hapa, mchukue na uende, awe mke wa mwana wa bwana wako, sawasawa na \nd Bwana\nd* alivyoongoza.” \p \v 52 Ikawa huyo mtumishi wa Abrahamu aliposikia waliyosema, alisujudu mpaka nchi mbele za \nd Bwana\nd*. \v 53 Ndipo huyo mtumishi akatoa vitu vilivyotengenezwa kwa dhahabu na kwa fedha pamoja na mavazi, akampa Rebeka, pia akawapa zawadi za thamani kubwa nduguye na mamaye. \v 54 Kisha yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye wakala, wakanywa na kulala palepale. \p Walipoamka asubuhi, yule mtumishi, akasema, “Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.” \p \v 55 Lakini ndugu yake Rebeka pamoja na mama yake wakajibu, “Acha binti akae kwetu siku kumi au zaidi, ndipo mwondoke.” \p \v 56 Lakini yule mtumishi akawaambia, “Msinicheleweshe, kwa kuwa \nd Bwana\nd* amefanikisha safari yangu, nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.” \p \v 57 Ndipo wakasema, “Acha tumwite huyo binti tumuulize, tusikie atakavyosema.” \v 58 Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je, utakwenda na mtu huyu?” \p Akasema, “Nitakwenda.” \p \v 59 Hivyo wakamwaga ndugu yao Rebeka aondoke, pamoja na mjakazi wake, mtumishi wa Abrahamu na watu wake. \v 60 Wakambariki Rebeka, wakamwambia, \q1 “Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu, \q2 mara elfu nyingi, \q1 nao wazao wako wamiliki \q2 malango ya adui zao.” \p \v 61 Rebeka na vijakazi wake wakajiandaa, wakapanda ngamia zao wakafuatana na yule mtu. Hivyo yule mtumishi akamchukua Rebeka akaondoka. \p \v 62 Basi Isaki alikuwa ametoka Beer-Lahai-Roi, kwa kuwa alikuwa anaishi nchi ya Negebu. \v 63 Isaki akatoka kwenda shambani kutafakari wakati wa jioni, alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja. \v 64 Rebeka pia akainua macho akamwona Isaki. Akashuka kutoka kwenye ngamia wake \v 65 na akamuuliza yule mtumishi, “Ni nani mtu yule aliye kule shambani anayekuja kutulaki?” \p Yule mtumishi akajibu, “Huyu ndiye bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika. \p \v 66 Kisha yule mtumishi akamweleza Isaki mambo yote aliyoyatenda. \v 67 Ndipo Isaki akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaki akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaki akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake. \c 25 \s1 Kifo Cha Abrahamu \p \v 1 Abrahamu alioa mke mwingine, ambaye jina lake aliitwa Ketura. \v 2 Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. \v 3 Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani, wazao wa Dedani walikuwa Waashuri, Waletushi na Waleumi. \v 4 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa Ketura. \p \v 5 Abrahamu akamwachia Isaki kila kitu alichokuwa nacho. \v 6 Lakini Abrahamu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaki. \p \v 7 Kwa jumla, Abrahamu aliishi miaka 175. \v 8 Ndipo Abrahamu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku, naye akakusanywa pamoja na watu wake. \v 9 Watoto wake Isaki na Ishmaeli wakamzika katika pango la Makpela karibu na Mamre, katika shamba lililokuwa la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, \v 10 Shamba ambalo Abrahamu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Abrahamu alipozikwa pamoja na mkewe Sara. \v 11 Baada ya kifo cha Abrahamu, Mungu akambariki mwanawe Isaki, ambaye baadaye aliishi karibu na Beer-Lahai-Roi. \s1 Wana Wa Ishmaeli \p \v 12 Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli mtoto wa Abrahamu, ambaye mjakazi wake Sara, Hagari Mmisri, alimzalia Abrahamu. \b \p \v 13 Haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, yaliyoorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, akafuatia Kedari, Adbeeli, Mibsamu, \v 14 Mishma, Duma, Masa, \v 15 Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. \v 16 Hawa walikuwa wana wa Ishmaeli na haya ni majina ya viongozi wa makabila kumi na mawili kulingana na makao yao na kambi zao. \v 17 Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka 137. Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake. \v 18 Wazao wa Ishmaeli waliishi kuanzia nchi ya Havila hadi Shuri, karibu na mpaka wa Misri, unapoelekea Ashuru. Hao waliishi kwa uhasama na ndugu zao wote. \s1 Yakobo Na Esau \p \v 19 Hivi ndivyo vizazi vya Isaki mwana wa Abrahamu. \b \p Abrahamu akamzaa Isaki, \v 20 Isaki alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu. \p \v 21 Isaki akamwomba \nd Bwana\nd* kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. \nd Bwana\nd* akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. \v 22 Watoto wakashindana tumboni mwake, akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza \nd Bwana\nd*. \p \v 23 \nd Bwana\nd* akamjibu, \q1 “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, \q2 na mataifa hayo mawili \q2 kutoka ndani yako watatenganishwa. \q1 Mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine, \q2 na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.” \p \v 24 Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake. \v 25 Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina lake Esau.\f + \fr 25:25 \ft Esau maana yake Mwenye nywele nyingi.\f* \v 26 Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo.\f + \fr 25:26 \ft Yakobo maana yake Ashikaye kisigino, au Atwaaye mahali pa mwingine, au Mdanganyaji, au Mwenye hila, au Mlaghai, au Mjanja.\f* Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa. \p \v 27 Watoto wakakua, naye Esau akakuwa mwindaji hodari, mtu wa mbugani, wakati Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa nyumbani. \v 28 Isaki, ambaye alikuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo. \p \v 29 Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu, Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali. \v 30 Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)\f + \fr 25:30 \ft Edomu maana yake Mwekundu.\f* \p \v 31 Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.” \p \v 32 Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu ya kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?” \p \v 33 Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya kuzaliwa. \p \v 34 Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake. \p Kwa hiyo Esau alidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza. \c 26 \s1 Isaki Na Abimeleki \p \v 1 Basi njaa kubwa ikawa katika nchi hiyo, kuliko ile njaa iliyotangulia iliyotokea wakati wa Abrahamu. Isaki akamwendea Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari. \v 2 \nd Bwana\nd* akamtokea Isaki, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia. \v 3 Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako. \v 4 Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa, \v 5 kwa sababu Abrahamu alinitii mimi akatunza kanuni zangu na maagizo yangu, amri zangu pamoja na sheria zangu.” \v 6 Hivyo Isaki akaishi huko Gerari. \p \v 7 Watu wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumuua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.” \p \v 8 Wakati Isaki alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona jinsi Isaki alivyomkumbatia Rebeka mke wake. \v 9 Abimeleki akamwita Isaki akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu?’ ” \p Isaki akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.” \p \v 10 Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotufanyia? Ingewezekana mtu yeyote akawa amekutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia juu yetu.” \p \v 11 Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.” \p \v 12 Isaki akapanda mazao katika nchi hiyo, kwa mwaka huo huo, akavuna mara mia, kwa sababu \nd Bwana\nd* alimbariki. \v 13 Isaki akawa tajiri, mali zake zikaendelea kuongezeka mpaka akawa tajiri sana. \v 14 Akawa na mifugo ya kondoo na ngʼombe, na watumishi wengi sana, kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu. \v 15 Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Abrahamu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo. \p \v 16 Ndipo Abimeleki akamwambia Isaki, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.” \p \v 17 Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. \v 18 Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa. \p \v 19 Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. \v 20 Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,\f + \fr 26:20 \ft Eseki maana yake ni Ugomvi.\f* kwa sababu waligombana naye. \v 21 Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.\f + \fr 26:21 \ft Sitna maana yake Upinzani.\f* \v 22 Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,\f + \fr 26:22 \ft Rehobothi maana yake ni Mungu ametufanyia nafasi.\f* akisema, “Sasa \nd Bwana\nd* ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.” \p \v 23 Kutoka pale akaenda Beer-Sheba. \v 24 Usiku ule \nd Bwana\nd* akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.” \p \v 25 Isaki akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la \nd Bwana\nd*. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima. \p \v 26 Wakati huo, Abimeleki alikuwa amemjia kutoka Gerari, akifuatana na Ahuzathi mshauri wake, pamoja na Fikoli jemadari wa majeshi yake. \v 27 Isaki akawauliza, “Mbona mmekuja kwangu na ninyi mlinichukia na kunifukuza?” \p \v 28 Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwa \nd Bwana\nd* alikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu, kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe \v 29 kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na \nd Bwana\nd*.’ ” \p \v 30 Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. \v 31 Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani. \p \v 32 Siku hiyo watumishi wa Isaki wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!” \v 33 Naye akakiita Shiba,\f + \fr 26:33 \ft Shiba kwa Kiebrania maana yake ni Saba.\f* mpaka leo mji huo unaitwa Beer-Sheba.\f + \fr 26:33 \ft Beer-Sheba maana yake ni Kisima cha wale saba, yaani wale kondoo saba ambao Abrahamu aliwatoa kama ushahidi kati yake na Abimeleki.\f* \p \v 34 Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akamwoa Yudithi binti Beeri Mhiti, kisha akamwoa Basemathi binti Eloni Mhiti. \v 35 Hawa walikuwa chanzo cha huzuni ya Isaki na Rebeka. \c 27 \s1 Yakobo Anaipata Baraka Ya Isaki \p \v 1 Isaki alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.” \p Akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 2 Isaki akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kifo changu. \v 3 Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu. \v 4 Uniandalie aina ya chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili niweze kukubariki kabla sijafa.” \p \v 5 Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta, \v 6 Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau, \v 7 ‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele za \nd Bwana\nd* kabla sijafa.’ \v 8 Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia: \v 9 Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyopenda. \v 10 Kisha umpelekee baba yako ale, ili apate kukubariki kabla hajafa.” \p \v 11 Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Lakini ndugu yangu Esau ana nywele mwilini, mimi nina ngozi nyororo. \v 12 Itakuwaje kama baba yangu akinigusa? Itaonekana kwake kama niliyemfanyia ujanja na kuleta laana juu yangu badala ya baraka.” \p \v 13 Mama yake akamwambia, “Mwanangu, laana na iwe juu yangu. Fanya tu ninalokuambia, nenda ukaniletee hao wana-mbuzi.” \p \v 14 Kwa hiyo alikwenda akawaleta, akampa mama yake, akaandaa chakula kitamu, kama vile alivyopenda baba yake. \v 15 Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. \v 16 Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi. \v 17 Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka. \p \v 18 Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.” \p Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?” \p \v 19 Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.” \p \v 20 Isaki akamuuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?” \p Akajibu, “\nd Bwana\nd* Mungu wako amenifanikisha.” \p \v 21 Kisha Isaki akamwambia Yakobo, “Mwanangu tafadhali sogea karibu nami ili nikupapase, nione kama hakika ndiwe Esau mwanangu, au la.” \p \v 22 Yakobo akasogea karibu na baba yake Isaki, ambaye alimpapasa na kusema, “Sauti ni ya Yakobo, bali mikono ni ya Esau.” \v 23 Hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na nywele kama ya ndugu yake Esau, kwa hiyo akambariki. \v 24 Akamuuliza, “Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?” \p Akajibu, “Mimi ndiye.” \p \v 25 Kisha akasema, “Mwanangu, niletee sehemu ya mawindo yako nile, ili nipate kukubariki.” \p Yakobo akamletea naye akala, akamletea na divai akanywa. \v 26 Kisha Isaki baba yake akamwambia, “Njoo hapa, mwanangu, unibusu.” \p \v 27 Kwa hiyo akamwendea akambusu. Isaki aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema, \q1 “Aha, harufu ya mwanangu \q2 ni kama harufu ya shamba \q2 ambalo \nd Bwana\nd* amelibariki. \q1 \v 28 Mungu na akupe umande kutoka mbinguni \q2 na utajiri wa duniani: \q2 wingi wa nafaka na divai mpya. \q1 \v 29 Mataifa na yakutumikie \q2 na mataifa yakusujudie. \q1 Uwe bwana juu ya ndugu zako, \q2 na wana wa mama yako wakusujudie. \q1 Walaaniwe wale wakulaanio, \q2 nao wale wakubarikio wabarikiwe.” \p \v 30 Baada ya Isaki kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni. \v 31 Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.” \p \v 32 Isaki baba yake akamuuliza, “Wewe ni nani?” \p Akajibu, “Mimi ni mwanao, mzaliwa wako wa kwanza, Esau.” \p \v 33 Isaki akatetemeka kwa nguvu sana, akasema, “Alikuwa nani basi, ambaye aliwinda mawindo akaniletea? Nilikula kabla tu hujaja na nikambariki, naye hakika atabarikiwa!” \p \v 34 Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!” \p \v 35 Lakini akasema, “Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu na akachukua baraka yako.” \p \v 36 Esau akasema, “Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!” Kisha akauliza, “Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?” \p \v 37 Isaki akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?” \p \v 38 Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa. \p \v 39 Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia, \q1 “Makao yako yatakuwa \q2 mbali na utajiri wa dunia, \q2 mbali na umande wa mbinguni juu. \q1 \v 40 Utaishi kwa upanga, \q2 nawe utamtumikia ndugu yako, \q1 lakini wakati utakapokuwa umejikomboa, \q2 utatupa nira yake \q2 kutoka shingoni mwako.” \s1 Yakobo Anakimbilia Kwa Labani \p \v 41 Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo.” \p \v 42 Rebeka alipokwisha kuambiwa yale aliyoyasema Esau mwanawe mkubwa, alimwita Yakobo mwanawe mdogo, akamwambia, “Ndugu yako Esau anajifariji kwa wazo la kukuua. \v 43 Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani. \v 44 Ukae naye kwa muda mpaka ghadhabu ya ndugu yako itulie. \v 45 Wakati ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze wote wawili kwa siku moja?” \p \v 46 Kisha Rebeka akamwambia Isaki, “Nimechukia kuishi kwa sababu ya hawa wanawake wa Kihiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake wa Kihiti kama hawa, sitakuwa na faida kuendelea kuishi.” \c 28 \p \v 1 Basi Isaki akamwita Yakobo, akambariki na akamwamuru, akisema, “Usioe mwanamke wa Kikanaani. \v 2 Nenda mara moja mpaka Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako. \v 3 Mungu Mwenyezi\f + \fr 28:3 \ft Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\f* na akubariki uwe na uzao uongezeke idadi yako upate kuwa jamii kubwa ya watu. \v 4 Na akupe wewe na uzao wako baraka aliyopewa Abrahamu, upate kumiliki nchi unayoishi sasa kama mgeni, nchi ambayo Mungu alimpa Abrahamu.” \v 5 Kisha Isaki akamuaga Yakobo, naye akaenda Padan-Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, ndugu wa Rebeka, aliyekuwa mama wa Yakobo na Esau. \p \v 6 Sasa Esau akajua kuwa Isaki amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,” \v 7 tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu. \v 8 Esau akatambua jinsi ambavyo baba yake Isaki anavyowachukia binti za Wakanaani. \v 9 Ndipo Esau akaenda kwa Ishmaeli, akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ishmaeli mwana wa Abrahamu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao. \s1 Ndoto Ya Yakobo Huko Betheli \p \v 10 Yakobo akatoka Beer-Sheba kwenda Harani. \v 11 Alipofika mahali fulani, akalala hapo kwa sababu jua lilikuwa limetua. Akachukua jiwe moja la mahali pale, akaliweka chini ya kichwa chake akajinyoosha akalala usingizi. \v 12 Akaota ndoto ambayo aliona ngazi imesimamishwa juu ya ardhi, ncha yake ikiwa imefika mbinguni na malaika wa Mungu wakawa wakipanda na kushuka juu yake. \v 13 Juu yake alisimama \nd Bwana\nd*, akasema, “Mimi ni \nd Bwana\nd*, Mungu wa baba yako Abrahamu na Mungu wa Isaki. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako. \v 14 Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako mataifa yote ya duniani yatabarikiwa. \v 15 Niko pamoja nawe nami nitakulinda kila uendako na nitakurudisha katika nchi hii. Sitakuacha mpaka nitakapofanya hayo niliyokuahidi.” \p \v 16 Yakobo alipoamka kutoka usingizini, akawaza, “Hakika \nd Bwana\nd* yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.” \v 17 Kwa hiyo akaogopa, akasema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo, hili ni lango la mbinguni.” \p \v 18 Asubuhi yake na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake. \v 19 Mahali pale akapaita Betheli,\f + \fr 28:19 \ft Betheli maana yake Nyumba ya Mungu.\f* ingawa mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. \p \v 20 Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, “Kama Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari niendayo, akinipa chakula nile na nguo nivae \v 21 na nirudi salama nyumbani kwa baba yangu, hapo ndipo \nd Bwana\nd* atakuwa Mungu wangu, \v 22 nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu na katika yote utakayonipa nitakutolea wewe sehemu ya kumi.” \c 29 \s1 Yakobo Awasili Padan-Aramu \p \v 1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika kwenye nchi za mataifa ya mashariki. \v 2 Huko akaona kisima katika shamba, pamoja na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu na kisima hicho kwa sababu walikuwa wanakunywa maji kutoka kwenye kisimani hicho. Jiwe lililokuwa mdomoni mwa kisima lilikuwa kubwa. \v 3 Wakati kondoo wanapokuwa wamekusanyika hapo, wachungaji huvingirisha jiwe hilo kutoka kwenye mdomo wa kisima na kunywesha kondoo. Kisha hulirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima. \p \v 4 Yakobo aliwauliza wachungaji, “Ndugu zangu, ninyi mmetoka wapi?” \p Wakamjibu, “Tumetoka Harani.” \p \v 5 Aliwaambia, “Je, mnamjua Labani, mjukuu wa Nahori?” \p Wakamjibu, “Ndiyo, tunamfahamu.” \p \v 6 Kisha Yakobo akawauliza, “Je, yeye ni mzima?” \p Wakasema, “Ndiyo, ni mzima, na hapa yuaja Raheli binti yake akiwa na kondoo.” \p \v 7 Akasema, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya mifugo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.” \p \v 8 Walijibu, “Haiwezekani, mpaka kondoo wote wakusanyike na jiwe liwe limevingirishwa kutoka mdomo wa kisima. Ndipo tutanywesha kondoo.” \p \v 9 Alipokuwa akizungumza nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa baba yake, kwa maana alikuwa mchunga kondoo. \v 10 Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alikwenda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake. \v 11 Kisha Yakobo akambusu Raheli na akaanza kulia kwa sauti. \v 12 Yakobo alikuwa amemwambia Raheli kuwa yeye alikuwa jamaa ya baba yake, na kwamba ni mwana wa Rebeka. Basi Raheli alikimbia na kumweleza baba yake. \p \v 13 Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu, halafu akamleta nyumbani kwake, kisha Yakobo akamwambia mambo yote. \v 14 Ndipo Labani akamwambia, “Wewe ni nyama yangu na damu yangu mwenyewe.” \s1 Yakobo Awaoa Lea Na Raheli \p Baada ya Yakobo kukaa kwa Labani mwezi mzima, \v 15 Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo sababu unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.” \p \v 16 Labani alikuwa na binti wawili, binti mkubwa aliitwa Lea na binti mdogo aliitwa Raheli. \v 17 Lea alikuwa na macho dhaifu, lakini Raheli alikuwa na umbo la kupendeza na mzuri wa sura. \v 18 Yakobo akampenda Raheli, akamwambia Labani, “Nitakutumikia kwa miaka saba kwa ajili ya kumpata Raheli binti yako mdogo.” \p \v 19 Labani akasema, “Ni bora zaidi nikupe Raheli kuliko kumpa mtu mwingine yeyote. Kaa pamoja na mimi hapa.” \v 20 Kwa hiyo Yakobo akatumika miaka saba ili kumpata Raheli, lakini ilionekana kwake kama siku chache tu kwa sababu ya upendo wake kwa Raheli. \p \v 21 Ndipo Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu. Muda wangu umekamilika, nami nataka nikutane naye kimwili.” \p \v 22 Basi Labani akaalika watu wote wa mahali pale na akafanya karamu. \p \v 23 Lakini ilipofika jioni, akamchukua Lea binti yake akampa Yakobo, naye Yakobo akakutana naye kimwili. \v 24 Naye Labani akamtoa Zilpa, mtumishi wake wa kike, kuwa mtumishi wa Lea, binti yake. \p \v 25 Kesho yake asubuhi, Yakobo akagundua kuwa amepewa Lea! Basi Yakobo akamwambia Labani, “Ni jambo gani hili ulilonitendea? Nilikutumikia kwa ajili ya Raheli, sivyo? Kwa nini umenidanganya?” \p \v 26 Labani akajibu, “Si desturi yetu kumwoza binti mdogo kabla ya kumwoza binti mkubwa. \v 27 Maliza juma la arusi ya binti huyu, kisha pia nitakupa huyu binti mdogo, kwa kutumika miaka mingine saba.” \p \v 28 Naye Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma na Lea, kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake. \v 29 Labani akamtoa Bilha mtumishi wake wa kike kwa Raheli ili kuwa mtumishi wake. \v 30 Pia Yakobo akakutana na Raheli kimwili, naye akampenda Raheli zaidi kuliko Lea. Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka mingine saba. \s1 Wana Wa Yakobo \p \v 31 \nd Bwana\nd* alipoona kwamba Lea hapendwi, akampa watoto, lakini Raheli alikuwa tasa. \v 32 Lea akapata mimba akazaa mwana. Akamwita Reubeni,\f + \fr 29:32 \ft Reubeni maana yake Ona mwana, yaani Yehova ameangalia taabu yangu.\f* kwa maana alisema, “Ni kwa sababu \nd Bwana\nd* ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.” \p \v 33 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababu \nd Bwana\nd* alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.\f + \fr 29:33 \ft Simeoni maana yake Anasikia, yaani sasa ataungana nami kama Raheli.\f* \p \v 34 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.\f + \fr 29:34 \ft Lawi maana yake Nimeunganishwa, yaani na mume wangu.\f* \p \v 35 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu \nd Bwana\nd*.” Kwa hiyo akamwita Yuda.\f + \fr 29:35 \ft Yuda maana yake Sifa, yaani Nitamsifu Yehova.\f* Kisha akaacha kuzaa watoto. \c 30 \p \v 1 Raheli alipoona hamzalii Yakobo watoto, akamwonea ndugu yake wivu. Hivyo akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!” \p \v 2 Yakobo akamkasirikia, akamwambia, “Je, mimi ni badala ya Mungu, ambaye amekuzuia usizae watoto?” \p \v 3 Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi pia niweze kuwa na uzao.” \p \v 4 Hivyo Raheli akampa Yakobo Bilha awe mke wake. Yakobo akakutana naye kimwili, \v 5 Bilha akapata mimba, naye akamzalia Yakobo mwana. \v 6 Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.\f + \fr 30:6 \ft Dani maana yake Anahukumu, yaani Mungu amenipa haki yangu.\f* \p \v 7 Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. \v 8 Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.\f + \fr 30:8 \ft Naftali maana yake Nimeshindana nami nimeshinda.\f* \p \v 9 Lea alipoona kuwa amekoma kuzaa watoto, alimchukua mtumishi wake wa kike Zilpa, naye akampa Yakobo awe mke wake. \v 10 Mtumishi wa Lea yaani Zilpa, akamzalia Yakobo mwana. \v 11 Ndipo Lea akasema, “Hii ni bahati nzuri aje!” Kwa hiyo akamwita Gadi. \p \v 12 Mtumishi wa kike wa Lea akamzalia Yakobo mwana wa pili. \v 13 Ndipo Lea aliposema, “Jinsi gani nilivyo na furaha! Wanawake wataniita furaha.” Kwa hiyo akamwita Asheri.\f + \fr 30:13 \ft Asheri maana yake Nimefurahi, yaani Mungu amenifurahisha.\f* \p \v 14 Wakati wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akakuta tunguja, ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.” \p \v 15 Lakini Lea akamwambia, “Haikukutosha kumtwaa mume wangu? Je, utachukua na tunguja za mwanangu pia?” \p Raheli akasema, “Vema sana! Yakobo atakutana nawe kimwili leo usiku, kwa malipo ya tunguja za mwanao.” \p \v 16 Kwa hiyo Yakobo alipokuja kutoka shambani jioni ile, Lea akaenda kumlaki, akamwambia, “Lazima ukutane nami kimwili. Nimekukodisha kwa tunguja za mwanangu.” Kwa hiyo akakutana naye kimwili usiku ule. \p \v 17 Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano. \v 18 Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.\f + \fr 30:18 \ft Isakari maana yake Zawadi, yaani Mungu amenizawadia.\f* \p \v 19 Lea akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa sita. \v 20 Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita Zabuloni.\f + \fr 30:20 \ft Zabuloni maana yake Heshima.\f* \p \v 21 Baadaye akamzaa mtoto wa kike akamwita Dina.\f + \fr 30:21 \ft Dina maana yake Tetea haki, yaani Mungu amenitetea katika mashindano yangu.\f* \p \v 22 Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake. \v 23 Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.” \p \v 24 Akamwita Yosefu\f + \fr 30:24 \ft Yosefu maana yake Yeye na aongeze, yaani Mungu na aniongezee.\f* na kusema, “\nd Bwana\nd* na anipe mwana mwingine.” \s1 Makundi Ya Yakobo Yaongezeka \p \v 25 Baada ya Raheli kumzaa Yosefu, Yakobo akamwambia Labani, “Nipe ruhusa nirudi katika nchi yangu. \v 26 Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.” \p \v 27 Lakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa njia ya uaguzi kwamba \nd Bwana\nd* amenibariki kwa sababu yako.” \v 28 Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.” \p \v 29 Yakobo akamwambia, “Unajua jinsi ambavyo nimekutumikia na jinsi ambavyo wanyama wako walivyolishwa vizuri chini ya uangalizi wangu. \v 30 Kidogo ulichokuwa nacho kabla sijaja kimeongezeka sana, naye \nd Bwana\nd* amekubariki popote nilipokuwa. Lakini sasa, ni lini nitashughulikia mambo ya nyumba yangu mwenyewe?” \p \v 31 Labani akamuuliza, “Nikupe nini?” \p Yakobo akamjibu, “Usinipe chochote lakini kama utanifanyia jambo hili moja, nitaendelea kuchunga na kuyaangalia makundi yako. \v 32 Niruhusu nipite katika makundi yako yote leo niondoe humo kila kondoo mwenye mabakabaka au madoadoa, kila mwana-kondoo mweusi na kila mbuzi mwenye madoadoa au mabakabaka. Hawa watakuwa ujira wangu. \v 33 Uadilifu wangu utanishuhudia siku zijazo, kila utakapochunguza ujira ambao umenilipa mimi. Mbuzi yeyote wangu ambaye hana mabakabaka wala madoadoa, au mwana-kondoo ambaye si mweusi, atahesabika ameibwa.” \p \v 34 Labani akasema, “Ninakubali na iwe kama ulivyosema.” \v 35 Siku ile ile Yakobo akawaondoa beberu wote waliokuwa na mistari au madoadoa na mbuzi wake wote waliokuwa na mistari au madoadoa (wote waliokuwa na alama nyeupe juu yao) na wana-kondoo weusi wote, akawaweka chini ya uangalizi wa wanawe. \v 36 Kisha Labani akamwacha Yakobo kwa mwendo wa safari ya siku tatu kati yake na Yakobo, wakati Yakobo akiendelea kuchunga lile kundi la Labani lililobaki. \p \v 37 Hata hivyo, Yakobo, akachukua fito mbichi zilizokatwa wakati huo huo za miti ya mlubna, mlozi na mwaramoni akazibambua ili mistari myeupe ionekane katika fito hizo. \v 38 Kisha akaweka fito alizozibambua kwenye mabirika yote ya kunyweshea mifugo, ili ziwe mbele ya makundi walipokuja kunywa maji. Wanyama walipokuja kunywa maji, hali wakiwa wanahitaji mbegu, \v 39 wakapandwa hizo fito zikiwa mbele yao. Wanyama waliopata mimba mbele ya hizo fito walizaa wanyama wenye mistari, madoadoa na mabakabaka. \v 40 Yakobo akawatenga wadogo wa kundi peke yao, lakini akazielekeza nyuso za hao waliobaki kwenye wale wenye mistari na weusi waliokuwa mali ya Labani. Hivyo akatenga makundi yake mwenyewe, na wala hakuwachanganya na wanyama wa Labani. \v 41 Kila mara wanyama wenye nguvu walipohitaji mbegu, Yakobo aliweka zile fito kwenye mabirika mbele ya hao wanyama, ili wapandwe karibu na hizo fito, \v 42 lakini ikiwa wanyama walikuwa wadhaifu hakuziweka hizo fito. Hivyo wanyama wadhaifu wakawa wa Labani, na wanyama wenye nguvu wakawa wa Yakobo. \v 43 Kwa njia hii Yakobo akastawi sana, tena akawa na makundi makubwa, watumishi wa kike na wa kiume na ngamia na punda. \c 31 \s1 Yakobo Akimbia Kutoka Kwa Labani \p \v 1 Yakobo akawasikia wana wa Labani wakisema, “Yakobo amechukua kila kitu kilichokuwa cha baba yetu naye amepata utajiri huu wote kutokana na vile vilivyokuwa mali ya baba yetu.” \v 2 Yakobo akatambua kwamba moyo wa Labani kwake haukuwa kama ulivyokuwa mwanzo. \p \v 3 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Yakobo, “Rudi katika nchi ya baba zako na kwa watu wako, nami nitakuwa pamoja nawe.” \p \v 4 Hivyo Yakobo akatuma ujumbe kwa Raheli na Lea waje machungani yalikokuwa makundi yake. \v 5 Akawaambia, “Naona moyo wa baba yenu kwangu sivyo kama ulivyokuwa mwanzoni, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami. \v 6 Mnajua kwamba nimemtumikia baba yenu kwa nguvu zangu zote, \v 7 hata hivyo baba yenu amenidanganya kwa kubadilisha ujira wangu mara kumi. Hata hivyo, Mungu hakumruhusu kunidhuru. \v 8 Kama alisema, ‘Wenye madoadoa watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye madoadoa, kama alisema, ‘Wenye mistari watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye mistari. \v 9 Hivyo Mungu amechukua mifugo ya baba yenu na amenipa mimi. \p \v 10 “Wakati fulani majira ya kuzaliana niliota ndoto ambayo niliinua macho na kuona kwamba wale mabeberu waliokuwa wakipanda kundi walikuwa wa mistari, madoadoa na mabakabaka. \v 11 Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, ‘Yakobo.’ Nikamjibu, ‘Mimi hapa.’ \v 12 Akasema, ‘Inua macho yako uone wale mabeberu wote wanaopanda kundi wana mistari, madoadoa au mabakabaka, kwa maana nimeona yale yote ambayo Labani amekuwa akikutendea. \v 13 Mimi ndiye Mungu wa Betheli, ulikomiminia ile nguzo mafuta na pale mahali uliponiwekea nadhiri. Sasa ondoka katika nchi hii mara moja urudi katika nchi uliyozaliwa.’ ” \p \v 14 Ndipo Raheli na Lea wakajibu, “Je bado tu tunalo fungu lolote katika urithi wa nyumba ya baba yetu? \v 15 Je, yeye hatuhesabu sisi kama wageni? Sio kwamba ametuuza tu, bali ametumia hata na vile vilivyolipwa kwa ajili yetu. \v 16 Hakika utajiri wote ambao Mungu ameuchukua kutoka kwa baba yetu ni mali yetu na watoto wetu. Hivyo fanya lolote lile Mungu alilokuambia.” \p \v 17 Ndipo Yakobo akawapandisha watoto wake na wake zake juu ya ngamia, \v 18 naye akawaswaga wanyama wote mbele yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa amechuma huko Padan-Aramu kwenda kwa baba yake Isaki katika nchi ya Kanaani. \p \v 19 Labani alipokuwa amekwenda kukata kondoo wake manyoya, Raheli aliiba miungu ya nyumba ya baba yake. \v 20 Zaidi ya hayo, Yakobo alimdanganya Labani Mwaramu kwa kutokumwambia kwamba anakimbia. \v 21 Hivyo akakimbia pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo na kuvuka Mto Frati akaelekea nchi ya vilima katika Gileadi. \s1 Labani Amfuatilia Yakobo \p \v 22 Siku ya tatu Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia. \v 23 Akiwachukua jamaa zake, akamfuatia Yakobo kwa siku saba na kumkuta kwenye nchi ya vilima katika Gileadi. \v 24 Ndipo Mungu akamjia Labani Mwaramu katika ndoto usiku na kumwambia, “Jihadhari usiseme neno lolote kwa Yakobo, liwe zuri au baya.” \p \v 25 Yakobo alikuwa amepiga hema lake katika nchi ya vilima katika Gileadi wakati Labani alipomkuta, Labani na jamaa yake wakapiga kambi huko pia. \v 26 Ndipo Labani akamwambia Yakobo, “Umefanya nini? Umenidanganya na umewachukua binti zangu kama mateka katika vita. \v 27 Kwa nini ulikimbia kwa siri na kunidanganya? Kwa nini hukuniambia ili nikuage kwa furaha na nyimbo za matari na vinubi? \v 28 Hata hukuniruhusu niwabusu wajukuu zangu na kuwaaga binti zangu. Umefanya kitu cha kipumbavu. \v 29 Nina uwezo wa kukudhuru, lakini usiku uliopita Mungu wa baba yako alisema nami, akaniambia, ‘Jihadhari, usiseme neno lolote kwa Yakobo liwe zuri au baya.’ \v 30 Sasa umeondoka kwa sababu umetamani kurudi nyumbani kwa baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu?” \p \v 31 Yakobo akamjibu Labani, “Niliogopa, kwa sababu nilifikiri ungeweza kuninyangʼanya binti zako kwa nguvu. \v 32 Lakini kama ukimkuta yeyote aliye na miungu yako, hataishi. Mbele ya jamaa yetu, angalia mwenyewe uone kama kuna chochote chako hapa nilicho nacho, kama kipo, kichukue.” Basi Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiba hiyo miungu. \p \v 33 Kwa hiyo Labani akaingia ndani ya hema la Yakobo na ndani ya hema la Lea na ndani ya hema la watumishi wawili wa kike, lakini hakukuta chochote. Baadaye alipotoka katika hema la Lea, akaingia hema la Raheli. \v 34 Basi Raheli ndiye alikuwa amechukua ile miungu ya nyumbani kwao na kuiweka katika matandiko ya ngamia na kukalia. Labani akatafuta kila mahali kwenye hema lakini hakupata chochote. \p \v 35 Raheli akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu kwa kuwa siwezi kusimama ukiwepo, niko katika hedhi.” Labani akatafuta lakini hakuweza kuipata miungu ya nyumbani kwake. \p \v 36 Yakobo akakasirika na kumshutumu Labani, akisema, “Uhalifu wangu ni nini?” Akamuuliza Labani, “Ni dhambi gani niliyofanya hata unaniwinda? \v 37 Sasa kwa kuwa umepekua vitu vyangu vyote umepata nini kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya jamaa yako na yangu, nao waamue kati yetu sisi wawili. \p \v 38 “Mpaka sasa nimekuwa pamoja nawe miaka ishirini. Kondoo wako na mbuzi wako hawajaharibu mimba, wala sijala kondoo dume kutoka makundi yako. \v 39 Sikukuletea mfugo aliyeraruliwa na wanyama pori, nilibeba hasara mimi mwenyewe. Tena ulinidai malipo kwa chochote kilichoibwa mchana au usiku. \v 40 Hii ndiyo iliyokuwa hali yangu: Niliumia kwa joto la mchana na baridi usiku, pia usingizi ulinipa. \v 41 Ilikuwa hivi kwa miaka ile ishirini niliyokuwa nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka ile kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, miaka sita kwa ajili ya makundi yako, nawe ulibadilisha ujira wangu mara kumi. \v 42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaki, hakuwa pamoja nami, hakika ungenifukuza mikono mitupu. Lakini Mungu ameona taabu yangu na kazi ngumu ya mikono yangu, naye usiku uliopita amekukemea.” \p \v 43 Labani akamjibu Yakobo, “Wanawake hawa ni binti zangu, watoto hawa ni watoto wangu na makundi haya ni makundi yangu. Vyote unavyoviona ni vyangu. Lakini hata hivyo ninaweza kufanya nini kuhusu hawa binti zangu, au kuhusu watoto waliowazaa? \v 44 Njoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.” \p \v 45 Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. \v 46 Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. \v 47 Labani akaliita Yegar-Sahadutha\f + \fr 31:47 \ft Yegar-Sahadutha maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiaramu.\f* na Yakobo akaliita Galeedi.\f + \fr 31:47 \ft Galeedi maana yake ni Lundo la ushahidi kwa Kiebrania.\f* \p \v 48 Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. \v 49 Pia liliitwa Mispa,\f + \fr 31:49 \ft Mispa maana yake Mnara wa ulinzi.\f* kwa sababu alisema, “\nd Bwana\nd* na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine. \v 50 Kama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.” \p \v 51 Pia Labani akamwambia Yakobo, “Hili ndilo lundo, na hii ndiyo nguzo niliyoisimamisha kati yako na mimi. \v 52 Lundo hili ni shahidi na nguzo hii ni shahidi, kwamba sitavuka lundo hili kuja upande wako kukudhuru, nawe kwamba hutavuka lundo hili na nguzo hii kuja upande wangu kunidhuru. \v 53 Mungu wa Abrahamu na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba zao, aamue kati yetu.” \p Hivyo Yakobo akaapa kwa jina la Hofu ya baba yake Isaki. \v 54 Yakobo akatoa dhabihu juu ya kilima na akawaalika jamaa zake kula chakula. Baada ya kula, wakalala huko. \p \v 55 Kesho yake asubuhi na mapema, Labani akawabusu wajukuu zake, binti zake na kuwabariki. Kisha akaondoka, akarudi nyumbani. \c 32 \s1 Yakobo Ajiandaa Kukutana Na Esau \p \v 1 Yakobo pia akaondoka akaenda zake, nao malaika wa Mungu wakakutana naye. \v 2 Yakobo alipowaona, akasema, “Hii ni kambi ya Mungu!” Kwa hiyo akapaita mahali pale Mahanaimu.\f + \fr 32:2 \ft Mahanaimu maana yake Kambi mbili.\f* \p \v 3 Yakobo akatuma wajumbe kumtangulia kwa Esau ndugu yake huko Seiri, katika nchi ya Edomu. \v 4 Akawaagiza akisema: “Hili ndilo mtakalomwambia bwana wangu Esau: ‘Mtumishi wako Yakobo anasema, nimekuwa nikiishi pamoja na Labani na nimekuwako huko mpaka sasa. \v 5 Ninao ngʼombe na punda, kondoo na mbuzi, watumishi wa kiume na wa kike. Sasa ninatuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili nipate kibali machoni pako.’ ” \p \v 6 Wajumbe waliporudi kwa Yakobo, wakamwambia, “Tulikwenda kuonana na ndugu yako Esau, naye sasa anakuja kukulaki akifuatana na wanaume 400.” \p \v 7 Kwa hofu kuu na huzuni, Yakobo akagawanya watu aliokuwa nao katika makundi mawili, pia akagawanya makundi ya kondoo na mbuzi, na vilevile ngʼombe na ngamia. \v 8 Yakobo alifikiri, “Kama Esau akija na kushambulia kundi moja, kundi lililobaki litaweza likanusurika.” \p \v 9 Ndipo Yakobo akaomba, “Ee Mungu wa baba yangu Abrahamu, Mungu wa baba yangu Isaki, Ee \nd Bwana\nd*, ambaye uliniambia, ‘Rudi katika nchi yako na jamaa yako, nami nitakufanya ustawi,’ \v 10 mimi sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa ninayo makundi mawili. \v 11 Nakuomba, uniokoe na mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia mama pamoja na watoto wao. \v 12 Lakini umeshasema, ‘Hakika nitakufanya ustawi na kuufanya uzao wako kuwa mwingi kama mchanga wa baharini ambao hauwezi kuhesabika!’ ” \p \v 13 Akalala pale usiku ule, miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake: \v 14 Mbuzi waume ishirini na mbuzi wake 200, kondoo dume ishirini na kondoo wake 200. \v 15 Ngamia wake thelathini pamoja na ndama zao, ngʼombe wake arobaini na mafahali kumi, punda wake ishirini na punda waume kumi. \v 16 Akaviweka chini ya uangalizi wa watumishi wake, kila kundi peke yake na kuwaambia, “Nitangulieni na kuacha nafasi kati ya makundi.” \p \v 17 Akamwagiza yule aliyetangulia kuwa, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, ‘Wewe ni wa nani? Unakwenda wapi? Wanyama hawa wote mbele yako ni mali ya nani?’ \v 18 Ndipo utakaposema, ‘Ni mali ya mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi ambazo zimetumwa kwa bwana wangu Esau, naye anakuja nyuma yetu.’ ” \p \v 19 Akamwagiza pia yule mtumishi wa kundi la pili, la tatu na yale mengine yote yaliyofuata akiwaambia, “Mtamwambia Esau maneno hayo hayo mtakapokutana naye. \v 20 Hakikisheni mmesema, ‘Mtumishi wako Yakobo anakuja nyuma yetu.’ ” Kwa kuwa alifikiri, “Nitaweza kumtuliza kwa zawadi hizi ninazotanguliza, hatimaye, nitakapomwona, huenda atanikubali.” \v 21 Kwa hiyo zawadi za Yakobo zilitangulia mbele yake, lakini yeye mwenyewe alilala kambini usiku ule. \s1 Yakobo Ashindana Mweleka Na Mungu \p \v 22 Usiku ule Yakobo akaamka akawachukua wake zake wawili, watumishi wake wawili wa kike na wanawe kumi na mmoja na akavuka kivuko cha Yaboki. \v 23 Baada ya kuwavusha ngʼambo ya kijito, alivusha pia mali zake zote. \v 24 Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko. \v 25 Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. \v 26 Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” \p Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.” \p \v 27 Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?” \p Akajibu, “Yakobo.” \p \v 28 Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli,\f + \fr 32:28 \ft Israeli maana yake Yeye ashindanaye na Mungu.\f* kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.” \p \v 29 Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.” \p Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko. \p \v 30 Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli,\f + \fr 32:30 \ft Penieli maana yake Uso wa Mungu, ambalo ni sawa na Penueli kwa Kiebrania.\f* akasema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso na bado maisha yangu yameokoka.” \p \v 31 Jua lilikuwa linachomoza Yakobo alipoondoka Penueli, naye alikuwa akichechemea kwa sababu ya nyonga yake. \v 32 Kwa hiyo mpaka leo Waisraeli hawali mshipa ulioungana na kiungio cha nyonga, kwa sababu kiungio cha nyonga ya Yakobo kiliteguliwa karibu na mshipa huo. \c 33 \s1 Yakobo Akutana Na Esau \p \v 1 Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike. \v 2 Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma. \v 3 Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake. \p \v 4 Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia. \v 5 Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?” \p Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.” \p \v 6 Kisha wale watumishi wa kike na watoto wao wakakaribia na kusujudu. \v 7 Kisha Lea na watoto wake wakaja na kusujudu. Mwisho wa wote wakaja Yosefu na Raheli, nao pia wakasujudu. \p \v 8 Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?” \p Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.” \p \v 9 Lakini Esau akamwambia, “Ndugu yangu, tayari nina wingi wa mali. Ulivyo navyo viwe vyako mwenyewe.” \p \v 10 Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako, ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa takabali kubwa. \v 11 Tafadhali ukubali zawadi iliyoletwa kwako, kwa kuwa Mungu amenineemesha na ninavyo vyote ninavyohitaji.” Kwa sababu Yakobo alisisitiza, Esau akapokea. \p \v 12 Ndipo Esau akasema, “Na tuendelee na safari, nitakuwa pamoja nawe.” \p \v 13 Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa kondoo wake na ngʼombe wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa. \v 14 Hivyo bwana wangu umtangulie mtumishi wako, wakati mimi nikija polepole kwa mwendo wa makundi yaliyo mbele yangu na mwendo wa watoto, mpaka nifike kwa bwana wangu huko Seiri.” \p \v 15 Esau akamwambia, “Basi na niwaache baadhi ya watu wangu pamoja nawe.” \p Yakobo akauliza, “Lakini kwa nini ufanye hivyo, niache tu nipate kibali machoni pa bwana wangu.” \p \v 16 Hivyo siku hiyo Esau akashika njia akarudi Seiri. \v 17 Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi,\f + \fr 33:17 \ft Sukothi maana yake Vibanda.\f* mahali alipojijengea makazi kwa ajili yake na mabanda kwa ajili ya mifugo yake. Hii ndiyo sababu sehemu ile inaitwa Sukothi. \p \v 18 Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji. \v 19 Akanunua kiwanja kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa bei ya vipande mia vya fedha, ambapo alipiga hema lake. \v 20 Pale akajenga madhabahu na kupaita El-Elohe-Israeli.\f + \fr 33:20 \ft El-Elohe-Israeli maana yake Mungu, Mungu wa Israeli au Mwenye Nguvu ni Mungu wa Israeli.\f* \c 34 \s1 Dina Na Washekemu \p \v 1 Basi Dina, binti wa Yakobo aliyezaliwa na Lea, akatoka nje kuwatembelea wanawake wa nchi ile. \v 2 Ikawa Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mtawala wa eneo lile alipomwona, akamchukua na kumnajisi. \v 3 Moyo wake ukavutwa sana kwa Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana na akazungumza naye kwa kumbembeleza. \v 4 Shekemu akamwambia baba yake Hamori, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.” \p \v 5 Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani. \p \v 6 Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo. \v 7 Basi wana wa Yakobo walikuwa wamerudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotokea. Walikuwa wamejawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti wa Yakobo, kitu ambacho hakingepasa kufanyika. \p \v 8 Lakini Hamori akawaambia, “Moyo wa mwanangu Shekemu umeelekea kwa binti yenu. Tafadhali mpeni awe mke wake. \v 9 Oaneni na sisi, tupeni binti zenu, nanyi mchukue binti zetu. \v 10 Mwaweza kuishi katikati yetu, nchi ni wazi kwenu. Ishini ndani yake, fanyeni biashara humu na mjipatie mali.” \p \v 11 Kisha Shekemu akamwambia baba yake Dina pamoja na ndugu zake, “Na nipate kibali machoni penu, nami nitawapa chochote mtakachosema. \v 12 Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoileta, hata iwe kubwa kiasi gani, nami nitawalipa chochote mtakachodai. Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.” \p \v 13 Kwa sababu ndugu yao Dina alikuwa amenajisiwa, wana wa Yakobo wakajibu kwa udanganyifu walipozungumza na Shekemu pamoja na baba yake Hamori. \v 14 Wakawaambia, “Hatuwezi kufanya jambo kama hili, hatuwezi kumtoa dada yetu kwa mtu ambaye hakutahiriwa. Hiyo itakuwa aibu kwetu. \v 15 Tutakuruhusu kwa sharti moja tu, kwamba mtakuwa kama sisi kwa kuwatahiri wanaume wenu wote. \v 16 Kisha tutawapa binti zetu na sisi tutawachukua binti zenu. Tutaishi kwenu na tutakuwa watu wamoja nanyi. \v 17 Lakini mkikataa kutahiriwa, tutamchukua ndugu yetu na kuondoka.” \p \v 18 Pendekezo lao likawa jema kwa Hamori na Shekemu mwanawe. \v 19 Kijana mdogo, ambaye alikuwa ameheshimiwa kati ya wote walioishi nyumbani mwa baba yake, hakupoteza muda kufanya waliyoyasema, kwa sababu alikuwa amependezwa sana na binti Yakobo. \v 20 Kwa hiyo Hamori na Shekemu mwanawe walikwenda kwenye lango la mji kuzungumza na wenzao wa mjini. \v 21 Wakasema, “Hawa watu ni marafiki kwetu, tuwaruhusu waishi katika nchi yetu na kufanya biashara ndani yake, nchi ina nafasi tele kwa ajili yao. Tunaweza kuoa binti zao. Nao wanaweza kuoa binti zetu. \v 22 Lakini watu hao watakuwa tayari kukubali kuishi nasi kama watu wamoja nao kwa sharti kwamba wanaume wetu watahiriwe, kama wao. \v 23 Je, si mifugo yao, mali zao na wanyama wao wengine wote watakuwa wetu? Basi na tuwape kibali, nao wataishi miongoni mwetu.” \p \v 24 Wanaume wote waliotoka nje ya lango la mji walikubaliana na Hamori na Shekemu mwanawe na kila mwanaume katika mji ule akatahiriwa. \p \v 25 Baada ya siku tatu, wakati wote wakiwa wangali katika maumivu, wana wawili wa Yakobo, yaani Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua panga zao na kuvamia mji ambao haukutazamia vita, wakaua kila mwanaume. \v 26 Wakawaua Hamori na Shekemu mwanawe kwa upanga kisha wakamchukua Dina kutoka nyumba ya Shekemu na kuondoka. \v 27 Wana wa Yakobo walipita juu ya maiti katika kuteka nyara mji ule ambamo dada yao alikuwa amenajisiwa. \v 28 Wakachukua kondoo na mbuzi, ngʼombe, punda na kila kitu kilichokuwa chao ndani ya mji ule na mashambani. \v 29 Walichukua utajiri wao wote pamoja na wanawake na watoto wao, wakachukua nyara kila kitu ndani ya nyumba zao. \p \v 30 Kisha Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, “Mmeleta taabu kwangu kwa kunifanya ninuke kama uvundo kwa Wakanaani na Waperizi, watu waishio katika nchi hii. Sisi ni wachache, kama wakiunganisha nguvu zao dhidi yangu na kunishambulia, mimi na nyumba yangu tutaangamizwa.” \p \v 31 Lakini wakamjibu, “Je, ilikuwa vyema kumtendea dada yetu kama kahaba?” \c 35 \s1 Yakobo Arudi Betheli \p \v 1 Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.” \p \v 2 Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. \v 3 Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipokwenda.” \v 4 Kwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mti wa mwaloni huko Shekemu. \v 5 Kisha wakaondoka, na hofu ya Mungu ikawapata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo. \p \v 6 Yakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. \v 7 Huko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli,\f + \fr 35:7 \ft El-Betheli maana yake Mungu wa Betheli.\f* kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alipojifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake. \p \v 8 Wakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mti wa mwaloni ulioko chini ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthi.\f + \fr 35:8 \ft Alon-Bakuthi maana yake Mwaloni wa Kilio.\f* \p \v 9 Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. \v 10 Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli. \p \v 11 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi,\f + \fr 35:11 \ft Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\f* ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. \v 12 Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” \v 13 Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye. \p \v 14 Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. \v 15 Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli.\f + \fr 35:15 \ft Betheli maana yake Nyumba ya Mungu.\f* \s1 Vifo Vya Raheli Na Isaki \p \v 16 Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. \v 17 Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” \v 18 Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni.\f + \fr 35:18 \ft Benoni maana yake Mwana wa huzuni yangu.\f* Lakini babaye akamwita Benyamini.\f + \fr 35:18 \ft Benyamini maana yake Mwana wa mkono wangu wa kuume.\f* \p \v 19 Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). \v 20 Juu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli. \p \v 21 Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema mbele mnara wa Ederi. \v 22 Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili. \b \m Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili: \li1 \v 23 Wana wa Lea walikuwa: \li2 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, \li2 Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni. \li1 \v 24 Wana wa Raheli walikuwa: \li2 Yosefu na Benyamini. \li1 \v 25 Wana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa: \li2 Dani na Naftali. \li1 \v 26 Wana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa: \li2 Gadi na Asheri. \p Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu. \b \p \v 27 Yakobo akarudi nyumbani kwa baba yake Isaki huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Abrahamu na Isaki. \v 28 Isaki aliishi miaka 180. \v 29 Kisha Isaki akapumua pumzi yake ya mwisho akafa, akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee wa miaka mingi. Nao wanawe Esau na Yakobo wakamzika. \c 36 \s1 Wazao Wa Esau \r (1 Nyakati 1:34-42) \p \v 1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu). \pm \v 2 Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi, \v 3 pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi. \pm \v 4 Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli, \v 5 Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani. \pm \v 6 Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. \v 7 Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. \v 8 Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri. \p \v 9 Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri. \b \li1 \v 10 Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: \li2 Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia. \li1 \v 11 Wana wa Elifazi ni: \li2 Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi. \li2 \v 12 Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau. \li1 \v 13 Wana wa Reueli ni: \li2 Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau. \li4 \v 14 Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni: \li2 Yeushi, Yalamu na Kora. \b \p \v 15 Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: \li1 Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: \li2 Temani, Omari, Sefo, Kenazi, \v 16 Kora, Gatamu na Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Ada. \li1 \v 17 Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni: \li2 Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau. \li1 \v 18 Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni: \li2 Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana. \p \v 19 Hawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao. \b \p \v 20 Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: \li2 Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, \v 21 Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori. \li1 \v 22 Wana wa Lotani walikuwa: \li2 Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani. \li1 \v 23 Wana wa Shobali walikuwa: \li2 Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. \li1 \v 24 Wana wa Sibeoni walikuwa: \li2 Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake. \li1 \v 25 Watoto wa Ana walikuwa: \li2 Dishoni na Oholibama binti wa Ana. \li1 \v 26 Wana wa Dishoni walikuwa: \li2 Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani. \li1 \v 27 Wana wa Eseri walikuwa: \li2 Bilhani, Zaavani na Akani. \li1 \v 28 Wana wa Dishani walikuwa: \li2 Usi na Arani. \li1 \v 29 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori: \li2 Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, \v 30 Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri. \s1 Watawala Wa Edomu \r (1 Nyakati 1:43-54) \p \v 31 Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala: \li2 \v 32 Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba. \li1 \v 33 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. \li1 \v 34 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. \li1 \v 35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. \li1 \v 36 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. \li1 \v 37 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake. \li1 \v 38 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. \li1 \v 39 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. \b \p \v 40 Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao: \li2 Timna, Alva, Yethethi, \v 41 Oholibama, Ela, Pinoni, \v 42 Kenazi, Temani, Mibsari, \v 43 Magdieli na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki. \p Huyu ndiye alikuwa Esau, baba wa Waedomu. \c 37 \s1 Ndoto Za Yosefu \p \v 1 Yakobo akaishi Kanaani katika nchi ambayo baba yake alikuwa ameishi. \b \p \v 2 Zifuatazo ni habari za Yakobo. \b \p Yosefu, kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akichunga makundi ya kondoo na mbuzi pamoja na ndugu zake wa mama wengine, yaani wana wa Bilha na wana wa Zilpa wake za baba yake, naye akawa akimletea baba yake taarifa mbaya kuhusu hao ndugu zake. \p \v 3 Basi, Israeli akampenda Yosefu kuliko yeyote miongoni mwa kaka zake, kwani ni mwanawe wa uzeeni, akamshonea joho lililorembwa vizuri sana. \v 4 Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yosefu kuliko yeyote mwingine miongoni mwao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema. \p \v 5 Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. \v 6 Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: \v 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.” \p \v 8 Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia. \p \v 9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.” \p \v 10 Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako na mimi na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe hadi nchi?” \v 11 Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni. \s1 Yosefu Auzwa Na Ndugu Zake \p \v 12 Basi, ndugu zake walikuwa wamekwenda kuchunga makundi ya baba yao karibu na Shekemu, \v 13 naye Israeli akamwambia Yosefu, “Kama ujuavyo, ndugu zako wanachunga makundi huko karibu na Shekemu. Njoo, nitakutuma kwao.” \p Yosefu akajibu, “Vema sana, niko tayari.” \p \v 14 Kwa hiyo akamwambia, “Nenda uone kama mambo yote ni salama kwa ndugu zako na makundi, kisha uniletee habari.” Ndipo akamtuma Yosefu kutoka Bonde la Hebroni. \p Yosefu alipofika Shekemu, \v 15 mtu mmoja akamkuta akizungukazunguka mashambani na akamuuliza, “Unatafuta nini?” \p \v 16 Akajibu, “Ninawatafuta ndugu zangu. Unaweza kuniambia wanachunga wapi makundi yao?” \p \v 17 Yule mtu akajibu, “Wamehama hapa. Nilisikia wakisema, ‘Twende Dothani.’ ” \p Kwa hiyo Yosefu akawafuatilia ndugu zake na kuwakuta karibu na Dothani. \v 18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga shauri baya la kumuua. \p \v 19 Wakaambiana, “Yule mwota ndoto anakuja! \v 20 Njooni sasa, tumuue na kumtupa katika shimo mojawapo na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo ya ndoto zake.” \p \v 21 Reubeni aliposikia jambo hili, akajaribu kumwokoa kutoka mikononi mwao akasema, “Tusiutoe uhai wake. \v 22 Tusimwage damu yoyote. Mtupeni katika shimo lililoko hapa jangwani, lakini msimguse.” Reubeni alisema hivyo ili amwokoe kutoka mikononi mwao, kisha amrudishe nyumbani kwa baba yake. \p \v 23 Kwa hiyo Yosefu alipowafikia ndugu zake, walimvua lile joho lake, lile joho lililorembwa vizuri alilokuwa amevaa. \v 24 Kisha wakamchukua wakamtupa katika shimo. Wakati huo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji ndani yake. \p \v 25 Walipokaa ili wale chakula chao, wakainua macho wakaona msafara wa Waishmaeli ukija kutoka Gileadi. Ngamia wao walikuwa wamepakizwa mizigo ya vikolezo, uvumba na manemane, nao walikuwa njiani kuvipeleka Misri. \p \v 26 Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutafaidi nini ikiwa tutamuua ndugu yetu na kuificha damu yake? \v 27 Njooni, tumuuze kwa hawa Waishmaeli. Tusimguse, kwa kuwa hata hivyo yeye ni ndugu yetu, nyama yetu na damu yetu wenyewe.” Ndugu zake wakakubali. \p \v 28 Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini\f + \fr 37:28 \ft Shekeli 20 ni sawa na gramu 200.\f* za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri. \p \v 29 Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake. \v 30 Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?” \p \v 31 Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu. \v 32 Wakalichukua lile joho lililorembwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.” \p \v 33 Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.” \p \v 34 Kisha Yakobo akararua nguo zake, akavaa nguo ya gunia na kumwombolezea mwanawe kwa siku nyingi. \v 35 Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia. \p \v 36 Wakati ule ule, Wamidiani wakamuuza Yosefu huko Misri kwa Potifa, mmojawapo wa maafisa wa Farao, aliyekuwa mkuu wa ulinzi. \c 38 \s1 Yuda Na Tamari \p \v 1 Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake, akaenda kuishi na Hira Mwadulami. \v 2 Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua, akamwoa na akakutana naye kimwili, \v 3 akapata mimba, akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri. \v 4 Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani. \v 5 Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu alimzalia mahali paitwapo Kezibu. \p \v 6 Yuda akampatia Eri, mzaliwa wake wa kwanza, mke aitwaye Tamari. \v 7 Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa \nd Bwana\nd*, kwa hiyo \nd Bwana\nd* akamuua. \p \v 8 Kisha Yuda akamwambia Onani, “Kutana kimwili na mke wa ndugu yako, na utimize wajibu wako kwake kama mke wa ndugu yako, ili umpatie ndugu yako uzao.” \v 9 Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao. \v 10 Alichofanya kilikuwa kiovu machoni pa \nd Bwana\nd*, hivyo, pia \nd Bwana\nd* akamuua Onani. \p \v 11 Kisha Yuda akamwambia Tamari mkwewe, “Ishi kama mjane nyumbani mwa baba yako mpaka mwanangu Shela atakapokua.” Kwa maana alifikiri, “Angeweza kufa pia kama ndugu zake.” Kwa hiyo Tamari alikwenda kuishi nyumbani kwa baba yake. \p \v 12 Baada ya muda mrefu mke wa Yuda binti wa Shua akafariki. Baada ya msiba, Yuda alikwenda Timna, kwa watu waliokuwa wakikata kondoo wake manyoya, naye alifuatana na rafiki yake Hira Mwadulami. \p \v 13 Tamari alipoambiwa, “Baba mkwe wako yuko njiani kwenda Timna kukata kondoo wake manyoya,” \v 14 alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe. \p \v 15 Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake. \v 16 Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.” \p Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?” \p \v 17 Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.” \p Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?” \p \v 18 Akamuuliza, “Nikupe amana gani?” \p Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake. \v 19 Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane. \p \v 20 Wakati ule ule, Yuda akamtuma rafiki yake Mwadulami apeleke yule mwana-mbuzi ili arudishiwe amana yake kutoka kwa yule mwanamke, lakini yule rafiki yake hakumkuta yule mwanamke. \v 21 Akawauliza watu wanaoishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa kuabudia miungu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?” \p Wakamjibu, “Hajawahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.” \p \v 22 Kwa hiyo akamrudia Yuda na kumwambia, “Sikumpata. Zaidi ya hayo, watu wanaoishi mahali pale walisema ‘Hapakuwahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.’ ” \p \v 23 Kisha Yuda akasema, “Mwache avichukue vitu hivyo, ama sivyo tutakuwa kichekesho. Hata hivyo, nilimpelekea mwana-mbuzi, lakini hukumkuta.” \p \v 24 Baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo ana hatia ya kuwa kahaba, na matokeo yake ana mimba.” \p Yuda akasema, “Mtoeni nje na achomwe moto hadi afe!” \p \v 25 Alipokuwa akitolewa nje, akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake kusema, “Nina mimba ya mtu mwenye vitu hivi.” Akaongeza kusema, “Angalia kama utatambua kwamba pete hii na kamba yake pamoja na fimbo hii ni vya nani.” \p \v 26 Yuda akavitambua na kusema, “Yeye ana haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumkabidhi kwa mwanangu Shela ili awe mkewe.” Tangu hapo hakukutana naye kimwili tena. \p \v 27 Wakati ulipofika wa kujifungua, kukawa na wana mapacha tumboni mwake. \v 28 Alipokuwa akijifungua, mmoja akatoa mkono wake nje, kwa hiyo mkunga akachukua uzi mwekundu na kuufunga mkononi mwa yule mtoto, akasema, “Huyu ametoka kwanza.” \v 29 Lakini alipourudisha mkono wake ndugu yake akaanza kutoka, naye akasema, “Hivi ndivyo ulivyotoka kwa nguvu!” Akaitwa Peresi. \v 30 Kisha ndugu yake, aliyekuwa na uzi mwekundu mkononi, akatoka, naye akaitwa Zera. \c 39 \s1 Yosefu Na Mke Wa Potifa \p \v 1 Wakati huu Yosefu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yosefu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. \p \v 2 \nd Bwana\nd* alikuwa pamoja na Yosefu, naye akastawi, Yosefu akaishi nyumbani kwa bwana wake Mmisri. \v 3 Potifa alipoona kuwa \nd Bwana\nd* alikuwa pamoja na Yosefu na kwamba \nd Bwana\nd* alimfanikisha kwa kila kitu alichokifanya, \v 4 Yosefu alipata kibali machoni pa Potifa, akamfanya mhudumu wake. Potifa akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, naye akamkabidhi kuwa mwangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho. \v 5 Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba na mali zake zote alizokuwa nazo, \nd Bwana\nd* aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yosefu. Baraka ya \nd Bwana\nd* ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani. \v 6 Kwa hiyo Potifa akamwachia Yosefu uangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho, Yosefu alipokuwa katika uongozi, Potifa hakuwa na sababu ya kujishughulisha na kitu chochote isipokuwa chakula alichokula. \p Yosefu alikuwa mwenye umbo zuri na sura ya kuvutia; \v 7 baada ya kitambo mke wa Potifa akamtamani Yosefu, akamwambia, “Njoo, ukutane nami kimwili!” \p \v 8 Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi. \v 9 Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi. Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?” \v 10 Ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi Yosefu siku baada ya siku, Yosefu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye. \p \v 11 Siku moja Yosefu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake, wala hapakuwepo na mfanyakazi yeyote ndani ya nyumba. \v 12 Mke wa Potifa akashika vazi Yosefu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yosefu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia. \p \v 13 Yule mwanamke alipoona kwamba Yosefu amemwachia vazi lake mkononi na kukimbilia nje ya nyumba, \v 14 akawaita watumishi wake wa nyumbani, akawaambia, “Tazameni! Huyu Mwebrania ameletwa hapa kutudhihaki! Aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga kelele. \v 15 Aliposikia kelele za kuomba msaada, akaacha vazi lake kando yangu akakimbilia nje.” \p \v 16 Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye mpaka Potifa aliporudi nyumbani. \v 17 Ndipo akamweleza kisa hiki, akisema: “Yule mtumwa wa Kiebrania uliyetuletea alinijia ili kunidhihaki. \v 18 Lakini mara nilipopiga kelele kuomba msaada, akaliacha vazi lake kando yangu akakimbia nje ya nyumba.” \p \v 19 Potifa aliposikia kisa hiki mkewe alichomweleza, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda.” Hasira ya Potifa ikawaka. \v 20 Potifa akamchukua Yosefu na kumweka gerezani, mahali ambapo wahalifu wa mfalme walikuwa wamefungwa. \p Lakini wakati Yosefu alipokuwa huko gerezani, \v 21 \nd Bwana\nd* alikuwa pamoja naye, akamhurumia na kumpa kibali mbele ya msimamizi wa gereza. \v 22 Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani. \v 23 Msimamizi wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote kilichokuwa chini ya uangalizi wa Yosefu, kwa sababu \nd Bwana\nd* alikuwa pamoja na Yosefu akimfanikisha kwa kila alichofanya. \c 40 \s1 Mnyweshaji Na Mwokaji \p \v 1 Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri. \v 2 Farao akawakasirikia hawa maafisa wake wawili, mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, \v 3 akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa kikosi cha ulinzi katika gereza lile lile alimofungwa Yosefu. \v 4 Mkuu wa kikosi cha ulinzi akawakabidhi kwa Yosefu, naye akawahudumia. \p Walipokuwa wamekaa chini ya ulinzi kwa muda, \v 5 kila mmoja wa hao wawili waliokuwa wamewekwa gerezani, yaani mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, waliota ndoto usiku mmoja, na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti. \p \v 6 Yosefu alipowajia asubuhi yake, akawaona kwamba walikuwa na huzuni. \v 7 Ndipo Yosefu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, akasema, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?” \p \v 8 Wakamjibu, “Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri.” \p Ndipo Yosefu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.” \p \v 9 Basi mkuu wa wanyweshaji akamweleza Yosefu ndoto yake. Akamwambia, “Katika ndoto yangu niliona mzabibu mbele yangu, \v 10 nao mzabibu ulikuwa na matawi matatu. Mara tu ulipoanza kuchipua, maua yalichanua na vishada vyake vikawa zabibu zilizoiva. \v 11 Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, na nikaweka kikombe mkononi mwake.” \p \v 12 Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu. \v 13 Katika siku hizi tatu, Farao atakutoa gerezani na kukuweka tena kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mikononi mwake, kama vile ulivyokuwa unafanya ulipokuwa mnyweshaji wake. \v 14 Lakini wakati mambo yatakapokuwia mazuri, unikumbuke, unifanyie wema, useme mema juu yangu kwa Farao ili niondoke huku gerezani. \v 15 Kwa maana nilichukuliwa kwa nguvu kutoka nchi ya Waebrania, na hata hapa nilipo sikufanya lolote linalostahili niwekwe gerezani.” \p \v 16 Yule mwokaji mkuu alipoona kuwa Yosefu amefasiri ikiwa na maana nzuri, akamwambia Yosefu, “Mimi pia niliota ndoto: Kichwani mwangu kulikuwepo vikapu vitatu vya mikate. \v 17 Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kwenye kikapu nilichokuwa nimebeba kichwani.” \p \v 18 Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. \v 19 Katika siku hizi tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako.” \p \v 20 Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake: \v 21 Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mikononi mwa Farao tena, \v 22 lakini akamwangika yule mwokaji mkuu, sawasawa na jinsi Yosefu alivyowaambia katika tafsiri yake. \p \v 23 Pamoja na hayo, mnyweshaji mkuu hakumkumbuka Yosefu, bali alimsahau. \c 41 \s1 Ndoto Za Farao \p \v 1 Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, \v 2 wakati ngʼombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete. \v 3 Baada yao ngʼombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Naili wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. \v 4 Wale ngʼombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka. \p \v 5 Farao akaingia usingizini tena akaota ndoto ya pili: Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja. \v 6 Baadaye, masuke mengine saba yakachipua, yakiwa membamba yaliyonyaushwa na upepo wa mashariki. \v 7 Masuke yale membamba yakameza yale masuke saba yenye afya na yaliyojaa. Basi Farao akaamka kutoka usingizini, kumbe ilikuwa ndoto. \p \v 8 Asubuhi yake, alifadhaika akilini, hivyo akawaita waaguzi wote pamoja na watu wenye busara wa Misri. Walipokuja, Farao akawaeleza ndoto zake, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumfasiria. \p \v 9 Ndipo mnyweshaji mkuu alipomwambia Farao, “Leo nimekumbushwa kuhusu kosa langu. \v 10 Wakati fulani Farao aliwakasirikia watumishi wake, akanifunga mimi na mwokaji mkuu katika nyumba ya mkuu wa ulinzi. \v 11 Kila mmoja wetu aliota ndoto katika usiku mmoja na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti. \v 12 Basi kijana wa Kiebrania aliyekuwa pamoja nasi huko, alikuwa mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi. Tulimweleza ndoto zetu, naye akatufasiria, akitupa kila mtu tafsiri ya ndoto yake. \v 13 Nayo mambo yakawa sawa kabisa na jinsi alivyotufasiria ndoto zetu: Mimi nilirudishwa kazini mwangu na huyo mtu mwingine akaangikwa.” \p \v 14 Basi, Farao akatuma Yosefu aitwe, naye akatolewa kifungoni haraka. Baada ya kunyoa na kubadilisha nguo zake akaenda mbele ya Farao. \p \v 15 Farao akamwambia Yosefu, “Nimeota ndoto, wala hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuifasiri. Lakini nimesikia ikisemwa kwa habari yako kwamba unapoelezwa ndoto waweza kuifasiri.” \p \v 16 Yosefu akamjibu Farao, “Siwezi kuifasiri, lakini Mungu atampa Farao jibu analolihitaji.” \p \v 17 Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Katika ndoto yangu nilikuwa nimesimama ukingoni mwa Mto Naili, \v 18 nikawaona ngʼombe saba, wazuri na wanono, wakijitokeza kutoka mtoni wakaja kujilisha kwenye matete. \v 19 Baada ya hao, ngʼombe wengine saba wadhaifu wakatokea, wabaya sana na waliokonda. Kamwe sikuwahi kuona ngʼombe wabaya jinsi hiyo katika nchi yote ya Misri. \v 20 Hao ngʼombe waliokonda na wabaya sana wakawala wale ngʼombe saba walionona waliojitokeza kwanza. \v 21 Lakini hata baada ya kuwala, hakuna mtu ambaye angeweza kusema kwamba wamekula, bado walionekana wabaya kama mwanzoni. Kisha nikaamka kutoka usingizini. \p \v 22 “Pia katika ndoto zangu niliona masuke saba ya nafaka, yamejaa na mazuri, yanakua katika bua moja. \v 23 Baada ya hayo masuke mengine saba yakachipua, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki. \v 24 Yale masuke membamba ya nafaka yakayameza yale masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka. Nimewaeleza waaguzi, wala hakuna yeyote aliyeweza kunifasiria.” \p \v 25 Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni ndoto iyo hiyo moja. Mungu amemfunulia Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. \v 26 Ngʼombe saba wazuri ni miaka saba, nayo masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka ni miaka saba, ni ndoto iyo hiyo moja. \v 27 Ngʼombe saba waliokonda na wabaya wale waliojitokeza baadaye ni miaka saba, vivyo hivyo masuke saba ya ngano yaliyodhoofika na kukaushwa na upepo wa mashariki, ni miaka saba ya njaa. \p \v 28 “Ni kama vile nilivyomwambia Farao: Mungu amemwonyesha Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. \v 29 Miaka saba ya neema inakuja katika nchi yote ya Misri, \v 30 lakini itafuata miaka saba ya njaa. Ndipo neema yote ya Misri itasahaulika na njaa itaikumba nchi. \p \v 31 “Neema iliyokuwa katika nchi haitakumbukwa, kwa sababu njaa itakayofuata itakuwa kali mno. \v 32 Sababu ya ndoto kumjia Farao kwa namna mbili ni kwamba jambo hilo Mungu ameshaamua kwa hakika, naye Mungu atalifanya karibuni. \p \v 33 “Basi sasa Farao na atafute mtu mwenye akili na hekima ili amweke kuwa msimamizi wa nchi ya Misri. \v 34 Farao na aweke wenye amri nchini kote wakusanye sehemu ya tano ya mavuno ya Misri katika miaka hii saba ya neema. \v 35 Wakusanye chakula chote katika miaka hii saba ya neema inayokuja na kuhifadhi nafaka chini ya mamlaka ya Farao, iwe akiba ya chakula katika miji. \v 36 Chakula hiki kitakuwa akiba ya tahadhari kwa ajili ya nchi, ili kitumike katika ile miaka saba ya njaa itakayokuja Misri, ili nchi isiharibiwe na njaa.” \p \v 37 Mpango huu ulionekana mzuri kwa Farao na kwa maafisa wake wote. \v 38 Hivyo Farao akawauliza, “Je tunaweza kumpata yeyote kama mtu huyu, ambaye Roho wa Mungu yumo ndani yake?” \p \v 39 Ndipo Farao akamwambia Yosefu, “Maadamu Mungu amekufunulia yote haya, hakuna mwingine yeyote mwenye akili na hekima kama wewe. \v 40 Wewe utakuwa msimamizi wa jumba langu la kifalme, na watu wangu wote watatii amri zako. Ni kuhusu kiti cha ufalme tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.” \s1 Yosefu Msimamizi Wa Misri \p \v 41 Kwa hiyo Farao akamwambia Yosefu, “Sasa nakuweka uwe msimamizi wa nchi yote ya Misri.” \v 42 Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yosefu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. \v 43 Akampandisha katika gari lake la farasi kama msaidizi wake, watu wakatangulia wakishangilia, wakisema, “Fungueni njia!” Ndivyo Farao alivyomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri. \p \v 44 Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Mimi ni Farao, lakini pasipo neno lako, hakuna mtu mwenye ruhusa kuinua mkono au mguu katika nchi yote ya Misri.” \v 45 Farao akamwita Yosefu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni,\f + \fr 41:45 \ft Yaani Heliopoli (Mji wa Jua).\f* kuwa mke wake. Ndipo Yosefu akaitembelea nchi yote ya Misri. \p \v 46 Yosefu alikuwa na miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao mfalme wa Misri. Naye Yosefu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri. \v 47 Katika ile miaka saba ya neema nchi ilizaa mazao kwa wingi sana. \v 48 Yosefu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya neema nchini Misri, akakihifadhi katika ghala za miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo. \v 49 Yosefu alihifadhi nafaka nyingi, mfano wa mchanga wa bahari, ilikuwa nyingi mno kiasi kwamba walishindwa kuweka kumbukumbu kwa sababu akiba ilizidi sana kupita kipimo. \p \v 50 Kabla ya miaka ya njaa kuanza, Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, alikuwa amemzalia Yosefu wana wawili wa kiume. \v 51 Yosefu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenifanya nisahau taabu zangu zote pamoja na jamaa yote ya nyumba ya baba yangu.” \v 52 Mwana wa pili akamwita Efraimu, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenistawisha katika nchi ya mateso yangu.” \p \v 53 Ile miaka saba ya neema huko Misri ikaisha, \v 54 nayo miaka ile saba ya njaa ikaanza, sawasawa na alivyosema Yosefu. Kulikuwa na njaa katika nchi nyingine zote, bali katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula. \v 55 Wakati nchi yote ya Misri ilipopatwa na njaa, watu wakamlilia Farao ili awape chakula. Ndipo Farao alipowaagiza Wamisri wote, akisema, “Nendeni kwa Yosefu, nanyi mfanye anachowaambia.” \p \v 56 Wakati njaa ilipokuwa imeenea katika nchi yote, Yosefu akafungua ghala za vyakula na kuwauzia Wamisri nafaka, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno katika nchi yote ya Misri. \v 57 Pia nchi nyingine zote zilikuja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yosefu, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno duniani kote. \c 42 \s1 Ndugu Za Yosefu Waenda Misri \p \v 1 Wakati Yakobo alipofahamu kuwa kuna nafaka huko Misri, akawaambia wanawe, “Mbona mnakaa tu hapa mnatazamana?” \v 2 Akaendelea kuwaambia, “Nimesikia kuwa huko Misri kuna nafaka. Telemkeni huko mkanunue chakula kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi wala tusife.” \p \v 3 Ndipo wale ndugu kumi wa Yosefu, wakateremka huko Misri kununua nafaka. \v 4 Lakini Yakobo hakumtuma Benyamini, ndugu yake Yosefu, pamoja na wengine, kwa sababu aliogopa asije akapatwa na madhara. \v 5 Hivyo wana wa Israeli walikuwa miongoni mwa wale waliokwenda Misri kununua nafaka, kwani njaa ilikuwa katika nchi ya Kanaani pia. \p \v 6 Wakati huo Yosefu alikuwa mtawala wa nchi ya Misri, naye alikuwa ndiye aliwauzia watu wote nafaka. Kwa hiyo wakati ndugu zake Yosefu walipofika, wakamsujudia hadi nyuso zao zikagusa ardhi. \v 7 Mara Yosefu alipowaona ndugu zake, akawatambua, lakini akajifanya mgeni na kuzungumza nao kwa ukali, akiwauliza, “Ninyi mnatoka wapi?” \p Wakamjibu, “Tumetoka katika nchi ya Kanaani kuja kununua chakula.” \p \v 8 Ingawa Yosefu aliwatambua ndugu zake, wao hawakumtambua. \v 9 Ndipo Yosefu alipokumbuka ndoto zake kuwahusu wao, akawaambia, “Ninyi ni wapelelezi! Mmekuja kuangalia mahali ambapo nchi yetu haina ulinzi.” \p \v 10 Wakamjibu, “Sivyo bwana wangu. Watumishi wako wamekuja kununua chakula. \v 11 Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Watumishi wako ni watu waaminifu, wala sio wapelelezi.” \p \v 12 Akawaambia, “La hasha! Mmekuja kuangalia mahali ambapo nchi yetu haina ulinzi.” \p \v 13 Lakini wakamjibu, “Watumishi wako walikuwa kumi na wawili, wana wa mtu mmoja ambaye anaishi katika nchi ya Kanaani. Sasa mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu na mwingine alikufa.” \p \v 14 Yosefu akawaambia, “Ni sawa kabisa kama nilivyowaambia: Ninyi ni wapelelezi! \v 15 Na hivi ndivyo mtakavyojaribiwa: Hakika kama Farao aishivyo, hamtaondoka mahali hapa mpaka ndugu yenu mdogo aje hapa. \v 16 Tumeni mmoja wenu akamlete huyo ndugu yenu, wengine mtawekwa gerezani, ili maneno yenu yajaribiwe kuona kama mnasema kweli. La sivyo, hakika kama Farao aishivyo ninyi ni wapelelezi!” \v 17 Akawaweka wote chini ya ulinzi kwa siku tatu. \p \v 18 Siku ya tatu Yosefu akawaambia, “Fanyeni hili nanyi mtaishi, kwa maana namwogopa Mungu: \v 19 Ikiwa ninyi ni watu waaminifu, mmoja wa ndugu zenu na abaki kifungoni, nanyi wengine pelekeni nafaka kwa jamaa yenu wanaoteseka kwa njaa. \v 20 Lakini ni lazima mniletee ndugu yenu mdogo hapa, ili maneno yenu yathibitike na kwamba msife.” Wakakubali kufanya hivyo. \p \v 21 Wakaambiana wao kwa wao, “Hakika tunaadhibiwa kwa sababu ya ndugu yetu. Tuliona jinsi alivyohuzunika alipokuwa anatusihi kuponya maisha yake, lakini hatukumsikiliza, hiyo ndiyo sababu dhiki hii imetupata.” \p \v 22 Reubeni akawajibu, “Sikuwaambieni msitende dhambi dhidi ya kijana? Lakini hamkunisikiliza! Sasa ni lazima tuadhibiwe kwa ajili ya damu yake.” \v 23 Hawakujua kuwa Yosefu angewaelewa, kwa sababu alitumia mkalimani. \p \v 24 Yosefu akajitenga nao akaanza kulia, kisha akawarudia na kuzungumza nao tena. Akataka Simeoni akamatwe na kufungwa mbele yao. \p \v 25 Yosefu akatoa amri ya kujaza magunia yao nafaka na kuweka fedha ya kila mmoja ndani ya gunia lake, kisha wapewe mahitaji ya njiani. Baada ya kufanyiwa hayo yote, \v 26 wakapakiza nafaka juu ya punda zao, wakaondoka. \p \v 27 Walipofika mahali pa kulala huko njiani mmoja wao akafungua gunia lake ili amlishe punda wake, akakuta fedha yake kwenye mdomo wa gunia lake. \v 28 Akawaambia ndugu zake, “Fedha yangu imerudishwa. Iko ndani ya gunia langu.” \p Mioyo yao ikazimia, na kila mmoja akamgeukia mwenzake wakitetemeka, wakaulizana, “Ni nini hiki Mungu alichotufanyia?” \p \v 29 Walipofika kwa Yakobo baba yao katika nchi ya Kanaani, wakamweleza mambo yote yaliyowapata. Wakasema, \v 30 “Huyo mtu ambaye ndiye bwana katika nchi hiyo alisema nasi kwa ukali, akatutendea kana kwamba sisi tulikuwa tunaipeleleza nchi. \v 31 Lakini tulimwambia, ‘Sisi ni watu waaminifu, sio wapelelezi. \v 32 Tulizaliwa ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja. Mmoja alikufa, na mdogo wetu wa mwisho yupo na baba yetu huko Kanaani.’ \p \v 33 “Ndipo huyo mtu aliye bwana katika nchi hiyo alipotuambia, ‘Hivi ndivyo nitafahamu kuwa ninyi ni watu waaminifu: Mwacheni mmoja wa ndugu zenu pamoja nami hapa, kisha nendeni mpeleke chakula kwa ajili ya jamaa yenu inayoteseka kwa njaa. \v 34 Lakini mleteni huyo ndugu yenu mdogo kwangu, ndipo nitajua kuwa ninyi sio wapelelezi, ila ni watu waaminifu. Kisha nitamrudisha ndugu yenu, nanyi mtaweza kufanya biashara katika nchi hii.’ ” \p \v 35 Walipokuwa wanamimina nafaka kutoka kwenye magunia yao, ndani ya gunia la kila mtu kulikuwa na mfuko wa fedha! Wakati wao na baba yao walipoona mifuko ya fedha, wakaogopa. \v 36 Yakobo baba yao akawaambia, “Ninyi mmenipokonya watoto wangu. Yosefu hayupo na Simeoni hayupo tena na sasa mnataka kumchukua Benyamini. Kila kitu ni kinyume nami!” \p \v 37 Ndipo Reubeni akamwambia baba yake, “Waweza kuwaua wanangu wote wawili, ikiwa sitamrudisha Benyamini kwako. Mkabidhi Benyamini katika uangalizi wangu, nami nitamrudisha.” \p \v 38 Lakini Yakobo akasema, “Mwanangu hatashuka huko pamoja nanyi; ndugu yake amekufa naye ndiye peke yake aliyebaki. Ikiwa atapatwa na madhara katika safari mnayoiendea, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini kwa masikitiko.” \c 43 \s1 Safari Ya Pili Ya Kwenda Misri \p \v 1 Wakati huu njaa ilikuwa bado ni kali mno katika nchi. \v 2 Hivyo wakati walikuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, Yakobo baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine zaidi.” \p \v 3 Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu yenu.’ \v 4 Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutakwenda kuwanunulia chakula. \v 5 Lakini ikiwa hutamruhusu aende, hatutakwenda, kwa sababu mtu yule alituambia, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje pamoja na ndugu yenu.’ ” \p \v 6 Israeli akauliza, “Kwa nini mkaniletea taabu hii kwa kumwambia yule mtu mlikuwa na ndugu mwingine?” \p \v 7 Wakamjibu, “Yule mtu alituhoji kwa undani sana habari zetu na za jamaa yetu. Alituuliza, ‘Je, baba yenu bado yungali hai? Je mnaye ndugu mwingine?’ Sisi tulimjibu maswali yake tu. Tungewezaje kujua kwamba angesema, ‘Mleteni mdogo wenu hapa’?” \p \v 8 Ndipo Yuda akamwambia baba yake Israeli, “Mtume kijana pamoja nami, nasi tutaondoka mara, ili sisi na wewe pamoja na watoto wetu tuweze kuishi, wala tusife. \v 9 Mimi mwenyewe nitakuhakikishia usalama wake, mimi mwenyewe nitawajibika kumrudisha. Ikiwa sitamrudisha kwako na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako maisha yangu yote. \v 10 Hakika, kama hatukuchelewa kuondoka, tungekuwa tumekwenda na kurudi mara mbili.” \p \v 11 Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni baadhi ya mazao bora ya nchi katika mifuko yenu na mpelekeeni yule mtu kama zawadi, zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi. \v 12 Chukueni fedha mara mbili, kwa kuwa mtazirudisha zile fedha zilizowekwa midomoni mwa magunia yenu. Labda ziliwekwa kwa makosa. \v 13 Mchukueni ndugu yenu pia mrudi kwa huyo mtu mara moja. \v 14 Naye Mungu Mwenyezi\f + \fr 43:14 \ft Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\f* awajalieni rehema mbele ya huyo mtu ili apate kumwachia yule ndugu yenu na Benyamini mweze kurudi pamoja. Kwangu mimi kama nikufiwa nimefiwa.” \p \v 15 Basi hao watu wakazichukua zile zawadi na zile fedha mara mbili pamoja na Benyamini. Wakafanya haraka kwenda Misri na walipofika wakajionyesha kwa Yosefu. \v 16 Yosefu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, “Wachukue watu hawa nyumbani kwangu, mchinje mnyama na kuandalia chakula kwa kuwa watakula chakula cha mchana pamoja nami.” \p \v 17 Yule Msimamizi akafanya kama Yosefu alivyomwambia na akawachukua wale watu nyumbani kwa Yosefu. \v 18 Basi watu hao wakaogopa walipopelekwa nyumbani kwa Yosefu. Wakafikiri, “Tumeletwa hapa kwa ajili ya zile fedha zilizorudishwa katika magunia yetu mara ile ya kwanza. Anataka kutushambulia na kutushinda, atuchukue sisi kama watumwa, na atwae hawa punda zetu.” \p \v 19 Hivyo wakamwendea msimamizi wa nyumba wa Yosefu na kuzungumza naye kwenye ingilio la nyumbani. \v 20 Wakasema, “Tafadhali bwana, tulikuja hapa mara ya kwanza kununua chakula. \v 21 Lakini mahali pale tulipotua wakati wa jioni tulifungua magunia yetu, na kila mmoja wetu akakuta fedha zake, kwenye mdomo wa gunia lake kiasi kile kile tulicholeta. Kwa hiyo tumezirudisha. \v 22 Pia tumeleta fedha nyingine kwa ajili ya kununulia chakula. Hatujui ni nani aliziweka fedha hizo katika magunia yetu.” \p \v 23 Akawaambia, “Vema, msiogope. Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, amewapa ninyi hazina katika magunia yenu; mimi nilipokea fedha yenu.” Ndipo akawaletea Simeoni. \p \v 24 Msimamizi akawapeleka wale watu katika nyumba ya Yosefu, akawapa maji ya kunawa miguu na kuwapa punda wao majani. \v 25 Wakaandaa zawadi zao ili wampe Yosefu wakati atakapofika adhuhuri, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba watakula chakula huko. \p \v 26 Yosefu alipokuja nyumbani, walimkabidhi zile zawadi walizokuwa nazo, ambazo walikuwa wamezileta mle nyumbani, nao wakamsujudia hadi nchi. \v 27 Akawauliza kuhusu hali yao, kisha akawaambia, “Yule baba yenu mzee mliyeniambia habari zake, yu hali gani? Je, bado yu hai?” \p \v 28 Wakamjibu, “Mtumishi wako baba yetu bado anaishi na ni mzima.” Kisha wakainama chini kumpa heshima. \p \v 29 Alipotazama na kumwona Benyamini ndugu yake, mwana wa mama yake hasa, akauliza, “Je, huyu ndiye ndugu yenu wa mwisho, ambaye mlinieleza habari zake?” Ndipo akasema, “Mungu na akufadhili, mwanangu.” \v 30 Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yosefu akatoka nje kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo. \p \v 31 Baada ya kunawa uso wake, akatoka nje na huku akijizuia akasema, “Pakueni chakula.” \p \v 32 Wakampakulia Yosefu peke yake, ndugu zake peke yao na Wamisri waliokula pamoja naye peke yao, kwa sababu Wamisri wasingeweza kula pamoja na Waebrania, kwa maana ilikuwa ni chukizo kwa Wamisri. \v 33 Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao. \v 34 Wakati walipelekewa sehemu ya chakula kutoka mezani mwa Yosefu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye. \c 44 \s1 Kikombe Cha Fedha Ndani Ya Gunia \p \v 1 Kisha Yosefu akampa yule msimamizi wa nyumbani mwake maagizo haya: “Jaza magunia ya watu hawa kiasi cha chakula ambacho wanaweza kuchukua, na uweke fedha ya kila mtu kwenye mdomo wa gunia lake. \v 2 Kisha weka kikombe changu kile cha fedha kwenye mdomo wa gunia la yule mdogo wa wote pamoja na fedha zake ambazo angenunulia nafaka yake.” Naye akafanya kama Yosefu alivyosema. \p \v 3 Kulipopambazuka, hao watu wakaruhusiwa kuondoka pamoja na punda zao. \v 4 Kabla hawajafika mbali kutoka mjini, Yosefu akamwambia mtumishi wake, “Wafuatilie wale watu mara moja, utakapowakuta, waambie, ‘Kwa nini mmelipiza wema kwa ubaya? \v 5 Je, kikombe hiki sicho anachonywea bwana wangu na pia hukitumia kwa kutabiri mambo yajayo? Hili ni jambo ovu mlilolitenda.’ ” \p \v 6 Alipowafikia, akarudia maneno haya kwao. \v 7 Lakini wakamwambia mtumishi, “Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Liwe mbali na watumishi wako wasije wakafanya jambo kama hilo! \v 8 Hata hivyo tulikurudishia zile fedha kutoka nchi ya Kanaani ambazo tulizikuta kwenye midomo ya magunia yetu. Hivyo kwa nini tuibe fedha au dhahabu kutoka nyumbani kwa bwana wako? \v 9 Ikiwa yeyote miongoni mwa watumishi wako atapatikana nacho, auawe, na sisi wengine tutakuwa watumwa wa bwana wangu.” \p \v 10 Akajibu, “Vema sana; na iwe kama msemavyo. Yeyote atakayekutwa nacho atakuwa mtumwa wangu, lakini ninyi wengine mtakuwa hamna lawama.” \p \v 11 Kila mmoja wao akafanya haraka kushusha gunia lake chini na kulifungua. \v 12 Ndipo msimamizi akaendelea kutafuta, akianzia kwa mkubwa wa wote na akaishia kwa mdogo wa wote. Basi kikombe kikapatikana katika gunia la Benyamini. \v 13 Kwa jambo hili, wakararua nguo zao. Ndipo wote wakapakiza mizigo yao juu ya punda zao na kurudi mjini. \p \v 14 Yosefu alikuwa bado yuko nyumbani mwake wakati Yuda na kaka zake walipoingia, wote wakajitupa chini mbele yake. \v 15 Yosefu akawaambia, “Ni jambo gani hili mlilolifanya? Hamjui kuwa mtu kama mimi anaweza kufahamu mambo kwa njia ya kutabiri?” \p \v 16 Yuda akajibu, “Tutaweza kusema nini kwa bwana wangu? Tutaweza kuzungumza nini? Tutawezaje kuthibitisha kwamba hatuna hatia? Mungu amefunua hatia ya watumishi wako. Sasa sisi tu watumwa wa bwana wangu, sisi wenyewe pamoja na yule aliyepatikana na kikombe.” \p \v 17 Lakini Yosefu alisema, “Liwe mbali nami kufanya jambo kama hili! Mtu yule tu aliyekutwa na kikombe ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Ninyi wengine, rudini kwa baba yenu kwa amani.” \p \v 18 Ndipo Yuda akamwendea na kumwambia: “Tafadhali bwana wangu, mruhusu mtumishi wako aseme neno kwa bwana wangu. Usimkasirikie mtumishi wako, ingawa wewe ni sawa na Farao mwenyewe. \v 19 Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, ‘Mnaye baba au ndugu?’ \v 20 Nasi tukakujibu, ‘Tunaye baba yetu ambaye ni mzee; pia yupo mwanawe mdogo aliyezaliwa katika uzee wake. Ndugu yake amekufa, na huyu mdogo ndiye mwana pekee kwa mama yake aliyebaki, naye baba yake anampenda.’  \p \v 21 “Ndipo ulipowaambia watumishi wako, ‘Mleteni kwangu ili niweze kumwona kwa macho yangu mwenyewe.’ \v 22 Nasi tukamwambia bwana wangu, ‘Kijana hawezi kumwacha baba yake; akimwacha, baba yake atakufa.’ \v 23 Lakini ukawaambia watumishi wako, ‘Ndugu yenu mdogo asiposhuka pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.’ \v 24 Tuliporudi nyumbani kwa mtumwa wako baba yangu, tulimwambia lile bwana wangu alilokuwa amesema. \p \v 25 “Ndipo baba yetu aliposema, ‘Rudini Misri mkanunue chakula kingine.’ \v 26 Lakini tukamwambia, ‘Hatuwezi kushuka Misri mpaka ndugu yetu mdogo awe pamoja nasi ndipo tutakapokwenda. Hatutaweza kuuona uso wa yule mtu mpaka ndugu yetu mdogo awe pamoja nasi.’ \p \v 27 “Mtumwa wako baba yangu alituambia, ‘Mnajua mke wangu alinizalia wana wawili. \v 28 Mmojawapo alipotea, nami nikasema, “Hakika ameraruliwa vipande vipande.” Nami sijamwona tangu wakati huo. \v 29 Ikiwa mtaniondolea huyu tena na akapatwa na madhara, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini nikiwa mwenye huzuni.’ \p \v 30 “Hivyo sasa, kama kijana hatakuwa pamoja nasi nitakaporudi kwa mtumishi wako baba yangu, na kama baba yangu, ambaye maisha yake yamefungamanishwa na uhai wa kijana huyu, \v 31 akiona kijana hayupo nasi, atakufa. Watumishi wako watashusha kichwa chenye mvi cha baba yetu kaburini kwa huzuni. \v 32 Mtumwa wako alimhakikishia baba yangu usalama wa kijana. Nikamwambia, ‘Kama sikumrudisha kwako nitakuwa mwenye lawama mbele yako, baba yangu, maisha yangu yote!’ \p \v 33 “Sasa basi, tafadhali mruhusu mtumishi abaki hapa kama mtumwa wa bwana wangu badala ya kijana, naye kijana umruhusu arudi na ndugu zake. \v 34 Ninawezaje kurudi kwa baba yangu kama kijana hatakuwa pamoja nami? La hasha! Usiniache nikaone huzuni ile itakayompata baba yangu.” \c 45 \s1 Yosefu Anajitambulisha \p \v 1 Hapo Yosefu hakuweza kujizuia zaidi mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye, akapaza sauti, akasema, “Mwondoeni kila mtu mbele yangu!” Kwa hiyo hapakuwepo mtu yeyote pamoja na Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake. \v 2 Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari. \p \v 3 Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yosefu! Je, baba yangu angali hai bado?” Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake. \p \v 4 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Sogeeni karibu nami.” Waliposogea, akasema, “Mimi ni ndugu yenu Yosefu, yule ambaye mlimuuza Misri! \v 5 Sasa, msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu ilikuwa ni ili kuokoa maisha ya watu ndiyo sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi. \v 6 Kwa miaka miwili sasa imekuwepo njaa katika nchi, pia kwa miaka mitano ijayo hapatakuwepo kulima wala kuvuna. \v 7 Lakini Mungu alinitanguliza mbele yenu ili kuhifadhi mabaki kwa ajili yenu katika nchi, na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu. \p \v 8 “Kwa hiyo basi, si ninyi mlionileta huku, bali ni Mungu. Alinifanya kuwa baba kwa Farao, bwana wa watu wa nyumbani mwake wote, na mtawala wa Misri yote. \v 9 Sasa rudini haraka kwa baba yangu na mwambieni, ‘Hili ndilo mwanao Yosefu asemalo: Mungu amenifanya mimi kuwa bwana wa Misri yote. Shuka uje kwangu, wala usikawie. \v 10 Nawe utaishi katika nchi ya Gosheni na kuwa karibu nami, wewe, watoto wako na wajukuu wako, makundi yako ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, pamoja na vyote ulivyo navyo. \v 11 Nitawatunza huko, kwa sababu bado iko miaka mingine mitano inayokuja ya njaa. La sivyo, wewe na nyumba yako na wote ulio nao mtakuwa fukara.’ \p \v 12 “Mnaweza kujionea wenyewe, hata ndugu yangu Benyamini, kwamba hakika ni mimi ninayezungumza nanyi. \v 13 Mwambieni baba yangu juu ya heshima yote niliyopewa huku Misri, na kuhusu kila kitu mlichokiona. Mleteni baba yangu huku haraka.” \p \v 14 Ndipo akamkumbatia Benyamini ndugu yake na kulia, naye Benyamini akamkumbatia akilia. \v 15 Pia akawabusu ndugu zake wote, huku akilia. Baada ya hayo ndugu zake wakazungumza naye. \p \v 16 Habari zilipofika kwenye jumba la Farao kwamba ndugu zake Yosefu wamefika, Farao na maafisa wake wote wakafurahi. \v 17 Farao akamwambia Yosefu, “Waambie ndugu zako, ‘Fanyeni hivi: Pakieni wanyama wenu mrudi mpaka nchi ya Kanaani, \v 18 mkamlete baba yenu na jamaa zenu kwangu. Nitawapa sehemu nzuri sana ya nchi ya Misri nanyi mtafurahia unono wa nchi.’ \p \v 19 “Mnaagizwa pia kuwaambia, ‘Fanyeni hivi: Chukueni magari ya kukokotwa kutoka Misri, kwa ajili ya watoto wenu na wake zenu, mkamchukue baba yenu mje. \v 20 Msijali kamwe kuhusu mali zenu, kwa sababu mema yote ya Misri yatakuwa yenu.’ ” \p \v 21 Hivyo wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yosefu akawapa magari ya kukokotwa, kama Farao alivyoagiza, pia akawapa mahitaji kwa ajili ya safari yao. \v 22 Kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli 300\f + \fr 45:22 \ft Shekeli 300 za fedha ni sawa na kilo 3.4.\f* za fedha, na jozi tano za nguo. \v 23 Hivi ndivyo vitu alivyotuma kwa baba yake: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri, punda wake kumi waliobeba nafaka, mikate na mahitaji mengine ya safari. \v 24 Akaagana na ndugu zake walipokuwa wakiondoka, akawaambia, “Msigombane njiani!” \p \v 25 Basi wakatoka Misri na kufika kwa baba yao Yakobo katika nchi ya Kanaani. \v 26 Wakamwambia baba yao, “Yosefu angali hai! Ukweli ni kwamba yeye ndiye mtawala wa Misri yote.” Yakobo akapigwa na bumbuazi; hakuwasadiki. \v 27 Lakini walipokwisha kumweleza kila kitu ambacho Yosefu alikuwa amewaambia, na alipoona magari ya kukokotwa Yosefu aliyokuwa amempelekea ya kumchukua aende Misri, roho ya baba yao Yakobo ikahuishwa. \v 28 Ndipo Israeli akasema, “Nimesadiki! Mwanangu Yosefu bado yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.” \c 46 \s1 Yakobo Aenda Misri \p \v 1 Hivyo Israeli akaondoka na vyote vilivyokuwa mali yake, naye alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaki baba yake. \p \v 2 Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!” \p Akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 3 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa. \v 4 Nitashuka Misri pamoja nawe, nami hakika nitakurudisha tena Kanaani. Mikono ya Yosefu mwenyewe ndiyo itakayofunga macho yako.” \p \v 5 Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha. \v 6 Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani, Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri. \v 7 Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri. \b \p \v 8 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri: \b \li1 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. \li1 \v 9 Wana wa Reubeni ni: \li2 Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. \li1 \v 10 Wana wa Simeoni ni: \li2 Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. \li1 \v 11 Wana wa Lawi ni: \li2 Gershoni, Kohathi na Merari. \li1 \v 12 Wana wa Yuda ni: \li2 Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). \li2 Wana wa Peresi ni: \li3 Hesroni na Hamuli. \li1 \v 13 Wana wa Isakari ni: \li2 Tola, Puva, Yashubu na Shimroni. \li1 \v 14 Wana wa Zabuloni ni: \li2 Seredi, Eloni na Yaleeli. \p \v 15 Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu pamoja na binti yake Dina. Jumla ya wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu. \b \li1 \v 16 Wana wa Gadi ni: \li2 Sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli. \li1 \v 17 Wana wa Asheri ni: \li2 Imna, Ishva, Ishvi na Beria. \li2 Dada yao alikuwa Sera. \li2 Wana wa Beria ni: \li2 Heberi na Malkieli. \p \v 18 Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambao Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita. \b \li1 \v 19 Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni: \li2 Yosefu na Benyamini. \v 20 Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni,\f + \fr 46:20 \ft Yaani Heliopoli (Mji wa Jua).\f* alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu. \li1 \v 21 Wana wa Benyamini ni: \li2 Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi. \p \v 22 Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne. \b \li1 \v 23 Mwana wa Dani ni: \li2 Hushimu. \li1 \v 24 Wana wa Naftali ni: \li2 Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu. \p \v 25 Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba. \b \p \v 26 Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita. \v 27 Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yosefu huko Misri, jumla yote ya jamaa ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini. \b \p \v 28 Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yosefu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni, \v 29 gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu. \p \v 30 Israeli akamwambia Yosefu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.” \p \v 31 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu. \v 32 Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ngʼombe pamoja na kila kitu walicho nacho.’ \v 33 Farao atakapowaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’ \v 34 Mjibuni, ‘Watumwa wako wamekuwa wachunga mifugo tangu ujana wetu mpaka sasa, kama baba zetu walivyofanya.’ Ndipo mtakaporuhusiwa kukaa katika nchi ya Gosheni, kwa kuwa wachunga mifugo wote ni chukizo kwa Wamisri.” \c 47 \s1 Yakobo Ambariki Farao \p \v 1 Yosefu akaenda na kumwambia Farao, “Baba yangu na ndugu zangu wamekuja kutoka nchi ya Kanaani wakiwa na makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, pamoja na kila kitu walicho nacho, nao sasa wapo huko Gosheni.” \v 2 Akachagua ndugu zake watano na kuwaonyesha kwa Farao. \p \v 3 Farao akawauliza hao ndugu zake, “Kazi yenu ni nini?” \p Wakamjibu, “Watumishi wako ni wachunga mifugo, kama vile baba zetu walivyokuwa.” \v 4 Pia wakamwambia Farao, “Tumekuja kukaa huku kwa muda mfupi, kwa sababu njaa ni kali huko Kanaani, na mifugo ya watumishi wako haina malisho. Kwa hiyo sasa, tafadhali uruhusu watumishi wako wakae huko Gosheni.” \p \v 5 Farao akamwambia Yosefu, “Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako, \v 6 nayo nchi ya Misri ipo mbele yako, uwakalishe baba yako na ndugu zako katika sehemu iliyo bora kupita zote katika nchi. Na waishi Gosheni. Kama unamfahamu yeyote miongoni mwao mwenye uwezo maalum, waweke wawe wasimamizi wa mifugo yangu.” \p \v 7 Ndipo Yosefu akamleta Yakobo baba yake na kumtambulisha mbele ya Farao. Baada ya Yakobo kumbariki Farao, \v 8 Farao akamuuliza, “Je una umri gani?” \p \v 9 Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka 130. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya kusafiri ya baba zangu.” \v 10 Kisha Yakobo akambariki Farao, naye akaondoka mbele ya uso wake. \p \v 11 Ndipo Yosefu akawakalisha baba yake na ndugu zake katika nchi ya Misri na kuwapa milki katika sehemu bora sana ya nchi, wilaya ya Ramesesi, kama Farao alivyoelekeza. \v 12 Pia Yosefu akampa baba yake, na ndugu zake na wote wa nyumbani mwa baba yake vyakula, kwa kulingana na hesabu ya watoto wao. \s1 Uongozi Wa Yosefu Wakati Wa Njaa \p \v 13 Hata hivyo, hapakuwepo chakula katika sehemu yote kwa kuwa njaa ilikuwa kali sana; Misri na Kanaani zote zikaharibiwa kwa sababu ya njaa. \v 14 Yosefu akakusanya fedha zote zilizopatikana kutoka mauzo ya nafaka huko Misri na Kanaani, akazileta kwenye jumba la kifalme la Farao. \v 15 Fedha za watu wa Misri na Kanaani zilipokwisha, Wamisri wote wakamjia Yosefu na kumwambia, “Tupatie chakula. Kwa nini tufe mbele ya macho yako? Fedha zetu zimekwisha.” \p \v 16 Yosefu akawaambia, “Basi leteni mifugo yenu, nitawauzia chakula kwa kubadilisha na mifugo yenu, kwa kuwa fedha zenu zimekwisha.” \v 17 Kwa hiyo wakaleta mifugo yao kwa Yosefu, naye akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi zao, kondoo na mbuzi zao, ngʼombe na punda zao. Katika mwaka huo wote Yosefu akawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote. \p \v 18 Mwaka ule ulipokwisha, wakamjia mwaka uliofuata na kumwambia, “Hatuwezi kuficha ukweli mbele za bwana wetu kwamba, kwa kuwa fedha zetu zimekwisha na wanyama wetu ni mali yako, sasa hakuna chochote kilichosalia kwa ajili ya bwana wetu isipokuwa miili yetu na ardhi yetu. \v 19 Kwa nini tuangamie mbele ya macho yako, sisi pamoja na nchi yetu? Utununue sisi pamoja na ardhi yetu ili kubadilishana kwa chakula. Nasi pamoja na nchi yetu tutakuwa watumwa wa Farao. Tupe sisi mbegu ili tuweze kuishi wala tusife, nchi yetu isije ikawa ukiwa.” \p \v 20 Kwa hiyo Yosefu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Wamisri, mmoja baada ya mwingine, waliuza mashamba yao, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana kwao. Nchi ikawa mali ya Farao, \v 21 naye Yosefu akawafanya watu watumike kama watumwa, kuanzia upande mmoja wa Misri hadi upande mwingine. \v 22 Hata hivyo, hakununua nchi ya makuhani, kwa sababu walikuwa wanapata mgawo wao wa kawaida kutoka kwa Farao, nao walikuwa na chakula cha kuwatosha kutokana na mgawo waliopewa na Farao. Hii ndiyo sababu hawakuuza ardhi yao. \p \v 23 Yosefu akawaambia watu, “Kwa vile nimewanunua ninyi pamoja na nchi yenu leo kuwa mali ya Farao, hapa kuna mbegu kwa ajili yenu ili mweze kuziotesha. \v 24 Lakini wakati mazao yatakapokuwa tayari, mpeni Farao sehemu ya tano. Sehemu hizo nne zitakazobaki mtaziweka kama mbegu kwa ajili ya mashamba na kwa ajili ya chakula chenu wenyewe na cha watu wa nyumbani mwenu na watoto wenu.” \p \v 25 Wakamwambia, “Umeokoa maisha yetu. Basi na tupate kibali mbele ya macho ya bwana wetu; tutakuwa watumwa wa Farao.” \p \v 26 Basi Yosefu akaiweka iwe sheria kuhusu nchi ya Misri, ambayo inatumika mpaka leo, kwamba, sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni nchi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao. \p \v 27 Basi Waisraeli wakaishi Misri katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali huko wakastawi na kuongezeka kwa wingi sana. \p \v 28 Yakobo akaishi Misri miaka kumi na saba, nayo miaka ya maisha yake ilikuwa 147. \v 29 Wakati ulipokaribia wa Israeli kufa, akamwita mwanawe Yosefu na kumwambia, “Kama nimepata kibali machoni pake, weka mkono wako chini ya paja langu na uniahidi kuwa utanifanyia fadhili na uaminifu. Usinizike Misri, \v 30 lakini nitakapopumzika na baba zangu, unichukue kutoka Misri, ukanizike walipozikwa.” \p Yosefu akamwambia, “Nitafanya kama unavyosema.” \p \v 31 Akamwambia, “Niapie.” Ndipo Yosefu akamwapia, naye Israeli akaabudu, akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake. \c 48 \s1 Manase Na Efraimu \p \v 1 Baada ya muda Yosefu akaambiwa kwamba, “Baba yako ni mgonjwa.” Kwa hiyo akawachukua wanawe wawili Manase na Efraimu, pamoja naye. \v 2 Yakobo alipoambiwa, “Mwanao Yosefu amekujia kukuona,” Israeli akakusanya nguvu zake, akaketi kitandani. \p \v 3 Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu Mwenyezi\f + \fr 48:3 \ft Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\f* alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani, huko akanibariki, \v 4 naye akaniambia, ‘Nitakufanya ustawi na kuongezeka hesabu yako, nitakufanya kuwa jamii ya mataifa, nami nitakupa nchi hii uimiliki milele wewe na wazao wako baada yako.’ \p \v 5 “Sasa basi, wanao wawili waliozaliwa kwako huku Misri kabla sijaja hapa kwako watahesabiwa kuwa ni wangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama vile Reubeni na Simeoni walivyo wangu. \v 6 Lakini watoto utakaowazaa baada yao watakuwa wako. Katika nchi watakayoirithi, watatambuliwa kwa jina la ndugu zao. \v 7 Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, katika huzuni yangu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tungali tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrathi. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrathi” (yaani Bethlehemu). \p \v 8 Wakati Israeli alipowaona wana wa Yosefu, akauliza, “Hawa ni nani?” \p \v 9 Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wana ambao Mungu amenipa nikiwa huku.” \p Ndipo Israeli akasema, “Walete kwangu ili niwabariki.” \p \v 10 Basi macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee, naye aliona kwa shida. Kwa hiyo Yosefu akawaleta wanawe karibu na baba yake, Israeli akawabusu na akawakumbatia. \p \v 11 Israeli akamwambia Yosefu, “Kamwe sikutazamia kuuona uso wako tena, lakini sasa Mungu ameniruhusu kuwaona watoto wako pia.” \p \v 12 Ndipo Yosefu akawaondoa wanawe magotini mwa Israeli naye akasujudu hadi nchi. \v 13 Yosefu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao. \v 14 Lakini Israeli akaupeleka mkono wake wa kuume, akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, ingawa alikuwa ndiye mdogo, na mkono wake wa kushoto akaukatisha, akauweka juu ya kichwa cha Manase, ingawa Manase alikuwa ndiye mzaliwa wa kwanza. \p \v 15 Ndipo akambariki Yosefu akisema, \q1 “Mungu ambaye baba zangu \q2 Abrahamu na Isaki walimtii, \q1 Mungu ambaye amekuwa mchungaji \q2 wa maisha yangu yote mpaka leo hii, \q1 \v 16 Malaika ambaye aliniokoa kutoka madhara yote, \q2 yeye na awabariki vijana hawa. \q1 Na waitwe kwa jina langu \q2 na kwa majina ya baba zangu Abrahamu na Isaki, \q1 wao na waongezeke kwa wingi \q2 katika dunia.” \p \v 17 Yosefu alipoona baba yake akiweka mkono wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, hakupendezwa, kwa hiyo akauchukua mkono wa baba yake kutoka kichwa cha Efraimu na kuuweka juu ya kichwa cha Manase. \v 18 Yosefu akamwambia, “Hapana, baba yangu, huyu ndiye mzaliwa wa kwanza; uweke mkono wako wa kuume juu ya kichwa chake.” \p \v 19 Lakini baba yake akakataa, akasema, “Ninajua, mwanangu, ninajua. Yeye pia atakuwa taifa, naye pia atakuwa mkuu. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, nao wazao wake watakuwa kundi la mataifa.” \v 20 Akawabarikia siku ile na kusema, \q1 “Kwa jina lenu Israeli watatamka baraka hii: \q2 ‘Mungu na awafanye kama Efraimu na Manase.’ ” \m Kwa hiyo akamtanguliza Efraimu mbele ya Manase. \p \v 21 Ndipo Israeli akamwambia Yosefu, “Mimi ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu. \v 22 Kwako wewe, kama aliye juu ya ndugu zako, ninakupa sehemu moja zaidi ya ndugu zako, lile eneo nililoteka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu.” \c 49 \s1 Yakobo Abariki Wanawe \p \v 1 Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo. \q1 \v 2 “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo, \q2 msikilizeni baba yenu Israeli. \b \q1 \v 3 “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, \q2 nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu, \q2 umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. \q1 \v 4 Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, \q2 kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, \q2 kwenye kitanda changu na kukinajisi. \b \q1 \v 5 “Simeoni na Lawi ni wana ndugu: \q2 panga zao ni silaha za jeuri. \q1 \v 6 Mimi na nisiingie katika baraza lao, \q2 nami nisiunganike katika kusanyiko lao, \q1 kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, \q2 walikata mishipa ya miguu ya mafahali \q2 kama walivyopenda. \q1 \v 7 Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, \q2 nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! \q1 Nitawatawanya katika Yakobo \q2 Na kuwasambaza katika Israeli. \b \q1 \v 8 “Yuda, ndugu zako watakusifu; \q2 mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; \q2 wana wa baba yako watakusujudia. \q1 \v 9 Ee Yuda, wewe ni mwana simba; \q2 unarudi toka mawindoni, mwanangu. \q1 Kama simba hunyemelea na kulala chini, \q2 kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha? \q1 \v 10 Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, \q2 wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, \q1 hadi aje yeye ambaye milki ni yake, \q2 ambaye utii wa mataifa ni wake. \q1 \v 11 Atamfunga punda wake katika mzabibu, \q2 naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; \q1 atafua mavazi yake katika divai, \q2 majoho yake katika damu ya mizabibu. \q1 \v 12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, \q2 meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa. \b \q1 \v 13 “Zabuloni ataishi pwani ya bahari \q2 na kuwa bandari za kuegesha meli; \q2 mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni. \b \q1 \v 14 “Isakari ni punda mwenye nguvu \q2 ambaye amelala kati ya mizigo yake. \q1 \v 15 Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika \q2 na jinsi nchi yake inavyopendeza, \q1 atainamisha bega lake kwenye mzigo \q2 na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu. \b \q1 \v 16 “Dani atahukumu watu wake kwa haki \q2 kama mmoja wa makabila ya Israeli. \q1 \v 17 Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, \q2 nyoka mwenye sumu kando ya njia, \q1 yule aumaye visigino vya farasi \q2 ili yule ampandaye aanguke chali. \b \q1 \v 18 “Ee \nd Bwana\nd*, nautafuta wokovu wako. \b \q1 \v 19 “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, \q2 lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa. \b \q1 \v 20 “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, \q2 naye atatoa chakula kitamu kimfaacho mfalme. \b \q1 \v 21 “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru \q2 azaaye watoto wazuri. \b \q1 \v 22 “Yosefu ni mzabibu uzaao, \q2 mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, \q2 ambao matawi yake hutanda ukutani. \q1 \v 23 Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, \q2 wakampiga mshale kwa ukatili. \q1 \v 24 Lakini upinde wake ulibaki imara, \q2 mikono yake ikatiwa nguvu, \q1 na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, \q2 kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, \q1 \v 25 kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, \q2 kwa sababu ya Mwenyezi,\f + \fr 49:25 \ft Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.\f* yeye anayekubariki \q1 kwa baraka za mbinguni juu, \q2 baraka za kilindi kilichoko chini, \q2 baraka za matitini na za tumbo la uzazi. \q1 \v 26 Baraka za baba yako ni kubwa \q2 kuliko baraka za milima ya kale, \q2 nyingi kuliko vilima vya kale. \q1 Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu, \q2 juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. \b \q1 \v 27 “Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu; \q2 asubuhi hurarua mawindo yake, \q2 jioni hugawa nyara.” \p \v 28 Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa. \s1 Kifo Cha Yakobo \p \v 29 Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti, \v 30 pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba. \v 31 Huko ndiko Abrahamu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaki na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea. \v 32 Shamba hilo na pango lililoko ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.” \p \v 33 Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake. \c 50 \p \v 1 Basi Yosefu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu. \v 2 Ndipo Yosefu akawaagiza matabibu waliokuwa wakimhudumia, wamtie baba yake Israeli dawa ili asioze. Hivyo matabibu wakamtia dawa asioze, \v 3 wakatumia siku arobaini, kwa maana ndio muda uliotakiwa wa kutia dawa ili asioze. Nao Wamisri wakamwombolezea Yakobo kwa siku sabini. \p \v 4 Siku za kumwombolezea zilipokwisha, Yosefu akawaambia washauri wa Farao, “Kama nimepata kibali machoni penu semeni na Farao kwa ajili yangu. Mwambieni, \v 5 ‘Baba yangu aliniapisha na kuniambia, “Mimi niko karibu kufa; unizike katika kaburi lile nililochimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani.” Sasa nakuomba uniruhusu niende kumzika baba yangu, nami nitarudi.’ ” \p \v 6 Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.” \p \v 7 Hivyo Yosefu akapanda kwenda kumzika baba yake. Maafisa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, watu mashuhuri wa baraza lake na watu mashuhuri wote wa Misri. \v 8 Hawa ni mbali na watu wote wa nyumbani kwa Yosefu, na ndugu zake, na wale wote wa nyumbani mwa baba yake. Ni watoto wao, makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe tu waliobakia katika nchi ya Gosheni. \v 9 Magari makubwa na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana. \p \v 10 Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yosefu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake. \v 11 Wakanaani walioishi huko walipoona maombolezo yaliyofanyika katika sakafu ile ya kupuria ya Atadi, wakasema, “Wamisri wanafanya maombolezo makubwa.” Kwa hiyo mahali pale karibu na Yordani pakaitwa Abel-Mizraimu.\f + \fr 50:11 \ft Abel-Mizraimu maana yake Maombolezo ya Wamisri.\f* \p \v 12 Hivyo wana wa Yakobo wakafanya kama baba yao alivyowaagiza: \v 13 Wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Abrahamu alilinunua kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia. \v 14 Baada ya Yosefu kumzika baba yake, akarudi Misri pamoja na ndugu zake na wale wote waliokuwa wamekwenda naye kumzika baba yake. \s1 Yosefu Awaondolea Ndugu Zake Mashaka \p \v 15 Ndugu zake Yosefu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje kama Yosefu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?” \v 16 Kwa hiyo wakampelekea Yosefu ujumbe, wakasema, “Kabla baba yako hajafa aliacha maagizo haya: \v 17 ‘Hili ndilo mtakalomwambia Yosefu: Ninakuomba uwasamehe ndugu zako dhambi na mabaya kwa vile walivyokutenda vibaya.’ Sasa tafadhali samehe dhambi za watumishi wa Mungu wa baba yako.” Ujumbe huu ulipomfikia, Yosefu akalia. \p \v 18 Ndipo ndugu zake wakaja na kujitupa chini mbele yake. Wakasema, “Sisi ni watumwa wako.” \p \v 19 Lakini Yosefu akawaambia, “Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? \v 20 Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. \v 21 Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu.” Akawahakikishia na kusema nao kwa wema. \s1 Kifo Cha Yosefu \p \v 22 Yosefu akakaa katika nchi ya Misri, yeye pamoja na jamaa yote ya baba yake. Akaishi miaka 110, \v 23 naye akaona kizazi cha tatu cha watoto wa Efraimu. Pia akaona watoto wa Makiri mwana wa Manase, wakawekwa magotini mwa Yosefu walipozaliwa. \p \v 24 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Abrahamu, Isaki na Yakobo.” \v 25 Naye Yosefu akawaapisha wana wa Israeli na kuwaambia, “Hakika Mungu atawasaidia, nanyi ni lazima mhakikishe mmepandisha mifupa yangu kutoka mahali hapa.” \p \v 26 Kwa hiyo Yosefu akafa akiwa na umri wa miaka 110. Baada ya kumtia dawa ili asioze, akawekwa kwenye jeneza huko Misri.