\id ZEC - Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version \rem Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc. \h Zekaria \toc1 Zekaria \toc2 Zekaria \toc3 Zek \mt1 Zekaria \c 1 \s1 Wito Wa Kumrudia \nd Bwana\nd* \p \v 1 Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la \nd Bwana\nd* lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema: \p \v 2 “\nd Bwana\nd* aliwakasirikia sana baba zako wa zamani. \v 3 Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \v 4 Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema \nd Bwana\nd*. \v 5 Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? \v 6 Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?” \p “Kisha walitubu na kusema, ‘\nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ ” \s1 Maono Ya Kwanza: Mtu Katikati Ya Miti Ya Mihadasi \p \v 7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la \nd Bwana\nd* lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido. \p \v 8 Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe. \p \v 9 Nikauliza, “Hivi ni vitu gani bwana wangu?” \p Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, “Nitakuonyesha kuwa ni nini.” \p \v 10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambao \nd Bwana\nd* amewatuma waende duniani kote.” \p \v 11 Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa \nd Bwana\nd*, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.” \p \v 12 Kisha malaika wa \nd Bwana\nd* akasema, “\nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?” \v 13 Kwa hiyo \nd Bwana\nd* akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami. \p \v 14 Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, “Tangaza neno hili: Hili ndilo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni, \v 15 lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’ \p \v 16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo \nd Bwana\nd*: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \p \v 17 “Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi na \nd Bwana\nd* atamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ” \s1 Maono Ya Pili: Pembe Nne Na Mafundi Wanne \p \v 18 Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! \v 19 Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?” \p Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.” \p \v 20 Kisha \nd Bwana\nd* akanionyesha mafundi wanne. \v 21 Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?” \p Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.” \c 2 \s1 Maono Ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia \p \v 1 Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! \v 2 Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?” \p Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.” \p \v 3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye \v 4 na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo. \v 5 Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema \nd Bwana\nd*, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’ \p \v 6 “Njooni! Njooni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asema \nd Bwana\nd*, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asema \nd Bwana\nd*. \p \v 7 “Njoo, ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!” \v 8 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake, \v 9 hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwamba \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote amenituma. \p \v 10 “Piga kelele na ufurahie, ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asema \nd Bwana\nd*. \v 11 “Mataifa mengi yataunganishwa na \nd Bwana\nd* siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. \v 12 \nd Bwana\nd* atairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu. \v 13 Tulieni mbele za \nd Bwana\nd*, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.” \c 3 \s1 Maono Ya Nne: Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu \p \v 1 Kisha akanionyesha Yoshua,\f + \fr 3:1 \ft Yoshua kwa Kiebrania ni Yeshua, maana yake ni Yehova ni wokovu.\f* kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa \nd Bwana\nd*, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki. \v 2 \nd Bwana\nd* akamwambia Shetani, “\nd Bwana\nd* akukemee Shetani! \nd Bwana\nd*, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?” \p \v 3 Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. \v 4 Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.” \p Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.” \p \v 5 Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa \nd Bwana\nd* akiwa amesimama karibu. \p \v 6 Malaika wa \nd Bwana\nd* akamwamuru Yoshua: \v 7 “Hivi ndivyo asemavyo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa. \p \v 8 “ ‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. \v 9 Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja. \p \v 10 “ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote.” \c 4 \s1 Maono Ya Tano: Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni Miwili \p \v 1 Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka usingizi wake. \v 2 Akaniuliza, “Unaona nini?” \p Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. \v 3 Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.” \p \v 4 Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?” \p \v 5 Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?” \p Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.” \p \v 6 Kisha akaniambia, “Hili ni neno la \nd Bwana\nd* kwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,’ asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \p \v 7 “Wewe ni kitu gani, ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ” \p \v 8 Kisha neno la \nd Bwana\nd* likanijia: \v 9 “Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu. \p \v 10 “Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli. \p “(Hizi saba ni macho ya \nd Bwana\nd* ambayo huzunguka duniani kote.)” \p \v 11 Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?” \p \v 12 Tena nikamuuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?” \p \v 13 Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?” \p Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.” \p \v 14 Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.” \c 5 \s1 Maono Ya Sita: Kitabu Kinachoruka \p \v 1 Nikatazama tena: na hapo mbele yangu kulikuwa na kitabu kilichoruka! \p \v 2 Akaniuliza, “Unaona nini?” \p Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka chenye, urefu wa dhiraa ishirini\f + \fr 5:2 \ft Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.\f* na upana wa dhiraa kumi.”\f + \fr 5:2 \ft Dhiraa 10 ni sawa mita 4.5.\f* \p \v 3 Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atafukuziwa mbali, pia kufuatana na yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atafukuziwa mbali. \v 4 \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote asema, ‘Nitaituma hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa Jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ” \s1 Maono Ya Saba: Mwanamke Ndani Ya Kikapu \p \v 5 Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone ni nini kile kinachojitokeza.” \p \v 6 Nikamuuliza, “Ni kitu gani?” \p Akanijibu, “Ni kikapu cha kupimia.” Kisha akaongeza kusema, “Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.” \p \v 7 Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuwako mwanamke ameketi! \v 8 Akasema, “Huu ni uovu,” tena akamsukumia ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu. \p \v 9 Kisha nikatazama juu: na pale mbele yangu, walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu na nchi. \p \v 10 Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Wanakipeleka wapi hicho kikapu?” \p \v 11 Akanijibu, “Wanakipeleka katika nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale mahali pake.” \c 6 \s1 Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita \p \v 1 Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! \v 2 Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, \v 3 la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. \v 4 Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?” \p \v 5 Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. \v 6 Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.” \p \v 7 Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote. \p \v 8 Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini.” \s1 Taji Kwa Ajili Ya Yoshua \p \v 9 Neno la \nd Bwana\nd* likanijia kusema: \v 10 “Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania. \v 11 Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki. \v 12 Umwambie, hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu la \nd Bwana\nd*. \v 13 Ni yeye atakayejenga Hekalu la \nd Bwana\nd*, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’ \v 14 Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu la \nd Bwana\nd*. \v 15 Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la \nd Bwana\nd*, nanyi mtajua ya kwamba \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii \nd Bwana\nd* Mungu wenu kwa bidii.” \c 7 \s1 Haki Na Rehema, Sio Kufunga \p \v 1 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno la \nd Bwana\nd* lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu. \v 2 Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi \nd Bwana\nd* \v 3 kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?” \p \v 4 Kisha neno la \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote likanijia kusema: \v 5 “Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu? \v 6 Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasherehekea kwa ajili ya nafsi zenu? \v 7 Je, haya sio maneno ya \nd Bwana\nd* aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ” \p \v 8 Neno la \nd Bwana\nd* likamjia tena Zekaria: \v 9 “Hivi ndivyo asemavyo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. \v 10 Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’ \p \v 11 “Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao. \v 12 Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote alikasirika sana. \p \v 13 “ ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \v 14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ” \c 8 \s1 \nd Bwana\nd* Anaahidi Kuibariki Yerusalemu \p \v 1 Neno la \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote likanijia tena. \v 2 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.” \p \v 3 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd*: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote utaitwa Mlima Mtakatifu.” \p \v 4 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake. \v 5 Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.” \p \v 6 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \p \v 7 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi. \v 8 Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.” \p \v 9 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba ya \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote, mikono yenu na iwe na nguvu ili Hekalu liweze kujengwa. \v 10 Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake. \v 11 Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,” asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \p \v 12 “Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao. \v 13 Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.” \p \v 14 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,” asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote, \v 15 “hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope. \v 16 Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu, \v 17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia yote haya,” asema \nd Bwana\nd*. \p \v 18 Neno la \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote likanijia tena. \v 19 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.” \p \v 20 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja, \v 21 na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi \nd Bwana\nd*, na kumtafuta \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’ \v 22 Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote na kumsihi.” \p \v 23 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watangʼangʼania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ” \c 9 \s1 Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli \p \v 1 Neno: \q1 Neno la \nd Bwana\nd* liko kinyume na nchi ya Hadraki \q2 na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, \q1 kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote \q2 za Israeli yako kwa \nd Bwana\nd*, \q1 \v 2 pia juu ya Hamathi inayopakana nayo, \q2 juu ya Tiro na Sidoni, \q2 ingawa wana ujuzi mwingi sana. \q1 \v 3 Tiro amejijengea ngome imara, \q2 amelundika fedha kama mavumbi \q2 na dhahabu kama taka za mitaani. \q1 \v 4 Lakini Bwana atamwondolea mali zake \q2 na kuuangamiza uwezo wake wa baharini, \q2 naye atateketezwa kwa moto. \q1 \v 5 Ashkeloni ataona hili na kuogopa; \q2 Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, \q1 pia Ekroni, kwa sababu \q2 matumaini yake yatanyauka. \q1 Gaza atampoteza mfalme wake \q2 na Ashkeloni ataachwa pweke. \q1 \v 6 Wageni watakalia mji wa Ashdodi, \q2 nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. \q1 \v 7 Nitaondoa damu vinywani mwao, \q2 chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao. \q1 Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu, \q2 nao watakuwa viongozi katika Yuda, \q2 naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi. \q1 \v 8 Lakini nitailinda nyumba yangu \q2 dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi. \q1 Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena, \q2 kwa maana sasa ninawachunga. \s1 Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni \q1 \v 9 Shangilia sana, ee Binti Sayuni! \q2 Piga kelele, Binti Yerusalemu! \q1 Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, \q2 ni mwenye haki, naye ana wokovu, \q2 ni mpole, naye amepanda punda, \q2 mwana-punda, mtoto wa punda. \q1 \v 10 Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu \q2 na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, \q2 nao upinde wa vita utavunjwa. \q1 Atatangaza amani kwa mataifa. \q2 Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, \q2 na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia. \q1 \v 11 Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe, \q2 nitawaacha huru wafungwa wako \q2 watoke kwenye shimo lisilo na maji. \q1 \v 12 Rudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini; \q2 hata sasa ninatangaza kwamba \q2 nitawarejesheeni maradufu. \q1 \v 13 Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu, \q2 nitamfanya Efraimu mshale wangu. \q1 Nitawainua wana wako, ee Sayuni, \q2 dhidi ya wana wako, ee Uyunani, \q2 na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita. \s1 \nd Bwana\nd* Atatokea \q1 \v 14 Kisha \nd Bwana\nd* atawatokea; \q2 mshale wake utamulika \q2 kama umeme wa radi. \q1 \nd Bwana\nd* Mwenyezi atapiga tarumbeta, \q2 naye atatembea katika tufani za kusini, \q2 \v 15 na \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote atawalinda. \q1 Wataangamiza na kushinda \q2 kwa mawe ya kutupa kwa kombeo. \q1 Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo; \q2 watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia \q2 kwenye pembe za madhabahu. \q1 \v 16 \nd Bwana\nd* Mungu wao atawaokoa siku hiyo \q2 kama kundi la watu wake. \q1 Watangʼara katika nchi yake \q2 kama vito vya thamani kwenye taji. \q1 \v 17 Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! \q2 Nafaka itawastawisha vijana wanaume, \q2 nayo divai mpya vijana wanawake. \c 10 \s1 \nd Bwana\nd* Ataitunza Yuda \q1 \v 1 Mwombeni \nd Bwana\nd* mvua wakati wa vuli; \q2 ndiye \nd Bwana\nd* atengenezaye mawingu ya tufani. \q1 Huwapa watu manyunyu ya mvua, \q2 pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu. \q1 \v 2 Sanamu huzungumza udanganyifu, \q2 waaguzi huona maono ya uongo; \q1 husimulia ndoto ambazo si za kweli, \q2 wanatoa faraja batili. \q1 Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo \q2 walioonewa kwa kukosa mchungaji. \b \q1 \v 3 “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, \q2 nami nitawaadhibu viongozi; \q1 kwa kuwa \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote \q2 atalichunga kundi lake, \q2 nyumba ya Yuda, \q1 naye atawafanya kuwa kama farasi \q2 mwenye kiburi akiwa vitani. \q1 \v 4 Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni, \q2 kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema, \q2 kutoka kwake utatoka upinde wa vita, \q2 kutoka kwake atatoka kila mtawala. \q1 \v 5 Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa \q2 wanaokanyaga barabara za matope \q2 wakati wa vita. \q1 Kwa sababu \nd Bwana\nd* yu pamoja nao, \q2 watapigana na kuwashinda wapanda farasi. \b \q1 \v 6 “Nitaiimarisha nyumba ya Yuda \q2 na kuiokoa nyumba ya Yosefu. \q1 Nitawarejesha kwa sababu \q2 nina huruma juu yao. \q1 Watakuwa kama watu ambao \q2 sijawahi kuwakataa \q1 kwa sababu mimi ndimi \nd Bwana\nd* Mungu wao, \q2 nami nitawajibu. \q1 \v 7 Waefraimu watakuwa kama mashujaa, \q2 mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai. \q1 Watoto wao wataona na kufurahi, \q2 mioyo yao itashangilia katika \nd Bwana\nd*. \q1 \v 8 Nitawaashiria na kuwakusanya ndani. \q2 Hakika nitawakomboa, \q1 nao watakuwa wengi \q2 kama walivyokuwa mwanzoni. \q1 \v 9 Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa, \q2 hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali \q2 watanikumbuka mimi. \q1 Wao na watoto wao watanusurika katika hatari \q2 nao watarudi. \q1 \v 10 Nitawarudisha kutoka Misri \q2 na kuwakusanya toka Ashuru. \q1 Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni, \q2 na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha. \q1 \v 11 Watapita katika bahari ya mateso; \q2 bahari iliyochafuka itatulizwa \q2 na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka. \q1 Kiburi cha Ashuru kitashushwa, \q2 nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka. \q1 \v 12 Nitawaimarisha katika \nd Bwana\nd*, \q2 na katika jina lake watatembea,” \q4 asema \nd Bwana\nd*. \c 11 \q1 \v 1 Fungua milango yako, ee Lebanoni, \q2 ili moto uteketeze mierezi yako! \q1 \v 2 Piga yowe, ee mti wa msunobari, \q2 kwa kuwa mwerezi umeanguka; \q2 miti ya fahari imeharibiwa! \q1 Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, \q2 msitu mnene umefyekwa! \q1 \v 3 Sikiliza yowe la wachungaji; \q2 malisho yao manono yameangamizwa! \q1 Sikia ngurumo za simba; \q2 kichaka kilichostawi sana \q2 cha Yordani kimeharibiwa! \s1 Wachungaji Wawili Wa Kondoo \p \v 4 Hili ndilo asemalo \nd Bwana\nd* Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. \v 5 Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘\nd Bwana\nd* asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. \v 6 Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema \nd Bwana\nd*. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.” \p \v 7 Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi. \v 8 Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu. \p Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao, \v 9 nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.” \p \v 10 Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote. \v 11 Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo wale waliodhurika katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la \nd Bwana\nd*. \p \v 12 Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha. \p \v 13 Naye \nd Bwana\nd* akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,” hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba ya \nd Bwana\nd*. \p \v 14 Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli! \p \v 15 Kisha \nd Bwana\nd* akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. \v 16 Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao. \q1 \v 17 “Ole wa mchungaji asiyefaa, \q2 anayeliacha kundi! \q1 Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume! \q2 Mkono wake na unyauke kabisa, \q2 jicho lake la kuume lipofuke kabisa!” \c 12 \s1 Maadui Wa Yerusalemu Kuangamizwa \p \v 1 Hili ni neno la \nd Bwana\nd* kuhusu Israeli. \nd Bwana\nd*, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema: \v 2 “Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia. \v 3 Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe. \v 4 Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa uwazimu,” asema \nd Bwana\nd*. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa. \v 5 Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’ \p \v 6 “Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake. \p \v 7 “\nd Bwana\nd* atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda. \v 8 Katika siku hiyo, \nd Bwana\nd* atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa \nd Bwana\nd* akiwatangulia. \v 9 Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu. \s1 Kumwombolezea Yule Aliyechomwa Mkuki \p \v 10 “Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema\f + \fr 12:10 \ft Au: Roho wa neema.\f* na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. \v 11 Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. \v 12 Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao, \v 13 ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, \v 14 na koo zote zilizobaki na wake zao. \c 13 \s1 Kutakaswa Dhambi \p \v 1 “Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi. \p \v 2 “Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi. \v 3 Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la \nd Bwana\nd*.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo. \p \v 4 “Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu. \v 5 Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’ \v 6 Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’ \s1 Mchungaji Apigwa, Nao Kondoo Watawanyika \q1 \v 7 “Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, \q2 dhidi ya mtu aliye karibu nami!” \q2 asema \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote. \q1 “Mpige mchungaji, \q2 nao kondoo watatawanyika, \q1 nami nitageuza mkono wangu \q2 dhidi ya walio wadogo, \q1 \v 8 katika nchi yote,” asema \nd Bwana\nd*, \q2 “theluthi mbili watapigwa na kuangamia; \q2 hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake. \q1 \v 9 Hii theluthi moja nitaileta katika moto; \q2 nitawasafisha kama fedha isafishwavyo \q2 na kuwajaribu kama dhahabu. \q1 Wataliitia Jina langu \q2 nami nitawajibu; \q1 nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ \q2 nao watasema, ‘\nd Bwana\nd* ni Mungu wetu.’ ” \c 14 \s1 \nd Bwana\nd* Yuaja Kutawala \p \v 1 Siku ya \nd Bwana\nd* inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu. \p \v 2 Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini. \p \v 3 Kisha \nd Bwana\nd* atatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita. \v 4 Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. \v 5 Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha \nd Bwana\nd* Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye. \p \v 6 Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. \v 7 Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na \nd Bwana\nd*. Jioni inapofika nuru itakuwepo. \p \v 8 Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,\f + \fr 14:8 \ft Yaani Bahari ya Chumvi au Bahari Mfu.\f* na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi\f + \fr 14:8 \ft Yaani Bahari ya Mediterania.\f* wakati wa kiangazi na wakati wa masika. \p \v 9 \nd Bwana\nd* atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo \nd Bwana\nd* mmoja na jina lake litakuwa jina pekee. \p \v 10 Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba.\f + \fr 14:10 \ft Araba maana yake Nchi tambarare.\f* Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme. \v 11 Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama. \p \v 12 Hii ndiyo tauni ambayo \nd Bwana\nd* atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao. \v 13 Katika siku hiyo \nd Bwana\nd* atawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana. \v 14 Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo. \v 15 Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walioko kwenye kambi za adui. \p \v 16 Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. \v 17 Ikiwa taifa lolote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao. \v 18 Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. \nd Bwana\nd* ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. \v 19 Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. \p \v 20 Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: \sc Takatifu kwa Bwana\sc*, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya \nd Bwana\nd* vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. \v 21 Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba ya \nd Bwana\nd* Mwenye Nguvu Zote.