\id JOB - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version \rem Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc. \h Ayubu \toc1 Ayubu \toc2 Ayubu \toc3 Ay \mt1 Ayubu \c 1 \ms1 Sehemu Ya Kwanza: Habari Za Awali \mr (Ayubu 1–2) \s1 Ayubu Na Jamaa Yake \p \v 1 Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu. \v 2 Alikuwa na wana saba na binti watatu, \v 3 naye alikuwa na kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia tano za maksai, na punda mia tano, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki. \p \v 4 Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika umbu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao. \v 5 Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu. \s1 Jaribu La Kwanza La Ayubu \p \v 6 Siku moja wana wa Mungu\f + \fr 1:6 \ft Wana wa Mungu hapa ina maana malaika au viumbe vya mbinguni.\f* walikwenda kujionyesha mbele za \nd Bwana\nd*. Shetani\f + \fr 1:6 \ft Shetani hapa ina maana ya mshtaki wa watakatifu.\f* naye akaja pamoja nao. \v 7 \nd Bwana\nd* akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?” \p Shetani akamjibu \nd Bwana\nd*, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.” \p \v 8 Ndipo \nd Bwana\nd* akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.” \p \v 9 Shetani akamjibu \nd Bwana\nd*, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? \v 10 Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima. \v 11 Lakini nyoosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.” \p \v 12 \nd Bwana\nd* akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.” \p Ndipo Shetani akatoka mbele za \nd Bwana\nd*. \p \v 13 Siku moja watoto wa Ayubu walipokuwa wakifanya karamu wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, \v 14 akaja mjumbe kwa Ayubu na kusema, “Maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakilisha karibu nao, \v 15 Waseba wakawashambulia na kuchukua mifugo. Kisha wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!” \p \v 16 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Moto wa Mungu ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kondoo na watumishi, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!” \p \v 17 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.” \p \v 18 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wana wako na binti zako walipokuwa wakifanya karamu, wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, \v 19 ghafula upepo wenye nguvu ukavuma kutoka jangwani, nao ukaipiga nyumba hiyo pembe zake nne. Ikawaangukia hao watoto nao wamekufa, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!” \p \v 20 Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu \v 21 na kusema: \q1 “Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi, \q2 nami nitaondoka uchi,\f + \fr 1:21 \ft Au: nitarudi huko uchi.\f* \q1 \nd Bwana\nd* alinipa, naye \nd Bwana\nd* ameviondoa, \q2 jina la \nd Bwana\nd* litukuzwe.” \p \v 22 Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya. \c 2 \s1 Jaribu La Pili La Ayubu \p \v 1 Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele za \nd Bwana\nd*. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake. \v 2 \nd Bwana\nd* akamuuliza Shetani, “Umetoka wapi?” \p Shetani akamjibu \nd Bwana\nd* “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.” \p \v 3 \nd Bwana\nd* akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, mtu asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.” \p \v 4 Shetani akamjibu \nd Bwana\nd*, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake. \v 5 Lakini nyoosha mkono wako na kuipiga nyama yake na mifupa yake, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.” \p \v 6 \nd Bwana\nd* akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, yeye yumo mikononi mwako, lakini lazima umwachie uhai wake.” \p \v 7 Basi Shetani akatoka mbele za \nd Bwana\nd* naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa. \v 8 Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu. \p \v 9 Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!” \p \v 10 Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu\f + \fr 2:10 \ft Mpumbavu hapa ina maana ya kupungukiwa maadili.\f* yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?” \p Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake. \s1 Marafiki Watatu Wa Ayubu \p \v 11 Basi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji. \v 12 Walipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua. Wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao. \v 13 Kisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba usiku na mchana. Hakuna yeyote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa. \c 3 \ms1 Sehemu Ya Pili: Mazungumzo Ya Ayubu Na Rafiki Zake Watatu \mr (Ayubu 3–31) \ms2 Hotuba Ya Kwanza Ya Ayubu \s1 Ayubu Anazungumza \p \v 1 Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake. \p \v 2 Kisha akasema: \q1 \v 3 “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, \q2 nao usiku ule iliposemekana, \q2 ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’ \q1 \v 4 Siku ile na iwe giza; \q2 Mungu juu na asiiangalie; \q2 nayo nuru isiiangazie. \q1 \v 5 Giza na kivuli kikuu kiikalie tena; \q2 wingu na likae juu yake; \q2 weusi na uifunike nuru yake. \q1 \v 6 Usiku ule na ushikwe na giza kuu; \q2 usihesabiwe katika siku za mwaka, \q2 wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote. \q1 \v 7 Usiku ule na uwe tasa; \q2 sauti ya furaha na isisikike ndani yake. \q1 \v 8 Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku, \q2 wale walio tayari kumwamsha Lewiathani.\f + \fr 3:8 \ft Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.\f* \q1 \v 9 Nyota zake za alfajiri na ziwe giza; \q2 nao ungojee mwanga bila mafanikio, \q1 wala usiuone mwonzi wa kwanza \q2 wa mapambazuko, \q1 \v 10 kwa sababu huo usiku haukunifungia \q2 mlango wa tumbo la mama yangu, \q1 ili kuyaficha macho yangu \q2 kutokana na taabu. \b \q1 \v 11 “Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa? \q2 Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni? \q1 \v 12 Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea \q2 na matiti ili nipate kunyonyeshwa? \q1 \v 13 Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani. \q2 Ningekuwa nimelala na kupumzika \q1 \v 14 pamoja na wafalme na washauri wa dunia, \q2 waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu, \q1 \v 15 pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu, \q2 waliozijaza nyumba zao kwa fedha. \q1 \v 16 Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu, \q2 kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga? \q1 \v 17 Huko waovu huacha kusumbua \q2 na huko waliochoka hupumzika. \q1 \v 18 Wafungwa nao hufurahia utulivu wao, \q2 hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa. \q1 \v 19 Wadogo na wakubwa wamo humo, \q2 na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake. \b \q1 \v 20 “Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni, \q2 na hao wenye uchungu kupewa uhai, \q1 \v 21 wale wanaotamani kifo ambacho hakiji, \q2 wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa, \q1 \v 22 ambao hujawa na furaha, \q2 na hushangilia wafikapo kaburini? \q1 \v 23 Kwa nini uhai hupewa mtu \q2 ambaye njia yake imefichika, \q2 ambaye Mungu amemzungushia boma? \q1 \v 24 Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula; \q2 kusononeka kwangu kunamwagika kama maji. \q1 \v 25 Lile nililokuwa naliogopa limenijia; \q2 lile nililokuwa ninalihofia limenipata. \q1 \v 26 Sina amani, wala utulivu; \q2 sina pumziko, bali taabu tu.” \c 4 \s1 Elifazi Anazungumza: Ayubu Ametenda Dhambi \p \v 1 Ndipo Elifazi Mtemani akajibu: \q1 \v 2 “Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe, \q2 kutakukasirisha? \q1 Lakini ni nani awezaye \q2 kujizuia asiseme? \q1 \v 3 Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi, \q2 jinsi ambavyo umeitia nguvu \q2 mikono iliyokuwa dhaifu. \q1 \v 4 Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa; \q2 umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu. \q1 \v 5 Lakini sasa hii taabu imekujia wewe, \q2 nawe unashuka moyo; \q1 imekupiga wewe, \q2 nawe unafadhaika. \q1 \v 6 Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa \q2 ndiyo matumaini yako \q1 na njia zako kutokuwa na lawama \q2 ndilo taraja lako? \b \q1 \v 7 “Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? \q2 Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa? \q1 \v 8 Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza, \q2 wale walimao ubaya \q1 na wale hupanda uovu, \q2 huvuna hayo hayo hayo. \q1 \v 9 Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; \q2 kwa mshindo wa hasira zake huangamia. \q1 \v 10 Simba anaweza kunguruma na kukoroma, \q2 lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika. \q1 \v 11 Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo, \q2 nao wana wa simba jike hutawanyika. \b \q1 \v 12 “Neno lililetwa kwangu kwa siri, \q2 masikio yangu yakasikia mnongʼono wake. \q1 \v 13 Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku, \q2 hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu, \q1 \v 14 hofu na kutetemeka kulinishika \q2 na kufanya mifupa yangu yote itetemeke. \q1 \v 15 Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu, \q2 nazo nywele za mwili wangu zikasimama. \q1 \v 16 Yule roho akasimama, \q2 lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani. \q1 Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu, \q2 kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti: \q1 \v 17 ‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu? \q2 Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake? \q1 \v 18 Kama Mungu hawaamini watumishi wake, \q2 kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea, \q1 \v 19 ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba \q2 za udongo wa mfinyanzi, \q1 ambazo misingi yake ipo mavumbini, \q2 ambao wamepondwa kama nondo! \q1 \v 20 Kati ya mawio na machweo \q2 huvunjwa vipande vipande; \q1 bila yeyote kutambua, \q2 huangamia milele. \q1 \v 21 Je, kamba za hema yao hazikungʼolewa, \q2 hivyo hufa bila hekima?’ \c 5 \s1 Elifazi Anaendelea \q1 \v 1 “Ita kama unataka, lakini ni nani atakayekujibu? \q2 Ni yupi kati ya hao watakatifu utakayemgeukia? \q1 \v 2 Kuweka uchungu moyoni humuua mpumbavu, \q2 nao wivu humchinja mjinga. \q1 \v 3 Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akistawi, \q2 lakini ghafula nyumba yake ikawa imelaaniwa. \q1 \v 4 Watoto wake wako mbali na usalama, \q2 hushindwa mahakamani bila mtetezi. \q1 \v 5 Wenye njaa huyala mavuno yake, \q2 wakiyatoa hata katikati ya miiba, \q2 nao wenye kiu huitamani sana mali yake. \q1 \v 6 Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo, \q2 wala udhia hauchipui kutoka ardhini. \q1 \v 7 Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, \q2 kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu. \b \q1 \v 8 “Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, \q2 ningeliweka shauri langu mbele zake. \q1 \v 9 Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, \q2 miujiza isiyoweza kuhesabika. \q1 \v 10 Yeye huipa nchi mvua, \q2 huyapeleka maji kunyesha mashamba. \q1 \v 11 Huwainua juu wanyonge, \q2 nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama. \q1 \v 12 Huipinga mipango ya wenye hila, \q2 ili mikono yao isifikie ufanisi. \q1 \v 13 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, \q2 nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali. \q1 \v 14 Giza huwapata wakati wa mchana; \q2 wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku. \q1 \v 15 Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao; \q2 huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu. \q1 \v 16 Kwa hiyo maskini analo tarajio, \q2 nao udhalimu hufumba kinywa chake. \b \q1 \v 17 “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; \q2 kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.\f + \fr 5:17 \ft Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania Shaddai (hapa na kila mahali katika kitabu hiki cha Ayubu).\f* \q1 \v 18 Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga; \q2 huumiza, lakini mikono yake pia huponya. \q1 \v 19 Kutoka majanga sita atakuokoa; \q2 naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe. \q1 \v 20 Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo, \q2 naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga. \q1 \v 21 Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi, \q2 wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia. \q1 \v 22 Utayacheka maangamizo na njaa, \q2 wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa \q2 wanyama wakali wa mwituni. \q1 \v 23 Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba, \q2 nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe. \q1 \v 24 Utajua ya kwamba hema lako li salama; \q2 utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua. \q1 \v 25 Utajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi, \q2 nao wazao wako wengi kama majani ya nchi. \q1 \v 26 Utaingia kaburini ukiwa na umri wa uzee mtimilifu, \q2 kama masuke ya ngano yakusanywapo kwa wakati wake. \b \q1 \v 27 “Tumelichunguza hili, nalo ni kweli. \q2 Hivyo lisikie na ulitendee kazi.” \c 6 \ms2 Hotuba Ya Pili Ya Ayubu \s1 Ayubu Anajibu: Malalamiko Yangu Ni Ya Haki \p \v 1 Kisha Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa, \q2 nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani! \q1 \v 3 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote, \q2 kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka. \q1 \v 4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, \q2 roho yangu inakunywa sumu yake; \q2 vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu. \q1 \v 5 Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani, \q2 au ngʼombe dume hulia akiwa na chakula? \q1 \v 6 Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi, \q2 au upo utamu katika ute mweupe wa yai? \q1 \v 7 Ninakataa kuvigusa; \q2 vyakula vya aina hii hunichukiza. \b \q1 \v 8 “Laiti ningepata haja yangu, \q2 kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia, \q1 \v 9 kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda, \q2 kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali! \q1 \v 10 Ndipo bado ningekuwa na hii faraja, \q2 furaha yangu katika maumivu makali: \q2 kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu. \b \q1 \v 11 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini? \q2 Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu? \q1 \v 12 Je, mimi nina nguvu za jiwe? \q2 Je, mwili wangu ni shaba? \q1 \v 13 Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe, \q2 wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami? \b \q1 \v 14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake, \q2 hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi. \q1 \v 15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa, \q2 ni kama vijito vya msimu, \q2 ni kama vijito ambavyo hufurika \q1 \v 16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo, \q2 ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka, \q1 \v 17 lakini hukauka majira ya ukame, \q2 na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake. \q1 \v 18 Misafara hugeuka kutoka njia zake; \q2 hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia. \q1 \v 19 Misafara ya Tema inatafuta maji, \q2 wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri \q2 hutazama kwa matarajio. \q1 \v 20 Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini; \q2 wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia. \q1 \v 21 Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote; \q2 mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa. \q1 \v 22 Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu, \q2 au mnilipie fidia kutoka mali zenu, \q1 \v 23 au niokoeni mikononi mwa adui, \q2 au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’? \b \q1 \v 24 “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya; \q2 nionyesheni nilikokosea. \q1 \v 25 Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli! \q2 Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini? \q1 \v 26 Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema, \q2 na kuyafanya maneno ya mtu anayekata tamaa kama upepo? \q1 \v 27 Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima, \q2 na kubadilishana rafiki yenu na mali. \b \q1 \v 28 “Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi. \q2 Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu? \q1 \v 29 Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu; \q2 angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu.\f + \fr 6:29 \ft Au: haki yangu bado inasimama.\f* \q1 \v 30 Je, pana uovu wowote midomoni mwangu? \q2 Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila? \c 7 \s1 Ayubu: Mateso Yangu Hayana Mwisho \q1 \v 1 “Je, mwanadamu hana kazi ngumu duniani? \q2 Siku zake si kama zile za mtu aliyeajiriwa? \q1 \v 2 Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni, \q2 au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake, \q1 \v 3 ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili, \q2 nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku. \q1 \v 4 Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ \q2 Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko. \q1 \v 5 Mwili wangu umevikwa mabuu na uchafu, \q2 ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha. \s1 Ayubu Anamlilia Mungu \q1 \v 6 “Siku zangu zinapita upesi kuliko mtande wa kufuma, \q2 nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini. \q1 \v 7 Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi; \q2 macho yangu kamwe hayataona tena raha. \q1 \v 8 Lile jicho linaloniona sasa halitaniona tena; \q2 utanitafuta, wala sitakuwepo. \q1 \v 9 Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, \q2 vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini\f + \fr 7:9 \ft Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.\f* harudi tena. \q1 \v 10 Kamwe harudi tena nyumbani mwake; \q2 wala mahali pake hapatamjua tena. \b \q1 \v 11 “Kwa hiyo sitanyamaza; \q2 nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, \q2 nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu. \q1 \v 12 Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini, \q2 hata uniweke chini ya ulinzi? \q1 \v 13 Ninapofikiri kwamba kitanda changu kitanifariji, \q2 nacho kiti changu cha fahari kitapunguza malalamiko yangu, \q1 \v 14 ndipo wanitisha kwa ndoto \q2 na kunitia hofu kwa maono, \q1 \v 15 hivyo ninachagua kujinyonga na kufa, \q2 kuliko huu mwili wangu. \q1 \v 16 Ninayachukia maisha yangu; nisingetamani kuendelea kuishi. \q2 Niache; siku zangu ni ubatili. \b \q1 \v 17 “Mwanadamu ni kitu gani hata umjali kiasi hiki, \q2 kwamba unamtia sana maanani, \q1 \v 18 kwamba unamwangalia kila asubuhi \q2 na kumjaribu kila wakati? \q1 \v 19 Je, hutaacha kamwe kunitazama, \q2 au kuniacha japo kwa kitambo kidogo tu? \q1 \v 20 Ikiwa nimetenda dhambi, nimekufanyia nini, \q2 Ewe mlinzi wa wanadamu? \q1 Kwa nini umeniweka niwe shabaha yako? \q2 Je, nimekuwa mzigo kwako? \q1 \v 21 Kwa nini husamehi makosa yangu \q2 na kuachilia dhambi zangu? \q1 Kwa kuwa hivi karibuni nitalala mavumbini; \q2 nawe utanitafuta, wala sitakuwepo.” \c 8 \s1 Bildadi Anasema: Yampasa Ayubu Atubu \p \v 1 Kisha Bildadi Mshuhi akajibu: \q1 \v 2 “Hata lini wewe utasema mambo kama haya? \q2 Maneno yako ni kama upepo mkuu. \q1 \v 3 Je, Mungu hupotosha hukumu? \q2 Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki? \q1 \v 4 Watoto wako walipomtenda dhambi, \q2 aliwapa adhabu ya dhambi yao. \q1 \v 5 Lakini ukimtafuta Mungu, \q2 nawe ukamsihi Mwenyezi, \q1 \v 6 ikiwa wewe ni safi na mnyofu, \q2 hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, \q2 na kukurudisha katika mahali pako pa haki. \q1 \v 7 Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, \q2 lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio. \b \q1 \v 8 “Ukaulize vizazi vilivyotangulia \q2 na uone baba zao walijifunza nini, \q1 \v 9 kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, \q2 nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu. \q1 \v 10 Je, hawatakufundisha na kukueleza? \q2 Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao? \q1 \v 11 Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope? \q2 Matete yaweza kustawi bila maji? \q1 \v 12 Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa, \q2 hunyauka haraka kuliko majani mengine. \q1 \v 13 Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; \q2 vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia. \q1 \v 14 Lile analolitumainia huvunjika upesi; \q2 lile analolitegemea ni utando wa buibui. \q1 \v 15 Huutegemea utando wake, lakini hausimami; \q2 huungʼangʼania, lakini haudumu. \q1 \v 16 Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua, \q2 ukieneza machipukizi yake bustanini; \q1 \v 17 huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, \q2 na kutafuta nafasi katikati ya mawe. \q1 \v 18 Unapongʼolewa kutoka mahali pake, \q2 ndipo mahali pale huukana na kusema, \q2 ‘Mimi kamwe sikukuona.’ \q1 \v 19 Hakika uhai wake hunyauka, \q2 na kutoka udongoni mimea mingine huota. \b \q1 \v 20 “Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia, \q2 wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya. \q1 \v 21 Bado atakijaza kinywa chako na kicheko, \q2 na midomo yako na kelele za shangwe. \q1 \v 22 Adui zako watavikwa aibu, \q2 nazo hema za waovu hazitakuwepo tena.” \c 9 \ms2 Hotuba Ya Tatu Ya Ayubu \s1 Hakuna Mpatanishi \p \v 1 Kisha Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Naam, najua hili ni kweli. \q2 Lakini mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? \q1 \v 3 Ingawa mtu angetaka kushindana naye, \q2 asingaliweza kumjibu Mungu hata mara moja miongoni mwa elfu moja. \q1 \v 4 Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. \q2 Ni nani aliyempinga naye akawa salama? \q1 \v 5 Aiondoa milima bila yenyewe kujua \q2 na kuipindua kwa hasira yake. \q1 \v 6 Aitikisa dunia kutoka mahali pake \q2 na kuzifanya nguzo zake zitetemeke. \q1 \v 7 Husema na jua, nalo likaacha kuangaza; \q2 naye huizima mianga ya nyota. \q1 \v 8 Yeye peke yake huzitandaza mbingu \q2 na kuyakanyaga mawimbi ya bahari. \q1 \v 9 Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu,\f + \fr 9:9 \ft Nyota za Dubu hapa ina maana ya kundi la nyota za kaskazini, ambazo zinaitwa kwa jina la Dubu Mkuu.\f* na Orioni,\f + \fr 9:9 \ft Orioni ni kundi la nyota kubwa.\f* \q2 Kilimia,\f + \fr 9:9 \ft Kilimia ni jina lililopewa nyota saba (Taurus).\f* na makundi ya nyota za kusini. \q1 \v 10 Hutenda maajabu yasiyopimika, \q2 miujiza isiyoweza kuhesabiwa. \q1 \v 11 Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; \q2 apitapo mbele yangu, simtambui. \q1 \v 12 Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia? \q2 Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’ \q1 \v 13 Mungu hataizuia hasira yake; \q2 hata jeshi kubwa la Rahabu\f + \fr 9:13 \ft Rahabu hapa ina maana ya Misri kwa fumbo.\f* lenye nguvu \q2 linajikunyata miguuni pake. \b \q1 \v 14 “Ni vipi basi mimi nitaweza kubishana naye? \q2 Nawezaje kupata maneno ya kuhojiana naye? \q1 \v 15 Ingawa sikuwa na hatia, sikuweza kumjibu; \q2 ningeweza tu kumsihi Mhukumu wangu anihurumie. \q1 \v 16 Hata kama ningemwita kwenye shauri, naye akakubali, \q2 siamini kama angenisikiliza. \q1 \v 17 Yeye angeniangamiza kwa dhoruba \q2 na kuongeza majeraha yangu pasipo na sababu. \q1 \v 18 Asingeniacha nipumue \q2 bali angenifunika kabisa na huzuni kuu. \q1 \v 19 Kama ni suala la nguvu, yeye ni mwenye nguvu! \q2 Kama ni suala la haki, ni nani awezaye kumwita mahakamani? \q1 \v 20 Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; \q2 kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia. \b \q1 \v 21 “Ingawa mimi sina kosa, \q2 haileti tofauti katika nafsi yangu; \q2 nauchukia uhai wangu. \q1 \v 22 Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema, \q2 ‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’ \q1 \v 23 Wakati pigo liletapo kifo cha ghafula, \q2 yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa. \q1 \v 24 Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu, \q2 yeye huwafunga macho mahakimu wake. \q2 Kama si yeye, basi ni nani? \b \q1 \v 25 “Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji; \q2 zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo. \q1 \v 26 Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo, \q2 mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula. \q1 \v 27 Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu, \q2 nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’ \q1 \v 28 bado ninahofia mateso yangu yote, \q2 kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia. \q1 \v 29 Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia, \q2 kwa nini basi nitaabishwe bure? \q1 \v 30 Hata kama ningejiosha kwa sabuni \q2 na kutakasa mikono yangu kwa magadi, \q1 \v 31 wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi \q2 kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana. \b \q1 \v 32 “Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu, \q2 ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani. \q1 \v 33 Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu, \q2 aweke mkono wake juu yetu sote wawili, \q1 \v 34 mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu, \q2 ili utisho wake usiendelee kunitia hofu. \q1 \v 35 Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa, \q2 lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza. \b \c 10 \s1 Ayubu: Nayachukia Maisha Yangu \q1 \v 1 “Nayachukia sana haya maisha yangu; \q2 kwa hiyo nitatoa malalamiko yangu kwa wazi bila kujizuia, \q2 nami nitanena kutokana na uchungu wa moyo wangu. \q1 \v 2 Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, \q2 bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu. \q1 \v 3 Je, inakupendeza wewe kunionea, \q2 kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, \q2 huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu? \q1 \v 4 Je, wewe una macho ya kimwili? \q2 Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo? \q1 \v 5 Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, \q2 au miaka yako ni kama ile ya mtu, \q1 \v 6 ili kwamba utafute makosa yangu \q2 na kuichunguza dhambi yangu; \q1 \v 7 ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, \q2 na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako? \b \q1 \v 8 “Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. \q2 Je, sasa utageuka na kuniangamiza? \q1 \v 9 Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. \q2 Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena? \q1 \v 10 Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa, \q2 na kunigandisha kama jibini, \q1 \v 11 ukanivika ngozi na nyama, \q2 na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa? \q1 \v 12 Umenipa uhai na kunitendea wema, \q2 katika uangalizi wako umeilinda roho yangu. \b \q1 \v 13 “Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, \q2 nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako: \q1 \v 14 Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, \q2 wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa. \q1 \v 15 Kama nina hatia, ole wangu! \q2 Hata kama ningekuwa sina hatia, \q2 siwezi kukiinua kichwa changu, \q1 kwa kuwa nimejawa na aibu, \q2 na kuzama katika mateso yangu. \q1 \v 16 Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, \q2 na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu. \q1 \v 17 Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu \q2 na kuzidisha hasira yako juu yangu; \q2 nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine. \b \q1 \v 18 “Kwa nini basi ulinitoa tumboni? \q2 Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona. \q1 \v 19 Laiti nisingekuwako kamwe, \q2 au ningekuwa nimechukuliwa moja kwa moja \q2 kutoka tumboni kwenda kaburini! \q1 \v 20 Je, siku zangu chache si zimekaribia kuisha? \q2 Niachie ili niweze kupata muda mfupi wa kufurahi \q1 \v 21 kabla sijaenda mahali ambapo hakuna kurudi tena, \q2 katika nchi ya giza na uvuli wa mauti, \q1 \v 22 nchi ya giza kuu sana, \q2 yenye uvuli wa giza na machafuko, \q2 mahali ambapo hata nuru ni giza.” \c 11 \s1 Sofari Anasema: Hatia Ya Ayubu Inastahili Adhabu \p \v 1 Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu: \q1 \v 2 “Je, maneno haya yote yapite bila kujibiwa? \q2 Je, huyu mnenaji athibitishwe kuwa na haki? \q1 \v 3 Je, maneno yako ya upuzi yawafanye watu wanyamaze kimya? \q2 Je, mtu asikukemee unapofanya dhihaka? \q1 \v 4 Unamwambia Mungu, ‘Imani yangu ni kamili \q2 nami ni safi mbele zako.’ \q1 \v 5 Aha! Laiti kwamba Mungu angesema, \q2 kwamba angefungua midomo yake dhidi yako, \q1 \v 6 naye akufunulie siri za hekima, \q2 kwa kuwa hekima ya kweli ina pande mbili. \q2 Ujue hili: Mungu amesahau hata baadhi ya dhambi zako. \b \q1 \v 7 “Je, waweza kujua siri za Mungu? \q2 Je, waweza kuyachunguza mambo yote kumhusu Mwenyezi? \q1 \v 8 Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? \q2 Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: \q2 wewe waweza kujua nini? \q1 \v 9 Kipimo chake ni kirefu kuliko dunia, \q2 nacho ni kipana kuliko bahari. \b \q1 \v 10 “Kama akija na kukufunga gerezani, \q2 na kuitisha mahakama, ni nani awezaye kumpinga? \q1 \v 11 Hakika anawatambua watu wadanganyifu; \q2 naye aonapo uovu, je, haangalii? \q1 \v 12 Mpumbavu aweza kuwa mwenye hekima, \q2 endapo mtoto wa punda-mwitu atazaliwa mwanadamu. \b \q1 \v 13 “Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake \q2 na kumwinulia mikono yako, \q1 \v 14 ukiiondolea mbali ile dhambi iliyo mkononi mwako \q2 wala usiuruhusu uovu ukae hemani mwako, \q1 \v 15 ndipo utainua uso wako bila aibu; \q2 utasimama imara bila hofu. \q1 \v 16 Hakika utaisahau taabu yako, \q2 utaikumbuka tu kama maji yaliyokwisha kupita. \q1 \v 17 Maisha yako yatangʼaa kuliko adhuhuri, \q2 nalo giza litakuwa kama alfajiri. \q1 \v 18 Utakuwa salama, kwa kuwa lipo tumaini; \q2 utatazama pande zote na kupumzika kwa salama. \q1 \v 19 Utalala, wala hakuna atakayekuogofya, \q2 naam, wengi watajipendekeza kwako. \q1 \v 20 Bali macho ya waovu hayataona, \q2 wokovu utawaepuka; \q1 tarajio lao litakuwa ni hangaiko \q2 la mtu anayekata roho.” \c 12 \ms2 Hotuba Ya Nne Ya Ayubu \s1 Ayubu Anajibu: Mimi Ni Mtu Wa Kuchekwa \p \v 1 Ndipo Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Bila shaka ninyi ndio watu, \q2 nayo hekima itakoma mtakapokufa! \q1 \v 3 Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi; \q2 mimi si duni kwenu. \q2 Ni nani asiyejua mambo haya yote? \b \q1 \v 4 “Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu, \q2 ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu: \q1 mimi ni mtu wa kuchekwa tu, \q2 ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia! \q1 \v 5 Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba \q1 kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza. \q1 \v 6 Hema za wanyangʼanyi hazisumbuliwi, \q2 wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: \q2 wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao. \b \q1 \v 7 “Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, \q2 au ndege wa angani, nao watawaambia; \q1 \v 8 au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, \q2 au acheni samaki wa baharini wawape taarifa. \q1 \v 9 Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua \q2 kwamba mkono wa \nd Bwana\nd* ndio uliofanya hili? \q1 \v 10 Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, \q2 na pumzi ya wanadamu wote. \q1 \v 11 Je, sikio haliyajaribu maneno \q2 kama vile ulimi uonjavyo chakula? \q1 \v 12 Je, hekima haipatikani katikati ya wazee? \q2 Je, maisha marefu hayaleti ufahamu? \b \q1 \v 13 “Hekima na nguvu ni vya Mungu; \q2 shauri na ufahamu ni vyake yeye. \q1 \v 14 Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; \q2 mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa. \q1 \v 15 Akizuia maji, huwa pana ukame; \q2 akiyaachia maji, huharibu nchi. \q1 \v 16 Kwake kuna nguvu na ushindi; \q2 adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake. \q1 \v 17 Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, \q2 naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi. \q1 \v 18 Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, \q2 na kuwafunga mishipi ya kiunoni. \q1 \v 19 Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, \q2 na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu. \q1 \v 20 Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, \q2 na kuondoa busara ya wazee. \q1 \v 21 Huwamwagia dharau wanaoheshimika, \q2 na kuwavua silaha wenye nguvu. \q1 \v 22 Hufunua mambo ya ndani ya gizani, \q2 na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana. \q1 \v 23 Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; \q2 hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya. \q1 \v 24 Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao; \q2 huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia. \q1 \v 25 Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga; \q2 huwafanya wapepesuke kama walevi. \b \c 13 \q1 \v 1 “Macho yangu yameona hili lote, \q2 masikio yangu yamesikia na kulielewa. \q1 \v 2 Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; \q2 mimi si mtu duni kuliko ninyi. \q1 \v 3 Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi \q2 na kuhojiana shauri langu na Mungu. \q1 \v 4 Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; \q2 ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! \q1 \v 5 Laiti wote mngenyamaza kimya! \q2 Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima. \q1 \v 6 Sikieni sasa hoja yangu; \q2 sikilizeni kusihi kwangu. \q1 \v 7 Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? \q2 Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake? \q1 \v 8 Mtamwonyesha upendeleo? \q2 Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake? \q1 \v 9 Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? \q2 Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu? \q1 \v 10 Hakika angewakemea \q2 kama mkiwapendelea watu kwa siri. \q1 \v 11 Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? \q2 Je, hofu yake isingewaangukia ninyi? \q1 \v 12 Maneno yenu ni mithali za majivu; \q2 utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi. \b \q1 \v 13 “Nyamazeni kimya nipate kusema; \q2 kisha na yanipate yatakayonipata. \q1 \v 14 Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari \q2 na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu? \q1 \v 15 Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; \q2 hakika nitazitetea njia zangu mbele zake. \q1 \v 16 Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, \q2 kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu \q2 atakayethubutu kuja mbele yake! \q1 \v 17 Sikilizeni maneno yangu kwa makini; \q2 nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho. \q1 \v 18 Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, \q2 ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki. \q1 \v 19 Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? \q2 Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife. \b \q1 \v 20 “Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, \q2 nami sitajificha uso wako: \q1 \v 21 Ondoa mkono wako uwe mbali nami, \q2 nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu. \q1 \v 22 Niite kwenye shauri nami nitajibu, \q2 au niache niseme, nawe upate kujibu. \q1 \v 23 Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? \q2 Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu. \q1 \v 24 Kwa nini kuuficha uso wako \q2 na kunihesabu mimi kuwa adui yako? \q1 \v 25 Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? \q2 Je, utayasaka makapi makavu? \q1 \v 26 Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu \q2 na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu. \q1 \v 27 Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. \q2 Unazichunga kwa makini njia zangu zote \q2 kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu. \b \q1 \v 28 “Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, \q2 kama vazi lililoliwa na nondo. \b \c 14 \q1 \v 1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke \q2 siku zake ni chache nazo zimejaa taabu. \q1 \v 2 Huchanua kama ua kisha hunyauka; \q2 huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu. \q1 \v 3 Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? \q2 Je, utamleta mbele yako katika hukumu? \q1 \v 4 Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi? \q2 Hakuna awezaye! \q1 \v 5 Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka; \q2 umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake \q2 na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka. \q1 \v 6 Hivyo angalia mbali umwache, \q2 hadi awe amekamilisha muda wake \q2 kama mtu aliyeajiriwa. \b \q1 \v 7 “Kwa maana lipo tumaini kwa mti; \q2 kama ukikatwa utachipuka tena, \q2 nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. \q1 \v 8 Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini \q2 na kisiki chake kufa udongoni, \q1 \v 9 lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua \q2 na kutoa machipukizi kama mche. \q1 \v 10 Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake; \q2 hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena! \q1 \v 11 Kama vile maji yatowekavyo katika bahari, \q2 au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu, \q1 \v 12 ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke; \q2 hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena, \q1 wanadamu hawataamka au kuamshwa \q2 kutoka kwenye usingizi wao. \b \q1 \v 13 “Laiti kama ungenificha kaburini,\f + \fr 14:13 \ft Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.\f* \q2 na kunisitiri hadi hasira yako ipite! \q1 Laiti ungeniwekea wakati, \q2 na kisha ukanikumbuka! \q1 \v 14 Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? \q2 Siku zote za kazi zangu ngumu \q2 nitangojea kufanywa upya kwangu. \q1 \v 15 Utaniita nami nitakuitika; \q2 utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba. \q1 \v 16 Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, \q2 lakini hutazifuatia dhambi zangu. \q1 \v 17 Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko, \q2 nawe utazifunika dhambi zangu. \b \q1 \v 18 “Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika \q2 na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake, \q1 \v 19 kama maji yamalizavyo mawe, \q2 na mafuriko yachukuavyo udongo, \q2 ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu. \q1 \v 20 Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka; \q2 waibadilisha sura yake na kumwondoa. \q1 \v 21 Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu; \q2 kama wakidharauliwa, yeye haoni. \q1 \v 22 Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe, \q2 naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.” \c 15 \s1 Elifazi Anaongea: Ayubu Anadhoofisha Imani \p \v 1 Kisha Elifazi Mtemani akajibu: \q1 \v 2 “Je, mtu mwenye hekima hujibu kwa mawazo matupu, \q2 au kujaza tumbo lake kwa upepo wenye joto wa mashariki? \q1 \v 3 Je, aweza kubishana juu ya maneno yasiyofaa, \q2 kwa hotuba zisizo na maana? \q1 \v 4 Lakini unadhoofisha hata uchaji wa Mungu \q2 na kuzuia ibada mbele za Mungu. \q1 \v 5 Dhambi yako inasukuma kinywa chako, \q2 nawe umechagua ulimi wa hila. \q1 \v 6 Kinywa chako mwenyewe kinakuhukumu, wala si changu; \q2 midomo yako mwenyewe inashuhudia dhidi yako. \b \q1 \v 7 “Je, wewe ni mtu wa kwanza kuzaliwa? \q2 Ulizaliwa kabla ya vilima? \q1 \v 8 Je, wewe husikiliza mashauri ya siri ya Mungu? \q2 Je, wewe unaizuia hekima iwe yako mwenyewe? \q1 \v 9 Wewe unajua kitu gani tusichokijua sisi? \q2 Unafahamu kitu gani tusichokifahamu sisi? \q1 \v 10 Wale wenye mvi na wazee wako upande wetu, \q2 watu ambao ni wazee hata kuliko baba yako. \q1 \v 11 Je, faraja za Mungu hazikutoshi, \q2 au maneno yaliyosemwa kwako kwa upole si kitu? \q1 \v 12 Kwa nini moyo wako unakudanganya, \q2 na kwa nini macho yako yanangʼaa, \q1 \v 13 ili kwamba upate kutoa hasira yako dhidi ya Mungu, \q2 na kumwaga maneno kama hayo kutoka kinywani mwako? \b \q1 \v 14 “Mwanadamu ni kitu gani, hata aweze kuwa safi, \q2 au yeye aliyezaliwa na mwanamke, hata aweze kuwa mwadilifu? \q1 \v 15 Kama Mungu hawaamini watakatifu wake, \q2 kama hata mbingu zenyewe si safi machoni pake, \q1 \v 16 sembuse mwanadamu ambaye ni mwovu na mpotovu, \q2 ambaye hunywa uovu kama anywavyo maji! \b \q1 \v 17 “Nisikilize mimi nami nitakueleza, \q2 acha nikuambie yale niliyoyaona, \q1 \v 18 ambayo watu wenye hekima wameyanena, \q2 bila kuficha lolote walilopokea toka kwa baba zao \q1 \v 19 (wakati ambao wao peke yao ndio walipewa nchi, \q2 hakuna mgeni aliyepita miongoni mwao): \q1 \v 20 Mtu mwovu siku zake zote hupata mateso, \q2 miaka yote aliwekewa mkorofi. \q1 \v 21 Sauti za kutisha hujaa masikioni mwake; \q2 katika kufanikiwa kwake, wanyangʼanyi humshambulia. \q1 \v 22 Hukata tamaa kuokoka gizani; \q2 amewekwa kwa ajili ya upanga. \q1 \v 23 Hutangatanga, akitafuta chakula; \q2 anajua kwamba siku ya giza iko karibu. \q1 \v 24 Taabu na maumivu makuu vinamtia hofu; \q2 humshinda kama mfalme aliye tayari kwa vita, \q1 \v 25 kwa sababu amemkunjia Mungu ngumi yake \q2 na kujigamba dhidi ya Mwenyezi, \q1 \v 26 kwa kiburi akishambulia dhidi ya Mungu \q2 akiwa na ngao nene, iliyo imara. \b \q1 \v 27 “Ingawa uso wake umefunikwa na mafuta kwa unene \q2 na kiuno chake kimevimba kwa kunenepa, \q1 \v 28 ataishi katika miji ya magofu, \q2 na katika nyumba ambazo haziishi mwanadamu yeyote, \q2 nyumba zinazokuwa vifusi. \q1 \v 29 Hatatajirika tena, nao utajiri wake hautadumu, \q2 wala mali zake hazitakuwa nyingi juu ya nchi. \q1 \v 30 Hatatoka gizani; \q2 mwali wa moto utanyausha machipukizi yake, \q2 nayo pumzi ya kinywa cha Mungu itamwondolea mbali. \q1 \v 31 Asijidanganye mwenyewe kutumainia ubatili, \q2 kwa kuwa hatapata malipo yoyote. \q1 \v 32 Atakuwa amelipwa kikamilifu kabla ya wakati wake, \q2 nayo matawi yake hayatastawi. \q1 \v 33 Atafanana na mzabibu uliopukutishwa matunda yake kabla hayajaiva, \q2 kama mzeituni unaodondosha maua yake. \q1 \v 34 Kwa kuwa jamii ya wasiomcha Mungu watakuwa tasa, \q2 nao moto utateketeza hema za wale wanaopenda rushwa. \q1 \v 35 Hutunga mimba ya madhara na kuzaa uovu; \q2 matumbo yao huumba udanganyifu.” \c 16 \ms2 Hotuba Ya Tano Ya Ayubu \s1 Ayubu Anathibitisha Tena Hali Yake Ya Kutokuwa Na Hatia \p \v 1 Kisha Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, \q2 nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha! \q1 \v 3 Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? \q2 Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno? \q1 \v 4 Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, \q2 kama mngekuwa katika hali yangu; \q1 ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, \q2 na kuwatikisia ninyi kichwa changu. \q1 \v 5 Lakini kinywa changu kingewatia moyo; \q2 faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu. \b \q1 \v 6 “Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; \q2 nami kama nikijizuia, wala hayaondoki. \q1 \v 7 Ee Mungu, hakika umenichakaza; \q2 umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote. \q1 \v 8 Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi; \q2 nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu. \q1 \v 9 Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, \q2 na kunisagia meno yake; \q2 adui yangu hunikazia macho yake makali. \q1 \v 10 Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; \q2 hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, \q2 na kuungana pamoja dhidi yangu. \q1 \v 11 Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, \q2 na kunitupa katika makucha ya waovu. \q1 \v 12 Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; \q2 amenikamata shingo na kuniponda. \q2 Amenifanya mimi kuwa shabaha yake; \q1 \v 13 wapiga upinde wake wananizunguka. \q2 Bila huruma, huchoma figo zangu, \q2 na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi. \q1 \v 14 Huniponda tena na tena; \q2 hunishambulia kama shujaa wa vita. \b \q1 \v 15 “Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu \q2 nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi. \q1 \v 16 Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, \q2 macho yangu yamepigwa na giza kuu. \q1 \v 17 Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, \q2 na maombi yangu ni safi. \b \q1 \v 18 “Ee nchi, usiifunike damu yangu, \q2 nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe. \q1 \v 19 Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni; \q2 wakili wangu yuko juu. \q1 \v 20 Mwombezi wangu ni rafiki yangu \q2 macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu; \q1 \v 21 kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu \q2 kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake. \b \q1 \v 22 “Ni miaka michache tu itapita \q2 kabla sijaenda safari ambayo sitarudi. \c 17 \q1 \v 1 Moyo wangu umevunjika, \q2 siku zangu zimefupishwa, \q2 kaburi linaningojea. \q1 \v 2 Hakika wenye mizaha wamenizunguka; \q2 macho yangu yamebaki kutazama uadui wao. \s1 Ayubu Anaomba Msaada \q1 \v 3 “Ee Mungu, nipe dhamana unayodai. \q2 Ni nani mwingine atakayeweka dhamana kwa ajili yangu? \q1 \v 4 Umezifunga akili zao zisipate ufahamu, \q2 kwa hiyo hutawaacha wapate ushindi. \q1 \v 5 Kama mtu akiwashutumu rafiki zake ili apate ujira, \q2 macho ya watoto wake yatashindwa kuona. \b \q1 \v 6 “Mungu amenifanya kitu cha dhihaka kwa kila mtu, \q2 mtu ambaye watu humtemea mate usoni. \q1 \v 7 Macho yangu yamefifia kwa ajili ya majonzi; \q2 umbile langu lote ni kama kivuli. \q1 \v 8 Watu wanyofu wanatishwa na hili; \q2 watu wasio na hatia wanasimama dhidi ya wasiomcha Mungu. \q1 \v 9 Hata hivyo, waadilifu watazishika njia zao, \q2 nao wale wenye mikono safi wataendelea kupata nguvu. \b \q1 \v 10 “Lakini ninyi njooni, ninyi nyote, jaribuni tena! \q2 Sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu. \q1 \v 11 Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika, \q2 vivyo hivyo shauku za moyo wangu. \q1 \v 12 Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana, \q2 kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’ \q1 \v 13 Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi,\f + \fr 17:13 \ft Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.\f* \q2 kama nikikitandika kitanda changu gizani, \q1 \v 14 kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’ \q2 na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’ \q1 \v 15 liko wapi basi tarajio langu? \q2 Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu? \q1 \v 16 Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti?\f + \fr 17:16 \ft Malango ya mauti hapa ina maana ya Kuzimu.\f* \q2 Je, tutashuka pamoja mavumbini?” \c 18 \s1 Bildadi Anasema: Mungu Huwaadhibu Waovu \p \v 1 Bildadi Mshuhi akajibu: \q1 \v 2 “Je, ni lini utafika mwisho wa maneno haya? \q2 Uwe mwenye busara, nasi ndipo tutakapoweza kuongea. \q1 \v 3 Kwa nini sisi tunafikiriwa kama wanyama, \q2 na kuonekana wajinga machoni pako? \q1 \v 4 Wewe unayejirarua mwenyewe vipande vipande \q2 katika hasira yako, \q1 je, dunia iachwe kwa ajili yako wewe? \q2 Au ni lazima miamba iondolewe mahali pake? \b \q1 \v 5 “Taa ya mwovu imezimwa, \q2 nao mwali wa moto wake umezimika. \q1 \v 6 Mwanga hemani mwake umekuwa giza; \q2 taa iliyo karibu naye imezimika. \q1 \v 7 Nguvu za hatua zake zimedhoofishwa; \q2 shauri lake baya litamwangusha. \q1 \v 8 Miguu yake imemsukumia kwenye wavu, \q2 naye anatangatanga kwenye matundu ya wavu. \q1 \v 9 Tanzi litamkamata kwenye kisigino; \q2 mtego utamshikilia kwa nguvu. \q1 \v 10 Kitanzi kimefichwa ardhini kwa ajili yake; \q2 mtego uko kwenye njia yake. \q1 \v 11 Vitisho vimemtia hofu kila upande, \q2 na adui zake humwandama kila hatua. \q1 \v 12 Janga linamwonea shauku; \q2 maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo. \q1 \v 13 Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; \q2 mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake. \q1 \v 14 Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, \q2 na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho. \q1 \v 15 Moto utakaa katika hema lake; \q2 moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake. \q1 \v 16 Mizizi yake chini itakauka \q2 na matawi yake juu yatanyauka. \q1 \v 17 Kumbukumbu lake litatoweka katika dunia, \q2 wala hatakuwa na jina katika nchi. \q1 \v 18 Ameondolewa nuruni na kusukumiwa gizani, \q2 naye amefukuzwa mbali atoke duniani. \q1 \v 19 Hana mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake, \q2 wala aliyenusurika mahali alipoishi. \q1 \v 20 Watu wa magharibi watashangaa yaliyompata; \q2 watu wa mashariki watapatwa na hofu. \q1 \v 21 Hakika ndivyo yalivyo makao ya mtu mwovu; \q2 ndivyo palivyo mahali pake mtu asiyemjua Mungu.” \c 19 \ms2 Hotuba Ya Sita Ya Ayubu \s1 Ayubu Anajibu: Najua Mkombozi Wangu Yu Hai \p \v 1 Ndipo Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini, \q2 na kuniponda kwa maneno yenu? \q1 \v 3 Mara kumi hizi mmenishutumu; \q2 bila aibu mnanishambulia. \q1 \v 4 Kama ni kweli nimepotoka, \q2 kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe. \q1 \v 5 Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu, \q2 na kutumia unyonge wangu dhidi yangu, \q1 \v 6 basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya, \q2 naye amekokota wavu wake kunizunguka. \b \q1 \v 7 “Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu; \q2 ingawa ninaomba msaada, hakuna haki. \q1 \v 8 Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita; \q2 ameyafunika mapito yangu na giza. \q1 \v 9 Amenivua heshima yangu, \q2 na kuniondolea taji kichwani pangu. \q1 \v 10 Amenibomoa kila upande hadi nimeisha; \q2 amelingʼoa tegemeo langu kama mti. \q1 \v 11 Hasira yake imewaka juu yangu; \q2 amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake. \q1 \v 12 Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu; \q2 yamenizingira, \q2 yamepiga kambi kulizunguka hema langu. \b \q1 \v 13 “Amewatenga ndugu zangu mbali nami; \q2 wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa. \q1 \v 14 Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali; \q2 rafiki zangu wamenisahau. \q1 \v 15 Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni; \q2 wananitazama kama mgeni. \q1 \v 16 Namwita mtumishi wangu, wala haitiki, \q2 ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe. \q1 \v 17 Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu; \q2 nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe. \q1 \v 18 Hata watoto wadogo hunidhihaki; \q2 ninapojitokeza, hunifanyia mzaha. \q1 \v 19 Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa; \q2 wale niwapendao wamekuwa kinyume nami. \q1 \v 20 Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu; \q2 nimeponea nikiwa karibu kufa. \b \q1 \v 21 “Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma, \q2 kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga. \q1 \v 22 Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo? \q2 Hamtosheki kamwe na mwili wangu? \b \q1 \v 23 “Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu, \q2 laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu, \q1 \v 24 kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma, \q2 au kuyachonga juu ya mwamba milele! \q1 \v 25 Ninajua kwamba Mkombozi\f + \fr 19:25 \ft Au: Mtetezi.\f* wangu yu hai, \q2 naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi. \q1 \v 26 Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, \q2 bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu; \q1 \v 27 mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: \q2 mimi, wala si mwingine. \q2 Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana! \b \q1 \v 28 “Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda, \q2 maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’ \q1 \v 29 ninyi wenyewe uogopeni upanga, \q2 kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga, \q2 nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.” \c 20 \s1 Sofari Anasema: Uovu Hupokea Malipo Ya Haki \p \v 1 Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu: \q1 \v 2 “Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, \q2 kwa sababu nimehangaika sana. \q1 \v 3 Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima, \q2 nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu. \b \q1 \v 4 “Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, \q2 tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani, \q1 \v 5 macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, \q2 nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu. \q1 \v 6 Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni \q2 na kichwa chake hugusa mawingu, \q1 \v 7 ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. \q2 Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’ \q1 \v 8 Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, \q2 amefukuziwa mbali kama maono ya usiku. \q1 \v 9 Jicho lililomwona halitamwona tena; \q2 mahali pake hapatamwona tena. \q1 \v 10 Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, \q2 nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu. \q1 \v 11 Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, \q2 zitalala naye mavumbini. \b \q1 \v 12 “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake \q2 naye huuficha chini ya ulimi wake, \q1 \v 13 ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, \q2 lakini huuweka kinywani mwake. \q1 \v 14 Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, \q2 nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake. \q1 \v 15 Atatema mali alizozimeza; \q2 Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika. \q1 \v 16 Atanyonya sumu za majoka; \q2 meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua. \q1 \v 17 Hatafurahia vijito, \q2 mito inayotiririsha asali na siagi. \q1 \v 18 Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; \q2 hatafurahia faida itokanayo na biashara yake. \q1 \v 19 Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu; \q2 amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga. \b \q1 \v 20 “Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana; \q2 hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake. \q1 \v 21 Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; \q2 kufanikiwa kwake hakutadumu. \q1 \v 22 Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; \q2 taabu itamjia kwa nguvu zote. \q1 \v 23 Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, \q2 Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, \q2 na kumnyeshea mapigo juu yake. \q1 \v 24 Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, \q2 mshale wa shaba utamchoma. \q1 \v 25 Atauchomoa katika mgongo wake, \q2 ncha ingʼaayo kutoka ini lake. \q1 Vitisho vitakuja juu yake; \q2 \v 26 giza nene linavizia hazina zake. \q1 Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, \q2 na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake. \q1 \v 27 Mbingu zitaweka wazi hatia yake, \q2 nayo nchi itainuka kinyume chake. \q1 \v 28 Mafuriko yataichukua nyumba yake, \q2 maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu. \q1 \v 29 Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, \q2 urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.” \c 21 \ms2 Hotuba Ya Saba Ya Ayubu \s1 Ayubu Anajibu: Waovu Mara Nyingi Huenda Bila Kuadhibiwa \p \v 1 Ndipo Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Yasikilizeni maneno yangu kwa makini; \q2 hii na iwe faraja mnayonipa mimi. \q1 \v 3 Nivumilieni ninapozungumza, \q2 nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki. \b \q1 \v 4 “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? \q2 Kwa nini nisikose subira? \q1 \v 5 Niangalieni mkastaajabu; \q2 mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu. \q1 \v 6 Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa, \q2 nao mwili wangu unatetemeka. \q1 \v 7 Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, \q2 wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu? \q1 \v 8 Huwaona watoto wao wakithibitika \q2 wakiwa wamewazunguka, \q2 wazao wao mbele za macho yao. \q1 \v 9 Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; \q2 fimbo ya Mungu haiko juu yao. \q1 \v 10 Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe; \q2 ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba. \q1 \v 11 Huwatoa watoto wao nje kama kundi; \q2 wadogo wao huchezacheza. \q1 \v 12 Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, \q2 nao huifurahia sauti ya filimbi. \q1 \v 13 Huitumia miaka yao katika mafanikio \q2 nao hushuka kaburini kwa amani. \q1 \v 14 Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ \q2 Hatuna haja ya kufahamu njia zako. \q1 \v 15 Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? \q2 Tutapata faida gani kumwomba? \q1 \v 16 Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe, \q2 hivyo najitenga mbali na shauri la waovu. \b \q1 \v 17 “Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa? \q2 Ni mara ngapi maafa huwajia, \q1 yale yawapatayo ambayo Mungu \q2 huwapangia katika hasira yake? \q1 \v 18 Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo, \q2 kama makapi yachukuliwayo na dhoruba? \q1 \v 19 Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu \q2 kwa ajili ya wanawe.’ \q1 Mungu na amlipe mtu mwenyewe, \q2 ili apate kulijua! \q1 \v 20 Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake; \q2 yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi. \q1 \v 21 Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma, \q2 miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho? \b \q1 \v 22 “Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa, \q2 iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote? \q1 \v 23 Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili, \q2 akiwa salama na mwenye raha kamili, \q1 \v 24 mwili wake ukiwa umenawiri, \q2 nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake. \q1 \v 25 Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi, \q2 akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri. \q1 \v 26 Hao wote hulala mavumbini, \q2 nao mabuu huwafunika wote. \b \q1 \v 27 “Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri, \q2 mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya. \q1 \v 28 Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu, \q2 mahema ambayo watu waovu walikaa?’ \q1 \v 29 Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri? \q2 Je, hamkutafakari taarifa zao: \q1 \v 30 kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa, \q2 kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu? \q1 \v 31 Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake? \q2 Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda? \q1 \v 32 Hupelekwa kaburini, \q2 nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake. \q1 \v 33 Udongo ulio bondeni ni mtamu kwake; \q2 watu wote watamfuata, \q2 nao umati wa watu usiohesabika umemtangulia. \b \q1 \v 34 “Hivyo ninyi mnawezaje kunifariji kwa upuzi wenu? \q2 Hakuna kilichosalia cha majibu yenu isipokuwa uongo!” \c 22 \s1 Elifazi Anasema: Uovu Wa Ayubu Ni Mkubwa \p \v 1 Ndipo Elifazi Mtemani akajibu: \q1 \v 2 “Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? \q2 Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi? \q1 \v 3 Je, Mwenyezi angefurahia nini \q2 kama ungekuwa mwadilifu? \q1 Au je, yeye angepata faida gani \q2 kama njia zako zingekuwa kamilifu? \b \q1 \v 4 “Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea \q2 na kuleta mashtaka dhidi yako? \q1 \v 5 Je, uovu wako si mkuu? \q2 Dhambi zako si hazina mwisho? \q1 \v 6 Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu; \q2 umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi. \q1 \v 7 Hukumpa maji aliyechoka, \q2 nawe ulimnyima chakula mwenye njaa, \q1 \v 8 ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi: \q2 mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake. \q1 \v 9 Umewafukuza wajane mikono mitupu \q2 na kuzivunja nguvu za yatima. \q1 \v 10 Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote, \q2 hatari ya ghafula inakutia hofu, \q1 \v 11 ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona, \q2 tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika. \b \q1 \v 12 “Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu? \q2 Juu kuliko nyota zilizo juu sana! \q1 \v 13 Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’ \q2 Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo? \q1 \v 14 Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi \q2 atembeapo juu ya anga la dunia. \q1 \v 15 Je, utaifuata njia ya zamani, \q2 ambayo watu waovu waliikanyaga? \q1 \v 16 Waliondolewa kabla ya wakati wao, \q2 misingi yao ikachukuliwa na mafuriko. \q1 \v 17 Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi! \q2 Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’ \q1 \v 18 Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri, \q2 hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu. \b \q1 \v 19 “Wenye haki wanaona maangamizi yao na kufurahi, \q2 nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema, \q1 \v 20 ‘Hakika adui zetu wameangamizwa, \q2 nao moto umeteketeza mali zao.’ \b \q1 \v 21 “Mjue sana Mungu ili uwe na amani, \q2 ndipo mema yatakapokujia. \q1 \v 22 Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake, \q2 na maneno yake uyaweke moyoni mwako. \q1 \v 23 Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya: \q2 Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako, \q1 \v 24 kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi, \q2 dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni, \q1 \v 25 ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako, \q2 naye atakuwa fedha yako iliyo bora. \q1 \v 26 Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi, \q2 nawe utamwinulia Mungu uso wako. \q1 \v 27 Utamwomba yeye, naye atakusikia, \q2 nawe utazitimiza nadhiri zako. \q1 \v 28 Utakusudia jambo nalo litatendeka, \q2 nao mwanga utaangazia njia zako. \q1 \v 29 Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’ \q2 ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo. \q1 \v 30 Atamwokoa hata yule ambaye ana hatia, \q2 ataokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.” \c 23 \ms2 Hotuba Ya Nane Ya Ayubu \s1 Ayubu Anajibu: Kulalamika Kwangu Ni Uchungu \p \v 1 Ndipo Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Hata leo malalamiko yangu ni chungu; \q2 mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua. \q1 \v 3 Laiti ningefahamu mahali pa kumwona; \q2 laiti ningeweza kwenda mahali akaapo! \q1 \v 4 Ningeliweka shauri langu mbele zake, \q2 na kukijaza kinywa changu na hoja. \q1 \v 5 Ningejua kwamba angenijibu nini, \q2 na kuelewa lile ambalo angelisema. \q1 \v 6 Je, angenipinga kwa nguvu nyingi? \q2 La, asingenigandamiza. \q1 \v 7 Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake, \q2 nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu. \b \q1 \v 8 “Lakini nikienda mashariki, hayupo; \q2 nikienda magharibi, simpati. \q1 \v 9 Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni; \q2 akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo. \q1 \v 10 Lakini anaijua njia niiendeayo; \q2 akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. \q1 \v 11 Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu; \q2 nimeishika njia yake bila kukengeuka. \q1 \v 12 Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake; \q2 nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku. \b \q1 \v 13 “Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga? \q2 Yeye hufanya lolote atakalo. \q1 \v 14 Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu, \q2 na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba. \q1 \v 15 Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake; \q2 nifikiriapo haya yote ninamwogopa. \q1 \v 16 Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia; \q2 yeye Mwenyezi amenitia hofu. \q1 \v 17 Hata hivyo sijanyamazishwa na giza, \q2 wala kwa giza nene linalofunika uso wangu. \b \c 24 \s1 Ayubu Analalamikia Jeuri Duniani \q1 \v 1 “Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? \q2 Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio? \q1 \v 2 Watu husogeza mawe ya mpaka; \q2 huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu. \q1 \v 3 Huwanyangʼanya yatima punda wao, \q2 na kumchukua rehani fahali wa mjane. \q1 \v 4 Humsukuma mhitaji kutoka njia, \q2 na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha. \q1 \v 5 Kama punda-mwitu jangwani, \q2 maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula; \q1 mahali palipo jangwa \q2 huwapa chakula cha watoto wao. \q1 \v 6 Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo \q2 katika mashamba ya mizabibu ya waovu. \q1 \v 7 Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi; \q2 hawana chochote cha kujifunika baridi. \q1 \v 8 Hutota kwa mvua za mlimani, \q2 nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri. \q1 \v 9 Mtoto yatima hupokonywa matitini; \q2 mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni. \q1 \v 10 Kwa kukosa nguo, hutembea uchi; \q2 hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa. \q1 \v 11 Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia; \q2 hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu. \q1 \v 12 Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, \q2 nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. \q1 Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote \q2 kwa kutenda mabaya. \b \q1 \v 13 “Wako wale wanaoiasi nuru, \q2 wasiofahamu njia zake \q2 wala hawakai katika mapito yake. \q1 \v 14 Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka \q2 naye huwaua maskini na mhitaji; \q2 wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi. \q1 \v 15 Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza, \q2 naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’ \q2 naye huuficha uso wake. \q1 \v 16 Katika giza, huvunja majumba, \q2 lakini wakati wa mchana hujifungia ndani; \q2 hawataki kufanya lolote nuruni. \q1 \v 17 Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao; \q2 hujifanya rafiki na vitisho vya gizani. \b \q1 \v 18 “Lakini wao ni povu juu ya maji; \q2 sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa, \q1 hivyo hakuna hata mmoja \q2 aendaye kwenye shamba la mizabibu. \q1 \v 19 Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka, \q2 ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi. \q1 \v 20 Tumbo lililowazaa huwasahau, \q2 nao huwa karamu ya mabuu; \q1 watu waovu hawakumbukwi tena, \q2 lakini huvunjika kama mti. \q1 \v 21 Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto, \q2 nao hawaonyeshi huruma kwa wajane. \q1 \v 22 Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake; \q2 ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha. \q1 \v 23 Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, \q2 lakini macho yake yanaona njia zao. \q1 \v 24 Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka; \q2 hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, \q2 hukatwa kama masuke ya nafaka. \b \q1 \v 25 “Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo, \q2 na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?” \c 25 \s1 Bildadi Anasema: Mwanadamu Awezaje Kuwa Mwadilifu Mbele Za Mungu? \p \v 1 Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu: \q1 \v 2 “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; \q2 yeye huthibitisha amani katika mbingu juu. \q1 \v 3 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? \q2 Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake? \q1 \v 4 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? \q2 Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi? \q1 \v 5 Ikiwa hata mwezi sio mwangavu \q2 nazo nyota si safi machoni pake, \q1 \v 6 sembuse mtu ambaye ni funza: \q2 mwanadamu ambaye ni buu tu!” \c 26 \ms2 Hotuba Ya Tisa Ya Ayubu \s1 Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki \p \v 1 Kisha Ayubu akajibu: \q1 \v 2 “Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo! \q2 Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu! \q1 \v 3 Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima? \q2 Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha! \q1 \v 4 Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo? \q2 Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako? \b \q1 \v 5 “Wafu wako katika maumivu makuu, \q2 wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake. \q1 \v 6 Mauti\f + \fr 26:6 \ft Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol.\f* iko wazi mbele za Mungu; \q2 Uharibifu\f + \fr 26:6 \ft Kwa Kiebrania ni Abadon.\f* haukufunikwa. \q1 \v 7 Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; \q2 naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu. \q1 \v 8 Huyafungia maji kwenye mawingu yake, \q2 hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. \q1 \v 9 Huufunika uso wa mwezi mpevu, \q2 akitandaza mawingu juu yake. \q1 \v 10 Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, \q2 ameweka mpaka wa nuru na giza. \q1 \v 11 Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, \q2 zinatishika anapozikemea. \q1 \v 12 Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; \q2 kwa hekima yake alimkata Rahabu\f + \fr 26:12 \ft Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.\f* vipande vipande. \q1 \v 13 Aliisafisha anga kwa pumzi yake; \q2 kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio. \q1 \v 14 Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; \q2 tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! \q1 Ni nani basi awezaye kuelewa \q2 ngurumo za nguvu zake?” \c 27 \ms2 Hotuba Ya Mwisho Ya Ayubu \s1 Ayubu Anadumisha Uadilifu Wake \p \v 1 Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema: \q1 \v 2 “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu, \q2 Mwenyezi ambaye amenifanya \q2 nionje uchungu wa nafsi, \q1 \v 3 kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, \q2 nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu, \q1 \v 4 midomo yangu haitanena uovu, \q2 wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu. \q1 \v 5 Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; \q2 hadi nife, sitakana uadilifu wangu. \q1 \v 6 Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha; \q2 dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi. \b \q1 \v 7 “Watesi wangu wawe kama waovu, \q2 nao adui zangu wawe kama wasio haki! \q1 \v 8 Kwa maana mtu asiyemcha Mungu \q2 analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali, \q2 Mungu anapouondoa uhai wake? \q1 \v 9 Je, Mungu husikiliza kilio chake, \q2 shida zimjiapo? \q1 \v 10 Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi? \q2 Je, atamwita Mungu nyakati zote? \b \q1 \v 11 “Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu; \q2 njia za Mwenyezi sitazificha. \q1 \v 12 Ninyi nyote mmeona hili wenyewe. \q2 Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana? \b \q1 \v 13 “Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, \q2 urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi: \q1 \v 14 Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, \q2 fungu lao ni kuuawa kwa upanga; \q1 wazao wake hawatakuwa kamwe \q2 na chakula cha kuwatosha. \q1 \v 15 Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, \q2 nao wajane wao hawatawaombolezea. \q1 \v 16 Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, \q2 na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi, \q1 \v 17 yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, \q2 naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake. \q1 \v 18 Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, \q2 kama kibanda alichotengeneza mlinzi. \q1 \v 19 Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; \q2 afunguapo macho yake, yote yametoweka. \q1 \v 20 Vitisho humjia kama mafuriko; \q2 dhoruba humkumba ghafula usiku. \q1 \v 21 Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; \q2 humzoa kutoka mahali pake. \q1 \v 22 Humvurumisha bila huruma, \q2 huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake. \q1 \v 23 Upepo humpigia makofi kwa dharau, \q2 na kumfukuza atoke mahali pake. \c 28 \s1 Mapumziko: Imani Inakopatikana \q1 \v 1 “Kuna machimbo ya fedha, \q2 na mahali dhahabu isafishwapo. \q1 \v 2 Chuma hupatikana ardhini, \q2 nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini. \q1 \v 3 Mwanadamu hukomesha giza; \q2 huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, \q1 kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini \q2 katika giza jeusi sana. \q1 \v 4 Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, \q2 mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu; \q2 mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba. \q1 \v 5 Ardhi, ambako chakula hutoka, \q2 chini hugeuzwa kwa moto; \q1 \v 6 yakuti samawi hutoka katika miamba yake, \q2 nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu. \q1 \v 7 Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika, \q2 wala hakuna jicho la mwewe lililoiona. \q1 \v 8 Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, \q2 wala simba azungukaye huko. \q1 \v 9 Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, \q2 na kuiacha wazi mizizi ya milima. \q1 \v 10 Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; \q2 macho yake huona hazina zake zote. \q1 \v 11 Hutafuta vyanzo vya mito \q2 na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru. \b \q1 \v 12 “Lakini hekima inaweza kupatikana wapi? \q2 Ufahamu unakaa wapi? \q1 \v 13 Mwanadamu hatambui thamani yake; \q2 haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai. \q1 \v 14 Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’; \q2 bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’ \q1 \v 15 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote, \q2 wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha. \q1 \v 16 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri, \q2 kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa. \q1 \v 17 Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo, \q2 wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu. \q1 \v 18 Marijani na yaspi hazistahili kutajwa; \q2 thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu. \q1 \v 19 Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo, \q2 wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi. \b \q1 \v 20 “Ni wapi basi hekima itokako? \q2 Ufahamu hukaa wapi? \q1 \v 21 Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai, \q2 imesitiriwa hata kwa ndege wa angani. \q1 \v 22 Uharibifu na Mauti husema, \q2 ‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’ \q1 \v 23 Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima \q2 na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa, \q1 \v 24 kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia \q2 na huona kila kitu chini ya mbingu. \q1 \v 25 Alipofanyiza nguvu za upepo \q2 na kuyapima maji, \q1 \v 26 alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua \q2 na njia kwa ajili ya umeme wa radi, \q1 \v 27 ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake, \q2 akaithibitisha na kuihakikisha. \q1 \v 28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu, \q2 ‘Kumcha \nd Bwana\nd*: hiyo ndiyo hekima, \q2 nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ” \c 29 \s1 Ayubu Anamaliza Utetezi Wake \p \v 1 Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema: \q1 \v 2 “Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, \q2 zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda, \q1 \v 3 wakati taa yake iliniangazia kichwani changu, \q2 na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza! \q1 \v 4 Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu, \q2 wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu, \q1 \v 5 wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami, \q2 nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka, \q1 \v 6 wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi, \q2 nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni. \b \q1 \v 7 “Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji \q2 na kuketi katika kiwanja, \q1 \v 8 vijana waliniona wakakaa kando, \q2 nao wazee walioketi wakasimama; \q1 \v 9 wakuu wakaacha kuzungumza \q2 na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao; \q1 \v 10 wenye vyeo wakanyamazishwa, \q2 nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao. \q1 \v 11 Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu, \q2 nao walioniona walinisifu, \q1 \v 12 kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada, \q2 naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia. \q1 \v 13 Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki, \q2 nami niliufanya moyo wa mjane kuimba. \q1 \v 14 Niliivaa haki kama vazi langu; \q2 uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu. \q1 \v 15 Nilikuwa macho ya kipofu \q2 na miguu kwa kiwete. \q1 \v 16 Nilikuwa baba kwa mhitaji; \q2 nilimtetea mgeni. \q1 \v 17 Niliyavunja meno makali ya waovu, \q2 na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao. \b \q1 \v 18 “Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe, \q2 nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga. \q1 \v 19 Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji, \q2 nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha. \q1 \v 20 Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu, \q2 upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’ \b \q1 \v 21 “Watu walinisikiliza kwa tumaini, \q2 wakingojea ushauri wangu kwa utulivu. \q1 \v 22 Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi; \q2 maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini. \q1 \v 23 Waliningojea kama manyunyu ya mvua \q2 na kuyapokea maneno yangu \q2 kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli. \q1 \v 24 Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha; \q2 nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao. \q1 \v 25 Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao; \q2 niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake; \q2 nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji. \b \c 30 \q1 \v 1 “Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, \q1 watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau \q2 kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. \q1 \v 2 Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, \q2 kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia? \q1 \v 3 Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, \q2 walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa. \q1 \v 4 Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi, \q2 nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio. \q1 \v 5 Walifukuzwa mbali na watu wao, \q2 wakipigiwa kelele kama wevi. \q1 \v 6 Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka, \q2 kwenye majabali na mahandaki. \q1 \v 7 Kwenye vichaka walilia kama punda, \q2 na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka. \q1 \v 8 Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya, \q2 waliofukuzwa watoke katika nchi. \b \q1 \v 9 “Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo; \q2 nimekuwa kitu cha dhihaka kwao. \q1 \v 10 Wananichukia sana na kujitenga nami, \q2 wala hawasiti kunitemea mate usoni. \q1 \v 11 Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa, \q2 wamekuwa huru kunitendea waonavyo. \q1 \v 12 Kuume kwangu kundi linashambulia; \q2 wao huitegea miguu yangu tanzi, \q2 na kunizingira. \q1 \v 13 Huizuia njia yangu, \q2 nao hufanikiwa katika kuniletea maafa, \q2 nami sina yeyote wa kunisaidia. \q1 \v 14 Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana; \q2 katikati ya magofu huja na kunishambulia. \q1 \v 15 Vitisho vimenifunika; \q2 heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo, \q2 salama yangu imetoweka kama wingu. \b \q1 \v 16 “Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; \q2 siku za mateso zimenikamata. \q1 \v 17 Usiku mifupa yangu inachoma; \q2 maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe. \q1 \v 18 Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; \q2 hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu. \q1 \v 19 Yeye amenitupa kwenye matope, \q2 nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. \b \q1 \v 20 “Ee \nd Bwana\nd*, ninakulilia wewe lakini hunijibu; \q2 ninasimama, nawe unanitazama tu. \q1 \v 21 Wewe unanigeukia bila huruma; \q2 unanishambulia kwa nguvu za mkono wako. \q1 \v 22 Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; \q2 umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali. \q1 \v 23 Ninajua utanileta mpaka kifoni, \q2 mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa. \b \q1 \v 24 “Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, \q2 anapoomba msaada katika shida yake. \q1 \v 25 Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? \q2 Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini? \q1 \v 26 Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; \q2 nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja. \q1 \v 27 Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; \q2 siku za mateso zinanikabili. \q1 \v 28 Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; \q2 ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada. \q1 \v 29 Nimekuwa ndugu wa mbweha, \q2 rafiki wa mabundi. \q1 \v 30 Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; \q2 mifupa yangu inaungua kwa homa. \q1 \v 31 Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo, \q2 nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio. \b \c 31 \q1 \v 1 “Nimefanya agano na macho yangu \q2 yasimtazame msichana kwa kumtamani. \q1 \v 2 Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu, \q1 urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu? \q1 \v 3 Je, si uharibifu kwa watu waovu, \q2 maangamizi kwa wale watendao mabaya? \q1 \v 4 Je, yeye hazioni njia zangu \q2 na kuihesabu kila hatua yangu? \b \q1 \v 5 “Kama nimeishi katika uongo \q2 au mguu wangu umekimbilia udanganyifu, \q1 \v 6 Mungu na anipime katika mizani za uaminifu, \q2 naye atajua kwamba sina hatia: \q1 \v 7 kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia, \q2 kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu, \q2 au kama mikono yangu imetiwa unajisi, \q1 \v 8 basi wengine na wale nilichokipanda, \q2 nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe. \b \q1 \v 9 “Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke, \q2 au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu, \q1 \v 10 basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine, \q2 nao wanaume wengine walale naye. \q1 \v 11 Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, \q2 naam, dhambi ya kuhukumiwa. \q1 \v 12 Ni moto uwakao kwa Uharibifu;\f + \fr 31:12 \ft Kwa Kiebrania ni Abadon (\+xt Ay 26:6; Mit 15:11\+xt*).\f* \q2 ungekuwa umengʼoa mavuno yangu. \b \q1 \v 13 “Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, \q2 walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu, \q1 \v 14 nitafanya nini Mungu atakaponikabili? \q2 Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu? \q1 \v 15 Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu, \q2 si ndiye aliwaumba? \q1 Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote \q2 ndani ya mama zetu? \b \q1 \v 16 “Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, \q2 au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike, \q1 \v 17 kama nimekula chakula changu mwenyewe, \q2 bila kuwashirikisha yatima; \q1 \v 18 lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya, \q2 nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane: \q1 \v 19 kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo, \q2 au mtu mhitaji asiye na mavazi \q1 \v 20 ambaye wala moyo wake haukunibariki \q2 kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu, \q1 \v 21 na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima, \q2 nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani, \q1 \v 22 basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu, \q2 nao na uvunjike kutoka kiungio chake. \q1 \v 23 Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu, \q2 nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo. \b \q1 \v 24 “Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu, \q2 au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’ \q1 \v 25 kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu, \q2 ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata, \q1 \v 26 kama nimelitazama jua katika kungʼaa kwake \q2 au mwezi ukienda kwa fahari yake, \q1 \v 27 hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri, \q2 au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu, \q1 \v 28 basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa, \q2 kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana. \b \q1 \v 29 “Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu, \q2 au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia, \q1 \v 30 lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi \q2 kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake; \q1 \v 31 kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema, \q2 ‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’ \q1 \v 32 Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani, \q2 kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri; \q1 \v 33 kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo, \q2 kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu, \q1 \v 34 kwa sababu ya kuogopa umati wa watu, \q2 na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa, \q2 nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango: \b \q1 \v 35 (“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia! \q2 Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu: \q2 Mwenyezi na anijibu; \q1 mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi. \q1 \v 36 Hakika ningeyavaa begani mwangu, \q2 ningeyavaa kama taji. \q1 \v 37 Ningempa hesabu ya kila hatua yangu, \q2 ningemwendea kama mwana wa mfalme.) \b \q1 \v 38 “Kama nchi yangu inalia dhidi yangu, \q2 na mifereji yake yote imelowana kwa machozi, \q1 \v 39 kama nimekula mazao yake bila malipo, \q2 au kuvunja mioyo ya wapangaji wake, \q1 \v 40 basi miiba na iote badala ya ngano, \q2 na magugu badala ya shayiri.” \p Mwisho wa maneno ya Ayubu. \c 32 \ms1 Sehemu Ya Tatu: Mazungumzo Ya Elihu \mr (Ayubu 32–37) \s1 Elihu Awakemea Rafiki Za Ayubu \p \v 1 Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe. \v 2 Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu ya kujihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu. \v 3 Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu hawakuweza kupata njia ya kuthibitisha ya kuwa hayo maneno ya Ayubu hayakuwa ya kweli, nao bado walikuwa wamemlaumu. \v 4 Basi Elihu alikuwa amesubiri kwanza waongee na Ayubu kwa sababu walikuwa na umri mkubwa kumliko yeye. \v 5 Lakini alipoona watu hao watatu hawakuwa na kitu zaidi cha kusema, hasira yake ikaamka. \p \v 6 Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: \q1 “Mimi ni mdogo kwa umri, \q2 nanyi ni wazee; \q1 ndiyo sababu niliogopa, \q2 sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua. \q1 \v 7 Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, \q2 nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’ \q1 \v 8 Lakini ni Roho iliyoko ndani ya mwanadamu, \q2 pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo yeye ufahamu. \q1 \v 9 Sio wazee peke yao walio na hekima, \q2 sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa. \b \q1 \v 10 “Kwa hiyo nasema: Nisikilizeni mimi; \q2 mimi nami nitawaambia lile ninalojua. \q1 \v 11 Nilingojea mlipokuwa mnaongea, \q2 nilizisikiliza hoja zenu; \q1 mlipokuwa mkitafuta maneno ya kusema, \q2 \v 12 niliwasikiliza kwa makini. \q1 Lakini hakuna hata mmoja wenu \q2 aliyethibitisha kwamba Ayubu amekosa; \q1 hakuna hata mmoja wenu \q2 aliyeweza kujibu hoja zake. \q1 \v 13 Msiseme, ‘Tumepata hekima; \q2 Mungu na amthibitishe kuwa mwongo, \q2 wala si mwanadamu.’ \q1 \v 14 Lakini Ayubu hajayapanga maneno yake dhidi yangu, \q2 nami sitamjibu kwa kutumia hoja zenu. \b \q1 \v 15 “Wametiwa hofu na hawana la zaidi la kusema; \q2 maneno yamewaishia. \q1 \v 16 Je, ningoje sasa kwa sababu wamekuwa kimya, \q2 kwa vile sasa wanasimama bila kuwa na la kujibu? \q1 \v 17 Mimi nami nitakuwa na la kusema; \q2 mimi nami nitasema lile nilijualo. \q1 \v 18 Kwa kuwa nimejawa na maneno, \q2 nayo Roho iliyomo ndani yangu yanisukuma; \q1 \v 19 ndani yangu niko kama chupa iliyojazwa divai, \q2 kama kiriba kipya cha divai kilicho tayari kupasuka. \q1 \v 20 Ni lazima niseme ili niweze kutulia; \q2 ni lazima nifumbue midomo yangu nipate kujibu. \q1 \v 21 Sitampendelea mtu yeyote, \q2 wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote; \q1 \v 22 kwa kuwa kama ningekuwa stadi wa kujipendekeza, \q2 Muumba wangu angeniondolea mbali kwa upesi. \c 33 \s1 Elihu Anamkemea Ayubu \q1 \v 1 “Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; \q2 zingatia kila kitu nitakachosema. \q1 \v 2 Karibu nitafungua kinywa changu; \q2 maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu. \q1 \v 3 Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; \q2 midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo. \q1 \v 4 Roho wa Mungu ameniumba; \q2 pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. \q1 \v 5 Unijibu basi, kama unaweza; \q2 jiandae kunikabili mimi. \q1 \v 6 Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; \q2 mimi pia nimetolewa kwenye udongo. \q1 \v 7 Huna sababu ya kuniogopa, \q2 wala mkono wangu haupaswi kukulemea. \b \q1 \v 8 “Lakini umesema nikiwa ninakusikia, \q2 nami nilisikia maneno yenyewe: \q1 \v 9 ‘Mimi ni safi na sina dhambi; \q2 mimi ni safi na sina hatia. \q1 \v 10 Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, \q2 naye ananiona kama adui yake. \q1 \v 11 Ananifunga miguu kwa pingu, \q2 tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’ \b \q1 \v 12 “Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, \q2 kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu. \q1 \v 13 Kwa nini unamlalamikia \q2 kwamba yeye hamjibu mwanadamu? \q1 \v 14 Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, \q2 au wakati mwingine kwa njia nyingine, \q2 ingawa mwanadamu anaweza asielewe. \q1 \v 15 Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, \q2 katika maono ya usiku, \q1 wakati usingizi mzito uwaangukiapo \q2 wanadamu wasinziapo vitandani mwao, \q1 \v 16 anaweza akasemea masikioni mwao, \q2 na kuwatia hofu kwa maonyo, \q1 \v 17 ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya \q2 na kumwepusha na kiburi, \q1 \v 18 kuiokoa nafsi yake na shimo, \q2 uhai wake usiangamizwe kwa upanga. \q1 \v 19 Mtu anaweza kutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, \q2 kwa dhiki za mfululizo katika mifupa yake, \q1 \v 20 kiasi kwamba maisha yake yenyewe yanakataa chakula \q2 nayo nafsi yake ikakichukia kabisa hata chakula kizuri. \q1 \v 21 Nyama ya mwili wake huisha kwa kukonda, \q2 nayo mifupa yake ambayo mwanzoni ilikuwa imefichika, \q2 sasa inatokeza nje. \q1 \v 22 Nafsi yake inakaribia kaburi, \q2 nao uhai wake karibu na wajumbe wa kifo. \b \q1 \v 23 “Kama bado kuna malaika upande wake \q2 kama mtetezi, mmoja miongoni mwa elfu, \q2 wa kumwambia mwanadamu lililo jema kwake, \q1 \v 24 kumwonea huruma na kusema, \q2 ‘Mwokoe asije akatumbukia shimoni; \q2 nimepata ukombozi kwa ajili yake’: \q1 \v 25 ndipo nyama ya mwili wake hufanywa mpya kama ya mtoto; \q2 hurudishwa upya kama siku za ujana wake. \q1 \v 26 Humwomba Mungu, akapata kibali kwake, \q2 huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha; \q2 Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu. \q1 \v 27 Ndipo huja mbele za watu na kusema, \q2 ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, \q2 lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili. \q1 \v 28 Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, \q2 nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’ \b \q1 \v 29 “Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; \q2 mara mbili hata mara tatu, \q1 \v 30 ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, \q2 ili nuru ya uzima imwangazie. \b \q1 \v 31 “Ayubu, zingatia, nisikilize mimi; \q2 nyamaza, nami nitanena. \q1 \v 32 Kama unalo lolote la kusema, unijibu; \q2 sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia. \q1 \v 33 Lakini kama huna la kusema, basi nisikilize mimi; \q2 nyamaza, nami nitakufundisha hekima.” \c 34 \s1 Elihu Anatangaza Haki Ya Mungu \p \v 1 Kisha Elihu akasema: \q1 \v 2 “Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima; \q2 nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa. \q1 \v 3 Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno \q2 kama vile ulimi uonjavyo chakula. \q1 \v 4 Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa, \q2 nasi tujifunze pamoja yaliyo mema. \b \q1 \v 5 “Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, \q2 lakini Mungu ameninyima haki yangu. \q1 \v 6 Ingawa niko sawa, \q2 ninaonekana mwongo; \q1 nami ingawa sina kosa, \q2 kidonda changu hakiponi.’ \q1 \v 7 Ni mtu gani aliye kama Ayubu, \q2 anywaye dharau kama maji? \q1 \v 8 Ashirikianaye na watenda mabaya \q2 na kuchangamana na watu waovu. \q1 \v 9 Kwa kuwa anasema, ‘Haimfaidi mwanadamu kitu chochote \q2 anapojitahidi kumpendeza Mungu.’ \b \q1 \v 10 “Hivyo nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye ufahamu. \q2 Kamwe Mungu hatendi uovu, \q2 Mwenyezi hafanyi kosa. \q1 \v 11 Humlipa mwanadamu kwa ajili ya lile alilotenda; \q2 huleta juu yake kile ambacho matendo yake yanastahili. \q1 \v 12 Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kwamba Mungu angefanya makosa, \q2 kwamba Mwenyezi angepotosha hukumu. \q1 \v 13 Je, ni nani aliyemtawaza juu ya dunia? \q2 Ni nani aliyemweka kuwa mwangalizi wa ulimwengu wote? \q1 \v 14 Kama lilikuwa kusudi la Mungu, \q2 naye akaiondoa Roho yake na pumzi yake, \q1 \v 15 wanadamu wote wangeliangamia kwa pamoja, \q2 na mtu angerudi mavumbini. \b \q1 \v 16 “Kama ninyi mnaufahamu, sikieni hili; \q2 sikilizeni hili nisemalo. \q1 \v 17 Je, yeye aichukiaye haki aweza kutawala? \q2 Je, utamhukumu mwenye haki, Aliye na Nguvu Zote? \q1 \v 18 Je, si ni yeye awaambiaye wafalme, ‘Ninyi hamfai kitu,’ \q2 nao watu mashuhuri, ‘Ninyi ni waovu,’ \q1 \v 19 yeye asiyependelea wakuu, \q2 wala haonyeshi upendeleo kwa matajiri kuliko maskini, \q2 kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake? \q1 \v 20 Wanakufa ghafula, usiku wa manane; \q2 watu wanatikiswa nao hupita; \q1 wenye nguvu huondolewa \q2 bila mkono wa mwanadamu. \b \q1 \v 21 “Macho yake yanazitazama njia za wanadamu; \q2 anaona kila hatua yao. \q1 \v 22 Hakuna mahali penye giza nene, wala uvuli mkubwa, \q2 ambapo watenda mabaya wanaweza kujificha. \q1 \v 23 Mungu hana haja ya kumchunguza mtu sana, \q2 ili apate kuja mbele zake kwa hukumu. \q1 \v 24 Bila kuuliza huwapondaponda wenye nguvu nyingi \q2 na kuwaweka wengine mahali pao. \q1 \v 25 Kwa sababu huyaangalia matendo yao yote, \q2 huwaondoa usiku, nao wakaangamia. \q1 \v 26 Anawaadhibu kwa ajili ya uovu wao \q2 mahali ambapo kila mmoja ataweza kuwaona, \q1 \v 27 kwa sababu wameacha kumfuata Mungu, \q2 nao hawakuiheshimu njia yake hata moja. \q1 \v 28 Wamesababisha kilio cha maskini kifike mbele zake, \q2 hivyo akasikia kilio cha wahitaji. \q1 \v 29 Lakini kama akinyamaza kimya, \q2 ni nani awezaye kumhukumu? \q1 Kama akiuficha uso wake, \q2 ni nani awezaye kumwona? \q1 Ikiwa ni taifa au mtu mmoja, kwake ni sawa, \q2 \v 30 ili kumzuia mtu mwovu kutawala, \q2 au wale ambao huwategea watu mitego. \b \q1 \v 31 “Kama mwanadamu akimwambia Mungu, \q2 ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena. \q1 \v 32 Nifundishe nisichoweza kuona; \q2 kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’ \q1 \v 33 Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako, \q2 wakati wewe umekataa kutubu? \q1 Yakupasa wewe uamue, wala si mimi; \q2 sasa niambie lile ulijualo. \b \q1 \v 34 “Wanadamu wenye ufahamu husema, \q2 wenye hekima wanaonisikia huniambia, \q1 \v 35 ‘Ayubu huongea bila maarifa; \q2 maneno yake hayana busara.’ \q1 \v 36 Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho, \q2 kwa sababu anajibu kama mtu mwovu! \q1 \v 37 Kwenye dhambi yake huongeza uasi; \q2 kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu, \q2 na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.” \c 35 \s1 Elihu Analaumu Mtu Kujiona Kuwa Mwenye Haki \p \v 1 Ndipo Elihu akasema: \q1 \v 2 “Je, unadhani hili ni haki? \q2 Wewe unasema, ‘Nina haki mbele za Mungu.’ \q1 \v 3 Bado unamuuliza, ‘Ni faida gani nimepata, \q2 na imenifaidi nini kwa kutokutenda dhambi?’ \b \q1 \v 4 “Ningependa nikujibu wewe \q2 pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe. \q1 \v 5 Tazama juu mbinguni ukaone; \q2 yaangalie mawingu yaliyo juu sana juu yako. \q1 \v 6 Je, ukitenda dhambi, inamdhuruje Mungu? \q2 Kama dhambi zako zikiwa nyingi, \q2 hilo linamfanyia nini Mungu? \q1 \v 7 Kama wewe ni mwadilifu, unampa nini, \q2 au yeye anapokea nini mkononi kwako? \q1 \v 8 Uovu wako unamdhuru tu mtu mwingine kama wewe, \q2 nayo haki yako inawafaa wanadamu tu. \b \q1 \v 9 “Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso; \q2 huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu. \q1 \v 10 Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu Muumba wangu, \q2 yeye anifanyaye niimbe usiku, \q1 \v 11 yeye atufundishaye sisi zaidi kuliko wanyama wa dunia, \q2 na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?’ \q1 \v 12 Yeye hajibu wakati watu waliapo \q2 kwa sababu ya kiburi cha watu waovu. \q1 \v 13 Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili; \q2 Mwenyezi hayazingatii. \q1 \v 14 Si zaidi sana kwamba hatakusikiliza \q2 wewe usemapo humwoni, \q1 tena ya kwamba shauri lako liko mbele zake \q2 na wewe lazima umngojee, \q1 \v 15 pia zaidi, kwamba hasira yake kamwe haiadhibu \q2 wala haangalii uovu hata kidogo? \q1 \v 16 Hivyo Ayubu hufumbua kinywa chake kwa maneno yasiyo na maana; \q2 anaongea maneno mengi bila maarifa.” \c 36 \s1 Elihu Atukuza Wema Wa Mungu \p \v 1 Elihu akaendelea kusema: \q1 \v 2 “Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha \q2 kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. \q1 \v 3 Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, \q2 nami nitamhesabia haki Muumba wangu. \q1 \v 4 Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; \q2 mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe. \b \q1 \v 5 “Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; \q2 ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake. \q1 \v 6 Hawaachi waovu waendelee kuishi, \q2 bali huwapa walioteswa haki yao. \q1 \v 7 Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; \q2 huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme \q2 na kuwatukuza milele. \q1 \v 8 Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, \q2 wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso, \q1 \v 9 huwaonyesha yale waliyoyatenda, \q2 kwamba wametenda dhambi kwa majivuno. \q1 \v 10 Huwafanya wao kusikia maonyo, \q2 na huwaagiza kutubu uovu wao. \q1 \v 11 Kama wakitii na kumtumikia, \q2 wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, \q2 na miaka yao katika utoshelevu. \q1 \v 12 Lakini wasiposikiliza, \q2 wataangamia kwa upanga, \q2 nao watakufa pasipo maarifa. \b \q1 \v 13 “Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; \q2 hata anapowafunga, hawamwombi msaada. \q1 \v 14 Wanakufa wangali vijana, \q2 miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. \q1 \v 15 Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, \q2 na kuzungumza nao katika dhiki zao. \b \q1 \v 16 “Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, \q2 ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, \q2 hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri. \q1 \v 17 Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu; \q2 hukumu na haki vimekukamata. \q1 \v 18 Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri; \q2 usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa. \q1 \v 19 Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi \q2 vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki? \q1 \v 20 Usiutamani usiku uje, \q2 ili uwaburute watu mbali na nyumba zao. \q1 \v 21 Jihadhari usigeukie uovu, \q2 ambao unaupenda zaidi kuliko mateso. \b \q1 \v 22 “Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. \q2 Ni nani aliye mwalimu kama yeye? \q1 \v 23 Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, \q2 au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’? \q1 \v 24 Kumbuka kuzitukuza kazi zake, \q2 ambazo watu wamezisifu katika wimbo. \q1 \v 25 Wanadamu wote wameiona; \q2 watu wanaikazia macho kwa mbali. \q1 \v 26 Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, \q2 kupita ufahamu wetu! \q2 Hesabu ya miaka yake haitafutiki. \b \q1 \v 27 “Yeye huvuta juu matone ya maji, \q2 ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito; \q1 \v 28 mawingu huangusha chini maji yake, \q2 nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu. \q1 \v 29 Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, \q2 jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake. \q1 \v 30 Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka, \q2 naye huvifunika vilindi vya bahari. \q1 \v 31 Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, \q2 na kuwapa chakula kwa wingi. \q1 \v 32 Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi, \q2 na kuuagiza kulenga shabaha yake. \q1 \v 33 Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; \q2 hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.\f + \fr 36:33 \ft Au: hutangaza kuja kwake.\f* \b \c 37 \q1 \v 1 “Kwa hili moyo wangu unatetemeka, \q2 nao unaruka kutoka mahali pake. \q1 \v 2 Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, \q2 sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake. \q1 \v 3 Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote \q2 na kuupeleka hata miisho ya dunia. \q1 \v 4 Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake; \q2 Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari. \q1 Wakati sauti yake ingurumapo tena, \q2 huuachilia umeme wake wa radi. \q1 \v 5 Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu; \q2 yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu. \q1 \v 6 Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ \q2 nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’ \q1 \v 7 Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, \q2 yeye humzuilia kila mtu shughuli zake. \q1 \v 8 Wanyama hujificha; \q2 hubakia kwenye mapango yao. \q1 \v 9 Dhoruba hutoka katika chumba chake, \q2 baridi hutoka katika upepo uendao kasi. \q1 \v 10 Pumzi ya Mungu hutoa barafu, \q2 eneo kubwa la maji huganda. \q1 \v 11 Huyasheheneza mawingu kwa maji, \q2 naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo. \q1 \v 12 Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, \q2 juu ya uso wa dunia yote, \q2 kufanya lolote ayaamuruyo. \q1 \v 13 Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu, \q2 au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake. \b \q1 \v 14 “Ayubu, sikiliza hili; \q2 nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu. \q1 \v 15 Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu, \q2 na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga? \q1 \v 16 Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia, \q2 hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa? \q1 \v 17 Wewe unayeshindwa na joto katika nguo zako \q2 wakati nchi imenyamazishwa kimya bila upepo wa kusini, \q1 \v 18 je, waweza kuungana naye katika kuzitandaza anga, \q2 zilizo ngumu kama kioo cha shaba ya kuyeyushwa? \b \q1 \v 19 “Tuambieni yatupasayo kumwambia; \q2 hatuwezi kutayarisha shauri letu kwa sababu ya ujinga wetu. \q1 \v 20 Je, aambiwe kwamba nataka kuongea? \q2 Je, yuko mtu ambaye angeomba kumezwa? \q1 \v 21 Basi hakuna awezaye kulitazama jua, \q2 jinsi linavyongʼaa angani, \q2 upepo ukishafagia mawingu. \q1 \v 22 Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu; \q2 Mungu huja katika utukufu wa kutisha. \q1 \v 23 Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza; \q2 katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea. \q1 \v 24 Kwa hiyo, wanadamu mheshimuni, \q2 kwa kuwa yeye hamstahi yeyote anayejidhania kuwa ana hekima.” \c 38 \ms1 Sehemu Ya Nne: Mungu Anazungumza \mr (Ayubu 38–41) \s1 \nd Bwana\nd* Anamjibu Ayubu \p \v 1 Kisha \nd Bwana\nd* akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: \q1 \v 2 “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza \q2 kwa maneno yasiyo na maarifa? \q1 \v 3 Jikaze kama mwanaume; \q2 nitakuuliza swali, \q2 nawe unijibu. \b \q1 \v 4 “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? \q2 Niambie, kama unafahamu. \q1 \v 5 Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? \q2 Hakika wewe unajua! \q2 Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake? \q1 \v 6 Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, \q2 au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni, \q1 \v 7 wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, \q2 na malaika wote walipokuwa wakipiga kelele kwa furaha? \b \q1 \v 8 “Ni nani aliyeifungia bahari milango \q2 ilipopasuka kutoka tumbo, \q1 \v 9 nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, \q2 na kuyafungia katika giza nene, \q1 \v 10 nilipoamuru mipaka yake, \q2 na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake, \q1 \v 11 niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi; \q2 hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’? \b \q1 \v 12 “Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, \q2 au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake, \q1 \v 13 yapate kushika miisho ya dunia, \q2 na kuwakungʼuta waovu waliomo? \q1 \v 14 Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri; \q2 sura yake hukaa kama ile ya vazi. \q1 \v 15 Waovu huzuiliwa nuru yao, \q2 nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa. \b \q1 \v 16 “Je, umepata kufika kwenye chemchemi za bahari? \q2 Au kutembea mahali pa ndani pa vilindi? \q1 \v 17 Umewahi kuonyeshwa malango ya mauti? \q2 Umewahi kuiona milango ya uvuli wa mauti? \q1 \v 18 Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? \q2 Niambie kama unajua haya yote. \b \q1 \v 19 “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? \q2 Nako maskani mwa giza ni wapi? \q1 \v 20 Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake? \q2 Unajua njia za kufika maskani mwake? \q1 \v 21 Hakika unajua, kwa kuwa ulikuwa umeshazaliwa! \q2 Kwani umeishi miaka mingi! \b \q1 \v 22 “Je, umeshawahi kuingia katika ghala za theluji, \q2 au kuona ghala za mvua ya mawe, \q1 \v 23 ambazo nimeziweka akiba kwa ajili ya wakati wa taabu, \q2 na kwa ajili ya wakati wa vita na mapigano? \q1 \v 24 Ni ipi njia iendayo mahali umeme wa radi unapotawanyiwa, \q2 au mahali upepo wa mashariki unaposambaziwa juu ya dunia? \q1 \v 25 Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi \q2 na njia ya umeme wa radi, \q1 \v 26 ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu, \q2 jangwa lisilo na yeyote ndani yake, \q1 \v 27 ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa, \q2 na majani yaanze kumea ndani yake? \q1 \v 28 Je, mvua ina baba? \q2 Ni nani baba azaaye matone ya umande? \q1 \v 29 Barafu inatoka tumbo la nani? \q2 Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni, \q1 \v 30 wakati maji yawapo magumu kama jiwe, \q2 wakati uso wa vilindi vya maji unapoganda? \b \q1 \v 31 “Je, waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia? \q2 Waweza kulegeza kamba za Orioni? \q1 \v 32 Waweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake, \q2 au kuongoza Dubu na watoto wake? \q1 \v 33 Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? \q2 Waweza kuweka utawala wa Mungu duniani? \b \q1 \v 34 “Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, \q2 na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji? \q1 \v 35 Je, wewe hutuma umeme wa radi kwenye njia zake? \q2 Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’? \q1 \v 36 Ni nani aliyeujalia moyo hekima \q2 au kuzipa akili ufahamu? \q1 \v 37 Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? \q2 Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni \q1 \v 38 wakati mavumbi yawapo magumu, \q2 na mabonge ya udongo kushikamana pamoja? \b \q1 \v 39 “Je, utamwindia simba jike mawindo, \q2 na kuwashibisha simba wenye njaa \q1 \v 40 wakati wao wamejikunyata mapangoni mwao, \q2 au wakivizia kichakani? \q1 \v 41 Ni nani ampaye kunguru chakula \q2 wakati makinda yake yanamlilia Mungu, \q2 yakizungukazunguka kwa ajili ya kukosa chakula? \b \c 39 \q1 \v 1 “Je, wajua ni wakati gani mbuzi wa mlimani wanapozaa? \q2 Je, watambua ni wakati gani kulungu jike azaapo mtoto wake? \q1 \v 2 Je, waweza kuhesabu miezi hadi wazaapo? \q2 Je, unajua majira yao ya kuzaa? \q1 \v 3 Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao; \q2 utungu wa kuzaa unakoma. \q1 \v 4 Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani; \q2 huenda zao wala hawarudi tena. \b \q1 \v 5 “Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? \q2 Ni nani aliyezifungua kamba zake? \q1 \v 6 Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake, \q2 nchi ya chumvi kuwa makao yake. \q1 \v 7 Huzicheka ghasia za mji, \q2 wala hasikii kelele za mwendesha gari. \q1 \v 8 Huzunguka vilimani kwa ajili ya malisho \q2 na kutafuta kila kitu kibichi. \b \q1 \v 9 “Je, nyati atakubali kukutumikia? \q2 Atakaa karibu na hori lako usiku? \q1 \v 10 Je, waweza kumfungia kwenye matuta kwa kamba? \q2 Je, atalima mabonde nyuma yako? \q1 \v 11 Je, utamtumainia kwa ajili ya nguvu zake nyingi? \q2 Utamwachia yeye kazi zako nzito? \q1 \v 12 Utaweza kumwamini akuletee nafaka yako nyumbani \q2 kutoka shambani na kuikusanya kwenye sakafu yako ya kupuria? \b \q1 \v 13 “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa furaha, \q2 lakini hayawezi kulinganishwa \q2 na mabawa na manyoya ya korongo. \q1 \v 14 Huyataga mayai yake juu ya ardhi, \q2 na kuyaacha yapate joto mchangani, \q1 \v 15 bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda, \q2 kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga. \q1 \v 16 Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake; \q2 hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure, \q1 \v 17 kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, \q2 wala hakumpa fungu la akili njema. \q1 \v 18 Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia, \q2 humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda. \b \q1 \v 19 “Je, wewe humpa farasi nguvu \q2 au kuivika shingo yake manyoya marefu? \q1 \v 20 Je, wewe humfanya farasi aruke kama nzige, \q2 akistaajabisha kwa tishio la mlio wake wa majivuno? \q1 \v 21 Huparapara bila woga, akizifurahia nguvu zake, \q2 husonga mbele kukabiliana na silaha. \q1 \v 22 Huicheka hofu, haogopi chochote, \q2 wala haukimbii upanga. \q1 \v 23 Podo hutoa sauti kando yake, \q2 pamoja na mkuki unaongʼaa na fumo. \q1 \v 24 Bila woga na kwa ghadhabu huimeza nchi, \q2 wala tarumbeta iliapo yeye hawezi kusimama. \q1 \v 25 Asikiapo sauti ya baragumu yeye hulia, ‘Aha!’ \q2 Hunusa harufu ya vita toka mbali, \q2 sauti ya mtoa amri na ukelele wa vita. \b \q1 \v 26 “Je, mwewe huruka kwa hekima yako \q2 na kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini? \q1 \v 27 Je, tai hupaa juu kwa amri yako \q2 na kujenga kiota chake mahali pa juu? \q1 \v 28 Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku; \q2 majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake. \q1 \v 29 Kutoka huko hutafuta chakula chake; \q2 macho yake hukiona kutoka mbali. \q1 \v 30 Makinda yake hujilisha damu, \q2 na pale palipo na machinjo, ndipo yeye alipo.” \c 40 \p \v 1 \nd Bwana\nd* akamwambia Ayubu: \q1 \v 2 “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? \q2 Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.” \p \v 3 Ndipo Ayubu akamjibu \nd Bwana\nd*: \q1 \v 4 “Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe? \q2 Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu. \q1 \v 5 Nimesema mara moja, lakini sina jibu; \q2 naam, nimesema mara mbili, \q2 lakini sitasema tena.” \p \v 6 Ndipo \nd Bwana\nd* akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli: \q1 \v 7 “Jikaze kama mwanaume; \q2 nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu. \b \q1 \v 8 “Je, utabatilisha hukumu yangu? \q2 Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe? \q1 \v 9 Je, una mkono kama wa Mungu, \q2 nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake? \q1 \v 10 Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, \q2 nawe uvae heshima na enzi. \q1 \v 11 Fungulia ukali wa ghadhabu yako, \q2 mtafute kila mwenye kiburi umshushe, \q1 \v 12 mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, \q2 waponde waovu mahali wasimamapo. \q1 \v 13 Wazike wote mavumbini pamoja; \q2 wafunge nyuso zao kaburini. \q1 \v 14 Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia \q2 kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa. \b \q1 \v 15 “Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,\f + \fr 40:15 \ft Huyu alikuwa mnyama wa nyakati za zamani ambaye hajulikani hasa ni gani.\f* \q2 niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, \q2 anayekula majani kama ngʼombe. \q1 \v 16 Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake, \q2 uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake! \q1 \v 17 Mkia wake hutikisika kama mwerezi; \q2 mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja. \q1 \v 18 Mifupa yake ni bomba za shaba, \q2 maungo yake ni kama fito za chuma. \q1 \v 19 Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu, \q2 lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake. \q1 \v 20 Vilima humletea yeye mazao yake, \q2 nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye. \q1 \v 21 Hulala chini ya mimea ya yungiyungi, \q2 katika maficho ya matete kwenye matope. \q1 \v 22 Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake; \q2 miti mirefu karibu na kijito humzunguka. \q1 \v 23 Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu; \q2 yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake. \q1 \v 24 Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho, \q2 au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake? \b \c 41 \q1 \v 1 “Je, waweza kumvua Lewiathani\f + \fr 41:1 \ft Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.\f* kwa ndoano ya samaki, \q2 au kufunga ulimi wake kwa kamba? \q1 \v 2 Waweza kupitisha kamba puani mwake, \q2 au kutoboa taya lake kwa kulabu? \q1 \v 3 Je, ataendelea kukuomba umhurumie? \q2 Atasema nawe maneno ya upole? \q1 \v 4 Je, atafanya agano nawe ili umtwae \q2 awe mtumishi wako maisha yake yote? \q1 \v 5 Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, \q2 au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako? \q1 \v 6 Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? \q2 Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara? \q1 \v 7 Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, \q2 au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki? \q1 \v 8 Kama ukiweka mkono wako juu yake, \q2 utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena! \q1 \v 9 Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; \q2 kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini. \q1 \v 10 Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. \q2 Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu? \q1 \v 11 Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? \q2 Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu. \b \q1 \v 12 “Sitashindwa kunena juu ya maungo yake, \q2 nguvu zake na umbo lake zuri. \q1 \v 13 Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje? \q2 Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu? \q1 \v 14 Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake, \q2 kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote? \q1 \v 15 Mgongo wake una safu za ngao \q2 zilizoshikamanishwa imara pamoja; \q1 \v 16 kila moja iko karibu sana na mwenzake, \q2 wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake. \q1 \v 17 Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine; \q2 zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa. \q1 \v 18 Akipiga chafya mwanga humetameta; \q2 macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko. \q1 \v 19 Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake; \q2 cheche za moto huruka nje. \q1 \v 20 Moshi hufuka kutoka puani mwake, \q2 kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete. \q1 \v 21 Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, \q2 nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake. \q1 \v 22 Nguvu hukaa katika shingo yake; \q2 utisho hutangulia mbele yake. \q1 \v 23 Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja; \q2 iko imara na haiwezi kuondolewa. \q1 \v 24 Kifua chake ni kigumu kama mwamba, \q2 kigumu kama jiwe la chini la kusagia. \q1 \v 25 Ainukapo, mashujaa wanaogopa; \q2 hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo. \q1 \v 26 Upanga unaomfikia haumdhuru, \q2 wala mkuki au mshale wala fumo. \q1 \v 27 Chuma hukiona kama unyasi, \q2 na shaba kama mti uliooza. \q1 \v 28 Mishale haimfanyi yeye akimbie; \q2 mawe ya kombeo kwake ni kama makapi. \q1 \v 29 Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu; \q2 hucheka sauti za kugongana kwa mkuki. \q1 \v 30 Sehemu zake za chini kwenye tumbo \q2 zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu, \q1 zikiacha mburuzo kwenye matope \q2 kama chombo chenye meno cha kupuria. \q1 \v 31 Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo, \q2 na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu. \q1 \v 32 Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta; \q2 mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi. \q1 \v 33 Hakuna chochote duniani kinacholingana naye: \q2 yeye ni kiumbe kisicho na woga. \q1 \v 34 Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna; \q2 yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.” \c 42 \ms1 Sehemu Ya Tano \mr (Ayubu 42) \s1 Ayubu Anamjibu \nd Bwana\nd* \p \v 1 Ndipo Ayubu akamjibu \nd Bwana\nd*: \q1 \v 2 “Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, \q2 wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika. \q1 \v 3 Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ \q2 Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi, \q2 mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua. \b \q1 \v 4 “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena; \q2 nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’ \q1 \v 5 Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, \q2 lakini sasa macho yangu yamekuona. \q1 \v 6 Kwa hiyo najidharau mwenyewe, \q2 na kutubu katika mavumbi na majivu.” \s1 Mwisho: Marafiki Wa Ayubu Wanafedheheshwa \p \v 7 Baada ya \nd Bwana\nd* kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu. \v 8 Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.” \v 9 Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kama \nd Bwana\nd* alivyowaambia; naye \nd Bwana\nd* akayakubali maombi ya Ayubu. \p \v 10 Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, \nd Bwana\nd* akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni. \v 11 Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote \nd Bwana\nd* aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu. \p \v 12 \nd Bwana\nd* akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja. \v 13 Tena alikuwa na wana saba na binti watatu. \v 14 Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki. \v 15 Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao. \p \v 16 Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne. \v 17 Hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee aliyekuwa ameshiba siku.