\id ZEP - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version \rem Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc. \h Sefania \toc1 Sefania \toc2 Sefania \toc3 Sef \mt1 Sefania \c 1 \p \v 1 Neno la \nd Bwana\nd* lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda: \b \s1 Onyo La Maangamizi Yanayokuja \q1 \v 2 \nd Bwana\nd* asema, \q2 “Nitafagia kila kitu \q2 kutoka kwenye uso wa dunia.” \q1 \v 3 “Nitafagilia mbali watu na wanyama; \q2 nitafagilia mbali ndege wa angani \q2 na samaki wa baharini. \q1 Wafanyao maovu watapata tu kokoto, \q2 nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke katika dunia,” \q4 asema \nd Bwana\nd*. \s1 Dhidi Ya Yuda \q1 \v 4 “Nitaiadhibu Yuda \q2 na wote wakaao Yerusalemu. \q1 Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali \q2 kila mabaki ya Baali, \q1 majina ya wapagani na makuhani \q2 waabuduo sanamu: \q1 \v 5 wale ambao husujudu juu ya mapaa \q2 kuabudu jeshi la vitu vya angani, \q1 wale ambao husujudu na kuapa kwa \nd Bwana\nd* \q2 na ambao pia huapa kwa Malkamu, \q1 \v 6 wale wanaoacha kumfuata \nd Bwana\nd*, \q2 wala hawamtafuti \nd Bwana\nd* \q2 wala kutaka shauri lake. \q1 \v 7 Nyamazeni mbele za \nd Bwana\nd* Mwenyezi, \q2 kwa maana siku ya \nd Bwana\nd* iko karibu. \q1 \nd Bwana\nd* ameandaa dhabihu, \q2 amewaweka wakfu wale aliowaalika. \q1 \v 8 Katika siku ya dhabihu ya \nd Bwana\nd* \q2 nitawaadhibu wakuu \q2 na wana wa mfalme \q1 na wale wote wanaovaa \q2 nguo za kigeni. \q1 \v 9 Katika siku hiyo nitaadhibu wote ambao \q2 hukwepa kukanyaga kizingiti, \q1 ambao hujaza hekalu la miungu yao \q2 kwa dhuluma na udanganyifu.” \b \q1 \v 10 \nd Bwana\nd* asema, “Katika siku hiyo \q2 kilio kitapanda juu kutoka lango la Samaki, \q2 maombolezo kutoka mtaa wa pili, \q2 na mshindo mkubwa kutoka vilimani. \q1 \v 11 Ombolezeni, ninyi mnaoishi katika eneo la sokoni; \q2 wafanyabiashara wenu wote wameangamizwa, \q1 wote ambao wanafanya biashara ya fedha \q2 wataangamizwa. \q1 \v 12 Wakati huo nitasaka mji wa Yerusalemu kwa taa, \q2 na kuwaadhibu wale ambao \q2 wanakaa katika hali ya kuridhika, \q1 ambao ni kama divai \q2 iliyobaki kwenye machicha, \q1 ambao hudhani, ‘\nd Bwana\nd* hatafanya lolote, \q2 jema au baya.’ \q1 \v 13 Utajiri wao utatekwa nyara, \q2 nyumba zao zitabomolewa. \q1 Watajenga nyumba, \q2 lakini hawataishi ndani yake; \q1 watapanda mizabibu \q2 lakini hawatakunywa divai yake. \s1 Siku Kubwa Ya \nd Bwana\nd* \q1 \v 14 “Siku kubwa ya \nd Bwana\nd* iko karibu: \q2 iko karibu na inakuja haraka. \q1 Sikilizeni! Kilio katika siku ya \nd Bwana\nd* \q2 kitakuwa kichungu, \q2 hata shujaa atapiga kelele. \q1 \v 15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, \q2 siku ya fadhaa na dhiki, \q1 siku ya uharibifu na ukiwa, \q2 siku ya giza na utusitusi, \q2 siku ya mawingu na giza nene, \q1 \v 16 siku ya tarumbeta na mlio wa vita \q2 dhidi ya miji yenye ngome \q2 na dhidi ya minara mirefu. \q1 \v 17 Nitawaletea watu dhiki, \q2 nao watatembea kama vipofu, \q1 kwa sababu wametenda dhambi \q2 dhidi ya \nd Bwana\nd*. \q1 Damu yao itamwagwa kama vumbi \q2 na matumbo yao kama taka. \q1 \v 18 Fedha yao wala dhahabu yao \q2 hazitaweza kuwaokoa \q2 katika siku hiyo ya ghadhabu ya \nd Bwana\nd*. \q1 Katika moto wa wivu wake \q2 dunia yote itateketezwa, \q1 kwa maana ataleta mwisho \q2 wa wote wanaoishi katika dunia ghafula.” \c 2 \q1 \v 1 Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja, \q2 enyi taifa lisilo na aibu, \q1 \v 2 kabla ya wakati ulioamriwa haujafika \q2 na siku ile inayopeperusha kama makapi, \q1 kabla hasira kali ya \nd Bwana\nd* haijaja juu yenu, \q2 kabla siku ya ghadhabu ya \nd Bwana\nd* \q2 haijaja juu yenu. \q1 \v 3 Mtafuteni \nd Bwana\nd*, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi, \q2 ninyi ambao hufanya lile analoamuru. \q1 Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu; \q2 labda mtahifadhiwa \q2 siku ya hasira ya \nd Bwana\nd*. \s1 Dhidi Ya Ufilisti \q1 \v 4 Gaza utaachwa \q2 na Ashkeloni utaachwa magofu. \q1 Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu \q2 na Ekroni utangʼolewa. \q1 \v 5 Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari, \q2 enyi Wakerethi; \q1 neno la \nd Bwana\nd* liko dhidi yenu, \q2 ee Kanaani, nchi ya Wafilisti. \b \q1 “Mimi nitawaangamiza, \q2 na hakuna atakayebaki.” \b \q1 \v 6 Nchi kando ya bahari, mahali ambapo wanaishi Wakerethi, \q2 patakuwa mahali pa wachungaji \q2 na mazizi ya kondoo. \q1 \v 7 Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, \q2 hapo watapata malisho. \q1 Wakati wa jioni watajilaza chini \q2 katika nyumba za Ashkeloni. \q1 \nd Bwana\nd* Mungu wao atawatunza, \q2 naye atawarudishia wafungwa wao. \s1 Dhidi Ya Moabu Na Amoni \q1 \v 8 “Nimeyasikia matukano ya Moabu \q2 nazo dhihaka za Waamoni, \q1 ambao waliwatukana watu wangu \q2 na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao. \q1 \v 9 Hakika, kama niishivyo,” \q2 asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote, \q2 Mungu wa Israeli, \q1 “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, \q2 Waamoni kama Gomora: \q1 mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, \q2 nchi ya ukiwa milele. \q1 Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; \q2 mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.” \b \q1 \v 10 Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao, \q2 kwa kutukana na kudhihaki \q2 watu wa \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \q1 \v 11 \nd Bwana\nd* atakuwa wa kuhofisha kwao \q2 atakapoangamiza miungu yote ya nchi. \q1 Mataifa katika kila pwani yatamwabudu, \q2 kila moja katika nchi yake. \s1 Dhidi Ya Kushi \q1 \v 12 “Ninyi pia, ee Wakushi, \q2 mtauawa kwa upanga wangu.” \s1 Dhidi Ya Ashuru \q1 \v 13 Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazini \q2 na kuangamiza Waashuru, \q1 akiiacha Ninawi ukiwa \q2 na pakame kama jangwa. \q1 \v 14 Makundi ya kondoo na ngʼombe yatajilaza pale, \q2 viumbe vya kila aina. \q1 Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba \q2 wataishi juu ya nguzo zake. \q1 Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, \q2 kifusi kitakuwa milangoni, \q2 boriti za mierezi zitaachwa wazi. \q1 \v 15 Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furaha \q2 wakijisikia salama. \q1 Ulisema moyoni mwako, \q2 “Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.” \q1 Jinsi gani umekuwa gofu, \q2 mahali pa kulala wanyama pori! \q1 Wote wanaopita kando yake wanauzomea \q2 na kutikisa mkono kwa dharau. \c 3 \s1 Hatima Ya Yerusalemu \q1 \v 1 Ole mji wa wadhalimu, \q2 waasi na waliotiwa unajisi! \q1 \v 2 Hautii mtu yeyote, \q2 haukubali maonyo. \q1 Haumtumaini \nd Bwana\nd*, \q2 haukaribii karibu na Mungu wake. \q1 \v 3 Maafisa wake ni simba wangurumao, \q2 watawala wake ni mbwa mwitu wa jioni, \q1 ambao hawabakizi chochote \q2 kwa ajili ya asubuhi. \q1 \v 4 Manabii wake ni wenye kiburi, \q2 ni wadanganyifu. \q1 Makuhani wake hunajisi patakatifu \q2 na kuihalifu sheria. \q1 \v 5 \nd Bwana\nd* aliye ndani yake ni mwenye haki, \q2 hafanyi kosa. \q1 Asubuhi kwa asubuhi hutoa haki yake, \q2 kila kukipambazuka huitimiza, \q2 bali mtu dhalimu hana aibu. \b \q1 \v 6 “Nimeyafutilia mbali mataifa, \q2 ngome zao zimebomolewa. \q1 Nimeziacha barabara ukiwa, \q2 hakuna anayepita humo. \q1 Miji yao imeharibiwa; \q2 hakuna mmoja atakayeachwa: \q2 hakuna hata mmoja. \q1 \v 7 Niliuambia huo mji, \q2 ‘Hakika utaniogopa na kukubali maonyo!’ \q1 Ndipo makao yake hayatafutiliwa mbali, \q2 wala adhabu zangu zote hazitakuja juu yake. \q1 Lakini walikuwa bado na shauku \q2 kutenda kwa upotovu katika yote waliyofanya.” \q1 \v 8 \nd Bwana\nd* anasema, \q2 “Kwa hiyo ningojee mimi, \q2 siku nitakayosimama kuteka nyara. \q1 Nimeamua kukusanya mataifa, \q2 kukusanya falme \q1 na kumimina ghadhabu yangu juu yao, \q2 hasira yangu kali yote. \q1 Dunia yote itateketezwa \q2 kwa moto wa wivu wa hasira yangu. \b \q1 \v 9 “Ndipo nitatakasa midomo ya mataifa, \q2 kwamba wote waweze kuliitia jina la \nd Bwana\nd* \q2 na kumtumikia kwa pamoja. \q1 \v 10 Kutoka ngʼambo ya mito ya Kushi \q2 watu wangu wanaoniabudu, \q1 watu wangu waliotawanyika, \q2 wataniletea sadaka. \q1 \v 11 Siku hiyo hutaaibishwa \q2 kwa ajili ya makosa yote ulionitendea, \q1 kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu \q2 wale wote wanaoshangilia \q2 katika kiburi chao. \q1 Kamwe hutajivuna tena \q2 katika kilima changu kitakatifu. \q1 \v 12 Lakini nitakuachia ndani yako \q2 wapole na wanyenyekevu, \q2 ambao wanatumaini jina la \nd Bwana\nd*. \q1 \v 13 Mabaki ya Israeli hayatafanya kosa; \q2 hawatasema uongo, \q1 wala udanganyifu hautakuwa \q2 katika vinywa vyao. \q1 Watakula na kulala \q2 wala hakuna yeyote \q2 atakayewaogopesha.” \b \q1 \v 14 Imba, ee Binti Sayuni; \q2 paza sauti, ee Israeli! \q1 Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, \q2 ee Binti Yerusalemu! \q1 \v 15 \nd Bwana\nd* amekuondolea adhabu yako, \q2 amewarudisha nyuma adui zako. \q1 \nd Bwana\nd*, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe; \q2 kamwe hutaogopa tena madhara yoyote. \q1 \v 16 Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu, \q2 “Usiogope, ee Sayuni; \q2 usiiache mikono yako ilegee. \q1 \v 17 \nd Bwana\nd* Mungu wako yu pamoja nawe, \q2 yeye ni mwenye nguvu kuokoa. \q1 Atakufurahia kwa furaha kubwa, \q2 atakutuliza kwa pendo lake, \q2 atakufurahia kwa kuimba.” \b \q1 \v 18 “Huzuni katika sikukuu zilizoamriwa \q2 nitaziondoa kwenu; \q2 hizo ni mzigo na fedheha kwenu. \q1 \v 19 Wakati huo nitawashughulikia \q2 wote waliokudhulumu; \q1 nitaokoa vilema na kukusanya \q2 wale ambao wametawanywa. \q1 Nitawapa sifa na heshima \q2 katika kila nchi ambayo waliaibishwa. \q1 \v 20 Wakati huo nitawakusanya; \q2 wakati huo nitawaleta nyumbani. \q1 Nitawapa sifa na heshima \q2 miongoni mwa mataifa yote ya dunia \q1 wakati nitakapowarudishia mateka yenu \q2 mbele ya macho yenu hasa,” \q4 asema \nd Bwana\nd*.