\id 1CH - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version \rem Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc. \h 1 Mambo Ya Nyakati \toc1 1 Mambo Ya Nyakati \toc2 1 Nyakati \toc3 1Nya \mt1 1 Mambo Ya Nyakati \c 1 \s1 Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Abrahamu \r (Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26) \s2 Adamu Hadi Wana Wa Noa \p \v 1 Adamu, Sethi, Enoshi, \v 2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi, \v 3 Enoki, Methusela, Lameki, Noa. \b \li1 \v 4 Wana wa Noa walikuwa: \li2 Shemu, Hamu na Yafethi. \s2 Wana Wa Yafethi \li1 \v 5 Wana wa Yafethi walikuwa: \li2 Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. \li1 \v 6 Wana wa Gomeri walikuwa: \li2 Ashkenazi, Rifathi na Togarma. \li1 \v 7 Wana wa Yavani walikuwa: \li2 Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. \s2 Wana Wa Hamu \li1 \v 8 Wana wa Hamu walikuwa: \li2 Kushi, Misraimu,\f + \fr 1:8 \ft Yaani Misri.\f* Putu na Kanaani. \li1 \v 9 Wana wa Kushi walikuwa: \li2 Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. \li1 Wana wa Raama walikuwa: \li2 Sheba na Dedani. \li1 \v 10 Kushi akamzaa \li2 Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi. \li1 \v 11 Misraimu akawazaa: \li2 Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, \v 12 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori. \li1 \v 13 Wana wa Kanaani walikuwa: \li2 Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, \v 14 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, \v 15 Wahivi, Waariki, Wasini, \v 16 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. \s2 Wana Wa Shemu \li1 \v 17 Wana wa Shemu walikuwa: \li2 Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. \li1 Wana wa Aramu walikuwa: \li2 Usi, Huli, Getheri na Mesheki. \li1 \v 18 Arfaksadi akamzaa Shela, \li2 Shela akamzaa Eberi. \li1 \v 19 Eberi alipata wana wawili: \li2 Mmoja wao aliitwa Pelegi,\f + \fr 1:19 \ft Pelegi maana yake Mgawanyiko.\f* kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. \li1 \v 20 Wana wa Yoktani walikuwa: \li2 Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, \v 21 Hadoramu, Uzali, Dikla, \v 22 Obali, Abimaeli, Sheba, \v 23 Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani. \b \li2 \v 24 Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela, \li2 \v 25 Eberi, Pelegi, Reu, \li2 \v 26 Serugi, Nahori, Tera, \li2 \v 27 Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu). \s1 Jamaa Ya Abrahamu \li1 \v 28 Abrahamu alikuwa na wana wawili: \li2 Isaki na Ishmaeli. \s2 Wazao Wa Hagari \r (Mwanzo 25:12-16) \li1 \v 29 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari: \li2 Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu, \v 30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, \v 31 Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. \s2 Wazao Wa Ketura \li1 \v 32 Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa: \li2 Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. \li1 Wana wa Yokshani walikuwa: \li2 Sheba na Dedani. \li1 \v 33 Wana wa Midiani walikuwa: \li2 Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. \li1 Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura. \s2 Wazao Wa Sara \li1 \v 34 Abrahamu alikuwa baba wa Isaki. \li1 Wana wa Isaki walikuwa: \li2 Esau na Israeli. \s1 Wana Wa Esau \r (Mwanzo 36:1-19) \li1 \v 35 Wana wa Esau walikuwa: \li2 Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora. \li1 \v 36 Wana wa Elifazi walikuwa: \li2 Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi; \li2 Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki. \li1 \v 37 Wana wa Reueli walikuwa: \li2 Nahathi, Zera, Shama na Miza. \s1 Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu \r (Mwanzo 36:20-30) \li1 \v 38 Wana wa Seiri walikuwa: \li2 Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani. \li1 \v 39 Wana wa Lotani walikuwa wawili: \li2 Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna. \li1 \v 40 Wana wa Shobali walikuwa: \li2 Alvani,\f + \fr 1:40 \ft Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian.\f* Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. \li1 Wana wa Sibeoni walikuwa: \li2 Aiya na Ana. \li1 \v 41 Mwana wa Ana alikuwa: \li2 Dishoni. \li1 Nao wana wa Dishoni walikuwa: \li2 Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani. \li1 \v 42 Wana wa Eseri walikuwa: \li2 Bilhani, Zaavani na Akani. \li1 Wana wa Dishani walikuwa: \li2 Usi na Arani. \s2 Watawala Wa Edomu \r (Mwanzo 36:31-43) \li1 \v 43 Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: \li2 Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba. \li2 \v 44 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. \li2 \v 45 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. \li2 \v 46 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. \li2 \v 47 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. \li2 \v 48 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake. \li2 \v 49 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. \li2 \v 50 Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. \v 51 Naye Hadadi pia akafa. \b \li1 Wakuu wa Edomu walikuwa: \li2 Timna, Alva, Yethethi, \v 52 Oholibama, Ela, Pinoni, \v 53 Kenazi, Temani, Mibsari, \v 54 Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu. \c 2 \s1 Wana Wa Israeli \li1 \v 1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli: \li2 Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni, \v 2 Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri. \s1 Yuda \s2 Hadi Wana Wa Hesroni \li1 \v 3 Wana wa Yuda walikuwa: \li2 Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa \nd Bwana\nd*, kwa hiyo \nd Bwana\nd* alimuua. \v 4 Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano. \b \li1 \v 5 Wana wa Peresi walikuwa: \li2 Hesroni na Hamuli. \li1 \v 6 Wana wa Zera walikuwa: \li2 Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano. \li1 \v 7 Mwana wa Karmi alikuwa: \li2 Akari,\f + \fr 2:7 \ft Akari maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (\+xt Yos 6:1-26; 22:20\+xt*).\f* ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu. \li1 \v 8 Mwana wa Ethani alikuwa: \li2 Azariya. \li1 \v 9 Wana wa Hesroni walikuwa: \li2 Yerameeli, Ramu na Kalebu. \s2 Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni \li1 \v 10 Ramu alimzaa \li2 Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda. \v 11 Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, \v 12 Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese. \li1 \v 13 Yese akawazaa \li2 Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,\f + \fr 2:13 \ft Au: Shima, maana yake Sifa njema (pia \+xt 1Sam 16:9; 17:13\+xt*).\f* \v 14 wa nne Nethaneli, wa tano Radai, \v 15 wa sita Osemu, na wa saba Daudi. \v 16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli. \v 17 Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli. \s2 Kalebu Mwana Wa Hesroni \li1 \v 18 Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni. \v 19 Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri. \v 20 Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli. \li1 \v 21 Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu. \v 22 Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi. \v 23 (Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi. \b \li1 \v 24 Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa. \s2 Yerameeli Mwana Wa Hesroni \li1 \v 25 Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa: \li2 Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. \v 26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu. \li1 \v 27 Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa: \li2 Maasi, Yamini na Ekeri. \li1 \v 28 Wana wa Onamu walikuwa: \li2 Shamai na Yada. \li1 Wana wa Shamai walikuwa: \li2 Nadabu na Abishuri. \li1 \v 29 Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi. \li1 \v 30 Wana wa Nadabu walikuwa \li2 Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto. \li1 \v 31 Apaimu akamzaa: \li2 Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani. \li2 Sheshani akamzaa Alai. \li1 \v 32 Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa: \li2 Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto. \li1 \v 33 Wana wa Yonathani walikuwa: \li2 Pelethi na Zaza. \li1 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli. \li1 \v 34 Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu. \li2 Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha. \v 35 Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai. \li1 \v 36 Atai akamzaa Nathani, \li2 Nathani akamzaa Zabadi, \li2 \v 37 Zabadi akamzaa Eflali, \li2 Eflali akamzaa Obedi, \li2 \v 38 Obedi akamzaa Yehu, \li2 Yehu akamzaa Azaria, \li2 \v 39 Azaria akamzaa Helesi, \li2 Helesi akamzaa Eleasa, \li2 \v 40 Eleasa akamzaa Sismai, \li2 Sismai akamzaa Shalumu, \li2 \v 41 Shalumu akamzaa Yekamia, \li2 naye Yekamia akamzaa Elishama. \s2 Koo Za Kalebu \li1 \v 42 Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa: \li2 Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni. \li1 \v 43 Hebroni alikuwa na wana wanne: \li2 Kora, Tapua, Rekemu na Shema. \v 44 Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai. \v 45 Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri. \li1 \v 46 Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi. \li1 \v 47 Wana wa Yadai walikuwa: \li2 Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu. \li1 \v 48 Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana. \v 49 Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa. \v 50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu. \b \li1 Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa: \li2 Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu, \v 51 Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi. \li1 \v 52 Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa: \li2 Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi, \v 53 pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli. \li1 \v 54 Wazao wa Salma walikuwa: \li2 Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori, \v 55 pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu. \c 3 \s2 Wana Wa Daudi \li1 \v 1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: \li2 Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; \li2 wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli; \li2 \v 2 wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri; \li2 wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi; \li2 \v 3 wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali; \li2 wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla. \li2 \v 4 Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita. \m Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu, \v 5 nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: \li2 mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua,\f + \fr 3:5 \ft Sawa na Shimea; maana yake ni Mashuhuri, Maarufu.\f* Shobabu, Nathani na Solomoni. \v 6 Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti, \v 7 Noga, Nefegi, Yafia, \v 8 Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa. \v 9 Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao. \s2 Wafalme Wa Yuda \li1 \v 10 Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu, \li2 mwanawe huyo alikuwa Abiya, \li2 mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati, \li2 mwanawe huyo alikuwa Asa, \li2 \v 11 mwanawe huyo alikuwa Yehoramu, \li2 mwanawe huyo alikuwa Ahazia, \li2 mwanawe huyo alikuwa Yoashi, \li2 \v 12 mwanawe huyo alikuwa Amazia, \li2 mwanawe huyo alikuwa Azaria, \li2 mwanawe huyo alikuwa Yothamu, \li2 \v 13 mwanawe huyo alikuwa Ahazi, \li2 mwanawe huyo alikuwa Hezekia, \li2 mwanawe huyo alikuwa Manase, \li2 \v 14 mwanawe huyo alikuwa Amoni \li2 na mwanawe huyo alikuwa Yosia. \li1 \v 15 Wana wa Yosia walikuwa: \li2 Yohanani mzaliwa wake wa kwanza, \li2 Yehoyakimu mwanawe wa pili, \li2 wa tatu Sedekia, \li2 wa nne Shalumu. \li1 \v 16 Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni: \li2 Yekonia mwanawe, \li2 na Sedekia. \s2 Ukoo Wa Kifalme Baada Ya Uhamisho \li1 \v 17 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka: \li2 Shealtieli mwanawe, \v 18 Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia. \li1 \v 19 Wana wa Pedaya walikuwa: \li2 Zerubabeli na Shimei. \li1 Wana wa Zerubabeli walikuwa: \li2 Meshulamu na Hanania. \li2 Shelomithi alikuwa dada yao. \li2 \v 20 Pia walikuwepo wengine watano: \li2 Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi. \li1 \v 21 Wazao wa Hanania walikuwa: \li2 Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania. \li1 \v 22 Wazao wa Shekania: \li2 Shemaya na wanawe: \li2 Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita. \li1 \v 23 Wana wa Nearia walikuwa: \li2 Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu. \li1 \v 24 Wana wa Elioenai walikuwa: \li2 Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba. \c 4 \s2 Koo Nyingine Za Yuda \li1 \v 1 Wana wa Yuda walikuwa: \li2 Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali. \li1 \v 2 Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Wasorathi. \li1 \v 3 Hawa ndio waliokuwa wana wa Etamu: \li2 Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi. \v 4 Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha. \li1 Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu. \li1 \v 5 Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. \li1 \v 6 Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari. \li1 \v 7 Wana wa Hela walikuwa: \li2 Serethi, Sohari, Ethnani, \v 8 na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu. \b \p \v 9 Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.” \v 10 Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba. \b \li1 \v 11 Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni. \v 12 Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Iri-Nahashi. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Reka. \b \li1 \v 13 Wana wa Kenazi walikuwa: \li2 Othnieli na Seraya. \li1 Wana wa Othnieli walikuwa: \li2 Hathathi na Meonathai. \v 14 Meonathai akamzaa Ofra. \li1 Seraya akamzaa Yoabu, \li2 baba wa Ge-Harashimu.\f + \fr 4:14 \ft Maana yake Bonde la Mafundi.\f* Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi. \li1 \v 15 Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu: \li2 Iru, Ela na Naamu. \li1 Naye mwana wa Ela alikuwa: \li2 Kenazi. \li1 \v 16 Wana wa Yahaleleli walikuwa: \li2 Zifu, Zifa, Tiria na Asareli. \li1 \v 17 Wana wa Ezra walikuwa: \li2 Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Mmojawapo wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa. \v 18 Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa. \li1 \v 19 Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa: \li2 baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi. \li1 \v 20 Wana wa Shimoni walikuwa: \li2 Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni. \li1 Wazao wa Ishi walikuwa: \li2 Zohethi na Ben-Zohethi. \li1 \v 21 Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa: \li2 Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi waliokuwa wakiishi huko Beth-Ashbea, \v 22 Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yashubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.) \v 23 Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme. \s1 Simeoni \li1 \v 24 Wazao wa Simeoni walikuwa: \li2 Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli. \li2 \v 25 Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma. \li1 \v 26 Wazao wa Mishma walikuwa: \li2 Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei. \p \v 27 Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda. \v 28 Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hasar-Shuali, \v 29 Bilha, Esemu, Toladi, \v 30 Bethueli, Horma, Siklagi, \v 31 Beth-Markabothi, Hasar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi. \v 32 Vijiji vilivyoizunguka vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani; jumla miji mitano: \v 33 pamoja na vijiji vyote kuizunguka hii miji hadi huko Baali. Haya yalikuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao. \b \mi \v 34 Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia, \v 35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli. \v 36 Pia Elioenai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya, \v 37 Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya. \b \p \v 38 Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao. Jamaa zao ziliongezeka sana, \v 39 wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao. \v 40 Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani. \p \v 41 Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao. \v 42 Watu wa kabila la wa Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri. \v 43 Wakawaua Waamaleki waliobaki, waliokuwa wamenusurika, nao wanaishi huko hadi leo. \c 5 \s1 Wana Wa Reubeni \p \v 1 Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa. \v 2 Na ingawa Yuda alikuwa na nguvu zaidi ya ndugu zake wote, na mtawala alitoka kwake, haki za mzaliwa wa kwanza zilikuwa za Yosefu.) \v 3 Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli walikuwa: \li1 Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. \li1 \v 4 Wazao wa Yoeli walikuwa: \li2 Shemaya mwanawe, Gogu mwanawe; \li2 Shimei mwanawe, \v 5 Mika mwanawe, \li2 Reaya mwanawe, Baali mwanawe, \li2 \v 6 na Beera mwanawe, ambaye Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alimchukua kwenda uhamishoni. Beera alikuwa kiongozi wa Wareubeni. \li1 \v 7 Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa kufuata koo zao kama ifuatavyo: \li2 Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria, \v 8 Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni. \v 9 Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi. \pi2 \v 10 Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi. \s1 Wana Wa Gadi \li1 \v 11 Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka. \li2 \v 12 Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani. \li1 \v 13 Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba: \li2 Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi. \li2 \v 14 Hawa walikuwa ndio wana wa Abihaili mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yahdo, mwana wa Buzi. \li2 \v 15 Ahi mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa ndiye kiongozi wa jamaa yao. \li1 \v 16 Wagadi waliishi Gileadi, huko Bashani pamoja na vijiji vilivyoizunguka, pia katika nchi yote ya malisho ya Sharoni kote walikoenea. \p \v 17 Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli. \b \p \v 18 Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo. \v 19 Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu. \v 20 Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea. \v 21 Walitwaa mifugo ya Wahagari: ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000. Pia wakateka watu 100,000, \v 22 na wengine wengi waliuawa kwa sababu vita vilikuwa ni vya Mungu. Nao waliendelea kuikalia nchi hiyo mpaka wakati wa uhamisho. \s1 Nusu Ya Kabila La Manase \p \v 23 Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni. \p \v 24 Hawa ndio waliokuwa viongozi wa jamaa za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yahdieli. Walikuwa askari shujaa watu maarufu, viongozi wa jamaa zao. \v 25 Lakini hawakuwa waaminifu kwa Mungu wa baba zao, nao wakafanya ukahaba kwa miungu ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameyaangamiza mbele yao. \v 26 Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo. \c 6 \s1 Wana Wa Lawi \li1 \v 1 Wana wa Lawi walikuwa: \li2 Gershoni, Kohathi na Merari. \li1 \v 2 Wana wa Kohathi walikuwa: \li2 Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. \li1 \v 3 Amramu alikuwa na wana: \li2 Aroni, Mose, na Miriamu. \li1 Aroni alikuwa na wana: \li2 Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. \li2 \v 4 Eleazari akamzaa Finehasi, \li2 Finehasi akamzaa Abishua, \li2 \v 5 Abishua akamzaa Buki, \li2 Buki akamzaa Uzi, \li2 \v 6 Uzi akamzaa Zerahia, \li2 Zerahia akamzaa Merayothi, \li2 \v 7 Merayothi akamzaa Amaria, \li2 Amaria akamzaa Ahitubu, \li2 \v 8 Ahitubu akamzaa Sadoki, \li2 Sadoki akamzaa Ahimaasi, \li2 \v 9 Ahimaasi akamzaa Azaria, \li2 Azaria akamzaa Yohanani, \li2 \v 10 Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu), \li2 \v 11 Azaria akamzaa Amaria, \li2 Amaria akamzaa Ahitubu, \li2 \v 12 Ahitubu akamzaa Sadoki, \li2 Sadoki akamzaa Shalumu, \li2 \v 13 Shalumu akamzaa Hilkia, \li2 Hilkia akamzaa Azaria, \li2 \v 14 Azaria akamzaa Seraya, \li2 Seraya akamzaa Yehosadaki. \li4 \v 15 Yehosadaki alihamishwa wakati \nd Bwana\nd* aliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza. \b \li1 \v 16 Wana wa Lawi walikuwa: \li2 Gershoni, Kohathi na Merari. \li1 \v 17 Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni: \li2 Libni na Shimei. \li1 \v 18 Wana wa Kohathi walikuwa: \li2 Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. \li1 \v 19 Wana wa Merari walikuwa: \li2 Mahli na Mushi. \b \li1 Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao: \li1 \v 20 Wazao wa Gershoni: \li2 Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, \li2 Yahathi akamzaa Zima, \v 21 Zima akamzaa Yoa, \li2 Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, \li2 Zera akamzaa Yeatherai. \li1 \v 22 Wazao wa Kohathi: \li2 Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, \li2 Kora akamzaa Asiri, \v 23 Asiri akamzaa Elikana, \li2 Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri, \li2 \v 24 Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, \li2 Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli. \li1 \v 25 Wazao wa Elikana walikuwa: \li2 Amasai na Ahimothi, \li2 \v 26 Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai, \li2 Sofai akamzaa Nahathi, \v 27 Nahathi akamzaa Eliabu, \li2 Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana, \li2 Elikana akamzaa Samweli. \li1 \v 28 Wana wa Samweli walikuwa: \li2 Yoeli mzaliwa wake wa kwanza, \li2 na Abiya mwanawe wa pili. \li1 \v 29 Wafuatao ndio wazao wa Merari: \li2 Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni, \li2 Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza, \li2 \v 30 Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, \li2 Hagia akamzaa Asaya. \s2 Waimbaji Wa Hekalu \p \v 31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya \nd Bwana\nd*, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. \v 32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la \nd Bwana\nd* huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa. \p \v 33 Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao: \li1 Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa: \li2 Hemani, mpiga kinanda, \li2 alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli, \li2 \v 34 mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu, \li2 mwana wa Elieli, mwana wa Toa, \li2 \v 35 mwana wa Sufu, mwana wa Elikana, \li2 mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai, \li2 \v 36 mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli, \li2 mwana wa Azaria, mwana wa Sefania, \li2 \v 37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, \li2 mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, \li2 \v 38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, \li2 mwana wa Lawi, mwana wa Israeli; \li1 \v 39 na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume: \li2 Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea, \li2 \v 40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, \li2 mwana wa Malkiya, \v 41 mwana wa Ethni, \li2 mwana wa Zera, mwana wa Adaya, \li2 \v 42 mwana wa Ethani, mwana wa Zima, \li2 mwana wa Shimei, \v 43 mwana wa Yahathi, \li2 mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi. \li1 \v 44 Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto: \li2 Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, \li2 mwana wa Maluki, \v 45 mwana wa Hashabia, \li2 mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia, \li2 \v 46 mwana wa Amsi, mwana wa Bani, \li2 mwana wa Shemeri, \v 47 mwana wa Mahli, \li2 mwana wa Mushi, mwana wa Merari, \li2 mwana wa Lawi. \b \p \v 48 Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. \v 49 Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu. \b \li1 \v 50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni: \li2 Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, \li2 Finehasi akamzaa Abishua, \v 51 Abishua akamzaa Buki, \li2 Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia, \li2 \v 52 Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, \li2 Amaria akamzaa Ahitubu, \v 53 Ahitubu akamzaa Sadoki, \li2 Sadoki akamzaa Ahimaasi. \b \p \v 54 Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): \pi1 \v 55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka. \v 56 Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune. \pi1 \v 57 Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, \v 58 Hileni, Debiri, \v 59 Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. \v 60 Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho. \pi1 Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi. \p \v 61 Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase. \p \v 62 Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani. \p \v 63 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni. \p \v 64 Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho. \v 65 Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu. \p \v 66 Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu. \pi1 \v 67 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, \v 68 Yokmeamu, Beth-Horoni, \v 69 Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho. \pi1 \v 70 Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho. \b \li1 \v 71 Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: \li1 Katika nusu ya kabila la Manase: \li2 walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi. \li1 \v 72 Kutoka kabila la Isakari \li2 walipokea Kedeshi, Daberathi, \v 73 Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho. \li1 \v 74 Kutoka kabila la Asheri \li2 walipokea Mashali, Abdoni, \v 75 Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho. \li1 \v 76 Kutoka kabila la Naftali \li2 walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho. \b \li1 \v 77 Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo: \li2 kutoka kabila la Zabuloni \li2 walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho. \li1 \v 78 Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko \li2 walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa, \v 79 Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho. \li1 \v 80 Na kutoka kabila la Gadi \li2 walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu, \v 81 Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho. \c 7 \s1 Wana Wa Isakari \li1 \v 1 Wana wa Isakari walikuwa: \li2 Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne. \li1 \v 2 Wana wa Tola walikuwa: \li2 Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600. \li1 \v 3 Mwana wa Uzi alikuwa: \li2 Izrahia. \li1 Wana wa Izrahia walikuwa: \li2 Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. \v 4 Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi. \li1 \v 5 Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000. \s1 Wana Wa Benyamini \li1 \v 6 Wana watatu wa Benyamini walikuwa: \li2 Bela, Bekeri na Yediaeli. \li1 \v 7 Wana wa Bela walikuwa: \li2 Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034. \li1 \v 8 Wana wa Bekeri walikuwa: \li2 Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. \v 9 Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200. \li1 \v 10 Mwana wa Yediaeli alikuwa: \li2 Bilhani. \li1 Wana wa Bilhani walikuwa: \li2 Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. \v 11 Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani. \li1 \v 12 Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri. \s1 Wana Wa Naftali \li1 \v 13 Wana wa Naftali walikuwa: \li2 Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha. \s1 Wana Wa Manase \li1 \v 14 Wana wa Manase walikuwa: \pi2 Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. \v 15 Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. \pi2 Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu. \pi2 \v 16 Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu. \li1 \v 17 Mwana wa Ulamu alikuwa: \li2 Bedani. \li1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase. \v 18 Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla. \li1 \v 19 Wana wa Shemida walikuwa: \li2 Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu. \s1 Wana Wa Efraimu \li1 \v 20 Wana wa Efraimu walikuwa: \li2 Shuthela, ambaye alimzaa Beredi, \li2 Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada, \li2 Eleada akamzaa Tahathi, \v 21 Tahathi akamzaa Zabadi, \li2 na Zabadi akamzaa Shuthela. \pi2 Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. \v 22 Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. \v 23 Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. \v 24 Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera. \li1 \v 25 Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu, \li2 Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani, \li2 \v 26 Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, \li2 Amihudi akamzaa Elishama, \v 27 Elishama akamzaa Nuni, \li2 Nuni akamzaa Yoshua. \p \v 28 Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. \v 29 Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii. \s1 Wana Wa Asheri \li1 \v 30 Wana wa Asheri walikuwa: \li2 Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera. \li1 \v 31 Wana wa Beria walikuwa: \li2 Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi. \li1 \v 32 Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao. \li1 \v 33 Wana wa Yafleti walikuwa: \li2 Pasaki, Bimhali na Ashvathi. \li2 Hawa walikuwa wana wa Yafleti. \li1 \v 34 Wana wa Shemeri walikuwa: \li2 Ahi, Roga, Yehuba na Aramu. \li1 \v 35 Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa: \li2 Sofa, Imna, Sheleshi na Amali. \li1 \v 36 Wana wa Sofa walikuwa: \li2 Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, \v 37 Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani\f + \fr 7:37 \ft Kwa jina lingine Yetheri.\f* na Beera. \li1 \v 38 Wana wa Yetheri walikuwa: \li2 Yefune, Pispa na Ara. \li1 \v 39 Wana wa Ula walikuwa: \li2 Ara, Hanieli na Risia. \p \v 40 Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000. \c 8 \s1 Ukoo Wa Sauli Mbenyamini \li1 \v 1 Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza, \li2 Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu, \li2 \v 2 Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano. \li1 \v 3 Wana wa Bela walikuwa: \li2 Adari, Gera, Abihudi, \v 4 Abishua, Naamani, Ahoa, \v 5 Gera, Shefufani na Huramu. \li1 \v 6 Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi: \li2 \v 7 Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni. \li1 \v 8 Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara. \v 9 Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, \v 10 Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. \v 11 Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali. \li1 \v 12 Wana wa Elpaali walikuwa: \li2 Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka), \v 13 na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi. \li1 \v 14 Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, \v 15 Zebadia, Aradi, Ederi, \v 16 Mikaeli, Ishpa, na Yoha. \li1 \v 17 Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, \v 18 Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali. \li1 \v 19 Yakimu, Zikri, Zabdi, \v 20 Elienai, Silethai, Elieli, \v 21 Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei. \li1 \v 22 Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, \v 23 Abdoni, Zikri, Hanani, \v 24 Hanania, Elamu, Anthothiya, \v 25 Ifdeya na Penueli. \li1 \v 26 Shamsherai, Sheharia, Athalia, \v 27 Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu. \p \v 28 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu. \b \li1 \v 29 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. \li2 Mke wake aliitwa Maaka. \v 30 Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, \v 31 Gedori, Ahio, Zekeri, \v 32 na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu. \li1 \v 33 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali. \li1 \v 34 Yonathani akamzaa: \li2 Merib-Baali,\f + \fr 8:34 \ft Merib-Baali maana yake ni Baali na Ashindane naye (\+xt Amu 6:32\+xt*); ni jina lingine la mwana wa Yonathani, Mefiboshethi ambalo nalo maana yake ni Mtu wa Aibu (ona \+xt 2Sam 4:4\+xt*).\f* naye Merib-Baali akamzaa Mika. \li1 \v 35 Wana wa Mika walikuwa: \li2 Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi. \li2 \v 36 Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. \v 37 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli. \li1 \v 38 Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao: \li2 Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli. \li1 \v 39 Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa: \li2 Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. \v 40 Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150. \li1 Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini. \b \c 9 \p \v 1 Waisraeli wote waliorodheshwa katika koo zilizoandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa Israeli. \s1 Watu Katika Yerusalemu \p Watu wa Yuda walichukuliwa mateka kwenda Babeli kwa sababu ya kukosa uaminifu kwa Mungu. \v 2 Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na watumishi wa Hekalu.\f + \fr 9:2 \ft Yaani \fqa Wanethini.\f* \p \v 3 Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa: \s2 Jamaa Za Yuda \li1 \v 4 Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda. \li1 \v 5 Wazao wa Washiloni waliorudi ni: \li2 Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe. \li1 \v 6 Kwa wana wa Zera: \li2 Yeueli. \li2 Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690. \s2 Jamaa Za Benyamini \li1 \v 7 Kwa Benyamini walikuwa: \li2 Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua; \li2 \v 8 Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya. \li2 \v 9 Watu kutoka Benyamini kama walivyoorodheshwa katika koo zao jumla yao ni 956. Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao. \s2 Jamaa Za Makuhani \li1 \v 10 Wa jamaa za makuhani walikuwa: \li2 Yedaya, Yehoyaribu na Yakini; \li2 \v 11 Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa afisa kiongozi wa nyumba ya Mungu. \li2 \v 12 Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yahzera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri. \li2 \v 13 Makuhani waliokuwa viongozi wa jamaa zao walikuwa 1,760. Walikuwa watu wenye uwezo, waliowajibika kuhudumu katika nyumba ya Mungu. \s2 Jamaa Za Walawi \li1 \v 14 Jamaa za Walawi walikuwa: \li2 Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari. \v 15 Bakbakari, Hereshi, Galali na Matania mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu. \v 16 Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elikana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi. \s2 Jamaa Za Mabawabu \li1 \v 17 Mabawabu katika Hekalu la \nd Bwana\nd* waliorudi walikuwa: \li2 Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu. \v 18 Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi. \v 19 Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya \nd Bwana\nd*. \v 20 Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye \nd Bwana\nd* alikuwa pamoja naye: \li2 \v 21 Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania. \p \v 22 Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli. \v 23 Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya \nd Bwana\nd*, nyumba iliyoitwa Hema. \v 24 Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. \v 25 Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba. \v 26 Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu. \v 27 Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi. \p \v 28 Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. \v 29 Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. \v 30 Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo. \v 31 Mlawi aliyeitwa Matithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka. \v 32 Baadhi ya ndugu zao wa ukoo wa Kohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate ya Wonyesho kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani. \p \v 33 Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana. \p \v 34 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa za Walawi, wakuu kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu. \s1 Ukoo Wa Sauli \r (1 Nyakati 8:29-38) \li1 \v 35 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka, \v 36 mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, \v 37 Gedori, Ahio, Zekaria na Miklothi. \v 38 Miklothi akamzaa Shimeamu. Wao pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu. \li1 \v 39 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli. Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.\f + \fr 9:39 \ft Anajulikana pia kwa jina la Ish-Boshethi, maana yake Mtu wa Aibu (\+xt 2Sam 2:8\+xt*).\f* \li1 \v 40 Yonathani akamzaa Merib-Baali,\f + \fr 9:40 \ft Pia anajulikana kwa jina la Mefiboshethi.\f* \li2 naye Merib-Baali akamzaa Mika. \li1 \v 41 Wana wa Mika walikuwa: \li2 Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi. \li2 \v 42 Ahazi akamzaa Yara, Yara akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. \v 43 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli. \li1 \v 44 Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao: \li2 Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Aseli. \c 10 \s1 Sauli Ajiua \r (1 Samweli 31:1-13) \p \v 1 Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika mlima Gilboa. \v 2 Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. \v 3 Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi. \p \v 4 Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.” \p Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. \v 5 Mbeba silaha wake alipoona kwamba Sauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake akafa. \v 6 Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote. \p \v 7 Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo. \p \v 8 Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa. \v 9 Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao. \v 10 Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni. \p \v 11 Wakazi wote wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yote Wafilisti waliyomtendea Sauli, \v 12 mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba. \p \v 13 Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa \nd Bwana\nd*. Hakulishika neno la \nd Bwana\nd*, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, \v 14 hakumuuliza \nd Bwana\nd*. Kwa hiyo \nd Bwana\nd* alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese. \c 11 \s1 Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Israeli \r (2 Samweli 5:1-10) \p \v 1 Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako. \v 2 Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye \nd Bwana\nd* Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ” \p \v 3 Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za \nd Bwana\nd*, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na \nd Bwana\nd* alivyoahidi kupitia kwa Samweli. \s1 Daudi Ateka Yerusalemu \p \v 4 Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo \v 5 wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi. \p \v 6 Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu. \p \v 7 Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi. \v 8 Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu. \v 9 Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye. \s1 Mashujaa Wa Daudi \r (2 Samweli 23:8-39) \p \v 10 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama \nd Bwana\nd* alivyoahidi. \v 11 Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi: \p Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja. \p \v 12 Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. \v 13 Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti. \v 14 Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye \nd Bwana\nd* akawapa ushindi mkubwa. \p \v 15 Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. \v 16 Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. \v 17 Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!” \v 18 Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za \nd Bwana\nd*. \v 19 Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa. \p Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu. \p \v 20 Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. \v 21 Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao. \p \v 22 Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. \v 23 Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano.\f + \fr 11:23 \ft Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25.\f* Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao. \v 24 Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. \v 25 Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake. \b \li1 \v 26 Wale watu mashujaa walikuwa: \li2 Asaheli nduguye Yoabu, \li2 Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu, \li2 \v 27 Shamothi Mharori, \li2 Helesi Mpeloni, \li2 \v 28 Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa, \li2 Abiezeri kutoka Anathothi, \li2 \v 29 Sibekai Mhushathi, \li2 Ilai Mwahohi, \li2 \v 30 Maharai Mnetofathi, \li2 Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi, \li2 \v 31 Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini, \li2 Benaya Mpirathoni, \li2 \v 32 Hurai kutoka mabonde ya Gaashi, \li2 Abieli Mwaribathi, \li2 \v 33 Azmawethi Mbaharumi, \li2 Eliaba Mshaalboni, \li2 \v 34 wana wa Hashemu Mgiloni, \li2 Yonathani mwana wa Shagee Mharari, \li2 \v 35 Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, \li2 Elifale mwana wa Uru, \li2 \v 36 Heferi Mmekerathi, \li2 Ahiya Mpeloni, \li2 \v 37 Hezro Mkarmeli, \li2 Naarai mwana wa Ezbai, \li2 \v 38 Yoeli nduguye Nathani, \li2 Mibhari mwana wa Hagri, \li2 \v 39 Seleki Mwamoni, \li2 Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya, \li2 \v 40 Ira Mwithiri, \li2 Garebu Mwithiri, \li2 \v 41 Uria Mhiti, \li2 Zabadi mwana wa Alai, \li2 \v 42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini, \li2 \v 43 Hanani mwana wa Maaka, \li2 Yoshafati Mmithni, \li2 \v 44 Uzia Mwashterathi, \li2 Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri, \li2 \v 45 Yediaeli mwana wa Shimri, \li2 nduguye Yoha Mtizi, \li2 \v 46 Elieli Mmahawi, \li2 Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, \li2 Ithma Mmoabu, \li2 \v 47 Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai. \c 12 \s1 Mashujaa Waungana Na Daudi \p \v 1 Hawa ndio watu waliomjia Daudi huko Siklagi, wakati alikuwa amefukuzwa mbele ya Sauli mwana wa Kishi (walikuwa miongoni mwa mashujaa waliomsaidia Daudi vitani, \v 2 walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini): \mi \v 3 Mkuu wao alikuwa Ahiezeri, na wa pili Yoashi, wote wana wa Shemaa Mgibeathi; pia Yezieli na Peleti wana wa Azmawethi; Beraka, Yehu Mwanathothi, \v 4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa miongoni mwa wale Thelathini, ambaye alikuwa kiongozi wa wale Thelathini; Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi, Mgederathi, \v 5 Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi; \v 6 Elikana, Ishia, Azareli, Yoezeri na Yashobeamu, wana wa Kora; \v 7 Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori. \b \p \v 8 Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani. \li1 \v 9 Ezeri alikuwa mkuu wao, \li1 Obadia alikuwa wa pili katika uongozi, Eliabu wa tatu, \li1 \v 10 Mishmana wa nne, Yeremia wa tano, \li1 \v 11 Atai wa sita, Elieli wa saba, \li1 \v 12 Yohanani wa nane, Elzabadi wa tisa, \li1 \v 13 Yeremia wa kumi, na Makbanai wa kumi na moja. \p \v 14 Hawa Wagadi walikuwa majemadari. Aliyekuwa wa mwisho kuliko wote aliweza kuongoza askari 100, na aliyekuwa na uweza zaidi ya wote aliongoza 1,000. \v 15 Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi. \p \v 16 Wabenyamini wengine na baadhi ya watu kutoka Yuda pia walikuja kwa Daudi katika ngome yake. \v 17 Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mimi mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.” \p \v 18 Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema: \q1 “Sisi tu watu wako, ee Daudi! \q2 Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese! \q1 Ushindi, naam, ushindi uwe kwako, \q2 pia ushindi kwa wale walio upande wako, \q3 kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.” \p Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi. \p \v 19 Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”) \v 20 Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase. \v 21 Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake. \v 22 Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu. \s1 Wengine Waungana Na Daudi Huko Hebroni \p \v 23 Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama \nd Bwana\nd* alivyokuwa amesema: \li1 \v 24 watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita. \li1 \v 25 Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100. \li1 \v 26 Watu wa Lawi walikuwa 4,600, \v 27 pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Aroni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700, \v 28 na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake. \li1 \v 29 Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo. \li1 \v 30 Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao. \li1 \v 31 Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000. \li1 \v 32 Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao. \li1 \v 33 Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000. \li1 \v 34 Watu wa Naftali, maafisa 1,000, pamoja na watu 37,000 waliochukua ngao na mikuki. \li1 \v 35 Watu wa Dani 28,600 waliokuwa tayari kwa vita. \li1 \v 36 Watu wa Asheri, askari 40,000 wenye uzoefu mkubwa waliondaliwa kwa ajili ya vita. \li1 \v 37 Na pia watu kutoka mashariki ya Yordani, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakiwa na kila aina ya silaha, watu 120,000. \p \v 38 Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme. \v 39 Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao. \v 40 Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ngʼombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli. \c 13 \s1 Kurudishwa Kwa Sanduku La Mungu \r (2 Samweli 6:1-11) \p \v 1 Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia. \v 2 Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi ya \nd Bwana\nd* Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao, waje waungane na sisi. \v 3 Sisi na tulirudishe Sanduku la Mungu wetu kwetu kwa maana hatukujali wakati wa utawala wa Sauli.” \v 4 Kusanyiko lote likakubaliana kufanya hivyo, kwa sababu ilionekana vyema kwa watu wote. \p \v 5 Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu. \v 6 Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu \nd Bwana\nd*, yeye anayeketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake, kutoka huko. \p \v 7 Wakalisafirisha Sanduku la Mungu kwa gari jipya la kukokotwa na maksai kutoka nyumba ya Abinadabu, Uza na Ahio wakiliongoza gari hilo. \v 8 Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta. \p \v 9 Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Kidoni, Uza akaunyoosha mkono wake ili kulizuia Sanduku, kwa sababu maksai walijikwaa. \v 10 Hasira ya \nd Bwana\nd* ikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu. \p \v 11 Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya \nd Bwana\nd* ilifurika dhidi ya Uza, mahali pale pakaitwa Peres-Uza\f + \fr 13:11 \ft Maana yake ni Gadhabu dhidi ya Uza.\f* hadi leo. \p \v 12 Siku ile Daudi akamwogopa Mungu naye akauliza. “Nitawezaje kulichukua Sanduku la Mungu kwangu?” \v 13 Hakulichukua hilo Sanduku akae nalo katika Mji wa Daudi. Badala yake, akalipeleka nyumbani kwa Obed-Edomu, Mgiti. \v 14 Sanduku la Mungu likabaki pamoja na jamaa ya Obed-Edomu, nyumbani kwake kwa miezi mitatu, naye \nd Bwana\nd* akaibariki nyumba yake pamoja na kila kitu alichokuwa nacho. \c 14 \s1 Nyumba Ya Daudi Na Jamaa Yake \r (2 Samweli 5:11-16) \p \v 1 Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme. \v 2 Naye Daudi akatambua kwamba \nd Bwana\nd* amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake. \p \v 3 Huko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi. \v 4 Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, \v 5 Ibihari, Elishua, Elpeleti, \v 6 Noga, Nefegi, Yafia, \v 7 Elishama, Beeliada na Elifeleti. \s1 Daudi Awashinda Wafilisti \r (2 Samweli 5:17-25) \p \v 8 Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao. \v 9 Basi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai, \v 10 Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” \p \nd Bwana\nd* akamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.” \p \v 11 Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu,\f + \fr 14:11 \ft Maana yake ni Bwana Afurikae.\f* akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. \v 12 Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto. \p \v 13 Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; \v 14 hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi. \v 15 Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.” \v 16 Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri. \p \v 17 Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, naye \nd Bwana\nd* akayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi. \c 15 \s1 Sanduku La Agano Laletwa Yerusalemu \r (2 Samweli 6:12-22) \p \v 1 Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake. \v 2 Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu \nd Bwana\nd* aliwachagua kulibeba Sanduku la \nd Bwana\nd* na kuhudumu mbele zake milele.” \p \v 3 Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la \nd Bwana\nd* na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake. \v 4 Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi: \li1 \v 5 Kutoka wazao wa Kohathi, \li2 Urieli kiongozi na ndugu zake 120, \li1 \v 6 Kutoka wazao wa Merari, \li2 Asaya kiongozi na ndugu zake 220. \li1 \v 7 Kutoka wazao wa Gershoni,\f + \fr 15:7 \ft Namna nyingine ya kutaja Gershomu.\f* \li2 Yoeli kiongozi na ndugu zake 130. \li1 \v 8 Kutoka wazao wa Elisafani, \li2 Shemaya kiongozi na ndugu zake 200. \li1 \v 9 Kutoka wazao wa Hebroni, \li2 Elieli kiongozi na ndugu zake 80. \li1 \v 10 Kutoka wazao wa Uzieli, \li2 Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112. \p \v 11 Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu. \v 12 Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake. \v 13 Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la \nd Bwana\nd* mara ya kwanza, hata ikasababisha \nd Bwana\nd* Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.” \v 14 Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku la \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli. \v 15 Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno la \nd Bwana\nd*. \p \v 16 Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi. \p \v 17 Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya; \v 18 hawa ndio waliochaguliwa kuwa wasaidizi wao: Zekaria, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaya, Maaseya, Matithia, Elifelehu, Mikneya, pamoja na mabawabu Obed-Edomu na Yehieli. \p \v 19 Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba; \v 20 Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti ya \it alamothi\it*,\f + \fr 15:20 \ft Huenda ni aina ya uimbaji.\f* \v 21 na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya \it sheminithi\it*.\f + \fr 15:21 \ft Huenda ni aina ya uimbaji.\f* \v 22 Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo. \p \v 23 Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku. \v 24 Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku. \p \v 25 Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd* kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe. \v 26 Kwa sababu Mungu alikuwa amewasaidia Walawi waliokuwa wanalichukua Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd*, mafahali saba na kondoo dume saba walitolewa dhabihu. \v 27 Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi. \v 28 Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd* kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi. \p \v 29 Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd* lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake. \c 16 \s1 Sanduku Lawekwa Ndani Ya Hema \p \v 1 Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. \v 2 Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la \nd Bwana\nd*. \v 3 Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu. \p \v 4 Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la \nd Bwana\nd* kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli: \v 5 Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, \v 6 nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu. \s1 Zaburi Ya Daudi Ya Shukrani \r (Zaburi 105:1-15; 96:1-13; 106:1, 47-48) \p \v 7 Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa \nd Bwana\nd*: \q1 \v 8 Mshukuruni \nd Bwana\nd*, liitieni jina lake; \q2 wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. \q1 \v 9 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; \q2 waambieni matendo yake yote ya ajabu. \q1 \v 10 Lishangilieni jina lake takatifu; \q2 mioyo ya wale wamtafutao \nd Bwana\nd* na ifurahi. \q1 \v 11 Mtafuteni \nd Bwana\nd* na nguvu zake; \q2 utafuteni uso wake siku zote. \q1 \v 12 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, \q2 miujiza yake na hukumu alizozitamka, \q1 \v 13 enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, \q2 enyi wana wa Yakobo, wateule wake. \b \q1 \v 14 Yeye ndiye \nd Bwana\nd* Mungu wetu; \q2 hukumu zake zimo duniani pote. \q1 \v 15 Hulikumbuka agano lake milele, \q2 neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, \q1 \v 16 agano alilolifanya na Abrahamu, \q2 kiapo alichomwapia Isaki. \q1 \v 17 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, \q2 kwa Israeli liwe agano la milele: \q1 \v 18 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani \q2 kuwa sehemu utakayoirithi.” \b \q1 \v 19 Walipokuwa wachache kwa idadi, \q2 wachache sana na wageni ndani yake, \q1 \v 20 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, \q2 kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. \q1 \v 21 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; \q2 kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: \q1 \v 22 “Msiwaguse niliowatia mafuta; \q2 msiwadhuru manabii wangu.” \b \q1 \v 23 Mwimbieni \nd Bwana\nd* dunia yote; \q2 tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. \q1 \v 24 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, \q2 matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. \q1 \v 25 Kwa kuwa \nd Bwana\nd* ni mkuu, \q2 mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; \q2 yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. \q1 \v 26 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, \q2 lakini \nd Bwana\nd* aliziumba mbingu. \q1 \v 27 Fahari na enzi viko mbele yake; \q2 nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. \q1 \v 28 Mpeni \nd Bwana\nd*, enyi jamaa za mataifa, \q2 mpeni \nd Bwana\nd* utukufu na nguvu, \q1 \v 29 mpeni \nd Bwana\nd* utukufu \q2 unaostahili jina lake. \q1 Leteni sadaka na mje katika nyua zake; \q2 mwabuduni \nd Bwana\nd* katika uzuri wa utakatifu wake. \q1 \v 30 Dunia yote na itetemeke mbele zake! \q2 Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa. \q1 \v 31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; \q2 semeni katikati ya mataifa, “\nd Bwana\nd* anatawala!” \q1 \v 32 Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; \q2 mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake. \q1 \v 33 Kisha miti ya msituni itaimba, \q2 itaimba kwa furaha mbele za \nd Bwana\nd*, \q2 kwa maana anakuja kuihukumu dunia. \b \q1 \v 34 Mshukuruni \nd Bwana\nd* kwa kuwa ni mwema; \q2 upendo wake wadumu milele. \q1 \v 35 Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe. \q2 Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa, \q1 ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, \q2 na kushangilia katika sifa zako.” \q1 \v 36 Atukuzwe \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli, \q2 tangu milele na hata milele. \m Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni \nd Bwana\nd*.” \b \p \v 37 Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd* ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku. \v 38 Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango. \p \v 39 Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya \nd Bwana\nd* katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni \v 40 ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa \nd Bwana\nd* kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya \nd Bwana\nd* ambayo alikuwa amempa Israeli. \v 41 Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa \nd Bwana\nd* shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.” \v 42 Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni. \p \v 43 Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake. \c 17 \s1 Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi \r (2 Samweli 7:1-17) \p \v 1 Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd* liko ndani ya hema.” \p \v 2 Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.” \v 3 Usiku ule neno la Mungu likamjia Nathani, kusema: \pm \v 4 “Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd*: Wewe hutanijengea mimi nyumba ili nikae humo. \v 5 Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine. \v 6 Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’  \pm \v 7 “Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli. \v 8 Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. \v 9 Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, \v 10 na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote. \pm “ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba \nd Bwana\nd* atakujengea nyumba: \v 11 Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake. \v 12 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele. \v 13 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia. \v 14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ” \p \v 15 Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya. \s1 Maombi Ya Daudi \r (2 Samweli 7:18-29) \p \v 16 Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za \nd Bwana\nd*, akasema: \pm “Mimi ni nani, Ee \nd Bwana\nd* Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? \v 17 Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, Ee \nd Bwana\nd* Mungu. \pm \v 18 “Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako, \v 19 Ee \nd Bwana\nd* Mungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana. \pm \v 20 “Hakuna aliye kama wewe, Ee \nd Bwana\nd* Mungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe. \v 21 Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? \v 22 Uliwafanya watu wako Israeli kuwa watu wako wewe mwenyewe milele, nawe, Ee \nd Bwana\nd* Mungu, umekuwa Mungu wao. \pm \v 23 “Sasa basi, \nd Bwana\nd* ahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi, \v 24 ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘\nd Bwana\nd* Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako. \pm \v 25 “Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya. \v 26 Ee \nd Bwana\nd*, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. \v 27 Basi imekupendeza kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu milele machoni pako; kwa ajili yako, Ee \nd Bwana\nd*, umeibariki, nayo itabarikiwa milele.” \c 18 \s1 Ushindi Wa Daudi \r (2 Samweli 8:1-18) \p \v 1 Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Gathi pamoja na vijiji vinavyouzunguka kutoka utawala wa Wafilisti. \p \v 2 Pia Daudi akawashinda Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru. \p \v 3 Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alikwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Frati. \v 4 Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100. \p \v 5 Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao. \v 6 Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumwa wa Daudi, na kumlipa ushuru. \nd Bwana\nd* akampa Daudi ushindi kote alipokwenda. \p \v 7 Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizokuwa za maafisa wa Hadadezeri na kuzileta Yerusalemu. \v 8 Kutoka miji ya Tibhathi na Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi sana, ambayo Solomoni aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba. \p \v 9 Tou mfalme wa Hamathi aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri mfalme wa Soba, \v 10 akamtuma mwanawe, Hadoramu kwa Mfalme Daudi ili kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Mfalme Hadadezeri, kwa kuwa alikuwa amepigana vita mara nyingi na Tou. Hadoramu akamletea Daudi vifaa mbalimbali vya dhahabu, fedha na shaba. \p \v 11 Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa \nd Bwana\nd* kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki. \p \v 12 Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi. \v 13 Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi. \nd Bwana\nd* akampa Daudi ushindi kila alipokwenda. \s1 Maafisa Wa Daudi \p \v 14 Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote. \v 15 Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu; \v 16 Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; Shausha alikuwa mwandishi; \v 17 naye Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa msimamizi wa Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi walikuwa maafisa wakuu katika utumishi wa mfalme. \c 19 \s1 Vita Dhidi Ya Waamoni \r (2 Samweli 10:1-19) \p \v 1 Baada ya muda, Nahashi mfalme wa Waamoni akafa, mwanawe akaingia mahali pake. \v 2 Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea wema.” \p Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji, \v 3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?” \v 4 Kwa hiyo Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa ndevu akakata nguo zao katikati kwenye matako, akawaacha waende zao. \p \v 5 Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mje.” \p \v 6 Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000\f + \fr 19:6 \ft Talanta 1,000 za fedha ni sawa na tani 34.\f* za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu,\f + \fr 19:6 \ft Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi.\f* Aramu-Maaka na Soba. \v 7 Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita. \p \v 8 Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji. \v 9 Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani. \p \v 10 Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu. \v 11 Akawaweka wale wanajeshi wengine waliobaki chini ya amri ya Abishai ndugu yake, nao wakapangwa ili wakabiliane na Waamoni. \v 12 Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe unisaidie; lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakusaidia. \v 13 Uwe hodari na tupigane kwa ujasiri kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu. \nd Bwana\nd* atafanya lile lililo jema machoni pake.” \p \v 14 Basi Yoabu na vikosi vyake wakasonga mbele kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia mbele yake. \v 15 Waamoni walipoona Waaramu wanakimbia, nao pia wakakimbia mbele ya nduguye Abishai na kuingia ndani ya mji. Basi Yoabu akarudi Yerusalemu. \p \v 16 Baada ya Waaramu kuona kwamba wameshindwa na Israeli, wakapeleka wajumbe na kuwataka Waaramu wengine kutoka ngʼambo ya Mto Frati, wakiongozwa na Shofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri. \p \v 17 Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake. \v 18 Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao. \p \v 19 Raiya wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi, wakawa watumishi wake. \p Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena. \c 20 \s1 Kutekwa Kwa Raba \r (2 Samweli 12:26-31) \p \v 1 Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni, na akaenda Raba na kuuzingira, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akashambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu. \v 2 Daudi akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu,\f + \fr 20:2 \ft Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.\f* nayo ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mjini huo. \v 3 Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu. \s1 Vita Na Wafilisti \r (2 Samweli 21:15-22) \p \v 4 Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai,\f + \fr 20:4 \ft Yaani majitu.\f* nao Wafilisti wakashindwa. \p \v 5 Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji. \p \v 6 Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. \v 7 Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua. \p \v 8 Hawa walikuwa ndio wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake. \c 21 \s1 Daudi Ahesabu Wapiganaji \r (2 Samweli 24:1-25) \p \v 1 Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli. \v 2 Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.” \p \v 3 Yoabu akajibu, “\nd Bwana\nd* na aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana wangu, kwani hawa wote si raiya wa bwana wangu? Kwa nini bwana wangu unataka kufanya hivi? Kwa nini kuleta hatia juu ya Israeli?” \p \v 4 Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu; kwa hiyo Yoabu akaondoka na kuzunguka Israeli yote kisha akarudi Yerusalemu. \v 5 Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000. \p \v 6 Lakini Yoabu hakuwahesabu Walawi na Wabenyamini, kwa sababu alichukizwa sana na amri ya mfalme. \v 7 Amri hii ilikuwa mbaya machoni pa Mungu pia; hivyo akaiadhibu Israeli. \p \v 8 Kisha Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Sasa, ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.” \p \v 9 \nd Bwana\nd* akamwambia Gadi, mwonaji wa Daudi, \v 10 “Nenda ukamwambie Daudi, hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ” \p \v 11 Kwa hiyo Gadi akamwendea Daudi akamwambia, “Hili ndilo \nd Bwana\nd* asemalo: ‘Chagua: \v 12 miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa \nd Bwana\nd*, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa \nd Bwana\nd* akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.” \p \v 13 Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa \nd Bwana\nd* kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.” \p \v 14 Basi \nd Bwana\nd* akatuma tauni katika Israeli, watu 70,000 wa Israeli wakafa. \v 15 Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo, \nd Bwana\nd* akaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa \nd Bwana\nd* alikuwa amesimama katika sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna\f + \fr 21:15 \ft Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania.\f* Myebusi. \p \v 16 Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa \nd Bwana\nd* akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi. \p \v 17 Daudi akamwambia Mungu, “Je, si mimi ndiye niliyeamuru watu wahesabiwe? Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Ee \nd Bwana\nd*, Mungu wangu, mkono wako na uwe juu yangu mimi na jamaa yangu, lakini usiache tauni hii iendelee juu ya watu wako.” \p \v 18 Kisha malaika wa \nd Bwana\nd* akamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengea \nd Bwana\nd* madhabahu kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi. \v 19 Kwa hiyo Daudi akakwea, akalitii lile neno ambalo Gadi alikuwa amelisema katika jina la \nd Bwana\nd*. \p \v 20 Arauna alipokuwa akipura ngano, akageuka akamwona yule malaika. Wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha, yeye akaendelea kupura ngano. \v 21 Kisha Daudi akakaribia, Arauna alipotazama na kumwona, akaondoka kwenye uwanja wa kupuria nafaka akamsujudia Daudi akiuinamisha uso wake ardhini. \p \v 22 Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu ya \nd Bwana\nd* tauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.” \p \v 23 Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.” \p \v 24 Lakini Mfalme Daudi akamjibu Arauna, “La hasha! Lakini ninasisitiza kwamba nitalipa bei yake kamili. Sitachukua kilicho chako kwa ajili ya \nd Bwana\nd* au kutoa sadaka ya kuteketezwa ambayo hainigharimu chochote.” \p \v 25 Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600\f + \fr 21:25 \ft Shekeli 600 za dhahabu ni sawa na kilo 7.\f* kwa ajili ya ule uwanja. \v 26 Kisha Daudi akamjengea \nd Bwana\nd* madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita \nd Bwana\nd* naye \nd Bwana\nd* akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. \p \v 27 Kisha \nd Bwana\nd* akanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake. \v 28 Wakati huo, Daudi alipoona kwamba \nd Bwana\nd* amemjibu kule kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna Myebusi, akatoa dhabihu huko. \v 29 Maskani ya \nd Bwana\nd* ambayo Mose aliitengeneza kule jangwani, pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa wakati huo vilikuwa viko mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni. \v 30 Lakini Daudi hakuthubutu kuisogelea ili kumuuliza Mungu, kwa sababu aliuogopa upanga wa yule malaika wa \nd Bwana\nd*. \c 22 \p \v 1 Ndipo Daudi akasema, “Nyumba ya \nd Bwana\nd* Mungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.” \s1 Maandalizi Kwa Ajili Ya Hekalu \p \v 2 Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. \v 3 Daudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika. \v 4 Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi. \p \v 5 Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili ya \nd Bwana\nd* inatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake. \p \v 6 Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili ya \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli. \v 7 Daudi akamwambia Solomoni: “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina la \nd Bwana\nd* Mungu wangu. \v 8 Lakini neno hili la \nd Bwana\nd* likanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu. \v 9 Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake. \v 10 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’ \p \v 11 “Sasa, mwanangu, \nd Bwana\nd* awe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba ya \nd Bwana\nd* Mungu wako, kama alivyosema utafanya. \v 12 \nd Bwana\nd* na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya \nd Bwana\nd* Mungu wako. \v 13 Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria \nd Bwana\nd* alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa. \p \v 14 “Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la \nd Bwana\nd*: talanta 100,000\f + \fr 22:14 \ft Talanta 100,000 za dhahabu ni sawa na tani 3,750.\f* za dhahabu, talanta 1,000,000\f + \fr 22:14 \ft Talanta 1,000,000 za fedha ni sawa na tani 37,500.\f* za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. \v 15 Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi \v 16 wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, naye \nd Bwana\nd* awe pamoja nawe.” \p \v 17 Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe. \v 18 Akawaambia, “Je, \nd Bwana\nd* Mungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini ya \nd Bwana\nd* na watu wake. \v 19 Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta \nd Bwana\nd* Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya \nd Bwana\nd* Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd* na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la \nd Bwana\nd*.” \c 23 \s1 Jamaa Za Walawi Na Utendaji Wao \p \v 1 Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli. \p \v 2 Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. \v 3 Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000. \v 4 Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu la \nd Bwana\nd* na 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi, \v 5 na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifu \nd Bwana\nd* kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.” \p \v 6 Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari. \s1 Wagershoni \li1 \v 7 Wana wa Wagershoni walikuwa wawili: \li2 Ladani na Shimei. \li1 \v 8 Wana wa Ladani walikuwa watatu: \li2 Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli. \li1 \v 9 Wana wa Shimei walikuwa watatu: \li2 Shelomothi,\f + \fr 23:9 \ft Yaani Shelomithi; maana yake ni Mpenda amani.\f* Hazieli na Harani. \li2 Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani. \li1 \v 10 Nao wana wa Shimei walikuwa wanne: \li2 Yahathi, Zina,\f + \fr 23:10 \ft Tafsiri zingine zinamwita Ziza.\f* Yeushi na Beria. \li2 \v 11 Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja. \s1 Wakohathi \li1 \v 12 Wana wa Kohathi walikuwa wanne: \li2 Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. \li1 \v 13 Wana wa Amramu walikuwa: \li2 Aroni na Mose. \li2 Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za \nd Bwana\nd*, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la \nd Bwana\nd* milele. \v 14 Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi. \li1 \v 15 Wana wa Mose walikuwa: \li2 Gershomu na Eliezeri. \li1 \v 16 Wazao wa Gershomu: \li2 Shebueli alikuwa wa kwanza. \li1 \v 17 Wazao wa Eliezeri: \li2 Rehabia alikuwa wa kwanza. \li2 Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana. \li1 \v 18 Wana wa Ishari: \li2 Shelomithi alikuwa wa kwanza. \li1 \v 19 Wana wa Hebroni walikuwa: \li2 Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu. \li1 \v 20 Wana wa Uzieli walikuwa: \li2 Mika wa kwanza na Ishia wa pili. \s1 Wamerari \li1 \v 21 Wana wa Merari walikuwa: \li2 Mahli na Mushi. \li1 Wana wa Mahli walikuwa: \li2 Eleazari na Kishi. \li2 \v 22 Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa. \li1 \v 23 Wana wa Mushi: \li2 Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu. \b \p \v 24 Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu la \nd Bwana\nd*. \v 25 Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vile \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele, \v 26 Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.” \v 27 Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi. \p \v 28 Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu la \nd Bwana\nd*: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu. \v 29 Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa. \v 30 Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu \nd Bwana\nd*. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni \v 31 na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa \nd Bwana\nd* siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za \nd Bwana\nd* mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo. \p \v 32 Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la \nd Bwana\nd*. \c 24 \s1 Migawanyo Ya Makuhani \p \v 1 Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni: \p Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. \v 2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani. \v 3 Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao. \v 4 Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari. \v 5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari. \p \v 6 Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari. \b \li1 \v 7 Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu, \li1 ya pili Yedaya, \li1 \v 8 ya tatu Harimu, \li1 ya nne Seorimu, \li1 \v 9 ya tano Malkiya, \li1 ya sita Miyamini, \li1 \v 10 ya saba Hakosi, \li1 ya nane Abiya, \li1 \v 11 ya tisa Yeshua, \li1 ya kumi Shekania, \li1 \v 12 ya kumi na moja Eliashibu, \li1 ya kumi na mbili Yakimu, \li1 \v 13 ya kumi na tatu Hupa, \li1 ya kumi na nne Yeshebeabu, \li1 \v 14 ya kumi na tano Bilga, \li1 ya kumi na sita Imeri, \li1 \v 15 ya kumi na saba Heziri, \li1 ya kumi na nane Hapisesi, \li1 \v 16 ya kumi na tisa Pethahia, \li1 ya ishirini Yehezkeli, \li1 \v 17 ya ishirini na moja Yakini, \li1 ya ishirini na mbili Gamuli, \li1 \v 18 ya ishirini na tatu Delaya, \li1 ya ishirini na nne Maazia. \b \p \v 19 Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la \nd Bwana\nd* kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru. \s1 Walawi Waliobaki \m \v 20 Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki: \li1 Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli; \li2 kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya. \li2 \v 21 Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe: \li2 Ishia alikuwa wa kwanza. \li1 \v 22 Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi, \li2 kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi. \li1 \v 23 Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne. \li1 \v 24 Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika; \li2 kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri. \li2 \v 25 Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia; \li2 na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria. \li1 \v 26 Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi. \li2 Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno. \li1 \v 27 Wana wa Merari: \li2 kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri. \li1 \v 28 Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana. \li1 \v 29 Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi: \li2 alikuwa Yerameeli. \li1 \v 30 Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi. \b \p Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao. \v 31 Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo. \c 25 \s1 Waimbaji \p \v 1 Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii: \b \li1 \v 2 Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa: \li2 Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme. \li1 \v 3 Wana wa Yeduthuni walikuwa sita: \li2 Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuza \nd Bwana\nd*. \li1 \v 4 Wana wa Hemani walikuwa: \li2 Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi. \v 5 Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu. \b \p \v 6 Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la \nd Bwana\nd* wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme. \v 7 Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa \nd Bwana\nd*. Idadi yao walikuwa 288. \v 8 Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura. \b \tr \tc1 \v 9 Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 Ya pili ikamwangukia Gedalia, //yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 10 Ya tatu ikamwangukia Zakuri, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 11 ya nne ikamwangukia Isri,\f + \fr 25:11 \ft Isri jina lingine ni Seri.\f* //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 12 ya tano ikamwangukia Nethania, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 13 ya sita ikamwangukia Bukia, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 14 ya saba ikamwangukia Yesarela,\f + \fr 25:14 \ft Yesarela jina lingine ni Asarela.\f* //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 15 ya nane ikamwangukia Yeshaya, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 16 ya tisa ikamwangukia Matania, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 17 ya kumi ikamwangukia Shimei, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 18 ya kumi na moja ikamwangukia Azareli,\f + \fr 25:18 \ft Azareli jina lingine ni Uzieli.\f* //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 19 ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 20 ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 21 ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 22 ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 23 Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 24 ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 25 ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 26 ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 27 ya ishirini ikamwangukia Eliatha, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 28 ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 29 ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 30 ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12 \tr \tc1 \v 31 ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, //wanawe na jamaa zake, \tcr2 12. \c 26 \s1 Mabawabu \p \v 1 Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu: \b \li1 Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu. \li1 \v 2 Meshelemia alikuwa na wana wafuatao: \li2 Zekaria mzaliwa wa kwanza, \li2 Yediaeli wa pili, \li2 Zebadia wa tatu, \li2 Yathnieli wa nne, \li2 \v 3 Elamu wa tano \li2 Yehohanani wa sita \li2 na Eliehoenai wa saba. \li1 \v 4 Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao: \li2 Shemaya mzaliwa wa kwanza, \li2 Yehozabadi wa pili, \li2 Yoa wa tatu, \li2 Sakari wa nne, \li2 Nethaneli wa tano, \li2 \v 5 Amieli wa sita, \li2 Isakari wa saba, \li2 na Peulethai wa nane. \li2 (Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.) \b \li1 \v 6 Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. \v 7 Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. \v 8 Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili. \li1 \v 9 Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane. \b \li1 \v 10 Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), \v 11 Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu. \p \v 12 Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa \nd Bwana\nd* kama jamaa zao walivyokuwa nazo. \v 13 Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. \p \v 14 Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.\f + \fr 26:14 \ft Shelemia jina lingine ni Meshelemia.\f* Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. \v 15 Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. \v 16 Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa. \p Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: \v 17 Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. \v 18 Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe. \p \v 19 Hii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari. \s1 Watunza Hazina Na Maafisa Wengine \p \v 20 Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. \p \v 21 Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, \v 22 wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la \nd Bwana\nd*. \p \v 23 Kutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli: \b \li1 \v 24 Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. \v 25 Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi. \v 26 Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. \v 27 Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la \nd Bwana\nd*. \v 28 Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake. \li1 \v 29 Kutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli. \li1 \v 30 Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za \nd Bwana\nd* na utumishi wa mfalme. \v 31 Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. \v 32 Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme. \c 27 \s1 Vikosi Vya Jeshi \p \v 1 Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000. \b \li1 \v 2 Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake. \v 3 Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza. \li1 \v 4 Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 5 Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000. \v 6 Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake. \li1 \v 7 Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 8 Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 9 Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 10 Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 11 Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 12 Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 13 Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 14 Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \li1 \v 15 Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000. \s1 Maafisa Wa Makabila \li1 \v 16 Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa: \b \li1 Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri; \li1 kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka; \li1 \v 17 kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli; \li1 kwa Aroni: Sadoki; \li1 \v 18 kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi; \li1 kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli; \li1 \v 19 kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia; \li1 kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli; \li1 \v 20 kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia; \li1 kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya; \li1 \v 21 kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria; \li1 kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri; \li1 \v 22 kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu. \p Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli. \b \p \v 23 Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu \nd Bwana\nd* alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani. \v 24 Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi. \s1 Wasimamizi Wa Mali Za Mfalme \p \v 25 Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme. \p Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia. \p \v 26 Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba. \p \v 27 Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu. \p Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa. \p \v 28 Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi. \p Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni. \p \v 29 Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni. \p Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni. \p \v 30 Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia. \p Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda. \p \v 31 Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi. \p Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi. \b \p \v 32 Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme. \p \v 33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme. \p Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme. \v 34 Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari. \p Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme. \c 28 \s1 Maandalizi Ya Daudi Ya Kujenga Hekalu \p \v 1 Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na askari wote walio hodari. \p \v 2 Mfalme Daudi akainuka na kusema: “Nisikilizeni ndugu zangu nanyi watu wangu. Nilikuwa na nia ya kujenga nyumba ili iwe mahali pa kukaa Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd* kwa ajili ya kuwa mahali pa kuwekea miguu ya Mungu wetu, nami nikafanya maandalizi ya kuijenga. \v 3 Lakini Mungu akaniambia, ‘Wewe hutajenga nyumba kwa Jina langu, kwa sababu wewe umepigana vita na umemwaga damu.’ \p \v 4 “Hata hivyo, \nd Bwana\nd*, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote. \v 5 Miongoni mwa wanangu wote, naye \nd Bwana\nd* amenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme wa \nd Bwana\nd* juu ya Israeli. \v 6 Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. \v 7 Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’ \p \v 8 “Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la \nd Bwana\nd* naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za \nd Bwana\nd* Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele. \p \v 9 “Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana \nd Bwana\nd* huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele. \v 10 Angalia basi, kwa maana \nd Bwana\nd* amekuchagua wewe ili ujenge Hekalu kuwa mahali patakatifu. Uwe hodari ukafanye kazi hiyo.” \p \v 11 Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho. \v 12 Akampa vielelezo vya yote Roho alikuwa ameviweka moyoni mwake kwa ajili ya kumbi za Hekalu la \nd Bwana\nd* na vyumba vyote vilivyolizunguka, kwa ajili ya hazina za Hekalu la Mungu na kwa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. \v 13 Mfalme pia akampa Solomoni maelekezo kwa ajili ya migawanyo ya huduma za makuhani na Walawi, pia kwa ajili ya kazi zote za huduma katika Hekalu la \nd Bwana\nd*. Akampa pia maelezo kuhusu vifaa vyote vya kutumika katika huduma ya Hekalu. \v 14 Akamwagizia uzito wa dhahabu kwa ajili ya vitu vyote vya dhahabu vya kutumika katika huduma mbalimbali, uzito wa fedha kwa ajili ya vitu vyote vya fedha vya kutumika katika huduma mbalimbali. \v 15 Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake, pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara; \v 16 uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha; \v 17 uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha; \v 18 na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano la \nd Bwana\nd*. \p \v 19 Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwa \nd Bwana\nd* ulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.” \p \v 20 Daudi pia akamwambia Solomoni mwanawe, “Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maana \nd Bwana\nd* aliye Mungu, Mungu wangu yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia mpaka kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu la \nd Bwana\nd* itakapokamilika. \v 21 Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yoyote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.” \c 29 \s1 Matoleo Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Hekalu \p \v 1 Ndipo Mfalme Daudi akaliambia kusanyiko lote: “Mwanangu Solomoni, yeye ambaye Mungu amemchagua, ni kijana mdogo na asiye na uzoefu. Kazi hii ni kubwa, kwa sababu Hekalu hili la fahari si kwa ajili ya mwanadamu bali ni kwa ajili ya \nd Bwana\nd*. \v 2 Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno. \v 3 Zaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu: \v 4 talanta 3,000\f + \fr 29:4 \ft Talanta 3,000 za dhahabu sawa na tani 110.\f* za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000\f + \fr 29:4 \ft Talanta 7,000 za fedha ni sawa na tani 260.\f* za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu, \v 5 kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa \nd Bwana\nd* leo?” \p \v 6 Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao. \p \v 7 Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000\f + \fr 29:7 \ft Talanta 5,000 za dhahabu ni sawa na tani 190.\f* na darkoni 10,000\f + \fr 29:7 \ft Darkoni 10,000 za dhahabu ni sawa na kilo 84.\f* za dhahabu, talanta 10,000\f + \fr 29:7 \ft Talanta 10,000 za fedha ni sawa na tani 375.\f* za fedha, talanta 18,000\f + \fr 29:7 \ft Talanta 18,000 za shaba ni sawa na tani 675.\f* za shaba na talanta 100,000\f + \fr 29:7 \ft Talanta 100,000 za chuma ni sawa na tani 3,750.\f* za chuma. \v 8 Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la \nd Bwana\nd* chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. \v 9 Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa \nd Bwana\nd*. Mfalme Daudi pia akafurahi sana. \s1 Maombi Ya Daudi \p \v 10 Daudi akamhimidi \nd Bwana\nd* mbele ya kusanyiko lote, akisema: \q1 “Uhimidiwe wewe, Ee \nd Bwana\nd*, \q2 Mungu wa Israeli baba yetu, \q2 tangu milele hata milele. \q1 \v 11 Ukuu na uweza, ni vyako, Ee \nd Bwana\nd*, \q2 na utukufu na enzi na uzuri, \q1 kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani \q2 ni chako wewe. \q1 Ee \nd Bwana\nd*, ufalme ni wako; \q2 umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote. \q1 \v 12 Utajiri na heshima vyatoka kwako; \q2 wewe ndiwe utawalaye vitu vyote. \q1 Mikononi mwako kuna nguvu na uweza \q2 ili kuinua na kuwapa wote nguvu, \q1 \v 13 Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru \q2 na kulisifu Jina lako tukufu. \p \v 14 “Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako. \v 15 Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini. \v 16 Ee \nd Bwana\nd* Mungu wetu, kwa wingi wote huu ambao tumekutolea kwa kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina lako Takatifu, vimetoka mkononi mwako, navyo vyote ni mali yako. \v 17 Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe. \v 18 Ee \nd Bwana\nd*, Mungu wa baba zetu Abrahamu, Isaki na Israeli, weka shauku hii ndani ya mioyo ya watu wako daima na uifanye mioyo yao iwe na uaminifu kwako. \v 19 Nawe umpe mwanangu Solomoni kujitolea kwako kwa moyo wote ili kuzishika amri zako, masharti yako, maagizo yako na kufanya kila kitu ili kujenga Hekalu hili la fahari ambalo kwa ajili yake nimetoa.” \p \v 20 Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini \nd Bwana\nd* Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi \nd Bwana\nd*, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za \nd Bwana\nd* na mfalme. \s1 Solomoni Akubalika Kuwa Mfalme \p \v 21 Siku ya pili yake wakamtolea \nd Bwana\nd* dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo dume 1,000 na wana-kondoo dume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli. \v 22 Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za \nd Bwana\nd* siku ile. \p Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya \nd Bwana\nd* ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani. \v 23 Solomoni akaketi kwenye kiti cha enzi cha \nd Bwana\nd* kuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii. \v 24 Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni. \p \v 25 \nd Bwana\nd* akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo. \s1 Muhtasari Wa Utawala Wa Daudi \p \v 26 Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote. \v 27 Alitawala Israeli kwa miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. \p \v 28 Daudi akafa akiwa mzee mwenye umri mwema, akiwa ameshiba siku, utajiri na heshima. Naye Solomoni mwanawe akawa mfalme baada yake. \p \v 29 Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi, \v 30 pamoja na habari zote za utawala wake, nguvu zake na matukio yaliyompata yeye, na Israeli, na falme za nchi nyingine zote.