\id EXO - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version \rem Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc. \h Kutoka \toc1 Kutoka \toc2 Kutoka \toc3 Kut \mt1 Kutoka \c 1 \s1 Waisraeli Waonewa \p \v 1 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli ambao walikwenda Misri na Yakobo, kila mmoja akiwa pamoja na jamaa yake: \v 2 Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda; \v 3 Isakari, Zabuloni na Benyamini; \v 4 Dani na Naftali, Gadi na Asheri. \v 5 Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yosefu alikuwa tayari yuko Misri. \p \v 6 Basi Yosefu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, \v 7 lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi. \p \v 8 Kisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yosefu akatawala Misri. \v 9 Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi. \v 10 Njooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.” \p \v 11 Basi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao. \v 12 Lakini walivyozidi kuteswa ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi; Wamisri wakawaogopa Waisraeli, \v 13 kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili. \v 14 Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili. \p \v 15 Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, \v 16 “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” \v 17 Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. \v 18 Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?” \p \v 19 Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.” \p \v 20 Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi. \v 21 Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe. \p \v 22 Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.” \c 2 \s1 Kuzaliwa Kwa Mose \p \v 1 Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, \v 2 naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. \v 3 Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili. \v 4 Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto. \p \v 5 Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua. \v 6 Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Kiebrania.” \p \v 7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?” \p \v 8 Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. \v 9 Binti Farao akamwambia, “Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa.” Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea. \v 10 Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose akisema, “Nilimtoa kwenye maji.” \s1 Mose Akimbilia Midiani \p \v 11 Siku moja, baada ya Mose kukua, akaondoka kwenda walikokuwa watu wake, na akachunguza jinsi walivyokuwa wakifanya kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmojawapo wa watu wake. \v 12 Mose akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha mchangani. \v 13 Kesho yake akatoka, akaona Waebrania wawili wakipigana. Akamuuliza yule aliyekosa, “Mbona unampiga Mwebrania mwenzako?” \p \v 14 Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Mose akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.” \p \v 15 Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumuua Mose, lakini Mose akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima. \v 16 Kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja kisimani ili kuchota maji na kujaza hori kwa ajili ya kunyweshea mifugo ya baba yao. \v 17 Baadhi ya wachungaji wakaja wakawafukuza hao wasichana. Ndipo Mose akainuka, akawasaidia na kunywesha mifugo yao. \p \v 18 Hao wasichana waliporudi nyumbani kwa Reueli baba yao, akawauliza, “Imekuwaje leo mmerudi mapema hivyo?” \p \v 19 Wakamjibu, “Mmisri mmoja alituokoa kutoka mikononi mwa wachungaji. Pia mtu huyo alituchotea maji na kunywesha mifugo.” \p \v 20 Akawauliza binti zake, “Yuko wapi? Mbona mmemwacha? Mkaribisheni ale chakula.” \p \v 21 Mose akakubali kukaa kwa huyo mtu, ambaye alimpa Mose binti yake aliyeitwa Sipora amwoe. \v 22 Sipora alizaa mtoto wa kiume, naye Mose akamwita Gershomu, akisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” \p \v 23 Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu. \v 24 Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka Agano alilofanya na Abrahamu pamoja na Isaki na Yakobo. \v 25 Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia. \c 3 \s1 Mose Na Kichaka Kinachowaka Moto \p \v 1 Basi Mose alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Mose akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu. \v 2 Huko malaika wa \nd Bwana\nd* akamtokea Mose katika mwali wa moto kutoka kichakani. Mose akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei. \v 3 Ndipo Mose akawaza, “Nitageuka sasa nione kitu hiki cha ajabu, nami nione ni kwa nini kichaka hiki hakiteketei.” \p \v 4 \nd Bwana\nd* alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, “Mose! Mose!” \p Naye Mose akajibu, “Mimi hapa.” \p \v 5 Mungu akamwambia, “Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu.” \v 6 Kisha akamwambia, “Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo.” Mose aliposikia hayo, akafunika uso wake kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu. \p \v 7 \nd Bwana\nd* akamwambia, “Hakika nimeona mateso ya watu wangu katika Misri. Nimesikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao, nami naguswa na mateso yao. \v 8 Basi nimeshuka niwaokoe kutoka mkono wa Wamisri, niwatoe na kuwapandisha kutoka nchi hiyo, niwapeleke katika nchi nzuri na kubwa, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \v 9 Sasa kilio cha Waisraeli kimenifikia, nami nimeona jinsi Wamisri wanavyowatesa. \v 10 Basi, sasa nenda. Ninakutuma kwa Farao ili kuwatoa watu wangu Waisraeli kutoka Misri.” \p \v 11 Lakini Mose akamwambia Mungu, “Mimi ni nani hata niende kwa Farao kuwatoa Waisraeli nchini Misri?” \p \v 12 Naye Mungu akasema, “Mimi nitakuwa pamoja nawe. Hii itakuwa ishara kwako kwamba ni Mimi nimekutuma: Hapo utakapokuwa umewatoa watu Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.” \p \v 13 Mose akamwambia Mungu, “Ikiwa nitawaendea Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakiniuliza, ‘Jina lake ni nani?’ Nitawaambia nini?” \p \v 14 Mungu akamwambia Mose, “\nd Mimi niko ambaye niko\nd*. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘\nd Mimi niko\nd* amenituma kwenu.’ ” \p \v 15 Vilevile Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli, ‘\nd Bwana\nd*, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’ Hili ndilo Jina langu milele, Jina ambalo mtanikumbuka kwalo kutoka kizazi hadi kizazi. \p \v 16 “Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘\nd Bwana\nd*, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyofanyiwa katika Misri. \v 17 Nami nimeahidi kuwapandisha kutoka mateso yenu katika nchi ya Misri, niwapeleke nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, nchi itiririkayo maziwa na asali.’ \p \v 18 “Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtakwenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘\nd Bwana\nd*, Mungu wa Waebrania ametutokea. Turuhusu twende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwa \nd Bwana\nd* Mungu wetu.’ \v 19 Lakini nafahamu kwamba mfalme wa Misri hatawaruhusu kwenda, mpaka mkono wenye nguvu umlazimishe. \v 20 Kwa hiyo nitaunyoosha mkono wangu na kuwapiga Wamisri kwa maajabu yote nitakayofanya miongoni mwao. Baada ya hayo, atawaruhusu mwondoke. \p \v 21 “Nami nitawapa hawa watu upendeleo mbele ya Wamisri, kwa hiyo mtakapoondoka nchini hamtaondoka mikono mitupu. \v 22 Kila mwanamke Mwisraeli atamwomba jirani yake Mmisri na mwanamke yeyote anayeishi nyumbani kwake ampe vyombo vya fedha, dhahabu na nguo, ambavyo mtawavika wana wenu na binti zenu. Hivyo mtawateka nyara Wamisri.” \c 4 \s1 Ishara Za Mose \p \v 1 Mose akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘\nd Bwana\nd* hakukutokea’?” \p \v 2 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?” \p Akajibu, “Fimbo.” \p \v 3 \nd Bwana\nd* akasema, “Itupe chini.” \p Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. \v 4 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia, “Nyoosha mkono wako umkamate mkiani.” Basi Mose akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. \v 5 \nd Bwana\nd* akasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa \nd Bwana\nd*, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.” \p \v 6 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia, “Weka mkono wako ndani ya joho lako.” Basi Mose akaweka mkono wake ndani ya joho lake, naye alipoutoa, ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji. \p \v 7 Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Mose akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake. \p \v 8 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia, “Kama hawatakuamini wewe, au kutojali ishara ya kwanza, wataamini ishara ya pili. \v 9 Lakini kama hawataamini ishara hizi mbili au hawatawasikiliza ninyi, chukua kiasi cha maji kutoka Mto Naili uyamimine juu ya ardhi kavu. Maji mtakayotoa mtoni yatakuwa damu juu ya ardhi.” \p \v 10 Mose akamwambia \nd Bwana\nd*, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.” \p \v 11 \nd Bwana\nd* akamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu kuona au upofu? Je, si mimi, \nd Bwana\nd*? \v 12 Sasa nenda, nitakusaidia kusema, nami nitakufundisha jambo la kusema.” \p \v 13 Lakini Mose akasema, “Ee Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine kufanya kazi hiyo.” \p \v 14 Ndipo hasira ya \nd Bwana\nd* ikawaka dhidi ya Mose, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Aroni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona. \v 15 Utazungumza naye na kuweka maneno kinywani mwake. Nitawasaidia ninyi wawili kusema, nami nitawafundisha jambo la kufanya. \v 16 Aroni ataongea na watu badala yako na itakuwa kwamba yeye amekuwa kinywa chako nawe utakuwa kama Mungu kwake. \v 17 Lakini chukua fimbo hii mkononi mwako ili uweze kuitumia kufanya ishara hizo za ajabu.” \s1 Mose Anarudi Misri \p \v 18 Kisha Mose akarudi kwa Yethro mkwewe akamwambia, “Niruhusu nirudi kwa watu wangu Misri kuona kama yuko hata mmoja wao ambaye bado anaishi.” \p Yethro akamwambia, “Nenda, nami nakutakia mema.” \p \v 19 Basi \nd Bwana\nd* alikuwa amemwambia Mose huko Midiani, “Rudi Misri kwa maana watu wote waliotaka kukuua wamekufa.” \v 20 Basi Mose akamchukua mkewe na wanawe, akawapandisha juu ya punda na kuanza safari kurudi Misri. Naye akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake. \p \v 21 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Utakaporudi Misri, hakikisha kwamba utafanya mbele ya Farao maajabu yote niliyokupa uwezo wa kuyafanya. Lakini nitafanya moyo wake kuwa mgumu ili kwamba asiwaruhusu watu waende. \v 22 Kisha mwambie Farao, ‘Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd*: Israeli ni mwanangu mzaliwa wa kwanza, \v 23 nami nilikuambia, “Ruhusu mwanangu aondoke, ili aweze kuniabudu mimi.” Lakini ukakataa kumruhusu kwenda, basi nitaua mwana wako mzaliwa wa kwanza.’ ” \p \v 24 Mose alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, \nd Bwana\nd* akakutana naye, akataka kumuua. \v 25 Lakini Sipora akachukua jiwe gumu, akakata govi la mwanawe na kugusa nalo miguu ya Mose. Sipora akasema, “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.” \v 26 Sipora alipomwita Mose, “Bwana arusi wa damu,” alikuwa anamaanisha ile tohara. Baada ya hayo \nd Bwana\nd* akamwacha. \p \v 27 \nd Bwana\nd* akamwambia Aroni, “Nenda jangwani ukamlaki Mose.” Basi akakutana na Mose kwenye mlima wa Mungu, akambusu. \v 28 Kisha Mose akamwambia Aroni kila kitu \nd Bwana\nd* alichomtuma kusema, vilevile habari za ishara na maajabu alizokuwa amemwamuru kufanya. \p \v 29 Mose na Aroni wakawakusanya wazee wote wa Waisraeli, \v 30 naye Aroni akawaambia kila kitu \nd Bwana\nd* alichokuwa amemwambia Mose. Pia akafanya ishara mbele ya watu, \v 31 nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa \nd Bwana\nd* anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu. \c 5 \s1 Matofali Bila Nyasi \p \v 1 Baadaye Mose na Aroni wakaenda kwa Farao, wakamwambia, “Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli: ‘Waruhusu watu wangu waende, ili waweze kunifanyia sikukuu huko jangwani.’ ” \p \v 2 Farao akasema, “Huyo \nd Bwana\nd* ni nani, hata nimtii na kuruhusu Israeli uende? Simjui huyo \nd Bwana\nd* wala sitawaruhusu Israeli waende.” \p \v 3 Ndipo Mose na Aroni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Sasa turuhusu tuwe na safari ya siku tatu ya jangwani ili tukamtolee \nd Bwana\nd* Mungu wetu dhabihu, la sivyo aweza kutupiga sisi kwa tauni au kwa upanga.” \p \v 4 Lakini mfalme wa Misri akasema, “Mbona ninyi Mose na Aroni mnawachukua watu waache kazi zao? Rudini kwenye kazi zenu!” \v 5 Kisha Farao akasema, “Tazama, sasa watu hawa ni wengi, nanyi mnawazuia kufanya kazi.” \p \v 6 Siku iyo hiyo Farao akatoa amri hii kwa viongozi wa watumwa na wasimamizi wa watu akawaambia: \v 7 “Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali. Wao wakusanye nyasi zao wenyewe. \v 8 Lakini watakeni kutengeneza matofali kiasi kile kile cha mwanzo, kiwango kisipunguzwe. Wao ni wavivu, ndiyo sababu wanalia, wakisema, ‘Turuhusiwe twende kumtolea Mungu wetu dhabihu.’ \v 9 Fanyeni kazi kuwa ngumu zaidi kwa watu hao ili kwamba wakazane na kazi na kuacha kusikiliza uongo.” \p \v 10 Basi viongozi wa watumwa na wasimamizi wakaenda kuwaambia watu, “Hivi ndivyo Farao asemavyo: ‘Sitawapa tena nyasi. \v 11 Nendeni mkatafute nyasi wenyewe popote mnapoweza kuzipata, lakini kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo.’ ” \v 12 Basi watu wakatawanyika kote nchini Misri kukusanya mabua ya kutumia badala ya nyasi. \v 13 Viongozi wa watumwa wakasisitiza, wakisema, “Timizeni kazi mnayotakiwa kwa kila siku, kama wakati ule mlipokuwa mkipewa nyasi.” \v 14 Wasimamizi wa Kiisraeli waliochaguliwa na viongozi wa watumwa wa Farao walipigwa na kuulizwa, “Kwa nini hamkutimiza kiwango chenu cha kutengeneza matofali jana na leo, kama mwanzoni?” \p \v 15 Ndipo wasimamizi wa Kiisraeli wakaenda kumlilia Farao, wakisema: “Mbona umewatendea watumishi wako hivi? \v 16 Watumishi wako hawapewi nyasi, hata hivyo tumeambiwa, ‘Tengenezeni matofali!’ Watumishi wako wanapigwa, lakini kosa ni la watu wako wenyewe.” \p \v 17 Farao akasema, “Ninyi ni wavivu ndiyo sababu mnasema, ‘Turuhusu twende tukamtolee \nd Bwana\nd* dhabihu.’ \v 18 Sasa nendeni kazini. Hamtapewa nyasi zozote, nanyi ni lazima mtengeneze matofali.” \p \v 19 Wasimamizi wa Kiisraeli walitambua kuwa wako taabani walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.” \v 20 Walipoondoka kwa Farao, wakawakuta Mose na Aroni wakingojea kukutana nao, \v 21 wakawaambia Mose na Aroni, “\nd Bwana\nd* na awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tunuke kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.” \s1 Mungu Anaahidi Ukombozi \p \v 22 Mose akarudi kwa \nd Bwana\nd* na kumwambia, “Ee Bwana, mbona umewaletea watu hawa taabu? Kwa nini basi ukanituma mimi? \v 23 Tangu nilipomwendea Farao kuzungumza naye kwa jina lako, amewaletea taabu watu hawa, nawe kamwe hujawakomboa watu wako.” \c 6 \p \v 1 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.” \p \v 2 Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimi \nd Bwana\nd*. \v 3 Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi,\f + \fr 6:3 \ft Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote).\f* ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. \v 4 Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. \v 5 Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu. \p \v 6 “Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi \nd Bwana\nd*, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu. \v 7 Nitawatwaa mwe watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi \nd Bwana\nd* Mungu wenu, niliyewatoa chini ya kongwa la Wamisri. \v 8 Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi \nd Bwana\nd*.’ ” \p \v 9 Mose akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya maumivu makuu ya moyoni na utumwa wa kikatili. \p \v 10 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 11 “Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.” \p \v 12 Lakini Mose akamwambia \nd Bwana\nd*, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?” \s1 Orodha Ya Jamaa Ya Mose Na Aroni \p \v 13 Ndipo \nd Bwana\nd* akanena na Mose na Aroni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri. \b \mi \v 14 Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao: \b \pi1 Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni. \pi1 \v 15 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni. \pi1 \v 16 Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. \pi1 \v 17 Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei. \pi1 \v 18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133. \pi1 \v 19 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. \pi1 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao. \pi1 \v 20 Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137. \pi1 \v 21 Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri. \pi1 \v 22 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri. \pi1 \v 23 Aroni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. \pi1 \v 24 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora. \pi1 \v 25 Eleazari mwana wa Aroni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi. \b \pi1 Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo. \b \p \v 26 Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambao \nd Bwana\nd* aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” \v 27 Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni. \s1 Aroni Kuzungumza Badala Ya Mose \p \v 28 \nd Bwana\nd* aliponena na Mose huko Misri, \v 29 akamwambia, “Mimi ndimi \nd Bwana\nd*. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.” \p \v 30 Lakini Mose akamwambia \nd Bwana\nd*, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?” \c 7 \p \v 1 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa Farao, naye Aroni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako. \v 2 Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Aroni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake. \v 3 Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Ingawa nitazidisha ishara na maajabu katika Misri, \v 4 hatawasikiliza. Kisha nitaupeleka mkono wangu juu ya Misri, na kwa matendo makuu ya hukumu nitavitoa vikundi vyangu, watu wangu Waisraeli. \v 5 Nao Wamisri watajua kuwa Mimi ndimi \nd Bwana\nd* nitakapounyoosha mkono wangu dhidi ya Misri na kuwatoa Waisraeli watoke humo.” \p \v 6 Mose na Aroni wakafanya sawasawa kama vile \nd Bwana\nd* alivyowaagiza. \v 7 Mose alikuwa na umri wa miaka themanini na Aroni alikuwa na umri wa miaka themanini na mitatu walipozungumza na Farao. \s1 Fimbo Ya Aroni Yawa Nyoka \p \v 8 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose na Aroni, \v 9 “Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni muujiza,’ basi mwambie Aroni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.” \p \v 10 Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile \nd Bwana\nd* alivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka. \v 11 Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao. \v 12 Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Aroni ikazimeza zile fimbo zao. \v 13 Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa amesema. \s1 Pigo La Kwanza: Damu \p \v 14 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwaachia watu kuondoka. \v 15 Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ngoja ukingoni mwa Naili ili uonane naye, na uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka. \v 16 Kisha umwambie, ‘\nd Bwana\nd*, Mungu wa Waebrania, amenituma nikuambie: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu jangwani. Lakini hadi sasa hujasikiliza. \v 17 Hili ndilo \nd Bwana\nd* asemalo: Kwa hili utajua kuwa Mimi ndimi \nd Bwana\nd*: Fimbo iliyo mkononi mwangu nitapiga nayo maji ya Naili nayo yatabadilika kuwa damu. \v 18 Samaki waliomo katika Mto Naili watakufa, nao mto utanuka vibaya, Wamisri hawataweza kunywa hayo maji yake.’ ” \p \v 19 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Chukua ile fimbo yako unyooshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya chemchemi na mifereji, juu ya madimbwi na mabwawa yote,’ navyo vitabadilika kuwa damu. Damu itakuwa kila mahali katika Misri, hata kwenye vyombo vya miti na vya mawe.” \p \v 20 Mose na Aroni wakafanya kama vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Naili, na maji yote yakabadilika kuwa damu. \v 21 Samaki katika Mto Naili wakafa, nao mto ukanuka vibaya sana kiasi kwamba Wamisri hawakuweza kunywa maji yake. Damu ilikuwa kila mahali katika nchi ya Misri. \p \v 22 Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa amesema. \v 23 Badala yake, Farao akageuka, akaenda kwenye jumba lake la kifalme, wala hakulitia hili moyoni. \v 24 Nao Wamisri wote wakachimba kandokando ya Mto Naili kupata maji ya kunywa, kwa sababu hawakuweza kunywa maji ya mto. \s1 Pigo La Pili: Vyura \p \v 25 Zilipita siku saba baada ya \nd Bwana\nd* kuyapiga maji ya Mto Naili. \c 8 \p \v 1 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd*: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. \v 2 Kama ukikataa kuwaruhusu kuondoka, basi nitaipiga nchi yako yote kwa kuwaletea vyura. \v 3 Mto Naili utafurika vyura. Watakuja kwenye jumba lako la kifalme na katika chumba chako cha kulala na kitandani mwako, katika nyumba za maafisa wako na kwa watu wako, vyura hao wataingia katika meko yenu na kwenye vyombo vya kukandia unga. \v 4 Vyura watapanda juu yako, juu ya watu wako na maafisa wako wote.’ ” \p \v 5 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Nyoosha mkono wako ukiwa na ile fimbo yako juu ya vijito, mifereji na madimbwi, fanya vyura waje juu ya nchi ya Misri.’ ” \p \v 6 Ndipo Aroni akaunyoosha mkono wake juu ya maji ya Misri, nao vyura wakatokea na kuifunika nchi. \v 7 Lakini waganga wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao, nao pia wakafanya vyura kuja juu ya nchi ya Misri. \p \v 8 Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kusema, “Mwombeni \nd Bwana\nd* awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea \nd Bwana\nd* dhabihu.” \p \v 9 Mose akamwambia Farao, “Ninakupa heshima ya kuamua ni wakati gani wa kukuombea wewe, maafisa wako na watu wako ili kwamba vyura watoke kwenu na kwenye nyumba zenu. Isipokuwa wale walio katika Mto Naili.” \p \v 10 Farao akasema, “Kesho.” \p Mose akamjibu, “Itakuwa kama unavyosema, ili upate kujua kwamba hakuna yeyote kama \nd Bwana\nd* Mungu wetu. \v 11 Vyura wataondoka kwako na katika nyumba zako, kwa maafisa wako na kwa watu wako, ila watabakia katika Mto Naili tu.” \p \v 12 Baada ya Mose na Aroni kuondoka kwa Farao, Mose akamlilia \nd Bwana\nd* kuhusu vyura aliokuwa amewaleta kwa Farao. \v 13 Naye \nd Bwana\nd* akafanya lile Mose alilomwomba. Vyura wakafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani. \v 14 Wakayakusanya malundo, nchi nzima ikanuka. \v 15 Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa amesema. \s1 Pigo La Tatu: Viroboto \p \v 16 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Nyoosha fimbo yako uyapige mavumbi ya ardhi,’ nayo nchi yote ya Misri mavumbi yatakuwa viroboto.” \v 17 Wakafanya hivyo, Aroni aliponyoosha mkono wake wenye fimbo na kuyapiga mavumbi ya nchi, viroboto wakawajia watu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi ya Misri yakawa viroboto. \v 18 Lakini waganga walipojaribu kutengeneza viroboto kwa siri ya uganga wao, hawakuweza. Nao viroboto walikuwa juu ya watu na wanyama. \p \v 19 Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile \nd Bwana\nd* alivyosema. \s1 Pigo La Nne: Mainzi \p \v 20 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi na usimame mbele ya Farao wakati anapokwenda mtoni nawe umwambie, ‘Hili ndilo \nd Bwana\nd* asemalo: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. \v 21 Kama hutawaachia watu wangu waondoke nitakupelekea makundi ya mainzi juu yako, kwa maafisa wako, kwa watu wako na kwenye nyumba zenu. Nyumba za Wamisri zitajazwa mainzi, hata na ardhi yote ya Misri. \p \v 22 “ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwepo na makundi ya mainzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, \nd Bwana\nd*, niko katika nchi hii. \v 23 Nitaweka tofauti kati ya watu wangu na watu wenu. Ishara hii ya ajabu itatokea kesho.’ ” \p \v 24 Naye \nd Bwana\nd* akafanya hivyo. Makundi makubwa ya mainzi yalimiminika katika jumba la kifalme la Farao na katika nyumba za maafisa wake, pia nchi yote ya Misri ikaharibiwa na mainzi. \p \v 25 Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.” \p \v 26 Lakini Mose akamwambia, “Hilo halitakuwa sawa. Dhabihu tutakazomtolea \nd Bwana\nd* Mungu wetu zitakuwa chukizo kwa Wamisri. Kama tukitoa dhabihu ambazo ni chukizo mbele yao, je, hawatatupiga mawe? \v 27 Ni lazima twende mwendo wa siku tatu mpaka tufike jangwani ili tumtolee \nd Bwana\nd* Mungu wetu dhabihu, kama alivyotuagiza.” \p \v 28 Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtolea \nd Bwana\nd* Mungu wenu dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.” \p \v 29 Mose akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwomba \nd Bwana\nd* na kesho mainzi yataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake. Hakikisha tu kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtolea \nd Bwana\nd* dhabihu.” \p \v 30 Ndipo Mose akamwacha Farao na kumwomba \nd Bwana\nd*, \v 31 naye \nd Bwana\nd* akafanya lile Mose alilomwomba. Mainzi yakaondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake, wala hakuna hata inzi aliyebakia. \v 32 Lakini wakati huu pia Farao akaushupaza moyo wake, wala hakuwaruhusu Waisraeli waondoke. \c 9 \s1 Pigo La Tano: Vifo Vya Mifugo \p \v 1 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo \nd Bwana\nd*, Mungu wa Waebrania asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.” \v 2 Kama ukikataa kuwaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia, \v 3 mkono wa \nd Bwana\nd* utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ngʼombe wako, kondoo na mbuzi. \v 4 Lakini \nd Bwana\nd* ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ” \p \v 5 \nd Bwana\nd* akaweka wakati na kusema, “Kesho \nd Bwana\nd* atalitenda hili katika nchi.” \v 6 Siku iliyofuata \nd Bwana\nd* akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa wana wa Israeli aliyekufa. \v 7 Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende. \s1 Pigo La Sita: Majipu \p \v 8 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose na Aroni, “Chukueni majivu ya tanuru, naye Mose ayarushe angani mbele ya Farao. \v 9 Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura juu ya watu na wanyama katika nchi yote.” \p \v 10 Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Mose akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea miilini mwa watu na wanyama. \v 11 Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote. \v 12 Lakini \nd Bwana\nd* akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa amemwambia Mose. \s1 Pigo La Saba: Mvua Ya Mawe \p \v 13 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd*, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu, \v 14 au wakati huu nitaleta mapigo yangu yenye nguvu dhidi yako, maafisa wako na watu wako, ili upate kujua kuwa hakuna mwingine kama Mimi katika dunia yote. \v 15 Kwa kuwa mpaka sasa ningelikuwa nimenyoosha mkono wangu na kukupiga wewe na watu wako kwa pigo ambalo lingekufutilia mbali juu ya nchi. \v 16 Lakini nimekuinua wewe kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote. \v 17 Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende. \v 18 Kwa hiyo, kesho wakati kama huu nitaleta mvua mbaya sana ya mawe ambayo haijapata kunyesha katika nchi ya Misri, tangu siku ilipoumbwa mpaka leo. \v 19 Sasa toa amri urudishe wanyama wote watoke malishoni na chochote ambacho kipo mashambani waje mpaka mahali pa usalama, kwa sababu mvua ya mawe itanyesha juu ya kila mtu na kila mnyama ambaye hajaletwa ndani ambao bado wako nje mashambani, nao watakufa.’ ” \p \v 20 Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la \nd Bwana\nd* wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani. \v 21 Lakini wale waliopuuza neno la \nd Bwana\nd* wakawaacha watumwa wao na mifugo yao shambani. \p \v 22 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.” \v 23 Mose alipoinyoosha fimbo yake kuelekea angani, \nd Bwana\nd* akatuma ngurumo na mvua ya mawe, umeme wa radi ulimulika hadi nchi. Kwa hiyo \nd Bwana\nd* akaifanya mvua ya mawe kunyesha juu ya nchi ya Misri, \v 24 mvua ya mawe ikanyesha na radi ikamulika pote. Ikawa dhoruba ya kutisha ambayo haijakuwako katika nchi ya Misri, tangu nchi hiyo iwe taifa. \v 25 Mvua ya mawe ikaharibu kila kitu katika nchi ya Misri kilichokuwa katika mashamba, watu na wanyama, ikaharibu kila kitu kinachoota mashambani na kuvunja kila mti. \v 26 Mahali pekee ambapo mvua ya mawe haikunyesha ni nchi ya Gosheni, ambako Waisraeli waliishi. \p \v 27 Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni akawaambia, “Wakati huu nimetenda dhambi. \nd Bwana\nd* ni mwenye haki, mimi na watu wangu ni wakosaji. \v 28 Mwombeni \nd Bwana\nd*, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kututosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.” \p \v 29 Mose akamjibu, “Nitakapokuwa nimetoka nje ya mji, nitanyoosha mikono yangu juu kumwomba \nd Bwana\nd*. Ngurumo zitakoma na hapatakuwepo mvua ya mawe tena, ili upate kujua kuwa, nchi ni mali ya \nd Bwana\nd*. \v 30 Lakini ninajua kuwa wewe na maafisa wako bado hammwogopi \nd Bwana\nd* Mungu.” \p \v 31 (Kitani na shayiri viliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa na masuke, na kitani ilikuwa katika kutoa maua. \v 32 Hata hivyo, ngano na jamii nyingine ya ngano hazikuharibiwa kwa sababu zilikuwa hazijakomaa bado.) \p \v 33 Kisha Mose akaondoka kwa Farao akaenda nje ya mji. Mose akanyoosha mikono yake kuelekea kwa \nd Bwana\nd*, ngurumo na mvua ya mawe vikakoma, mvua haikuendelea tena kunyesha nchini. \v 34 Farao alipoona kwamba mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akafanya dhambi tena. Yeye na maafisa wake wakafanya mioyo yao kuwa migumu. \v 35 Kwa hiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waende, kama vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa amesema kupitia Mose. \c 10 \s1 Pigo La Nane: Nzige \p \v 1 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake kuwa mgumu na mioyo ya maafisa wake ili kwamba nipate kutenda ishara hizi zangu za ajabu miongoni mwao \v 2 ili upate kuwaeleza watoto wako na wajukuu wako jinsi nilivyowatendea Wamisri kwa ukali na jinsi nilivyofanya ishara zangu miongoni mwao, nanyi mpate kujua kuwa Mimi ndimi \nd Bwana\nd*.” \p \v 3 Kwa hiyo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo \nd Bwana\nd*, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. \v 4 Kama ukikataa kuwaachia waende, kesho nitaleta nzige katika nchi yako. \v 5 Nao watafunika uso wa ardhi hata usionekane. Watatafuna mabaki machache yaliyobakizwa baada ya ile mvua ya mawe, yaani pamoja na kila mti unaoota katika mashamba yenu. \v 6 Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii mpaka leo hii.’ ” Ndipo Mose akageuka na kumwacha Farao. \p \v 7 Maafisa wa Farao wakamwambia, “Mpaka lini huyu mtu atakuwa tanzi kwetu? Waachie hao watu waende zao, ili wapate kumwabudu \nd Bwana\nd* Mungu wao. Je, bado hutambui kuwa Misri imeangamia?” \p \v 8 Ndipo Mose na Aroni wakaletwa kwa Farao. Farao akawaambia, “Nendeni, mkamwabudu \nd Bwana\nd* Mungu wenu. Lakini ni nani hasa watakaokwenda?” \p \v 9 Mose akajibu, “Tutakwenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na kondoo zetu, ngʼombe, mbuzi, farasi na punda kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwa \nd Bwana\nd*.” \p \v 10 Farao akasema, “\nd Bwana\nd* awe pamoja nanyi, kama nikiwaruhusu mwondoke pamoja na wanawake wenu na watoto wenu! Ni wazi kwamba mna makusudi mabaya. \v 11 La hasha! Wanaume peke yao na waende, wakamwabudu \nd Bwana\nd*, kwa kuwa hilo ndilo mmekuwa mkiomba.” Kwa hiyo Mose na Aroni wakaondolewa mbele ya Farao. \p \v 12 Basi \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako juu ya Misri ili kundi la nzige liweze kuingia juu ya nchi na kutafuna kila kitu kiotacho katika mashamba na kila kitu kilichosazwa na ile mvua ya mawe.” \p \v 13 Kwa hiyo Mose akanyoosha fimbo yake juu ya Misri, \nd Bwana\nd* akauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige. \v 14 Wakaivamia Misri yote na kukaa kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe hapajapata kuwepo pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwepo tena. \v 15 Wakafunika ardhi yote mpaka ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kile chote kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe, kila kitu kiotacho mashambani pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu chochote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri. \p \v 16 Farao akawaita Mose na Aroni kwa haraka na kuwaambia, “Nimetenda dhambi dhidi ya \nd Bwana\nd* Mungu wenu na dhidi yenu pia. \v 17 Sasa unisamehe dhambi yangu mara moja tena na umwombe \nd Bwana\nd* Mungu wako aondoe pigo hili baya kwangu.” \p \v 18 Kisha Mose akaondoka kwa Farao akamwomba \nd Bwana\nd*. \v 19 Naye \nd Bwana\nd* akaugeuza upepo ukavuma kutoka magharibi, wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki popote katika nchi ya Misri. \v 20 Lakini \nd Bwana\nd* akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke. \s1 Pigo La Tisa: Giza \p \v 21 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.” \v 22 Kwa hiyo Mose akaunyoosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. \v 23 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi. \p \v 24 Ndipo Farao akamwita Mose na kusema, “Nendeni, mkamwabudu \nd Bwana\nd*. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ngʼombe wenu waacheni.” \p \v 25 Lakini Mose akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele za \nd Bwana\nd* Mungu wetu. \v 26 Sisi ni lazima tuondoke na mifugo yetu pia, wala hakuna ukwato utakaoachwa nyuma. Inatupasa kutumia baadhi ya hiyo mifugo katika kumwabudu \nd Bwana\nd* Mungu wetu, kwa kuwa mpaka tutakapofika huko hatutakuwa tumefahamu ni nini tutakachotumia katika kumwabudu \nd Bwana\nd*.” \p \v 27 Lakini \nd Bwana\nd* akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hakuwa radhi kuwaachia waondoke. \v 28 Farao akamwambia Mose, “Ondoka mbele yangu! Hakikisha kuwa hutakuja mbele yangu tena! Siku ile utakapouona uso wangu utakufa.” \p \v 29 Mose akamjibu, “Iwe kama ulivyosema! Kamwe sitauona uso wako tena.” \c 11 \s1 Pigo La Kumi: Kuuawa Wazaliwa Wa Kwanza \p \v 1 Basi \nd Bwana\nd* alikuwa amemwambia Mose, “Nitaleta pigo moja zaidi kwa Farao na katika nchi ya Misri. Baada ya hilo, atawaacha mwondoke hapa na atakapofanya hivyo, atawafukuza mtoke kabisa. \v 2 Waambie watu wote waume kwa wake wawaombe majirani zao vitu vya fedha na vya dhahabu.” \v 3 (\nd Bwana\nd* akawafanya Wamisri wawe na moyo wa ukarimu kwa Waisraeli, naye Mose mwenyewe akaheshimiwa sana na maafisa wa Farao na watu wote katika nchi ya Misri.) \p \v 4 Kwa hiyo Mose akasema, “Hili ndilo \nd Bwana\nd* asemalo: ‘Panapo usiku wa manane Mimi nitapita katika nchi yote ya Misri. \v 5 Kila mwanaume kifungua mimba katika Misri atakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Farao, aketiye penye kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mtumwa wa kike, anayesaga nafaka kwa jiwe, pamoja na kila mzaliwa wa kwanza wa mifugo. \v 6 Patakuwepo kilio kikubwa katika nchi yote ya Misri, kilio kibaya ambacho hakijakuwepo wala kamwe hakitakuwepo tena. \v 7 Lakini miongoni mwa Waisraeli hakuna hata mbwa atakayembwekea mwanadamu wala mnyama yeyote.’ Ndipo mtakapojua kuwa \nd Bwana\nd* huweka tofauti kati ya Misri na Israeli. \v 8 Maafisa hawa wako wote watanijia, wakisujudu mbele yangu, wakisema, ‘Ondoka, wewe pamoja na watu wako wote wanaokufuata!’ Baada ya haya nitaondoka.” Kisha Mose, huku akiwa amewaka hasira, akamwacha Farao. \p \v 9 \nd Bwana\nd* alikuwa amemwambia Mose, “Farao atakataa kukusikiliza, ili maajabu yangu yapate kuongezeka katika nchi ya Misri.” \v 10 Mose na Aroni wakafanya maajabu haya yote mbele ya Farao, lakini \nd Bwana\nd* akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke katika nchi yake. \c 12 \s1 Pasaka \p \v 1 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose na Aroni katika nchi ya Misri, \v 2 “Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani mwezi wa kwanza wa mwaka wenu. \v 3 Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya familia yake, mmoja kwa kila nyumba. \v 4 Ikiwa nyumba yoyote ina watu wachache wasioweza kumaliza huyo mwana-kondoo mzima, nyumba hiyo itabidi ishirikiane na nyumba ya jirani wa karibu, baada ya kuzingatia idadi ya watu waliomo. Mtaangalia ni kiasi gani cha nyama kitahitajika kulingana na mahitaji ya kila mtu. \v 5 Wanyama mtakaowachagua, lazima wawe wa kiume wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari, mwaweza kuwachukua kati ya kondoo au mbuzi. \v 6 Tunzeni wanyama hao mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi, ambapo lazima watu wa jumuiya yote ya Israeli wachinje wanyama hao wakati wa jioni. \v 7 Ndipo watakapochukua baadhi ya hiyo damu na kuipaka kwenye vizingiti vya juu na miimo ya milango ya nyumba ambamo watakula wana-kondoo hao. \v 8 Usiku huo huo watakula nyama iliyookwa kwenye moto, pamoja na mboga chungu za majani na mikate isiyotiwa chachu. \v 9 Msile nyama mbichi wala iliyochemshwa, lakini iwe imeokwa kwenye moto, kichwa, miguu na nyama zake za ndani. \v 10 Msibakize nyama yoyote mpaka asubuhi; nazo kama zitabakia mpaka asubuhi, lazima mziteketeze kwa moto. \v 11 Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka ya \nd Bwana\nd*. \p \v 12 “Usiku huo huo nitapita katika nchi yote ya Misri na kumuua kila mzaliwa wa kwanza, wa wanadamu na wa wanyama, nami nitaihukumu miungu yote ya Misri. Mimi ndimi \nd Bwana\nd*. \v 13 Damu itakuwa ishara kwa ajili yenu ya kuonyesha nyumba ambazo mtakuwamo; nami nitakapoiona damu, nitapita juu yenu. Hakuna pigo la uharibifu litakalowagusa ninyi nitakapoipiga Misri. \p \v 14 “Siku hii itakuwa kumbukumbu kwenu, mtaiadhimisha kuwa sikukuu kwa \nd Bwana\nd*, katika vizazi vyenu vyote: mtaishika kuwa amri ya kudumu. \v 15 Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. Katika siku ya kwanza mtaondoa chachu yote ndani ya nyumba zenu, kwa maana yeyote atakayekula chochote chenye chachu kuanzia siku ya kwanza hadi ya saba lazima akatiliwe mbali kutoka Israeli. \v 16 Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, na kusanyiko jingine katika siku ya saba. Katika siku hizo msifanye kazi kamwe isipokuwa kutayarisha chakula cha kila mmoja; hilo ndilo tu mtakalofanya. \p \v 17 “Mtaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa sababu hiyo ndiyo siku ile niliyovitoa vikosi vyenu kutoka Misri. Mtaiadhimisha siku hii kwa vizazi vyenu vyote kuwa amri ya kudumu. \v 18 Katika mwezi wa kwanza mtakula mikate isiyotiwa chachu, kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne hadi jioni ya siku ya ishirini na moja. \v 19 Kwa muda wa siku saba isionekane chachu yoyote katika nyumba zenu. Yeyote alaye chochote chenye chachu ndani yake, lazima akatiliwe mbali kutoka jumuiya ya Israeli, akiwa ni mgeni au mzawa. \v 20 Msile chochote kilichotiwa chachu. Popote muishipo, ni lazima mle mikate isiyotiwa chachu.” \p \v 21 Ndipo Mose akawaita wazee wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni mara moja mkachague wanyama kwa ajili ya jamaa zenu, mkachinje mwana-kondoo wa Pasaka. \v 22 Chukueni kitawi cha hisopo, kichovyeni kwenye damu iliyopo kwenye sinia na kuipaka baadhi ya hiyo damu kwenye vizingiti na kwenye miimo yote miwili ya milango. Mtu yeyote asitoke nje ya mlango wa nyumba yake mpaka asubuhi. \v 23 \nd Bwana\nd* apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi. \p \v 24 “Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu. \v 25 Mtakapoingia katika nchi \nd Bwana\nd* atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii. \v 26 Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’ \v 27 Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa \nd Bwana\nd*, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo watu wa Israeli waliposujudu na kuabudu. \v 28 Waisraeli wakafanya kama vile \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose na Aroni. \p \v 29 Ilipofika usiku wa manane, \nd Bwana\nd* akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia. \v 30 Farao, na maafisa wake wote, na Wamisri wote wakaamka usiku, na kulikuwa na kilio kikubwa katika nchi ya Misri, kwa kuwa haikuwepo nyumba ambayo hakufa mtu. \s1 Kutoka \p \v 31 Wakati huo Farao akawaita Mose na Aroni na kuwaambia, “Ondokeni! Tokeni kwa watu wangu, ninyi pamoja na Waisraeli! Nendeni mkamwabudu \nd Bwana\nd* kama mlivyoomba. \v 32 Chukueni makundi yenu ya kondoo na mbuzi pamoja na ngʼombe, kama mlivyosema, nanyi mwende zenu. Nanyi pia mnibariki.” \p \v 33 Wamisri wakawahimiza Waisraeli waondoke kwa haraka na kuacha nchi yao. Kwa kuwa walisema, “La sivyo, tutakufa wote!” \v 34 Hivyo watu wakachukua donge lao la unga kabla ya kutiwa chachu, wakaweka ndani ya mabakuli ya kukandia, wakayaviringisha katika vitambaa na kuyabeba mabegani mwao. \v 35 Waisraeli wakafanya kama Mose alivyowaelekeza, nao wakawaomba Wamisri wawapatie vitu vya fedha, dhahabu na nguo. \v 36 Basi \nd Bwana\nd* alikuwa amewafanya Wamisri kuwa wakarimu kwa hawa watu, wakawapatia Waisraeli vile walivyotaka kwao; kwa hiyo wakawateka nyara Wamisri. \p \v 37 Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi. Walikuwepo wanaume wapatao 600,000 waendao kwa miguu bila kuhesabu wanawake na watoto. \v 38 Watu wengine wengi wakafuatana nao, pamoja na makundi makubwa ya mifugo wakiwemo kondoo, mbuzi na ngʼombe. \v 39 Wakatengeneza maandazi yasiyotiwa chachu kwa ule unga uliokandwa waliokuwa wameutoa Misri, donge hilo la unga halikuwa limetiwa chachu, kwa kuwa walikuwa wameondolewa Misri kwa haraka nao hawakuwa na muda wa kuandaa chakula chao. \p \v 40 Waisraeli walikuwa wameishi Misri kwa muda wa miaka 430. \v 41 Ilikuwa ni siku ya mwisho ya hiyo miaka 430, vikosi vyote vya \nd Bwana\nd* vilipokuwa vimeondoka Misri. \v 42 Kwa sababu \nd Bwana\nd* aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, katika usiku huu Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu \nd Bwana\nd* katika vizazi vijavyo. \s1 Masharti Kwa Ajili Ya Pasaka \p \v 43 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose na Aroni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka: \p “Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka. \v 44 Mtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri, \v 45 lakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula. \p \v 46 “Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote. \v 47 Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo. \p \v 48 “Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya \nd Bwana\nd* ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila. \v 49 Sheria iyo hiyo itamuhusu mzawa na mgeni anayeishi miongoni mwenu.” \p \v 50 Waisraeli wote walifanya kama vile \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose na Aroni. \v 51 Siku ile ile \nd Bwana\nd* akawatoa Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao. \c 13 \s1 Kuwekwa Wakfu Kwa Wazaliwa Wa Kwanza \p \v 1 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 2 “Niwekeeni wakfu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume. Kila mtoto wa kwanza aliye kifungua tumbo miongoni mwa Waisraeli ni mali yangu, akiwa wa mwanadamu au wa mnyama.” \p \v 3 Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu \nd Bwana\nd* aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu. \v 4 Leo, katika mwezi wa Abibu,\f + \fr 13:4 \ft Abibu ni jina la mwezi wa kwanza kwa Wayahudi, ambao ni mwezi wa nne katika kalenda yetu.\f* mnatoka. \v 5 \nd Bwana\nd* atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu: \v 6 Kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu na katika siku ya saba utamfanyia \nd Bwana\nd* sikukuu. \v 7 Kwa muda wa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu, pasionekane kitu chochote kilicho na chachu miongoni mwako, wala chachu yoyote isionekane popote ndani ya mipaka yako. \v 8 Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo \nd Bwana\nd* alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ \v 9 Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya \nd Bwana\nd* inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa \nd Bwana\nd* alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. \v 10 Ni lazima uishike amri hii kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka. \p \v 11 “Baada ya \nd Bwana\nd* kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako, \v 12 inakupasa kumtolea \nd Bwana\nd* mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya \nd Bwana\nd*. \v 13 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo, lakini kama hukumkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa. \p \v 14 “Katika siku zijazo, mwanao akikuuliza, ‘Hii ina maana gani?’ Mwambie, ‘Kwa mkono wenye nguvu \nd Bwana\nd* alitutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. \v 15 Farao alipokataa kwa ukaidi kuturuhusu kuondoka, \nd Bwana\nd* aliua kila mzaliwa wa kwanza wa Wamisri, mwanadamu na wa mnyama. Hii ndiyo sababu ninatoa dhabihu kwa \nd Bwana\nd* mzaliwa wa kwanza wa kiume, wa kila tumbo na kumkomboa kila mzaliwa wa kwanza wa wana wangu.’ \v 16 Jambo hili litakuwa kama ishara kwenye mkono wako na kama alama kwenye paji la uso wako, kwamba \nd Bwana\nd* alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu.” \s1 Nguzo Ya Wingu Na Moto \p \v 17 Farao alipowaachia watu waende, Mungu hakuwaongoza kufuata njia ipitiayo katika nchi ya Wafilisti, ingawa njia hiyo ilikuwa fupi zaidi. Kwa maana Mungu alisema, “Wakikabiliana na vita, wanaweza kubadili mawazo yao na kurudi Misri.” \v 18 Kwa hiyo Mungu akawaongoza watu kupitia njia ya kuzunguka kupitia jangwani, kuelekea Bahari ya Shamu. Waisraeli walipanda kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiandaa kwa vita. \p \v 19 Mose akachukua mifupa ya Yosefu kwa sababu Yosefu alikuwa amewaapisha wana wa Israeli. Alikuwa amewaambia, “Hakika Mungu atakuja kuwasaidia, nanyi ni lazima mwiichukue mifupa yangu mwende nayo kutoka mahali hapa.” \p \v 20 Baada ya Waisraeli kuondoka Sukothi wakapiga kambi huko Ethamu pembeni mwa jangwa. \v 21 Wakati wa mchana \nd Bwana\nd* aliwatangulia kwa nguzo ya wingu kuwaongoza katika njia yao, na wakati wa usiku aliwatangulia kwa nguzo ya moto kuwaangazia, ili waweze kusafiri mchana au usiku. \v 22 Ile nguzo ya wingu wakati wa mchana au ile nguzo ya moto wakati wa usiku haikuondoka mahali pake mbele ya watu. \c 14 \s1 Kuvuka Bahari Ya Shamu \p \v 1 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 2 “Waambie Waisraeli wageuke nyuma na wapige kambi karibu na Pi-Hahirothi, kati ya Migdoli na bahari. Watapiga kambi kando ya bahari, mkabala na Baal-Sefoni. \v 3 Farao atafikiri kwamba, ‘Hao Waisraeli wanatangatanga katika nchi kwa kuchanganyikiwa, nalo jangwa limewafungia.’ \v 4 Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi \nd Bwana\nd*.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo. \p \v 5 Mfalme wa Misri alipoambiwa kuwa Waisraeli wamekimbia, Farao na maafisa wake wakabadili nia zao kuhusu Waisraeli, wakasema, “Tumefanya nini? Tumewaachia Waisraeli waende zao na tumeukosa utumishi wao!” \v 6 Kwa hiyo akaandaliwa gari lake la vita, naye akaenda pamoja na jeshi lake. \v 7 Akachukua magari bora mia sita, pamoja na magari mengine yote ya Misri, pamoja na maafisa wa magari hayo yote. \v 8 \nd Bwana\nd* akaufanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri. \v 9 Nao Wamisri, yaani farasi wote wa Farao na magari ya vita, wapanda farasi na vikosi vya askari, wakawafuatia Waisraeli, wakawakuta karibu na Pi-Hahirothi, mkabala na Baal-Sefoni walipokuwa wamepiga kambi kando ya bahari. \p \v 10 Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia \nd Bwana\nd*. \v 11 Wakamwambia Mose, “Je, ni kwamba hayakuwako makaburi huko Misri hata umetuleta tufe huku jangwani? Umetufanyia nini kututoa Misri? \v 12 Hatukukuambia tulipokuwa huko Misri, tuache tuwatumikie Wamisri? Ingekuwa vyema zaidi kwetu kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani!” \p \v 13 Mose akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu \nd Bwana\nd* atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena. \v 14 \nd Bwana\nd* atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu.” \p \v 15 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Kwa nini wewe unanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele. \v 16 Inua fimbo yako na unyooshe mkono wako juu ya bahari ili kuyagawa maji, hivyo kwamba Waisraeli wapate kupita mahali pakavu baharini. \v 17 Nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu kusudi waingie baharini wakiwafuatia. Nami nitajipatia utukufu kupitia Farao pamoja na jeshi lake lote, kupitia magari yake ya vita na wapanda farasi wake. \v 18 Nao Wamisri watajua kwamba Mimi ndimi \nd Bwana\nd* nitakapojipatia utukufu kupitia Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake.” \p \v 19 Ndipo malaika wa Mungu, aliyekuwa akisafiri mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akakaa nyuma yao. Pia ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao na kusimama nyuma, \v 20 ikakaa kati ya majeshi ya Misri na Israeli. Usiku kucha wingu likaleta giza upande mmoja na nuru kwa upande mwingine, kwa hiyo hakuna aliyemkaribia mwenzake usiku kucha. \p \v 21 Ndipo Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, naye \nd Bwana\nd* akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika, \v 22 nao Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, maji yakiwa ukuta upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto. \p \v 23 Wamisri wakawafuatia ndani ya bahari, pamoja na farasi wote wa Farao, magari ya vita na wapanda farasi. \v 24 Karibia mapambazuko, \nd Bwana\nd* akaliangalia jeshi la Wamisri kutoka ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha. \v 25 Mungu akayaondoa magurudumu ya magari yao, kwa hivyo wakayaendesha kwa shida. Nao Wamisri wakasema, “Tuachane na Waisraeli! \nd Bwana\nd* anawapigania dhidi ya Misri.” \s1 Wafuatiaji Wazama \p \v 26 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudiane yawafunike Wamisri, magari yao ya vita na wapanda farasi wao.” \v 27 Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, wakati wa mapambazuko bahari ikarudiana na kuwa kama kawaida. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini \nd Bwana\nd* akawasukumia ndani ya bahari. \v 28 Maji yakarudiana na kuyafunika magari ya vita na wapanda farasi pamoja na jeshi lote la Farao lililokuwa limewafuata Waisraeli ndani ya bahari. Hakuna hata mmoja wao aliyenusurika. \p \v 29 Lakini Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, ukiwepo ukuta wa maji upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto. \v 30 Siku ile \nd Bwana\nd* akawaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wamisri, nao Waisraeli wakawaona Wamisri wamelala ufuoni mwa bahari wakiwa wamekufa. \v 31 Basi Waisraeli walipoona uwezo mkubwa \nd Bwana\nd* aliodhihirisha dhidi ya Wamisri, watu wakamwogopa \nd Bwana\nd* na wakaweka tumaini lao kwake na kwa Mose mtumishi wake. \c 15 \s1 Wimbo Wa Mose Na Miriamu \p \v 1 Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia \nd Bwana\nd* wimbo huu: \q1 “Nitamwimbia \nd Bwana\nd*, \q2 kwa kuwa ametukuzwa sana. \q1 Farasi na mpanda farasi \q2 amewatosa baharini. \q1 \v 2 \nd Bwana\nd* ni nguvu zangu na wimbo wangu; \q2 amekuwa wokovu wangu. \q1 Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, \q2 Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. \q1 \v 3 \nd Bwana\nd* ni shujaa wa vita; \q2 \nd Bwana\nd* ndilo jina lake. \q1 \v 4 Magari ya vita ya Farao na jeshi lake \q2 amewatosa baharini. \q1 Maafisa wa Farao walio bora sana \q2 wamezamishwa katika Bahari ya Shamu. \q1 \v 5 Maji yenye kina yamewafunika, \q2 wamezama mpaka vilindini kama jiwe. \b \q1 \v 6 “Mkono wako wa kuume, Ee \nd Bwana\nd* \q2 ulitukuka kwa uweza. \q1 Mkono wako wa kuume, Ee \nd Bwana\nd*, \q2 ukamponda adui. \q1 \v 7 Katika ukuu wa utukufu wako, \q2 ukawaangusha chini wale waliokupinga. \q1 Uliachia hasira yako kali, \q2 ikawateketeza kama kapi. \q1 \v 8 Kwa pumzi ya pua zako \q2 maji yalijilundika. \q1 Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta, \q2 vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. \b \q1 \v 9 “Adui alijivuna, \q2 ‘Nitawafuatia, nitawapata. \q1 Nitagawanya nyara; \q2 nitajishibisha kwa wao. \q1 Nitafuta upanga wangu \q2 na mkono wangu utawaangamiza.’ \q1 \v 10 Lakini ulipuliza kwa pumzi yako, \q2 bahari ikawafunika. \q1 Wakazama kama risasi \q2 kwenye maji makuu. \b \q1 \v 11 “Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee \nd Bwana\nd*? \q2 Ni nani kama Wewe: \q3 uliyetukuka katika utakatifu, \q3 utishaye katika utukufu, \q3 ukitenda maajabu? \q1 \v 12 Uliunyoosha mkono wako wa kuume \q2 na nchi ikawameza. \b \q1 \v 13 “Katika upendo wako usiokoma utawaongoza \q2 watu uliowakomboa. \q1 Katika nguvu zako utawaongoza \q2 mpaka makao yako matakatifu. \q1 \v 14 Mataifa watasikia na kutetemeka, \q2 uchungu utawakamata watu wa Ufilisti. \q1 \v 15 Wakuu wa Edomu wataogopa, \q2 viongozi wa Moabu watatetemeka kwa hofu, \q1 watu wa Kanaani watayeyuka, \q2 \v 16 vitisho na hofu vitawaangukia. \q1 Kwa nguvu ya mkono wako \q2 watatulia kama jiwe, \q1 mpaka watu wako waishe kupita, Ee \nd Bwana\nd*, \q2 mpaka watu uliowanunua wapite. \q1 \v 17 Utawaingiza na kuwapandikiza \q2 juu ya mlima wa urithi wako: \q1 hapo mahali, Ee \nd Bwana\nd*, ulipopafanya kuwa makao yako, \q2 mahali patakatifu, Ee \nd Bwana\nd*, ulipopajenga kwa mikono yako. \q1 \v 18 \nd Bwana\nd* atatawala \q2 milele na milele.” \p \v 19 Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, \nd Bwana\nd* aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini wana wa Israeli walipita baharini mahali pakavu. \v 20 Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. \v 21 Miriamu akawaimbia: \q1 “Mwimbieni \nd Bwana\nd*, \q2 kwa maana ametukuka sana. \q1 Farasi na mpanda farasi \q2 amewatosa baharini.” \s1 Maji Ya Mara Na Elimu \p \v 22 Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji. \v 23 Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara\f + \fr 15:23 \ft Mara maana yake ni Chungu.\f*) \v 24 Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?” \p \v 25 Ndipo Mose akamlilia \nd Bwana\nd*, naye \nd Bwana\nd* akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu. \p Huko \nd Bwana\nd* akawapa amri na sheria na huko akawajaribu. \v 26 Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya \nd Bwana\nd* Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi \nd Bwana\nd*, niwaponyaye.” \p \v 27 Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji. \c 16 \s1 Mana Na Kware \p \v 1 Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka Elimu, wakafika Jangwa la Sini, lililokuwa kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka Misri. \v 2 Huko jangwani hiyo jumuiya yote wakawanungʼunikia Mose na Aroni. \v 3 Waisraeli wakawaambia, “Laiti tungelikufa kwa mkono wa \nd Bwana\nd* huko Misri! Huko tuliketi tukizunguka masufuria ya nyama na tukala vyakula tulivyovitaka, lakini ninyi mmetuleta huku jangwani ili mpate kuua mkutano huu wote kwa njaa.” \p \v 4 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nitanyesha mikate kutoka mbinguni kwa ajili yenu. Watu watatoka kila siku na kukusanya kitakachowatosha kwa siku ile, kwa njia hii, nitawajaribu nione kama watafuata maelekezo yangu. \v 5 Siku ya sita watatayarisha kile waletacho ndani, nacho kitakuwa mara mbili kuliko ya kile walichokusanya kila siku.” \p \v 6 Kwa hiyo Mose na Aroni wakawaambia Waisraeli wote, “Jioni mtajua kwamba \nd Bwana\nd* ndiye aliwatoa Misri, \v 7 kisha asubuhi mtauona utukufu wa \nd Bwana\nd*, kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani hata mtunungʼunikie?” \v 8 Pia Mose akasema, “Mtajua kuwa alikuwa \nd Bwana\nd* wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnungʼuniki dhidi yetu, bali dhidi ya \nd Bwana\nd*.” \p \v 9 Kisha Mose akamwambia Aroni, “Iambie jumuiya yote ya Waisraeli kwamba, ‘Mje mbele zake \nd Bwana\nd*, kwa maana amesikia manungʼuniko yenu.’ ” \p \v 10 Aroni alipokuwa akizungumza na jumuiya yote ya Waisraeli, wakatazama kuelekea jangwani, na huko wakaona utukufu wa \nd Bwana\nd* ukitokeza katika wingu. \p \v 11 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 12 “Nimesikia manungʼuniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua ya kwamba Mimi ndimi \nd Bwana\nd* Mungu wenu.’ ” \p \v 13 Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na tabaka la umande kuzunguka kambi. \v 14 Wakati umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya uso wa jangwa. \v 15 Waisraeli walipoona, wakaambiana, “Hiki ni nini?” Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani. \p Mose akawaambia, “Huu ndio mkate ambao \nd Bwana\nd* amewapa mle. \v 16 Hivi ndivyo \nd Bwana\nd* alivyoamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi\f + \fr 16:16 \ft Pishi ni kipimo cha ujazo, kwa Kiebrania ni omeri, ambacho ni sawa na kilo mbili.\f* moja kwa kila mtu mliye naye katika hema yenu.’ ” \p \v 17 Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. \v 18 Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji. \p \v 19 Kisha Mose akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.” \p \v 20 Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Mose, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Mose akawakasirikia. \p \v 21 Kila asubuhi, kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji na jua lilipokuwa kali, iliyeyuka. \v 22 Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwarifu Mose. \v 23 Mose akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza \nd Bwana\nd*: ‘Kesho itakuwa siku ya mapumziko, Sabato takatifu kwa \nd Bwana\nd*. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke mpaka asubuhi.’ ” \p \v 24 Kwa hiyo wakavihifadhi mpaka asubuhi, kama Mose alivyoagiza, na havikunuka wala kuwa na mabuu. \v 25 Mose akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa \nd Bwana\nd*. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. \v 26 Kwa siku sita mtakusanya, lakini siku ya saba, yaani Sabato, hakutakuwepo chochote.” \p \v 27 Hata hivyo, baadhi ya watu wakatoka kwenda kukusanya siku ya saba, lakini hawakupata chochote. \v 28 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu mpaka lini? \v 29 Fahamuni kuwa \nd Bwana\nd* amewapa ninyi Sabato, ndiyo sababu katika siku ya sita amewapa mikate ya siku mbili. Kila mmoja inampasa kukaa pale alipo katika siku ya saba. Hata mmoja haruhusiwi kutoka.” \v 30 Kwa hiyo watu wakapumzika siku ya saba. \p \v 31 Watu wa Israeli wakaita ile mikate mana\f + \fr 16:31 \ft Mana maana yake ni mkate kutoka mbinguni.\f* Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. \v 32 Mose akasema, “Hivi ndivyo alivyoagiza \nd Bwana\nd*: ‘Chukueni pishi ya mana na kuhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo ili vione mikate niliyowapa mle jangwani nilipowatoa katika nchi ya Misri.’ ” \p \v 33 Kwa hiyo Mose akamwambia Aroni, “Chukua gudulia na uweke pishi moja ya mana ndani yake. Kisha uweke mbele za \nd Bwana\nd* ili kihifadhiwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.” \p \v 34 Kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose, hatimaye Aroni alikuja kuihifadhi ndani ya Sanduku la Ushuhuda. \v 35 Waisraeli wakala mana kwa miaka arobaini, mpaka walipofika katika nchi iliyokaliwa na watu; walikula mana hadi walipofika mpakani mwa Kanaani. \p \v 36 (Pishi moja ni sehemu ya kumi ya kipimo cha efa.\f + \fr 16:36 \ft Efa moja ni sawa na kilo 22.\f*) \c 17 \s1 Maji Kutoka Kwenye Mwamba \r (Hesabu 20:1-13) \p \v 1 Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama \nd Bwana\nd* alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. \v 2 Kwa hiyo wakagombana na Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.” \p Mose akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu \nd Bwana\nd*?” \p \v 3 Lakini watu walikuwa na kiu huko, wakanungʼunika dhidi ya Mose, wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri, ukatuleta hapa utuue kwa kiu sisi, watoto wetu na mifugo yetu?” \p \v 4 Kisha Mose akamlilia \nd Bwana\nd*, akasema, “Niwafanyie nini watu hawa? Sasa wanakaribia kunipiga kwa mawe.” \p \v 5 \nd Bwana\nd* akamjibu Mose, “Pita mbele ya watu. Wachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa Israeli, ichukue mkononi mwako ile fimbo uliyopiga nayo Mto Naili, nawe uende. \v 6 Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Mose akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli. \v 7 Naye akapaita mahali pale Masa,\f + \fr 17:7 \ft Masa maana yake ni Kujaribu.\f* na Meriba\f + \fr 17:7 \ft Meriba maana yake ni Kugombana.\f* kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu \nd Bwana\nd* wakisema, “Je, \nd Bwana\nd* yu pamoja nasi au la?” \s1 Vita Na Waamaleki \p \v 8 Waamaleki wakaja na kuwashambulia Waisraeli huko Refidimu. \v 9 Mose akamwambia Yoshua, “Chagua baadhi ya watu wetu na uende kupigana na Waamaleki. Kesho nitasimama juu ya kilima nikiwa na fimbo ya Mungu mkononi mwangu.” \p \v 10 Kwa hiyo Yoshua akapigana na Waamaleki kama Mose alivyomwagiza, nao Mose, Aroni na Huri wakapanda juu ya kilima. \v 11 Ikawa wakati wote Mose alipokuwa amenyanyua mikono yake, Waisraeli walikuwa wakishinda, lakini kila aliposhusha mikono yake Waamaleki walishinda. \v 12 Mikono ya Mose ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Aroni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Mose, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti mpaka jua lilipozama. \v 13 Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga. \p \v 14 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Andika mambo haya katika kitabu ili yakumbukwe, na uhakikishe kwamba Yoshua amesikia, kwa sababu nitafuta kabisa kumbukumbu la Amaleki chini ya mbingu.” \p \v 15 Mose akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi.\f + \fr 17:15 \ft Yehova Nisi maana yake ni \+nd Bwana\+nd* ni Bendera yangu.\f* \v 16 Mose akasema, “Kwa maana mikono iliinuliwa mpaka kwenye kiti cha enzi cha \nd Bwana\nd*. \nd Bwana\nd* atakuwa na vita dhidi ya Waamaleki kutoka kizazi hata kizazi.” \c 18 \s1 Yethro Amtembelea Mose \p \v 1 Basi Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wa Mose, akawa amesikia kila kitu Mungu alichomfanyia Mose na watu wake wa Israeli, pia jinsi \nd Bwana\nd* alivyowatoa Israeli Misri. \p \v 2 Baada ya Mose kumrudisha mkewe Sipora, Yethro baba mkwe wake alimpokea \v 3 pamoja na wanawe wawili. Jina la mmoja aliitwa Gershomu, kwa kuwa Mose alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” \v 4 Mwingine aliitwa Eliezeri, kwa kuwa alisema, “Mungu wa baba yangu alikuwa msaada wangu, akaniokoa kutoka upanga wa Farao.” \p \v 5 Yethro, baba mkwe wa Mose, pamoja na wana wawili wa Mose na mkewe, wakamjia Mose huko jangwani, mahali alipokuwa amepiga kambi karibu na mlima wa Mungu. \v 6 Yethro alikuwa ametuma ujumbe kwake Mose, kusema, “Mimi Yethro baba mkwe wako ninakuja kwako pamoja na mke wako na wanao wawili.” \p \v 7 Kwa hiyo Mose akatoka kumlaki baba mkwe wake, akainama na kumbusu. Wakasalimiana, kisha wakaingia hemani. \v 8 Mose akamwambia baba mkwe wake kuhusu kila kitu \nd Bwana\nd* alichomfanyia Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na pia kuhusu shida zote walizokutana nazo njiani na jinsi \nd Bwana\nd* alivyowaokoa. \p \v 9 Yethro akafurahishwa sana kusikia juu ya mambo yote mazuri \nd Bwana\nd* aliyowatendea Waisraeli kuwaokoa kutoka mkono wa Wamisri. \v 10 Yethro akasema, “Sifa na ziwe kwa \nd Bwana\nd*, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri. \v 11 Sasa najua ya kuwa \nd Bwana\nd* ni mkuu kuliko miungu mingine yote, kwa kuwa amewatendea hivi wale waliowatenda Israeli kwa ujeuri.” \v 12 Kisha Yethro, baba mkwe wa Mose, akaleta sadaka ya kuteketezwa na dhabihu nyingine kwa Mungu, naye Aroni pamoja na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula pamoja na baba mkwe wa Mose mbele za Mungu. \s1 Ushauri Wa Yethro \r (Kumbukumbu 1:9-18) \p \v 13 Siku iliyofuata, Mose akachukua nafasi yake kama hakimu wa watu, nao wakasimama kumzunguka kuanzia asubuhi hadi jioni. \v 14 Baba mkwe wake alipoona yote Mose anayowafanyia watu, akasema, “Ni nini hiki unachowafanyia watu? Kwa nini wewe unakuwa mwamuzi wa watu hawa peke yako, wakati watu hawa wamesimama wakikuzunguka tangu asubuhi mpaka jioni?” \p \v 15 Mose akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu. \v 16 Kila wakiwa na shauri huletwa kwangu, nami huamua kati ya mtu na mwenzake na kuwajulisha juu ya amri na sheria za Mungu.” \p \v 17 Baba mkwe wa Mose akamjibu, “Unachofanya sio kizuri. \v 18 Wewe pamoja na watu hawa wanaokujia mtajichosha bure. Kazi ni nzito sana kwako, huwezi kuibeba mwenyewe. \v 19 Sasa nisikilize mimi, nitakupa shauri, naye Mungu na awe pamoja nawe. Yapasa wewe uwe mwakilishi wa watu mbele za Mungu na ulete mashauri yao kwake. \v 20 Uwafundishe amri na sheria, tena uwaonyeshe namna ya kuishi na kazi zinazowapasa wao kufanya. \v 21 Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. \v 22 Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe. \v 23 Kama ukifanya hivi, na ikiwa Mungu ameagiza hivyo, utaweza kushinda uchovu, nao watu hawa wote watarudi nyumbani wameridhika.” \s1 Kuchaguliwa Kwa Waamuzi \p \v 24 Mose akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. \v 25 Mose akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. \v 26 Wakatumika kama waamuzi wa watu kwa wakati wote. Mashauri magumu wakayaleta kwa Mose, lakini yale yaliyo rahisi wakayaamua wenyewe. \p \v 27 Kisha Mose akaagana na Yethro baba mkwe wake, naye akarudi kwa nchi yake. \c 19 \s1 Waisraeli Kwenye Mlima Sinai \p \v 1 Mnamo mwezi wa tatu baada ya Waisraeli kuondoka Misri, siku kama iyo hiyo, wakafika katika Jangwa la Sinai. \v 2 Baada ya kuondoka Refidimu, waliingia katika Jangwa la Sinai na Israeli wakapiga kambi pale jangwani mbele ya mlima. \p \v 3 Kisha Mose akakwea kwenda kwa Mungu, naye \nd Bwana\nd* akamwita kutoka kwenye ule mlima akasema, “Hivi ndivyo utakavyosema na nyumba ya Yakobo na utakachowaambia watu wa Israeli: \v 4 ‘Ninyi wenyewe mmeona nililofanya huko Misri, jinsi nilivyowabeba kwenye mbawa za tai na kuwaleta kwangu. \v 5 Sasa kama mkinitii kikamilifu na kutunza Agano langu, basi ninyi mtakuwa mali yangu ya thamani kubwa miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, \v 6 ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli.” \p \v 7 Kwa hiyo Mose akarudi, akawaita wazee wa watu na kuwaambia maneno yote ambayo \nd Bwana\nd* alikuwa amemwamuru ayaseme. \v 8 Watu wote wakajibu kwa pamoja, “Tutafanya kila kitu \nd Bwana\nd* alichokisema.” Naye Mose akarudisha majibu yao kwa \nd Bwana\nd*. \p \v 9 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nitakujia katika wingu zito, ili watu wanisikie nikinena nawe na kila mara waweke tumaini lao kwako.” Kisha Mose akamwambia \nd Bwana\nd* yale ambayo watu walikuwa wamesema. \p \v 10 Naye \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nenda kwa watu ukawaweke wakfu leo na kesho. Waambie wafue nguo zao \v 11 na wawe tayari siku ya tatu, kwa sababu siku hiyo, \nd Bwana\nd* atashuka juu ya mlima Sinai machoni pa watu wote. \v 12 Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu, uwaambie, ‘Mwe waangalifu, msije mkapanda mlimani au kuugusa. Yeyote atakayeugusa mlima hakika atauawa. \v 13 Hakika atapigwa mawe au kupigwa mishale; mkono wa mtu hautamgusa. Akiwa mwanadamu au mnyama, hataruhusiwa kuishi.’ Ila tu wakati baragumu itakapopigwa kwa mfululizo, ndipo watu wote watakapopanda mlimani.” \p \v 14 Baada ya Mose kushuka kutoka mlimani akawaendea watu na kuwaweka wakfu, wakafua nguo zao. \v 15 Kisha akawaambia watu, “Jitayarisheni kwa ajili ya siku ya tatu. Mwanaume yeyote asimkaribie mwanamke.” \p \v 16 Asubuhi ya siku ya tatu kulikuwa na ngurumo na radi pamoja na wingu nene juu ya mlima na mlio mkubwa sana wa tarumbeta. Kila mmoja aliyekuwa kambini akatetemeka. \v 17 Kisha Mose akawaongoza watu kutoka kambini kukutana na Mungu, nao wakasimama chini ya mlima. \v 18 Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu \nd Bwana\nd* alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka kwenye tanuru kubwa na mlima wote ukatetemeka kwa nguvu nyingi, \v 19 nayo sauti ya tarumbeta ikawa kubwa zaidi na zaidi. Kisha Mose akazungumza na sauti ya \nd Bwana\nd* ikamjibu. \p \v 20 \nd Bwana\nd* akashuka juu ya Mlima Sinai na akamwita Mose apande juu mlimani. Kwa hiyo Mose akapanda juu, \v 21 naye \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Shuka ukawaonye watu ili wasijipenyeze kutafuta kumwona \nd Bwana\nd* na wengi wao wakafa. \v 22 Hata makuhani, watakaomkaribia \nd Bwana\nd* ni lazima wajiweke wakfu, la sivyo \nd Bwana\nd* atawaadhibu.” \p \v 23 Mose akamwambia \nd Bwana\nd*, “Watu hawawezi kupanda mlima Sinai kwa sababu wewe mwenyewe ulituonya ukisema, ‘Wekeni mipaka kuuzunguka mlima na kuutenga kama patakatifu.’ ” \p \v 24 \nd Bwana\nd* akajibu, “Shuka ukamlete Aroni pamoja nawe. Lakini makuhani pamoja na watu wasije wakalazimisha kuja kwa \nd Bwana\nd*, nisije nikawaadhibu.” \p \v 25 Basi Mose akashuka kwa watu na kuwaambia lile aliloambiwa. \c 20 \s1 Amri Kumi \r (Kumbukumbu 5:1-21) \p \v 1 Ndipo Mungu akasema maneno haya yote: \b \pi3 \v 2 “Mimi ndimi \nd Bwana\nd* Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. \li \v 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. \li \v 4 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. \v 5 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, \nd Bwana\nd* Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, \v 6 lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu. \li \v 7 Usilitaje bure jina la \nd Bwana\nd* Mungu wako, kwa kuwa \nd Bwana\nd* hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. \li \v 8 Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. \v 9 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, \v 10 lakini siku ya saba ni Sabato kwa \nd Bwana\nd* Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. \v 11 Kwa kuwa kwa siku sita, \nd Bwana\nd* aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo \nd Bwana\nd* akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu. \li \v 12 Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa \nd Bwana\nd* Mungu wako. \li \v 13 Usiue. \li \v 14 Usizini. \li \v 15 Usiibe. \li \v 16 Usimshuhudie jirani yako uongo. \li \v 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.” \s1 Watu Wanaogopa \r (Kumbukumbu 5:22-33) \p \v 18 Watu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali \v 19 na wakamwambia Mose, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.” \p \v 20 Mose akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.” \p \v 21 Watu wakabaki mbali, wakati Mose alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa. \s1 Sanamu Na Madhabahu \p \v 22 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli hivi: ‘Mmejionea wenyewe kwamba nimesema nanyi kutoka mbinguni: \v 23 Msijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu. \p \v 24 “ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo zako, mbuzi na ngʼombe zako. Popote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki. \v 25 Ikiwa unanitengenezea madhabahu ya mawe, usiijenge kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia chombo cha kuchongea mtaitia unajisi. \v 26 Msitumie ngazi kupandia kwenye madhabahu yangu, uchi wako usije ukadhihirika kwa chini.’ \c 21 \s1 Watumishi Wa Kiebrania \r (Kumbukumbu 15:12-18) \p \v 1 “Hizi ndizo sheria utakazoweka mbele ya Waisraeli: \b \p \v 2 “Kama ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye atakwenda zake pasipo kulipa chochote. \v 3 Kama akija peke yake, atakwenda huru peke yake, lakini kama akija na mke, ataondoka pamoja naye. \v 4 Kama bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake na huyo mwanaume ataondoka peke yake. \p \v 5 “Lakini kama mtumishi akisema, ‘Ninampenda bwana wangu, mke wangu pamoja na watoto na sitaki kuwa huru,’ \v 6 ndipo bwana wake atakapolazimika kumpeleka mbele ya waamuzi. Kisha atampeleka kwenye mlango au kizingiti na kutoboa sikio lake kwa shazia. Naye atamtumikia bwana wake maisha yake yote. \p \v 7 “Kama mtu akimuuza binti yake kuwa mtumwa, hataachwa huru kama watumwa wa kiume waachiwavyo. \v 8 Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumuuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu. \v 9 Kama akimchagua aolewe na mwanawe, ni lazima ampe haki za kuwa binti yake. \v 10 Ikiwa huyo mwana aliyeozwa mtumwa mwanamke ataoa mwanamke mwingine, ni lazima aendelee kumtosheleza huyo mke wa kwanza kwa chakula, mavazi na haki zote za ndoa. \v 11 Iwapo hatamtosheleza kwa mambo hayo matatu, huyo mke wa kwanza ataondoka na kuwa huru bila malipo yoyote ya fedha. \s1 Majeraha Ya Mwilini \p \v 12 “Yeyote ampigaye mtu na kumuua ni lazima auawe hakika. \v 13 Hata hivyo, kama hakumuua kwa makusudi, lakini Mungu akaruhusu itendeke, basi atakimbilia mahali nitakapomchagulia. \v 14 Lakini kama mtu akipanga na kumuua mwingine kwa makusudi, mwondoe katika madhabahu yangu na kumuua. \p \v 15 “Yeyote amshambuliaye baba yake au mama yake ni lazima auawe. \p \v 16 “Yeyote amtekaye nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe. \p \v 17 “Yeyote atakayemlaani baba yake au mama yake ni lazima auawe. \p \v 18 “Kama watu wakigombana na mmoja akimpiga mwingine kwa jiwe au kwa ngumi yake na hakufa bali akaugua na kulala kitandani, \v 19 yule aliyempiga ngumi hatahesabiwa kuwa na hatia kama mwenzake ataamka na kujikongoja kwa fimbo yake, lakini hata hivyo, ni lazima amlipe fidia ya muda wake aliopoteza na awajibike mpaka apone kabisa. \p \v 20 “Kama mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe \v 21 lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake. \p \v 22 “Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. \v 23 Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai, \v 24 jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, \v 25 kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, mchubuko kwa mchubuko. \p \v 26 “Ikiwa mtu atampiga mtumwa mwanaume au mwanamke kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho. \v 27 Kama akimvunja jino mtumwa wa kiume au wa kike, ni lazima amwache huru huyo mtumwa kwa kufidia hilo jino. \p \v 28 “Kama fahali akimuua mwanaume au mwanamke kwa kumpiga kwa pembe, fahali huyo ni lazima auawe kwa kupigwa mawe, na nyama yake haitaliwa. Lakini mwenye fahali huyo hatawajibika. \v 29 Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe. \v 30 Lakini ikiwa malipo yatatakiwa kwake, basi anaweza kulipa kinachodaiwa ili kuukomboa uhai wake. \v 31 Sheria hii pia itatumika ikiwa fahali atampiga kwa pembe mwana au binti. \v 32 Ikiwa fahali atampiga mtumwa wa kike au wa kiume, mwenye fahali atalipa shekeli thelathini\f + \fr 21:32 \ft Shekeli 30 ni sawa na gramu 300.\f* za fedha kwa bwana mwenye mtumwa, na fahali ni lazima auawe kwa mawe. \p \v 33 “Kama mtu akiacha shimo wazi, ama akachimba shimo kisha asilifukie, na ngʼombe au punda akatumbukia ndani yake, \v 34 mwenye shimo ni lazima alipe hasara iliyotokea; ni lazima amlipe mwenye mnyama. Mnyama aliyekufa atakuwa wake. \p \v 35 “Kama fahali wa mtu fulani atamuumiza fahali wa mtu mwingine na akafa, watamuuza yule aliye hai na wagawane sawa fedha pamoja na mnyama aliyekufa. \v 36 Hata hivyo, kama ikifahamika kwamba fahali huyo alikuwa na tabia ya kupiga kwa pembe na mwenyewe hakumfunga, ni lazima mwenye fahali alipe mnyama kwa mnyama, na mnyama aliyekufa atakuwa wake. \c 22 \s1 Ulinzi Wa Mali \p \v 1 “Kama mtu akiiba maksai au kondoo na kumchinja au kumuuza, ni lazima alipe ngʼombe watano badala ya maksai mmoja na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. \p \v 2 “Kama mwizi akishikwa anavunja nyumba akapigwa hata akafa, aliyemuua hana hatia ya kumwaga damu; \v 3 lakini jambo hilo likitokea wakati jua limechomoza, huyo mtu atakuwa na hatia ya kumwaga damu. \p “Mwizi huyo sharti alipe, lakini kama hana kitu, lazima auzwe ili alipe kwa ajili ya wizi wake. \p \v 4 “Kama mnyama aliyeibwa akikutwa hai mikononi mwake, ikiwa ni maksai au punda au kondoo, lazima alipe mara mbili. \p \v 5 “Kama mtu akichunga mifugo yake katika shamba au shamba la mizabibu, na akawaachia wajilishe katika shamba la mtu mwingine, ni lazima alipe vitu bora kutoka kwenye shamba lake mwenyewe au kutoka shamba lake la mizabibu. \p \v 6 “Kama moto ukiwaka na kuenea kwenye vichaka vya miiba na kuteketeza miganda ya nafaka au nafaka ambayo haijavunwa, au kuteketeza shamba lote, mtu yule aliyewasha moto lazima alipe. \p \v 7 “Kama mtu akimpa jirani yake fedha au mali nyingine amtunzie, na kama vikiibwa kutoka nyumba ya huyo jirani, kama mwizi atashikwa, lazima alipe mara mbili. \v 8 Lakini mwizi asipopatikana, mwenye nyumba atafika mbele ya waamuzi ili kuthibitisha kuwa hakuchukua mali ya mwenzake. \v 9 Pakiwepo jambo lolote la mali isiyo halali, ikiwa ni maksai, punda, kondoo, mavazi, ama mali yoyote iliyopotea ambayo fulani atasema, ‘Hii ni mali yangu,’ pande zote mbili wataleta mashauri yao mbele ya waamuzi. Yule ambaye waamuzi watamwona kuwa na hatia atamlipa jirani yake mara mbili. \p \v 10 “Kama mtu akimpa jirani yake punda, ngʼombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, akifa au akijeruhiwa au akichukuliwa wakati haonekani na mtu yeyote, \v 11 jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za \nd Bwana\nd*, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika. \v 12 Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama. \v 13 Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa. \p \v 14 “Kama mtu akimwazima mnyama kutoka kwa jirani yake, na kama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama. \v 15 Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara. \s1 Uwajibikaji Wa Kijamii \p \v 16 “Kama mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akilala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo. \v 17 Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu huyo msichana wake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira. \p \v 18 “Usiruhusu mwanamke mchawi aishi. \p \v 19 “Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe. \p \v 20 “Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa \nd Bwana\nd*, lazima aangamizwe. \p \v 21 “Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri. \p \v 22 “Usimdhulumu mjane wala yatima. \v 23 Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. \v 24 Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima. \p \v 25 “Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba. \v 26 Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama, \v 27 kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma. \p \v 28 “Usimkufuru Mungu au kumlaani mtawala wa watu wako. \p \v 29 “Usiache kutoa sadaka kutoka ghala lako au mapipa yako. \p “Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako. \v 30 Ufanye vivyo hivyo kwa ngʼombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe. \p \v 31 “Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa. \c 23 \s1 Sheria Za Haki Na Rehema \p \v 1 “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine. \p \v 2 “Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu, \v 3 nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake. \p \v 4 “Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake. \v 5 Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia. \p \v 6 “Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. \v 7 Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia. \p \v 8 “Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki. \p \v 9 “Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri. \s1 Sheria Za Sabato \p \v 10 “Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao, \v 11 lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kutoka kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni. \p \v 12 “Kwa siku sita fanya kazi zako, lakini siku ya saba usifanye kazi, ili maksai wako na punda wako wapate kupumzika, naye mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwako, pamoja na mgeni, wapate kustarehe. \p \v 13 “Uzingatie kutenda kila kitu nilichokuambia. Usiombe kwa majina ya miungu mingine, wala usiyaruhusu kusikika kinywani mwako. \s1 Sikukuu Tatu Za Mwaka \r (Kutoka 34:18-26; Kumbukumbu 16:1-17) \p \v 14 “Mara tatu kwa mwaka utanifanyia sikukuu. \p \v 15 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu; kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu kama nilivyokuagiza. Fanya jambo hili kwa wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa sababu katika mwezi huo ulitoka Misri. \p “Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu. \p \v 16 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako. \p “Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani. \p \v 17 “Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele za \nd Bwana\nd* Mwenyezi. \p \v 18 “Msitoe damu ya dhabihu kwangu pamoja na kitu chochote kilicho na chachu. \p “Mafuta ya mnyama wa sadaka ya sikukuu yangu yasibakizwe mpaka asubuhi. \p \v 19 “Utaleta malimbuko bora ya ardhi yako katika nyumba ya \nd Bwana\nd* Mungu wako. \p “Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake. \s1 Malaika Wa Mungu Kuandaa Njia \p \v 20 “Tazama, ninamtuma malaika akutangulie mbele yako akulinde njiani na kukuleta mpaka mahali nilipoandaa. \v 21 Mtamtii na kusikiliza kile anachokisema. Usiasi dhidi yake; hatakusamehe uasi wako, kwa maana Jina langu limo ndani yake. \v 22 Kama ukitii kweli kweli kile asemacho na kufanya yote nisemayo, nitakuwa adui wa adui zako, na nitawapinga wale wakupingao. \v 23 Malaika wangu atatangulia mbele yako na kukuleta katika nchi ya Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanaani, Wahivi na Wayebusi, nami nitawafutilia mbali. \v 24 Usiisujudie miungu yao, au kuiabudu, wala kufuata desturi yao. Utayabomoa kabisa na kuvunjavunja mawe yao ya ibada vipande vipande. \v 25 Utamwabudu \nd Bwana\nd* Mungu wako, na baraka zake zitakuwa juu ya vyakula vyako na maji yako. Nami nitaondoa maradhi miongoni mwako, \v 26 na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu. \p \v 27 “Nitapeleka utisho wangu mbele yako na kufadhaisha kila taifa utakalolifikia. Nitafanya adui zako wote wakupe kisogo na kukimbia. \v 28 Nitatanguliza manyigu mbele yako kuwafukuza Wahivi, Wakanaani na Wahiti waondoke njiani mwako. \v 29 Lakini sitawafukuza kwa mara moja, kwa sababu nchi itabaki ukiwa na wanyama pori watakuwa wengi mno kwako. \v 30 Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, mpaka uwe umeongezeka kiasi cha kutosha kuimiliki nchi. \p \v 31 “Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto Frati. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako. \v 32 Usifanye agano lolote nao wala na miungu yao. \v 33 Usiwaache waishi katika nchi yako, la sivyo watakusababisha utende dhambi dhidi yangu, kwa sababu ibada ya miungu yao hakika itakuwa mtego kwako.” \c 24 \s1 Agano Lathibitishwa \p \v 1 Kisha Mungu akamwambia Mose, “Njooni huku juu kwa \nd Bwana\nd*, wewe na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali, \v 2 lakini Mose peke yake ndiye atakayemkaribia \nd Bwana\nd*; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.” \p \v 3 Mose alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za \nd Bwana\nd*, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema \nd Bwana\nd* tutakifanya.” \v 4 Ndipo Mose akaandika kila kitu \nd Bwana\nd* alichokuwa amesema. \p Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli. \v 5 Kisha akawatuma vijana wanaume wa Kiisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa \nd Bwana\nd*. \v 6 Mose akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. \v 7 Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema \nd Bwana\nd*, nasi tutatii.” \p \v 8 Ndipo Mose akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo \nd Bwana\nd* amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.” \p \v 9 Mose na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani, \v 10 nao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu. \v 11 Lakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa. \p \v 12 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.” \p \v 13 Basi Mose akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Mose akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. \v 14 Mose akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.” \p \v 15 Mose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, \v 16 nao utukufu wa \nd Bwana\nd* ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba \nd Bwana\nd* akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu. \v 17 Kwa Waisraeli utukufu wa \nd Bwana\nd* ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. \v 18 Kisha Mose akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana. \c 25 \s1 Sadaka Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu \r (Kutoka 35:4-9) \p \v 1 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 2 “Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa. \v 3 Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: dhahabu, fedha na shaba; \v 4 nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi; \v 5 ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;\f + \fr 25:5 \fq Pomboo \ft hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. \f* mbao za mshita; \v 6 mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; \v 7 na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani. \p \v 8 “Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. \v 9 Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha. \s1 Sanduku La Agano \r (Kutoka 37:1-9) \p \v 10 “Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,\f + \fr 25:10 \ft Dhiraa mbili na nusu ni sawa na sentimita 112.5.\f* upana wa dhiraa moja na nusu,\f + \fr 25:10 \ft Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.\f* na kimo cha dhiraa moja na nusu. \v 11 Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. \v 12 Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. \v 13 Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. \v 14 Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. \v 15 Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa. \v 16 Kisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa. \p \v 17 “Tengeneza kifuniko cha upatanisho cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu. \v 18 Tengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. \v 19 Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; watengeneze makerubi hao wawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. \v 20 Makerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko. \v 21 Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. \v 22 Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli. \s1 Meza Ya Mikate Ya Wonyesho \r (Kutoka 37:10-16) \p \v 23 “Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,\f + \fr 25:23 \ft Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.\f* upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu. \v 24 Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. \v 25 Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,\f + \fr 25:25 \ft Nyanda nne ni sawa na sentimita 8.\f* na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. \v 26 Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. \v 27 Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza. \v 28 Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza. \v 29 Tengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka. \v 30 Utaweka mikate ya Wonyesho juu ya meza hii iwe mbele yangu daima. \s1 Kinara Cha Taa \r (Kutoka 37:17-24) \p \v 31 “Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja. \v 32 Matawi sita yatatokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. \v 33 Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa. \v 34 Juu ya kinara chenyewe vitakuwepo vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. \v 35 Tovu moja litakuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla. \v 36 Matovu na matawi yote yatakuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakifuliwa kwa dhahabu safi. \p \v 37 “Kisha tengeneza taa zake saba na uziweke juu ya kinara hicho ili ziangaze mbele yake. \v 38 Mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote zitakuwa za dhahabu safi. \v 39 Utatumia talanta moja\f + \fr 25:39 \ft Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.\f* ya dhahabu safi kutengeneza hicho kinara na vifaa vyake vyote. \v 40 Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani. \c 26 \s1 Maskani Ya Mungu \r (Kutoka 36:8-38) \p \v 1 “Tengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo. \v 2 Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,\f + \fr 26:2 \ft Dhiraa 28 ni sawa na mita 13.\f* na upana wa dhiraa nne\f + \fr 26:2 \ft Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.\f* \v 3 Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. \v 4 Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. \v 5 Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vielekeane. \v 6 Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya Hema liwe kitu kimoja. \p \v 7 “Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. \v 8 Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,\f + \fr 26:8 \ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\f* na upana wa dhiraa nne. \v 9 Unganisha hayo mapazia matano yawe fungu moja, na hayo mengine sita yawe fungu lingine. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya maskani. \v 10 Tengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. \v 11 Kisha tengeneza vifungo hamsini vya shaba, uviingize katika vile vitanzi ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. \v 12 Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia la Hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaningʼinizwa upande wa nyuma wa Hema. \v 13 Mapazia ya hema yatakuwa na urefu wa dhiraa moja zaidi pande zote, sehemu itakayobaki itaningʼinia pande zote za Hema ili kuifunika. \v 14 Tengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.\f + \fr 26:14 \fq Pomboo \ft hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. \f* \p \v 15 “Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. \v 16 Kila mhimili uwe na urefu wa dhiraa kumi\f + \fr 26:16 \ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.\f* na upana wa dhiraa moja na nusu, \v 17 zikiwa na ndimi mbili zilizo sambamba kila mmoja na mwingine. Tengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. \v 18 Tengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, \v 19 kisha tengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. \v 20 Kuhusu upande wa kaskazini wa maskani, tengeneza mihimili ishirini \v 21 na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \v 22 Kisha tengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, \v 23 na pia utengeneze mihimili miwili ya pembe za upande ulio mbali. \v 24 Katika pembe hizi mbili ni lazima mihimili yake iwe miwili kuanzia chini mpaka juu, na iingizwe kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili itafanana. \v 25 Kwa hiyo itakuwepo mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \p \v 26 “Pia tengeneza mataruma ya mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, \v 27 matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili ya mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. \v 28 Taruma la katikati litapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. \v 29 Funika hiyo mihimili kwa dhahabu, kisha tengeneza pete za dhahabu ambazo zitashikilia hayo mataruma. Pia funika hayo mataruma kwa dhahabu. \p \v 30 “Simamisha Hema sawasawa na mfano ulioonyeshwa kule mlimani. \p \v 31 “Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia. \v 32 Litundike kwa kulabu za dhahabu kwenye nguzo nne za mti wa mshita ambazo zimefunikwa kwa dhahabu, zikiwa zimesimamishwa kwenye vitako vinne vya fedha. \v 33 Ningʼiniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu. \v 34 Weka kifuniko cha kiti cha rehema juu ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. \v 35 Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa Hema, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa Hema. \p \v 36 “Kwa ajili ya ingilio la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. \v 37 Tengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya hilo pazia, na nguzo tano za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Kisha mimina vitako vitano vya shaba kwa ajili yake. \c 27 \s1 Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa \r (Kutoka 38:1-7) \p \v 1 “Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu;\f + \fr 27:1 \ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\f* itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano,\f + \fr 27:1 \ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\f* na upana wake dhiraa tano. \v 2 Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba. \v 3 Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto. \v 4 Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu. \v 5 Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. \v 6 Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba. \v 7 Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa. \v 8 Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani. \s1 Ua Wa Kukutania \r (Kutoka 38:9-20) \p \v 9 “Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,\f + \fr 27:9 \ft Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.\f* na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, \v 10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \v 11 Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \p \v 12 “Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,\f + \fr 27:12 \ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.\f* nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi. \v 13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. \v 14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \v 15 Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano\f + \fr 27:15 \ft Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.\f* kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \p \v 16 “Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini\f + \fr 27:16 \ft Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.\f* la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. \v 17 Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. \v 18 Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. \v 19 Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba. \s1 Mafuta Ya Kinara Cha Taa \r (Walawi 24:1-4) \p \v 20 “Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo. \v 21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za \nd Bwana\nd*. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo. \c 28 \s1 Mavazi Ya Kikuhani \r (Kutoka 39:1-7) \p \v 1 “Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. \v 2 Mshonee Aroni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima. \v 3 Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Aroni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani. \v 4 Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Aroni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. \v 5 Waambie watumie dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani safi. \s1 Kisibau \p \v 6 “Tengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi. \v 7 Kitakuwa na vipande viwili vya mabegani vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kufungia kisibau. \v 8 Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri. \p \v 9 “Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli \v 10 kufuatana na walivyozaliwa: majina sita katika kito kimoja, na mengine sita katika kito kingine. \v 11 Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu, \v 12 na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kisibau yawe kama vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli. Aroni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele za \nd Bwana\nd*. \v 13 Tengeneza vijalizo vya dhahabu \v 14 na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo. \s1 Kifuko Cha Kifuani \r (Kutoka 39:8-21) \p \v 15 “Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. \v 16 Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja\f + \fr 28:16 \ft Shibiri moja ni sawa na sentimita 22.\f* na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili. \v 17 Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; \v 18 katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; \v 19 safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; \v 20 na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu. \v 21 Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili. \p \v 22 “Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani, tengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. \v 23 Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili yake, uzifungie kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. \v 24 Funga ile mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete zilizo katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, \v 25 nazo zile ncha nyingine za mkufu zifunge kwenye vile vijalizo viwili, na uzishikamanishe na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele. \v 26 Tengeneza pete mbili za dhahabu, uzishikamanishe kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau. \v 27 Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uzishikamanishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau. \v 28 Pete za kifuko cha kifuani zitafungwa kwenye pete zile za kisibau kwa kamba ya buluu, ziunganishwe na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau. \p \v 29 “Wakati wowote Aroni aingiapo Mahali Patakatifu, atakuwa na yale majina ya wana wa Israeli moyoni mwake juu ya kile kifuko cha kifuani cha uamuzi kama kumbukumbu ya kudumu mbele za \nd Bwana\nd*. \v 30 Pia weka Urimu na Thumimu\f + \fr 28:30 \ft Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.\f* ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Aroni kila mara aingiapo mbele za \nd Bwana\nd*. Kwa hiyo siku zote Aroni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za \nd Bwana\nd*. \s1 Mavazi Mengine Ya Kikuhani \r (Kutoka 39:22-31) \p \v 31 “Shona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, \v 32 na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike. \v 33 Tengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kuzunguka pindo la hilo joho, na uweke pia vikengele vya dhahabu kati ya hayo makomamanga. \v 34 Hivyo vikengele vya dhahabu na makomamanga vitapishana kuzunguka upindo wa joho lile. \v 35 Ni lazima Aroni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za \nd Bwana\nd*, ili asije akafa. \p \v 36 “Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: \sc Mtakatifu kwa Bwana\sc*. \v 37 Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba. \v 38 Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwa \nd Bwana\nd*. \p \v 39 “Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi. \v 40 Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. \v 41 Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. \p \v 42 “Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. \v 43 Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. \p “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake. \c 29 \s1 Kuweka Wakfu Makuhani \r (Walawi 8:1-36) \p \v 1 “Hili ndilo utakalofanya ili kuwaweka wakfu makuhani ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani: Chukua fahali mchanga mmoja na kondoo dume wawili wasio na dosari. \v 2 Kutokana na unga laini wa ngano usiotiwa chachu, tengeneza mikate na maandazi yaliyokandwa kwa mafuta, pamoja na mikate midogo myembamba. \v 3 Viwekwe vyote ndani ya kikapu na kuvitoa pamoja na yule fahali na wale kondoo dume wawili. \v 4 Kisha mlete Aroni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. \v 5 Chukua yale mavazi na umvike Aroni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi. \v 6 Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba. \v 7 Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake. \v 8 Walete wanawe na uwavike makoti, \v 9 pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe. \p \v 10 “Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. \v 11 Mchinje huyo fahali mbele za \nd Bwana\nd* kwenye mlango wa Hema la Kukutania. \v 12 Chukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuipaka kwenye pembe za hayo madhabahu kwa kidole chako, na damu iliyobaki uimwage sehemu ya chini ya madhabahu. \v 13 Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu. \v 14 Lakini nyama ya huyo fahali na ngozi yake na matumbo yake utavichoma nje ya kambi. Hii ni sadaka ya dhambi. \p \v 15 “Chukua mmoja wa wale kondoo dume, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. \v 16 Mchinje huyo kondoo dume, chukua damu yake na uinyunyize pande zote za hayo madhabahu. \v 17 Mkate huyo kondoo dume vipande vipande na usafishe sehemu za ndani pamoja na miguu, ukiviweka pamoja na kichwa na vipande vingine. \v 18 Kisha mteketeze huyo kondoo dume mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa \nd Bwana\nd*, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa \nd Bwana\nd* kwa moto. \p \v 19 “Mchukue yule kondoo dume mwingine, naye Aroni na wanawe waweke mikono yao juu ya kichwa chake. \v 20 Mchinje, uchukue sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye masikio ya Aroni na wanawe, kwenye vidole gumba vya mikono yao ya kuume, pia kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Kisha nyunyiza hiyo damu pande zote za madhabahu. \v 21 Pia chukua sehemu ya damu iliyo juu ya madhabahu na sehemu ya mafuta ya upako, umnyunyizie Aroni na mavazi yake, pia wanawe na mavazi yao. Ndipo Aroni na wanawe pamoja na mavazi yao watakuwa wamewekwa wakfu. \p \v 22 “Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani yale yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu.) \v 23 Kutoka kwenye kile kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichoko mbele za \nd Bwana\nd*, chukua mkate, andazi lililokandwa kwa mafuta na mkate mdogo mwembamba. \v 24 Viweke vitu hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe na uviinue mbele za \nd Bwana\nd* kuwa sadaka ya kuinuliwa. \v 25 Kisha vichukue vitu hivyo kutoka mikononi mwao, uviteketeze juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kupendeza kwa \nd Bwana\nd*, sadaka iliyotolewa kwa \nd Bwana\nd* kwa moto. \v 26 Baada ya kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kuwekwa wakfu kwa Aroni, kiinue mbele za \nd Bwana\nd* kuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako. \p \v 27 “Weka wakfu zile sehemu za kondoo dume aliyetumika kwa kumweka wakfu Aroni na wanawe: kidari kile kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa. \v 28 Siku zote hili litakuwa fungu la kawaida kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Aroni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwa \nd Bwana\nd* kutoka sadaka zao za amani. \p \v 29 “Mavazi matakatifu ya Aroni yatakuwa ya wazao wake ili kwamba waweze kutiwa mafuta na kuwekwa wakfu wakiwa wameyavaa. \v 30 Mwana atakayeingia mahali pake kuwa kuhani na kuja kwenye Hema la Kukutania kuhudumu katika Mahali Patakatifu atayavaa kwa siku saba. \p \v 31 “Chukua nyama ya huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu uipike katika Mahali Patakatifu. \v 32 Aroni na wanawe wataila ile nyama ya huyo kondoo dume pamoja na ile mikate iliyo kwenye hicho kikapu wakiwa hapo ingilio la Hema la Kukutania. \v 33 Watakula sadaka hizi ambazo upatanisho ulifanywa kwazo kwa ajili ya kuwaweka wakfu na kuwatakasa. Lakini hakuna mtu mwingine yeyote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu. \v 34 Ikiwa nyama yoyote ya huyo kondoo dume iliyotumika kwa kuwaweka wakfu au mkate wowote umebaki mpaka asubuhi, vichomwe. Kamwe visiliwe, kwa sababu ni vitakatifu. \p \v 35 “Hivyo utamfanyia Aroni na wanawe kila kitu kama vile nilivyokuamuru: Utachukua muda wa siku saba kuwaweka wakfu. \v 36 Utatoa dhabihu ya fahali kila siku kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho. Takasa madhabahu kwa kufanya upatanisho kwa ajili yake, nayo uitie mafuta na kuiweka wakfu. \v 37 Kwa muda wa siku saba fanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuiweka wakfu. Ndipo madhabahu itakuwa takatifu sana na chochote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu. \p \v 38 “Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. \v 39 Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. \v 40 Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja\f + \fr 29:40 \ft Efa moja ni sawa na kilo 22.\f* ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini\f + \fr 29:40 \ft Robo ya hini ni sawa na lita moja.\f* ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji. \v 41 Huyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa \nd Bwana\nd* kwa moto. \p \v 42 “Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za \nd Bwana\nd*. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi, \v 43 Huko ndipo nitakapokutana na Waisraeli, nalo Hema la Kukutania litatakaswa na utukufu wangu. \p \v 44 “Kwa hiyo nitaliweka wakfu Hema la Kukutania pamoja na madhabahu, nami nitamweka wakfu Aroni na wanawe ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani. \v 45 Ndipo nitakapofanya makao miongoni mwa Waisraeli na kuwa Mungu wao. \v 46 Nao watajua kuwa Mimi Ndimi \nd Bwana\nd* Mungu wao, aliyewatoa Misri ili nipate kufanya makao miongoni mwao. Mimi Ndimi \nd Bwana\nd* Mungu wao. \c 30 \s1 Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba \r (Kutoka 37:25-28) \p \v 1 “Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba. \v 2 Madhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja,\f + \fr 30:2 \ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\f* na kimo cha dhiraa mbili,\f + \fr 30:2 \ft Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.\f* nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo. \v 3 Funika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka. \v 4 Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu. \v 5 Tengeneza mipiko kwa miti ya mshita na uifunike kwa dhahabu. \v 6 Weka hayo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya Sanduku la Ushuhuda, mahali ambapo nitakutana nawe. \p \v 7 “Itampasa Aroni kufukiza uvumba wenye harufu nzuri juu ya madhabahu kila siku asubuhi wakati anapowasha zile taa. \v 8 Itampasa afukize uvumba tena wakati anapowasha taa wakati wa machweo ili uvumba ufukizwe daima mbele za \nd Bwana\nd* kwa vizazi vijavyo. \v 9 Usifukize uvumba mwingine wowote juu ya madhabahu haya au sadaka nyingine yoyote ya kuteketezwa wala sadaka ya nafaka, wala usimimine sadaka ya kinywaji juu yake. \v 10 Mara moja kwa mwaka Aroni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa \nd Bwana\nd*.” \s1 Fedha Ya Upatanisho \p \v 11 Naye \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 12 “Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa \nd Bwana\nd* fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu. \v 13 Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli,\f + \fr 30:13 \ft Nusu shekeli ni sawa na gramu 6.\f* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.\f + \fr 30:13 \ft Gera 20 ni sawa na shekeli moja au gramu 12.\f* Hii nusu shekeli ni sadaka kwa \nd Bwana\nd*. \v 14 Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa \nd Bwana\nd*. \v 15 Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa \nd Bwana\nd* kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu. \v 16 Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za \nd Bwana\nd* kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.” \s1 Sinia La Kunawia \p \v 17 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 18 “Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake. \v 19 Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia. \v 20 Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili kwamba wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa \nd Bwana\nd* kwa moto, \v 21 watanawa mikono na miguu yao ili kwamba wasije wakafa. Hii itakuwa ni amri ya kudumu kwa ajili ya Aroni na wazao wake kwa vizazi vijavyo.” \s1 Mafuta Ya Upako \p \v 22 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 23 “Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 500\f + \fr 30:23 \ft Shekeli 500 ni sawa na kilo 6.\f* za manemane ya maji, shekeli 250\f + \fr 30:23 \ft Shekeli 250 ni sawa na kilo 3.\f* za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri, \v 24 shekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini\f + \fr 30:24 \ft Hini moja ni sawa na lita 4.\f* ya mafuta ya zeituni. \v 25 Vitengeneze vikolezi hivi kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako. \v 26 Kisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda, \v 27 meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, \v 28 madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote na sinia pamoja na kitako chake. \v 29 Utaviweka wakfu ili viwe vitakatifu sana na kila kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu. \p \v 30 “Mtie Aroni na wanawe mafuta na uwaweke wakfu ili waweze kunitumikia katika kazi ya ukuhani. \v 31 Waambie Waisraeli, ‘Haya yatakuwa mafuta matakatifu yangu ya upako kwa vizazi vijavyo. \v 32 Usiyamimine juu ya miili ya wanadamu wala usitengeneze mafuta ya aina nyingine kwa utaratibu huu. Ni mafuta matakatifu na ni lazima myaone kuwa ni matakatifu. \v 33 Mtu yeyote atakayetengeneza manukato kama hayo na yeyote atakayeyamimina juu ya mtu yeyote ambaye si kuhani atakatiliwa mbali na watu wake.’ ” \s1 Uvumba \p \v 34 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Chukua vikolezi vyenye harufu nzuri vifuatavyo: natafi, shekelethi, kelbena na uvumba safi vyote vikiwa na vipimo sawa, \v 35 pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu. \v 36 Saga baadhi yake kuwa unga na uweke mbele ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, mahali ambapo nitakutana nawe. Itakuwa takatifu sana kwenu. \v 37 Msitengeneze uvumba mwingine wowote wa namna hii kwa ajili yenu wenyewe; uoneni kuwa ni mtakatifu kwa \nd Bwana\nd*. \v 38 Yeyote atakayetengeneza uvumba kama huu ili kufurahia harufu yake nzuri lazima akatiliwe mbali na watu wake.” \c 31 \s1 Bezaleli Na Oholiabu \r (Kutoka 35:30–36:1) \p \v 1 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 2 “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, \v 3 nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, \v 4 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, \v 5 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi. \v 6 Tena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe: \v 7 Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema juu yake, pia na vifaa vyote vya kwenye hema, \v 8 meza na vifaa vyake, kinara cha taa cha dhahabu safi na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, \v 9 madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, sinia na kinara chake, \v 10 pamoja na mavazi matakatifu yaliyofumwa ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe wakati wanahudumu katika kazi ya ukuhani, \v 11 pia mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri kwa ajili ya Mahali Patakatifu. Watavitengeneza sawasawa kama vile nilivyokuagiza wewe.” \s1 Sabato \p \v 12 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, \v 13 “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi \nd Bwana\nd*, niwafanyaye ninyi watakatifu. \p \v 14 “ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake. \v 15 Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, takatifu kwa \nd Bwana\nd*. Yeyote afanyaye kazi yoyote siku ya Sabato ni lazima auawe. \v 16 Waisraeli wataishika Sabato, kuiadhimisha kwa vizazi vijavyo kuwa Agano la milele. \v 17 Itakuwa ishara kati yangu na Waisraeli milele, kwa kuwa kwa muda wa siku sita \nd Bwana\nd* aliumba mbingu na dunia, na siku ya saba akaacha kufanya kazi, akapumzika.’ ” \p \v 18 \nd Bwana\nd* alipomaliza kusema na Mose juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vile vibao viwili vya Ushuhuda, vibao vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu. \c 32 \s1 Ndama Wa Dhahabu \r (Kumbukumbu 9:6-29) \p \v 1 Watu walipoona kuwa Mose amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Aroni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.” \p \v 2 Aroni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.” \v 3 Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Aroni. \v 4 Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akavifanyiza kwa kusubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.” \p \v 5 Aroni alipoona hili, akajenga madhabahu mbele ya yule ndama na kutangaza, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa \nd Bwana\nd*.” \v 6 Kwa hiyo siku iliyofuata watu wakaamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketeza na sadaka za amani. Baadaye watu wakaketi kula na kunywa, nao wakasimama, wakajizamisha katika sherehe. \p \v 7 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Shuka, kwa sababu watu wako, uliowatoa Misri, wamepotoka. \v 8 Wamekuwa wepesi kugeuka na kuacha niliyowaamuru, na wamejitengenezea sanamu ya kuyeyusha yenye umbo la ndama. Wameisujudia na kuitolea dhabihu, nao wamesema, ‘Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli iliyokupandisha kutoka Misri.’ ” \p \v 9 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nimeona watu hawa, nao ni watu wenye shingo ngumu. \v 10 Sasa niache ili hasira yangu ipate kuwaka dhidi yao, nami nipate kuwaangamiza. Kisha nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa.” \p \v 11 Lakini Mose akamsihi \nd Bwana\nd* Mungu wake, akasema, “Ee \nd Bwana\nd*, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu? \v 12 Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako. \v 13 Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote ambayo niliwaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ” \v 14 Kisha \nd Bwana\nd* akawaonea huruma, wala hakuleta juu ya watu wake maafa aliyokuwa amekusudia. \p \v 15 Mose akageuka, akashuka kutoka mlimani akiwa na vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake. Vilikuwa vimeandikwa pande zote mbili, mbele na nyuma. \v 16 Vibao hivyo vilikuwa kazi ya Mungu; maandishi yalikuwa mwandiko wa Mungu, yaliyochorwa kama muhuri juu ya vibao. \p \v 17 Yoshua aliposikia sauti za watu wakipiga kelele, akamwambia Mose, “Kuna sauti ya vita kambini.” \p \v 18 Mose akajibu: \q1 “Si sauti ya ushindi, \q2 wala si sauti ya kushindwa; \q2 ni sauti ya kuimba ninayosikia.” \p \v 19 Mose alipoikaribia kambi na kuona yule ndama na ile michezo, hasira yake ikawaka, akatupa vile vibao vilivyokuwa mikononi mwake, akavipasua vipande vipande pale chini ya mlima. \v 20 Kisha akamchukua yule ndama waliokuwa wamemtengeneza na kumchoma kwenye moto, kisha akamsaga kuwa unga, akanyunyiza kwenye maji na kuwafanya Waisraeli wanywe. \p \v 21 Mose akamwambia Aroni, “Watu hawa walikufanyia nini, hata ukawaongoza kufanya dhambi kubwa hivyo?” \p \v 22 Aroni akamwambia, “Usikasirike bwana wangu. Unajua jinsi watu hawa walivyo tayari kwa maovu. \v 23 Wao waliniambia, ‘Tufanyie miungu itakayotuongoza. Kwa kuwa huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatufahamu yaliyompata.’ \v 24 Kwa hiyo nikawaambia, ‘Yeyote aliye na kito chochote cha dhahabu avue.’ Kisha wakanipa hiyo dhahabu, nami nikaitupa motoni, akatokea huyu ndama!” \p \v 25 Mose akaona kuwa watu wameasi, kwa kuwa Aroni alikuwa amewaacha waasi, na hivyo kuwa kichekesho kwa adui zao. \v 26 Kwa hiyo Mose akasimama kwenye ingilio la kambi, akasema, “Yeyote aliye upande wa \nd Bwana\nd*, aje upande wangu.” Walawi wote wakamjia. \p \v 27 Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ” \v 28 Walawi wakafanya kama Mose alivyoamuru, siku ile wakafa watu wapatao 3,000. \v 29 Kisha Mose akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa \nd Bwana\nd*, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.” \p \v 30 Siku iliyofuata Mose akawaambia watu, “Mmefanya dhambi kubwa. Lakini sasa nitapanda juu kwa \nd Bwana\nd*, labda nitaweza kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.” \p \v 31 Hivyo Mose akarudi kwa \nd Bwana\nd* na kumwambia, “Lo! Hawa watu wamefanya dhambi kubwa namna gani! Wamejitengenezea miungu ya dhahabu. \v 32 Lakini sasa nakusihi, wasamehe dhambi yao; lakini kama sivyo, basi nifute kutoka kwenye kitabu ulichoandika.” \p \v 33 \nd Bwana\nd* akamjibu Mose, “Yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta kutoka kwenye kitabu changu. \v 34 Sasa nenda, uongoze hao watu mpaka mahali nilipokuambia, naye malaika wangu atakutangulia. Pamoja na hayo, wakati utakapofika wa mimi kuwaadhibu, nitawaadhibu kwa ajili ya dhambi yao.” \p \v 35 Ndipo \nd Bwana\nd* akawapiga watu kwa ugonjwa wa tauni kwa sababu ya yale waliyoyafanya kwa ndama yule ambaye alitengenezwa na Aroni. \c 33 \s1 Amri Ya Kuondoka Sinai \p \v 1 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Ondoka mahali hapa, wewe pamoja na hao watu uliowapandisha kutoka Misri, mpande mpaka nchi niliyomwahidi Abrahamu, Isaki na Yakobo kwa kiapo, nikisema, ‘Nitawapa wazao wenu nchi hii.’ \v 2 Nitamtuma malaika mbele yenu, naye atawafukuza Wakanaani, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \v 3 Pandeni mwende katika nchi itiririkayo maziwa na asali. Lakini mimi sitakwenda pamoja nanyi, kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu, nisije nikawaangamiza njiani.” \p \v 4 Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote. \v 5 Kwa kuwa \nd Bwana\nd* alikuwa amemwambia Mose, “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni watu wenye shingo ngumu. Kama ningefuatana nanyi hata kwa muda mfupi, ningewaangamiza. Sasa vueni mapambo yenu, nami nitaamua nitakalowatendea.’ ” \v 6 Hivyo Waisraeli wakavua mapambo yao katika Mlima wa Horebu. \s1 Hema La Kukutania \p \v 7 Basi Mose alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania.” Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa \nd Bwana\nd*, angelikwenda katika Hema la Kukutania nje ya kambi. \v 8 Wakati wowote Mose alipokwenda kwenye Hema, watu wote waliinuka na kusimama kwenye maingilio ya mahema yao, wakimwangalia Mose mpaka aingie kwenye Hema. \v 9 Kila mara Mose alipoingia ndani ya hema, nguzo ya wingu ingeshuka chini na kukaa kwenye ingilio, wakati Mungu akizungumza na Mose. \v 10 Kila mara watu walipoona hiyo nguzo ya wingu ikiwa imesimama kwenye ingilio la hema, wote walisimama wakaabudu, kila mmoja kwenye ingilio la hema lake. \v 11 \nd Bwana\nd* angezungumza na Mose uso kwa uso, kama vile mtu azungumzavyo na rafiki yake. Kisha Mose angerudi kambini, lakini msaidizi wake kijana Yoshua mwana wa Nuni hakuondoka mle Hemani. \s1 Mose Na Utukufu Wa \nd Bwana\nd* \p \v 12 Mose akamwambia \nd Bwana\nd*, “Umekuwa ukiniambia, ‘Ongoza watu hawa,’ lakini hujanifahamisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Umesema, ‘Ninakujua wewe kwa jina lako, nawe umepata kibali mbele zangu.’ \v 13 Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako. Kumbuka kuwa taifa hili ni watu wako.” \p \v 14 \nd Bwana\nd* akajibu, “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.” \p \v 15 Kisha Mose akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa. \v 16 Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipokwenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?” \p \v 17 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.” \p \v 18 Kisha Mose akasema, “Basi nionyeshe utukufu wako.” \p \v 19 Ndipo \nd Bwana\nd* akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, \nd Bwana\nd*, mbele ya uso wako. Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.” \v 20 Lakini Mungu akasema, “Hutaweza kuuona uso wangu, kwa kuwa hakuna mtu yeyote awezaye kuniona akaishi.” \p \v 21 Kisha \nd Bwana\nd* akasema, “Kuna mahali karibu nami ambapo unaweza kusimama juu ya mwamba. \v 22 Utukufu wangu unapopita, nitakuweka gengeni kwenye mwamba na kukufunika kwa mkono wangu mpaka nitakapokwisha kupita. \v 23 Kisha nitaondoa mkono wangu nawe utaona mgongo wangu; lakini kamwe uso wangu hautaonekana.” \c 34 \s1 Vibao Vipya Vya Mawe \r (Kumbukumbu 10:1-5) \p \v 1 \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja. \v 2 Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. \v 3 Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ngʼombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.” \p \v 4 Kwa hiyo Mose akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama \nd Bwana\nd* alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake. \v 5 Kisha \nd Bwana\nd* akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, \nd Bwana\nd*. \v 6 \nd Bwana\nd* akapita mbele ya Mose, akitangaza, “\nd Bwana\nd*, \nd Bwana\nd*, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, \v 7 akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.” \p \v 8 Mara Mose akasujudu na kuabudu. \v 9 Mose akasema, “Ee \nd Bwana\nd*, kama nimepata kibali mbele zako, basi \nd Bwana\nd* uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.” \s1 Kufanya Agano Upya \r (Kutoka 23:14-19; Kumbukumbu 7:1-5; 16:1-17) \p \v 10 Kisha \nd Bwana\nd* akasema: “Tazama ninafanya Agano mbele ya watu wako wote. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza ile kazi nitakayowafanyia mimi \nd Bwana\nd* wenu. \v 11 Tii yale ninayokuamuru leo. Tazama nawafukuza mbele yako Waamori, Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. \v 12 Uwe mwangalifu, usifanye agano na wale wanaokaa katika nchi ile unayoiendea, la sivyo watakuwa mtego katikati yako. \v 13 Bomoa madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia na ukatekate nguzo zao za Ashera. \v 14 Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa \nd Bwana\nd*, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu. \p \v 15 “Uwe mwangalifu usifanye agano na wale watu wanaoishi katika nchi, kwa maana wakati wanapojifanyia ukahaba kwa miungu yao na kuwatolea kafara, watakualika wewe nawe utakula sadaka za matambiko yao. \v 16 Unapowachagua baadhi ya binti zao kuwa wake wa wana wenu na binti hao wakajifanyia ukahaba kwa miungu yao, watawaongoza wana wenu kufanya vivyo hivyo. \p \v 17 “Usijifanyie sanamu za kusubu. \p \v 18 “Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, kama nilivyokuamuru. Fanya hivi kwa wakati ulioamriwa, katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa kuwa katika mwezi huo ndipo wewe ulipotoka Misri. \p \v 19 “Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ngʼombe au wa kondoo au mbuzi. \v 20 Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume. \p “Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu. \p \v 21 “Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike. \p \v 22 “Utaadhimisha Sikukuu ya Majuma kwa malimbuko ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Mavuno mwishoni mwa mwaka. \v 23 Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote watakuja mbele za \nd Bwana\nd* Mwenyezi, Mungu wa Israeli. \v 24 Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na \nd Bwana\nd* Mungu wako. \p \v 25 “Usinitolee damu ya dhabihu pamoja na kitu chochote chenye chachu, wala usibakize dhabihu yoyote ya Sikukuu ya Pasaka mpaka asubuhi. \p \v 26 “Leta matunda ya kwanza yaliyo bora zaidi ya ardhi yako katika nyumba ya \nd Bwana\nd* Mungu wako. \p “Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.” \p \v 27 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya Agano na wewe pamoja na Israeli.” \v 28 Mose alikuwa huko pamoja na \nd Bwana\nd* kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi. \s1 Mngʼao Wa Uso Wa Mose \p \v 29 Mose alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa ukingʼaa, kwa sababu alikuwa amezungumza na \nd Bwana\nd*. \v 30 Aroni na Waisraeli wote walipomwona Mose, kuwa uso wake unangʼaa, waliogopa kumkaribia. \v 31 Lakini Mose akawaita, kwa hiyo Aroni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. \v 32 Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote \nd Bwana\nd* alizompa katika Mlima wa Sinai. \p \v 33 Mose alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake. \v 34 Lakini kila wakati Mose alipoingia mbele za \nd Bwana\nd* kuzungumza naye, aliondoa ule utaji mpaka alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa, \v 35 waliona kuwa uso wake unangʼaa. Kisha Mose angeliweka tena utaji juu ya uso wake mpaka alipokwenda kuzungumza na \nd Bwana\nd*. \c 35 \s1 Masharti Ya Sabato \p \v 1 Mose akakusanya jumuiya yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndiyo mambo ambayo \nd Bwana\nd* amewaamuru ninyi mfanye: \v 2 Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba itakuwa takatifu kwenu, Sabato ya kupumzika kwa \nd Bwana\nd*. Yeyote atakayefanya kazi yoyote siku hiyo ni lazima auawe. \v 3 Msiwashe moto mahali popote katika makazi yenu siku ya Sabato.” \s1 Vifaa Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu \r (Kutoka 25:1-9) \p \v 4 Mose akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo \nd Bwana\nd* aliloamuru: \v 5 Toeni sadaka kwa \nd Bwana\nd* kutoka mali mliyo nayo. Kila mmoja aliye na moyo wa kupenda atamletea \nd Bwana\nd* sadaka ya dhahabu, fedha na shaba; \v 6 nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi; singa za mbuzi; \v 7 ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;\f + \fr 35:7 \fq Pomboo \ft hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. \f* mbao za mshita; \v 8 mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; \v 9 vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani. \p \v 10 “Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu \nd Bwana\nd* alichoamuru: \v 11 Maskani pamoja na hema lake na kifuniko chake, vibanio, mihimili, mataruma, nguzo na vitako; \v 12 Sanduku la Agano pamoja na mipiko yake, kifuniko cha kiti cha rehema na pazia linalokizuia; \v 13 meza na mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, mikate ya Wonyesho; \v 14 kinara cha taa kwa ajili ya mwanga pamoja na vifaa vyake vyote, taa na mafuta kwa ajili ya mwanga; \v 15 madhabahu ya kufukiza uvumba pamoja na mipiko yake, mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri; pazia la mlangoni mahali pa kuingilia ndani ya maskani; \v 16 madhabahu ya sadaka za kuteketeza pamoja na wavu wake wa shaba, mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote; sinia la shaba pamoja na tako lake; \v 17 pazia la eneo la ua pamoja na nguzo zake na vitako vyake, pazia la ingilio la kwenye ua; \v 18 vigingi vya hema kwa ajili ya maskani pamoja na ua na kamba zake; \v 19 mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu kwa ajili ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.” \p \v 20 Ndipo jumuiya yote ya Waisraeli ilipoondoka mbele ya Mose, \v 21 na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa \nd Bwana\nd*, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu. \v 22 Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa \nd Bwana\nd*. \v 23 Kila mmoja aliyekuwa na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi, au singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, au ngozi za pomboo, wakavileta. \v 24 Wale waliotoa sadaka ya fedha au shaba wakavileta kama sadaka kwa \nd Bwana\nd*, na kila aliyekuwa na mti wa mshita kwa ajili ya kazi yoyote ile akauleta. \v 25 Kila mwanamke aliyekuwa na ujuzi alisokota kwa mikono yake na alileta kile alichosokota, iwe ni nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi. \v 26 Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi. \v 27 Viongozi wakaleta vito vya shohamu pamoja na vito vingine vya thamani kwa ajili ya kuweka kwenye kisibau na kwenye kifuko cha kifuani. \v 28 Wakaleta pia vikolezi na mafuta ya zeituni kwa ajili ya mwanga, kwa ajili ya mafuta ya upako na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri. \v 29 Waisraeli wote waume kwa wake waliokuwa wanapenda wakaleta mbele za \nd Bwana\nd* kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya \nd Bwana\nd* aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Mose. \s1 Bezaleli Na Oholiabu \r (Kutoka 31:1-11) \p \v 30 Kisha Mose akawaambia Waisraeli, “Tazameni, \nd Bwana\nd* amemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, \v 31 naye amemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, na uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, \v 32 ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, \v 33 kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi wa kupendeza. \v 34 Tena amempa yeye pamoja na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, uwezo wa kufundisha wengine. \v 35 Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zifanywazo na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari. \c 36 \nb \v 1 Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu \nd Bwana\nd* aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile \nd Bwana\nd* alivyoagiza.” \p \v 2 Ndipo Mose akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye \nd Bwana\nd* alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi. \v 3 Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi. \v 4 Ikafika wakati mafundi wote wenye ujuzi waliokuwa wakiifanya kazi yote ya mahali patakatifu wakasimamisha kazi zao, \v 5 wakaja na kumwambia Mose, “Watu wanaleta vitu vingi kuliko tunavyohitaji kwa ajili ya kazi hii ambayo \nd Bwana\nd* ameagiza ifanyike.” \p \v 6 Ndipo Mose akatoa agizo, nao wakapeleka neno hili katika kambi yote: “Mtu yeyote mwanaume au mwanamke asilete tena kitu chochote kwa ajili ya sadaka ya mahali patakatifu.” Hivyo watu wakazuiliwa kuleta zaidi, \v 7 kwa sababu walivyokuwa navyo tayari vilitosha na kuzidi kuifanya kazi yote. \s1 Maskani Ya Mungu \r (Kutoka 26:1-37) \p \v 8 Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. \v 9 Mapazia yote yalitoshana kwa ukubwa: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,\f + \fr 36:9 \ft Dhiraa 28 ni sawa na mita 12.6.\f* na upana wa dhiraa nne\f + \fr 36:9 \ft Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8.\f* \v 10 Wakayaunganisha mapazia matano pamoja, pia wakafanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. \v 11 Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. \v 12 Wakatengeneza pia vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vikaelekeana. \v 13 Kisha wakatengeneza vifungo hamsini vya dhahabu, na wakavitumia kufunga na kuunganisha zile fungu mbili za mapazia pamoja ili maskani ipate kuwa kitu kimoja. \p \v 14 Wakatengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. \v 15 Mapazia hayo kumi na moja yalikuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,\f + \fr 36:15 \ft Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.\f* na upana wa dhiraa nne. \v 16 Wakaunganisha mapazia matano kuwa fungu moja, na hayo mengine sita kuwa fungu lingine. \v 17 Kisha wakatengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. \v 18 Wakatengeneza vifungo hamsini vya shaba ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. \v 19 Kisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.\f + \fr 36:19 \fq Pomboo \ft hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. \f* \p \v 20 Wakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. \v 21 Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi,\f + \fr 36:21 \ft Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.\f* na upana wa dhiraa moja na nusu,\f + \fr 36:21 \ft Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.\f* \v 22 zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. \v 23 Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, \v 24 na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. \v 25 Kwa upande wa kaskazini wa maskani wakatengeneza mihimili ishirini \v 26 na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \v 27 Wakatengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, \v 28 na mihimili miwili ikatengenezwa kwa ajili ya pembe za maskani za upande uliokuwa mbali. \v 29 Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana. \v 30 Kwa hiyo kulikuwa na mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. \p \v 31 Wakatengeneza pia mataruma kwa mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, \v 32 matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. \v 33 Wakatengeneza taruma la katikati, likapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. \v 34 Wakaifunika hiyo mihimili kwa dhahabu, na wakatengeneza pete za dhahabu za kushikilia hayo mataruma. Pia wakayafunika hayo mataruma kwa dhahabu. \p \v 35 Wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye hilo pazia. \v 36 Wakatengeneza nguzo nne za mti wa mshita kwa ajili yake na kuzifunika kwa dhahabu. Wakatengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya nguzo hizo, na kusubu vitako vinne vya fedha. \v 37 Kwa ajili ya ingilio la hema wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. \v 38 Pia wakatengeneza nguzo tano zenye kulabu. Wakafunika ncha za juu za hizo nguzo pamoja na tepe zake kwa dhahabu, na pia wakatengeneza vitako vyake vitano vya shaba. \c 37 \s1 Sanduku La Agano \r (Kutoka 25:10-22) \p \v 1 Bezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu,\f + \fr 37:1 \ft Dhiraa moja na nusu ni sawa na mita 1.13.\f* upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. \v 2 Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. \v 3 Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. \v 4 Kisha akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. \v 5 Akaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. \p \v 6 Akatengeneza kifuniko cha upatanisho kwa dhahabu safi: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. \v 7 Kisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. \v 8 Akatengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; akawatengeneza kuwa kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. \v 9 Makerubi hao walikuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, wakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao walielekeana, wakitazama hicho kifuniko. \s1 Meza \r (Kutoka 25:23-30) \p \v 10 Akatengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,\f + \fr 37:10 \ft Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.\f* upana wa dhiraa moja,\f + \fr 37:10 \ft Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.\f* na kimo cha dhiraa moja na nusu. \v 11 Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. \v 12 Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,\f + \fr 37:12 \ft Nyanda nne ni sawa na sentimita 8.\f* na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. \v 13 Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. \v 14 Pete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. \v 15 Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu. \v 16 Vyombo vyote vya mezani vilitengenezwa kwa dhahabu safi: yaani sahani zake, masinia, na bakuli na bilauri zake kwa ajili ya kumiminia sadaka za vinywaji. \s1 Kinara Cha Taa \r (Kutoka 25:31-40) \p \v 17 Akatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja. \v 18 Matawi sita yalitokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. \v 19 Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vilikuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyotokeza kwenye kile kinara cha taa. \v 20 Juu ya kinara chenyewe kulikuwepo na vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. \v 21 Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, matawi sita kwa jumla. \v 22 Matovu na matawi yote yalikuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakiwa yamefuliwa kwa dhahabu safi. \p \v 23 Akatengeneza taa zake saba, na pia mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote kwa dhahabu safi. \v 24 Akatengeneza kinara hicho cha taa pamoja na vifaa vyake vyote kutumia talanta\f + \fr 37:24 \ft Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.\f* moja ya dhahabu safi. \s1 Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba \r (Kutoka 30:1-5) \p \v 25 Akatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo. \v 26 Akafunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia zile pembe zake kwa dhahabu safi, na akayafanyizia ukingo wa dhahabu kuizunguka. \v 27 Akatengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, zikiwa mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko iliyotumika kuyabebea madhabahu. \v 28 Akatengeneza mipiko kwa miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu. \p \v 29 Pia akatengeneza mafuta matakatifu ya upako, na uvumba safi wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. \c 38 \s1 Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa \r (Kutoka 27:1-8) \p \v 1 Akatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu;\f + \fr 38:1 \ft Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35.\f* nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wa dhiraa tano\f + \fr 38:1 \ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\f* \v 2 Akatengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu zikawa zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. \v 3 Akatengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama na vyombo vya kuchukulia moto. \v 4 Akatengeneza wavu wa shaba chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. \v 5 Akasubu pete za shaba za kushikilia ile mipiko kwa ajili ya zile pembe nne za huo wavu wa shaba. \v 6 Akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuifunika kwa shaba. \v 7 Akaiingiza ile mipiko kwenye zile pete, ili iwe pande mbili za madhabahu kwa ajili ya kuibeba. Akaitengeneza madhabahu yenye uvungu ndani yake akitumia mbao. \s1 Sinia La Kunawia \r (Kutoka 30:18) \p \v 8 Akatengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kutoka kwa vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake waliohudumu pale ingilio la Hema la Kukutania. \s1 Ua Wa Hema La Kukutania \r (Kutoka 27:9-19) \p \v 9 Kisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja,\f + \fr 38:9 \ft Dhiraa 100 ni sawa na mita 45.\f* na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, \v 10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \v 11 Upande wa kaskazini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \p \v 12 Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini\f + \fr 38:12 \ft Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5.\f* na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. \v 13 Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, pia ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini. \v 14 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano\f + \fr 38:14 \ft Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75.\f* yalikuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \v 15 Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yalikuwa upande mwingine wa ingilio la ua, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. \v 16 Mapazia yote yaliyozunguka ua yalikuwa ya kitani iliyosokotwa vizuri. \v 17 Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha. \p \v 18 Pazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano, \v 19 likiwa na nguzo nne na vitako vinne vya shaba. Kulabu zake na tepe zake zilikuwa za fedha, na ncha zake zilikuwa zimefunikwa kwa fedha. \v 20 Vigingi vyote vya maskani na vya ua ulioizunguka vilikuwa vya shaba. \s1 Vifaa Vilivyotumika \p \v 21 Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani, maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Mose, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni. \v 22 (Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, alifanya kila kitu \nd Bwana\nd* alichomwamuru Mose, \v 23 akiwa pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, fundi stadi wa kutia nakshi, kubuni michoro, mtarizi kwa rangi ya buluu, ya zambarau, nyekundu na kitani safi.) \v 24 Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730,\f + \fr 38:24 \ft Talanta 29 na shekeli 730 ni sawa na tani moja.\f* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. \p \v 25 Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775,\f + \fr 38:25 \ft Talanta 100 na shekeli 1,775 za fedha ni sawa na tani 3.4.\f* kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. \v 26 Kila mtu alitoa beka moja, ambayo ni sawa na nusu shekeli ya fedha, kwa kazi ya mahali patakatifu, kutoka kwa kila mtu aliyekuwa amehesabiwa mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi, ambao jumla yao walikuwa wanaume 603,550. \v 27 Talanta hizo 100 za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na pazia: vitako mia moja kwa talanta mia, yaani, talanta moja kwa kila kitako. \v 28 Akatumia zile shekeli hizo 1,775 kutengeneza kulabu za nguzo, kufunika ncha za nguzo na kutengeneza vitanzi vyake. \p \v 29 Shaba iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa ilikuwa na uzito wa talanta 70 na shekeli 2,400.\f + \fr 38:29 \ft Talanta 70 na shekeli 2,400 ni sawa na tani 2.4.\f* \v 30 Akaitumia hiyo shaba kutengeneza vitako vya ingilio la Hema la Kukutania, madhabahu ya shaba pamoja na ule wavu wake na vyombo vyake vyote, \v 31 vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya Maskani pamoja na ule ua uliozunguka. \c 39 \s1 Mavazi Ya Kikuhani \r (Kutoka 28:1-14) \p \v 1 Kutokana na nyuzi za rangi ya buluu, ya zambarau na nyekundu akatengeneza mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Pia akamshonea Aroni mavazi matakatifu, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \s1 Kisibau \p \v 2 Akatengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kitani iliyosokotwa vizuri. \v 3 Akafua vipande vyembamba vya dhahabu kwa nyundo na kutengeneza nyuzi nyembamba ili kuzifuma pamoja na hizo nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi, kazi ya fundi stadi. \v 4 Akatengeneza vipande vya mabegani vya kisibau, vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kukifungia kisibau. \v 5 Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho: ulikuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao ulitengenezwa kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \p \v 6 Akatengeneza vito vya shohamu vilivyowekwa katika vijalizo vya dhahabu, navyo vilichorwa na majina ya wana wa Israeli kama vile muhuri huchorwa. \v 7 Kisha akavifungia kwenye vipande vya mabega ya kisibau kuwa vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \s1 Kifuko Cha Kifuani \r (Kutoka 28:15-30) \p \v 8 Akafanyiza kifuko cha kifuani, kazi ya fundi stadi. Akakitengeneza kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. \v 9 Kifuko hicho kilikuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja\f + \fr 39:9 \ft Shibiri moja ni sawa na sentimita 22.\f* na upana wa shibiri moja, nacho kilikunjwa mara mbili. \v 10 Kifuko hicho kilipambwa kwa safu nne za vito vya thamani. Safu ya kwanza ilikuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; \v 11 safu ya pili ilikuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; \v 12 safu ya tatu ilikuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; \v 13 katika safu ya nne ilikuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Vito hivyo vilitiwa kwenye vijalizo vya dhahabu. \v 14 Palikuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kikiwa na jina mojawapo la wana wa Israeli; kila kimoja kilichorwa kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili. \p \v 15 Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani akakitengenezea mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. \v 16 Akatengeneza vijalizo viwili vya dhahabu na pete mbili za dhahabu, na kuzifungia pete hizo kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. \v 17 Akafunga hiyo mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, \v 18 nazo zile ncha nyingine za mkufu akazifunga kwenye vile vijalizo viwili, na kuzishikamanisha na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele. \v 19 Akatengeneza pete mbili za dhahabu na kuzishikamanisha kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau. \v 20 Kisha akatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu na kuzishikamanisha sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau. \v 21 Akafunga pete za hicho kifuko cha kifuani kwenye pete za kisibau kwa kamba ya buluu, wakiziunganisha na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \s1 Mavazi Mengine Ya Kikuhani \r (Kutoka 28:31-43) \p \v 22 Akashona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, kazi ya mfumaji, \v 23 na lilikuwa na nafasi ya shingo katikati ya joho lile iliyofanana na ukosi, na utepe ulioshonwa kuizunguka nafasi hiyo ili isichanike. \v 24 Akatengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na ya kitani iliyosokotwa vizuri kuzunguka pindo la hilo joho. \v 25 Kisha akatengeneza vikengele vya dhahabu safi na kuvishikamanisha kuzunguka pindo hilo kati ya hayo makomamanga. \v 26 Hivyo vikengele na makomamanga vilipishana kuzunguka upindo wa joho ili livaliwe kwa kuhudumu, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \p \v 27 Pia akamtengenezea Aroni na wanawe makoti ya kitani safi, kazi ya mfumaji, \v 28 na kilemba cha kitani safi, tepe za kichwani za kitani, na nguo za ndani za kitani iliyosokotwa vizuri. \v 29 Mshipi ulikuwa wa kitani iliyosokotwa vizuri ya rangi ya buluu, na zambarau, na nyekundu, kazi ya mtarizi, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \p \v 30 Kisha akatengeneza lile bamba, taji takatifu, kwa dhahabu safi na kuchora juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: \sc Mtakatifu kwa Bwana\sc*. \v 31 Kisha wakalifunga kwa kamba ya rangi ya buluu ili kulishikamanisha na kile kilemba kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \s1 Mose Akagua Maskani Ya Mungu \r (Kutoka 35:10-19) \p \v 32 Kwa hiyo kazi yote ya maskani, Hema la Kukutania ikakamilika. Waisraeli wakafanya kila kitu sawasawa kama vile \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \v 33 Ndipo wakaleta maskani kwa Mose: hema pamoja na vifaa vyake vyote, vibanio vyake, mihimili yake, mataruma yake, nguzo na vitako vyake; \v 34 kifuniko cha ngozi za kondoo dume kilichotiwa rangi nyekundu, kifuniko cha ngozi za pomboo,\f + \fr 39:34 \fq Pomboo \ft hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. \f* pazia la kufunikia; \v 35 Sanduku la Ushuhuda pamoja na mipiko yake na kiti cha rehema, \v 36 meza pamoja na vyombo vyake vyote na mikate ya Wonyesho; \v 37 kinara cha taa cha dhahabu safi, safu zake za taa pamoja na vifaa vyake vyote pamoja na mafuta kwa ajili ya taa; \v 38 madhabahu ya dhahabu, mafuta ya upako, uvumba wenye harufu nzuri na pazia la ingilio la hema; \v 39 madhabahu ya shaba, pamoja na wavu wa shaba, nguzo zake na vyombo vyake vyote, sinia, na tako lake; \v 40 mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia kwa ajili ya ingilio la kwenye ua; kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani, Hema la Kukutania; \v 41 na mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani. \p \v 42 Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa amemwagiza Mose. \v 43 Mose akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa kama vile \nd Bwana\nd* alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Mose akawabariki. \c 40 \s1 Kuweka Wakfu Maskani Ya Mungu \p \v 1 Kisha \nd Bwana\nd* akamwambia Mose: \v 2 “Simika Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. \v 3 Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake. \v 4 Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake. \v 5 Weka madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba mbele ya Sanduku la Ushuhuda kisha uweke pazia kwenye lango la Maskani ya Mungu. \p \v 6 “Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania; \v 7 weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake. \v 8 Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua. \p \v 9 “Chukua mafuta ya upako, ipake Maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani mwake, nayo itakuwa takatifu. \v 10 Kisha yapake mafuta hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka pamoja na vifaa vyake vyote; weka wakfu madhabahu nayo yatakuwa takatifu sana. \v 11 Paka sinia mafuta pamoja na kishikilio chake na uviweke wakfu. \p \v 12 “Mlete Aroni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. \v 13 Kisha mvike Aroni yale mavazi matakatifu, umtie mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia katikati ya ukuhani. \v 14 Walete wanawe na uwavike makoti. \v 15 Kisha watie mafuta kama ulivyomtia baba yao, ili nao pia wanitumikie katika kazi ya ukuhani. Kutiwa mafuta kwao kutakuwa kwa ajili ya ukuhani utakaoendelea kwa vizazi vyote vijavyo.” \v 16 Mose akafanya kila kitu sawa kama vile \nd Bwana\nd* alivyomwagiza. \p \v 17 Kwa hiyo Maskani ya Mungu ilisimikwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, katika mwaka wa pili. \v 18 Mose alipoweka wakfu Maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo. \v 19 Kisha akalitandaza hema juu ya Maskani ya Mungu na kuifunika hema, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza. \p \v 20 Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake. \v 21 Kisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza. \p \v 22 Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia \v 23 na kupanga mikate juu yake mbele za \nd Bwana\nd*, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza. \p \v 24 Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu \v 25 na kuziweka taa mbele za \nd Bwana\nd*, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza. \p \v 26 Mose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia \v 27 na kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza. \v 28 Kisha akaweka pazia kwenye ingilio la Maskani ya Mungu. \p \v 29 Mose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza. \p \v 30 Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia, \v 31 Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. \v 32 Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama \nd Bwana\nd* alivyomwagiza Mose. \p \v 33 Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi. \s1 Utukufu Wa \nd Bwana\nd* \r (Hesabu 9:15-23) \p \v 34 Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa \nd Bwana\nd* ukaijaza Maskani ya Mungu. \v 35 Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa \nd Bwana\nd* ukaijaza Maskani ya Mungu. \p \v 36 Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya Maskani ya Mungu, wangeondoka; \v 37 lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, mpaka siku lilipoinuka. \v 38 Kwa hiyo wingu la \nd Bwana\nd* lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.